Friday 23 July 2021
SPIKA JOB NDUGAI : TOZO ZA MIAMALA YA SIMU NI HALALI, FEDHA ZITACHAGIZA MAENDELEO
MTANGAZAJI MAARUFU JOSEPHINE CHARLES ASHEREHEKEA 'BIRTHDAY' YAKE
Nafasi 23 za Kazi BRELA, Mwisho wa Kutuma ni Tarehe 6/08/2021
BRELA Wametangaza Nafasi 23 za Kazi( Transfer) kama ifuatavyo;
1.Senior Legal Officer-
2.Legal Officer II
3.Procurement Officer II
4. Senior ICT Officer (ICT System security)
5. ICT Officer I (Database Administrator)
6.Licensing Officer II
7.Registration Officer II
8.Internal auditor II
9.Planning Officer II
10.Senior Records Officer
11.Executive Assistance II
12. Office Management Secretary II
13.Personal Secretary II
14.Records Management Assistance II
15. Senior Receptionist
16. Receptionist II
17. Driver II
18. Office Assistance II
==>>Kujua Zaidi Pamoja na Kutuma Maombi <<BOFYA HAPA>>
__________________
WAZIRI AKERWA NA MRUNDIKANO WA BODABODA VITUO VYA POLISI
RC MTAKA AKIPONGEZA CHUO CHA DODOMA VOCATIONAL TRAINING CENTRE KWA KUTOA UJUZI
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka akizungumza na wahitimu katika Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akisisitiza jambo kwa wahitimu wakati akizungumza nao katika Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima Nchimbi,akisoma risali wakati wa Mahafali ya tano ya chuo hicho kilichopo jijini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akizungumza katika Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka akikata keki wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka akilishwa keki na Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima Nchimbi wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima Nchimbi akiwa katika meza kuu na baadhi ya viongozi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akiwa na Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima Nchimbi pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa meza Kuu wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akimsikiliza Kiongozi wa Wazee Bw.Ezekiel Chadwanga wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akisimikwa Wazee Bw.Ezekiel Chadwanga kuwa kiongozi wao wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akipokea zawadi ya Mbuzi kutoka katika uongozi wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre mara baada ya kuhudhuria Mahafali ya tano ya chuo hicho kilichopo jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka akigawa vyeti kwa wahitimu mbalimbali kulia kwake ni Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima Nchimbi wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo hicho kilichopo jijini Dodoma.
..........................................................................................
Na Alex Sonna,Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka amewataka vijana wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanakuwa na ujuzi ili kwendana na kasi ya Mkoa huo kuwa Makao Makuu ya Nchi.
Akizungumza leo,Julai 22,2021,katika mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre(Dodoma VCT)Mkuu huyo wa Mkoa amewataka vijana wa Mkoa huo kuwa na ujuzi ili kuzikimbilia fursa mbalimbali ambazo zitapatikana kutokana na Mkoa huo kuwa Makao Makuu ya Nchi.
“Wito wangu kwa vijana wa Mkoa wa Dodoma niwatake kuwa na ujuzi katika Makao Makuu ya Nchi niwatake kila mmoja apate ujuzi tumieni vyuo vya kati wazazi niwaombe watoto wapate ujuzi kama hajafaulu apate nafasi ya kusoma ujuzi wowote, Dodoma na Dunia tunayoiendea itakuwa na fursa nyingi lakini kama huna ujuzi utapishana na fursa
“Mtu anaenda Garage anakuwa ni msafisha vioo lakini baadae anajifunza umakenika baadae anajifunza udereva anakuwa dereva,vijana wengi ni bodaboda wewe (wahitimu) kuwa fundi bodaboda utakuwa umepata ajira lazima vijana mhakikishe mna ujuzi na kuna kozi zingine ni fupi tu,”amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
“Dodoma ni Makao Makuu hivyo mnafaida mjiandae miradi inayokuja ikukute una ujuzi hapa ujenzi ni mkubwa sana kama unakaa nyumbani hakuna kibarua ni wewe tu,tumia fursa.Tunajenga hapo Msalato likiwanja likubwa kabisa wakikuuliza una ujuzi wewe upo tu tafuta ujuzi.
“Kama unakaa hapa usidhani unapoteza muda kuna siku utamkumbuka huyu mama wazazi viombeeni hivi vyuo vya ujuzi kama kuna mtu anakudanganya fundi amekosa ajira huyo anakudanganya.Kama unasoma ujuzi shikilia hivyo ninyi hamjapoteza na wazazi mliopo nyumbani usikae na mototo ambaye hana ujuzi.
“Nakuombea Madame kazi zote duniani tunaanzia chini kazi moja tu ndio unaanzia juu kwenda chini kazi hiyo ni kuchimba kaburi na hapa tumeanza.Endelea kusoma mazingira kozi gani utaziongeza ili washindane na tembelea vyuo vingine uone ambavyo wanavyo wewe huna na mitaala pamoja na walimu,”amesema
Mkuu huyo wa Mkoa pia amekitaka Chuo hicho kuongeza ubunifu pamoja na kozi mbalimbali ili watu wengi waweze kupata ujuzi ambao utasaidia kuondokona na changamoto ya ajira.
“Madame nakushauru sana ongeza kozi tujitahidi tuweke matangazo kwamba Chuo kinafundisha kozi hizi na hizi local radio zungumza uwaokoe watoto wa Dodoma,tukitaka vijana wa Mkoa huu wawe washindani tuwapeleke kwenye elimu zote ya darasani,ufundi,elimu dunia aghera.Dunia tunayoiendea tunahitaji maeneo ya namna hiyo nimeona kozi zako ongeza kozi ili watu wajifunze kuwe na ujuzi”amesema.
Pia,amewataka wanafunzi licha ya kujifunza masomo mbalimbali pia wanatakiwa kuwa wabunifu ili wanapomaliza masomo yao waweze kuajirika kirahisi.
“Mjifunze vyote ujuzi na ubunifu ukienda mahali kutafuta vibarua unakuwa umekamilika kwa kila kitu,tunapeleka umeme vijiji vyote vya Tanzania kule vijijini hakuna mafundi maana yake fundi ni wewe.Tunapeleka umeme na maji katika vituo vya afya bomba likiharibika au kuziba wewe ndio fundi,”amesema.
Kuhusiana na changamoto ya eneo la ardhi la chuo hicho,RC Mtaka ameutaka uongozi wa Chuo kwenda makao makuu ya kata ili kukutana na timu ambayo inazunguka Mkoa wa Dodoma kumaliza changamoto za migogoro ya ardhi.
“Nikuombe kama utatumia nafasi vizuri,wanalalamikiana waende makao makuu ya Kata ili waweze kulitatua.Nakuomba uwezekutumia nafasi hiyo kupata muafaka katika siku hizo 10 ambazo tumeziongeza kwani tulitenga siku 10 na tuliongeza siku 10 zingine,”amesema RC Mtaka.
Awali akisoma risala Mkuu wa Chuo hicho,Jemima Nchimbi amesema wanakabiliwa na changamoto kukosa eneo la kujenga chuo kutokakana na eneo walilolipata kukabiliwa na mgogoro.
Amezitaja changamoro zingine ni vijana kutokupata mikopo kwa kozi za ufundi stadi,uelewa mdogo wa wazazi kutambua kozi zote ni kwa ajili ya jinsia zote.
Amesema mafanikio ambayo wameyapata ni pamoja na kufundisha vijana 679 wa kozi fupi,kufundisha vijana wa kike na wa kiume kwa kozi ndefu zaidi ya 333 ambapo vijana 1002 wameweza kupata mafunzo ambapo asilimia 75 wameajiriwa na asilimia 25 wamejiajiri.
Vilevile,amesema wamefanikiwa wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa kina mama zaidi ya 197 kwa kozi za ujasiriamali na baadhi yao wamefungua maduka na kuuza bidhaa walizojifunza kutengeneza.
PROF : CHAGGU: MATUMIZI YA MAKAA YA MAWE HUPUNGUZA UKATAJI MITI OVYO
Tanzania Yairudisha Selous Kwenye Urithi Wa Dunia
Happy Lazaro,Arusha
Arusha.Katibu Mkuu wa Wizara ya maliasili na utalii Dk.Allan Kijazi amesema serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa shirika la umoja wa mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) waliopo hapa nchini wamefanikiwa kuirudisha Poli la akiba la selous ili iendelee kuwepo kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia .
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi kilichoendeshwa kwa njia ya mtandao na kuhudhuriwa na nchi wanachama 21 Dk Kijazi amesema taarifa zilizokuwa zimetumika kutaka selous iondolewa kwenye orodha zilikuwa sio sahihi kwakuwa zilikuwa zimetegemea kusikia na sio kupata taarifa kamili kutoka kwa nchi husika.
“Kama ambavyo tuliripoti wakati wa mkutano wa unesco ulipoanza kulikuwa na mapendekezo ya selous kuondolewa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia sisi na wataalamu tumekaa na kuona taarifa zilizotumika si sahihi na zilikuwa na uongo mwingi “amesema .
Dk Kijazi ameongeza kuwa, mapendekezo ambayo yalikuwa yametolewa na IUCN pamoja na World heritage cental ambayo yalitumika kuishauri UNESCO kuiondoa selous yalikuwa hayajafuata utaratibu kwa kuwa walikuwa hawajashirikishwa kitu ambacho ni tofauti na miongozo walikubaliana kwenye kuchagua na kusimamia maeneo hayo .
“Wataalamu wamefanya kazi kubwa kueleza ukweli kuhusu hali ilivyo na kuziambia nchi wanachama ishirini na moja ambazo zinapiga kula kuwa utaratibu umekosea na taarifa zilizotolewa sio sahihi kwahiyo selous iendelee kubaki na kuwaomba IUCN pamoja na world heritage cental kukusanya taarifa zenye usahihi na sio za kupotosha dunia” ameongeza .
Kwa upande wake Profesa Hamisi Malebo ambaye ni Katibu mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema taarifa iliyokuwa imetolewa ilikuwa imetiwa chumvi kwakuwa walikuwa wamesema selous ilikuwa imepoteza sifa kwa kuwa wamefyeka miti yote na kusababisha uharibifu kitu ambacho sio kweli kwakuwa eneo lililokuwa limefyekwa ni dogo sana .
“Walisema tumefyeka miti yote kwaajili ya kujenga bwawa akati ni sehemu chache sana iliyofyekwa miti na pia walise tembo wamepungua wakati tukiangalia tembo wamezaliana sana katika pori hili kwaiyo tunashukuru kuwa tumeweza kuionesha dunia ukweli wote ambao ulipindishwa na mataifa wameelewa na kupingana na IUCN katika taarifa waliyokuwa wameotoa” amesema
Malebo ameongeza kuwa ,kazi ya kitaalamu huwa ni kuchambua vile vitu ambavyo sio vya kweli kwa kuwa IUCN ni wataalamu washauri wa unesco ni rahisi kukukandamiza usipokuwa makini kwa kuchambua vitu ambavyo ni muhimu .
Naye Evelin Swai ambaye ni Mratibu wa masuala ya unesco kutoka wizarani amewashukuru wataalamu wote waliosaidia kuitetea selous kurudishwa kwenye maeneo ya urithi wa dunia na kusema kuwa ujenzi wa bwawa haukuwa tishio kwenye hifadhi hiyo na kuahidi kuendelea kuishauri serikali ili kuendelea kuhifadi vizuri maeneo ya urithi.
Edward Ishengoma ni Kaimu kamishina wa wizara ya nishati amesema wao kama wahusika wakuu katika kusimamia mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere ambao unayekelezwa na serikali waliamua kuanzisha mradi huo ili uweze kuisadia nchi kwakuwa unafaida nyingi tofauti la IUCN walivyokuwa wameishauri unesco .
“Mradi huu una manufaa makubwa sana tofauti na wao wanavyodhani kwa kuwa una manufaa kwanza kimazingira ,kupata nishati , kuzuia mafuriko na mengine mengi na hatutarudi nyuma “
Waziri Mkuu Aitaka Bodi Ya Korosho Kutafuta Masoko Ya Uhakika
Pia, Waziri Mkuu ameitaka bodi hiyo isimamie mwenendo wa ujenzi wa viwanda vidogo na vikubwa vya kubangulia korosho katika maeneo yote yanayolima zao hilo ili kuondokana na uuzwaji wa korosho ghafi.
Mheshimiwa Majaliwa ametoa maagizo hayo jana (Alhamisi, Julai 22, 2021) wakati akizungumza na Wakuu wa mikoa ya Lindi, Pwani, Mtwara na Ruvuma, Mrajisi wa Ushirika, Viongozi wa vyama Vikuu vya Ushirika wa Korosho katika kikao kilichohusu upatikanaji wa pembejeo za korosho kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa mkoani wa Lindi.
Amesema lazima bodi hiyo ambayo ameizindua lazima iwajibike ipasavyo katika kuhakikisha inaongeza uzalishaji wa zao hilo na iwapo itashindwa Serikali haitosita kuivunja.
“Lazima mfuatilie na kuufahamu mwenendo wa zao mnalolisimamia na mjue mfumo unaotumika katika mauzo yake. Pia muwe na takwimu za wakulima na ukubwa wa mashamba yao ili kuweza kuwahudumia kwa urahisi.”
Waziri Mkuu amesema bodi hiyo inatakiwa iandae kalenda maalumu inayoonesha hatua zote zinazopaswa kufuatwa katika kilimo cha zao hilo kuanzia hatua za uandaaji wa shamba hadi mavuno kwa kuzingatia hali ya hewa ya eneo husika na ipelekwe kwa wakulima.
Amesisiza kwamba utaalamu lazima ufuatwe na uzingatiwe katika kilimo hilo kwa lengo la kuongeza tija kwa wakulima. Pia, Waziri Mkuu ameitaka bodi hiyo ihakikishe pembejeo ikiwemo miche bora na viuatilifu vinapatikana kwa urahisi.
Kadhalika, Waziri Mkuu ameigiza bodi ya korosho iweke mkakati wa utoaji wa elimu kwa wakulima kuhusu kilimo cha zao hilo ikiwa ni pamoja na faida ya kulima zao la korosho. “Tumieni magari maalumu kwa ajili ya kwenda kuwafuata wakulima katika maeneo yao na kuwapa elimu.”
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema tayari mchakato wa kuviwezesha vyama vya wakulima kuanza ubanguaji wa korosho umeanza ambapo katika msimu wa mwaka huu TANECU imepata mkopo kutoka CRDB na itaanza kubangua tani 2,500.
Amesema vyama vingine vitakavyofuata utaratibu huo baada ya TANECU ni TAMCU, MAMCU na RUNALI ambavyo vyote vinampango wa kuanzisha viwanda vyenye uwezo wa kuchakata tani 2,5000 za korosho kwa mwaka.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho, Brigedia Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile amesema wamepokea maelekezo na maagizo yote kwamba watayafanyia kazi kwa kusirikiana na wajumbe wa bodi hiyo na Menejimenti na kwamba hawatafanyakazi kwa mazoea.
Makamu Wa Rais Kuanza Ziara Ya Kikazi Mtwara
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, leo Julai 23, 2021 anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tano mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais akiwa mkoani Mtwara anatarajiwa kushiriki misa ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati Rais wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso Wilaya ya Masasi.
Aidha Makamu wa Rais anatarajiwa kuzindua stendi ya mabasi Wilaya ya Nanyumbu, soko la kisasa la matunda na mbogamboga la Jidah wilayani Masasi, kuzindua kiwanda cha kubangua korosho Wilaya ya Newala pamoja na kuzungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali atakayotembelea.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais anatarajiwa kuweka jiwe la msingi Hospitali ya Kanda ya kusini iliopo Wilaya ya Mtwara na baadaye kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya sabasaba Mtwara mjini.