Friday 31 March 2023

WAZIRI NDALICHAKO AWAPA SOMO WAJASIRIAMALI MTWARA



***************

Na Mwandishi Wetu, Mtwara

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof.Joyce Ndalichako amewaasa wajasiriamali mkoani Mtwara kutumia Mwenge wa Uhuru kama chachu ya kukuza biashara na huduma.

Akifungua maonesho ya biashara, uwekezaji na fursa kwenye viwanja vya mashujaa park Mtwara Machi 30, 2023, Prof. Ndalichako, amesema kupitia Mwenge fursa mbalimbali ziibuliwe na kutengeneza ajira huku akiwapongeza walioona fursa na kuzitumia. Aidha, amelitaka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kuweka mkakati endelevu wa kuwasaidia wajasiriamali hao kupata masoko ya kudumu nchini na nje ya nchi.

“Wajasiriamali kumbukeni kuwa soko la Afrika Mashariki lipo wazi kwa nchi zote wanachama hivyo tuwe wabunifu ili kuweza kulitumia soko hilo na kuonesha ushindani wa bidhaa baina yetu na wenzetu,”amesema.
Share:

RC DODOMA APOKEA TUZO YA RAIS SAMIA NI KATIKA MASUALA YA MAENDELEO YA  ELIMU.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara,Hezbon Mwera ,akimkabidhi Tuzo ya Heshima Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule iliyotolewa na Taasisi ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wake Katika maendeleo ya sekta ya Elimu nchini wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw Ally Gugu.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara,Hezbon Mwera ,akimkabidhi Tuzo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule kwa kumpongeza yeye pamoja na wasaidizi wake katika kuongeza ufaulu mkoani humo iliyotolewa na Taasisi ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara,Hezbon Mwera,akielezea tuzo zilizotolewa na taasisi hiyo kwa viongozi kwa kutambua mchango wa Elimu nchini wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.


MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mh. Rosemary Senyamule,akiipongeza taasisi hiyo kwa kazi nzuri inazofanya katika sekta ya elimu kwenye mikoa mbalimbali nchini wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.


KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw Ally Gugu,akizungumza wakati wa Mkutano wa wadau wa Sekta ya Elimu katika Mkoa wa Dodoma.




Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara,Hezbon Mwera ,akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule ,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw Ally Gugu wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.


SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.



Na.Alex Sonna-DODOMA

TAASISI ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara inayojishughulisha na masuala ya elimu imempa tuzo Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kutokana na mchango wake katika maendeleo ya sekta ya elimu nchini.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mh. Rosemary Senyamule na Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Hezbon Mwera Machi 30, 2023 katika mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Prof. Mwera,Mkurugenzi wa Taasisi hiyo,Hezbon Mwera amesema kwa kutambua jitihada na mchango katika sekta ya elimu unaotolewa na Rais Samia wameamua kumpa tuzo hiyo ya heshima.

Amesema Taasisi hiyo inajishughulisha na mambo ya kijamii na wamepewa kibali na ofisi ya Tamisemi kufanya shughuli zao ndani ya Mikoa 10 ya Tanzania.

Amesema shughuli wanazozifanya ni pamoja na kuhamasisha vijana kujiunga na vyuo vya ufundi kwani kila mmoja anajua umuhimu wa vijana kupata mafunzo ya Elimu ya ufundi baada ya kumaliza darasa la saba na kidato cha nne wakati wakisubiri matokeo.

"Nipende kumpongeza Rais Samia kwa kuanzisha vyuo katika kila Wilaya.Taasisi yetu hii pia inashirikiana na Ofisi za Mikoa kutoa tuzo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa ya darasa la saba, kidato Cha nne na sita,"amesema

Mkurugenzi huyo wa Taasisi hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Ufundi Kanda ya Ziwa, amesema wametoa tuzo katika Mikoa ya Mwanza,Kigoma,Simiyu,Shinyanga,Geita ,Mara.

Pia alimkabidhi tuzo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule kwa kumpongeza yeye pamoja na wasaidizi wake katika kuongeza ufaulu mkoani humo.

Tuzo za jumla zilizotolewa katika hafla hiyo zilidhaminiwa na taasisi ya ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara.

Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mh. Rosemary Senyamule,ameipongeza taasisi hiyo kwa kazi nzuri inazofanya katika sekta ya elimu kwenye mikoa mbalimbali nchini.



RC Senyamule amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya jitihada kubwa kuhakikisha watoto wote wanaenda shuleni na matarajio ya Serikali ya awamu ya sita ni kuona elimu bora inatolewa pamoja na changamoto zote zinatatuliwa.

"Ili Mkoa uweze kusonga mbele kielimu ni lazima tuhakikishe watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa na wanahudhuria shule wakati wote,"amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

Mkuu huyo wa Mkoa ameupongeza Mkoa huo kwa kushika nafasi ya 10 kitaifa kwa matokeo ya mwaka 2022.

"Niendelee kusisitiza yale tutakayokubaliana tukayatekeleze,niwaombe tuzidi kupambana kuhakikisha tunafanya vizuri,"amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

Naye,Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw Ally Gugu,amesema wataliendeleza tukio hilo na litakuwa la kila mwaka.

Amesema ili ipatikane Dodoma yenye maendeleo lazima wawe wamoja katika kusimamia ubora wa elimu.

Amesema lengo la kikao hicho ni kuangalia namna bora ya kuongeza ubora wa elimu mkoani humo na kuongeza ufaulu wa Kitaifa.

Ameyataja malengo ya Mkoa ni kutoka katika asilimia 83.01 mwaka 2022 hadi 85 kwa mwaka 2023 katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.

Amelitaja lengo la pili ni kutoka asilimia 91.27 mwaka 2022 Hadi 100 mwaka 2023 katika upimaji wa elimu kitaifa katika darasa la nne.
Share:

TCRA KUKAGUA VIFAA VYA MAWASILIANO NJE YA NCHI


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) John Daffa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na vifaa vya mawasiliano kukaguliwa kabla ya kuingia nchini , Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waagizaji wa vifaa vya Mawasiliano wakifatilia agizo kwenye mkutano , jijini Dar es Salaam.

******************

*Kazi ya Ukaguzi inafanywa na wakala waliongia mkataba

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuanzia Mei 23, mwaka huu vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki vinavyoingizwa nchini vitatakiwa kukaguliwa kwenye nchi vinakoagizwa ili kuepusha kuingiza vifaa vilivyokwisha muda wa matumizi.

Aidha, imewataka watengenezaji na waingizaji wa vifaa hivyo, kulipa ada ya usimamizi wa taka za kielektroniki kwa kila kifaa kinachoingizwa kama gharama za usimamizi wa vifaa hivyo vinapofika mwisho wa matumizi.

Hatua hiyo ni katika kutekeleza maazimio ya mkutano wa tano wa Taasisi za Mawasiliano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACO) kudhibiti ongezeko la taka za kielektroniki.

Akizungumza katika mkutano uliowakutanisha Wasambazaji wa vifaa vya kielektroniki Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, John Daffa alisema kuwa kanuni za ubora wa vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki na usimamizi wa taka za kielektroniki za mwaka 2020 zinaelekeza kuhakikisha vifaa vyote vinavyoingia nchini havijafika mwisho wa matumizi.

Pia alisema kanuni hizo zinataka kuhakikisha kuwa vifaa vyote vilivyofika mwisho wa matumizi vinapelekwa kwa watoa huduma wenye leseni za kukusanya taka , kukarabati au kuendesha mitambo ya kuchakatwa vifaa vya mawasiliano pale vinapofika mwisho wa matumizi.

Daffa alisema TCRA ina jukumu la kusajili taarifa za vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki ambavyo vimeingizwa au kutengenezwa nchini pamoja na kuweka makubaliano na watoa huduma waliopewa leseni kwa ajili ya kukusanya na kuendesha mitambo ya kuchakatwa taka za kielektroniki.

"Kuanzia Mei 23 mwaka huu maombi yote 6a kuingiza vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki yatawasilishwa kwa njia ya mtandao kupitia https://ift.tt/ylc9EdX ili kuwezesha uwasilishaji wa taarifa zote za vifaa vinavyoingizwa," alisema Daffa.

Alieleza kuwa baada ya maombi yao kupokelewa, uchambuzi na tathmini kuhusiana na vifaa vitakavyoingizwa pamoja na ada ya usimamizi wa taka za kielektroniki itafanyika ili kuruhusu hatua za utekelezaji.

Alifafanua kuwa uingizaji wa vifaa vya mawasiliano nchini unahitaji leseni tofauti yaani Importation License na vifaa vyote vitakavyoingizwa nchini vinatakiwa kuhakikiwa ili kutathmini ulinganifu na mwingiliano wakati wa matumizi.

Hata hivyo, alisema kuwa mtumiaji wa vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki hatahusika katika gharama hizo na kwamba hakutakuwa na ongezeko la gharama za ununuzi wa vifaa hivyo hapa nchini.

Pia alisema suala hilo ni jipya kuanza kutekelezwa nchini licha ya kuwepo kwa kampuni ambazo zilikuwa zinakusanya taka za kielektroniki bila kufuata utaratibu maalum.

Alisisitiza kuwa TCRA itashirikiana na Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa mazingira (NEMC), katika usimamizi wa taka za kielektroniki.
Share:

TASAC MTWARA KUELEKEZA NGUVU ELIMU KWA JAMII



Na Mwandishi wetu, Mtwara 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu)Joyce Ndalichako ametoa rai kwa wananchi wa Mtwara kuzichangamkia fursa za kibiashara zilizopo mkoani humo ili kukuza uchumi.

Ndalichako amesema hayo Mkoani Mtwara wakati akifungua maonesho ya biashara,Uwekezaji na fursa yanayofanyika katika viwanja vya mashujaa kuanzia Machi 19 hadi Machi 31,mwaka huu.

 Amesema kuwa Mkoa huo unakuwa kwa kasi kiuchumi hivyo ni vyema kila mwananchi akatambua kuwa hiyo ni fursa katika kukuza uchumi kibiashara.

"Maonesho haya ya Biashara, Uwekezaji na Fursa  ni maonesho ya Kwanza kufanyika Mkoani Mtwara yakiwa na lengo la kuwaleta pamoja wadau mbalimbali katika Sekta hiyo ili kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kujifunza biashara na uwekezaji wa kisasa pamoja na fursa zilizopo katika sekta hiyo na Mkoa wa Mtwara kwa ujumla,"amesema Ndalichako.

Aidha  Ndalichako alitumia fursa hiyo kuwakaribisha  wananchi katika uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru utakaowashwa   Aprili 1 mwaka huu katika kiwanja cha Nangwanda sijaona,Mkoani hapo.

Akizungumza  na Vyombo ya habari Kaimu Afisa Mfawidhi wa  TASAC Mkoa wa  Mtwara katika maonesho hayo Mha. Joseph Myaka amesema kuwa katika kutekeleza majukumu yao Shirika hilo limejikita katika kutoa elimu kwa wananchi kufahamu shirika hilo linavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria. 

Amesema kuwa licha ya majukumu makubwa waliyonayo pia TASAC imeshiriki maonesho hayo ili kuwapa elimu wananchi kuhusu  fursa za biashara zilizopo katika Sekta ya Usafiri kwa njia ya Maji  sambamba na elimu kuhusu Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa mazingira majini jukumu linalotekelezwa na Shirika hilo. 

“TASAC tunashiriki maonesho haya ya Biashara Uwekezaji na Fursa mkoani Mtwara ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yanayotekezwa Kisheria kama mdhibiti wa shughuli za usafiri kwa njia ya maji tunasimamia huduma zinazotolewa na Bandari, tunadhibiti na kusimamia ulinzi, usalama na utunzaji wa mazingira na kuratibu shughuli za uokoaji na utafutaji pale panapotokea dhoruba majini,

“Pia tunatoa elimu kwa wananchi wa Mtwara na wadau wa usafiri kwa njia ya maji katika jukumu letu la Udhibiti wa Safari kwa njia ya Maji na udhibiti Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira majini, wanaweza kufanya shughuli zao kwa usalama na kupata maendeleo na kuongeza pato la Taifa,"ameeleza Myaka.

Aidha ameeleza kuwa kwa  mujibu wa Sheria, TASAC ina wajibu wa kusimamia kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhimiza usimizi na shughuli za uwakala wa meli wenye ufanisi, kuhimiza shughuli za bandari na huduma za meli zenye ufanisi, kuhakikisha kunakuwepo usalama na ulinzi wa shehena, kuhimiza na kutunza mazingira, usalama na ulinzi wa bahari, maziwa na mito.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 31,2023



























Share:

Thursday 30 March 2023

NAMIBIA YAVUTIWA NA TANZANIA INAVYOKABILIANA NA TATIZO LA AJIRA



Na Mwandishi Wetu, DODOMA

UJUMBE wa Bunge la Namibia umeimwagia sifa Serikali ya Tanzania namna ilivyojipanga kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana kupitia programu zinazotekelezwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Kiongozi wa ujumbe huo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge hilo ya Rasilimali watu na Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni Mbunge, Mhe. Nono Katjingisua, ametoa pongezi hizo leo Machi 30, 2023 baada ya kukutana na Mofisa wa Ofisi hiyo wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii, Festo Fute.

Mhe.Katjingisua amesema Serikali ya Namibia mwaka 2022 ilikumbwa na tatizo la ajira kwa vijana hivyo hali hiyo imewasukuma kuja Tanzania kujifunza namna inavyokabiliana na tatizo hilo.

“Tumepata maelezo ambayo na sisi tutakaporejea bungeni tutazingatia kama vile kuwa na program ya taifa ya kukuzaji ujuzi ili kuwajengea uwezo vijana kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri au kuajiriwa kulingana na mahitaji ya soko la ajira,tumeona wenzetu wana mfuko wa maendeleo ya vijana ambao unatoa mitaji kwa vijana, tumejifunza mengi,”amesema.

Naye, Mjumbe wa Kamati hiyo ya Bunge, Tjiveze, Herlinde, amevutiwa na Tanzania inavyofanya jitihada mbalimbali za kuwakwamua vijana ikiwamo kutunga sheria ya manunuzi ya umma inayoelekeza asilimia fulani ya zabuni iwe ya vijana na namna inavyowajumuisha vijana wenye ulemavu kwenye fursa zilizopo za ajira.

Awali, akiwaongoza Maofisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu kueleza namna inavyotekeleza program za vijana na uratibu wa ajira, Mkurugenzi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii, Festo Fute, amesema ofisi hiyo ni mratibu mkuu wa masuala ya vijana na kuna sera ya vijana ambayo kwasasa inafanyiwa mapitio ili iendane na wakati.

Share:

PIGA PESA KASINO YA MTANDAONI NA SLOTI YA PUMPKIN PATCH


Jisajili Meridianbet upate mizunguko 50 bure ya kucheza moja ya mchezo wa kasino ya mtandaoni utakaopenda! Kujisajili bonyeza hapa https://a.meridianbet.co.tz/c/RGCCr7


Sloti ya Pumpkin Patch

Hawajawahi kukosea hata kidogo  Meridianbet kutoa bonasi kubwa, Odds kubwa na Promosheni za kumwaga. Wiki hii kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuletea mchezo wa kukata na shoka na utakao kutengenezea faida uitwao Pumpkin Patch.

Pumpkin Patch ni mchezo wenye maudhui ya siku ya Halloween uliotengenezwa na watengenezaji maarufu wa michezo ya kasino Habanero. Licha ya mchezo huu wenye maudhui ya siku maruhani (Halloween), Sloti ya Pumpkin Patch imekuwa ni moja ya mchezo unaopendwa zaidi kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Mchezo huu wa kusisimua una kolamu 5 na mistari 25 ya malipo na kubwa Zaidi unakujia na jakipoti kubwa mbili. Unasubiri nini? Jiunge na familia ya mabingwa ya Meridianbet ili uweze kuwa mshindi.

Namna ya Kucheza Sloti ya Pumpkin Patch

Jinsi ya kucheza mchezo huu wa kasino ya mtandaoni ni rahisi sana. Unachotakiwa kuwafanya ni kubofya kitufe chenye neno *Spin kuanzisha mzunguko ambapo Sloti ya Pumpkin Patch ina alama kuu mbili.

 

Alama ya Boga linalo cheza likiwa kwenye kifukuzia kunguru na alama ya Wild. Ikiwa alama ya Kunguru ikaangukia pembeni ya Boga, itasababisha boga hilo kusambaa kwenye kolamu ya sloti na kutengeneza alama ya ushindi yenye kukuletea malipo ya kiwango kikubwa iitwayo Complex Wild.

 

Kama Kindi (Squirrel) akiangukia pembeni ya Boga, basi Boga hilo litabadilika na kuwa alama ya ushindi ambayo itakutea malipo mara mbili ya mwanzo iitwayo Wild.

 

Ndio! Ni Meridianbet pekee ndio inayo kuhakishia ushindi kwa kukupa Bonasi, Odds kubwa na Promosheni za kipekee. Sio hivyo tu, Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet ya sloti ya Pumpkin Patch inakupa nafasi ya kushinda mizunguko kibao ya bure. Jiunge sasa kupitia  https://www.meridianbet.co.tz na upate bonasi ya bure ya kuanzia.

 


Share:

WATSWANA WAVUTIWA NA MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA TAASISI YA OSHA

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka ya Botswana, Bw.Gopolang Maakwe akizungumza na viongozi wa Menejimenti ya OSHA wakati wa ziara yake ya kutembelea Ofisi za OSHA Dar es salaam akiambatana na baadhi ya watumishi wa Ofisi yake kwa lengo la kuijifunza jinsi taasisi ya OSHA inavyotumia mifumo ya TEHAMA katika usimamizi wa masula ya usalama na afya mahali pa kazi.



Meneja wa Afya wa OSHA, Dkt. Jerome Materu akikabidhi zawadi kwa Kaimu, Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka ya Botswana, Bw.Gopolang Maakwe mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea ofisi za OSHA Dar es salaam.



Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka ya Botswana, Bw.Gopolang Maakwe pamoja na watumishi wa Ofisi yake (waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi katika Menejimenti ya OSHA katika Ofisi za Dar es salaam.

*************************





Na Mwandishi Wetu

Wataalam kutoka Ofisi ya Kumbukumbu na Nyaraka ya Botswana wamefanya ziara katika Ofisi za Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa lengo la kujifunza jinsi Taasisi hiyo inavyotumia mifumo ya TEHAMA katika usimamizi wa masuala ya Afya na Usalama mahali pa kazi.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Serikali wa Botswana, Bw. Gopolang Maakwe, Nchi yake ipo katika mchakato wa kutengeneza mfumo wake wa ofisi mtandao kwa ajili ya kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.

Akizungumza alipotembelea Ofisi za OSHA na kufanya kikao na menejimenti hivi karibuni, amesema wameona ni muhimu kujifunza kwa nchi ambazo zimepiga hatua katika matumizi ya mifumo hiyo.

“Tumekuja hapa kujifunza namna ambavyo Tanzania imefanikiwa kujenga na kutumia mfumo wa ofisi mtandao katika Taasisi zake zaidi ya 200. Tuliposikia kwamba Tanzania wamefanikiwa katika eneo hili tukaona ni vyema akawa mshirika wetu katika zoezi lililopo mbele yetu la kuhakikisha kwamba Serikali nzima ya Botswana inaingia katika matumizi ya ofisi mtandao kuanzia mwaka 2024/2025,” amesema Bw. Maakwe.

Ameongeza kuwa: “Katika ziara yao wamefurahi kusikia kwamba mfumo unaotumika Tanzania umeandaliwa kwa kutumia wataalam wa ndani hivyo hata uangalizi na matengenezo yake hayatakuwa na gharama kubwa kwani mara nyingi uundaji wa mifumo ya TEHEMA umekuwa ukitegemea watoa huduma wa nje ya serikali jambo ambalo limekuwa likiongeza gharama za uendeshaji.”

Aidha, ameishukuru OSHA na serikali ya Tanzania kwa ujumla kwa ukarimu wao na ameahidi kwamba wataendelea kuja kujifunza zaidi hadi hapo watakapokamilisha mfumo wa nchi yao.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa OSHA, Dkt. Jerome Materu, amemshukuru Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Taasisi ya OSHA kutumia mfumo wa ofisi mtandao na mifumo mingine ya serikali ambayo imesaidia kuongeza ufanisi katika utendaji wa OSHA.

“Mfumo wa ofisi mtandao pamoja na mifumo mingine iliyoandaliwa na serikali yetu imesaidia sana kupunguza urasimu na kutuongezea kasi ya kuwahudumia Watanzania. Sisi kama OSHA tunao mfumo wetu wa ndani wa Usimamizi wa Taarifa za maeneo ya kazi nchini ujulikanao kama WIMS ambao tunautumia sambamba na mfumo wa ofisi mtandao na mifumo mingine ya serikali katika kuwahudumia wadau wetu,” alieleza Dkt. Materu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Huduma za Usalama na Afya, kabla ya kuanza kutumia mifumo hiyo kulikuwa na changamoto katika upatikanaji wa huduma za OSHA ambapo cheti cha usajili wa eneo la kazi kilikuwa kinapatikana baada ya siku saba huku cheti cha kukidhi viwango vya usalama na afya kikiandaliwa kwa mwezi mzima.

“Kwasasa mdau anaweza kusajili eneo lake la kazi ndani ya masaa machache na kupata cheti cha kukidhi viwango vya usalama na afya ndani ya siku tatu,” amefafanua Mkurugenzi Materu.

OSHA ni Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambayo inasimamia utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003. Usimamizi wa Sheria hii unahusisha kuyatambua maeneo ya kazi kwa kuyapa usajili na kisha kuyafikia kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa kitaalam juu ya uboreshaji wa mazingira ya kazi kwa minajili ya kuwakinga wafanyakazi dhidi ya vihatarishi vya ajali na magonjwa mahali pa kazi.
Share:

WAJIBU YAZIPIKA AZAKI, WAANDISHI WA HABARI USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA



TAASISI ya WAJIBU imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari na Asasi za Kiraia (AZAKI) namna ya kufanya uchambuzi wa masuala ya uwajibikaji na usimamizi wa fedha za umma.Akizungumza mbele ya wadau hao wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo ya siku mbili jana Machi 29, 2023,jijini Dodoma Meneja wa Fedha na Utawala wa Taasisi ya WAJIBU, Jackson Mmary ameeleza hatua kwa hatua umuhimu wa kuwa na wadau kutoka maeneo mbalimbali ili kujengeana uwezo wa kuchambua ripoti zinazohusu uwajibikaji wa fedha za umma.

Amefafanua kuwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) ambayo inahusu masuala ya fedha ni nyenzo muhimu ya kufuatilia mipango ya Serikali Kuu ama Serikali za Mitaa na taasisi za kiraia.

“Tumekuwa tukifanya uchambuzi wa ripoti ya CAG peke yetu kwa kipindi cha miaka sita iliyopita, sasa tumeona kuna umuhimu wa kuwashirikisha wadau. Kwa muelekeo wa WAJIBU tukasema ukitaka kwenda haraka nenda peke yako lakini ukitaka kwenda mbali nenda na wenzako, kwa hiyo tukaona ni muda muafaka kuanza kwenda na wenzako,” amesema Mmary na kuongeza:

“Miaka iliyopita tulikuwa tunafanya uchambuzi halafu tunawaletea, sasa hivi tunataka kuwaongeza ili sisi na ninyi tufanye uchambuzi kwa pamoja halafu tukitoka hapa twende mbele. Kwa kufanya hivyo tutawezesha kujenga kwa pamoja yale tuliyokuwa tunayachambua na kuwaletea.

Kwa hiyo hivi sasa nanyi mtakuwa na uwezo wa kuchambua, kwa hiyo tutakuwa na nguvu zaidi kwa sababu ya kuhusika sote kwa pamoja. Kingine kitatuongezea mawanda ya uchambuzi kwani tumekuwa tukifanya uchambuzi kama sisi na kama tulikuwa watu 20 hapa leo wapo zaidi ya 40.”

Kutokana na uwezeshaji uliofanywa, kwa sasa amesema kutakuwa na macho mengine 80 zaidi yale yaliyokuwa yanafanya uchambuzi mwanzoni.

“Sisi WAJIBU na ninyi kuanzia leo tukitembea kwa pamoja tutakuwa tumejijengea uwezo, ninyi mtakuwa mmetujengea uwezo na sisi tunawajengea uwezo, kwa hiyo tutaongeza uzoefu na hasa ninyi mnaofanya kazi mikoani katika halmashauri.

Pia kuna mambo ambayo inawezekana tusiyaone namna ambavyo yanaathiri jamii na kila mtu anahoji ndio maana hapa kuna redio za jamii, magazeti ya kitaifa pamoja na kuna asasi za kiraia. Kwa hiyo tukiweka huo mchanganyiko tutaongeza mawanda, uzoefu zaidi katika kufanya uchambuzi wa mambo yanayoathiri jamii,” amesema Mmary.
Meneja wa Fedha na Utawala wa Taasisi ya WAJIBU, Jackson Mmary akizungumza mbele ya Wanahabari na Wadau wa Asasi za Kiraia (AZAKI) kutoka maeneo mbalimbali nchini wakati wa ufunguzi wa Mafunzo siku mbili yanayoendelea jijini Dodoma yaliyohusu namna ya kufanya uchambuzi wa masuala ya uwajibikaji na usimamizi wa fedha za umma,lengo mojawapo ikiwa ni kujengeana uwezo wa kuchambua ripoti zinazohusu uwajibikaji wa fedha za umma.
Baadhi ya Wanahabari na Wadau wa Asasi za Kiraia (AZAKI) kutoka maeneo mbalimbali nchini wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati mafunzo yakiendelea.
Mmoja wa Wandishi wa habari akichangia jambo katika suala zima la kujengeana uwezo wa kuchambua ripoti zinazohusu uwajibikaji wa fedha za umma.

Ofisa Utafiti na Uchambuzi wa Fedha kutoka Taasisi ya WAJIBU Maureen Mboka akieleza jambo mbele ya Wanahabari na Wadau wa Asasi za Kiraia (AZAKI) kutoka maeneo mbalimbali nchini wakati wa ufunguzi wa Mafunzo siku mbili yanayoendelea jijini Dodoma yaliyohusu namna ya kufanya uchambuzi wa masuala ya uwajibikaji na usimamizi wa fedha za umma,lengo mojawapo ikiwa ni kujengeana uwezo wa kuchambua ripoti zinazohusu uwajibikaji wa fedha za umma.

Wakifuatilia baadhi ya vitabu vinavyohusu Ripoti ya uwajibikaji vinavyoandaliwa na Taasisi ya WAJIBU ikiwa ni sehemu ya kujengeana uwezo wa kuchambua ripoti zinazohusu uwajibikaji wa fedha za umma.
Picha mbalimbali wakati wa Majadiliano wa mafunzo hayo yakiendelea
Ofisa Mawasiliano wa Taasisi ya WAJIBU Hassan Kissena akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiibuliwa wakati wa majadiliano kwenye mafunzo hayo yaliyowakutanisha Waandishi wa habari pamoja na Wadau wa Asasi za Kiraia (AZAKI) kutoka maeneo mbalimbali nchini
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger