Wednesday 28 December 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DESEMBA 29,2022




Share:

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AWASILI MAKAO MAKUU YA WIZARA JIJINI DODOMA, NAIBU KATIBU MKUU AONGOZA MAPOKEZI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akipokea maua kutoka kwa mtumishi wa wizara hiyo,Aisha Juma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.Katikati ni Naibu Katibu Mkuu,Dkt.Maduhu Kazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa wizara hiyo,Amani Mashaka wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na Mkaguzi Mkuu wa Ndani,Martina Nguluma wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na mtumishi wa wizara hiyo,Mariamu Omary wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na mtumishi wa wizara hiyo,Juma Mnyanile wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Share:

MFANYABIASHARA WA M-PESA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI


Mwanaume mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi waliomvamia usiku katika daka lake katika katika soko la Khayega eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega nchini Kenya.

Majambazi watatu waliojihami kwa silaha kali walimvamia Kevin Orata katika duka lake la M-Pesa usiku wa Jumatatu - Disemba 26,2022 na kutekeleza unyama huo. 

Akithibitisha kisa hicho Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Kakamega Mashariki Robert Makau alisema kuwa Orata aliyekuwa na umri wa miaka 23 alipigwa risasi na kuaga dunia papo hapo.

Ripoti zinasema kuwa majambazi hao walishuka kutoka kwa pikipiki mwendo wa saa mbili usiku na kuelekea katika duka la M-Pesa karibu na kituo cha mafuta kwenye barabara kuu ya Kakamega kuelekea Kisumu.

Watatu hao kisha walimwamuru mwanaume huyo kuwapa pesa alizokuwa amepata katika biashara hiyo siku hiyo. 

“Waliamuru Orata na mwajiri wake kuwapa pesa na simu zilizokuwa kwenye duka hilo. Alipokataa, mmoja wa majambazi aliyekuwa na bunduki aina ya AK47 alimpiga risasi na kumuua papo hapo,” raia mmoja aliyeshuhudia aliambia waandishi wa habari.

 Genge hilo kisha liliiba kwa haraka kiasi cha pesa kisichojulikana kabla ya kutoroka eneo la tukio kwa kutumia pikipiki. Makau anasema kuwa msako wa kuwatia mbaroni washukiwa hao umeanza.

Chanzo -Tuko News
Share:

JOKATE APOST PICHA YA MTOTO WAKE



Mheshimiwa Jokate Mwegelo Amemuonesha Mtoto wake kwa mara ya kwanza kwa kupost picha na Kuandika yafuatayo:

Jokatemwegelo:
Her name is Totoo. Call me Mama Totoo 🥰
Glory to God 🙌🏽
Share:

HALMASHAURI YA SHINYANGA INAVYOLIPA KIPAUMBELE SUALA LA VYUMBA VYA KUJISTIRI NA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI


Mfano wa taulo za kike

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Watoto wa kike wanaotokea kwenye familia duni mara nyingi hukosa kuhudhuria masomo wanapokuwa katika siku za hedhi kutokana na kukosa vifaa salama vya kujihifadhia kama taulo za kile au ‘Pedi’ kama wengi wanavyoita.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inakadiriwa msichana mmoja kati ya 10 kutoka nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara hukosa kwenda shule aingiapo kwenye mzunguko wake wa hedhi.

Kwa wastani wasichana wanaripotiwa kukosa kuhudhuria masomo kuanzia siku 3 hadi tano kwa mwezi yaani kwa mwaka ni siku 36 hadi 60 hali inayochangia kutofanya vizuri katika masomo yao.

Changamoto ya Taulo za kike pia bado inawakabili wanafunzi katika kata ya Mwamala Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na katika kukabiliana na hali hiyo Halmashauri hiyo imeanza kuchukua hatua kusaidia watoto wa kike.

Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Shinyanga Mkoani Shinyanga Christina Bukoli amesema serikali inalipa kipaumbele suala la taulo za kike ambapo tayari wameliingiza kwenye Bajeti za Halmashauri na wanaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuwapatia wanafunzi taulo za kike.

Bukoli amesema pia kipaumbele kingine ni suala la vyumba vya kujistiri watoto wa kike ambapo maelekezo yaliyopo hivi sasa vyoo vinavyojengwa shuleni ni lazima viwe na chumba cha kujistiri na kwa upande wa suala la taulo za kike.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwamala, Suzana Kayange ameeleza kuwa kati ya shule tano zilizopo katika kata hiyo (moja ya Sekondari, nne za msingi), chumba cha Usiri kipo katika shule ya msingi Bunonga kilichojengwa na Shirila la Life Water International na shule ya Msingi Igegu kuna chumba cha usiri kilichojengwa na wananchi na kwamba taulo za kike zimekuwa zikitolewa na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika.

Nao baadhi ya wanafunzi wameambia Malunde 1 blog kuwa wakati mwingine wanashindwa kuhudhuria masomo yao wanapokuwa kwenye Hedhi hali inayochangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwenye mitihani kutokana na kukosa mada zinazofundishwa darasani.

"Endapo serikali itatenga bajeti ya taulo za kike, tutahudhuria masomo siku za hedhi na tutasoma kwa kujiamini na hatupata magonjwa ambayo yanaweza kutokea kwa ukosefu wa taulo za kike  lakini pia bajeti hiyo itaziba pengo ambalo wazazi wetu hawawezi kuliziba kwa sababu ya changamoto nyingi zinazowakabili zikiwemo za kiuchumi’’,wameongeza.

Baadhi ya wazazi katika kata ya Mwamala waliozungumza na Malunde 1 blog akiwemo Pius Bundala na Merciana Genea wanashauri kuwe na vyumba vya usiri kwa watoto wa kike na itengwe bajeti ya taulo za kike shuleni badala ya kutegemea misaada ya wadau yakiwemo mashirika.

Share:

WAZAZI MWAMALA WAHAMASISHWA KUCHANGIA CHAKULA KWA WANAFUNZI SHULENI

Mfano wa mwanafunzi akipata chakula shuleni


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Wazazi na walezi katika kata ya Mwamala Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wamehamasishwa kuchangia chakula kwa ajili ya wanafunzi shuleni ili kuondoa utoro na kuongeza ufaulu kwenye mitihani.


Akizungumza na Malunde 1 blog hivi karibuni Afisa Mtendaji kata ya Mwamala Suzana Kayange amesema licha ya umuhimu wa chakula shuleni kwa wanafunzi lakini wazazi na walezi wamekuwa wakisuasua kuchangia chakula na kwenye baadhi ya shule chakula kinatolewa kwenye madarasa yenye mitihani tu.


“Nimekaa kwenye vikao vingi na wazazi kusisitiza chakula shuleni kwa wanafunzi kutokana na kwamba wanafunzi wakipata chakula ufaulu unakuwa mzuri lakini bado wazazi wanasuasua kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wakiwa shuleni”,amesema Kayange.

“Tunaendelea kuhamasisha wazazi kuchangia chakula shuleni licha ya kwamba wazazi ni wabishi kutokana na kwamba hawajajua umuhimu wa chakula shuleni”,ameongeza Kayange.


Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Shinyanga Christina Bukoli amesema ili kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni wameelekeza kila shule yenye mashamba ili mazao ya chakula lakini pia Maafisa watendaji wa vijiji na kata, maafisa elimu na wakuu wa shule wahamasishe wazazi na walezi kuchangia chakula kwa ajili ya wanafunzi shuleni.


Mmoja wa wazazi, Martha Tungu amesema zoezi la kuchangia chakula limekuwa likisuasua kutokana na wazazi kuwa na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa chakula shuleni.

“Ushauri wangu wazazi tuchangie chakula ili kuinua kiwango cha ufaulu..Tuache mitazamo ya kwamba chakula kikitolewa kitaliwa na wasiohusika”,amesema Shija Kanambu mkazi wa kijiji cha Bunonga.


Nao Masesa Masele, Kang’wa Cherehani na Nyamizi Manoni wamesema kutokana na hali ngumu ya maisha wameiomba serikali itoe chakula bure shuleni.

Share:

Tuesday 27 December 2022

BINTI AZIKATA NA KUZIONDOA KABISA NYETI ZA BABA YAKE

Mwanamke anayefahamika kwa jina Grace Kihumba(30) mkazi wa Wang'ing'ombe mkoani Njombe anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumshambulia baba yake mdogo akiwa usingizini na kisha kuzikata sehemu za siri na kuziondoa.



Baada ya kukamatwa na kufanyiwa mahojiano na maofisa wa jeshi la polisi mwanamke huyo amesema amefanya hivyo kutokana na kukasirishwa na kitendo cha wanafamilia kuendelea kusherekea wakati yeye anaendelea kuumwa licha ya kutoa hela za matibabu kwa mzee huyo ambaye anadaiwa kuwa ni mtaalamu wa tiba asilia,kama ambavyo Kamanda wa jeshi la polisi mkowa Njombe Hamis Issa alivyobainisha wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.


Katika tukio jingine Kamanda Issa amesema jeshi hilo linamshikilia kijana anayefahamika kwa jina la Baraka Alfonce mkazi wa kitongoji cha Kimbila Ludewa mjini kwa tuhuma za kuhusika kumkata kiganja cha mkono bosi wake baada ya kutomlipa fedha kiasi cha elfu 65.

Share:

UWEKEZAJI NCHINI WAONGEZEKA TIC YADHIBITISHA


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Ndugu Mathew Mnali ameongea na vyombo vya habari na kusema kuwa miradi iliyosajiliwa katika Kituo Cha Uwekezaji katika kipindi cha Julai hadi Novemba, 2022 imepanda kwa zaidi ya asilimia 22.2 ukilinganisha na kipindi kama hiki mwaka 2021.


Katika taarifa hiyo iliyotolewa katika ukumbi wa mikutano wa Kituo uliopo Mtaa wa Shabani Robert jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Disemba, 2022


Ndg. Mnali amesema kuwa katika kipindi cha Julai hadi Novemba 2022 Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimesajili jumla ya miradi 132 ikilinganishwa na miradi 108 iliyosajiliwa katika kipindi hicho hicho mwaka 2021.


Amesema kati ya miradi hiyo, miradi ya 50 inamilikiwa na wageni (foreigners) wakati Miradi 30 inamilikiwa na Watanzania (locals) na miradi 52 inamilikiwa kwa ubia kati ya watanzania na wageni (Joint ventures). Miradi hii ina jumla ya thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 3.16 na inatarajiwa kutoa ajira 21,297.


Mnali ameongeza kuwa mgawanyo wa miradi iliyosajiliwa – Kisekta
unaonyesha kuwa Sekta ya Viwanda iliweza kuongoza kwa kuvutia miradi mingi (67), ikifuatiwa na Sekta ya Usafirishaji miradi (25), Utalii miradi (12), Kilimo (9), Huduma (8), Majengo ya Biashara (7), Rasilimaliwatu (3) na Sekta ya Fedha (1).


Aidha, thamani ya miradi (USD bilioni 3.16) iliyosajiliwa katika kipindi cha Julai – Novemba 2022 imeongezeka kwa asilimia 259 ikilinganishwa na thamani ya miradi (USD milioni 881) iliyosajiliwa katika kipindi cha Julai - Novemba 2021.


Vilevile, kiwango cha ajira kinachaotarajiwa kutokana na miradi iliyosajiliwa Julai – Novemba 2022 kimeongezeka kwa asilimia 57 kutoka ajira 13,578 (Julai – Novemba 2021) hadi ajira 21,297 (Julai - Novemba 2022).


Ongezeko kubwa la Miradi iliyosajiliwa na Kituo cha Uwekezaji linatokana na Jitihada za Serikali ya Awamu ya sita(6) ya kutangaza fursa mbalimbali za Uwekezaji zilizoko hapa nchini kupitia Ziara mbalimbali za Viongozi wa Kitaifa nje ya nchi pamoja na juhudi kubwa za Serikali katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.

Share:

WADAIWA KUUA MTOTO KWA KUMZIKA AKIWA HAI SHAMBANI WAPATE UTAJIRI


Wa kwanza kulia ni Zawadi Msagaja (20), ambaye ni mama wa mtoto na anayefuatia ni dada wa Zawadi
**
Watu watatu akiwemo mkazi wa Kijiji cha Mahaha wilayani Magu mkoani Mwanza, Zawadi Msagaja (20), (Wa kwanza kulia), wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kike mwenye umri wa miezi sita kwa kumzika shambani akiwa hai ili wapate mali.


Ni kesi ya mauaji namba saba ya mwaka 2022 ambayo imesomwa na Mwendesha Mashtaka wa serikali Mwanahawa Changale, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Fortunatus Kubaja, wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza ambapo amesema washtakiwa hao watatu akiwemo Zawadi Masaga ambaye ni mama wa mtoto huyo, Elizabeth Kaswa ambae ni dada wa Zawadi pamoja na Mume wa Elizabeth ambae pia ni mganga wa kienyeji aitwaye Mussa Mazuri kwa pamoja walitenda kosa hilo Novemba 13 mwaka huu kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha sheria ya kanuni ya adhabu marejeo namba 16 ya mwaka 2022.

Baada ya washtakiwa hao kusomewa shtaka hilo la mauaji linalowakabili, Hakimu Mkazi Mwandamizi Kubaja akaiahirisha kesi hiyo hadi kesho Desemba 28 itakapotajwa tena na washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kisheria ya kusikiliza shauri hilo.

Chanzo - EATV
Share:

AMUUA KAKAAKE WABISHANA JUKUMU LA KUPIKA WALI



Msiba umegubika familia moja katika kijiji cha Ikorongo, kata ya Miruka, Kaunti ya Nyamira, baada ya mvulana wa miaka 15 kumuua kakake kwa kuzozania jukumu la kupika.

Tukio hilo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Nyamira Kusini (SCPC) Moses Kirong’ baada ya naibu chifu wa kata ya Miruka Robert Maugo kupiga ripoti kuhusu tukio hilo.

Ripoti zinasema kwamba kaka hao wawili walikuwa na mdogo wao wakipika wali walioachiwa na bibi yao wale mchana wakati hakuwa.

Kwa mujibu wa Kenya News Agency, kila mmoja alikuwa na zamu ya kuangalia iwapo wali umeiva, ila kaka yao mdogo alikataa jukumu hilo na vita vikaibuka na kusababisha kifo.

“Wakati zamu ya mwendazake ilipowadia ya kuangalia wali uliokuwa jikoni, alikataa hadi kakae mkubwa akasisitiza ila hakukubali na kuendelea kucheza na kaka yake mdogo wa miaka 7,” naibu chifu alisimulia.

Kirong’ alisema kulingana na kakaake mdogo aliyeshuhudia tukio hilo, mwendazake alipigwa kwenye kifua wakati wa fujo hizo na kupoteza fahamu baada ya kugongwa ngumi kwenye mbavu.

Mkuu huyo wa polisi alisema hatimaye kaka hao wawili waligundua kwamba amezirai na, kaka mkubwa akajaribu kumfufua ila haikufua dafu, hata alipomwagia maji baridi mwilini mwake.
Share:

NABII MKUU DKT GEORDAVIE KUWAPA MITAJI WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SAMUNGE (NMC)

 

 Na Woinde Shizza ARUSHA 


Nabii Mkuu wa kanisa la Ngurumo ya Upako ambaye pia ni balozi wa Amani Afrika Dkt. Geordavie Kasambale ameahidi kuwaunga mkono wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la Samunge (NMC) waliopata janga la kuunguliwa na soko mwaka 2020 kwa kuwagawia fedha za mitaji pamoja na kuwatengenezea baadhi ya miundombinu ya soko.


Akiongea katika ibada iliyofanyika katika kanisa Ngurumo ya upako alisema kuwa anatarajia kwenda kuwapa misaada ya mitaji pamoja na vitu vingine vya sokoni Desemba 30 mwaka huu.


"Nilipokea barua kutoka Kwa wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) wa soko la Samunge wakiwa wanataka msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo mitaji ,miundombinu ya soko napenda kuwaambia nimekubali na mwezi huu tarehe 30 nitaenda sokoni hapo Kwa ajili ya kuwasaidia", alisema nabii Mkuu Dkt GeorDavie 


Akizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa soko la Samunge (NMC)Mraji Njola alisema kuwa wao kama wafanyabiashara wadogo walikaa chini na kuamua kumuandikia barua nabii mkuu Dr. GeorDavie ya kumuomba msaada wa miundombinu ya soko ikiwemo mageti ,mitaro pamoja na mitaji .


"Mwaka 2020 tuliunguliwa na soko hili la Kilombero na wafanyabiashara wengi walipoteza mitaji yao na hata sisi unavyotuona tumeanza upya na hatuna mitaji hivyo tukaona tumtumie nabii barua ya kuomba msaada na tunashukuru Mungu amekubali na ametuhaidi kuja kutuunga mkono Desemba 30 mwaka huu tumefurahi sana na tunamsubiri kwa hamu",alisema 


Alisema kuwa soko lao lina ukosefu wa miundombinu kama mageti ambayo iwapo yatawekwa itasaidia kupunguza wizi unaotokea mara kwa mara katika soko hilo,pia kutengenezwa mitaro ya maji itapunguza tatizo la maji kujaa katika soko haswa katika kipindi cha mvua .


"Katika soko hili kuna wanawake wengi ambao ni wajane wanaotegemea kufanya biashara kwenye soko hilo waweze kulea familia zao na wengi wao walipoteza mitaji kipindi kile ambacho soko liliungua hivyo ujio wa kiongozi huyu wa dini itatusaidia kurudisha tumaini jipya na ndoto zetu ambazo tulikuwa nazo kabla ya kuunguliwa kwa soko"alibainisha


Aidha aliwataka viongozi wengine wa madhehebu mengine ya dini kuiga mfano wa nabii Mkuu wa kusaidia jamii haswa zile za maisha duni ili kuweza kusaidia serikali kuwaondoa watu kwenye umaskini.


"Unajua nabii Mkuu amekuwa ni kiongozi wa dini ambaye anasaidia sana jamii ukiangalia amesaidia vijana kuna aliowapa pikipiki,Kuna aliowapa bajaji ,kunawanawake wamepewa mitaji ,kunaanao walipia wanafunzi ada hii yote ni kuhakikisha anawatoa watu katika kujikwamua kwenye umaskini tukipata viongozi wa dini wengine kama huyu kwakweli watasaidia sana kuosaidia serikali kutoa ajira na kupambana na umaskini "alisema Mwaji Daudi (Mama Shilooo) mfanyabiashara mdogo wa soko la Samunge


Naye mfanya biashara mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel Mangenyi aliitaka serikali kuendelea kuwaunga mkono viongozi wa dini ambao wanasaidia jamii kujikwamua katika umaskini.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 27,2022









Share:

Monday 26 December 2022

MLETE MWANAO BECO PRE & PRIMARY SCHOOL APATE ELIMU BORA

Share:

MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MSISHA AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA

Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Msisha halmashauri ya wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Joyce Exavery (13) ameuawa kwa kukatwa mapanga  akiwa nyumbani kwao katika kijiji cha Ruhita kata ya Kamuli.


Tukio hilo limetokea jana mchana Jumapili Desemba 25,2022 ambapo inaelezwa kuwa mwanafunzi huyo alifanyiwa ukatili (kuchinjwa) na mtu/watu ambao bado hawajafahamika.

Kamanda wa Polisi wa Kagera William Mwampagale amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akizungumza na Malunde 1 blog
Share:

MCHUNGAJI MASEMBO ATAKA UPENDO WA KWELI, KUEPUkA UNAFIKI

Mchungaji Daniel Masembo kutoka Kanisa la EAGT Runzewe akiwasihi waumini kuwa na upendo wa kweli .

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Mchungaji wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Runzewe ambaye pia ni katibu wa kanisa hilo jimbo la Bukombe Mchungaji Daniel Masembo , amewaasa waumini wa kanisa hilo na watanzania kusherehekee siku kuu ya Krismasi (Noeli) kwa kuonyesha upendo kwa watu wote kuliko kuonesha upendo wa kinafiki ambao ni chukizo kwa mwenyezi Mungu.


Mchungaji Masembo amebainisha hayo leo Desemba 25 ,2022 kwenye ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga.


Amesema Sikukuu ya Krismasi ni sherehe ya kuzaliwa mkombozi Yesu Kristo, hivyo ni vyema watu wakaisherehekea kwa upendo, amani na kusaidia watu wenye uhitaji, na siyo kuonyesha upendo wa kinafiki kwa watu wengine.


“Nawaombeni waumini wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center na watanzania wote tusherehekee sikukuu hii ya Krismasi kwa kuonyesha upendo wa kweli kwa watu wote ,na siyo kusherekea sikukuu huku ukiwa na upendo wa kinafiki kwa wenzako ,ukimnafikia mwenzako ipo siku na wewe watakunafikia hadharani,”amesema mchungaji Masembo.


Aidha, amesema Chimbuko la Amani pekee ni kumpokea Yesu Kristo ndani ya mioyo yao na kuonyesha upendo wa kweli , na hakutakuwa tena na migogoro ,mafarakano, na ugomvi katika kanisa na kwenye jamii.


"Kuna watu wako kama Helode wanajifanya wana upoendo na wewe kumbe wana upendo wakinafiki na ndicho chanzo cha mambo yote hayo niliyoyataja ,”ameongeza mchungaji Masembo.


Ibada hiyo imekwenda sambamba na ubatizo ambapo zaidi ya waumini 20 wamebatizwa na kumpokea Yesu Kristo kuwa mwokozi wa maisha yao katika Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga.
Mchungaji Daniel Masembo akiendelea na Ibada ya Ubatizo.
Mwimbaji Daniel Chaula akisifu na kuabudu.
Mwimbaji Kutoka kwaya ya El Shadai akisifu na kuabudu.

Katibu wa kanisa la EAGT Ushirika Mhandisi Fransis Kuya akimkaribisha mchungaji kwenye ibada.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger