Friday 2 June 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 2,2023



SHARE



 

Share:

UONGOZI BANDARI ZA ZIWA VICTORIA WAFURAHIA MAFANIKIO,WAPONGEZA MABORESHO YALIYOFANYWA NA SERIKALI


Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Ferdinand Nyathi akiongea na waandishi wa habari akielezea utendaji kazi wa maboresho ya bandari hizo

***************

Na Mwandishi Wetu, Mwanza


MENEJA wa Bandari za Ziwa Victoria Ferdinand Nyathi ameelezea mafanikio makubwa ambayo yamepatikana kwenye bandari hizo ikiwemo kuvuka lengo la kuhudumia shehena kwani mpaka Mei mwaka huu wameshahudumia jumla ya tani 246, 0000 ambazo ni sawa na asilimia 101.1.

Ameongeza kwa muda uliobakia upo uwezekana wa kuongezeka kiwango cha kuhudumia shehena lakini mafanikio mengine ni kuongezeka kwa mapato pamoja na meli zinazoingia kwenye bandari za Ziwa Victoria.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Ferdinand Nyathi amefafanua mwaka wa fedha 2022/2023 bandari hizo ziliwekewa lengo la kuhudumia shehena tani 228,000 ambapo hadi kufikia Mei, mwaka huu jumla ya tani 246,000 zimeshahudumiwa.

"Bandari zetu zimefanya vizuri katika maeneo yote ikiwemo mapato, kuhudumia shehena na idadi ya meli zinazoingia katika bandari hizo, ", amesema na kuongeza kuhusu miradi yote ya maboresho katika bandari za Ziwa Victoria imelenga kuboresha maeneo yote ya bandari hizo.

Amesema kuwa maeneo yaliyoboreshwa ni kuongeza kina cha maji, maegesho ya meli, kuhudumia meli kubwa, miundombinu ya reli zinazoingia bandarini, majengo ya abiria, maeneo ya kuhifadhia mizigo, mifumo ya TEHAMA pamoja na mifumo ya ulinzi na usalama.

Pamoja na hayo ametoa rai kwa wafanyabiashara kuendelea kutumia bandari za Ziwa Victoria kwani huduma zao ni nzuri, zimeboreshwa na wamekuwa wakitoa kipaumbele katika kuwasikiliza wafanyabiashara.

" Pia bandari zetu hivi sasa zinahudumia shehena ya mizigo inayokwenda bandari ya Kisumu jambo ambalo halikuwepo katika miaka miwili iliyopita.Tulikuwa hatupati mizigo inayokwenda bandari ya Kisumu,ila kuanzia mwaka huu wa fedha tumeanza kupata mizigo ya kwenda katika bandari hiyo.”

Amefafanua mizigo inayotoka na kwenda nchi jirani inachangia asilimia 50 ya mizigo yote inayohudumiwa katika bandari zetu za ziwa Victoria.

Kuhusu miradi inayotekelezwa kwa sasa, ametumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali kwa kutenga fedha kuboresha bandari za Ziwa Victoria huku akisisitiza tayari kuna miradi imeshaanza kutekelezwa katika bandari za Bukoba na Kemondo ikiwa thamani ya takribani sh bilioni 40”

Wakati huo huo mmoja wa Wakala wa Forodha Peter Zakayo amesema, wanapata ushirikiano wa kutosha kutoka viongozi na watumishi wa bandari za ziwa Victoria huku akieleza pia huduma wanazopatiwa ni nzuri kwani hata mizigo hutolewa kwa wakati.
Mwonekano wa bandari za Mwanza Kusini na Mwanza Kaskazini ambazo ni miongoni mwa bandari za ziwa Victoria ikiwa ndio bandari kubwa zaidi.

 
Mhandisi Meli ambaye pia ni Kaimu Mhandisi Mkuu wa kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Mhandisi Abel Gwanafyo akiongea na waandishi wa habari kuhusu ujio wa meli kubwa itakayofanya kazi katika bandari za ziwa Victoria kufuatia miradi maboresho ya kuendeleza bandari hizo



Share:

Thursday 1 June 2023

Wimbo Mpya : NYASANI - MILELE



Msanii Nyasani anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa Milele... Sikiliza hapa
Share:

SERIKALI KUPOKEA NDEGE YA KUSAFIRISHIA MIZIGO BOEING 767-300

Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Juni Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 -300 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini Juni 3,2023

**************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI inatarajia kupokea ndege ya kwanza ya kusafirisha mizigo aina ya Boeing 767 -300 mnamo tarehe tatu Juni itakayokwenda kutatua changamoto za usafirishaji wa mizigo kwa wafanyabiashara nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Juni 1,2023 Jijini Dar es Salaam, Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kukosekana kwa ndege ya mizigo toka nchini kwenda nchi za nje kumechangia ucheleweshwaji wa bidhaa pamoja na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji.

"Zaidi ya Tani elfu 24 za bidhaa ya samaki, mbogamboga na maua toka nchini zimekuwa zikisafirishwa kupitia mashirika mengine hivyo ujio wa ndege hii utatoa fursa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kutekeleza majukumu yao kwa urahisi". Amesema Prof.Mbarawa

Aidha amesema tukio hilo la kupokea ndege litafanyika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi ambaye ataongoza kupokea ndege hiyo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Nae Afisa uhusiano wa Shirika la Ndege Tanzania Bi.Sarah Ruben amewahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji nchini kuwa ndege hiyo itakuwa na ratiba maalum itakayotoa fursa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kuweza kuitumia. Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Juni Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 -300 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini Juni 3,2023
Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari leo Juni Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 -300 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini Juni 3,2023
Share:

HOSPITALI YA BUGANDO YAPOKEA VIFAA TIBA KUTOKA SHIRIKA LA AMERICARES

Hospitali ya Rufaa Kanda Bugando jijini Mwanza imepokea vifaa tiba vya upasuaji wa ugonjwa wa fistula ya uzazi kutoka shirika la Americares, vyenye thamani ya shilingi milioni 234.2 vitakavyosaidia utoaji huduma ya matibabu ya ugonjwa huo.

Akizungumza Juni 01, 2023 kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amesema vitasaidia kutoa huduma ya matibabu kwa akina mama wanaougua fistula ya uzazi na hivyo kuzuia vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.

Makilagi ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla amesema suala la kuboresha huduma za afya ni kipaumbele cha Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan lakini pia ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/25.

“Nitoe rai kwa uongozi wa Hospitali ya Bugando kuhakikisha vifaa hivi vinatunzwa vyema na kufanya kazi iliyokusudiwa ya kuokoa maisha ya mama na mtoto” amesema Makilagi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kanda Bugando, Dkt. Fabias Massaga amesema zaidi ya wanawake 300 wanaougua fistula kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, wamekuwa wakitibiwa katika hospitali hiyo ambapo kwa mwaka 2022 waliopata tiba walikuwa wanawake 373 na kati yao, 207 walifanyiwa upasuaji huku 166 wakipata tiba ya viungo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi Shirika la Americares, Nguke Mwakatunde amesema takribani wanawake elfu tatu huugua fistula kila mwaka hapa nchini ambapo wanaofika katika matibabu ni takribani wanawake elfu mbili huku wanawake elfu moja wakikosa huduma kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa elimu ya kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya.

“Vifaa hivi vitasaidia kuboresha huduma za upasuaji wa fistula ya uzazi hapa Bugando, lakini pia shirika la Americares kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya litaendelea kushiriki juhudi mbalimbali za kutokomeza fistula hadi kufikia mwaka 2030” amesema Mwakatunde huku akishauri Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kusogeza huduma za fistula karibu na wananchi hadi ngazi za hospitali za rufaa za mikoa.

Nao baadhi ya mashujaa wa fistula wanaopata matibabu katika hospitali ya Bugando akiwemo Pendo Dodo kutoka mkoani Mara na Christina kutoka mkoani Mwanza wamelishukuru shirika la Americares kwa msaada wa vifaa hivyo na kueleza kuwa vitasaidia kuboresha huduma kwa wanawake wanaougua ugonjwa huo.

Wamesema ugonjwa huo unaosababishwa na uchungungu pingamizi wakati wa kujifungua unasababisha changamoto mbalimbali kwa wanawake ikiwemo unyanyapaa na hivyo kutumia fursa hiyo kuwasihi wanajamii kuacha tabia hiyo na badala yake kuwasaidia wagonjwa kufika mapema kwenye matibabu kwani fistula inatibika.

Kwa Kanda ya Ziwa, mikoa ya Shinyanga na Geita imetajwa kuwa na wagonjwa wengi wa fistula ambapo wataalamu kutoka hospitali ya Kanda Bugando kupitia huduma ya tiba mkoba (Outrich Program) wamekuwa wakifika katika mikoa hiyo ili kuwajengea uwezo watoa huduma za afya ili kuwasaidia akina mama wakati wa kujifungua na kuwaepusha na hatari ya kupata ugonjwa huo.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi (katikati) akikata upete kuashiria uzinduzi na makabidhiano ya vifaa tiba vya upasuaji wa fistula ya uzazi katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando jijini Mwanza ambapo vimetolewa na shirika la Americares.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo.
Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dkt. Fabian Massaga akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Americares akieleza namna shirika hilo limekuwa likishirikiana na hospitali ya Bugando kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo za fistula.
Shujaa wa fistula anayepata matibabu hospitali ya Bugando, Pendo Dodo (kushoto) kutoka mkoani Mara akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewahimiza akina mama wajawazito kuwahi katika vituo vya afya wakati wa kujifungua ili kupata msaada wa haraka wanapokumbwa na uchungu pingazi hatua itakayosaidia kukabiliana na ugonjwa wa fistula.
Wadau wa afya wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi ya Hospitali ya Bugando na shirika la Americares.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi (katikati) waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa hospitali ya Bugando na shirika la Americares.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi (katikati) waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa hospitali ya Bugando na shirika la Americares.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi (katikati) waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa hospitali ya Bugando.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi (katikati) waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Bugando, Americares na mashujaa wa fistula.
SOMA PIA>>> Habari zaidi hapa
Share:

WATU 15 WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA KUNYWA UJI



Watu 15 wa familia moja wameaga dunia nchini Namibia baada ya kunywa uji ulioharibika.

Hili ni miongoni mwa matukio mabaya zaidi nchini humo ya maafa yanayotokana na chakula kibovu.


Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa familia hiyo ambayo ilikuwa imepigwa na njaa kupitiliza ilikunywa uji huo kutoka kwa mabaki ya nafaka ya kutengeneza pombe. 

Polisi wanasema kuwa wanatoka katika familia ya watu 21 katika kijiji kimoja eneo la Kavango Mashariki linalopatikana Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

 Kwa mujibu wa msemaji wa polisi Kauna Shikwambi, watu hao 15 waliofariki walianza kuugua baada ya kula chajio mnamo Jumamosi na kukimbizwa hospitalini.

"Kufikia sasa hii ndio idadi kubwa zaidi ya vifo kuwa kutokea kwa sababu ya kula chakula chenye sumu au kilichoharibika," Shikwambi amenukuliwa na AFP. 

Shikwambi anasema kuwa Jumatano, watu 15 walikuwa wamefariki na kuongeza kuwa uchunguzi umeanza huku majibu ya upasuaji na vipimo vya maabara vikisubiriwa.
Share:

MUME WANGU KAMEGA TUNDA LA HOUSE GIRL NA KUNIACHA

Jina langu naitwa Farida mkazi wa mkoa wa Katavi, umri wangu ni miaka 38, nipo kwenye maisha ya ndoa miaka 10 sasa na mume wangu yazidi, tulifunga ndoa ya kimila ambayo ilihudhuriwa na wazazi wa pande zote mbili.


Baada ya kuolewa mume wangu alinifungulia biashara ya kuuza nguo kwa ajili ya kuweza kujipatia fedha ndogo ndogo kwa ajili ya kujinunulia baadhi ya vitu kama mama wa nyumbani.

Nilijituma kadiri ya uwezo wangu kuendesha biashara ile vizuri na Mungu aliniwekea mkono wake, kila siku nilikuwa natengeneza faida na siyo hasara.


Siku zilipita na hatimaye nikapata ujauzito, hivyo ikanibidi nitafute mtu wa kunisaidia kazi nyumbani hata dukani pia, katika harakati za kutafuta mtu wa kunisaidia kazi, mume wangu aliweza kumpata msichana kutoka kijijini kwao.


Msichana huyo aliitwa Swaum, mara moja alianza majukumu yake ya kila siku pale nyumbani na hata dukani alikuja kunisaidia mara chache.

Mimi binafusi nilivutiwa jinsi alivyokuwa anafanya kazi zake kwa wakati, pia heshima aliyokuwa nayo, kama mtu angekuja nyumbani kwetu kwa mara ya kwanza asingejua kuwa Swaum ni msichana wa kazi, bali angejua ni mtoto wetu kwa jinsi ambavyo tulikuwa tunaishi naye.


Miezi tisa ilitimia nikajifungua mtoto wa kiume, hivyo Swaum ilibidi mara nyingi awe anaenda dukani kuuza nguo akiwa amemaliza kazi za nyumbani.

Ratiba yake ilikuwa anatakiwa kuondoka nyumbani saa nne asubuhi akiwa ameandaa kila kitu kwa ajili yangu kisha anaenda dukani, na kutoka dukani ni saa tatu usiku na mume wangu ndiye alikuwa anamrudisha.

Baada ya siku kadhaa ratiba ya kurudi nyumbani ilianza kubadilika baada ya kurudi saa tatu walianza kurudi saa nne au tano, nilivyokuwa namuuliza mbona mmechelewa mume wangu alikuwa anatoa sababu ambazo hazikuwa na maana kwangu.

Siku zilizidi kwenda na mume wangu alianza kumpa Swaum zawadi nyingi kama simu, nguo n.k, na hakuishia hapo, akanambia kuwa inabidi tumuongeze Swaum mshahara zaidi ya mara mbili. Nilimuuliza kwa nini akaniambia kwa sasa Swaum anafanya kazi nyingi sana pia anafanya kazi yake vizuri ndio maana anataka tumuongeze mshahara.

Nilivyotazama mwenyewe kweli Swaum alikuwa anafanya kazi vizuri tena kwa wakati, hivyo nilikubari aongezwe mshahara japo nikaanza kuwa na wasiwasi kuwa huenda mume wangu ana mahusiano ya kimapenzi na Swaum.

Baada ya miezi mitano ilibidi nirejee kazini kwangu na kuacha mtoto nyumbani akiwa na Swaumu na wakati wa kumnyonyesha Swaum alikuwa anamleta dukani kwa sababu duka halikuwa mbali sana na nyumbani.

Nilivyoanza kwenda kazini mume wangu alianza kutoka nyumbani akiwa amechelewa, nilipomuuliza akasema kuwa ratiba ya kazini kwake imebadilika, hivyo haina maana kwenda kazini kabla ya muda.

Siku moja Swaum alinikosea nikamsema na kutaka kumpiga, ndipo mume wangu alitoka chumbani na kunipiga makofi kisha kunisema vibaya mbele ya Swaumu. Nilimbeba mtoto wangu na kwenda chumbani kulala japo machozi yalikuwa yananitoka kwa wingi sana.

Tangu siku hiyo maisha yalizidi kuwa mabaya sana kwangu ikafika hatua nikipika chakula mume wangu anasema chakula siyo kitamu hivyo analala njaaa ila Swaumu akipika chakula anakula vizuri na kukisifia.

Siku moja niliamka mapema kama kawaida yangu kisha nikaelekea dukani kwangu nilipofika dukani nikagundua kuwa nimesahau funguo nyumbani ikanibidi nirudi nyumbani kuchukua.

Nilipofika nyumbani nikagundua kuwa gari ya mme wangu bado ipo, nilipofika Sebleni nikakuta mtoto analia sana nipoingia jikoni kuona kama Swaum anapika sikumkuta, ikabidi nifungue mlango wa chumba zetu ndipo nilimkuta mume wangu na Swaumu wakifanya mapenzi.

Nilipigiwa na butwaaa na kumzaba makofi Swaumu na kumtukana mme wangu kutokana na hasira nilizokuwa nazo muda ule, ndipo mume wangu alinisukuma nje na kunambia kuwa hataki kuniona tena katika nyumba yake.

Nilianza kulala kwenye chumba cha wageni, mume wangu analala kwenye chumba chetu na wakati mwingine namsikia chumbani na Swaumu wakifanya mapenzi kwa sauti kwa lengo la kunikomesha.

Wakiwa wanafurahia mapenzi yao mimi nilikuwa natumia muda huo Facebook na WhatsApp kuchati na marafiki zangu, nikiwa Facebook niliona mwanaume ametoa ushuhuda jinsi African Doctors alivyoweza kumsaidia kurudisha mke wake baada ya miaka mitatu ya kuachana.

Nilipozidi kusoma nikakutana na namba ya African Doctors ambazo ni +254 769 404965, kesho yake niliweza kuwasiliana naye, baada ya mazungumzo aliniambia nisubiri kwa masaa 72 pekee Swaum ataondoka mwenyewe nyumbani na furaha ya ndoa yangu itarejea kama mwanzo.

Kabla ya masaa 72 kutumia Swaum alinipigia simu nikiwa bado nipo kazini kisha kuniomba msamaha na kusema amerudi kwao na hataweza kumkaribia mume wangu tena maisha yake yote.

Usiku huo mme wangu alinifuata chumbani kwangu kisha akaniomba msamaha, tangu kipindi hicho mume wangu amekuwa mwaminifu sana kwangu, hata alipokuja dada mwingine wa kazi, mume wangu ameendelea kuniheshimu.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.


Share:

HEKARI 101 NA MAGUNIA 482 YA BANGI YATEKETEZWA ARUSHA

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya (DCEA) imefanikiwa  kukamata gunia 482 za bangi iliyokuwa tayari kusafirishwa kwenye masoko na  imeteketeza jumla ya hekari 101 za mashamba ya bangi yanayokadiriwa kuwa na bangi mbichi gunia 550 katika eneo la Kisimiri Juu kata ya Uwalu, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.


Ukamataji huo umefanyika Mei 31,2023 kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya operesheni nchi nzima ili kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa nchini.

Akizungumza operesheni hiyo maalumu iliyofanyika mkoani Arusha Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo amesema, Mamlaka kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama itaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara katika maeneo hayo ili kuhakikisha bangi inatokomea kabisa na hatimaye wakulima na wananchi kwa ujumla wanaoishi katika eneo ya Kisimiri juu na chini wanaachana na kilimo cha bangi na kujikita katika mazao mengine ya biashara badala ya bangi.


Kamishna Lyimo amesema kuwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) katika kuhakikisha agizo la Mheshimiwa Rais linatekelezwa, ameelekeza kufanyika kwa utafiti kujua ni mazao gani mbadala yanaweza kulimwa katika maeneo hayo ambayo yamekithiri kwa kilimo cha dawa za kulevya, ili wananchi wa maeneo husika waweze kupewa mbinu mbadala za kulima mazao mbalimbali ya chakula na biashara badala ya kuendelea na kilimo cha bangi. 

‘‘Tumewasiliana na Wizara ya Kilimo na Afisa kilimo wa kata ya Uwalu hapa Kisimiri ambaye ameeleza tayari utafiti huo umefanyika",amesema.


Aidha, Kamishna Lyimo amesema, elimu juu ya athari za biashara na matumizi ya dawa za kulevya itatolewa kupitia shule za msingi na sekondari. 

"Hii inafanyika kufuatia agizo la Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mheshimiwa Jenista Mhagama (Mb) kuitaka Mamlaka kushirikiana na wadau kutoa elimu katika maeno hayo. ambapo tayari maafisa elimu Kata wameanza kutoa elimu kwa wanafunzi, ili baadaye wasijihusishe na kilimo cha bangi na mirungi badala yake wajikite kwenye mazao mengine",ameongeza.

Katika kuhakikisha maagizo ya Waziri Mkuu yanatekelezwa, Afisa kilimo Kata ya Uwelu, Samwel Palangyo, amesema kuwa,utafiti uliofanywa na Wizara ya Kilimo kupitia kituo cha utafiti wa kilimo cha TARI Tengeru, imebaini kuwa yapo mazao yanayostawi katika maeneo hayo kama vile pareto, karoti na viazi mviringo na kuwa mbadala wa zao haramu la bangi ambalo halifai katika jamii.

 Ameiomba Serikali kuangalia namna ya kuwawezesha wananchi wa maeneo hayo kwa kutoa ruzuku ya mazao hayo.


Operesheni hii imefanyika ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mheshimiwa Jenista Mhagama (Mb) kutoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini kwa mwaka 2022 ambapo katika taarifa hiyo alitaja mikoa inayojihusisha na kilimo cha Bangi kwa kiasi kikubwa, Mkoa wa Arusha ukiwa kinara ukifuatiwa na Iringa, Morogoro na Manyara.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger