Thursday 27 April 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 27,2023


Magazetini leo Alhamisi April 27 2023

Share:

Wednesday 26 April 2023

WATU WALIOGOPA KUMSOGELEA; RAIS SAMIA AKAMSHIKA MKONO NA KUOKOA MAISHA YAKE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitazama maendeleo ya mkono wa Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye ni mkazi wa Nyakanazi Mkoani Kagera mara baada ya kuzungumza naye na kumpa Mkono wa Eid Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Samia aligharamia matibabu ya mtoto huyo kwa muda wa miezi sita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.


* Hatimaye, ndoto ya mtoto Hamimu ya kukutana na Rais yatimia

* "Ni mimi" Rais Samia alimwambia mtoto huyo baada ya kushindwa kuamini macho yake alipofika Ikulu

Mwandishi Wetu

HAYAWI, hayawi... sasa yamekuwa. Ndoto ya mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) aliyokuwa akiililia kwa muda mrefu ya kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan hatimaye imetimia. 

Hamimu, ambaye alilazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili kwa miezi 6 akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa ngozi kwa ufadhili wa Rais Samia, aliinama chini na kijishika kichwa baada ya ombi lake la kukutana na Rais kutimia.

Mtoto huyo aliomba akutane na Rais kumshukuru kwa kuokoa maisha yake kwa kumpatia matibabu hadi kupona.

Wakati watu walikuwa wanamnyanyapaa na kumkimbia kutokana na ugonjwa wake wa ngozi, Rais Samia alimshika mkono na kukagua mikono yake kwa upendo wa ajabu.

Mwanzo hakutanabahi kuwa aliye mbele yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, lakini baada ya kugundua, mtoto Hamimu alishikwa na hisia kali. 

Mtoto huyo alishikwa na butwaa pale ambapo Rais Samia alipojitambulisha kwake huku akiinama chini bila kuamini.

"Sura inakuja kama ya Mama Samia," alisema Hamimu baada ya kukutana uso kwa uso na Rais.

Rais Samia akamjibu mtoto huyo: "Sasa huyu ndiyo Mama Samia, si ulisema unataka kumuona?"

Huku akiinamisha kichwa chake na kujishika na mikono usoni, Hamimu huku akiwa haamini kama ndoto yake kweli imetimia akamuuliza Rais, kweli "ni wewe?"

Baada ya mtoto huyo kushikwa na butwaa, Rais Samia huku akitabasamu akamuuliza: "Hamimu, vipi sasa? Si ulisema unataka kuniona."

Ndipo Hamimu alipojibu: "Nimefurahi kukuona, Asante."

Hamimu alifika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumshukuru Rais Samia kwa msaada wa matibabu aliompatia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Rais Samia alimuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza wakati wa ziara yake ya kikazi Nyakanazi, mkoani Kagera, tarehe 16 Oktoba, 2022 na kuagiza apatiwe matibabu haraka baada ya familia ya mtoto huyo kuhangaika kwa muda mrefu bila msaada wowote.

Akiwa Muhimbili, Hamimu alisimulia mtihani wa maisha aliopitia akiwa na umri mdogo tu wa miaka 15.

"Nilisikia Rais Samia anapita Nyakanazi na mimi kwetu ni pale pale Nyakanazi. Wazazi walinikataza, wewe usiende na hali hiyo uliyokua nayo watu wanakukimbia. Unaenda kufanya nini, watakupiga," alisema. 

"Kaka yangu akaniambia wewe nenda, itakavyokuwa itakuwa. Ninachojua (Rais) anaweza kukusaidia. Mimi kweli niliamka usiku sana ili wazazi wasinione, maana kama wangeniona wangenikataza."

Hamimu, ambaye wazazi wake walihangaika kumpeleka kwa waganga wa kienyeji na hata kuuza mali za familia bila mafanikio, alikuwa amekata tamaa kama angekuja kupona ugonjwa wake wa ajabu 

Ngozi yake ilikuwa imeharibika, uso wake ukawa hautazamiki hadi watu wazima na watoto wakawa wanamkimbia na alishindwa hata kukunja na kukunjua vidole vya mikono yake kutokana na maradhi hayo.

Wahenga wanasema penye nia pana njia. Rais Samia alipofika Nyakanazi wakati wa ziara yake ya mkoa wa Kagera, alimuona mtoto huyo amekaa pembeni ya barabara akiwa amenyong'onyea akawatuma wasaidizi wake waende kuongea naye wajue tatizo lake ni nini.

Kufuatia ushauri wa daktari, Samia aliagiza mtoto huyo asafirishwe haraka kutoka Nyakanazi hadi hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili iliyopo Dar es Salaam kwa uchunguzi na matibabu.

Siku chache baada ya maagizo ya Rais, Hamimu akaanza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili tarehe 21 Oktoba, 2022 hadi tarehe 19 Aprili 2023, madaktari wake walipomruhusu kwenda nyumbani baada ya matibabu.

Mwisho
Share:

NIMESHINDA MILIONI TISA YA BAHATI NASIBU KWA KUFANYA HIVI

Frank ndilo jina langu mtoto wa kwanza kwenye familia yetu ya waliosoma, mimi tu ndiye niliyekataa shule mapema wenzangu wote ni wasomi tena waliofanikiwa na wenye kazi nzuri maishani mwao.


Kazi yangu kubwa ni kuuza makava ya simu mtaji wenyewe nilipewa na wadogo zangu angalau na mimi nijitafute kidogokidogo huko, mchana nilifanya kazi hiyo lakini kila jioni nilitembelea kwenye mabanda ya casino hususani meridian bet kutafuta bahati yangu huko.

Nimejifunza kucheza mchezo huu wa bahati nasibu kuanzia nikiwa mwenye umri wa miaka kumi na nane mara tu baada ya kuacha shule.

Nimecheza mara nyingi sana na kila nilipokuwa ninajaribu niliishia kuambulia pesa za nauli tu na vichenji vidovidogo.Kabla ya msaada nilioupata kutoka kwa daktari bingwa BAKONGWA hapo nyuma sikuwahi kupata pesa ya maana ya kufanyia lolote katika shughuli zangu za kubet –ninakumbuka pesa kubwa ambayo niliwahi kushinda ilikuwa ni laki nne na nusu tu pesa ambayo haifikiia hata kwenye mtaji ambao wadogo zangu walinipa nijichangechange.

Jumapili mmoja wadogo zangu walinitembelea ili kujuwa biashara zangu za makava zinaendeleaje lakini kwa bahati mbaya hawakunikuta ofisini walikwenda mahali kukaa kunywa ili kungoja giza liingie kisha wakanifuata nyumbani mida ya saa nne na nusu hivi wakati ambao mimi nimetoka kwenye jukumu langu la kubet.Waliponiuilza niliwaambia nilikuwa meridian bet,mdogo wangu hekima alishangazwa na tabia hii akapuuza kisha akasema kwa ujasiri kama unapenda sana kubet angalau ubet kwa akili safisha nyota yako kwa daktari halafu ndio ubet sio kufanya kienyejienyeti tu.


Kisha akanipa tovuti za daktari https://bakongwadoctors.com nilipomtafuta huko kwenye tovuti zake nikakutana na nambari zake za whatsapp +243990627777 nikazichukuwa na kuzipiga.

Daktari akanipa maelekezo na dawa ya kujisafisha kwa muda wa siku mbili kabla ya kwenda kucheza beti, baada ya muda wa siku hiyo nilikwenda huko meridian nakumbuka siku hiyo ilikuwa ni game la arsenal na tottenham msimu jana wa 2022 mzunguko wa pili, niliweka bet yangu na kumpa hotspurs kisha nikaenda zangu nyumbani.


Siku ya pili baada ya kuisha siku ya kubeti nilipigiwa simu na meneja wa meridian akinitaka nimfuate ofisini kwao HQ dar es salaam na wao wakanikabidhi donge langu nono, nilikuwa nimeshinda milioni tisa za kitanzania.

Kwa uwezo wangu ule wa kubashiri na kwa nguvu ya dawa za daktari nilizotumia meneja akashawishika sana na mimi akaamuwa kuniajiri hapohapo ili niwe mpanga odds kwenye bet zake sasa nina kila kitu kama wadogo zangu walivyo ninasema asante kwa daktari.


Share:

RAIS SAMIA ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 59 YA MUUNGANO





Share:

RC DODOMA ATAKA BUNIFU ZOTE KUINGIZWA SOKONI ZIKATATUE CHANGAMOTO KATIKA JAMII


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano VETA Bw.Sitta Peter mara baada ya kutembelea banda la VETA wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la VETA wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Wanafunzi na wananchi mbalimbali wakipata maelezo katika banda la VETA wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.





Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la VETA wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akiwa ndani ya gari akiendeshwa na wanafunzi waliobuni gari mara baada ya kutembelea Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akizungumza na washiriki wa maonyesho (hawapo pichani) mara baada ya kutembelea na kukagua Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi -VETA Ndg.Abdallah Ngodu,akielezea bunifu zinazofanywa na VETA katika Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Maulilio Kipanyula,akizungumzia Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akigawa Vyeti pamoja na zawadi kwa washindi wa bunifu zao ambazo zimeshindanishwa na kukidhi viwango Vilivyotolewa na VETA wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa bunifu mbalimbali walioshinda wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna -DODOMA


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule amekoshwa na bunifu mbalimbali zilizopo katika maonesho ya wiki ya ubunifu huku akiwaomba watanzania kufika katika uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kujionea.

Wiki ya ubunifu inawakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi na ilianza Aprili 24,2023 katika uwanja wa Jamhuri na yanatarajia kumalizika Ijumaa Aprili 28 mwaka huu.

Akizungumza leo,Aprili 25,2023 mara baada ya kutembelea mabanda,Mkuu huyo wa Mkoa amesema ameshuhudia mambo makubwa ambayo yamefanywa na wabunifu hao.

Ametoa shime kwa watanzania wengine kufika kwenye mabanda hayo kwa ajili ya kujionea bunifu hizo.

RC Senyamule amesema mambo mazuri aliyoyaona ni kijana mmoja kwenye banda la VETA ambaye ametengeneza miwani ambayo dereva akivaa kama akisinzia inamkumbusha kwa kupiga kengele kwa kumwambia asisinzie.

"Tunafahamu kwamba Serikali imekuwa ikihangaika muda mrefu jinsi gani ya kuzuia ajali sasa kijana wa kitanzania ametupatia ufumbuzi tunaimani teknolojia hiyo itaendelea kitumika kupunguza ajali nchini,"amesema Senyamule.

Amesema ubunifu huo ni wa kipekee kwani utasaidia sana hasa kwenye suala la usalama.

Aidha amesema pia amefurahishwa na banda la DIT ambao wametengeza gari linalotumia gesi.

"Na wamesema wameishaunganisha mfumo wa gesi kwenye magari mengi zaidi 2000 nimekuwa nikisikia leo nimejionea, inapunguza gharama za mafuta kwa zaidi ya asilimia 50,"amesema

Amesema kitu kingine kilichomfurahisha ni shule moja ya Arusha wametengeneza gari la kutumia solar.

"Nimeona mabadiliko makubwa ya matumizi ya teknolojia na ubunifu mkubwa,nipongeze sana Wizara ya Elimu kwa kazi nzuri mnayofanya,"amesema RC Senyamule.

Aidha,RC Senyamule amesema maonesho hayo yamepiga hatua kwani ni halisi na kila mwaka yanaendelea kupiga hatua.

"Tumeweza kushuhudia baadhi ya bidhaa ambazo zinaweza kutumika katika maisha yetu ya kawaida majumbani na maofisi.

"Kwa ujumla mimi nipongeze sana Serikali,nipongeze Wizara ya Elimu na taasisi zote ambazo zimeshiriki maonesho haya kwani yameendelea kuongeza thamani,"amesema RC Senyamule.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi -VETA Ndg.Abdallah Ngodu amesema kuwa maonesho ya wiki ya Ubunifu kwa mwaka huu yamekuwa tofauti sana kwani wamepewa nafasi ya kuwa na siku maalumu kwa ajili ya VETA ambayo imekwenda kwa jina la "VETA DAY"

Amesema wameandaa vitu mbalimbali kutoka katika vyuo vya Veta.

Amesema wamekuwa na matukio muhimu ikiwemo mdahalo kwa ajili ya umuhimu wa elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi- katika ubunifu.

"Mdahalo huo utasimamiwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ndugu Gerson Msigwa,"amesema.

Amesema wamekuwa na mashindano ya umahiri wa vijana ambao wanapata mafunzo katika vyuo vyao.

Ameeleza kuwa vijana hao wameshindanishwa katika fani za ujenzi,Umeme na urembo.

Amesema wanalenga kujua vijana wamepata ujuzi na wameweza kumudu stadi zipi.

"Kutokana na tukio hili wamependekeza kwamba itakuwa endelevu na hao watakaoshinda watapata tuzo na vyeti,"amesema Ngodu.

Amesema mashindano hayo wamewashirikisha vijana waliohitimu au wale ambao ni wanufaika ambao wamekuja kuonesha kazi wanazofanya.

"Bahati nzuri katika hawa vijana waliomaliza vyuo vyetu wapo ambao wamaliza vyuo vikuu lakini kutokana na mazingira magumu ya ajira basi wamekuja VETA na wameweza kutengeneza vitu mbalimbali,"amesema Mkurugenzi huyo.

Aidha ametoa wito kwa wananchi wafike katika uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kujionea kazi zinazofanywa na Veta.

"Sasa hivi tunatakribani vyuo 50 Nchi nzima ambavyo vinatoa mafunzo na Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kujenga vyuo na kutakuwa na vyuo zaidi ya 140 maana yake kila Wilaya itakuwa na chuo,"amesema Mkurugenzi huyo.

Ngodu amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa wananchi kupata stadi za ujuzi ili waweze kujiajiri.


Naye Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Prof.Maulilio Kipanyula amesema kuwa Maonesho ya wiki ya Ubunifu mwaka 2023 yamekuwa tofauti kwani imeanzi katika ngazi za mikoa na huko wabunifu walianza kuonesha bunifu zao katika ngazi hizo na sasa maonesho hayo yamefikia katika ngazi ya taifa hivyo imewapa nafasi wabunifu wengi kuonesha bunifu zao.

Prof. Kipanyula ameongeza kuwa katika maonesho hayo kutakuwa na siku maalumu kwa ajili ya Taasisi za VETA na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC)

"VETA leo wameonesha bunifu zao na ndio maana leo ni VETA DAY dhumuni ni kuona ni namna gani uwekezaji uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika elimu ya ufundi imefanyiwa kazi na kuzalisha wabunifu wenye uwezo wa kuigiza sokoni bunifu kwa ajili ya kutatua changamoto za jamii,"

Na kuongeza kuwa "kwa upande wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) nao watakuwa na TAEC DAY ambapo dhumuni la siku hiyo ni kuifanya Tume hiyo ijulikane na wananchi ,majukumu yake ni yapi, nini faida yake na mengine mengi ambayo yataelezwa.

Prof.Kipanyuka amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ili kujionea bunifu mbalimbali ambayo zimebuniwa na wabunifu wa ndani huku ikichagizwa na wabunifu kutoka nchini Afrika Kusini kwani lengo la serikali na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ni kuifanya wiki ya Ubunifu Tanzania kuwa ya kimataifa.
Share:

CHUO CHA TAIFA CHA UTALII (NCT) CHAFANYA MDAHALO KUADHIMISHA MIAKA 59 YA MUUNGANO




Kaimu Mkuu wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt. Florian Mtey akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya kufungua rasmi Mdahalo wa maadhimisho wa sherehe za miaka ya 59 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Chuo hicho Jijini Dar es Salaam.

Mkufunzi katika Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt. Naiman Mbise akizungumza alipokuwa akitoa mada iliyohusu kutengeneza Viwango ili kutoa Huduma bora katika Seka ya Utalii.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Idara ya Sayansi, Siasa na Utawala wa Umma, Dkt. Richard Mbunda akitoa mada iliyohusu Umoja na Mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu katika Sekta ya Utalii.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Taaluma, Tafiti, na Ushauri Bi. Jesca William akizungumza alipokuwa akitoa salamu za utangulizi na kuwatambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria Mdahalo huo.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

Kaimu Mkuu wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt. Florian Mtey amesema katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Sekta ya Utalii inaendelea kuchangia pato la Taifa, tayari chuo hicho kimeanza kutekeleza Programu mbalimbali ili kuendana na uhitaji wa soko la ajira nchini. Dkt Mteyi ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa Mdahalo wa maadhimisho wa sherehe za miaka ya 59 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo amesema kwa mwaka 2022 pekee Sekta ya Utaii imefanikiwa kukusanya Dola za Kimarekani Bilioni 1.4. Amesema fedha hizo zimetokana na matunda ya Filamu ya ‘Tanzania – The Royal tour’ iliyozinduliwa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na mambo mengine, Watalii wameendelea kuongezeka kutoka Mataifa mbalimbali na kuongeza mchango wa Pato la Taifa (GDP). ”Tangu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan azindue Filamu ya ‘The Royal Tour’ tumeona wawekezaji wengi wamemiminika katika mbuga zetu, haya ni matunda ya ile Filamu na sisi kama Chuo tunaendelea kuunga mkono jitihada hizi hasa kwa kushirikiaa na wadau pamoja na Sekta Binafsi” Amesema Dkt. Mtey. Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Idara ya Sayansi Siasa na Utawala wa Umma Dkt. RIchard Mbunda amesema muungano umeleta faida katika Sekta ya Utalii ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa masoko hasa kwa wawekezaji wanaowekezaZanzibar na Tanzania Bara. ”Muungano huu umewasaidia sana wawekezaji hasa kweye upande wa masoko ndmana leo watalii wanaenda Zanzibar lakini wamefikia Dar es salaam au wengine wanaenda kutalii katika visiwa vya Zanzibar lakini wamefikia Dar es salaam” Amesema Dkt Mbunda. Itakumbukwa kuwa mwaka 2015 hadi 2020 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Tanzania Bara zilifanya vikao takribani 85 kujadili kero mbalimbali za Muungano ambapo katika vikao hivyo kero 18 ziliibuliwa huku kero 11 zikipatiwa ufumbuzi.
PICHA MBALIMBALI ZA WASHIRIKI
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger