Wednesday 31 May 2023

IFC YAZINDUA PROGRAMU YA JINSIA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI

Mkurugenzi Kanda wa IFC Jumoke Jagun-Dokunmu,

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalumu Dkt.Doroth Gwajima.

Na Dotto Kwilasa,Dodoma.

Katika kuwezesha wanawake kiuchumi, Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Benki ya Dunia (IFC) imezindua programu mpya ya Jinsia "ANAWEZA" itakayo tekelezwa kwa miaka mitano na kugharimu zaidi ya Dola za kimarekani milioni 10.

Akizungumza leo Mei 31,2023 Jijini Dodoma kwenye uzinduzi huo,Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalumu Dkt.Doroth Gwajima IFC ikiwa ni Taasisi tanzu ya Benki ya Dunia ina lengo la kuwezesha wananchi kiuchumi na kuachana na utegemezi.

Katika kuunga mkono juhudi hizo Waziri Gwajima amesema hadi kufikia Aprili mwaka huu serikali ilikuwa  imetoa sh.bilioni 30.9 kwa vikundi 5,120 vya wanawakea katika Halmashauri 184 nchini.

Fedha hizo zimetolewa Kwa lengo la kuboresha kipato na kuondoa umaskini kwa wanawake na wanaume nchini.

Amesema kupitia sheria ya fedha za mamlaka za serikali za mitaa ya mwaka 2018 inayozitaka Halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa Makundi maalum ikiwemo wanawake asilimia nne, vijana asilimia nne na watu wenye ulemavu asilimia mbili.

Dk.Gwajima ameeleza kuwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) unaosimamiwa na wizara anayoisimamia imetoa mikopo yenye thamani ya sh.milioni 664.5 kwa wanawake wajasiriamali 104 katika kipindi cha Julai 2022 hadi Aprili,mwaka huu.

"Tanzania ni miongoni mwa  Mataifa yanayotekeleza malengo ya jukwaa la kimataifa ya kukuza usawa wa kijinsia ambapo Rais  Dk. Samia ni kinara wa utekelezaji wa Jukwaa hilo hususan kuhusu haki na usawa wa Kiuchumi,tumetengeneza programu inayotekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali na Sekta binafsi ili ifikiapo mwaka 2026 hali ya Wanawake iwe imebadilika kwa kiasi kikubwa,"amesema 

Pamoja na jitihada hizo amesema Programu hiyo iliyozinduliwa inajumuisha kutengeneza mazingira bora ya malezi ya awali na uangalizi wa watoto katika ngazi ya jamii ikiwemo masokoni lakini pia katika maofisi ili kuhakikisha huduma za msingi kama vile maji na umeme zinafika kwa ukamilifu vijijini ili kutatua changamoto zinazowakumba wanawake,”alieleza

Amefafanua kuwa Programu ya ANAWEZA itachangia kufanikisha utekelezaji programu wa kizazi chenye usawa hapa nchini na kuwezesha wanawake kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi 

“Ni matarajio yangu kuwa mpango utashirikisha sekta binafsi hapa nchini ili kukuza upatikanaji wa fursa za wanawake katika nafasi za uongozi na ajira bora ili kuchochea ukuaji wa uchumi nchini;

Utafiti unaonyesha kuwa kuziba pengo la kijinsia kati ya ajira za wanaume na wanawake kunaweza kuongeza Pato la Taifa la muda mrefu kwa kila mtu kwa asilimia 4.8.

Kwa upande wake Mkurugenzi Kanda wa IFC Jumoke Jagun-Dokunmu, alisema program ya ANAWEZA itatekelezwa kwa miaka mitano na inalenga kushughulikia changamoto zilizopo ili kuwezesha ushiriki wa wanawake katika sekta binafsi,  nafasi za uongozi na ujasiriamali wenye ufanisi endelevu.

Amesema programu hiyo itakagharimu fedha za Kimarekani milioni 7.5, inaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

“Wanawake wanaweza kuwa injini ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania, hivyo kuwawezesha wanawake kunachukua jukumu kubwa la kukuza uchumi na kuwezesha upatikanaji wa maisha bora kwa watu binafsi na familia zao” amesema.

Katika kusisitiza hilo amesema hakuna nchi inayoweza kupata maendeleo bila mwanamke na hivyo kupitia Uwekezaji huo Tanzania inaenda kuwa kinara na mfano wa kuigwa na mataifa mengine kuhusu uwezeshaji wanawake.

"Tunajipanga kusaidia wanawake wengi zaidi kupata Mafanikio kiuchumi ,tutafanya pia na sekta binafsi kuwekeza kwenye kilimo kuongeza ufanisi wa Wanawake kwenye masuala ya kiuchumi na kuweka usawa kwenye masuala ya jinsia,"anasisitiza 

Amefafanua kwa tathmini ya Benki ya Dunia ya mwaka 2022 kuhusu hali ya jinsia Tanzania inaonyesha kuwa  imepiga hatua katika kuongeza usawa wa kijinsia kwa kufanya jitihada za kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia katika Nyanja zote za maisha ya wanawake.

Naye Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar, Riziki Pembe amesema kuwa Serikali ya Muungano inathamini kazi zinazofanywa na wanawake Katika kuchochea maendeleo ya uchumi hivyo imekuwa akiwateu kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

"Tunatambua juhudi za wanawake katika uongozi na sisi tupo nyuma yenu kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma,lazima tushirikiane kufika mbali zaidi,"anasisitiza
Share:

AMEKULA TUNDA LA MKE WANGU ILA FIMBO YAKE IMEKWAMA NDANI

Tuliishi na mke wangu katika jiji la Nairobi ambapo nilikuwa nafanya biashara, ndoa yetu haikukumbwa na misukosuko kwani tuliaminiana sana na mapenzi yetu alikuwa moto kweli kweli, hakuna ambaye angeweza kutugombanisha.

Kutokana mke wangu alikuwa anazunguka huko na kule kusambaza bidhaa ambazo anauza, niliamua kumtafutia Bodaboda ambaye atakuwa anafanya kazi hiyo, yeye mke wangu kazi yake ikawa ni kupokea oda tu kutoka kwa wateja.

Baada ya siku kadhaa za kazi, Bodaboda yule alitumia fursa ile kumtongoza mke wangu, akachukua namba yake ya simu na kuanza kuwasiliana kila mara bila ya mimi kufahamu lolote.

Siku moja nilikuta SMS kwenye simu ya mke wangu kutoka kwa Bodaboda yule, alikuwa akimsifia kuwa ni mrembo sana, hivyo hastahili kupendwa na mwanaume tu yeyote bali mtu kama yeye. Ujumbe huu ulinipandisha hasira na nilipomuuliza mke wangu kilichokuwa kikiendelea alikana kuwa na uhusiano na kijana yule.

Lakini nilifahamu kuwa Bodaboda yule alikuwa akichovya asali yangu, sikusitisha kazi yake kwani nilitaka siku moja nije kumnasa akiwa na mke wangu ingawa roho yangu ilikuwa ikiuma sana.

Siku moja rafiki yangu Kenny alinitembelea kwenye duka langu na akashangaa nilivyokuwa na msongo wa mawazo, nilimueleza yote yaliyokuwa yanaendelea kwenye ndoa yangu.

Kenny alinifungulia mtandao wa www.african-doctors.com ambapo kulikua na simulizi kutoka kwa watu mbalimbali ambao waliwahi kupitia changamoto kama yangu, nilichukua namba ya African Doctors na kuweza kuwasiliana naye.

Siku iliyofuatia nilifika Ofisini kwa African Doctors, alinihudumia kwa muda wa dakika 30 akawa amemaliza na kuniambia kila kitu sasa ni shwari kabisa. 

Nilirejea nyumbani, nilipigwa na butwaa kuona umati mkubwa wa watu nyumbani kwangu, nilipofika ndani nilimkuta yule Bodaboda akiwa amenasa kwa mke wangu baada ya kuanza kufanya mapenzi, walikuwa wanalia kwa maumivu makali sana.

Hapo hapo nikajua kuwa dawa ya African Doctors imefanya kazi yake, baadaye nilimpigia simu na kumueleza yote niliyoyakuta nyumbani kwangu, alinipatia maelekezo ya kufanya ili waweze kuachana, pia yule Bodaboda alipigwa faini ya Ksh50,000.

Tangu siku ile tuliishi kwa amani na mke wangu kwani tuliaminiana hata zaidi, tuliishi kwa upendo na furaha, vile vile pale mtaani hakuna mtu ambaye anathubutu hata kumsogelea mke wangu.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.

Share:

Tuesday 30 May 2023

WADAU WA USAFIRI WA ANGA WAFANYA MKUTANO KWENYE UWANJA WA NDEGE SHINYANGA... UKARABATI NA UPANUZI KUKAMILIKA 2024 FURSA KIBAO

Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga leo Jumanne Mei 30,2023 wakati wa Mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ulioenda sanjari na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli. 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Serikali imeitaka Wakala ya Barabara nchini (TANROADS) kusimamia kikamilifu ujenzi wa Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga ili kuondoa changamoto ya wananchi wa Shinyanga kulazimika kusafiri kwenda mkoani Mwanza kupata huduma ya usafiri wa anga.

Agizo hilo limetolewa leo Mei 30,2023 na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa Mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS uliofanyika katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.

Samizi amesema ni muhimu ujenzi wa uwanja wa Ndege Shinyanga uzingatie viwango vinavyotakiwa kulingana na thamani ya pesa na ukamilike ndani ya wakati ili kupunguza adha ya wananchi kusafiri kwenda Mkoa wa Mwanza kupata huduma ya usafiri wa anga.

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu kwa kutuletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege. Kwa muda mrefu watu wa Shinyanga wamekuwa na shauku kubwa ya kupata uwanja wa ndege kwani wamekuwa wakilazimika kusafiri kwenda mkoani Mwanza kupanda ndege umbali wa kilomita 164”,amesema Samizi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati Wadau wa Usafiri wa Anga wakitembelea uwanja wa Ndege wa Shinyanga.

“Tumekutana hapa kwa ajili ya mkutano wa wadau wa usafiri wa anga lakini pia mkutano huu tuutumie kama uzinduzi rasmi wa ujenzi wa mradi huu. Rai yangu kwa wananchi wa Shinyanga ni kuchangamkia fursa kupitia mradi huu, tengenezeni shughuli ambazo zitachochea uchumi na tuhakikishe tunaulinda mradi huu”,ameongeza Samizi.

Amesema uwanja huo wa ndege wa Shinyanga unatarajiwa kurahisisha usafiri kwa wananchi pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi hususani katika sekta ya madini
Meneja Mradi Viwanja vya ndege,TANROADS kutoka makao makuu Mhandisi Neema Joseph amesema mradi wa Ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga unajengwa na Mkandarasi China Hennan International Corperation Group Co. Ltd (CHICO) kwa gharama ya shilingi 49,179,439,633.00/= pamoja na VAT na unasimamiwa na Wakandarasi kutoka Kampuni ya SMEC International ya nchini Australia kwa gharama ya Dola za Marekani 2,602,343 na Shilingi 23,735,554/= pamoja na VAT.

Mhandisi Neema amesema mradi huo ambao ujenzi wake umeanza Aprili 4,2023 unatarajia kukamilika ifikapo Oktoba 3,2024 (ndani miezi 18) kwa ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB).

“Kazi zikatazofanyika ni ukarabati wa barabara ya kutua na kurukia ndege (Runway) kwa kiwango cha lami, ukarabati wa barabara ya kiungio na maegesho ya ndege kwa kiwango cha lami, ujenzi wa jingo la abiria pamoja na ATC na huduma za hali ya hewa, ujenzi wa barabara ya kuingia uwanjani”,amesema Mhandisi Neema.

Amezitaja kazi zingine kuwa ni ujenzi wa maegesho ya magari, ujenzi wa uzio wa usalama, ununuzi na usimikaji wat aa za kuongozea ndege (AGL), ununuzi na usimikaji wa mitambo ya usalama (DVOR/DME) na ujenzi wa kituo cha umeme (energy centre).

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Mibara Ndirimbi amewataka wakazi wa Shinyanga kulinda mradi huo na kuepuka vitendo vya kuhujumu kama vile wizi wa mafuta na vifaa vingine vya ujenzi huku akisisitiza kuwa mradi huo utawanufaisha wananchi wa maeneo ya karibu kupata ajira ya muda na kupata fursa mbalimbali za kiuchumi.

“Tunawahakikishia kuwa ujenzi wa mradi tutausimamia kwa viwango vinavyotakiwa kwa kuzingatia thamani ya pesa iliyotolewa. Naomba tushirikiane. Wananchi tuwe walinzi wa mali za mkandarasi na tutoe taarifa kama mnaona kuna mtu anataka kuhujumu mradi huu”,amesema Ndirimbi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma za ufundi kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Dk. Pascal Waniha amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi huo.

Nao wadau wa usafiri wa anga akiwemo Mchungaji Greyson Kinyaha kutoka kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa Jumanne Wagana na Catherine Mlandaja kutoka Mgodi wa Williamson Diamonds wamesema muda uliopangwa ni mwingi hivyo wajaribu kuharakisha ili kuweza kukamilisha kabla ya mikataba ulivyopangwa kwani shauku kubwa ya wana Shinyanga ni kuona uwanja wa ndege unatumika.
Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga leo Jumanne Mei 30,2023 wakati wa. Mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ulioenda sanjari na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga leo Jumanne Mei 30,2023 wakati wa. Mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ulioenda sanjari na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli. 
Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga leo Jumanne Mei 30,2023 wakati wa Mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ulioenda sanjari na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli. 
Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga leo Jumanne Mei 30,2023 wakati wa Mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ulioenda sanjari na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli. 
Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga leo Jumanne Mei 30,2023 wakati wa Mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ulioenda sanjari na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli. 
Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga leo Jumanne Mei 30,2023 wakati wa Mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ulioenda sanjari na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli. 
Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga leo Jumanne Mei 30,2023 wakati wa Mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ulioenda sanjari na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli. 
Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga leo Jumanne Mei 30,2023 wakati wa Mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ulioenda sanjari na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli. 

Msimamizi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli Shinyanga Mhandisi Donatus Binemungu akiwaelezea Wadau wa Usafiri wa Anga ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati Wadau wa Usafiri wa Anga wakitembelea uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Mhandisi Mkazi kutoka Kampuni ya SMEC International ya nchini Australia, Nasser Elgohary akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ramani ya ujenzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli Shinyanga.
Mhandisi Mkazi kutoka Kampuni ya SMEC International ya nchini Australia, Nasser Elgohary akionesha ramani ya ujenzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli Shinyanga.
Mhandisi Mkazi kutoka Kampuni ya SMEC International ya nchini Australia, Nasser Elgohary akionesha ramani ya ujenzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli Shinyanga.
Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa uwanja wa Ndege Shinyanga kutoka TANROADS, Donatus Binemungu akielezea kuhusu ramani ya ujenzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.

Meneja Mradi Viwanja vya ndege,TANROADS kutoka makao makuu Mhandisi Neema Joseph akitoa taarifa ya upanuzi na ukarabati wa uwanja wa Ndege Shinyanga wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Mibara Ndirimbi akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kishapu,  Peter Mashenji akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa uwanja wa Ndege Shinyanga kutoka TANROADS, Donatus Binemungu akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
 Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
 Catherine Mlandaja kutoka Mgodi wa Williamson Diamonds  akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger