Saturday 28 November 2020

MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AFANYA ZIARA TARURA-CHALINZE, AAHIDI KUPIGANIA KUONGEZA BAJETI ZAIDI


Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Meneja wa TARURA- Chalinze, Mhandisi Enrico Shauri (kulia).
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameendelea na ziara maalum ambapo leo ametembelea ofisi za Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini-Tanzania (TARURA)- Chalinze ili kuona namna wanavyofanya kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara korofi za Halmashauri hiyo.

Awali akifanya mazungumzo na Meneja wa TARURA- Chalinze, Mhandisi Enrico Shauri leo, Mbunge Ridhiwani alitaka kufahamu mpango mkakati wa namna ya kuboresha baadhi ya barabara zilizo katika Kata hiyo ambazo zimekuwa kero kwa kipindi kirefu.

"Chalinze tuna barabara nyingi lakini baadhi ya barabara hizo zina usumbufu mkubwa hasa baada ya wakati wa mvua hazipitiki kirahisi; je Tarura tumejipangaje na ni kwa namna zitakavyokuwa zinapitika muda wote.?"

Pamoja na hoja hiyo Mheshimiwa Mbunge alitamani kujua wamejipangaje kufungua baadhi ya barabara ambazo zikifunguliwa zitakuwa msaada mkubwa kwa Wananchi wa Chalinze kufikia malengo.

Kwa upande wake Meneja wa TARURA- Chalinze, Mhandisi Enrico Shauri alianza kwa kupongeza ziara hiyo ya Mbunge ambapo pia aliahidi kuyafanyia kazi maagizo na ushauri wote  uliotolewa kayoka mazungumzo yao.

Mhandisi Shauri alieleza changamoto kubwa wanayokabili ni ufinyu wa Bajeti ambao unasababisha ufanisi wa kazi zao kusuasua" akifafamua Muhandisi Shauri alisema kuwa TARURA- Chalinze ina kilometa (KM) 679 ambazo ni nyingi sana kwa bejeti inayotengwa ya mfuko wa barabara ni  Milioni 700.44. 

Kwa mwaka huu 2020-2021 tumeshapewa milioni 200 na zingine zitaendelea kutolewa kwa awamu.utolewaji wa haraka wa mafungu ndiyo utawezesha kukamilika kwa kazi mapema.

Mh. Mbunge alimuahidi Meneja wa Tarura kwenda kushauriana na madiwani wenzake kwa kujenga hoja ili aongezewe mafungu ili kuwezesha ujenzi wa Miundo mbinu ya Halmashauri ufanyike haraka kwa faida ya Maendeleo ya Chalinze na Tanzania kwa jumla.

Kwa upande wa Mh. Mbunge alimshukuru Mkandarasi na Tarura kwa jinsi walivyojitahidi kujenga miundombinu pamoja na changamoto hiyo ya kibajeti.

Pamoja na kusikia toka Tarura, Mh.Mbunge alitumia nafasi hiyo kuhimiza maandalizi ya marekebisho na ujenzi wa barabara korofi zote za halmashauri zikiwemo zile za kata ya Kimange, Miono, Mkange, Vigwaza, Ubena, Talawanda, Mandela, Mji wa Chalinze na maeneo mengine kama sehemu za kutolewa macho sana kutokana na shughuli za kimaendeleo na kuchangia uchumi katika Halmashauri hiyo.

Mheshimiwa Mbunge alimaliza kwa kuwaahidi Ushirikiano mkubwa ili kufikia malengo makubwa waliyopanga kuyasimamia kwa pamoja wakishirikiana na Wananchi.

Ziara ya Kata kwa kata inaanza Jumatatu tarehe 30 ambapo Mbunge anatarajia kwenda kata Kata kukagua miradi ya Maendeleo na kuzungumza na Wananchi kusikia kero na matarajio waliyonayo kwa Serikali yao inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Share:

Picha: MAONYESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA YAZINDULIWA

 



Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, (watatu kutoka kulia) akizindua maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga, wa pili kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wakwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Zainab Telack, akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi.



Na Marco Maduhu -Shinyanga.

MKUU wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, amezindua rasmi maonyesho ya biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga, na kuwataka wawekezaji wa madini kwenda kuwekeza mkoani humo, ili kuunyanyua mkoa huo kichumi na kukua kimaendeleo.


Uzinduzi wa maonyesho hayo umefanyika leo katika eneo la Butulwa Kata ya Old Shinyanga manispaa ya Shinyanga, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa madini, akiwemo na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi na Elias Kwandikwa wa Ushetu, ambayo yatakoma Desemba Mosi mwaka huu.

Akizungumza kwenye maonyesho hayo, mkuu wa mkoa wa Geita, aliupongeza mkoa wa Shinyanga kwa kuanzisha maonyesho hayo, ambayo yatakuwa ni chachu kubwa ya kukuza uchumi wa mkoa huo.

“Naupongeza sana mkoa wa Shinyanga kwa kuanzisha maonyesho haya ya Biashara na Teknolojia ya madini, ambayo ni muhimu sana katika kutangaza fursa za uwekezaji, pamoja na wawekezaji wadogo wa madini kujifunza namna ya kutumia Teknolojia za kisasa za kuchimba madini na kupata mali nyingi,” amesema Gabriel.

“Pia nawaomba wawekezaji wakubwa wa migodi mkoani Shinyanga, mtoe kipaumbele kwa wazawa katika ajira za migodini, ikiwamo na kusambaza bidhaa mbalimbali ndani ya migodi hiyo ili wapate kunufaika na rasilimali za nyumbani na siyo kutoa ajira kwa watu wanje,”ameongeza.

Katika hatua nyingine ameitaka migodi hiyo mikubwa kuwekeza miradi mikubwa ya kiuchumi mkoani Shinyanga, ambayo itaacha alama na kuleta maendeleo ili kuubadilisha mkoa huo kimaendeleo na kuendana na hadhi ya rasirimali ilizonazo, na siyo kuwaachia mashimo na umaskini mkubwa.

Naye mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amesema wameanzisha maonyesho hayo ya biashara na Teknolojia ya madini, ili kutoa fursa kwa wawekezaji na wafanyabiashara kuwekeza mkoani humo kwa sababu ni mkoa ambao una madini mengi.

Amesema katika mauzo ya Almasi kuanzia Julai 2020 hadi Novemba, wameuza Almasi zaidi ya Shilingi Bilioni 42.5, hivyo haoni sababu ya mkoa huo kuendelea kuwa maskini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geoffrey Mwangulumbi, amesema wazo hilo la kuanzisha maonyesho hayo lilianza mwaka 2017 hadi 2019, mara baada ya kufanya utafiti, na kuona Shinyanga imedumaa kimaendeleo kwa sababu ya kukosekana kwa mzunguko wa kifedha

Aidha amesema maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya madini yatakuwa yakifanyika kila mwaka mwezi Julai, ili kuongeza thamani ya mnyororo katika Sekta ya madini na kuuinua kiuchumi mkoa wa Shinyanga.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI.


Mgeni Rasmi mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, akizungumza kwenye maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akisoma taarifa kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.

Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akisoma taarifa ya maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi, akizungumza kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Mkadam, akizungumza kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.
Mwenyekiti wa Chemba ya wafanyabiashara na viwanda mkoani Shinyanga Meshack Kulwa, akitoa shukrani kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.
Wananchi wakiwa kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.

Wananchi wakiwa kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.
Wananchi wakiwa kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.

Wananchi wakiwa kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini, mwenye kofia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga Hoja Mahiba.

Wananchi wakiwa kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.

Wananchi wakiwa kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, (watatu kutoka kulia) akizindua maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga, wapili kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Zainab Telack, akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi.

Zaoezi la ukaguzi wa mabanda kwenye maonyesho hayo likiendelea.
Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel, kulia, akiwa kwenye Banda la Tume ya Madini, akiwa ameshika madini ya Almasi.

Zoezi la ukaguzi wa mabanda likiendelea kwenye maonyesho hayo ya Biashara ya Teknolojia ya Madini.

Zoezi la ukaguzi wa mabanda likiendelea kwenye maonyesho hayo ya Biashara ya Teknolojia ya Madini.

Zoezi la ukaguzi wa mabanda likiendelea kwenye maonyesho hayo ya Biashara ya Teknolojia ya Madini.

Zoezi la ukaguzi wa mabanda likiendelea kwenye maonyesho hayo ya Biashara ya Teknolojia ya Madini.

Zoezi la ukaguzi wa mabanda likiendelea kwenye maonyesho hayo ya Biashara ya Teknolojia ya Madini.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi, akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa, kwenye Banda la chama cha wachimbaji wadogo mkoani Shinyanya (SHIREMA).

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa, wakiwa kwenye Banda la Shirika la umeme Tanesco mkoani Shinyanga.

Awali mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wapili kutoka kulia, akimpokea Mgeni Rasmi mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel, kuja kuzindua maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga, wakwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel kushoto akisalimia na Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Partobas Katambi.

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandis Robert Gabriel, akisalimiana na Mstahiki Meya mteule wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila.

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandis Robert Gabriel, akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Debora Magilingimba.

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandis Robert Gabriel, akisalimiana na Miss utalii Tanzania 2020.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, kushoto akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kushoto, akiwa na mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi, katikati, wakiwa na Miss Utalii Tanzania 2020, wakiteta jambo.

Burudani zikitolewa kwenye maonyesho hayo, ambapo kwaya AICT Shinyanga ikitoa burudani na kusindikizwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Kwaya ya AICT Shinyanga ikitoa burudani, na kusindikizwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi, Mbunge wa Ushetu Elias Kwandikwa, akifuatia katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela.

Awali mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wapili kutoka kushoto, akikagua mazingira ya eneo hilo kabla ya mgeni Rasmi kufika na kukagua mabanda kwenye maonyesho hayo.

Eneo la maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga, lililopo eneo la Butulwa Kata ya Oldshinyanga.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.














Share:

Madini kuchangia 10% ya pato la Taifa hadi 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewataka wataalamu wa jiolojia nchini kutekeleza wajibu wao kwa weledi ili kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa kutoka 5.2% mwaka 2019 hadi kufikia 10% mwaka 2025.

Mongella ametoa wito huo katika mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha wanajiolojia nchini, unaofanyika jijini Mwanza na kushirikisha wataalamu pamoja na wadau wa jiolojia kutoka sekta mbalimbali zikiwemo za madini na nishati.

Rais wa Chama cha Wanajiolojia Tanzania, Prof. Abdulkarim Mruma, amesema ongezeko la mchango wa sekta ya madini katika pato la Taifa kutoka 3.2% mwaka 2012 hadi 5.2% mwaka jana, limetokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo mabadiliko ya sheria zinazosimamia maliasili na rasilimali za Taifa ya mwaka 2017.

Prof. Mruma amesema usimamizi makini utawezesha sekta ya madini kuchangia 10% ya pato la Taifa ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini, James Mataragio, amesema Serikali imejipanga kusambaza nishati ya gesi asilia ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya nishati hiyo ndani na nje ya nchi.

Kupitia mkutano huo utakaofikia tamati Novemba 29, baadhi ya wachimbaji wadogo watapata mafunzo kuhusu namna ya kuendesha uchimbaji wenye tija
.

Share:

WANANCHI WILAYANI SHINYANGA WAPEWA HATIMILIKI YA ARDHI

 



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akimpatia hatimiliki mwananchi wa kijiji cha Jomu Leticia Mhoja.

Na Marco Maduhu -Shinyanga.

Wananchi wa kijiji cha Jomu na Kasingili halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wamepewa hatimiliki ya ardhi.

Zoezi la kugawa hati hizo limefanyika jana, likiongozwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hati miliki za ardhi, Mboneko amesema zitasaidia wananchi kuondoa migogoro ya ardhi, pamoja na kuongeza thamani ya ardhi yao.

"Natoa wito kwa wananchi wa Shinyanga mmpime viwanja vyenu, pamoja na kupata hatimiliki, ambayo itawasaidia kuondoa migogoro, kuongeza thamani ya ardhi, ikiwamo na kukopa fedha na kuendesha maisha yenu," amesema Mboneko.

"Pia kwenye ardhi zenu hizo katika kipindi hiki cha mvua, naomba mpande miti kwa wingi ili mvua za upepo zitakaponyesha, zisiweze kuezua mapaa ya nyumba zenu," ameongeza.

Naye Kamishina wa ardhi msaidizi mkoa wa Shinyanga Ezekiel Kitilya, amesema katika kijiji cha Jomu wametoa hatimiliki 20 na Kijiji cha Kasingili hatimiliki 172 za kimila.

Kwa upande wake mkuu wa idara ya ardhi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Julius Maira, amesema zoezi hilo la upimaji ardhi na kugawa hatimiliki ni endelevu, na kubainisha kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha hadi ifikapo 2025 ardhi yote ya Tanzania iwe imeshapimwa.

Nao baadhi ya wananchi ambao wamepata hatimiliki akiwemo Nassoro Seif, wameipongeza Serikali kwa kuwapatia hati hizo pamoja na kusogeza huduma kuwa karibu, tofauti na zamani ambapo walilazimika kwenda mkoani Simiyu kufuata huduma.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wananchi kwenye zoezi la ugawaji wa hatimiliki.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wananchi kwenye zoezi la ugawaji wa hatimiliki.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, akizungumza kwenye zoezi la ugwaji wa hatimiliki kwa wananchi wilayani humo.

Kamishina wa ardhi msaidizi mkoani Shinyanga Ezekiel Kitilya, akizungumza kwenye zoezi la ugwaji wa hatimiliki.

Mkuu wa idara ya ardhi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Julius Maira, akitoa taarifa namna wanavyofanya kazi ya kupima ardhi pamoja na kutoa hatimiliki.

Leticia Mhoja akiishukuru Serikali kwa kumpatia hatimiliki.

Wananchi wakiwa kwenye zoezi la ugawaji wa hatimiliki.

Wananchi wakiwa kwenye zoezi la ugawaji wa hatimiliki.

Wananchi wakiwa kwenye zoezi la ugawaji wa hatimiliki.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akimkabidhi hatimiliki mzee Nassoro Seif .

Zoezi la ugawaji hatimiliki likiendelea.

Zoezi la ugawaji hatimiliki likiendelea.

Zoezi la ugawaji hatimiliki likiendelea.

Zoezi la ugawaji hatimiliki likiendelea.

Zoezi la ugawaji hatimiliki likiendelea.

Zoezi la ugawaji hatimiliki likiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akipanga mti.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba akipanda mti.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipiga picha ya pamoja na wananchi mara baada ya kumaliza kugawa hatimiliki.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipiga picha ya pamoja na wananchi mara baada ya kumaliza kugawa hatimiliki.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger