Sunday 3 April 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 3,2022

Magazetini leo Jumapili April 3 2022

Share:

RAIS SAMIA APEWA TUZO YA HESHIMA

Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezi Mohamed Mchengerwa akiwa ameshikilia tuzo ya Heshima ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Samia Suluhu Hassan ambayo amepewa na Chama cha Muziki wa Dansi nchini
Katibu Mtendaji wa Chama cha Muziki wa Dansi Agape Msumari akikabidhi Tuzo ya Heshima ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezi Mohamed Mchengerwa

Khadija Seif na Humphrey Shao, Michuzi Tv

Kutoka katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere ambapo leo Aprili 2, 2021 kunafanyika hafla ya utoaji tuzo za muziki zilizoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia BASATA ambapo tukio limeanza kwa kutoa tuzo za heshima na tuzo maalum iliyotolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuthamini mchango wake mkubwa katika sekta ya sanaa nchini.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Matiko Mniko akizungumza na wadau wa Muziki na wageni waalikwa katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere katika hafla ya utoaji Tuzo ambapo tayari amegawa Tuzo za Heshima 4.

Mniko amemtaja Msanii wa Bongofleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond platinum Kwa kutambua Mchango wake katika Muziki wa Bongofleva na kuleta Mapinduzi makubwa na kupelekea Muziki wa Bongofleva Kimataifa na kushirikiana na wasanii mbalimbali wa Kimataifa.

Aidha, Miongoni mwa waliopokea Tuzo za heshima ni pamoja na Mkuu wa Majeshi CDF Jenerali Venance salvatory Mabeyo Kwa Mchango mkubwa uliofanyika katika Vita Vya Uganda na nyimbo nyingi kutungwa kipindi hiko ikiwa ni sehemu ya kuendelea kukuza Muziki nchini.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Matiko Mniko akizungumza na wadau wa Muziki na wageni waalikwa katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere katika hafla ya utoaji Tuzo ambapo tayari amegawa Tuzo za Heshima 4.
Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo Mohamed Mchengerwa akizungumza na Wadau wa Muziki

Share:

Saturday 2 April 2022

TEA YAISHUKURU SERIKALI KWA KUENDELEA KUIJENGEA UWEZO

NA GODFREY NNKO

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi.Bahati Geuzye ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwezesha Mfuko wa Elimu wa Taifa unaoratibiwa na mamlaka hiyo ili kugharamia uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya elimu nchini.

Ameyasema hayo leo Aprili Mosi, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa TEA jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina ya waandishi wa habari iliyoangazia majukumu mbalimbali ya mamlaka hiyo.

"Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita, kwani kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaoratibiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), katika mwaka wa fedha 2021/2022 zaidi ya shilingi Bilioni 8.6 ziliidhinishwa kwa ajili ya kugharimia ufadhili wa miradi 160 ya kuboresha miundombinu ya elimu katika shule 151 nchini.

"Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa madarasa 210 katika shule 70, maabara mbili za sayansi katika shule za sekondari zenye mahitaji maalum, matundu ya vyoo 2,040 katika shule 80, vifaa vya kujifunzia na kufundishia na uendelezaji wa miundombinu katika shule za watoto wenye mahitaji maalum,"amesema.

Kuhusu Mfuko wa Elimu

Sheria Na. 8 ya Mfuko wa Elimu ya Mwaka 2001 pamoja na marekebisho yake (2013), imeainisha madhumuni na majukumu makuu ya Mamlaka ya Elimu Tanzania ikiwemo kufadhili miradi ya elimu katika ngazi zote.
Mratibu Msaidizi Mradi wa Kuendeleza Ujuzi (TEA), Bw.Lusungu Kaduma akichangia jambo katika Semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili Mosi, 2022 jijini Dar es Salaam.

Lengo likiwa ni kuinua kiwango cha ubora wa elimu na kuongeza upatikanaji wake kwa usawa kulingana na mipango na sera za kitaifa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya kijamii na kiuchumi.
Wakati huo huo, Bi.Geuzye amebainisha kuwa, tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo, imefadhili miradi 3,314 ya elimu yenye thamani ya shilingi bilioni 212.64 ambapo shilingi Bilioni 200.38 ni ruzuku na shilingi Bilioni 12.26 ni mikopo nafuu kwa shule za awali, msingi, sekondari, vyuo vya ualimu, vyuo vya ufundi na vyuo vikuu.

"Pia inajumuisha ujenzi wa mabweni 73, vyumba vya madarasa 1,050, matundu ya vyoo 5,880 na nyumba za walimu 560 katika shule 791 za msingi na sekondari, ukarabati wa shule 17 za sekondari kongwe,"amesema.

Katika hatua nyingine, Bi.Geuzye amesema, TEA ambayo ni mamlaka ya Serikali iliyopo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mbali na miradi ya Mfuko wa Elimu wa Taifa,mamlaka hiyo inatekeleza mradi wa miaka mitano (2016/17-2020/21) unaotoa ruzuku za utekelezaji wa miradi ya kuendeleza ujuzi kutoka kwenye Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (Skills Development Fund-SDF).
Afisa Habari wa TEA, Bi.Eliafile Solla akiwasilisha mada kwenye semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili Mosi, 2022 jijini Dar es Salaam.

Mwaka 2017, TEA ilipewa jukumu la kusimamia na kuratibu Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) ikiwa ni sehemu ya Programu ya Kuendeleza Elimu ya Ujuzi na Mafunzo ya Stadi za Kazi zenye Kuleta tija katika Ajira (Education and Skills for Productive Jobs-ESPJ) na Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kukuza na Kuendeleza Ujuzi nchini (National Skills Development Strategy-NSDS).

“Mfuko wa SDF unalenga kuendeleza ujuzi kwa Watanzania ili kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa kwa urahisi na kuchangia uchumi wa Taifa. Mpango umelenga kunufaisha vijana 38,000,”amesema Mkurugenzi Mkuu huyo.
Kaimu Mkurugenzi Huduma za Taasisi (TEA), Bi. Tija Ukondwa akifuatilia semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili Mosi, 2022 jijini Dar es Salaam.

Bi.Geuzye amefafanua kuwa, kupitia mfuko huo ujuzi kiasi cha sh.milioni 385.8 zinatarajiwa kunufaisha vijana 1,018 katika mpango wa Uanagenzi na Utarajari (Internship and Apprenticeship) katika sekta za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Utalii na huduma za Ukarimu, Nishati, Ujenzi na Uchukuzi.

Aidha, amaesema Mfuko wa SDF pia unafadhili mafunzo kwa wanufaika 4,000 kutoka kaya maskini na makundi maalum (Bursary Scheme) hadi Agosti 2021, jumla ya wanufaika 1,627 walipata mafunzo katika Awamu ya Kwanza ya Mpango huo huku Awamu ya Pili ya Mpango wa Ufadhili inatarajiwa kuanza mwezi huu wa Aprili 2022, ambapo wanufaika 2,373 wanatarajiwa kupata mafunzo kabla ya Juni, 2022.
Kaimu Mkurugenzi wa Miradi na Utafutati Rasilimali (TEA), Bi. Anna Makundi akifuatilia semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili Mosi, 2022 jijini Dar es Salaam.

Pia ameeleza kuwa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi pia uko katika hatua za mwisho kuanza kutekeleza ufadhili wa mafunzo ya kiubunifu kwa njia ya mtandao (innovative training through e-learning) ambapo umelenga wanufaika 4,305 ifikapo Juni 2022.

Amesema, zaidi ya shilingi Bilioni 2.3 zitatumika kufadhili mradi huo ambapo zinatokana na ruzuku.
Afisa Utafutaji Rasilimali na Hamasa Mkuu (TEA), Bw.Hamza Hassan akichangia jambo katika semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili Mosi, 2022 jijini Dar es Salaam.

TEA nini?

Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tanzania Education Authority-TEA) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge ya Mfuko wa Elimu Na. 8 ya mwaka 2001 chini ya kifungu 5 (1) pamoja na marekebisho yake (2013) kwa lengo la kuratibu uendeshaji wa Mfuko wa Elimu.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Bi.Bahati Geuzye akiwa pamoja na watuumishi wa TEA wakipata picha ya pamoja na waandishi wa habari katika semina ya waandishi wa habari kuhusu majukumu ya TEA iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TEA leo Aprili Mosi, 2022 jijini Dar es Salaam.

Madhumuni ya Mfuko wa Elimu ni kuongeza nguvu za Serikali katika kugharamia miradi ya elimu ili kuinua ubora wa elimu na upatikanaji wake kwa usawa, katika ngazi zote za Elimu kwa Tanzania Bara na Elimu ya Juu kwa Tanzania Zanzibar.
Share:

OJADACT, ERC WATOA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI ZA UCHOKONOZI KWENYE UHALIFU WA MAZINGIRA

Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred  akifungua Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la  Environmental Reporting Collective la Nchini Malaysia (ERC) kimeendesha mafunzo ya siku moja ya  Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye Sekta ya  Uhifadhi wa Mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumamosi Aprili 2,2022 katika Ukumbi wa Nyakahoja Jijini Mwanza na kukutanisha pamoja waandishi wa habari 20 kutoka Vyombo mbalimbali ya Habari ambapo Mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Hassan Masala.

Akifungua Mafunzo hayo, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Afisa Tawala wa Nyamagana Bwana  Yonas Alfred   ameipongeza OJADACT kwa kuandaa mafunzo kwa waandishi wa habari ili waweze kuwa wabobezi wa kuandika habari za uhalibifu wa mazingira na kwamba elimu watakayopata waandishi hao itawasaidia na kuwawezesha kufanya kazi kwa weledi mkubwa.

“Suala la uhifadhi wa mazingira kwa sasa ni Ajenda ya Kidunia. Bila Mazingira viumbe akiwemo binadamu kesho yetu haiwezi kukamilika, hivyo kuandika habari za uhifadhi wa mazingira ni jambo muhimu sana”,amesema.

Amefafanua kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inatoa kipaumbele kwenye suala la mazingira ndiyo maana kuna Sera ya Mazingira na Kanuni mbalimbali zinazosisitiza kutunza na kuhifadhi mazingira.

“Kuna mfano wazi kuwa wilaya yetu ya Nyamagana na Mkoa wa Mwanza una changamoto nyingi za kimazingira, kuna uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria, kuna ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya shughuli za uchomaji wa mkaa. Naomba changamoto hizi zote baada ya kupata mafunzo haya maalumu ya kuandika habari za uhifadhi wa mazingira basi nendeni mkafichue uhalibifu huo wa mazingira kwa kutumia kalamu zenu”,amesema Alfred.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko amesema mafunzo hayo yamelenga kuwa mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye Sekta ya Mazingira yamelenga kuwajengea uwezo waandishi wa Habari ili kuhakikisha kuwa wanakuwa wabobezi katika uandishi wa habari za uhalifu wa mazingira ili kuwa na uhifadhi wa Mazingira.

“Leo tumekutana na waandishi wa habari 20 wa mkoa wa Mwanza lakini Aprili 9,2022 tutafanya mafunzo mengine kama haya yatakayoshirikisha waandishi wa habari 20 kutoka mikoa mbalimbali”,amesema Soko.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred  akifungua Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza leo Jumamosi Aprili 2,2022 katika Ukumbi wa Nyakahoja Jijini Mwanza. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko, kulia ni Katibu Msaidizi wa OJADACT Isack Wakuganda. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred  akifungua Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko akizungumza wakati wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.

Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Lucyphine Kilanga akiwasilisha mada kuhusu masuala ya uhalifu wakati wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.

Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Martine Nyoni akizungumza wakati wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.

Katibu Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Isaack Wakuganda akizungumza wakati wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko akiwasilisha mada kuhusu Uandishi wa Habari za Uchunguzi kwenye Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira 

Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred  akipiga picha ya kumbukumbu na Waandishi wa habari walioshiriki Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira 
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred  akipiga picha ya kumbukumbu na Waandishi wa habari walioshiriki Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchokonozi (Investigative Journalism) kwenye uhalifu  wa masuala ya uhifadhi wa mazingira.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

MUME MWENYE HASIRA AMUUA JAMAA ALIEMFUMANIA AKIRARUA TUNDA LAKE LIVE KITANDANI

Mume wa umri wa miaka 53 aliyapandwa na mori amemuua jamaa mwenye umri wa miaka 35 baada ya kumpata akirarua tunda lake.

Ripoti ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ilifichua Edwin Komen aliuawa kwa kukatwakatwa Alhamisi, Machi 31, usiku huko Ukwala, Keringet, kaunti ndogo ya Kuresoi Kusini. 

Kisa hicho kilitokea baada ya jamaa ambaye jina lake halikutajwa kumpiga mwanaume huyo akijivinjari na mkewe nyumbani kwake.

 “Akiwa na hasira, mzee huyo mwenye umri wa miaka 53 alinyoosha mkono kuchukua panga na kumshukia jamaa huyo bila huruma akamkata kichwa mara tatu na kumuua papo hapo.

"Katika harakati hiyo mwanamke huyo alikimbia eneo la tukio hadi kwenye mashamba ya karibu na hajaonekana tena," sehemu ya taarifa ya DCI ilisema.

Wanakijiji waliofurika eneo la tukio baada ya kusikia zogo walibaki vinywa wazi kutokana na tukio hilo la kutisha lililotokea katika kijiji chao tulivu. 

Chifu wa eneo hilo Peter Lang'at alisema kifo cha Komen kilikuwa cha kusikitisha. 

Aliwatahadharisha wakazi kutojichukulia sheria mkononi bali wahakikishe wanazingatia sheria. Mshukiwa alikamatwa na polisi na atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji. 

Kwingineko, mwanamke mmoja wa Mombasa alipatikana amefariki dunia katika nyumba yake huko Bamburi baada ya kile kinachoaminika kuwa usiku wa kimahaba na jamaa. 

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Alice Wasike inadaiwa aliaga dunia usiku akilishana uroda na mwanaume ambaye alitoroka baadaye.

Baadaye mtu huyo alitiwa nguvuni.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger