Thursday 30 July 2020

Jeshi la Polisi latoa taarifa kwa vyombo vya habari




Share:

Picha: Rais Magufuli Akipita Kwenye Daraja La Mkapa Rufiji Mkoani Pwani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipita na kukagua Daraja la Mkapa linalopita katika Mto Rufiji mkoani Pwani wakati akitokea Masasi Mtwara kwenye msiba wa Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa leo tarehe 30 Julai 2020.

Daraja hilo linalounganisha Pwani na Mikoa ya Lindi na Mtwara lilijengwa na Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William  Mkapa


Share:

Halima Bulembo Aongoza Kura Za Maoni Ubunge UVCCM Kagera.

Na Allawi Kaboyo Bukoba.
Mchakato wa uchaguzi wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi umeendelea leo julai 30 mwaka huu ili kuwapata wagombea watakao peperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 28 mwaka huu.

Jumuiya ya umoja wa vijana CCM nchini wamefanya uchaguzi wa kuwapata wagombea wa uwakilishi wa ubunge viti maalumu vijana ambapo kwa mkoa wa Kagera uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Bukoba ukiwajumuisha watia nia 19 huku wajumbe halali wa mkutano huo wakiwa 48.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi mkuu wa uchaguzi ambaye amekuja kwa niaba ya mkuu wa mkoa Geita Said Nkumba mkuu wa wilaya ya Bukombe amemtangaza Mhe. Halima Abdallah Bulembo mbunge aliyemaliza muda wake kuwa ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 35 akifatiwa na Bi. Joanfaith Kataraia ambaye amepaata kura 9 na Bi.Koku Fatuma Ruta ambaye amepata kura 2, Doris Robert kura 1 na Jacrine Elias kura 1 huku wengine waliobaki wakiambulia kura 0.

Nkumba ameongeza kuwa uchaguzi huu ni mchakato wa kura za maoni hivyo mchakato mwingine unaendelea vikiwemo vikao na kuwaasa wagombea wote kushikamana na kutokata tamaa kwa matokeo huku walioongoza wasishangilie maana mchakato bado unaendelea.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo wagombea wote wamepewa nafasi ya kushukuru ambapo wote wameahidi kutoa ushirikiano kwenye uchaguzi mkuu ambao upo mbele yao ambapo Halima Bulembo amesema kuwa yeye kama mbunge aliyemaliza muda wake na kuendelea kutetea nafasi yake kuwa ataendelea kuwatetea vijana kwenye bunge na kuhakikisha haki za vijana zinapatikana.

Awali akiongea kwenye mkutano huo mkuu wa wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro amewasihi vijana kutunza nidhamu ya chama na kulinda misingi ya chama chao na kuhakikisha wanashinda katika uchaguzi ujao.

Kinawiro amewataka vijana hao kutotumika vibaya katika uchaguzi huu na kupelekea kujenga picha mbaya ya chama na kuwakemea kutojihusisha na vitendo vya Rushwa na kusimamia haki huku wakiwaunga mkono wagombea wote watakao letwa na chama chau kwenye uchaguzi mkuu.

“Vijana ni jeshi kubwa kwenye chama chetu na ni viongozi wa sasa na viongozi wajao, viongozi wengi mnaotuona tumepikwa kwa kupitia umoja wa vijana sasa itakuwa ni aibu kubwa kumuona kijana wa CCM akijihusisha na vitendo vya Rushwa, uvunjifu wa Amani na matukio ya hovyo.” Amesisitiza Kinawiro

Aidha Kinawiro amewataka vijana waliowawakilisha vijana wenzao kwenye uchaguzi huu kuwa wawakilishe wazuri na kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wa vyama vingine vya siasa.


Share:

Wananchi wa Somanga Mkoani Lindi Wamshukuru Rais Magufuli, Mzee Amkabidhi Zawadi ya Jogoo

Wananchi wa Somanga Mkoani Lindi wamemshukuru Rais Magufuli kwa kuwapa fedha na kujengwa Kituo cha Afya. Mzee Kimbwembwe amempa zawadi ya jogoo.


Share:

Tazama Picha : AZIMANA ARIF AMIR ASHINDA UCHAGUZI KURA ZA MAONI UBUNGE VITI MAALUM KUNDI LA VIJANA CCM SHINYANGA

Azimina Arif Amir 

Azimina Arif Amir ameibuka mshindi katika uchaguzi wa kura za maoni Ubunge Viti Maalum Kupitia Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga kwa kupata kura 13 kati ya kura 28 zilizopigwa huku Janeth Dutu akipata kura 6 na Leah Mbeke akipata kura 5.

Akitangaza Matokeo ya uchaguzi wa Mkutano wa Baraza la Vijana UVCCM mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Julai 30,2020 Msimamizi wa uchaguzi huo, Dkt. Philemon Sengati ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Tabora amesema uchaguzi huo umekuwa wa huru na haki ambapo maamuzi zaidi yatatolewa katika Mkutano wa Baraza la Vijana UVCCM taifa.

Aliwataja vijana 14 wa CCM waliojitokeza katika kinyang’anyiro cha nafasi ya ubunge viti maalum kupitia kundi la Vijana CCM kuwa ni Azimina Arif Amir ambaye amepata kura 13, akifuatiwa na Janeth Dutu aliyepata kura 6 na Leah Donald Mbeke aliyepata kura 5 akifuatiwa na Sikitu Elson Samwel kura 2,Suzana Reuben Jilili kura 1 na Jackline Emanuel Ndombile kura 1.

Wengine ni Cecilia Peter Mhande,Husna Salam Zahrani, Jesca Jumanne Masehese,Mercy Athanas Lukuba,Mercy Gasper Kyando,Prisca Lazaro Mawoo, Rebeca Boniphace Giti na Theresia Masanja ambao hawakupata kura.

“Mara baada ya kuchaguzi huu kama hapatakuwa na mapingamizi huyu mshindi tutampeleka katika hatua nyingine. Hapa tunahitaji mshindi mmoja tu atayewakilisha mkoa wa Shinyanga atayeingia kwenye kinyanganyiro kitaifa ili kupata wabunge sita Tanzania Bara.
Mkuu wa mkoa wa Tabora  Dkt. Philemon Sengati  akizungumza katika uchaguzi wa kura za maoni kuchagua mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana UVCCM mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Julai 30,2020. Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu,kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge akizungumza katika uchaguzi wa kura za maoni kuchagua mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Kundi la Vijana CCM.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge akizungumza katika uchaguzi wa kura za maoni kuchagua mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Kundi la Vijana CCM.
Wagombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM wakiwa ukumbini.
Wagombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM wakiwa ukumbini.
Wagombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM wakiwa ukumbini.
Wagombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM wakiwa ukumbini.
Wagombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM wakiwa ukumbini.
Wagombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM wakionesha namba zao wakati za zoezi la kupiga kura
Azimina Arif Amir akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM 
Janeth Dutu akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM.
Leah Mbeke akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM 
Wajumbe wakiwa ukumbini.
Wajumbe wakiwa ukumbini.
Wajumbe wakipiga kura
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea
Mkuu wa mkoa wa Tabora  Dkt. Philemon Sengati  akitangaza matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni kuchagua mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana UVCCM mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Julai 30,2020.
Leah Mbeke akitoa neno la shukrani baada ya kuibuka  mshindi wa tatu kwa kupata kura 5 
Janeth Dutu akitoa neno la shukrani baada ya kuibuka  mshindi wa pili kwa kupata kura 6 
Azimina Arif Amir  akitoa neno la shukrani baada ya kuibuka  mshindi wa kwanza  kwa kupata kura 13
Azimina Arif Amir  akitoa neno la shukrani baada ya kuibuka  mshindi wa kwanza  kwa kupata kura 13.
Cecilia Peter Mhande akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM 
Husna Salam Zahrani akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM 
Jackline Emanuel Ndombile akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM 
Jesca Jumanne  Masehese akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM 
Mercy Athanas Lukuba akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM 
Mercy Gasper Kyando akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM 
Prisca Lazaro Mawoo akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM 
Rebeca Boniphace Giti akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM 
Sikitu Elson Samwel akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM 
Susani Reuben Jilili akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM 
Theresia Masanja akiomba kura kwa wajumbe ili achaguliwe kuwa Mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia kundi la Vijana CCM.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Live : RAIS MAGUFULI ANAZUNGUMZA NA WANANCHI

LIVE:  Rais Magufuli Anazungumza na Wananchi


Share:

Tundu Lissu Akwama Kuhudhuria Kesi Yake Mahakamani

Kesi ya uchochezi inayomkabili Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu leo Julai 30, 2020, imeahirishwa hadi Agosti 26, baada ya mtuhumiwa kushindwa kufika mahakamani.

Kesi hiyo namba 236 ya mwaka 2017, ilifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam hii leo Julai 30, 2020, kwa ajili ya kutajwa, mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Cassian Matembele.

Akizungumza Mahakamani hapo Wakili wa Upande wa Utetezi Peter Kibatala amesema kuwa, Lissu hakuweza kufika mahakamani hapo kwa kuwa amejiweka karantini kwa lengo la kujiangalia hali yake ya kiafya, kutokana na yeye kuugua kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Wakili wa Serikali Wankyo Simon, hakuwa na pingamizi katika hilo na kuruhusu ipangwe tarehe nyingine


Share:

PICHA: Rais Magufuli, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Jakaya Mrisho Kikwete Walivyoweka Shada La Maua Kwenye Kaburi La Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuliakiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakijiandaa kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais Mstaafu wa Awamu ya Hayati Tatu Mzee Benjamin William Mkapa wakati wa mazishi kijijini Lupaso, Masasi, Mtwara Jumatano Julai 29, 2020



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger