Saturday 29 April 2023

MTOTO WA MIAKA 7 ACHOMWA MOTO NA MAMA YAKE KISA KALA KIPORO CHA WALI



Mikono ya mtoto aliyochomwa moto na mama yake mzazi

Na Suzy Luhende, Shinyanga 

Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga linamshikilia Grace Godwin(23) Mkazi wa Mtaa wa Sido Kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga kwa tuhuma za kumchoma moto mikono yote miwili mtoto wake kwa tuhuma za kula wali.

Tukio hilo lilitokea  April 27, 2023 katika Mtaa huo wa Sido baada ya mama huyo kumchoma moto mtoto wake mwenye umri wa miaka saba anayesoma darasa la kwanza kwa madai ya kula wali uliobaki (kiporo) bila kuruhusiwa.


Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wanamshikilia mwanamke huyo kwa hatua zaidi za kisheria na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.


“Tunamshikilia mtuhumiwa ambaye anaitwa Grace ni mama mzazi wa mtoto anayedaiwa kuchomwa moto mikono yake yote miwili,tukio hili ni baya na vitendo hivyo vya ukatili tunalaani vikali visijirudie”amesema Kamanda Magomi.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Sido Kata ya Ibinzamata Emmanuel Kayange amesema alipata taarifa za tukio hilo na kuamua kufuatilia na kubaini kweli mtoto kachomwa moto na mama yake mzazi kama inavyodaiwa.

Mwenyekiti amesema kutokana na tukio hilo walimuita mama mzazi wa mtoto pamoja na bibi yake Agnes Mgaya na kuwahoji ambapo walibaini mtoto huyo ana siku mbili amechomwa moto wakiendelea kumpa matibabu nyumbani.


Aidha mtoto aliyechomwa moto mikono yote miwili amesema mama yake alimchoma moto kwa kutumia mfuko ambao aliuwasha na kuniwekea mikononi kwa sababu nilikula wali uliokuwa umebaki.

Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Sido wamesema kitendo kilichofanywa na Grace Godwin kumchoma moto mtoto wake kwa madai ya kula chakula ni ukatili mkubwa ambao unapaswa kukemewa vikali ili kukomesha matukio hayo.


Fatuma Ramadhan mkazi wa mtaa huo amesema mtoto aliyefanyiwa ukatili na mama yake mzazi amekuwa akipigwa mara kwa mara na kuiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukubwa wa tatizo kwa kuwahoji mama na bibi wa mtoto huyo.


“Kwa kweli nashindwa kuelewa kwanini watu hawataki kusema ukweli, huyu mtoto anaishi kwa shida anapigwa mno hata ukimuangalia mgongoni na kwenye mikono ana alama za fimbo hili tukio la kuchomwa moto ndilo ambalo limeonekana”, amesema Fatuma.


Shaaban Juma mkazi wa eneo hilo amesema tukio hilo linasikitisha kwani mtoto alikuwa na haki ya kula chakula kwa kuwa hapo ndiyo nyumbani badala ya kuanza kuzunguka mitaani akiomba omba chakula.


Juma amewataka wazazi na walezi kuwa na moyo wa upendo na hofu ya Mungu kwani watu wanaogopa moto, lakini wengine wanachukuwa moto huo na kumchoma binadamu mwenzio ambaye ni mtoto wako jambo ambalo linasikitisha.


Kwa upande wao wadau wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto akiwemo Anascholastika Ndagiwe,amesema mtoto huyo amefanyiwa unyama na mama yake na kuziomba mamlaka husika kuchukuwa hatua kali.


Amesema matukio ni mengi ya ukatili kwa watoto yanafanyika hivyo na serikali inatakiwa kuchukuwa hatua kali kwa watu wanaofanya matukio hayo ili kuyakomesha na kuwawezesha watoto kuishi katika mazingira salama.
Mtoto aliyechomwa moto na mama yake mzazi
Anascholastika Ndagiwe mdau wa kupinga vitendo vyaukatili mkoani Shinyanga





Share:

TCRA YAWATAKA WASFIRISHAJI WA VIPETO KUJISAJILI NA WENGINE KUHUISHA LESENI

*Matapeli kutuma ujumbe mfupi waibukia Viwanja vya ndege


Na Chalila Kibuda,

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imetoa wito kwa wadau wa posta wenye leseni kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu, kanuni na sheria pamoja na kuhuisha leseni zao ili wafanye kazi zao kwa ufanisi na kutambulika zaidi.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Meneja TCRA Kanda ya Mashariki Ikuja Jumanne katika utoaji mafunzo kwa wadau wa posta kupitia kampeni walioanzisha ya kutambua umuhimu wa kukata leseni na ambao bado wakate kwani itawasaidia kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi.

Aidha amesema kuwa elimu hiyo imekuja kutokana na uwepo wa malakamiko ya wateja kupotelewa na vipeto na vifurushi vyao kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha hivyo kutapeli watu na kushindwa kujua wamdai nani.

Hata hivyo amesema kupitia kampeni walioanzisha ya “Tumachapuchapu kwa Usalama “ itawezesha elimu kuwafikia wananchi wengi kupitia vipeperushi, vyombo vya habari, vituo vya usafiri na elimu zinazoendelea kutolewa na TCRA ili kupunguza wimbi la upotevu wa vipeto na vifurushi.

Ameongeza kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) haihusiki tu na usimamizi wa Mawasiliano bali pia wana kitengo cha posta ambacho hushughulikia utumwaji wa vipeto vyenye kilogramu 2 na vifurushi vyenye kilogramu 30 ndani na nje ya nchi kupitia kampuni zilizosajiliwa na mamlaka hiyo.

Amesema kuwa kuanzishwa kwa kitengo hich cha posta kumewezesha ongezeko la pato la taifa kkutokana na kusajiliwa kwa nakampuni hayo ya utumaji vifurushi na vipeto pamoja na kuongeza ajira kwa watanzania.

Kwa upande wao wada wa posta walioshiriki katika mafunzo hayo wamemshukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kwa kuwapatia elimu hiyo ambayo itasaidia kutatua changamoto mbalimbali walizokuwa wanakumbana nazo wakati wa utumaji wa vipeto na vifurushi.

Hatahivyo wameiomba Mamlaka hiyo kuendelea kushirikiana na wadau hao wa posta katika kukabiliana na wimbi la watu wasiofuata taratibu za usajili ambao huwasababishia usumbufu pindi mteja anapopoteza kipeto au kifurushi na kushindwa kujua amdai nani kwani aliowapa watume hawajasajiliwa.

Meneja wa Basi la Gallaxy Magreth Kibiki amesema kuwa wapo watu hawana mabasi lakini wanafanyabiashara ya kusafirisha vipeto na kuleta usumbufu kwao wakati mzigo umepotea na kudai walipwe wakati hawana stakabadhi ya malipo ya basi husika.

Kibiki amesema wananchi wanatakiwa kuwa na uangalifu wa kutuma mizigo kwenda katika kampuni ambazo zinafanya biashara kwa ya kusafirisha vipeto kwa njia ya halali.

Afisa Mauzo na Masoko wa ATCL Hellon anasema kuwa wanapata changamoto na matepeli wanawatumia ujumbe mfupi kuwatumia watu kuwa na mzigo ATCL wakiomba watume fedha ambapo waliotumiwa ujumbe wanatuma na kuanza kufatilia ATCL kupatiwa mzigo na kuleta usumbufu kwao.

Amesema kuna baadhi wanasafirisha mizigo kwenda nje wanatumia mwanya wa abiria wasio na mizigo hali amabayo ni changamoto kwa wenye leseni kukosa kufanya biashara na hao baadhi ya watu wanaotumia fursa isiyo halali kwao.


Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Kanda ya Mashariki Mhandisi Jumanne Ikuja akizungumza na waandishi habari kuhusiana na wasafirishaji wa vipeto kufuata sheria jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya watoa huduma za vipeto wakiwa katika mkutano wa elimu ya utoaji wa huduma hiyo iliyoandaliwa na TCRA Kanda ya Mashariki.

Afisa Masoko na Mauzo wa ATCL Hellon akizungumza kuhusiana na matapeli wanaowatumia watu ujumbe wa mizigo wakati wao wakiwa hawajafanya huduma kwa mhusika ambaye alitumiwa ujumbe, jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Basi la Gallaxy Magreth Kibiki akizungumza kuhusiana na TCRA kuwasaidia kwa watu wanaofanya biasharara ya kusafirisha vipeto bila kusajiliwa, jijini Dar es Salaam.
Share:

GGML YAIBUKA MUONESHAJI BORA KATIKA MAONESHO YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI 2023

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo Afisa Uhusiano wa GGML, Doreen Denis baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi ya kundi la muoneshaji bora katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayoendelea mkoani Morogoro.
Baadhi ya wafanyakazi wa GGML, wakiwa katika picha ya pamoja kufurahia ushindi wa muonesha bora na mbunifu bora katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayofanyika mkoani Morogoro.
Afisa Uhusiano wa GGML, Doreen Denis (kushoto) akimfafanulia jambo mwananchi aliyetembelea banda la maonesho la kampuni hiyo katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayoendelea katika Viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro. Wapili kushoto ni Afisa Mawasiliano Afisa Mawasiliano mwandamizi wa GGML, Laurian Theophil Pima.
Daktari wa Kituo cha Afya cha GGML kutoka Idara ya Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo ya GGML, Dk. Subira Joseph akitoa huduma za matibabu kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la huduma za afya la kampuni hiyo kwenye maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayofanyika mkoani Morogoro.
KATIKA maadhimisho ya siku ya afya na usalama mahali pa kazi yanayoratibiwa na Wakala wa afya na usalama mahali pa kazi (OSHA), Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetangazwa muoneshaji bora (Overall best exhibitor) miongoni mwa kampuni zote zilizoshiriki maonesho hayo mjini Morogoro.

Pia imetangazwa kuwa mbunifu bora wa maonesho hayo yaliyoanza Aprili 26 na kutarajiwa kuhitimishwa Aprili 30 mwaka huu katika viwanja vya Tumbaku mkoani humo.

Kilele cha maonesho hayo yenye kauli mbiu Mazingira Salama na Afya ni Kanuni na Haki ya Msingi Mahali pa Kazi.” kimefanyika Aprili 28,2023 mkoani Morogoro.

Share:

WANANCHI WATEMBELEA BANDA LA CHUO CHA TAKWIMU MASHARIKI MWA AFRIKA WIKI YA UBUNIFU 2023 DODOMA




MKUU wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika, Eusebius Mwisongo,akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la Chuo hicho wakati wa Kilele cha Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


Mhadhiri Msaidizi na Mratibu wa maswala ya Udahili Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika,Samuel Marandu,akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea banda la Chuo hicho wakati wa Kilele cha Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


WANANCHI mbalimbali wakiendelea kupata elimu katika banda la Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika,walipotembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika Dr.Tumaini Katunzi akisaini kitabu Cha wageni katika Banda la Chuo hicho wakati wa Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


WANAFUNZI wakisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembela banda la Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika,wakati wa Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


WASHIRIKI kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda la Chuo hicho mara baada ya kumalizika kwa Kilele cha Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma

Na.Alex Sonna-DODOMA Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika, Eusebius Mwisongo amesema wamebuni mifumo itakayomsaidia mwananchi kufanya shughuli zake kiurahisi ili kuwa na mafanikio kwa haraka.

Hayo ameyasema leo Aprili 28,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Chuo hicho katika Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yanayofanyika uwanja wa Jamhuri Dodoma

Bw.Mwisongo amesema kuwa lengo ni kuujulisha umma umuhimu na faida za mifumo ya TEHAMA inayotengenezwa chuoni hapo.

“Tumekuja na mifumo sita ambayo inahusu ufatiliaji wa magari, mkulima, kufatilia mahudhulio ya wanafunzi na pamoja na mfumo wa vikoba”, amesema Mwisongo.

Ameitaja mifumo hiyo ni pamoja na E- Task Management,Vehicle Management System, e-mkulima,Class Tracking Attendance System, e-management

Ameeleza kuwa Mifumo hiyo inafanya kazi tofauti kulingana na mahitaji ya mteja mfano kwa taasisi za elimu kuna mfumo wa class tracking attendance ambao huonyesha idadi ya wanafunzi walio hudhulia kipindi husika pamoja na mwalimu.

Lakini ameongeza kuwa wana mfumo wa e- task manengment ambao unawezesha mkuu wa kitengo kupanga majukumu kwa watu wake na wahusika hupata ujumbe wa majukumu waliopangiwa na kutekeleza majukumu yao na kuleta taarfa kupitia mfumo huo.

Hivyo ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda lao hili kujua ni mafunzo gani wanatoa na huduma zinazopatikana katika banda lao hususani mifumo katika kuendesha shughuli za kijamii.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 29,2023

























Share:

Friday 28 April 2023

CPB YATANGAZA FURSA KWA WADAU WA MAZAO



Baadhi ya wadau waliokusanyika katika kikao cha wadau wa mazao na CPB kilichofanyika Iringa janaa.
Mkurugenzi wa Biashara na Masoko  wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB)  Evans Mwaning'go akiongea na wadau wa mazao katika kikao kilichofanyika Jana Iringa

Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ( CPB)  Salum Awadh akiongea na wadau wa mazao
 katika kikao cha wadau na CPB kilichofanyika Iringa jana.

Na Mwandishi wetu, Malunde I Blog-IRINGA.

MWENYEKITI wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Salum Awadh ametangaza fursa mbalimbali zinazotolewa na CPB kwa wakulima na wafanyabiashara wa Mazao hapa nchini.

Ametaja baadhi ya fursa zinazotolewa na CPB ni pamoja kilimo cha mkataba ambacho kitaanzia na hekali 1000 na kuendelea.

Akizungumza katika kikao cha wadau kilichofanyika leo Iringa Awadh alisema Kilimo cha mkataba CPB kitakuwa na uwezo mkubwa kutoa maelekezo na ufuatiliaji kwa urahisi.

" Kilimo cha mkataba kitasaidia kuwa na uhakika wa wakulima watakaotuletea mazao, yatakuwa katika ubora"' alisema Awadh.

Mwenyekiti huyo amesema fursa zingine ni pamoja na kuhitaji Mawakala ambao wataingia nao mkataba kwaajili ya uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa CPB na kununua mazao kutoka kwa wakulima na wafanyabishara.

Awadh amesema CPB ni Shirika la Kibiashara la Serikali hivyo linafanya biashara kwa lengo la kuinua Uchumi wa Nchi lakini na mtu mmoja mmoja.

"Biashara ambayo CPB inafanya hatuwezi kumlalia mkulima au mfanyabiashara wa mazao, Sisi lengo letu, Sisi tupate na nyie mpate,alisema Mwenyekiti huyo wa Bodi.

Aidha Awadh amesema CPB ina maghala ambayo hutumia kuhifadhia mazao na bidhaa zao, hivyo wanafanya pia biashara ya kuhifadhi mazao katika maghala hayo ambayo yapo katika Mikoa mbalimbali.

vilevile Mwenyekiti huyo amesema kuwa CPB pia inatafuta masoko kwa Wakulima kama wanunuaji lakini kuwatafutia wakulima na wafanyabiashara kuwa inganisha na masoko ya nje.

" CPB inaongezea thamani mazao kwa kuchakata mazao kama Mpunga, Mahindi, Ngano, Alizeti na Siagi kupitia Viwanda vya CPB vilivyopo katika baadhi ya Mikoa ikiwemo Iringa,"amesema Mwenyekiti huyo akiwataka wafanyabiashara na wakulima wa mazao watumie fursa hiyo ili kuinuana kiuchumi.

Mwenyekiti huyo pia amesema katika kujiimarisha katika uchakataji wa mazao wanatarajia kujenga viwanda vingi zaidi katika Mikoa mbalimbali.

Ametaja Mikoa ambayo tayari kuna viwanda vya kuchakata mazao kuwa ni , Dodoma ambapo kuna kiwanda cha kuchakata Mahindi na Alizeti.

Mikoa mingine ni Arusha kuna kiwanda cha kuchakata Mahindi na Ngano, Iringa kiwanda cha kuchakata Mahindi, Mwanza kiwanda cha kuchakata Mpunga na Dar eslaam kuna Kiwanda cha kuchakata Siagi ya Korosho.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa  Iringa Elia Luvanda  ambaye alifungua kikao hicho aliitaka CPB kuangalia uwezekano wa kujenga kiwanda cha unga wa lishe kwaajili ya wanafunzi mashuleni.

"Unajua ukanda huu wa Nyanda za juu kuna tatizo la watoto kukosa lishe,hivyo niwaombe CPB mbali na kufanya biashara ya mazao,wajenge kiwanda cha kutengeneza lishe ili watoto wetu waondokane na utapiamlo', amesema Luvanda.

VvBjanaJG56ao katika kikao kilichofanyika Jana Iringa

Nnnnm
Hawa no wadau nbNnUeudJh katika kikao cha wadau wa mazao na CPB kilichofanyika Iringa janaa
Share:

UTEUZI: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAADILI

Share:

BODI YA MFUKO WA BARABARA YASHIRIKI MANESHO YA TEKNOLOJIA NA UBUNIFU

Kaimu Meneja wa Mfuko wa Barabara Eng. Rashid Kalimbaga, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mfumo wa ufuatiliaji hali ya barabara unaotumiwa na wananchi katika kutoa taarifa za hali ya barabara, katika kilele cha maonesho ya Teknolojia na Ubunifu jijini Dodoma.
Meneja Msaidizi Utawala na Fedha CPA John Aswile, kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara (wa kwanza kushoto), akiwa kwenye banda la Bodi hiyo baada ya kutembelea maonesho ya Teknolojia na Ubunifu jijini Dodoma.
Bwana Comfort Mgalula kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara akigawa vipeperushi vinavyoelezea matumizi ya mfumo wa ufuatiliaji wa hali ya barabara (BARABARA APP) kwa baadhi ya watoto waliotembelea banda la la Bodi hiyo. Kwenye maonesho ya Teknolojia na Ubunifu jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Agnes Agustine na Joseph Mwabulwa
Bw. Comfort Mgalula kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara akizungumza na Bw. Elibariki Eliud (wa kwanza kushoto) kuhusu utendaji kazi wa mfumo wa ufuatiliaji wa hali ya barabara unaotumiwa na wananchi kupitia simu ya kiganjani katika maonesho ya Teknolojia na Ubunifu jijini Dodoma

Picha na RFB

Share:

RAIS SAMIA AONGEZA PESA MAGOLI YA SIMBA NA YANGA....MAGOLI YA PENATI HAPANA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kuongeza fedha za motisha kwa timu za Simba na Yanga kutoka shilingi Milioni 5 hadi Shilingi Milioni 10 endapo timu hizo zitafuzu kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Simba inacheza mchezo wa marudiano leo dhidi ya Wydad Casablanca nchini Morocco wakati Yanga itacheza mchezo wa marudiano siku ya Jumapili (keshokutwa) dhidi ya Rivers United ya Nigeria katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba inacheza mchezo wa marudiano ikiwa na mtaji wa ushindi wa 1-0 ilioupata katika mchezo wa kwanza wa robo fainali uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam wakati Yanga itacheza mchezo wa marudiano ikiwa na mtaji wa ushindi wa 2-0 ilioupata ugenini huko nchini Nigeria.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anazitakia kila la kheri Simba na Yanga na amewataka wachezaji kujituma uwanjani na kutumia maarifa yao yote kuhakikisha wanashinda michezo ya kukamilisha robo fainali ili wafanikiwe kuingia nusu fainali ambapo kila goli litakuwa shilingi Milioni 10.

Aidha, Msigwa amesema magoli yatakayolipiwa shilingi Milioni 10 ni yale yatakayofungwa katika dakika 90 za mchezo au dakika 120 na sio magoli ya penati.


Chanzo - Michuzi blog
Share:

GGML YAJA NA TEKNOLOJIA ZA KISASA MAONESHO YA OSHA, WANANCHI WAVUTIWA MIFUMO YA USALAMA

Afisa Mwandamizi wa Usalama na afya mahali pa kazi, Sospeter Mkombati akifafanua kuhusu chumba maalumu cha dharura wakati wa uokozi ndani ya mgodi (refugee chamber) ambacho kimebuniwa na kampuni hiyo katika uokozi wa wafanyakazi wake. Chumba hicho kipo kwenye maonesho ya usalama na afya mahali pa kazi yanayoendelea mkoani Morogoro.



NA MWANDISHI WETU

KATIKA kuadhimisha siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani - 2023 ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Morogoro, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imekuja na teknolojia mpya za kisasa katika kudumisha usalama na afya mahala pa kazi hali ambayo imekuwa kivutio kwa wananchi wanaotembelea banda la kampuni hiyo kwenye uwanja wa Tumbaku.

Teknolojia hizo ambazo ni mahsusi kwa afya na usalama wa wafanyakazi wanaofanya kazi migodini, zimetajwa kuwa za kipekee kutokana na ubunifu wa uhakika uliotekelezwa na kampuni hiyo kuleta mageuzi kwenye sekta ya uchimbaji madini.

Akifafanua kuhusu bunifu hizo mjini Morogoro katika banda la maonesho GGML, Afisa Mwandamizi wa Usalama na afya mahali pa kazi, Sospeter Mkombati amesema licha ya kwamba kampuni hiyo ni mdau namba moja wa maonesha hayo, mwaka huu imeamua kuja na vitu tofauti.

Amesema GGML kwa miaka mingi iliyoshiriki maonesha hayo yanayoratibiwa na Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa kazi (OSHA), ililenga kuelimisha umma kuhusu masuala ya usalama mahala pa kazi, lakini safari hii inataka kuwafundisha ili wananchi wanaotembelea banda hilo wakalete mageuzi kwenye kampuni zao.

Amesema teknolojia hizo ambazo GGML imekuja nazo katika maonesho ya mwaka huu ambayo kauli mbiu yake inasema “Mazingira salama na afya ni kanuni na haki ya msingi mahali pa kazi”, zinathibitisha kipaumbele cha kwanza cha kampuni hiyo ambacho ni usalama na afya mahali pa kazi.

Mkombati ametaja teknolojia ya kwanza kuwa ‘Refugee chamber’ ambayo ni chumba maalumu cha dharura ambacho huwekwa ndani ya mgodi chini ya ardhi ili kuwawezesha wafanyakazi waliopo ndani ya mgodi kwenda kukusanyika hapo wakati wakisubiri uokozi mwingine kutoka juu.

“Refugee chamber ni kifaa ambacho hutumia underground kwa kumsaidia mfanyakazi pale kunapotokea ajali mbalimbali labda mwamba umeshuka au ajali ya moto, mfanyakazi badala ya kuhaha namna ya kutoka anakwenda kwenye chumba hicho chenye uwezo wa kuchukua zaidi ya watu 20 huku kikiwa kimesheheni vifaa mbalimbali vya uokozi kama vile mitungi ya hewa ya oksijeni pamoja na mitambo ya kutoa taarifa.

“Kwa hiyo waliopo nje watajua waandae uokoaji wa aina gani kuelekea kwenye chumba hicho ambacho hakiwezi kupenya moto wala mawe ya miamba huko chini ya ardhi,” amesema.

Ameitaja teknolojia nyingine waliokuja nayo kuwa ni ya mifumo ya kudhibiti ajali za moto kwenye magari ambapo sasa magari yote ya kampuni hiyo ikiwamo mitambo, imefungwa mifumo hiyo kwenye injini.

Amesema mifumo hiyo inauwezo wa kutoa maji maalumu kuzima moto wowote unaoweza kutokea ndani ya injini ya gari au mtambo bila dereva kuamuru au kushuka kwenye gari kutafuta kizima moto.

Mkombati ameongeza kuwa teknolojia ya tatu ambayo GGML imekuja nayo kwenye maonesho hayo, ni matumizi ya ndege zisizo na rubani (drone) katika kupiga picha na video ndani ya mgodi ili kutambua usalama wa miamba kabla ya mfanyakazi kwenda kuchimba.

“Wafanyakazi walikuwa wanakwenda kuchimba, muda mwingine ndani ya miamba wanakuta mawe hayajakaa vizuri na kuleta wasiwasi kuhusu uthabiti wa miamba hiyo lakini sasa tumekuja na teknolojia ya drone ambayo huenda ndani kuchukua picha kisha tunaangalia wapi pako salama na sio salama ili kuhakikisha mazingira salama kwa wafanyakazi wetu,” amesema.

Teknolojia nyingine ameitaja kuwa ni ngazi maalumu ya uokozi ambayo inatumika kwenye njia ya dharura wakati wa kujiokoa kutoka ndani ya mgodi mbali na njia kuu ya kuingia na kutoka mgodini.

“Ukiacha chumba cha dharura “refugee chamber”, GGML imebuni njia ya dharura au escape way ambayo ina ngazi za kisasa zinazomuwezesha mfanyakazi anayejiokoa kutoka mgodini kupanda ngazi hizo bila kuteleza lakini pia kila baada ya mita sita anaweza kupumzika maana muda mwingine kunaweza kuwa na umbali wa mita 150 kutoka ndani ya mgodi kuja nje.

“Teknolojia hii inatumia kitu kama drum za plastic ambapo ndani kuna ngazi zisizoteleza na sehemu za kupumzika (platform) hivyo ni teknolojia mpya ambayo makampuni ya sekta hii ya madini yanaweza kuiga na kuitumia,” amesema.

Ofisa huyo mwandamizi wa usalama, pia ameongeza kuwa GGML sasa imekuja na choo maalumu ambacho kimebuniwa kwa ajili ya kuwasitiri wafanyakazi wanaochimba madini ndani ya mgodi.

Amesema choo hicho kinawawezesha wafanyakazi kujisitiri humohumo ndani ya mgodi bila kutoka nje ya mgodi kwenda kujisaidia haja kubwa au ndogo.

“Vyoo hivi vinapelekwa ndani ya mgodi ambapo mfanyakazi anatembea mita chache na kujisitiri. Ni vyoo vya kisasa, vina dawa za kuua wadudu na vikikaribia kujaa vinachukuliwa na mashine kupelekwa nje ya mgodi kusafishwa,” anasema.

Ameongeza kuwa wananchi waliotembelea banda hilo wameeleza kuvutiwa na vifaa hivyo vya ubunifu hali inayozidi kuwaongezea ari wafanyakazi wa kampuni hiyo kuzidi kuzingatia masuala ya usalama na afya mahali pa kazi na kufanya kazi kwa bidii.

Mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML, Novatus Chuwa amesema amejifunza vitu vingi ambavyo ni vigeni, lakini sasa vinamvuti kuchagua kufanya kazi migodini kwa sababu ya uhakika wa usalama mahali pa kazi.

Naye Alice Kyando amesema uwingi wa watu wanaokimbilia kwenye banda la GGML umethibitisha kuwa namna gani kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha mazingira ya kazi yanaandaliwa vema na kumfanya mfanyakazi anafanya kazi mahali salama na kwa kufuata miongozo ya kimataifa usalama na afya mahala pa kazi.
Share:

CHANZO CHA SISI KUHAMISHIWA KWENYE NYUMBA YA SERIKALI GHOROFANI



Wilayani Kyela Mbeya ndipo nilipokulia huko ila kuzaliwa nilizaliwa Tabora mjini pale Cheyo ‘A’ sijui ni lini familia yetu ilihamia huko Kyela kwa kuwa tumeanza kuishi huko kuanzia nikiwa mdogo kabisa. 

Mafuriko ndio changamoto kubwa sana ni sehemu ya familia zote za wanakyela kila mwaka mwezi wanne  angalau familia nyingi huwa zimejiandaa kwa janga hilo la mafuriko.

Mwaka wa 2022 kabla ya kuanza kwa mafuriko tulikuwa na changamoto kubwa sana ya umeme, hakukuwahi kuisha siku nzima bila ya umeme kukatika, mwanzoni tulipata shida lakini baadaye tulizoea na serikali ilitoa tamko kuwa changamoto hiyo ni kwa sababu vyanzo vya maji vimepunguwa sana na mvua zitakapoanza kunyesha vina vya maji vikirejea kila mahali tatizo hili litakwisha, tukavumilia.


Miezi mitatu tu baadaye tukaingia kipindi cha mafuriko awamu hii hali haikuwa shwari kabisa wapo walioingiliwa na mamba, wadudu ndani lakini sisi tuliingiliwa na maji na kila kitu kinachotumia umeme kilikufa palepale choo chetu cha shimo cha nje kilijaa na kufukiwa kabisa tukaanza kuishi bila ya choo, serikali iliamuu kila aishiye mahali pale ahame lakini kwetu hatukuwa na pahali pakukimbilia tulinyong'onyea na kuendelea kuishi hapohapo.


Mafuriko yakaendelea na serikali ikageuka mbogo sasa ikaamua kuwaleta migambo mtaani watutoe kwa nguvu sote tuliokatalia kwenye miji yetu, walifanikiwa wakatufukuza kwa jitihada zao na kwa mabavu.


Baba kichwa cha familia akaanza kupambana kupata haki kupitia marafiki zake wa serikalini na viongozi wadogowadogo wa mtaa lakini haikuleta matunda, kesi dhidi ya Jamhuri ni nzito siyo ya mtu mmoja hakuna aliyetusikiliza.


Miezi saba tukawa tunaishi kama wakimbizi kwenye nyumba za kupanga huku na huko, mpaka pale tulipopata msaada wa daktari BAKONGWA kupitia whatsapp +243990627777.

Mjomba wangu, shemeji wa baba ndiye aliyetupa taarifa hizi kuwa tunaweza kupewa rejesho letu kama tukimpata mtu sahihi wa kutusaidia akamtaja daktari huyo.

Tulimtafuta daktari na kwenye tovuti zake https://bakongwadoctors.com tukatembelea akatupa dawa ya kutusafisha nyota na kuondoa pingamizi tuliporudi serikalini tena waliliona hilo na kutupa haki yetu stahiki walituhamishia kwenye nyumba za serikalini New Forest tena kwenye ghorofa sasa tumeanza maisha mapya na shida za nyuma zote tumesahau, asante sana kwa daktari bakongwa na tiba zako.

 


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger