Thursday 4 May 2023

MRADI UJENZI BWAWA LA MEMBE WAFIKIA ASILIMIA 45.83%.



Kamati ya siasa ya wilaya ya Chamwino ikiongozwa na katibu ndugu Sylivester Yaledi (Chief Yaledi) imetembelea mradi wa Bwawa la maji Membe lililopo kata ya Membe halmashauri ya Chamwino kukagua hatua ya utekelezaji mradi huo.

Kamati hiyo imeipongeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji NIRC kwa usimamizi makini wa ujenzi wa bwawa la maji Membe litakaloweze kumwagilia zaidi ya hekari 8,000 katika mashamba ya wakulima wa eneo hilo ikiwa ni miongoni mwa miradi ya Umwagiliaji inayoendelea kutekelezwa na tume.

Akielezea maendeleo ya mradi huo msimamizi wa mradi wa ujenzi bwawa hilo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Saleh Madebe (mwenye T-shirt ya njano kwenye picha) amesema mradi huo umefikia asilimia 45.83%.

Hata hivyo kamati hiyo imemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuongeza kasi ya ujenzi wa bwawa hilo ili kuendana na muda wa mkataba na hatimaye mradi huo uwe na tija kwa wakulima na kuchochea uchumi wa nchi.

Mradi huo unatarajiwa kukamilika Septemba 1, 2023 kwa mujibu wa mkataba ambapo matokeo ya kukamilika kwa mradi huo utawezesha halmashauri ya wilaya ya Chamwino na mkoa wa Dodoma kuwa na chakula cha kutosha na kuzalisha ajira kwa vijana kupitia sekta ya kilimo.



Share:

WAUGUZI HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO TANGA WATOA HUDUMA ZA UPIMAJI KWA WANANCHI

 


Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Andrew Tusiwe akiwa kwenye eneo ambaalo huduma za upimaji kwa wananchi zinaendelea kwenye Hospitali hiyo ikiwa ni kuelekea siku ya maadhimisho ya Wauguzi Duniani 

Wananchi wa Jiji la Tanga wakipatiwa huduma ya upimaji katikati Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Andrew Tusiwe

Wananchi wakiendelea kupata huduma mbalimbali


Wananchi wakiendelea kupata huduma mbalimbali


Na Oscar Assenga Tanga



WAUGUZI katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo leo wameanza kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo utoaji wa Elimu ya Lishe Bora,utoaji wa chanjo ya Uviko 19,upimaji wa magonjwa mbalimbali ikiwa ni kuelekea siku ya maadhimisho ya sherehe ya wauguzi duniani inayo adhimishwa kesho Mei 5 mwaka huu.

Akizungumza leo Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Andrew Tusiwe alisema kwamba watasherehekea siku ya wauguzi ambayo mwanzilishi wake Florence Nightingale; "Mwanamke wa Taa" ambaye alisimama kidete katika kuinua viwango vya uuguzi pamoja na kuwaelimisha Wauguzi kuwa na upendo kwa watu wenye uhitaji.

Tusiwe alisema kwa upande wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wao wataadhimisha siku hiyo kwa kutoa zawadi kwa wagonjwa na kuwafariji.

Tusiwe alisema kwamba pia watafanya upimaji wa sukari,Presha,VVU na Satarani ya Shingo ya Kizazi, shinikizo la damu ,huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kupima afya zao na kama kuna dalili za viashiria vyoyote aweze kupata huduma mapema.

Hata hivyo alitoa ushauri kwa wananchi ni muhimu wakajiwekea utaratibu mzuri wa kucheki afya zao mara kwa mara ili wanapogundulika na matatizo waanze kupata huduma za matibabu kwa haraka.
Share:

AOTA SEHEMU YA SIRI USONI KISA KUTEMBEA NA MKE WA MTU

Katika dhehebu moja kulikuwa na kiongozi mmoja wa dini ambaye alikuwa maarufu kutokana na uwezo wake, alibadilisha maisha ya watu wengi kwani kila aliposimama kueneza neno maisha ya wengi yalibadilika.

Hata hivyo, rafiki yangu mmoja alikuwa analalamikia kwamba mke wake kila alipoenda katika dhehebu hilo alichelewa kurejea nyumbani, alirejea nyumbani usiku kwa madai alikuwa na mkutano wa faragha na kiongozi huyo.

Baada ya tabia ya mkewe kuzidi kuwa mbaya, tulimshauri amtembelee African Doctors kwa ajili ya ushauri na kumfanya mkewe kuwa mwaminifu na kutokuwa na mwanaume mwingine nje ya ndoa yao.

Basi alienda kwa African Doctors na akahudumiwa na kurejea nyumbani kwani alipewa hakikisho kwamba yeyote atayejaribu kula tunda lake basi atapata cha mtema kuni kwa wakati wowote.

Basi mke wake kama kawaida alienda katika dhehebu lile na hakujua kuwa mume wake alikuwa amemkinga kutoka nje ya ndoa, alirejea nyumbani mwendo wa jioni na mume wake alipomuuliza alipokuwa alisema kwamba alikuwa kwenye mkutano wa faragha na kiongozi yule.

Jumapili ilipofika waumini walishangazwa na kiogozi yule wa kidini kwani kila mara alikuwa anajikuna sehemu za siri wakati akitoa neno, ghafla hali ile ilimzidi na kutupa chini vitabu vyake ambavyo alitumia kufundishia.

Baadaye alianguka chini na kuanza kugaragara mithili ya mtu aliyekuwa anataka kufa, kilichoshangaza katika uso wake kuna kitu kama sehemu ya kike ya mwanamke kilijichora kitu kilichopelekea waumini wake kupigwa na butwaa.

Hadi hapo yule mwenye mke alijua fika kwamba siku za mtu aliyekuwa akila tunda lake zilikuwa zimefika, basi Richard alienda kwa kiongozi yule na kumuuliza iwapo alikuwa amewahi kutembea na mke wake.

Uzuri alikiri ni kweli aliwahi kufanya jambo hilo, basi alimpigia simu African Doctors na kumueleza kuhusu tukio hilo, African Doctors alimueleza kiongozi yule kuwa anapaswa kulipa Ksh40,000 ili hali yake iweze kurejea kama kawaida. 

Mke wake alituma fedha zile kwa njia ya simu na hapo hapo akarejeshewa kwenye hali yake ya kawaida, tangu siku ile aliacha kuwa kiongozi wa dini na kuamua kuwa mkulima.

Kumbuka African Doctors anaweza kutibu magojwa kama vile kifafa, kisonono na mengineyo, anaweza kukukinga na maadui zako, kukuwezesha kupata kazi, kupandishwa cheo kazi na hata kuongezewa mshahara.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.


Share:

Wednesday 3 May 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 4,2023



















Share:

MKE ASHINDWA KULINDA UNYUMBA KWA HEDHI ISIYOKOMA

Naitwa Aines kabla ya kuolewa niliishi kwa furaha sana na baada ya kuolewa siku za mwanzo wa ndoa yangu sikuzijua karaha nilizo hadithiwa na mashosti zangu kuhusu ndoa mpaka yaliponikuta, kwa kweli mwenye niliolewa nikiwa binti mdogo sana wa miaka ishirini na mmoja tena sikuwahi kuwa na mahusiano yoyote yale kabla ya mimi kuolewa kiufupi ni kwamba mume wangu ameniowa mimi nikiwa bado bikira simjuwi mwanaume yoyote tena kwa sheria za kwetu huko Songea kwa Wamwera nilifundwa na kukalisha kuyajua mambo ya ndoa.

Ndani ya ndoa sikuwahi kubahatika kupata mtoto kabla ya sisi kutambulishwa kwa daktari BAKONGWA , yaani mwanzoni ilikuwa ni rahisi na furaha tulifanya kila kitu ndani ya ndoa na mume wangu ariridhika kwa ufundi niliofundwa kwetu kila mtindo alioutaka na kila mahali alipotaka nilimpa.

Kama wengi wanavyojua kwa sisi wanawake huwa tunaingia hedhi kutowa uchafu na taka za mwiili –hapa ndipo hali yangu ilianza kubadilika na kuwa mbaya zaidi ndoa ikawa chungu kwangu nikaichukia kwa kiasi kikubwa mno, mwanzoni nilidhania kuwa ni kawaida au labda kwa sababu za mimi kutokuzoea kuwa na mwanamume kila siku lakini haikuwa hivyo.

Kipidi cha nyuma nilikuwa nikiingia hedhi kwa siku tatu tu lakini nilishangaa awamu hii nilipoingia hedhi kwa  zaidi ya siku tatu nikafikiri labda kwa siku ya nne hali itakwisha lakini ilikuwa ndio mwanzo wa hedhi ikaendelea hali ile kwa zaidi ya mwezi mzima mume wang akafanya mpango tukaenda hospitali wao wa kafikiria kuwa ilikuwa mimba imeharibika wakatupa dawa na kutusafisha lakini baada ya siku ne tu hali ile ikarudi tena damu zikaanza kuvuja upya.Tukaweka ratiba za kuwaona madaktari wa uzazi lakini hata kwao pia hawakujuwa nini kinaendelea zaidi ya kutupa dawa ya kujisafisha na kufikiria kuwa labda mimi nilikuwa nimetowa mimba au kuharibika yenyewe.

Hasira ndani ya ndoa zikaongezeka sasa ikawa ni zaidi ya mwaka mzima ninavuja damu na ume wangu hajapata unyumba kutoka kwangu nikaona dalili za kila aina kuwa mume wangu anachepuka.Aliamuwa kunidhihirishia hili na kuniambia kuwa anataka aowe mwanamke wa pili nyumba ndogo kwa kuwa mimi simpi haki yake ya ndoa.

Msongo wa mawazo ukaongezeka na kila nilipofikiri kuwa hata mtoto naye sina nikaona ni mwisho wa ndoa yangu kabisa, zaidi ya miaka miwili sasa sikuwa nimefanya mapenzi na mume wangu na dmau hazikuisha kuvuja.

Kwa kuogopa aibu za watu na maneno ya walimwengu mtu pekee wa karibu niliyemshirikisha hili ni wifi yangu ndiye aliyenitambulisha kwa daktari bakongwa na kunipa nambari zake za whatsapp +243990627777 akanishauri nimtafute akisema yawezekna akatatuwa shida niliyokuwa nayo.

Nilifanya hivyo na kwenye tovuti zake https://bakongwadoctors.com  niliandaa miadi naye , daktari alinisikiliza kwa makini kisha akaniambia kuwa hedhi ile ni y kutengenezwa na maadui zangu waliokuwa wapenzi wa mume wangu kipindi cha nyuma, alinipa dawa ya kutumia wiki nzima kwa kuwa tatizo langu lilikuwa limekomaa sana ila baada ya kama siku tisa nilikuwa nimekwisha ona mabadiliko hedhi ilikata hakukuwa na damu yoyote iliyoendelea kutoka kwangu.

Furaha kwenye ndoa yetu ilirui upya nikamshirikisha mume wangu na kumueleza kuwa aliyekuwa ametufanyia hayo ni huyo mke wa pili ambaye alipanga kumuowa hakika bila daktari bakongwa tusingejuwa haya wala kupona, asante sana daktari bakongwa.

 


Share:

Video Mpya Kali balaa!! NTEMI OMABALA 'Ng'wana Kang'wa' - MERINA


Msanii maarufu wa Nyimbo za asili Ntemi Omabala 'Ng'wana Kang'wa' ameachia ngoma mpya inaitwa Merina...Tazama Video hapa chini

Tazama Video hapa chini
Share:

NAIBU WAZIRI ASISITIZA KAMPUNI ZA MADINI KUTOA FURSA ZA AJIRA, ZABUNI KWA WATANZANIA

Mfanyakazi wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Omary Faustine Matulanya akitoa maelezo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi (kushoto) kuhusu matairi yanayotumika kwenye mitambo ya ubebaji  mawe na mchanga wa dhahabu kutoka ndani ya migodi. Katambi alitembelea banda la kampuni hiyo kwenye maoneosho ya afya na usalama mahali pa kazi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro kuanzia tarehe 26 hadi 30 Aprili mwaka huu.
Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya GGML alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yaliyofikia tamati tarehe 30 Aprili 2023.
Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya GGML alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yaliyofikia tamati tarehe 30 Aprili 2023.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako ambaye juzi Jumapili alitembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya wiki ya afya na usalama mahali pa kazi na kufanyika kwenye viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro. Katika maonesho hayo GGML imeibuka mshindi wa jumla kama muoneshaji bora na kampuni bora yenye ubunifu wa vifaa vya kisasa vinavyozingatia afya na usalama mahali pa kazi.



NA MWANDISHI WETU, MOROGORO

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu, Patrobas Katambi ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kutoa fursa za ajira kwa Watanzania zaidi ya asilimia 90 ndani ya mgodi huo pamoja na kuwapatia wazawa fursa za kutoa huduma za kuuza bidhaa za ndani kwenye kampuni hiyo.



Pia ameipongeza kampuni hiyo kwa kuibuka mshindi wa ubunifu na banda bora kwenye maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yaliyofanyika katika viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro kuanzia tarehe 26 hadi 30 Aprili mwaka huu.

Katambi alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho hayo yaliyoratibiwa na Wakala wa Afya na Usalama mahali pa kazi (OSHA).


“Niwapongeze hasa kwa kupunguza ulemavu kazini, magonjwa yanayotokana na kazi lakini pia kuhakikisha kwamba mazingira yote ya kufanyia kazi yanakuwa salama.


“Nafurahi kuona kwamba banda zima na hata ndani ya kampuni asilimia kubwa ya wafanyakazi ni watanzania wenzetu kwa maana hiyo tunazidi kusisitiza kwamba kwenye maeneo yote ya kazi watanzania ni kipaumbele,” alisema.


Alisema mgeni anaposhika nafasi ya ajira ina maana kwamba ujuzi huo ni adimu, mtanzania hana sifa wala vigezo lakini pamoja na hilo Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza watanzania wajengewe uwezo kushika nafasi hizo.

“Ameelekeza kuhakikisha wakati wote kwamba wakiwepo wageni wenye ujuzi nyuma yake awepo mtanzania anayejifunza hizo kazi na baada ya muda, utaalamu tubaki nao wenyewe,” alisema.


Alisema GGML imekuwa mfano wa kuigwa katika manunuzi yanayofanyika kwenye migodi yake kwa sababu Serikali kupitia mpango wa kuwezesha wazawa kutoa huduma na kuuza bidhaa ndani ya mgodi (local content) inasisitiza kwamba vitu kama vipo hapa nchini vinunuliwe hapa hapa ili kiuongeza ukwasi ndani ya nchi ili fedha nyingi isitoke nje.

“Lakini pia mmezingatia usalama wa mazingira kwa ujumla ili tusipate watu wenye ulemavu unaotokana na migodi hata pia mazingira na ardhi yetu inabaki kuwa salama kwa hiyo nyinyi watanzania mliopo huko ni wawakilishi wa kuhakikisha usalama unakuwepo...wa kwetu sisi, viumbe hai,” alisema.

Aidha, akimkaribisha katika banda hilo, Meneja anayehusika na usalama kazini kutoka GGML, Isack Senya alisema zaidi ya wananchi 3000 wametembelea banda hilo na kujifunza mambo mbalimbali kuhusu teknolojia zinazotumika kufanya kazi katika mazingira yenye afya na usalama.


Alisema mwaka huu GGML ilileta vifaa vya kiteknolojia na kisasa kiasi cha kuiwezesha kampuni hiyo kuibuka kampuni bora yenye ubunifu kwenye vifaa hivyo.

Pia alimuahidi Naibu Waziri kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali inayosaidia jamii kuondokana na umaskini pamoja na kupata huduma bora kwa kushirikiana na serikali.

Pamoja na mambo mengine, Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako naye alipita katika banda hilo na kuipongeza kampuni hiyo kwa kuwa mdau muhimu katika kuzingatia matakwa ya sheria yanayosisitiza afya na usalama mahali pa kazi.

Share:

BENKI YA CRDB YAPATA LESENI KUFANYA BIASHARA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO (DRC)


Kinshasa DRC 2 Mei 2023 – Benki Kuu ya Congo (BCC) imeipatia leseni ya kufungua kampuni tanzu nchini humo Benki ya CRDB. Leseni hiyo imekabidhiwa leo katika mkutano maalum kati ya BCC na ujumbe wa Benki ya CRDB ulioongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha wa Kundi, Fredrick Nshekanabo.

Akikabidhi leseni hiyo Naibu Gavana wa kwanza wa BCC, Dieudonné Fikiri Alimasi aliipongeza Benki ya CRDB kwa hatua hiyo muhimu ambapo alisema itakwenda kuchochea ushindani katika sekta ya fedha nchini humo kwa kutambua kuwa benki hiyo ni moja ya benki zinazofanya vizuri katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

“Tulipopokea ombi lenu la kufungua kampuni tanzu hapa DRC tulifurahi na tulilichukulia kwa umuhimu mkubwa hasa ukizingatia mahusiano yaliyopo baina ya nchi zetu. Niwapongeze kwa namna ambavyo mlikuwa mkitoa ushirikiano katika kila ambalo tuliwaambia kutekeleza, hii inaonyesha jinsi gani mmedhamiria kuingia DRC na kufanya biashara hapa,” alisema Naibu Gavana BCC.

Katika taarifa yake kwa ujumbe wa Benki ya CRDB, Naibu Gavana pia alieleza kuwa BCC imepitisha mapendekezo ya uteuzi wa Bi. Jessica Nyachiro kama Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB nchini DRC.

BCC pia imewaidhinisha Dr. Fredrick Msemwa (Tanzania), Prof. Faustine Bee (Tanzania), Jeannot Okit’Otete (DRC), Olivier Duterme (DRC) Bi. Ornella Bomine (DRC), Bi. Rama Bweya (DRC) kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Congo.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB aliishukuru BCC kwa kuipatia Benki hiyo leseni ya kufanya biashara nchini humo, na kueleza kuwa Benki ya CRDB imeshafanya maandalizi yote ya kufungua milango nchini humo. Nshekanabo alimuhakikishia Naibu Gavana kuwa Benki ya CRDB itashirikiana kwa karibu na BCC ili kusaidia kuimarisha sekta ya fedha nchini DRC.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Congo, Jessica Nyachiro amesema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanatoa huduma bora na bunifu zitakazoendana na soko la DRC. Jessica alisema Benki ya CRDB itatumia uzoefu wake katika masoko ya Tanzania, na Burundi kuhakikisha ina kabiliana na ushindani nchini humo.

Akielezea mkakati wa kufikisha huduma kwa wateja, Jessica amesema Benki hiyo itaanza na tawi katika mji wa Lubumbashi, huku akieleza kuwa katika mkakati wake wa biashara wa miaka mitatu Benki ya CRDB Congo inatazamia kupanua wigo wake katika miji mengine mikubwa ikiwamo Kinshasa, Lualaba, Kasai, Kisangani, Tanganyika, pamoja na Kivu kaskazini na kusini.

“Benki yetu inasifika kwa uwekezaji mkubwa katika mifumo ya kidijitali hivyo pamoja na mtandao wa matawi tunatarajia pia kutumia njia mbadala za ufikishaji huduma kama vile CRDB Wakala, SimBanking, na Internet banking kuwaunganisha wananchi wengi wa Congo katika huduma zetu,” amesema Jessica.

Jessica aliongezea kuwa malengo ya Benki ya CRDB ni kuwa mshirika namba moja wa maendeleo nchini DRC. Aliihakikishia Serikali na wadau wa sekta binafsi nchini humo kuwa Benki hiyo ipo tayari katika kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na sekta ya umma na binafsi.

“Benki yetu ina mizania kubwa ambayo inawezesha sekta zote za maendeleo. Kama ambavyo tumekuwa tukifanya Tanzania na Burundi huku pia tumejipanga kufanya hivyo,” huku akitoa mifano ya miradi ya Reli ya Kisasa (SGR) na ujenzi wa bandari ya Kigoma ambayo Benki hiyo inasaidia kuifadhili nchini Tanzania ambayo ikikamilika itasaidia pia nchi ya DRC.

Jessica aliwashukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Felix Tshisekedi Tshilombo kwa kazi nzuri ya kuboresha mahusiano baina ya Tanzania na DRC ambayo yamesaidia kurahisha Benki hiyo kupata kibali nchini humo.
Kwa upande wake Israel Tshimanga Mutamba, Afisa Mahusiano kwa Wateja wa Benki ya CRDB Congo aliwakaribisha wajasiriamali nchini humo hususan vijana na wanawake kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki hiyo huku akibainisha kuwa benki hiyo ina huduma mahsusi kwa ajili ya kundi hilo ikijumuisha mifumo ya kidijitali ya usimamizi wa biashara na mikopo nafuu.

“Napenda kuwajulisha Wacongo wenzangu, hii ndio Benki ambayo tukiitumia vizuri tutaweza kuboresha maisha yetu. Uwe mwanafunzi, mfanyakazi, mkulima, mfanyabiashara, Benki ya CRDB ipo tayari kukuhudumia. Niwasihi tuchangamkie fursa hii,” aliongezea Israel.

Ujumbe wa Benki ya CRDB uliambatana na viongozi waandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Congo wakiongozwa na Mkuu wa Utawala, Netho Yatega ambao wamekuwa sehemu muhimu ya mchakato mzima wa kuhakikisha Benki ya CRDB inapata leseni ya kutoa huduma nchini humo.
Naibu Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Congo, Dieudonné Fikiri Alimasi (watatu kushoto) akikabidhi leseni ya kutoa huduma za kibenki nchini humo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Jessica Nyachiro. Wakishuhudia zoezi hilo ni Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo (katikati), Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Congo, Netho Yatega (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa (watatu kulia), Mkurugenzi wa Hazina na Masoko ya Mitaji, Alex Ngusaru (wakwanza kulia), na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB, Yolanda Uriyo.





Naibu Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Congo, Dieudonné Fikiri Alimasi akiongoza kikao kabla ya kukaidhi leseni ya kutoa huduma za kibenki nchini Congo kwa uongozi wa Benki ya CRDB.

Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo akizungumza wakati akiishukuru BCC kwa kuipatia Benki hiyo leseni ya kufanya biashara nchini humo,

Share:

Tuesday 2 May 2023

MWALIKO WA MISA YA SHUKRANI YA MPENDWA WETU RENATUS SOSPETER LUHUNGA JUMAMOSI JIJINI DODOMA


Share:

KATAMBI AFAFANUA MFUMO WA KUWALIPA KIINUA MGONGO WAZEE



Na Mwandishi Wetu, DODOMA

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema serikali inazingatia watanzania wote wanaojenga nchi yao na imeweka utaratibu wa kupata pensheni kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa waajiriwa na waliopo kwenye sekta isiyo rasmi.

Mhe.Katambi ameyasema hayo Mei 2, 2023 bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Magu (CCM), Mhe. Boniventura Kiswaga ambaye amehoji lini serikali italipa kiinua mgongo kwa wazee ambao hawajawahi kuajiriwa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Katambi amesema kiinua mgongo ni malipo ambayo hulipwa na mwajiri pindi mfanyakazi wake anapostaafu kufanya kazi.

Mhe. Katambi amefafanua kuwa, kutokana na kuwepo kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii mwajiriwa na mwajiri huchangia, mfanyakazi hulipwa pensheni badala ya kiinua mgongo na hupokea mafao ya mkupuo mara anapostaafu na baadae kuendelea kulipwa pensheni ya kila mwezi kwa maisha yake yote na kwasasa hakuna mfumo wa kulipa kiinua mgongo kwa wazee ambao hajawahi kuajiriwa.

Hata hivyo, amesema kwa watu waliopo kwenye sekta isiyo rasmi ikiwamo wajasiriamali, wakulima na wafugaji, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) ndio wenye jukumu la kushughulikia sekta hiyo na umeanza kukusanya michango kwa kuwatambua waliyo kwenye makundi hayo.
Share:

MSANII WA NYIMBO ZA ASILI 'DAWA DAWA' ATUPWA JELA KWA KUMTUKANA RAIS KWENYE WIMBO WAKE


Na Daniel Limbe, JamhuriMedia, Chato

Msanii wa nyimbo za asili ya Kisukuma, Dawa Juma,mkazi wa kijiji cha Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita,amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela au kulipa faini ya shilingi milioni 10 baada ya kupatikana na hatia ya kumtukana rais Samia Suluhu Hassan.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Chato,Amalia Mushi,baada ya mshitakiwa kukiri kosa mbele ya mahakama hiyo.

Awali Mwendesha Mashitaka wakili mwandamizi wa Serikali,Robert Magige,ameiambia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alitunga wimbo wenye lengo la kumtukana matusi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,licha ya kujua wazi kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Kwamba akiwa na nia ovu alirekodi wimbo huo na kuusambaza kwenye mitandao ya kijamii ili kupeleka ujumbe wake kwa umma huku akijinadi kuwa haogopi kukamatwa.
Mwendesha mashitaka huyo,amesema kitendo cha kuchapisha taarifa za uongo na matusi kisha kusambaza kwenye mitandao ya kijamii (You tube) ni kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mtandao,sheria namba 14 ya mwaka 2015.

Hata hivyo mshitakiwa baada ya kusomewa mashitaka yanayomkabili amekiri kutenda kosa hilo, licha ya kudai kuwa hakuwa na nia mbaya kwa kuwa alikusudia kuonyesha hali ilivyo mbaya kwa jamii baada ya bidhaa kupanda bei.

Aidha baada ya mshitakiwa kukiri kosa,wakili wa Serikali Magige ameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye lengo la kumtukana rais kutokana na sababu zao binafsi.

Akitoa hukumu,hakimu wa mahakama hiyo,amesema kuwa kwa kuzingatia kuwa mshitakiwa hakuisumbua mahakama hiyo,kwa kukiri kosa kwa kinywa chake mwenyewe mahakama inamhukumu kifungo cha miaka sita jela au kulipa faini ya shilingi milioni 10.

Hata hivyo mshitakiwa amepelekwa gerezani kuanza kutumikia kifungo chake baada ya kushindwa kulipa faini iliyoelekezwa na mahakama hiyo.

CHANZO - JAMHURI MEDIA

Dawa dawa kali ni msanii wa nyimbo za asili lakini katika uimbaji wake amekuwa akimuimba mh. Samia Suluhu mara nyingi amekuwa akiimba huku akimkosoa Raisi kile anachokifanya na kuweka utani uliopitiliza kwenye nyimbo zake.

Huu hapa wimbo wa Msanii Ryamapetroli akimshauri msanii Dawa Dawa kuacha tabia ya kutukana
Share:

WAZIRI WA KAZI CHARLES ENGOLA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI


Waziri wa Kazi, Ajira na Uhusiano wa Viwanda Nchini Uganda, Charles Okello Engola ameuawa asubuhi hii kwa kupigwa risasi na Mlinzi wake (Bodyguard), Spika wa Bunge la Uganda Anitha Among amethibitisha Bungeni leo.

Tukio hilo limetokea asubuhi hii ambapo imeripotiwa kuwa Waziri Okello alikuwa anatoka nyumbani kwenda kazini ambapo ghafla Mlinzi wake alimpiga risasi kisha akaanza kupiga risasi juu huku akikimbiakimbia Mtaani.

Majirani wamesema Mlinzi huyo alisikika akisema hajalipwa mshahara kwa muda mrefu licha ya kufanya kazi na Waziri huyo.

Inaripotiwa kuwa Mlinzi huyo baadaye aliingia Saluni moja iliyopo Jirani na nyumba ya Waziri kisha akawataka waliokuwa ndani kutoka nje na akajifungia na kujipiga risasi na kufariki pia.
Share:

NTOBI : PUUZENI HICHO KIPEPERUSHI KINACHOSAMBAA MTANDAONI

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi amewataka wananchi kupuuza kipeperushi kinachosambaa mtandaoni kinachoeleza amesimamishwa uongozi.

Akizungumza na Mwandishi wetu, Ntobi amesema :  "Taarifa hizo sina hakika nazo mpaka sasa, kwani sijapata barua rasmi kutoka kwa yeyote Kanda wala Taifa. Nimeona kwenye mitandao ya kijamii kipeperushi chenye taarifa kwa umma. Ninachofahamu nilitegenezewa mashtaka ya uongo na uzushi ili kuchafua na kushusha heshima yangu na zaidi sikupata nafasi ya kusikilizwa".


"Hizi ni ajali za kisiasa zinazotengenezwa tu na hata Mwl Nyerere alitengenezewa na wakoloni, Freeman Mbowe, Tundu Lissu na wanasiasa wengi tu hutengenezewa zengwe. Kwa sasa niwatake viongozi na wanachama wa CHADEMA Shinyanga kuendelea kuwa watulivu na waamini bado nipo imara sana kuliko jana. Naamini CHADEMA ni taasisi imara nikipata barua rasmi nitaweza kuzungumza na Wana Shinyanga, wanaChadema na Watanzania wote kwa ujumla.


Kwa sasa sina maoni mazuri kuhusu hili kwa sababu sifahamu hata ni kifungu gani cha Katiba yetu kinachotamka adhabu kama hiyo",amesema Ntobi.

Katika taarifa hiyo inayosambaa mtandaoni, Kamati tendaji ya CHADEMA Kanda ya Serengeti imemsimamisha uongozi Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi kutokana na makosa ya nidhamu.

Hata hivyo Katibu wa Kamati ya Uenezi CHADEMA Kanda ya Serengeti, Golden Charles Marcus amesema :
"Taratibu za chama zinampa nafasi mhusika kukata rufaa ya ndani ya siku 30 ,Ntobi ni mwanasiasa mkongwe anajua hatua zote za kuzingatia kuhusu rufaa yake na ana tambua yote juu ya barua hiyo kwa kuwa vikao halali alishirikishwa hadi hatua ya mwisho ya barua hiyo kutolewa na uongozi wa CHADEMA".

Taarifa inayosambaa mtandaoni


Share:

SASA NAPELEKA MOTO HATARI BAADA YA KUACHWA NA WAKE WAWILI

Mimi ni mwanaume ambaye naheshimu na kumjali mwanamke yoyote katika dunia hii, naheshimu sana jinsia ya kike kwa sababu Baba yangu mzazi alimuacha Mama yangu nikiwa bado mdogo kabisa, Mama yangu alijitahidi kadiri awezavyo kunitunza. 

Mwaka 2015 nilipata mke, kutokana na malezi ambayo nilipata kwa Mama yangu mzazi nilimuheshimu, kumpenda na kumjali mke wangu. Nilifanya kila kitu niwezacho kwa ajili ya kumfurahisha mke wangu ila hayo yote yakawa bure kwani mwaka 2016 aliniacha bila sababu yoyote.

Haikuchukua muda nilipata mwanamke mwingine kutoka mkoa wa Mara, pia nilimpenda mke wangu wa pili kadiri niwezavyo hadi ilifikia hatua mke wangu ananikosea nashindwa kusema kisa naogopa aibu endapo akiondoka kama mke wangu wa kwanza.

Maisha yaliendelea pole pole ila baada ya miezi sita mke wangu akaanza tabia ya kutoka nje ya ndoa jambo ambalo liliniumiza sana kama mume wake.

Nilimkalisha chini na kumuuliza kitu gani amekosa kwangu hadi anaanza kutembea na wanaume nje na kunivunjia heshima, ndipo kwa kinywa chake akasema kuwa kitandani sijiwezi, hivyo mwili wake kuna kitu unakosa ndio maana yeye analala na wanaume wengine nje.

Moyo wangu uliumia sana ila sikuweza kukataa kwa sababu kuna muda hata mimi nilikuwa nahitaji kumridhisha ila uwezo wa mashine yangu kukaa uwanjani muda mrefu ulikuwa ni mdogo.

Nilikuwa najikuta kwa wiki naweza kuwa uwanjani mara mbili na kupiga bao mbili tu, zaidi nilimuomba mke wangu anivumilie, lakini mke wangu kipenzi alifikia hatua ya kuondoka japo niliweza kupata mtoto moja kutoka kwake.

Kwa kuwa nilikuwa nimeisha pata mtoto kutoka kwa mke wangu wa pili hivyo sikuwa na mawazo ya kutafuta mwanamke mwingine zaidi ya kumuhudumia mtoto wangu.

Maisha yangu yaliendelea vizuri ila kila siku moyo wangu ulikuwa unaniuma sana haswa nilipokuwa naalikwa katika sherehe tofauti na kadi yangu inakuja imeandikwa kuwa nahitajika na mke wangu.

Kutokana na heshima niliyokuwa nayo katika jamii na kazini kwangu, kitendo cha kutokuwa na mwanamke ni jambo ambalo lilikuwa la kushangaza.

Siku moja nikiwa natoka ofisini na rafiki yangu mmoja nilimueleza kinachosababisha wanawake kuniacha, ndipo akaniambia kuwa kuna mtaalamu ambaye anamfahamu anaweza nisaidia ila yupo nchi jirani ya Kenya. Niliomba mawasiliano ya African Doctors na kuwasiliana naye.

Kwa haraka sana niliweza kuongea na African Doctors kisha nikamuomba kufika ofisini kwake, alipangia siku ambayo naweza kumuona, siku ilipofika niliweza kufika ofisini kwake kisha nikapewa dawa na kurudi kwetu Tanzania.

Nilitumia ile dawa kwa siku 14 tu, ndani ya hizo siku mashine yangu kila mara ilikuwa inahitaji kuwa uwanjan kwa ajili ya mechi ya kukata na shoka.

Siku ya kwanza kuingia uwanjani kweli hata mimi nilikubali maana tangu nizaliwe nilikuwa sijawai kuwa uwanjani kwa dakika 90 na zaidi kuweza kucheza mechi tatu ndani ya usiku mmoja.

African Doctors alinieleza kuwa wanashughulika mambo tofauti hasa yanayotokea katika jamii zetu kila siku kama kumrudisha mpenzi aliyekuwacha, kupata mpenzi wa ndoto zako, kusafirisha nyota yako na kurejesha furaha, upendo na amani katika familia.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger