Monday 28 August 2023

VIJANA WAFURAHIA PROGRAMU YA JENGA KESHO ILIYO BORA ‘BBT’ INAVYOLETA MAPINDUZI KATIKA KILIMO


Vijana 820 wa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) inayotekelezwa na Wizara ya Kilimo, ambao wamehitimu mafunzo yao katika vituo atamizi mbalimbali hapa nchini (Vyuo vya Kilimo), wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tamzania kwa mpango huo mzuri wa kuwapa vijana ajira kupitia kilimo.


Wakizungumza na mwandishi wetu baada ya kuhitimu mafunzo ya kilimo kwenye vituo atamizi vijana hao wameeleza kufurahishwa na kile ambacho Programu ya BBT imelenga.

Janeth Fredrick Moshi kutoka Mkoa wa Manyara aliyekuwa kituo cha KATC Moshi anasema “Kwa kweli nimejifunza mengi, ila hili la kuanzia sokoni kisha nirudi shambani kuzalisha, nimetoka nalo, kwani hapo awali nilikuwa nazalisha chochote na mwisho wa siku sipati soko. Lakini kwa sasa lazima nifanye utafiti kwanza wa hali ya soko ndipo nizalishe, na hicho ndicho Kilimo Biashara”.


Aidha, ameiomba serikali iendelee kutoa mafunzo kwa vijana wengine, maana huo ni ukombozi wao.

Ameshukuru kwani amefundishwa kilimo bora kwa sababu alizoea kilimo cha mazoea hivyo ameahidi kuwafundisha vijana wenzake.

Revina Dastan kutoka Mkoa wa Mwanza anasema “Nimejifunza mazuri maana nimelima mwenyewe na nimekabiliana na changamoto za shambani, hivyo kuna kitu nimejifunza sana. Namshukuru Rais wetu na namshukuru sana Waziri wetu wa Kilimo kwa fursa hii. Vijana twende kulima, tutumie mitandao kwa faida. Tusipoteze muda, tuache kukaa vijiweni, Kilimo kina pesa”.

Naye Papaye Njiday kutoka Mkoa wa Manyara aliyekuwa kituo atamizi cha Horti Tengeru ameomba programu iwe endelevu, iwaguse vijana wengi. Hili likifanikiwa kufikia wengi kutakuwa na mapinduzi ya kilimo hapa nchini na nchi zingine zitalishwa chakula kutoka Tanzania.

“Hii ni fursa ya pekee, yaani kama ningekuwa na elimu hii tangu awali ningekuwa mbali. Elimu hii ya kilimo ipelekwe shuleni na vyuoni pia”,amesema.

Amewataka vijana wachangamkie kilimo na kwamba ataajiri vijana na kutoa elimu kwa wale ambao hawakupata nafasi hiyo.

Aidha, ameishukuru serikali kwa mpango huo.

Daud S. Laizer kutoka Arusha, Sada Omary toka Dodoma, Rabia Mtega Alkariti na Naomi Lau toka Dar es Salaam, Bishwa Ngonga Alphonce toka Mkoa wa Kigoma, Neema Samsoni Katumba kutoka Mkoa wa Geita na Phares Chacha kutoka Mkoa wa Katavi, kwa niaba ya wenzao ambao hawakupata nafasi katika mahojiano hayo, Kwa nyakati tofauti walipohojiwa, wameonesha kufurahishwa na program hii ya BBT.
Wamempongeza Mbeba Maono hayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Mtekeleza Maono ya BBT, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, na wote wanaohusika katika programu hiyo.

Wanashauri vijana kuangalia fursa iliyoko katika kilimo kwani kinalipa, waache mazoea ya kukipa kilimo nafasi ya mwisho, wakipe nafasi ya kwanza, maana ni uti wa mgongo kuna chakula, malighafi na ajira katika kilimo.

Wamesema Kilimo ni fursa, kinalimwa shambani, siyo kwenye mitandao, watoke ardhi ipo, watoke wakalime kwani wasipotoka hawataona mashamba na kwamba kuna maeneo yana ardhi ya kutosha, lakini vijana bado wanalalamikia ajira.

“Tutoke vijana, fedha ziko kwenye kilimo”,wamesema.

Vijana wa kike wao pia wameshukuru kukumbukwa katika programu. hiyo.

“Mafunzo tuliyopata ya kilimo yapelekwe shuleni na vyuo vyote. Vijana wenye elimu ya darasa la saba na wasio na elimu nao pia wakumbukwe, hususan wale ambao tayari wamejikita kwenye kilimo. Watapata kitu kama sisi tulivyopata. Kule vituoni, mafunzo yaliyotolewa asilimia 80 ni vitendo na asilimia 20 ndiyo nadharia, hivyo wataweza”,wameeleza.

Wamesema watakuwa mabalozi kupeleka kile walichopata kwa wakulima wengine.

Aidha wameshukuru kwa mpango huo uliokumbuka makundi haya ya vijana, wanawake na walemavu huku wakisema kazi iendelee kwa kufikia lengo la AGENDA 10/30.
Share:

KAMA UTANI NIMEMPATA MUME TAJIRI INGAWA NILIKUWA MASKINI SANA!

Jina langu ni Koome, maisha yangu hayakuwa rahisi, wazazi wangu wote walifariki nilipokuwa msichana mdogo na nilienda kuishi na shangazi yangu, shangaza pia hakuwa tajiri na hakuweza hata kunipeleka chuoni baada ya shule ya upili.

Kwa hivyo nilianza kwenda kwenye saluni kupata mafunzo na pia kupata ujuzi ambao utanisaidia kupata fedha, miezi sita baadaye, nilimaliza na mafunzo lakini sikuweza kupata fedha nyingi za kuweza kunisaidia kujikwamua kimaisha.

Ilifika hatua shangazi yangu akanitaka niondoke nyumbani kwake kwa kuwa nilikuwa mtu mzima, kuishi peke yangu ilikuwa ngumu sana sembuse nilikuwa sina kazi.

Niliamua kwenda kijijini na kukaa huko, baada ya miezi miwili nikiwa bado kijijini na Bibi yangu, kulikuwa na shughuli ya mahali iliyofanyika katika nyumba ya jirani ambapo binti wa nyumba hiyo alikuwa amepata mume mzuri na tajiri wa kumuoa.

Wakati tu nilipomuona mtu huyo akiingia, nilijua mara moja kuwa alikuwa tajiri kweli, magari yalijaza kiwanja hicho na alilipiwa kiasi kikubwa sana cha mahari. Baada ya sherehe, nilimuuliza ni vipi alipa bahati kupata mtu tajiri kama huyo na kweli akafunguka juu ya siri hiyo.

 Alisema alikuwa akiishi maisha ya kusikitisha lakini alimtembelea African Doctors ambaye alitumia dawa zake kumuunganisha na tajiri huyo.

Nilimuomba anipe namba ya African Doctors  ili nami nipate tajiri mzuri wa kunioa, alinipa mawasiliano hayo na mara moja nikampigia na kuzungumza naye, siku iliyofuata nilienda ofisini kwake na kuzungumza naye, aliweza kunifanyia tiba zake na kuniahidi nitafanikiwa.

Siku mbili baadaye nilipokuwa kwenye ukurasa wangu wa Facebook, mwanaume kwa jina Muli, alinizimia na kuanza kunitongoza, tuliweza kukuta na uhusiano wetu ukaanza mara moja, kwa muda wote amekuwa akihudumia chochote kile ninachotaka.

Sasa ni mwaka wa pili tangu tumefunga ndoa na tunaisha vizuri tu, maisha ni mazuri na yenye furaha na tayari tumejaliwa kupata mtoto mmoja.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com

Mwisho.


Share:

RAIS DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AONGOZA PROGRAMU YA UZAZI NI MAISHA WOGGING YENYE LENGO LA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akiongoza Matembezi na mbio fupi za Uzazi Ni Maisha Wogging 2023 yalioanzia viwanja vya Butros Kiembe Samaki na Kumalizikia Viwanja vya Maisara Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezipongeza jitihada zinazochukuliwa na wadau wa maendeleo, wahisani na mashirika kwa juhudi wanazozichukua katika kuiunga mkono serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo jana katika viwanja vya Maiasra vilivyopo Zanzibar alipokuwa akizungumza kwenye kampeni ya ' Uzazi ni Maisha Wogging Marathon (Walk-Jog-Run) kwa mwaka 2023 “ iliyoandaliwa kwa ushirikiano baina ya wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Kimataifa la Amref Health Afrika Tanzania chini ya udhamini wa benki ya Absa.

Alisema wadau wa maendeleo na mashirika yana mchango mkubwa katika kusaidia maendeleo ya jamii na kulipongeza shirika la Amref Tanzania kwa kuanzisha kampeni ya 'Uzazi ni Maisha Wogging yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akilishukuru shirika la Amref Health Africa Tanzania pamoja na Mdhamini wa Matembezi na mbio fupi hizo benki ya Absa na wadau wake wote Mara baada ya kumaliza kampeni ya Uzazi ni Maisha wogging Zanzibar.


"Napenda niwashukuru Amref Health Africa kwa kutoa msaada wa gari maalum ambayo itasaidia kusafirisha wataalamu, kusafirisha sampuli, kutoa huduma za upimaji na ushauri nasaha kwa wananchi katika vituo vya afya hapa Zanzibar", alisema.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Amref Health Africa, Githinji Gitahi (Wapili kulia) akikabidhi gari kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi


Dk. Mwinyi alibainisha kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mikakati ya kuzikabili changamoto zinazosababisha vifo vya mama wajawazito na watoto, hivyo kampeni hiyo ya AMREF itasaidia na kufanikisha kwa malengo.

Alibainisha kuwa hivi sasa kiwango cha vifo vya mama wajawazito na watoto kipo juu hapa Zanzibar, hivyo kampeni ya 'Uzazi ni Maisha' ya Amref Tanzania itasaidia kuliondosha tatizo hilo.


Alisema takwimu za mwaka 2017, zinaonesha vifo vya kina mama 134 kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka na vifo 28 vya watoto wachanga kati ya vizazi hai 1,000, ambapo husababishwa na changamoto za huduma duni za mama na mtoto katika hospitali na vituo vya afya zikiwemo uhaba wa wahudumu a tatizo la kukosekana kwa dawa.


Dkt. Mwinyi, alieleza matumaini yake kupitia kampeni hiyo, kwamba serikali itaongeza vifaa tiba kwa vituo vya afya 28, sawa na asilimia 40.5 ya vituo vote 69 vinavyotoa huduma za mama na mtoto Zanzibar.

Pia, alieleza jitihada za serikali kumarisha huduma za afya ya msingi kwa ajili ya uzazi salama, italeta mafanikio makubwa ya kulinda maisha ya mama na mtoto.

Akizungumza kwenye hafla hivo, Naibu Waziri wa Afya, Hassan Khamis Hafidh, alisema lengo la kuanzishwa kwa kampeni ya "Uzazi ni Maisha" ni kupunguza vifo vya mama wajawazito a watoto chini.
Naibu Waziri wa Afya, Hassan Khamis Hafidh

Alisema, katika kulikabili tatizo hilo kivitendo, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mikakati ikiwemo kuwachukulia hatua kali za kisheria na nidhamu watumishi wote wa sekta ya afya wanaokiuka sheria na taratibu za utumishi kutokana na uzembe kazini.

Aidha alisema serikali haitovumilia kauli chafu kutoka kwa watendaji wa sekta ya afya, utovu wa nidhamu unaosababisha athari maya kwa mama na watoto hasa wakati wa kujifungua.


Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Zlatan Milisic alisema “Tunashukuru kwa kupata fursa ya kuwa sehemu ya hafla hii iliyoandaliwa na Amref na wizara ya afya zanzibar, michango itokanayo na mpango huu wa Uzazi Ni Maisha Wogging wa kuchangisha fedha yatakwenda katika ununuzi wa vifaa tiba ili kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya mama na mtoto Zanzibar. Wakati maendeleo yamepatikana, bado kuna kazi kubwa ya kupunguza viwango vya vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.Umoja wa Mataifa bado una nia ya dhati ya kusaidia Tanzania na Zanzibar katika jambo hili muhimu.Kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko na kutoa huduma bora za afya na matunzo kwa akina mama na watoto wachanga." alisema
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Zlatan Milisic

Naye, Mkurugenzi mkaazi wa Shirika la Amref Health Afrika kwa upande wa Tanzania, Dk. Florence Temu, alisema lengo la kuanzishwa kampeni hiyo ya "Uzazi ni maisha ni kukusanya shilingi bilioni moja kwajili ya kununuliwa vifaa tiba vya hospitali a vito vya afya 69 vinavyotoa huduma za mama na mtoto, Zanzibar.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu

Alisema, wakiwa mwenye mwaka wa pili wa kampeni yao, Shirika la Amref Health Afrika tayari limefanikiwa kukusanya shilingi milioni 557 na wamepokea ahadi za shilingi milioni 883 ambayo itafikisha lengo la kampeni hiyo kufikia 2024.


Kampeni ya "Uzazi ni Maisha" ilianza mwaka jana na inatarajiwa kukamilika mwakani inatekelezwa kwa kaulimbiu isemayo" changia vifaa tiba kwa uzazi salama" ambayo imechangia kufikia malengo ya kuanzishwa kwake mwaka wa pili sasa wa utekelezaji wake.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Obedi S.Laiser alisema ushirika kati ya Amref na Absa ulikuwa na thamani kubwa na kiasi kilichochangwa na benki ni mwendelezo wa juhudi za benki hiyo katika kutimiza sera yake ya kurudisha kiasi cha faida Kwa jamii (CSR) kunakosukumwa na utayari wa kushirikiana na jamii ambako benki inatoa huduma ili kuimarisha sekta ya afya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Obedi S.Laiser


Matukio katika Picha
Mgeni Rasmi, RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akiongoza na kuambatana na viongozi wengine wa serikali na taasisi mbalimbali katika matembezi na mbio fupi za Uzazi ni Maisha Wogging 2023 Zanzibar, 26/08/2023
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Zlatan Milisic akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi  mara baada ya matembezi na mbio fupi za Uzazi Ni Maisha Wogging 2023 zilizofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki iliyopita kwa lengo la kuchangisha vifaatiba kwa uzazi salama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Obedi S.Laiser (Wapili kulia)ambayo benki ya Absa ndio wadhamini wakuu wa Matembezi na mbio fupi za Uzazi ni Maisha Wogging 2023, akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mgeni Rasmi, RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi

Afisa Mkuu Mtendaji wa Amref Health Africa, Githinji Gitahi (Wapili kulia) akikabidhi gari kwa : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Vifaa Tiba kutoka kwa wadau mbalimbali wakati akiongoza Matembezi na mbio fupi za Uzazi Ni Maisha Wogging 2023 yalioanzia viwanja vya Butros Kiembe Samaki na Kumalizikia Viwanja vya Maisara
Wananchi mbalimbali wakati wa hitimisho za Matembezi na mbio fupi za Uzazi ni Maisha Wogging katika viwanja vya Maisara, Zanzibar. Matembezi hayo yenye Kauli mbiu “Changia Vifaa Tiba kwa Uzazi Salama.
Picha ya pamoja kati ya Mgeni Rasmi, RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi na wadau mbalimbali waliochangia vifaa Tiba kwa Uzazi Salama katika programu ya Uzazi ni Maisha Wogging 2023 ikiwemo ( Mdhamini Mkuu Benki ya Absa; M & D Chemical & Surgical Ltd, Tanzania Ports Authority, NMB Bank, ITV/ Radio One, Swahili Sweatshop, Dalberg Tanzania, Siemens Healthcare LLC, benki ya CRDB, Strategis Insurance, NBC na kila mmoja aliyewezesha Programu ya Uzazi ni Maisha Wogging Marathon (Walk-Jog-Run) kwa mwaka 2023 kufanikiwa.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 28,2023



























































Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger