Thursday 22 July 2021

POLISI WASEMA MBOWE ANAKABILIWA NA TUHUMA ZA KUPANGA NJAMA ZA KUFANYA VITENDO VYA KIGAIDI



Baada ya kushikiliwa kwa takribani siku mbili, Jeshi la Polisi limesema kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi na kuua viongozi wa Serikali.

Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imesema kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa kwamba, Mbowe alikamatwa kwa kuhuma za kupanga na kuandaa kongamano la Katiba mpya jijini Mwanza, jambo ambalo si kweli.

“Mbowe alikuwa anafahamu fika kuwa tuhuma zinazomkabili zilikuwa zinachunguzwa na wakati wowote angehitajika Polisi kwa hatua za kisheria mara tu uchunguzi wake utakapokamilika. Hatua hiyo imefikiwa sasa,” alisema Misime.

Share:

RAIS SAMIA AOMBOLEZA KIFO CHA ANNA MGHWIRA


Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira kilichotokea leokatika hospitali ya rufaa ya Mount Meru mkoani Arusha alipokuwa akipatiwa matibabu.

Rais Samia amesema amepokea taarifa za kifo cha Anna Mghwira kwa majonzi na masikitiko makubwa, hasa akikumbuka mchango wake mkubwa alioutoa katika ujenzi wa Taifa.

Amewaomba Wanafamilia wote wawe na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amemuombea marehemu Anna Mghwira apumzike mahali pema peponi, Amina.




Share:

ANNA HENGA : MATATIZO YA NDOA YANASABABISHA WANAWAKE KULEA WATOTO PEKE YAO

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga

Na Jackline Lolah Minja - Morogoro.

Katika kuendelea kutokomeza vitendo vya ukatili katika jamii , Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimesema kimeandaa mpango maalumu wa kulinda na kutetea haki za makundi maalumu wakiwemo wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.

Akifungua kikao kazi cha kupitia ubora wa mabaraza ya ndoa na sheria za uasili watotokilichofanyika mkoani Morogoro,  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Anna Henga amesema matatizo ya ndoa yamekuwa ni changamoto katika jamii na kupelekea wanawake kuishia kubaki na watoto na kulea wenyewe hivyo huathiri jamii kwa ujumla.

"Watoto huathiriwa zaidi na migogoro ya ndoa kwani wengi hutelekezwa na huingia katika wimbi la vitendo vya kikatili hasa pale familia zinapovunjika na watoto wengi hukosa muongozo, hivyo idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani inaongezeka",amesema Anna Henga.

Kwa upande wake Twaha Kibarula ambaye ni  Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto amesema kikao hicho kitajalidi na kuweka utaratibu bora utakaowasaidia watoaji huduma za usuluhishi wa migogoro ya ndoa kutoka ngazi mbalimbali.

"Hapa tutajadili njia bora zaidi ya wazazi au walezi kupata vibali kisheria ili waweze kupata huduma za malezi ya kambo na kuwasili kwa kiingereza tunaita fostcare and adoption, kutokana na utendaji wa jambo hili ulikuwa hauko sawa", amesema twaha.



Share:

GOLD FM YATAMBULISHWA RASMI IKIUNGURUMA KUTOKA KAHAMA, TCRA YAKABIDHI LESENI ,KANUNI ZA UTANGAZAJI


Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akimkabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen.

****
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio kwa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu'  kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.

Leseni hiyo ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio na Kanuni za Utangazaji imekabidhiwa leo Alhamis Julai 22, 2021 na Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.

Mhandisi Mihayo amesema Leseni hiyo ni ngao ya Gold Fm kufanya kazi huku akiwasihi viongozi wa Gold Fm, kila wanapoamka warejee kwenye kanuni za utangazaji.

“Nawapongeza Gold Fm, haikuwa kazi rahisi, mmepitia michakato mbalimbali, na ndoto yenu leo inatimia baada ya kuwapa leseni. Meneja amejipambanua akisema kituo kitakuwa karibu zaidi na wananchi kuelimisha na kuhabarisha wananchi. Nisingependa kuona Gold fm mnafanya makosa kwa kutofuata kanuni za utangazaji”,amesema Mhandisi Mihayo.

Mkuu huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa ameitaka Gold Fm kuwa ya mfano kwa kutumia lugha fasaha na yenye staha kwenye matangazo yao akiwakumbusha kutojiachia kwani kuna vipindi vinatakiwa visikilizwe muda flani na vingine havitakiwi.

“Leseni yenu inasema mtatumia lugha ya Kiswahili kufanya matangazo, natumaini kuwa mtatumia Kiswahili Fasaha.Hakikisheni mnafuata ratiba ya vipindi vyenu, kama kuna mabadiliko ya vipindi tupeni taarifa TCRA, Msibadilishe vipindi bila kutoa taarifa TCRA”,ameeleza Mhandisi Mihayo.

Mhandisi Mihayo amefafanua kuwa kuanzishwa kwa Gold Fm kunaifanya Kanda ya Ziwa kuwa na idadi ya redio ya 42 kwa upande wa wilaya ya Kahama kuwa na Redio 4 na mkoa wa Shinyanga kuwa na Redio 5.

Ameongeza kuwa katika mkoa wa Shinyanga kuna redio ipo kwenye mchakato wa kuanzishwa huku akiweka wazi kuwa katika Kanda ya Ziwa bado kuna masafa ya uanzishwaji wa redio hivyo wanaohitaji kuanzisha redio wawasiliane na TCRA ili wapatiwe utaratibu.

Akipokea Leseni ya Utangazaji, Mkurugenzi wa Gold Fm, Neema Mghen amesema wamedhamiria kuleta mapinduzi ya vyombo vya habari Kanda ya Ziwa akibainisha kuwa wanatamani kuwa mfano wa vyombo vya habari vingine kwa kutoa habari zenye usawa bila kupendelea upande wowote.

“Lengo kuu la kuanzishwa kwa Gold Fm ni kuelimisha jamii,kuhabarisha, kuburudisha, kuchangia uchumi kwa kuhamasisha ulipaji wa kodi za serikali, kuhamasisha amani kwa taifa letu pamoja na kukumbusha wananchi kanuni,sheria na taratibu za nchi”,amesema Neema.

"Nitumie  nafasi kuwatambulisha kwenu rasmi kituo kipya cha Redio katika Manispaa ya Kahama, Gold Fm, labda katika siku za hivi karibuni mlisikia uanzishwaji wa kituo kipya cha Redio lakini hamkuwa na taarifa za undani zaidi kuhusu Gold Fm.
Mchakato wa kuanzisha Redio hii ulianza takribani miaka mitatu iliyopita na sasa ni rasmi Gold Fm inasikika hewani kupitia masafa ya 88.7 Mhz",amesema Neema.

“Ujio wetu huu wa kishindo wa Gold Fm ‘Sauti ya dhahabu’tukitumia kauli mbiu ya Baba Kaingia Mjini, Mdundo unasikika, burudani iendelee  tunaamini kabisa jamii itanufaika vya kutosha na wenye matangao tunawakaribisha wote kuja kutangaza kupitia kituo chetu cha matangazo”,ameongeza Neema.

Meneja wa Redio Gold Fm, Faraji Mfinanga amesema kibali chao ni kusikika ndani ya mkoa mmoja ambao ni Shinyanga.

Mfinanga ameyataja baadhi ya maeneo ambako sasa Gold Fm inasikika kuwa ni Manispaa ya Kahama, Ushetu, Msalala, Shinyanga vijijini na mikoa ya jirani ikiwemo Geita wilaya ya Bukombe, Mbogwe na kwa upande wa Tabora, Nzega ,Kaliua na Urambo pamoja na maeneo mengine yaliyo jirani na Kahama ikiwemo wilaya ya Biharamulo na Ngara mkoani Kagera.

Naye Mkuu wa Maudhui na Uzalishaji wa Vipindi Bakari Khalid amewahakikishia wasikilizaji wa vipindi kuwa Gold Fm ni ya kipekee sana kwani wamejipanga kikamilifu kuihabarisha jamii na kutatua matatizo ya wananchi huku akibainisha kuwa watadumisha na kuimarisha ushirikiano na waandishi wa habari na media zingine.

ANGALIA PICHA
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akimkabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen (kulia) leo Alhamis Julai 22,2021 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi leseni iliyofanyika katika Hoteli ya Submarine Mjini Kahama. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akimkabidhi Kanuni za Utangazaji wa Vipindi vya Redio Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi. Neema Mghen (kulia).
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio kwa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, kilichopo Mjini Kahama.
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio kwa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, kilichopo  Mjini Kahama.
Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi. Neema Mghen akizungumza wakati Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akikabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio kwa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, kilichopo  Mjini Kahama.
Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi. Neema Mghen akizungumza wakati Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akikabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio kwa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, kilichopo Mjini Kahama.
Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi. Neema Mghen akizungumza wakati Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akikabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio kwa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, kilichopo Mjini Kahama.
Meneja wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Faraji Mfinanga akizungumza wakati Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akikabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio kwa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, kilichopo Mjini Kahama.
Mkuu wa Maudhui na Uzalishaji wa Vipindi Gold Fm, Bakari Khalid akizungumza wakati Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akikabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio kwa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, kilicho Mjini Kahama.
Meneja wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Faraji Mfinanga akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi. Neema Mghen (kushoto).
Watangazaji wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, iliyopo Mjini Kahama wakiwa ukumbini
Kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi. Neema Mghen akifuatiwa na Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo na Meneja wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm Faraji Mfinanga akiteta jambo na  (kulia) wakiwa ukumbini.
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakipiga picha ya pamoja na Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo baada ya hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio.
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakipiga picha ya pamoja na Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo baada ya hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio.
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakipiga picha ya pamoja na Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo baada ya hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

TCRA YAHAMASISHA WATUMIAJI WA SIMU ZA MKONONI 'KUJANJARUKA'

Share:

Tanzia: ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ANNA MGHWIRA AFARIKI DUNIA




Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Elisha Mghwira


Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, na mgombea Urais nchini Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Anna Elisha Mghwira, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru, Arusha.

Imeelezwa kuwa Mama Mghwira amefariki dunia leo Julai 22, 2021, majira ya mchana, ambapo taarifa zinadai kwamba wiki moja iliyopita alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Nkoaranga kwa tatizo la kupumua ambapo baadaye hali yake kuwa mbaya alihamishiwa hospitali ya Mount Meru

Chanzo- EATV
Share:

MUME AUA MKE AKIOMBWA HELA YA ADA YA MTOTO


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi (ACP) Stella Mutabihirwa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya jeshi hilo mkoani hapa leo hii.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi (ACP) Stella Mutabihirwa, akiwaonesha  waandishi wa habari (hawapo pichani) misokoto ya bangi iliyokamatwa na jeshi hilo.
 
Na Dotto Mwaibale, Singida

MWANAMKE mmoja Moshi Mkimbu (40)  mkazi wa Kijiji cha Ndulungu Tarafa ya Ndago Wilaya ya Iramba  mkoani Singida ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali  na mume wake aitwaye Juma Shabani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi (ACP) Stella Mutabihirwa akizungumza na waandishi wa habari leo  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo lilitokea Julai 18, 2021 katika  kitongoji cha Misughaa na kuwa  mtuhumiwa  alikamatwa na atafikishwa mahakamani  kujibu shitaka  lake. 

Mutabihirwa alisema kuwa uchunguzi  wa  awali wa Jeshi la polisi  umebaini kuwa chanzo kikubwa cha mauaji  hayo  ni  ugomvi  wa  kifamilia  pamoja  na ulevi  baada ya  marehemu  kudai  pesa za  mahindi  yaliyouzwa  kwa  ajili ya ada ya mtoto shuleni, ndipo mume wake  huyo alianza  kumshambulia kwa kumpiga na fimbo na kitu  chenye  ncha kali na kusababisha kifo cha mke wake. 

Katika tukio lingine alisema jeshi hilo mkoani Singida linaendelea na misako mbalimbali ya kubaini uhalifu kutokana na mikakati iliyojiwekea ya kuweka mkoa wa singida salama ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu Aprili hadi Julai 2021, Jeshi la polisi limefanya misako na kufanikiwa kukakamata dawa aina bhangi misokoto 757 watuhumiwa tisa (9), watuhumiwa saba kesi zipo mahakamani hatua ya kusikilizwa na watuhumiwa wawili wametiwa hatiana.

Alisema mtuhumiwa mmoja wa dawa za kulevya  aina heroine kete moja alikamatwa  na kesi ipo mahakamani na  Pombe ya moshi (gongo) lita 113 zilikamatwa na watuhumiwa  24   ambapo watuhumiwa walifikishwa  mahakamani.  

"Kesi 16 watuhumiwa walitiwa hatiani na watuhumiwa 8 kesi bado zinaendelea mahakamani hatua ya kusikilizwa na pia pikipiki moja aina ya SANLG ilikamatwa baada ya pikipiki hiyo kuporwa  na mtuhumiwa mmoja ambaye alikamatwa na alifikishwa mahakamani na tayari  amehukumiwa kutumikia jela mwaka mmoja," alisema.

Mutabihirwa  ametoa shukrani kwa wananchi na raia wema kwa kutoa ushirikiano na kupata mafanikio hayo hivyo  wito wa jeshi hilo kwa  wananchi  wote hususani  wanandoa  kuacha tabia na vitendo  vya  ukatili wa kijinsia katika  familia zinazo wazunguka na kuwatengemea kwani vitendo hivi hupelekea madhara makubwa  na  kusababisha  vifo  katika jamii. 

Aidha Mutabihirwa amewataka wananchi kuacha tabia ya ulevi uliopindukia na matumizi ya dawa kulevya bali waishi  kwa amani, furaha na  kufuata sheria za nchi na pindi matatizo ya kifamilia yanapotokea wafike kwenye vituo vya Polisi kwenye madawati maalumu ya kushughulikia  masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na watoto na si kujichukulia sheria 
mkononi.

Share:

Project Manager at BRAC Tanzania

Project Manager    Full TimeTanzaniaPosted 4 hours ago BRAC Tanzania The ideal candidate will be responsible for the overall daily management of the Project including supervision of staff, planning, budgeting, implementation, and M&E. The specific responsibilities include. Responsibilities Project Planning   Ensuring that all program activities are developed and implemented in accordance with the organization’s […]

This post Project Manager at BRAC Tanzania has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Njombe:Wapenzi wafia chumbani kwa jiko la mkaa


Na Amiri Kilagalila,Njombe
Watu wawili wamepoteza maisha mkoani Njombe baada ya kuingia na jiko la mkaa ndani ya chumba cha kulala kwa lengo la kupunguza baridi Mkoani Njombe.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amethibitisha kutokea kwa tukioa hilo lililowakuta Benitho Mbatha (23) mpiga debe wa mjini Njombe na Jazila Said Mndendeule (27) mkazi wa Namtumbo.

“Baada ya kufariki hakuna mtu ambaye aligundua kama kuna watu wamefariki,tukio hili limetokea tarehe 17 mwezi wa saba majira ya saa tano na nusu huko mtaa nwa National Housing kata ya Njombe mjini wakiwa wamelala kwenye chumba kimoja”alisema Kamanda Hamis Issa

Aidha amesema “Sababu ya kifo chao inaonyesha wakati wakiwa hai waliweka moto wa mkaa kwa ajili ya kujihifadhi na baridi na huu mtindo wa kuweka mkaa kwa watu wa Njombe ndio mtindo wao”alisema Hamis Issa

Aidha kamanda Issa ametowa wito kwa wananchi wa Njombe kutumia njia nyingine kujikinga na baridi na si kuota moto kama ambavyo wengi wamekuwa wakifanya kwa kwani kufanya hivyo ni hatari kwa maisha yao.

“Niwaombe wananchi wewe unaona Chumba chako ni kidogo na unatumia mkaa ndani hiyo ni hatari nyingine na huko lilikotokea tukio chumba ni kidogo na kina dirisha moja na dogo sana.Acheni kulala na jiko ndani ya nyumba sasa hivi ni hatari tafuteni nguo nzito nzito za kuzuia baridi lakini sio moto wa mkaa”alisema kamanda Issa

Kamanda Issa amesema tukio hilo ni la tatu kutokea mkoani Njombe kutokana na tukio jingine kumkuta dada mkazi wa Songea aliyekuwa mhudumu wa baa moja mjini Njombe kufariki ndani kwa jiko la mkaa huku mwingine akifariki wilayani Wanging’ombe kwa jiko la mkaa.

Amani Samsoni Mwalongo ni mmiliki wa Nyumba aliyokuwa akiishi marehemu Benitho Mbata huku akiwa ni mtu wa kwanza kushuhudia tukio hilo baada ya yeye kwenda kumtembelea marehemu na kuwaona wote wawili wakiwa wamefariki

“Lakini bado mimi nilifuatilia kwa majirani wanasema yule mwanamke alikuwa anaelekea Madaba,alikosa nauli na huyu kijana kwa kuwa yupo pale kwenye magari akamwambia njoo upumzike kwanza na kesho nitakusaidia nauli ya kukufikisha kwenu kwa hiyo hiki kitu kinahuzunisha sana”alisema Amani Samson

Kwa upande wao Majirani wanasema “Marehemu huwa anapenda sana kuja hapa na alikuja pia akachukua moto na akachukua chipsi Mayai akasema nina mgeni wangu huko ndani lakini siku baada ya siku tukashangaa haonekani mpaka tulipoona wanakuja polisi,lakini sio vizuri kwenda kulala sehemu usioijua kwa mfano hapo huyo mwanaume angefariki halafu angebaki mwanamke tayari angekuwa na kesi ya kujibu”alisema mmoja wa majirani
.

Share:

Kauli Ya Serikali Kuhusu samaki waliokutwa wamekufa ufukweni Dar es Salaam


Tarehe 21 mwezi Julai, 2021 saa 3:30 asubuhi, ofisi ndogo ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mkoa wa Dar es Salaam ilipokea taarifa kutoka kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala kuhusu tukio la kuelea kwa samaki waliokufa katika ufukwe uliyopo karibu na Hospitali za Agha Khan na Ocean Road jijini Dar es Salaam.


Kufuatia taarifa hiyo maafisa uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi waliuomba uongozi wa kipolisi Ilala kuimarisha ulinzi eneo hilo ili kuzuia wananchi kuchukua samaki waliokuwa wakielea ufukweni hapo wakati hatua zaidi za haraka zikichukuliwa kuzuia uingizaji wa samaki hao katika Soko la Magogoni Feri lililopo karibu na eneo la tukio.


Baada ya kuimarisha ulinzi eneo la Soko la Magogoni Feri na eneo la tukio, wananchi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, maafisa wa wizara, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), maafisa uvuvi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa na meneja wa Soko la Magogoni Feri walikusanya samaki kiasi cha Kilogramu 164 na kufikisha Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Baada ya kutolewa kwa ufafanuzi wa hali iliyojitokeza ilikubaliwa kuwa sampuli za samaki hao zichukuliwe kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara ili kubaini sababu za vifo vya samaki hao.


Sampuli zilichukuliwa kwa ajili ya maabara ya TAFIRI, maabara ya Taifa ya Uvuvi (Dar es Salaam) na Polisi Kitengo cha Sayansi ya Uchunguzi (Forensic Investigation) kwa ajili ya kupeleka maabara ya mkemia mkuu wa serikali.


Kiasi cha Kilogramu 156 kilichosalia kilikabidhiwa kwa afisa uvuvi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kuteketezwa na tukio la kuteketezwa lilishuhudiwa na maafisa wa wizara, uongozi wa Soko la Feri, ofisi ya uvuvi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na wananchi waliokuwepo eneo la Soko la Magogoni Feri.


Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi inapenda kuwashukuru wananchi wote waliokuwepo kwenye ufukwe wa hospitali za Agha Khan na Ocean Road pamoja na Soko la Magogoni Feri wakati wa tukio hili kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha uliofanikisha kuzuia kuingizwa kwa samaki hao sokoni na hatimaye kuteketezwa na afisa uvuvi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.


Aidha, Wizara inapenda kuwaasa wananchi kuendelea na biashara ya samaki katika masoko ya Jiji la Dar es Salaam kama ilivyo kawaida na umma utajulishwa kuhusu sababu za vifo vya samaki hao walioteketezwa mara baada ya kupatikana kwa mujibu wa uchunguzi wa kimaabara.


Imetolewa:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini




Share:

Waziri Mkenda Na Mkakati Wa Kuimarisha Bei Za Mazao Ya Kilimo


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda ameeleza kuwa serikali inaendelea na mkakati wa kuimarisha bei za mazao ya kilimo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam ambapo amebainisha kuwa Serikali inapenda kuwaona wakulima wanapata faida kutokana na kilimo, ndiyo maana haijaweka kodi yoyote kwenye mbolea kama wengine wanavyozusha.

Amesema kuwa uzalishaji wa mazao una gharama kubwa japo bei za mazao kuna wakati zinakuwa hazieleweki.

“Bei ya mazao ya mahindi kwa sasa inazua taaruki kwenye baadhi ya mikoa, kwani yanauzwa kwa bei ndogo tofauti na gharama za uzalishaji alizotumia mkulima, hii inamkandamiza anaweza kushindwa kumudu gharama za pembejeo,” Amesema.

Kuhusu suala la mbolea, Waziri Mkenda amesema kuwa suala la mbolea limezua taaruki ambapo baadhi ya watu wamedai kuwa kupanda kwa bei ya pembejeo hiyo inachangiwa na kodi iliyowekwa na serikali.

“Hakuna kodi yoyote iliyowekwa kwenye mbolea kwa kuwa Serikali imelenga katika kuhakikisha inapatikana kwa bei nafuu ili kuwahamasisha wakulima kutumia mbolea ambayo inawasaidia kuvuna mazao mengi,” Amesema Waziri Mkenda na kuongeza kuwa

“Tunaamini hatua hii itasaidia mbolea kuingia kwa wingi nchini hivyo wafanyabishara watakuwa na bei ya ushindani ambayo haimuumizi mkulima, pia tunachoangalia sisi mbolea inayoagizwa iwe na viwango vya ubora unaotakiwa,”

Amesema mfumo wa zabuni haujawasaidia kwa kuwa licha ya kuwa makampuni mengi yalikuwa yanajitokeza yanachakuliwa machache kisha bei inapangwa lakini siyo rafiki kwa wakulima. 

“Japo hatuna uwezo wa kushusha bei kwenye soko la dunia lakini tunahitaji kuona wafanyabiashara wanasaidia kuwezesha mbolea kupatikana kwa wingi, Serikali inafanya juhudi kila inavyoweza ikiwamo hata kupunguza gharama za kulipia maghala ya kuhifadhia nafaka,” Amekaririwa Mhe Waziri

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Dkt Anselm Moshi amewaeleza waandishi wa habari kuwa Bodi hiyo inanunua mahindi kwa bei nzuri ukilinganisha na bei iliyopo sokoni.

Dkt Moshi ameeleza kuwa ununuzi wa mahindi ni kati ya shilingi 250 hadi 480 ambapo bei inatofautiana kwenye mikoa husika.

“Wilaya ya Nkasi mahindi yanauzwa 250 hadi 270 kwa kilo moja, kanda ya kaskazini yanauzwa kwa bei ya shilingi 450 hadi 485 kwa kilo, hivyo bodi imeshatuma jumla ya shilingi bilioni 7.47 ya kununua jumla ya tani 14,948 kwa wastani wa shillingi 500 kwa kilo,”  Amesema Dkt Moshi

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Militon Lupa amesema  kuwa wakala unatarajia kununua takribani tani 165,000 za aina tatu za nafaka kwa msimu wa mwaka 2021/2022 kutoka kwenye mikoa yenye uzalishaji mkubwa kati ya hizo mahindi yatanunuliwa tani 150,000.

Lupa amesema kuwa katika kipindi kirefu NFRA imekuwa ikinunua mahindi pekee ambapo hivi sasa imeanza kununua nafaka aina ya mahindi, Mtama na mpunga

MWISHO



Share:

Communication Officer at HPSS-Tuimarishe Afya

Job Title: Communication Officer Reporting to : Project Manager Location : Dodoma Level of Engagement :Full time Similar Jobs Summary of the Position The Health Promotion and System Strengthening Project (HPSS-Tuimarishe Afya) is a Swiss-Tanzania Corporation project being executed by the Swiss Tropical and Public Health Institute (SwissTPH) with its headquarter in Dodoma Tanzania. The HPSS project is being implemented since […]

This post Communication Officer at HPSS-Tuimarishe Afya has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Accountant at Medical Teams International

ACCOUNTANT                                                                                 Medical Teams International Tanzania Department : Finance Reports to: Direct: Senior Finance Officer Technical: NA […]

This post Accountant at Medical Teams International has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

CHUO CHA CCOHAS KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO DIPLOMA YA UFAMASIA NA UTABIBU


Share:

Mpyaa : PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOGTUWE TUNAKUTUMIA HABARI BURE MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO

Share:

YANGA WATUA KIGOMA KUKIPIGA NA SIMBA SC JUMAPILI


Wachezaji wa Yanga wakishuka kwenye Ndege baada ya kufika mkoani Kigoma

Kikosi cha Yanga SC kimefika salama mkoani Kigoma tayari kwa maandalizi ya mchezo wa fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya watani zao Simba SC mchezo utakaochezwa siku ya Jumapili Julai 25, 2021 katika dimba la Lake Tanganyika.

Timu hiyo ya wananchi iliondoka leo Asubuhi jijini Dar es salaam kwa usafiri wa ndege, na wamewatangulia watani zao Simba ambao bado wapo Dar es salaam. Huu utakuwa ni mchezo wa nne timu hizi zinakutana msimu huu kwenye mashindano yote, kwenye michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu Yanga wameshinda mchezo mmoja na wametoka sare mchezo mmoja lakini pia Yanga waliifunga Simba kwenye fainali ya Mapinduzi Cup kule visiwani Zanzibar kwa mikwaju ya penati 4-3.

Na kueleka mchezo huu wa fainali tayari shirikisho la soka nchini TFF limetangaza waamuzi watakao chezesha mchezo huu, ambapo mwamuzi wa kati ni Ahmed Arajiga kutoka Manyara, mwambuzi msaidizi namba moja yani Line 1 ni Ferdnand Chacha kutoka Mwanza, msainizi namba mbili Line 2 ni Mohamed Mkono wa Tanga na mwamuzi wa akiba yani fourth official ni Elly Sassi wa Dar es salaam.

Chanzo -
Share:

POLISI WENYE MABOMU NA MBWA WAZUIA KONGAMANO LA CHADEMA


Mbwa na Polisi waliozuia kongamano la CHADEMA Mwanza

Kongamano la Chama cha Siasa cha CHADEMA la kudai Katiba mpya lililokuwa lifanyike leo Jijini Mwanza, limeshindwa kufanyika baada ya polisi waliobeba mabomu ya machozi, silaha za moto pamoja na magari yenye mbwa kutanda katika eneo la hoteli mahali ambapo kongamano hilo lingefanyika.

Hapo jana Julai 20, 2021, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, alipiga marufuku mikusanyiko isiyo ya lazima katika mkoa huo kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa hatari wa Corona.

Via EATV

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger