Tuesday 4 April 2023

WIZARA YA ARDHI YAFUTURISHA WATUMISHI WAKE

Na Munir Shemweta, WANMM


Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewafuturisha watumishi wake waliopo Wizarani na ofisi ya Kmishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dodoma.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na Naibu wake Geofrey Pinda waliwaongoza viongozi wa wizara hiyo kujumuika na watumishi katika futari iliyofanyika tarehe 3 April 2023 jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa futari hiyo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula aliwaeleza watumishi kuwa, uamuzi wa kuandaliwa futari ya pamoja unalenga kuwaweka pamoja watumishi wa wizara hususan kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kwa rezma.

‘’Uamuzi wa kuandaa futari ya pamoja unalenga kuwaweka pamoja watumishi wa wizara yetu na ninaomba tuwe na umoja na kushirikiana katika kazi zetu’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Geofrey Pinda alishukuru uamuzi wa Wizara kukutanisha pamoja watumishi kuanzia ngazi ya chini hadi juu jambo alilolieleza kuwa ni nadra sana kutokea watumishi kukutana kwa wakati mmoja kuanzia kada ya chini hadi juu.

‘’Nishukuru uamuzi wa kuwakutanisha watumishi wa sekta ya ardhi pamoja maana ni nadra sana watumishi wa wizara kuanzia kada za chini hadi juu kukutana kwa mara moja’’ alisema Pinda

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anthony Sanga alihimiza watumishi wa sekta ya ardhi kuwa na umoja wakati wote wa utendaji kazi.

Aidha, aliwaeleza watumishi wa wizara ya ardhi kuwa, wizara hiyo kwa sasa iko kwenye juhudi za kuboresha mifumo yake ya ulipaji kodi ya pango la ardhi ambapo alieleza kuwa mfumo huo utakapokamilika wamiliki wa ardhi nchini watakuwa wakipata ujumbe utakaowawezesha kulipa kodi bila kufika ofisi za ardhi.


Hii ni mara ya kwanza kwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuandaa futari ya pamoja ya watumishi wake tangu serikali ilipohamia rasmi mkoani Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa futari ya pamoja ya watumishi wa wizara ya ardhi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 3 April 2023. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Lucy Kabyemera na katikati ni Kaimu Mkuu wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Ardhi Isabela Chilumba.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anthony Sanga akiwaongoza watumishi wa wizara ya ardhi kupata futari ya pamoja jijini Dodoma tarehe 3 April 2023.
Sehemu ya watumishi wa wizara ya ardhi wakipata futari ya pamoja tarehe 3 April 2023.






Watumishi wa Wizara ya Ardhi wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa futari ya pamoja ya watumishi wa wizara hiyo jijini Dodoma tarehe 3 April 2023.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda akizungumza wakati wa futari ya pamoja ya watumishi wa wizara ya ardhi jijini Dodoma tarehe 3 April 2023.
Kamishna wa Ardhi nchini Nathaniel Methew Nhonge akitoa neon la shukran wakati wa futari ya pamoja ya watumishi wa wizara ya ardhi jijini Dodoma tarehe 3 April 2023.
Share:

AUAWA KWA KUPIGWA JIWE AKINYWA POMBE BAA MJINI SHINYANGA, MWINGINE AKIIBA MAHINDI SHAMBANI


Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Watu wawili wamefariki Dunia katika matukio mawili tofauti yaliyotokea katika Manispaa ya Shinyanga likiwemo la mwanaume kuuawa akiiba mahindi shambani na mwingine kupigwa jiwe akiwa Baa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu amewataja watu hao kuwa ni Tumaini Manyele Malima mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa mtaa wa Kambarage Manispaa ya Shinyanga na mwanaume mwingine anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 mpaka 40 ambaye hakufahamika jina na makazi yake.




Amesema Tumaini Malima amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Mwawaza baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa jiwe katika sikio la kushoto na Yohana Daniel akiwa Bar ya Heinken mjini Shinyanga wakiendelea kunywa pombe kisha kuanza kupigana.

Kaimu Kamanda Nyandahu amesema tukio la pili ni kuhusu mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 – 40 ambaye hakufahamika jina wala makazi yake ameuawa kwa kushambuliwa baada kukamatwa na wananchi kwa tuhuma za kuiba Mahindi mabichi shambani katika kijiji cha Mwamalili kilichopo Manispaa ya Shinyanga usiku wa kuamkia leo Aprili 4,2023.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Leonard Nyandahu ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi matukio ya uhalifu yanapotokea.
Share:

DITOPILE AGAWA FUTARI KONDOA, ASISITIZA KUIOMBEA NCHI NA KUMUOMBEA RAIS SAMIA



Katika Muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile amegawa Futari kwa Wazee, Wajane na watu wasio jiweza Wilaya Kondoa Mkoani Dodoma.


"Kwa imani yetu miezi yote ni bora lakini mwezi mtukufu wa Ramadhani ni bora zaidi, na pia tunaambiwa katika mwezi huu dua yoyote utakayoiomba mbingu ziko wazi na Mwenyezi Mungu ametukumbusha kupitia suratul Insan aya ya 8 tuwafuturishe kile tunachokipenda"

Ameongeza kuwa huu ni utaratibu ambao anautumia mwezi huu mzima kuzunguka Mkoa wa Dodoma kufanya zoezi hilo.


"Nimetumia mwezi huu wa Ramadhani kuzunguka Mkoa wote wa Dodoma kufuturisha, nimeanza pale Dodoma mjini kwa kufuturu na yatima na wajane zaidi ya 300 na kisha kuwapa sadaka, nimeshafuturisha wilaya za Bahi, Kongwa na leo nipo Kondoa. Pale Kongwa nilienda kijiji cha Mkoka pamoja na futari na nilienda kutembelea shule ya watoto wenye uhitaji maalum, ambako wapo watoto wadogo wenye ulemavu lakini walikuwa wamefunga"


Pia Mbunge Ditopile amewaomba kuendelea kuiombea Nchi na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.



"Sisi ni viongozi mmetuamini lakini juu yetu yupo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, mama Samia amepewa majukumu ya kutuongoza na Mwenyezi Mungu, hata majukumu yake ya kifamilia ameyasahau kidogo na muda mwingi anahangaika na wananchi wa Kondoa, Kasulu na kila mahali nchini leo, anawaza leo nipeleke mradi wa maji wapi, leo nipeleke mradi wa umeme wapi ni na dhamira yake njema ya kuwatumikia Watanzania wapo ambao hawaipendi, hasad haikosekani katika jambo lolote linaloambatana na neema, ili hasad isimkute ni jukumu letu sote kumuombea kwa Mwenyezi Mungu"




Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe Mariam Ditopile anaendelea kuwatakia Waislamu wote nchini Ramadhani njema.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRILI 4, 2023





















Share:

Monday 3 April 2023

ALIYESHINDA TSH MIL 54 KASINO YA MTANDAONI ATOA SIRI



Mchezo uupendao kuna Aviator, Poker, Titan Roulette na mingine mingi. Kujisajili bonyeza hapa https://a.meridianbet.co.tz/c/GLd6O8

 

 

Safari moja huanzisha nyingine ni usemi ambao unafanya kazi haswa kwa majokeri ambao huishi kwa kutegemea ubashiri wa Soka unaopewa odds kubwa, au Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet yenye Sloti nyingi pendwa na rahisi kushinda kama vile Aviator, Poker na Titan Roulette.

 

Moja ya mtu ambaye atakua ni shahidi kwenye hili ni Mwarabu mkazi wa Dar Es Salaam ambaye Meridianbet wamemtanganza kuwa mshindi mkubwa wa Tsh 54,700,000/= (Milioni Hamsini na Nne na Laki Saba) ambapo alicheza dau dogo la Elfu Hamsini tu (50,000/=) kupitia kasino ya mtandaoni hii ni bahati iliyoje.

 

Gwiji huyu ambaye majina yake kamili yamehifadhiwa alicheza sloti ya 100 Burning Hot inayopatikana kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet, sloti hii inalipa sana kwani ushindi ni rahisi kuupata kwa dau dogo tu la kuanzia Tsh 100/=

 

Alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu ushindi huo alijibu “Najisikia furaha sana mwanzoi nilikua nikicheza nakula pesa ndogo ndogo hatimaye leo nimepiga mkwanja huu wa Mamilioni. Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet haijawahi niangusha hata siku moja ndiyo maana nacheza kila siku”

 

“Naipenda sloti ya 100 Burning Hot kwa sababu inanipa sloti nyingi za kucheza na zote ni rahisi” Mshindi wa Milioni 54

 

Sloti ya 100 Burning Hot ni miongoni mwa michezo pendwa ya kasino inayotoa mkwanja muda wowote, lakini pia sloti nyingine rahisi kushinda ni Aviator, Poker na Titan Roulette yote unaipata kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet kupitia www.meridianbet.co.tz

 

 

Je Unahitaji kufahamu Sloti hii Inakuaje?

 

100 Burning Hot ni sloti rahisi sana kuicheza ina mistari 5 ya ushindi huku kukiwa na mingine 100 ya ziada, sloti hii inakuja na machaguo mengi ya ushindi kama vile namba 7, alama ya dola, na alama ya ushindi mkubwa kabisa ya “Wild’ hiyo inakupa bonasi ya kushinda mara nyingi. Cheza sasa kwa dau dogo la kuanzia Tsh 100/=  kubwa Zaidi Sloti hii inakupatia mizunguko 100 ya bure.



Share:

Video : YALEO KALI - FAGILIA YA ANITHA

 

Share:

LEMBELI ASHIRIKI SHEREHE YA MWANZILISHI WA TAASISI YA JANE GOODALL NCHINI MAREKANI

Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kahama-James Lembeli ( maarufu Ng'wana Maria) katika picha kwenye hafla ya kumpongeza Mwanzilishi wa Taasisi ya Jane Goodall Dk. Jane Goodall na Balozi wa heshima wa Umoja wa Mataifa wa Amani kutimiza miaka 89 iliyofanyika katika Hotel ya Litz Carlton, New York - Marekani iliyohudhuriwa na wanasayansi,wahifadhi,Wana mazingira na viongozi mbalimbali duniani.


Dk. Jane Goodall alifika Tanzania, wakati huo Tanganyika mwaka 1960 na kuanzia utafiti wa wanyama aina ya Sokwe katika hifadhi ya Gombe utafiti ambao unaendelea mpaka leo.

Katika ghafla hiyo,watu mbalimbali walimtakia Jane Goodall afya njema na maisha marefu.
Pia walimpa zawadi ikiwa pamoja pesa,ambazo zote zitapelekwa Gombe, Kigoma kuendeleza kazi za utafiti na uhifadhi katika Hifadhi hiyo nchini Tanzania.
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kahama, James Lembeli akizingumza na Dk. Jane Goodall.
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kahama, James Lembeli katika picha ya pamoja na baadhi ya waalikwa.
Share:

Video Mpya Kaliii!! LIMBU LUCHAGULA - MUNGU WANGU

 

Share:

Sunday 2 April 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 3,2023





























Share:

JAMES LEMBELI AENDA NEW YORK, MAREKANI

 
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kahama-James Lembeli ( maarufu Ng'wana Maria) amendoka nchini mwishoni mwa wiki iliyopita kwenda New York nchini Marekani.


Akiwa mjini,humo Lembeli alitarajiwa kuhudhuria sherehe maalum ya kutimiza miaka 89, muasisi wa taasisi ya Jane Goodall ambayo chimbuko lake ni  Hifadhi ya Taifa ya Gombe,Kigoma ambako alifika mwaka 1960 kuanzia kufanya utafiti wa mnyama aina ya sokwe.


Utafiti huo wa Sokwe,umedumu Kwa zaidi ya miaka 60 na unaendeshwa na taasisi hiyo ya Jane Goodall ambao hivi Sasa unaendeshwa na watanzania.


Jane Goodall,raia wa Uingereza pia ni Balozi wa heshima wa Umoja wa Mataifa wa Amani.


Sherehe hiyo,ilihudhuriwa na wanasayansi na viongozi mashuhuri mbalimbali wa nchini Marekani.


Aidha Lembeli atahudhuria kikao cha Bodi ya Wakurungenzi ya Jane Goodall-Marekani ambako yeye ni mjumbe pekee toka Afrika.


Taasisi ya Jane Goodall ambayo Ina ofisi katika nchi zaidi 100 ulimwenguni inajihusisha hasa na utafiti na uhifadhi wa Sokwe barani Afrika na jamii ya wanyama aina ya nyani.


Nchini Tanzania,mbali ya utafiti katika Hifadhi ya Gombe,taasisi hiyo inaendesha miradi mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira hasa misitu ya asili sambamba na miradi ya afya na maendeleo ya jamii ktk mikoa ya Kigoma na Katavi.


Lembeli,ambaye ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo hapa nchini aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira ambaye ripoti yake juu ya madudu yaliyojitokeza katika utekelezaji wa operesheni tokomeza ilipelekea mawaziri watatu kutumbuliwa na mmoja kujiuzulu.


Lembeli anatarajiwa kurudi nchini tarehe 13.4. 2023.

Share:

YANGA SC YAICHAPA TP MAZEMBE 1-0 UGENINI


**********************

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Yanga imefanikiwa kuondoka na ushindi kwenye mechi yake ya mwisho hatua ya makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufanikiwa kuichapa TP Mazembe kwa bao 1-0 , mchezo uliopigwa nchini DR Congo.

Yanga SC imefanikiwa kupata bao kipindi cha pili likifungwa na kiungo mshambuliaji Farid Musa ambaye aliingia akitokea benchi akipihwa na Mudathir Yahya mabadiliko ambayoyalizaa matunda.

Yanga sasa inaenda hatua ya Robo Fainali akiwa anaongoza kundi akijikusanyia alama 13 katika michezo sita hatua ya makundi.

Yanga iliwakosa baadhi ya wachezaji kikosi cha kwanza ambapo walimkosa Djidji Diara ambaye ni goli kipa namba moja, Khalid Aucho, Aziz Ki na Morrison .
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger