Friday 6 January 2023

AJALI YA BASI LA LORI YAUA WATU 16


Takriban watu 16 wamepoteza maisha wakati basi la abiria lilipogonga lori moja Ijumaa asubuhi kwenye barabara kuu ya Uganda inayounganisha mji mkuu, Kampala, na mji wa kaskazini wa Gulu.

Polisi wanasema watu 12 walifariki papo hapo huku wengine wanne wakifariki baadaye hospitalini. Wasafiri wengine kadhaa kwenye basi hilo walijeruhiwa.

Lori hilo lilisemekana kuegeshwa na kupakia mizigo takriban kilomita moja kutoka Kamdini Corner - kituo maarufu cha kusimama na ukaguzi kaskazini mwa nchi.

Kumekuwa na viwango vya kutisha vya ajali za barabarani nchini katika wiki za hivi karibuni na haswa katika msimu wa sikukuu.

Ripoti ya polisi wa trafiki mapema wiki hii ilifichua kuwa ajali 104 za barabarani zilirekodiwa kati ya 30 Desemba na 1 Januari.

Takriban watu 35 waliuawa katika ajali hizi za barabara pekee.

Ajali za barabarani zimekuwa janga la muda mrefu nchini. Polisi wa trafiki walisajili zaidi ya ajali 4,000 kote nchini Uganda mnamo 2021, nyingi zikiwa mbaya.

Chanzo - BBC SWAHILI


Share:

IGP WAMBURA AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa mikoa katika kuboresha na kuongeza ufanisi wa utendaji kwenye mikoa mitatu.


Kupitia taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Januari 06, 2023 na Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime imeeleza kuwa katika mabadiliko hayo, IGP Wambura amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Muslim kwenda Kitengo cha Mipango Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Alex Mukama ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.

IGP Wambura amemhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Theopista Mallya kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.

Aidha amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Shadrack Masija ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Namba Moja Mkoa wa Simiyu kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.
Share:

BABA AJIUA BAADA YA KUUA MKE, MAMA MKWE NA WATOTO WATANO


Michael Haight mwenye umri wa miaka 42 nchini Marekani amemuua mke wake, mama mkwe na watoto wake 5 na yeye kujiua baada ya mke wake kuwasilisha ombi la talaka jambo ambalo yeye hakulitaka.

Tukio hilo limetokea katika jimbo la Utah nchini Marekani ambapo miili ya watu hao imepatikana ndani ya nyumba ya mashambani katika Jiji la Enoch wakati wa ukaguzi katika boma lao.

Waliofariki ni mke wake Tausha mwenye umri wa miaka 40, mama mkwe wake Gail Earl mwenye umri wa miaka 78 na watoto wake watano pamoja na mhusika huyo Michael Haight.

Polisi wamesema chanzo cha mauaji hayo ni mwaume huyo kutofurahishwa na ombi la talaka lililowasilishwa na mke wake tarehe Desemba 21/2022.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 6,2023


Share:

Thursday 5 January 2023

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI... YUMO DAVID KAFULILA

Share:

DODOMA YAJIPANGA KIVINGINE KUBORESHA ELIMU



Idara ya elimu Mkoa wa Dodoma imefanya kikao kazi cha wadau wa elimu Mkoa kilichohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiwa ndiye mgeni rasmi wa kikao hicho kililichofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) eneo la Mipango Jijini Dodoma.

Katika kikao hicho kilicholenga kujadili mpango kazi wa muelekeo wa namna ya kuanza mwaka mpya wa masomo 2023, kimejadili mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wa Elimu kwa Mkoa wa Dodoma na kupanga mikakati ya kufanya vizuri kwa mwaka huu mpya.

Mkuu wa Mkoa amebainisha mambo kadhaa ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameboresha kwa kiasi kikubwa kwenye sekta ya elimu.

“Rais amefanya mambo mengi kuboresha sekta ya elimu kama vile kuondoa ada kuanzia shule za awali mpaka kidato cha sita, ujenzi wa madarasa ya kutosha kupokea idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha kwanza ambapo kwa awamu ya kwanza ya fedha za Uviko – 19 mwaka 2021 Mkoa wa Dodoma ulipata fedha za kujenga madarasa 776 na kwa mwaka huu tumepatiwa fedha shilingi Bilioni 15.6 kujenga madarasa 339. Pia Rais ametoa ruzuku kwa shule kila mwezi shilingi Milioni 200” Amesema Mhe. Senyamule

Aidha, Mkuu wa Mkoa ametoa hamasa kwa walimu kufanya kazi kwa bidii kwani wao ndio wanaoweza kusaidia kuinua Mkoa katika kupata matokeo mazuri kwenye mitihani ya kitaifa“Nasisitiza walimu ni kundi linaloweza kujenga nchi au kuibomoa. Nitoe rai kwa maafisa na walimu wakuu kusimamia uandikishwaji wanafunzi wa shule za awali na darasa la kwanza. Mpaka sasa wanafunzi walioandikishwa kwa shule za awali wamefikia 57,617 ambapo lengo ni kuandikisha wanafunzi takribani elfu 70 na kwa darasa la kwanza wameandikishwa wanafunzi 74,230 sawa na 82.4% wakati lengo ni kuandikisha wanafunzi 90,122 hivyo uandikishaji haujafikia lengo. Niwatake Halmashauri zote kufuatilia uandikishwaji ili tuweze kufikia asilimia 100 kwani Watoto bado wapo wengi amabo hawajaandikishwa” Amesisitiza Mhe. Senyamule


Share:

RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA KAMISHNA DIWANI ATHUMAN MSUYA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani Msuya, aliyemteua tarehe 03 Januari, 2023 kuwa Katibu Mkuu Ikulu.

Aidha, Rais Samia amemteua Bw. Mululi Majula Mahendeka kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Bw. Mahendeka alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu.

Share:

POLISI ALIYEOA MWEZI ULIOPITA AFUMANIWA AKICHEPUKA NA MKE WA MTU


Polisi

Afisa wa polisi nchini Kenya aliyefunga ndoa Desemba mwaka jana, amefumaniwa chumbani akiwa na mke wa mtu, katika nyumba moja mtaa wa Eastlands jijini Nairobi.

Mwanamume huyo aliyemfumania Afisa wa Polisi, imeelezwa kwamba alikuwa amesafiri kwenda kijijini na aliporudi nyumbani akamkuta mkewe akimsaliti.

Baada ya majibizano ya muda mfupi, mwanaume ambaye amefahamika kwa jina la Ali Abdul Majid, alihisi kutishiwa maisha na kuamua kupiga ripoti katika Kituo cha Polisi cha Dondora.

Maafisa wenzake mtuhumiwa waliotoa michango katika sherehe yake ya harusi walishangazwa kabisa na kisa hicho.
Share:

GARI LA WAGONJWA 'AMBULANCE' LAUA MUUGUZI NA MAMA MJAMZITO KWENYE KONA SPIDI KALI KUELEKEA HOSPITALI

Mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 21, na mtoto wake aliyekuwa tumboni walifariki dunia wakati gari la wagonjwa lililokuwa likimkimbiza hospitalini kupoteza mwelekeo na kuanguka.


Ripoti zinaeleza kuwa muuguzi wa kiume aliyekuwa ameandamana na mwanamke huyo pia alifariki dunia katika ajali hiyo mbaya iliyotokea kwenye kona ya barabara ya Hospitali ya Mukobeko nchini Zambia. 

Zambia Daily Mail inaripoti kuwa ajali hiyo iliyotokea mwendo wa saa kumi na mbili jioni, dereva ndiye analaumiwa kwa kuendesha gari kwa mwendo wa kasi zaidi wakielekea hospitalini.


Mama huyo mjamzito Agatha Chanda na muuguzi Simon Lukama walikuwa safarini kuelekea Hospitali Kuu ya Kabwe ambako alipewa rufaa kutoka Kliniki ya Katondo walipopata ajali.


“Kutokana na mwendo wa kasi, gari la wagonjwa lililokuwa likiendeshwa na Charles Makasa (40), lilipoteza mwelekeo barabarani na kugonga mti,” ilisoma sehemu ya ripoti hiyo.

 Aliyekuwemo pia ndani ya gari hilo ni mamaake Chanda, Ellen mwenye umri wa miaka 41, ambaye alinusurika kifo lakini alipata majeraha pamoja na dereva wa gari hilo la wagonjwa. 

Maoni kutoka kwa wananchi yaligawanyika kuhusu iwapo dereva ndiye anapaswa kulaumiwa kwa kuendesha gari kwa kasi katika juhudi za kuokoa maisha.

Kufuatia ajali hiyo mbaya, wananchi walimlaumu dereva wa gari hilo la wagonjwa kwa mwendo wa kasi.

Wengine, hata hivyo, walihoji kwamba dereva huyo hakuwa na makosa kuendesha gari kwa mwendo wa kasi kwani alikuwa akijaribu kuokoa maisha ya mama na mtoto.

 Warren Chisanga: "Kabla ya kumlaumu dereva, wafanye uchunguzi wa kina wa gari ambalo limetajwa kuwa ni gari la wagonjwa na kama linafaa kuwa barabarani. Ikiwa ni dharura dereva hawezi kutembea polepole."

Cyn Chuma Sibeso: "Tunaelewa magari ya kubebea wagonjwa hayatakiwi kutembea taratibu lakini niamini madereva hawa wanatia chumvi. Nimebebwa na kadhaa, hawa jamaa huhisi wanamiliki barabara."

 Patricia Chikwete: "Kuokoa maisha inakuwa haina maana pale mtu anapozembea kuendesha gari. Madereva hawa wanaweza kuongeza kasi, jambo ambalo si salama." 

Elita T Mwanza: "Alikuwa anaendesha kwa kasi ili wawahi hospitali kwa wakati kwa sababu kuzaa mtoto ni suala la maisha na kifo."

Via - Tuko news
Share:

Wednesday 4 January 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 5,2023













Share:

MWAMBA AOA WANAWAKE WAWILI SIKU MOJA



 
Mwanaume mmoja raia wa Nigeria aliyetambulika kwa jina la Nkanu, amefunga pingu za maisha na wanawake wawili siku moja katika jimbo la Cross River.

Nkanu aliwaoa Mary na Jennet siku moja katika sherehe ya harusi iliyofanyika Jumamosi, Disemba 31, 2022, katika Uwanja wa Michezo wa Bazohure.

Picha za karamu hiyo ya kufana zilipakiwa kwenye mitandao ya kijamii na kuwachangamsha wengi.



Share:

VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA VYATOA MAPENDEKEZO KUHUSU BAJETI YA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM


Veronica Wana kutoka Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule akisoma maoni na mapendekezo katika eneo la masuala mtambuka ya Jinsia hasa kwenye vipaumbele muhimu kwenye upangaji wa Bajeti yenye mrengo wa Usawa wa Kijinsia kwa wadau wa Usawa wa Kijinsia(Bajeti Jumuishi) kwenye Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
Mwanakituo wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Majohe Rehema Shunda akisoma uwasilishwaji wa Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwenye sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo pamoja na mapendekezo ya kisera kwa Halmashauri kwenye sekta ya kilimo wakati uwasilishwaji wa mapendekezo ya vipaumbele muhimu kwenye upangaji wa Bajeti yenye mlego wa Usawa wa Kijinsia kwa wadau wa Usawa wa Kijinsia(Bajeti Jumuishi) kwenye Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
Mwanakituo wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kipunguni Tausi Msangi akisoma kuhusu hali ya Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa mwaka wa fedha wa 2022/23 pamoja na Mapato ya Jiji hilo wakati uwasilishwaji wa mapendekezo ya vipaumbele muhimu kwenye upangaji wa Bajeti yenye mrengo wa Usawa wa Kijinsia kwa wadau wa Usawa wa Kijinsia(Bajeti Jumuishi) kwenye Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule Erick Anderson akisoma utangulizi wa Uchambuzi wa Mapitio ya Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha wa 2022/23 kwa kuzingatia vipaumbele vya wanajamii kwa mtazamo wa usawa wa kijinsia


*****




Vituo vya Taarifa na Maarifa kata za Kipunguni, Kivule, Zingiziwa na Majohe vimetoa mapendekezo ya vipaumbele muhimu kwenye upangaji wa Bajeti yenye mlego wa Usawa wa Kijinsia kwa wadau wa Usawa wa Kijinsia(Bajeti Jumuishi) kwenye Bajeti ijayo ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya mwaka 2023/24 ili kuweza kunufaisha wanajamii kwa ujumla.


Wamesema kipaumbele cha kwanza ni Viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi ili mazao yaliyolimwa katika maeneo mbalimbali ya Ilala yanahitaji kuongezewa thamani kama mboga mboga na matunda zinazolimwa katika Eneo la Kituo cha Kilimo la Kinyamwezi litumike pia kama kiwanda cha wananchi cha kuzalisha bidhaa mbalimbali za kilimo na kuzitafutia masoko ndani na nje ya nchi.


Pia katika Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya Watu wamesema bado kuna ombwe kubwa kati ya hali halisi ya Jamii na dhana ya ukuaji wa uchumi kwa kuzingatia kwamba uchumi unatakiwa kugusa maisha ya watu moja kwa moja hivyo basi tunapendeleza serikali kuwekeza zaidi kwenye Nyanja za uchumi mdogo wa watu hasa katikia uzalishaji na masoko.


Wamesema Jiji la Dar es Salaam lifanye maboresho ya mfumo wa kusajili viwanda vidogo na kuondoa tozo au kuboresha mlolongo wa kupata usajili ili kuwezesha kuanzishwa kwa viwanda vingi vya wanawake vya usindikaji kwani wazalishaji wa Bidhaa za kilimo kama viungo hawapati usajili wa Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) kwa urahisi, hii imechangia kuzagaa kwa bidhaa nyingi za wajasiriamali wadogo mitaani ambazo hazijafanyiwa vipimo na uhakiki kutokana na urasimu wa TBS kupata usajili na tozo kubwa za kulipia.


Wamesisitiza kuwa ni muhimu sana kutenga bajeti ya kusimamia utekelzaji na kufuatilia Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA1) na kuweka nguvu katika kuharakisha uandwaaji wa Mpango wa II kwa kuwa Halmashauri nyingi hazilipi suala la Ukatili wa Kijinsia kipaumbele, licha ya kutumia fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo hasa sekta ya elimu bado hakuna jitihada za dhati kuzuia kabisa au kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kama ulinzi wa mtoto wa kike asibakwe, kukeketwa, kuolewa au kupata ujauzito.


Pia huduma za ustawi wa jamii kwa Jiji la Dar es salaam haithaminiwi na kuwekewa rasilimali fedha na Bajeti ya kutosha ya kukabiliana na vitendo vya Ukatili wa Kijinsia hivyo wamependekeza kuongezwa kwa fedha kwa ajili ya kuwezesha dawati la ustawi wa Jamii ili kufanya kazi zao kwa ufanisi ili kuwawezesha manusura wa Ukatili wa Kijinsia kupata huduma za uokozi kwa haraka.


Kutokana na kutokuwepo kwa uelewa mpana juu ya masuala ya Kijinsia kwa watunga sera, wataalamu na watendaji wametoa ushauri kwa afisa jinsia wa Halmashauri aandae utaratibu wa mafunzo ya Jinsia na bajeti yenye mlengo wa Kijinsia kwa Halmashauri ili wataalamu kutoka Mtandano wa Jinsia Tanzania (TGNP) waweze kutoa elimu hiyo.


Wamesisitiza kuwa bado viongozi na watendaji wengi hawazingatii umuhimu wa kutenga fedha kwenye bajeti kwaajili ya kutoa taulo za kike kwa wanafunzi walioko mashuleni hasa wanaotoka kwenye familia masikini kwani Fedha zilizotengwa kwa Halmashauri ya Jiji kwa mwaka wa fedha 2022/23 hazijatolewa kwa lengo hilo, na sehemu ya fedha zimetumika kwa matumizi mengine hivyo wameshauri wasichana walioko mashuleni wapatiwe taulo ili waweze kushiriki kikamilifu masomo wanapokuwa kwenye hedhi, ili kuongeza ufaulu kwa wasichana.
Share:

RAIS WA BRAZIL AONGOZA MAZISHI YA BINGWA WA SOKA DUNIANI PELE



Jeneza la mfalme wa soka duniani hayati Pele.

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva Jumanne anaongoza mazishi ya bingwa wa kandanda Pele ambaye atakumbukwa kama mchezaji bora zaidi katika historia ya kandanda.

Baada ya siku tatu za maombolezo, wananchi wa Brazil walitoa heshima zao za mwisho kwa Pele ambaye amepewa jina la mfalme, aliaga dunia Alhamisi wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 82, baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Sherehe za Jumapili za kuapishwa Lula kuchukua madaraka zilianza kwa dakika moja ya kukaa kimya ili kutoa heshima kwa Pele, na leo yuko mji wa kusini mashariki wa Santos, ili kutoa heshima zake za mwisho kwa mfalme huyo wa kandanda kabla ya muda wa maombolezo uliowekwa ambao ulimalizika rasmi saa tatu asubuhi kwa saa za Brazil.

Maelfu ya waombolezaji pamoja na maafisa wa ngazi ya juu kwenye fani ya kandanda akiwemo rais wa FIFA Gianni Infantino wamepita karibu na jeneza la Pele ili kutoa heshima zao za mwisho kwenye uwanja wa michezo ya Vila Belniro ambako Pele na timu yake ya Santos FC waliutumia kwa muda mrefu.Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva akitoa hotuba baada ya kuapishwa wakati wa sherehe za uzinduzi wa urais wake katika Bunge la Taifa mjini Brasilia, Jan. 1, 2023.

Akizungumza na wanahabari alipofika kutoa heshima zake, Infantino alisema kwamba Pele atakumbukwa milele, akiongeza kwamba FIFA itaomba mataifa wanachama yakipatie angalau kiwanja kimoja cha mpira nchini humo jina la Pele kama njia ya kumkumbuka.

Gianni Infatino, kiongozi wa FIFA alisema: “Nafikiri ameacha wasia wa kipekee wakati akifanya mambo ambayo asilimia 99 ya wachezaji hawawezi kuyafikia kamwe. Asilimia 1 ya wachezaji wanaweza kufanya tu labda jambo moja alilofanya. Pele alikuwa wa kwanza kufanya aliyoyafanya na kwa hakika atabaki moyoni mwetu.

Tutahakikisha kwamba jina lake litabaki milele kwenye ulimwengu wa soka. Hiyo ndiyo sababu kubwa kwetu sisi kuwa hapa. Tunatoa heshima zetu kwa kuyaomba mashirika yote ya soka kuwa na dakika moja ya ukimya.”

Kundi kubwa la wachezaji, wanasiasa, watu mashuhuri pamoja na mashabiki wa kandanda wamesafiri hadi mji wa Santos na kusubiri kwa saa nyingi ili kumuaga Pele japo baadhi wameathiriwa na sherehe za kuukaribisha mwaka mpya.

Nahuel Nunes mwenye umri miaka 35 kutoka Argentina ni mmoja wao. Nunes ambaye ni shabiki wa soka anaeleza:

Namheshimu sana kama mshindi wa kombe la dunia mara tatu. Timu yetu ya Argentina pia ni washindi wa kombe hilo mara tatu. Japo sisi tumeshinda kwenye kombe la dunia lililomalizika hivi karibuni, bado ni na heshima kubwa sana kwake. Ilinibidi kufika hapa ili kuhudhuria tukio hili la kihistoria.

Jeneza la Pele lilipelekwa kwenye uwanja huo Jumatatu likiwa limebebwa na watu waliovalia mavazi meusi wakiongozwa na mwanawe wa kiume Edinho.

Mke wake Marecia Cibele Aoki ambaye ni wa tatu na aliolewa 2016 alionekana akisononeka wakati akikaribia kuushika mwili wake pale jeneza lilipofunguliwa.

Jeneza hilo lililofunikwa kwa bendera za Brazil pamoja na ile ya Santos pia lilizungukwa na mashada ya maua yenye rangi tofauti kutoka kwa watu mashuhuri kama mchezaji wa PSG ya Ufaransa na pia nyota wa sasa wa Brazil Neymar, ambaye alikuwa ameandamana na baba yake.

Mazishi yalianza asubuhi kwa saa za huko huku baadhi ya waombolezaji wakiwasili kwenye uwanja huo tangu Jumatatu ili kutoa heshima zao za mwisho kwa Pele, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Edson Arantes do Nascimento.

Msafara wa jeneza lake litazunguka mji wa Santos na utapitia karibu na nyumba ya mama yake Celeste Arantes mwenye umri wa miaka 100 na ambaye yupo hai licha ya kwamba haelewi kwamba Pele amefariki.

Mazishi yatafanyika kwa mujibu wa madhehebu ya Kanisa Katoliki kwenye makaburi ya Santos ambako mwili wa Pele utahifadhiwa kwenye Jumba maalum.
Share:

WAANDISHI WA HABARI LINDI WAHIMIZWA KUTHAMINI KAZI NA TAALUMA YAO

Waandishi wa habari mkoani Lindi wamehimizwa wathamini kazi na taaluma yao ya uandishi wa habari ili taaluma hiyo na wao wenyewe waweze kuthaminiwa.

Wito huo ulitolewa juzi na mkuregenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Eston Ngilangwa wakati wa mkuu mkutano mkuu maalumu wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Lindi (Lindi Regional Press Club) uliofanyika katika manispaa ya Lindi.

Ngilangwa ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, alisema ili taaluma ya uandishi wa habari na waandishi wa habari wenyewe waweze kuthaminiwa hawana budi kuthamini taaluma hiyo kwa kulinda miiko na sheria, ikiwemo kuzingatia maadili. Kwani iwapo watapuuza wajue wanaanda mazingira ya kupuuzwa.

Alisema katika kufanikisha azima hiyo hawana budi waongeze ujuzi kupitia vyuo, mafunzo, semina na kubadilishana uzoefu na wanataaluma wenzao.

Alisema licha ya kuwafanya wathaminiwe, lakini pia kuongeza ujuzi kutasababisha kupanua wigo wa ajira na masilahi kupitia kazi yao ya uandishi.

Katika mkutano huo wanachama wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Lindi walifanya marekebisho ya baadhi ya ibara na vifungu mbalimbali vya katiba ya klabu hiyo na kuunga mkono maazimio kumi ya Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC).
Share:

RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO YA VIONGOZI SERIKALINI... AFUMUA FUMUA IKULU USALAMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya nafasi za uongozi katika Serikali ambapo amemteua Balozi Hussein Othman Katanga kuwa Balozi wa Tanzania mjini New York, nchini Marekani na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa.


Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus leo Jumanne Januari 03, 2022 imeeleza kuwa Balozi Katanga amechukua nafasi ya Balozi Profesa Kennedy Gaston ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huu balozi Katanga alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Rais Samia amemteua Bw. Moses Mpogole Kusiluka kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ambapo Kabla ya Uteuzi huo Bw. Kusiluka alikuwa Katibu Mkuu Ikulu

Kamishna Diwani Athumani Msuya ameteulwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu ambapo Kabla ya uteuzi huo Kamishna Diwani alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Pia Rais Samia amemteua Bw. Said Hussein Masoro kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ambapo Kabla ya uteuzi huo Bw. Masoro alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Shughuli za Ndani wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger