Tuesday 29 December 2020

Dkt. Ndugulile Ahimiza Taasisi Za Serikali Kutumia Kituo Cha Taifa Cha Data Kuhifadhi Taarifa Zao


 Na Prisca Ulomi, WMTH
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amehimiza taasisi za Serikali kutumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC) kuhifadhi taarifa zao kwa kuwa ni sehemu salama, ina miundombinu na mifumo ya TEHAMA ya kisasa na ina wataalamu wabobezi na ina nafasi ya kutosha kwa ajili ya kupangisha mifumo

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea NIDC, Dar es Salaam ambapo aliambatana na Naibu Waziri wake, Mhandisi Kundo A. Mathew, Katibu Mkuu, Dkt. Zainabu Chaula, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba na watendaji wa Wizara hiyo na kubaini kuwa ni taasisi 84 tu za Serikali zinatumia NIDC kati ya taasisi 149 zinazohifadhi taarifa zake kwenye kituo hicho

Amezikumbusha taasisi za Serikali kuzingatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alilolitoa alipotembelea NIDC kuzindua Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato (electronic Revenue Collection System - eRCS) mwaka 2017 ambapo umeiwezesha NIDC kuongeza makusanyo ya mapato yake kutoka shilingi bilioni 1.4 mwaka 2019 na kufikia shilingi bilioni 2.76 mwaka 2020

Naye Naibu Waziri, Mhandisi Kundo A. Mathew ameipongeza NIDC kwa kutengeneza mifumo mbali mbali ya TEHAMA ambayo inaiwezesha Serikali kuongeza makusanyo ya mapato na kurahisisha  maisha kuendana na mahitaji ya wananchi ikiwemo kulipa tiketi ya mabasi ya njia ya mtandao; kuweka mafuta kwenye gari; kulipa kiingilio kwenye uwanja wa mpira wa Benjamin Mkapa; usafiri wa kivuko cha Kigamboni; usajili wa leseni BRELA;  na maegesho ya magari uwanja wa ndege wa Dar es Salaam

Katibu Mkuu, Dkt. Zainab Chaula amewaeleza watendaji wa NIDC washirikiane kwa karibu na wataalamu wa Wizarani ili kuhakikisha kuwa Serikali inaendelea kuwahudumia wananchi kwa kutumia TEHAMA ili kuokoa muda wao kutafuta huduma za Serikali badala yake watumie kufanya kazi na kuongeza uzalishaji mali

Meneja wa NIDC, Geofrey Mpangala amesema kuwa wateja wanaotumia kituo hicho wamepunguza gharama za uendeshaji na uwekezaji kwenye taasisi zao kwa kuwa hawajengi miundombinu na mifumo ya TEHAMA; wateja wanapata viwango vya juu vya data yenye kasi na uhakika wa usalama wa data zao na huduma zinatolewa kituni hapo kwa saa 24.

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amemshukuru Dkt. Ndugulile kwa ziara yake kwa kuwa imeongeza ari na shauku ya utendaji kazi kwa wataalamu wa NIDC ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wateja na mifumo ya TEHAMA ili kurahisisha huduma kwa wananchi

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari




Share:

Waziri Bashungwa Kuongoza Waombolezaji Kumuaga Mngereza


Na Eleuteri Mangi, WHUSM-Dar es salaam

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa atawaongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza, aliyefariki Desemba 24, 2020 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alipokuwa anapatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na BASATA na familia, mwili wa marehemu Mngereza utawasili viwanja vya Karimujee jijini Dar es salaam kesho Jumanne Desemba 29, 2020 saa 3:20 asubuhi.

Mara baada ya mwili wa marehemu kuwasili katika viwanja hivyo, pamoja na taratibu nyingine za mazishi, kutakuwa na ibada fupi ya kumuombea, salamu za rambirambi pamoja na nyimbo maalum za maombollezo kutoka kwa wasanii na vikundi vya sanaa watakaoimba kumsindikiza kiongozi huyo.

Pamoja na Mhe. Waziri Bashungwa, watakuwepo  pia  viongozi mbalimbali wa Serikali, familia, watumishi wa Wizara na taasisi ya BASATA, wasanii, wadau wa tasnia ya sanaa, ndugu, jamaa, marafiki na baadaye safari ya kuelekea Suji wilaya ya Same mkoa wa Kilimanjaro itaanza ambapo mwili wa mrehemu Mngereza utazikwa Jumatano, Desemba 30,2020.

Marehemu Mngereza atakumbukwa kwa umahiri wake mkubwa wa kuisimamia Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya mwaka 1984 na Kanuni zake na uwezo wake wa kusimia maadili katika kazi za Sanaa pamoja na kuifahamu sekta kwa mapana yake hatua iliyosaidia kukuza maendeleo na utengenezaji wa kazi za Sanaa nchini zenye kujali ubora na maadili.


Share:

Waziri Bashungwa: Tutahakikisha Michezo inaendelea kuipa heshima nchi


Na Shamimu Nyaki –WHUSM,Dar es Salaam
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema kuwa katika uongozi wake atahakikisha heshima ya michezo hapa nchini inarejea.

Mhe. Bashungwa ameyasema hayo Desemba 28,2020 Jijini Dar  es  Salaam ambapo alifanya kikao na makocha pamoja na wanamichezo wa zamani na ameeleza kuwa  Serikali imeanza kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Michezo.

“Lengo la kikao hiki ni kupokea mawazo kutoka kwenu namna bora ya kuendesha michezo ili tupate mafanikio kama ambayo tulipata hapo zamani wakati nyie mkilitumikia taifa letu katika soka” alisema, Mhe. Waziri Bashungwa.

Mhe. Bashungwa ameongeza kuwa marekebisho yaliyofanywa katika Sheria za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ya mwaka 1967 kuhusu michezo ya ridhaa na kulipwa, Kwa hivi  sasa inatambua  michezo ya kulipwa  ambapo kuna wachezaji zaidi ya 2000 wanaocheza michezo ya kulipwa ndani ya nchi na wanamichezo takriban 28 wanacheza michezo ya kulipwa nje ya nchi.

Aidha, Mhe. Waziri Bashungwa amewapongeza wachezaji wa zamani kwa jinsi walivyojituma kwa nidhamu na moyo wa kizalendo kuipigania nchi na kufanikiwa kufuzu  katika mashindano ya AFCON mwaka 1979.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega ameiagiza Idara ya Michezo kusimamia maazimio yote ya kikao hicho kufanyiwa kazi na matokeo yaonekane.

“Nia yetu ni kuendeleza michezo, na hili tutalisimamia vyema hivyo tunaomba mawazo mazuri kutoka kwenu namna ya kuendeleza michezo” alisema Mhe.Ulega.

Mhe. Ulega ameongeza kuwa dhamira ya vikao na wadau wa michezo ni kutathmini michezo ilipotoka, ilipo na wapi ielekee kwa maslahi ya taifa.

Naye Mdau wa michezo michezo Bw. Ally Mayai Tembele ameishukuru Serikali kwa kuandaa vikao vya kukutana na wadau kupokea mawazo kuhusu maendeleo ya michezo nchini, huku akieleza kuwa michezo inahitaji nidhamu na kuwekeza kwa Watoto wa shule za msingi na sekondari, vifaa vya michezo na miundombinu bora ya michezo.


Share:

Joe Biden: Trump ameharibu idara muhimu za usalama


Vitengo muhimu vya usalama vimefanyiwa uharibifu mkubwa chini ya utawala wa rais Donald Trump , rais mteule wa Marekani Joe Biden amesema.
 

Biden amesema kwamba timu yake haipati habari inazohitaji kutoka kwa idara ya ulinzi wakati ambapo inajiandaa kuchukua madaraka.
 

Kiongozi huyo mteule ametoa kauli hiyo wakati akizungumza baada ya kupatiwa habari na Maafisa wa Usalama pamoja na wale wa masuala ya sera za kigeni.

Biden anatarajiwa kuapishwa Januari 20, mwakani kuwa rais, hata hivyo Rais Trump amekataa kukubali kushindwa katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Kwa wiki kadhaa baada ya uchaguzi huo wa Novemba 3 , Biden alizuiliwa kupata habari muhimu za kijasusi , ikiwa ni muhimu na utaratibu wa kawaida katika mchakato wa kumkabidhi rais mteule madaraka.

Kufuatia matamshi ya Joe Biden siku ya Jumatatu , kaimu waziri wa ulinzi Christopher Miller amesema kwamba maafisa wamekuwa wakifanya kazi kwa utaalamu mkubwa kuunga mkono mpito.



Share:

Rais Magufuli Akagua Maendeleo Ya Ujenzi Wa Daraja La Kigongo-Busisi Mkoani Mwanza


Rais Dkt John Magufuli amekagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi ambalo litakuwa na urefu wa Kilometa 3.2, na hivyo kuwa daraja refu kuliko yote Afrika Mashariki na Kati.

Daraja hilo ambalo linajengwa na Mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kwa gharama ya takribani Shilingi Bilioni 700, linatarajiwa kukamilika mwezi Februari mwaka 2024.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Mwanza, – Mhandisi Vedastus Maribe amesema ujenzi wa daraja hilo ulioanza Februari 25 mwaka huu umefikia asilimia 11.18 ikiwemo ujenzi wa daraja la muda ambao umefikia asilimia 51.6 na kwamba hadi kukamilika kwake linatarajiwa kuwa na nguzo 67 zikiwemo tatu kubwa.

Akizungumza baada ya kujionea kazi ya uchimbaji wa mashimo yenye urefu wa Meta tatu ndani ya mwamba kwa ajili ya ujenzi wa nguzo hizo, Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa na hatua iliyofikiwa, lakini amemtaka Mkandarasi CCECC kuongeza kasi ya ujenzi kwa kufanya kazi usiku na mchana ili likamilike haraka na kuanza kutumika.

Rais Magufuli amesema daraja hilo lina umuhimu mkubwa kwa Watanzania na nchi jirani za Uganda, Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Amewapongeza wananchi wa Kanda ya Ziwa kwa kujengwa kwa daraja hilo ambalo litaepusha ajali za mara kwa mara za kuzama kwa mitumbwi inayovusha watu na bidhaa mbalimbali kati ya Kigongo na Busisi.

Ametoa wito kwa Wananchi hasa vijana wanaopata ajira katika mradi huo, kufanya kazi kwa bidii na uadilifu badala ya kuiba vifaa vya ujenzi.

Tayari Rais Magufuli amewasili nyumbani kwake Chato mkoani Geita.



 


Share:

District Coordinators,Tools for Integrated Management of Childhood Illness at PATH

District Coordinators, Tools for Integrated Management of Childhood Illness     Job Description PATH is a global organization that works to accelerate health equity by bringing together public institutions, businesses, social enterprises, and investors to solve the world’s most pressing health challenges. With expertise in science, health, economics, technology, advocacy, and dozens of other specialties, PATH […]

The post District Coordinators,Tools for Integrated Management of Childhood Illness at PATH appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Accountant (5- Posts) at Bugando Medical Centre

Bugando Medical Centre is a consultant and teaching hospital for the Lake and Western zones of the United Republic of Tanzania. It is situated along the shores of Lake Victoria in Mwanza City. It has 900 beds and over 1200 employees. It is a referral centre for tertiary specialist care for eight regions, namely: – […]

The post Accountant (5- Posts) at Bugando Medical Centre appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Public Relations Officer (2 – Posts) at Bugando Medical Centre

Bugando Medical Centre is a consultant and teaching hospital for the Lake and Western zones of the United Republic of Tanzania. It is situated along the shores of Lake Victoria in Mwanza City. It has 900 beds and over 1200 employees. It is a referral centre for tertiary specialist care for eight regions, namely: – […]

The post Public Relations Officer (2 – Posts) at Bugando Medical Centre appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Procurement and Supplies Officer (3 – Posts) at Bugando Medical Centre

Bugando Medical Centre is a consultant and teaching hospital for the Lake and Western zones of the United Republic of Tanzania. It is situated along the shores of Lake Victoria in Mwanza City. It has 900 beds and over 1200 employees. It is a referral centre for tertiary specialist care for eight regions, namely: – […]

The post Procurement and Supplies Officer (3 – Posts) at Bugando Medical Centre appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Accounts Clerk (5- Posts) at Bugando Medical Centre

Bugando Medical Centre is a consultant and teaching hospital for the Lake and Western zones of the United Republic of Tanzania. It is situated along the shores of Lake Victoria in Mwanza City. It has 900 beds and over 1200 employees. It is a referral centre for tertiary specialist care for eight regions, namely: – […]

The post Accounts Clerk (5- Posts) at Bugando Medical Centre appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

CCTV-Operator (2- Posts) at Bugando Medical Centre

Bugando Medical Centre is a consultant and teaching hospital for the Lake and Western zones of the United Republic of Tanzania. It is situated along the shores of Lake Victoria in Mwanza City. It has 900 beds and over 1200 employees. It is a referral centre for tertiary specialist care for eight regions, namely: – […]

The post CCTV-Operator (2- Posts) at Bugando Medical Centre appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Radiographer (5-Posts) at Bugando Medical Centre

Bugando Medical Centre is a consultant and teaching hospital for the Lake and Western zones of the United Republic of Tanzania. It is situated along the shores of Lake Victoria in Mwanza City. It has 900 beds and over 1200 employees. It is a referral centre for tertiary specialist care for eight regions, namely: – […]

The post Radiographer (5-Posts) at Bugando Medical Centre appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Assistant Nursing Officer (20-Posts) at Bugando Medical Centre

Bugando Medical Centre is a consultant and teaching hospital for the Lake and Western zones of the United Republic of Tanzania. It is situated along the shores of Lake Victoria in Mwanza City. It has 900 beds and over 1200 employees. It is a referral centre for tertiary specialist care for eight regions, namely: – […]

The post Assistant Nursing Officer (20-Posts) at Bugando Medical Centre appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Laboratory Technologist II (4- Posts) at Bugando Medical Centre

Bugando Medical Centre is a consultant and teaching hospital for the Lake and Western zones of the United Republic of Tanzania. It is situated along the shores of Lake Victoria in Mwanza City. It has 900 beds and over 1200 employees. It is a referral centre for tertiary specialist care for eight regions, namely: – […]

The post Laboratory Technologist II (4- Posts) at Bugando Medical Centre appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Nursing Officer (5-Posts) at Bugando Medical Centre

Bugando Medical Centre is a consultant and teaching hospital for the Lake and Western zones of the United Republic of Tanzania. It is situated along the shores of Lake Victoria in Mwanza City. It has 900 beds and over 1200 employees. It is a referral centre for tertiary specialist care for eight regions, namely: – […]

The post Nursing Officer (5-Posts) at Bugando Medical Centre appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne Disemba 29



Share:

Monday 28 December 2020

WAZIRI UMMY: TRA MSICHOKE KUTOA ELIMU YA MLIPA KODI


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu katikati akizungumza leo wakati wa kikao cha Jukwaa la Wadau wa TRA mkoa wa Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ni Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa kikao hicho
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari akizungumza wakati wa kikao hicho
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza wakati wa kikao hicho
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga  Abdurhamani Shiloo
KATIBU wa JWT Mkoa wa Tanga Ismail Masoud akizungumza jambo kwenye kikao hicho
AFISA Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho akieleza jambo kwenye kikao hicho
Meneja wa Benki ya NMB  Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga akieleza jambo kwenye kikao hicho
Wadau wa kikao hicho wakifuatlia matukio mbalimbali
Wadau wa kikao hicho wakifuatlia matukio mbalimbali
Wadau wa kikao hicho wakifuatlia matukio mbalimbali

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu ameitaka mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga wasichoke kutoa elimu ya mlipa kodi kutokana na kwamba kodi ndio msingi na uhai wa maendeleo ya Taifa.

 

Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga(CCM) aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha Jukwaa la Wadau wa TRA Mkoa wa Tanga kilichofunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella ambapo alisema suala la elimu kwa walipa kodi ni muhimu ili waweze kutambua umuhimu wake.

 

Alisema  suala la utoaji wa elimu ni muhimu sana na iendelee kutolewa kwa kila mtu yupo tayari kulipa kodi na tupo kutokana na maendeleo lakini kikubwa waendeele kutoa elimu ambayo itakuwa ni chachu kubwa ya kuweza kufikia malengo yao waliojiwekea ya ukusanyaji wa kodi.

 

“Ndugu zangu TRA mnafanya kazi kubwa na nzuri lakini msichoke endelee kutoa elimu na wanatambue umuhimu wa kulipa kodi kwa sababu msipotoa elimu kuna watu wanaingia kwenye gharama kubwa zaidi kutokana na ujanja ujanga na kwa sababu hawana elimu ndio wanakwepa kulipa kodi”Alisema

 

“Lakini pia kuna baadhi ya watumishi sio waaminifu kesho anakwenda anachukua elfu ishirini na siku inayofuatia elfu 50 jamani tubadilike tuachane na masuala hayo lazima tusisitze umuhimu wa kulipa kodi kwa wafanyabiashara “Alisema

 

Akizungumzia masuala ya makadirio, Waziri Ummy aliitaka mamlaka hiyo kuhakikisha wanatenda haki kwa kuangalia uhalisia wa biashara au huduma inayotolewa kwa sababu unaweza kumpa mtu makadirio ya bei ya juu badala ya kumsaidia ukidhani kwamba ndio utapata kodi kumbe hupati.

 

“Mkiwapa kodi ambayo ni halali watajua ni wajibu wao na wataweza lakini niwaambie kwamba Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli inawapenda walipa kodi na wafanyabiashara na nihimize kuhakikisha mnalipa kodi”Alisema

 

Awali akizungumza wakati akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alisema ulipaji wa kodi ndio ute wa mgongo wa Taifa lolote hivyo hawana budi kujipanga vizuri kuhakikisha watumishi wa TRA na wafanyabiashara hawajengeani mazingira ya chuki

 

Alisema mazingira hayo yanatokana na wao kudhani watu wa TRA wanakuja na makadirio yasikuwa na utaratibu hivyo aliwataka kuhakikisha wanafanya biashara kwa uwazi na watoe ushirikianokwa  TRA na TRA wahakikishe wanaendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria na maadili ya utumishi wa umma.

 

Awali akizungumza katika kikao hicho Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga, Specioza Owure alisema kwamba hivi sasa watawakamata watu wasiodai risiti huku akieleza kwamba kampeni hiyo wanataka kuanzisha wakati wowote ule.

 

Akizungumzia lengo lao la ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2020/2021ambapo alisema kwa upande wa Idara za kodi za ndani inalengo la kukusanya Bilioni 66 na mpaka sasa wana asilimia 120 ya hilo lengo huku kodi za Forodha ikiwa ni bilioni 66 na asilimia 83 lakini kimkoa lengo kuu kukusanya Bilioni 138.9 hivyo wan kazi kubwa ya kufanya

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger