Monday 28 August 2023

RAIS DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AONGOZA PROGRAMU YA UZAZI NI MAISHA WOGGING YENYE LENGO LA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akiongoza Matembezi na mbio fupi za Uzazi Ni Maisha Wogging 2023 yalioanzia viwanja vya Butros Kiembe Samaki na Kumalizikia Viwanja vya Maisara Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezipongeza jitihada zinazochukuliwa na wadau wa maendeleo, wahisani na mashirika kwa juhudi wanazozichukua katika kuiunga mkono serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo jana katika viwanja vya Maiasra vilivyopo Zanzibar alipokuwa akizungumza kwenye kampeni ya ' Uzazi ni Maisha Wogging Marathon (Walk-Jog-Run) kwa mwaka 2023 “ iliyoandaliwa kwa ushirikiano baina ya wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Kimataifa la Amref Health Afrika Tanzania chini ya udhamini wa benki ya Absa.

Alisema wadau wa maendeleo na mashirika yana mchango mkubwa katika kusaidia maendeleo ya jamii na kulipongeza shirika la Amref Tanzania kwa kuanzisha kampeni ya 'Uzazi ni Maisha Wogging yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akilishukuru shirika la Amref Health Africa Tanzania pamoja na Mdhamini wa Matembezi na mbio fupi hizo benki ya Absa na wadau wake wote Mara baada ya kumaliza kampeni ya Uzazi ni Maisha wogging Zanzibar.


"Napenda niwashukuru Amref Health Africa kwa kutoa msaada wa gari maalum ambayo itasaidia kusafirisha wataalamu, kusafirisha sampuli, kutoa huduma za upimaji na ushauri nasaha kwa wananchi katika vituo vya afya hapa Zanzibar", alisema.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Amref Health Africa, Githinji Gitahi (Wapili kulia) akikabidhi gari kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi


Dk. Mwinyi alibainisha kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mikakati ya kuzikabili changamoto zinazosababisha vifo vya mama wajawazito na watoto, hivyo kampeni hiyo ya AMREF itasaidia na kufanikisha kwa malengo.

Alibainisha kuwa hivi sasa kiwango cha vifo vya mama wajawazito na watoto kipo juu hapa Zanzibar, hivyo kampeni ya 'Uzazi ni Maisha' ya Amref Tanzania itasaidia kuliondosha tatizo hilo.


Alisema takwimu za mwaka 2017, zinaonesha vifo vya kina mama 134 kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka na vifo 28 vya watoto wachanga kati ya vizazi hai 1,000, ambapo husababishwa na changamoto za huduma duni za mama na mtoto katika hospitali na vituo vya afya zikiwemo uhaba wa wahudumu a tatizo la kukosekana kwa dawa.


Dkt. Mwinyi, alieleza matumaini yake kupitia kampeni hiyo, kwamba serikali itaongeza vifaa tiba kwa vituo vya afya 28, sawa na asilimia 40.5 ya vituo vote 69 vinavyotoa huduma za mama na mtoto Zanzibar.

Pia, alieleza jitihada za serikali kumarisha huduma za afya ya msingi kwa ajili ya uzazi salama, italeta mafanikio makubwa ya kulinda maisha ya mama na mtoto.

Akizungumza kwenye hafla hivo, Naibu Waziri wa Afya, Hassan Khamis Hafidh, alisema lengo la kuanzishwa kwa kampeni ya "Uzazi ni Maisha" ni kupunguza vifo vya mama wajawazito a watoto chini.
Naibu Waziri wa Afya, Hassan Khamis Hafidh

Alisema, katika kulikabili tatizo hilo kivitendo, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mikakati ikiwemo kuwachukulia hatua kali za kisheria na nidhamu watumishi wote wa sekta ya afya wanaokiuka sheria na taratibu za utumishi kutokana na uzembe kazini.

Aidha alisema serikali haitovumilia kauli chafu kutoka kwa watendaji wa sekta ya afya, utovu wa nidhamu unaosababisha athari maya kwa mama na watoto hasa wakati wa kujifungua.


Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Zlatan Milisic alisema “Tunashukuru kwa kupata fursa ya kuwa sehemu ya hafla hii iliyoandaliwa na Amref na wizara ya afya zanzibar, michango itokanayo na mpango huu wa Uzazi Ni Maisha Wogging wa kuchangisha fedha yatakwenda katika ununuzi wa vifaa tiba ili kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya mama na mtoto Zanzibar. Wakati maendeleo yamepatikana, bado kuna kazi kubwa ya kupunguza viwango vya vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.Umoja wa Mataifa bado una nia ya dhati ya kusaidia Tanzania na Zanzibar katika jambo hili muhimu.Kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko na kutoa huduma bora za afya na matunzo kwa akina mama na watoto wachanga." alisema
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Zlatan Milisic

Naye, Mkurugenzi mkaazi wa Shirika la Amref Health Afrika kwa upande wa Tanzania, Dk. Florence Temu, alisema lengo la kuanzishwa kampeni hiyo ya "Uzazi ni maisha ni kukusanya shilingi bilioni moja kwajili ya kununuliwa vifaa tiba vya hospitali a vito vya afya 69 vinavyotoa huduma za mama na mtoto, Zanzibar.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu

Alisema, wakiwa mwenye mwaka wa pili wa kampeni yao, Shirika la Amref Health Afrika tayari limefanikiwa kukusanya shilingi milioni 557 na wamepokea ahadi za shilingi milioni 883 ambayo itafikisha lengo la kampeni hiyo kufikia 2024.


Kampeni ya "Uzazi ni Maisha" ilianza mwaka jana na inatarajiwa kukamilika mwakani inatekelezwa kwa kaulimbiu isemayo" changia vifaa tiba kwa uzazi salama" ambayo imechangia kufikia malengo ya kuanzishwa kwake mwaka wa pili sasa wa utekelezaji wake.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Obedi S.Laiser alisema ushirika kati ya Amref na Absa ulikuwa na thamani kubwa na kiasi kilichochangwa na benki ni mwendelezo wa juhudi za benki hiyo katika kutimiza sera yake ya kurudisha kiasi cha faida Kwa jamii (CSR) kunakosukumwa na utayari wa kushirikiana na jamii ambako benki inatoa huduma ili kuimarisha sekta ya afya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Obedi S.Laiser


Matukio katika Picha
Mgeni Rasmi, RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akiongoza na kuambatana na viongozi wengine wa serikali na taasisi mbalimbali katika matembezi na mbio fupi za Uzazi ni Maisha Wogging 2023 Zanzibar, 26/08/2023
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Zlatan Milisic akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi  mara baada ya matembezi na mbio fupi za Uzazi Ni Maisha Wogging 2023 zilizofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki iliyopita kwa lengo la kuchangisha vifaatiba kwa uzazi salama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Obedi S.Laiser (Wapili kulia)ambayo benki ya Absa ndio wadhamini wakuu wa Matembezi na mbio fupi za Uzazi ni Maisha Wogging 2023, akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mgeni Rasmi, RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi

Afisa Mkuu Mtendaji wa Amref Health Africa, Githinji Gitahi (Wapili kulia) akikabidhi gari kwa : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Vifaa Tiba kutoka kwa wadau mbalimbali wakati akiongoza Matembezi na mbio fupi za Uzazi Ni Maisha Wogging 2023 yalioanzia viwanja vya Butros Kiembe Samaki na Kumalizikia Viwanja vya Maisara
Wananchi mbalimbali wakati wa hitimisho za Matembezi na mbio fupi za Uzazi ni Maisha Wogging katika viwanja vya Maisara, Zanzibar. Matembezi hayo yenye Kauli mbiu “Changia Vifaa Tiba kwa Uzazi Salama.
Picha ya pamoja kati ya Mgeni Rasmi, RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi na wadau mbalimbali waliochangia vifaa Tiba kwa Uzazi Salama katika programu ya Uzazi ni Maisha Wogging 2023 ikiwemo ( Mdhamini Mkuu Benki ya Absa; M & D Chemical & Surgical Ltd, Tanzania Ports Authority, NMB Bank, ITV/ Radio One, Swahili Sweatshop, Dalberg Tanzania, Siemens Healthcare LLC, benki ya CRDB, Strategis Insurance, NBC na kila mmoja aliyewezesha Programu ya Uzazi ni Maisha Wogging Marathon (Walk-Jog-Run) kwa mwaka 2023 kufanikiwa.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 28,2023



























































Share:

Sunday 27 August 2023

MATANO KUHUSU KLABU YA CELTA VIGO MIAKA 100!!



Moja ya klabu za kihistoria kabisa katika soka la Hispania ni RC Celta, timu iliyoko katika mji wa Vigo huko Galicia. Katika msimu wa 2023/24, klabu ya Galician itasherehekea miaka 100 tangu kuanzishwa kwake, na hapa kuna mambo matano ambayo huenda usiyajue kuhusu timu hiyo ambayo hupewa odds kubwa na Meridianbet.

 

Kwa nini RC Celta huvaa rangi ya bluu hadi uhamisho wao wa uwanja kwa wachezaji waliovalia nembo hiyo katika miaka yote hii ya historia.

 

Uhamisho ulioipeleka timu Balaídos

 

RC Celta ilianzishwa mwaka 1923, baada ya kuungana kwa klabu kubwa mbili za mji huo, Real Fortuna na Vigo Sporting, na hadi mwaka 1928, RC Celta ilicheza mechi za nyumbani katika vituo vya michezo huko Coia.

 

Hata hivyo, ujenzi wa njia mpya ya reli ya umeme ulilazimisha klabu kuhamia uwanja mpya. Ilipofika wakati huo, kundi la wanachama walijipatia lengo la kutoa timu uwanja unaofanana na umuhimu ambao klabu ilikuwa inalenga, hivyo walinunua ardhi ambayo Balaídos ingejengwa baadaye.

 

Kwa sasa ni moja ya viwanja vya LALIGA EA SPORTS vya zamani zaidi, hufahamika siku hizi kama Abanca-Balaídos kwa sababu za udhamini. Kusanya maokoto yako ukibeti na Meridianbet kwa odds kubwa, michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni ni sehemu pekee ya kuchota mikwanja.

 

Sababu ya Jezi za rangi ya bluu

 

RC Celta haikuwa ikitumia rangi ya bluu ya anga, rangi ambayo sasa inatambulisha timu ya Vigo. Walipoanza, baada ya kuungana kwa Real Fortuna na Vigo Sporting, sare ya kwanza ya klabu ilikuwa nyekundu yenye mamlaka ya ushindi uwanjani, nan je ya uwanja kama Meridianbet.

 

Waliamua kuvaa rangi sawa na timu ya taifa ya Hispania, lakini mkurugenzi Juan Baliño Ledo, mmoja wa watu muhimu sana katika historia ya klabu, alipendekeza timu ingeweza kuwakilisha rangi za bendera ya Galicia. Hii ilisababisha klabu kubadilisha muundo na kuanza kuvaa bluu mwepesi ambayo tunayofahamu na kutambua RC Celta leo.

 

Magwiji wa klabu.

 

Katika historia ya RC Celta, kuna watu wengi muhimu, kama vile Hugo Mallo, Aleksandr Mostovoi, Valeri Karpin, Gustavo López au Javier Maté Berzal. Lakini, kuna mchezaji mmoja tu aliye na rekodi ya idadi kubwa ya mechi akiwa na jezi hiyo nae ni Manolo, beki kutoka Pontevedra ambaye aliicheza klabu hiyo kuanzia 1966/67 hadi 1981/82, akidumu na klabu katika daraja la kwanza, daraja la pili, na Segunda B, akiichezea mechi 533.

 

 

 

Pia akiwa na mechi 457 alikuwa ni mfungaji bora wa muda wote wa klabu, Iago Aspas. Mchezaji kutoka Moaña amefunga magoli 195, maana yake yuko mbele ya Mbosnia Vladimir Gudelj kwenye orodha ya wafungaji.

 

Pichichi mmoja na tuzo tatu za Zamora

 

Ingawa RC Celta haijawahi kushinda ubingwa wa Kihispania, wachezaji wao wamekuwa kwenye orodha ya heshima za msimu mara kadhaa, taji moja na tuzo tatu za Zamora kwenye jina la klabu. Katika msimu wa 1947/48, Pahíño alikuwa mfungaji bora wa mashindano na magoli 23 katika mechi 22, akiiongoza timu yake kufikia nafasi ya nne kihistoria kwenye msimamo.

 

Kuhusu ulinzi na Tuzo ya Zamora, kumekuwa na makipa watatu wa RC Celta ambao wamekuwa walinzi bora wa msimu na rekodi nzuri. Santi Cañizares alifanikiwa hilo katika msimu wa 1992/93, Pablo Cavallero alifanya hivyo katika msimu wa 2002/03, na José Manuel Pinto pia alishinda tuzo hii katika msimu wa 2005/06. Shinda mtonyo ukicheza kasino ya mtandaoni ya Meridianbet au ukibashiri soka kwa dau dogo la Tsh 250/= tu Piga *149*10#

 

RC Celta walikuwa mabingwa barani Ulaya

 

Ingawa kabati la tuzo la klabu linajivunia sanaa za kikanda kwa kiasi kikubwa, kwani hawajawahi kushinda LALIGA EA SPORTS au Copa del Rey, RC Celta wana tuzo moja ya Ulaya katika historia yao. Timu ya Vigo ilishinda Kombe la Intertoto mwaka 2000, mashindano yaliyowapa nafasi katika UEFA Cup.

 

Celta Vigo Iliishinda dhidi ya timu ya Masedonia, Pelister, kabla ya kuishinda timu ya Uingereza Aston Villa katika nusu fainali na timu ya Urusi Zenit St Petersburg katika fainali, na Benni McCarthy kutoka Afrika Kusini akawa mfungaji bora.

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.





Share:

MCHENGERWA AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI RUFIJI BENKI YA CRDB IKIZINDUA TAWI LAKE IKWIRIRI


Rufiji. Tarehe 25 Agosti 2023: Baada ya Benki ya CRDB kufungua tawi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa amewakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya Tanzania kuja kuwekeza kwenye fursa tele zilizopo wilayani Rufiji.


Mchengerwa amesema Rufiji ambayo ni kati ya wilaya kongwe nchini inazidi kukua kila siku kwa kuimarisha miundombinu ya huduma za jamii kwani tayari serikali imejenga zahanati 24, shule za msingi 45 na sekondari 9 ndani ya vijiji 38 ilivyonavyo zinazotoa nafasi kwa wananchi kutibiwa na watoto kupata elimu itakayowasaidia kujikomboa katika maisha yao hivyo ujio wa Benki ya CRDB inawaongezea fursa za kujiimarisha kiuchumi.
“Uamuzi wa serikali kujenga Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) umeleta neema nyingi zitakazowanufaisha wananchi na halmashauri hii yenye utajiri mkubwa wa ardhi, maliasili na utamaduni. Ukiacha bwawa hili, kuna hekta 300,000 limetengwa kwa ajili ya kilimo kitakachoendeshwa kwa mfumo wa umwagiliaji. Ni wakati sahihi sasa kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya Tanzania kuja kuwekeza wilayani Rufiji kwani kuna usalama wa kutosha kuanzia namna ya kuhifadhi fedha zao mpaka kutekeleza miradi watakayoianzisha,” amesema Mchengerwa.


Ili kutoachwa nyuma, Mchengerwa ambaye ni mbunge wa Rufiji tangu mwaka 2015 amewahimiza wananchi wenzake kulitumia tawi hilo la Benki ya CRDB hivyo kunufaika na huduma zinazotolewa na kujihakikishia usalama wa fedha, kukopa kwa ajili ya miradi na mipango binafsi hata kufanya uwekezaji.
“Rufiji ni kati ya wilaya kongwe nchini lakini kwa muda mrefu haikuwa imefunguka ila leo hii Benki ya CRDB imeonyesha njia. Ili kuwa wilaya ya sita wakati wa mkoloni na ya 13 baada ya uhuru. Mimi ni mteja wa siku nyingi wa Benki ya CRDB hivyo nawasihi wananchi wenzangu nanyi mjiunge kutumia huduma za benki hii.


Benki hii ya CRDB inayo huduma ya imbeju ambayo ni programu maalumu ya kuwawezesha vijana na wanawake. Makundi haya muhimu kwa jamii yetu yapo wilayani Rufiji na kwa kufika kwenye tawi hili ndivyo yataweza kunufaika na programu hii inayotoa mtaji wezeshi kwao. Kwa kuwa Rufiji ina kila kitu kinachohitajika kwa mjasiriamali kujikwamua kiuchumi, mtaji huu unaotolewa na Benki ya CRDB na mikopo ya aina tofauti iliyopo ni msingi mkubwa wa kuwakomboa wananchi kiuchumi,” amesema Mchengerwa.


Mchengerwa amezitaja fursa nyingine zilizopo wilayani humo kuwa ni pamoja na kilomita za mraba 6,500 ambazo ni hifadhi na misitu zinazofaa kwa utalii. Nyingine amesema ni uvuvi, huduma za kijamii na ukarimu zikiwamo hoteli. Kwenye kilimo, amesema ufuta, korosho na mazao mengine mengi ya biashara yanastawi vyema wilayani humo na hivi karibuni kiwanda kikubwa cha sukari kitajengwa wilayani humu.
Kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema wamejipanga vyema kukidhi mahitaji ya mtaji kwa ajili ya wateja wao wakiwamo wawekezaji wanaohitaji shilingi hata fedha za kigeni.

“Jana benki yetu imepata kibali za kuorodhesha hatifungani ya kijani yenye thamani ya dola milioni 300 za Marekani ambazo ni sawa na shilingi bilioni 780. Fedha zitakazokusanywa kutokana na mauzo ya hatifungani hii zitaelekezwa kwenye miradi inayolinda na kujali mazingira. Rufiji ni kati ya maeneo yanayostahili kuzitumia hivyo nawakaribisha mje tuwahudumie,” amesema Raballa.
Afisa huyo amesema kupitia tawi hilo, wananchi wa wilaya nzima ya Rufiji wanafunguliwa milango kunufaika na mtandao mpana wa matawi 260 yanayoifanya Benki ya CRDB kuwa na idadi kubwa zaidi ikilinganishwa na benki nyingine nchini.


Licha ya huduma matawini, kupitia mawakala wa benki, mashine za kutolea fedha na zile zinazopokea malipo ya kadi au kupitia simu ya mkononi, amesema Benki ya CRDB inatoa ushauri na elimu kuhusu masuala ya fedha, uwekezaji na namna bora ya uendeshaji wa biashara.
“Watu wengi hudhani benki ni kuweka, kutoa pesa au kuomba mkopo tu lakini ukweli wasioujua ni kuwa tunatoa elimu na ushauri na tumekuwa tukifanya hivyo kwa wateja wetu ingawa wengi hawaitumii huduma hii. Hivyo niwakaribishe katika Benki yenu ya CRDB kupata ushauri.


Na kupitia taasisi yetu ya CRDB Bank Foundation, tunafanya uwezeshaji kwa wanawake na vijana kwa kuwapa mitaji wezeshi kwa masharti nafuu ili kuwapa nafasi ya kuimarisha kipato chao na kushiriki kujenga uchumi wa taifa,” amesema Raballa.


Benki ya CRDB ndio taasisi pekee ya kizalendo yenye matawi nje ya mipaka ya Tanzania ikitoa huduma nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger