Thursday 30 July 2020

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi July 30






















Share:

Wednesday 29 July 2020

Picha 13: Rais John Pombe Magufuli Aongoza Watanzania Katika Mazishi Ya Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Tatu Benjamin William Mkapa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka udongo kwenye kaburi la Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Lupaso Masasi Mkoani Mtwara.



Share:

PICHA: Jeneza ambalo lina mwili wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa likiingizwa kaburini kijijini kwao Lupaso.

PICHA: Jeneza ambalo lina mwili wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa likiingizwa kaburini kijijini kwao Lupaso.


Share:

PICHA: Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo akiweka udongo katika kaburi la Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo akiweka udongo katika kaburi la Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, na kisha akapiga saluti kama ishara ya heshima.




Share:

PICHA: Mama Anna Mkapa akielekea kaburini kuweka udongo katika kaburi la Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.

Mama Anna Mkapa akielekea kaburini kuweka udongo katika kaburi la mume wake, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.


Share:

PICHA: Wanajeshi wakitoa heshima zao za mwisho kwa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa

Wanajeshi wakitoa heshima zao za mwisho kwa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa katika mazishi yako Lupaso, Masasi mkoani Mtwara. 


Share:

Rais Magufuli: Mkapa Alikataa Kuzikwa Dodoma

Rais John Magufuli amesema rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin  Mkapa alipenda nyumbani kwao Masasi ndiyo maana alikataa kuzikwa katika eneo lililotengwa jijini Dodoma kwa ajili ya viongozi wa ngazi za juu za serikali.

Magufuli amesema hayo leo Jumatano, Julai 29, 2020, katika Kijiji cha Lupaso, Masasi mkoani Mwtara wakati wa maziko ya  Mkapa.

“Tulipangiwa kuzikiwa Dodoma.   Mzee Mkapa akaniuliza, ‘Mlipanga maziko yawe Dodoma?  Mimi msinizike Dodoma.’  Nikasema, ‘wewe unataka wakuzike wapi?’  Akasema Lupaso.  Nikamuuliza Mzee Kikwete akasema ‘mimi mnizike Msoga’.  Mimi nilisema nitazikwa Chato.”

“Niliogopa kumuuliza Mwinyi azikiwe wapi kwa sababu alikuwa na miaka zaidi ya 90, nikaona nikimuuliza halafu likatokea la kutokea nitaonekana mimi nimemletea uchuro, nikaona hilo eneo labda atazikiwa Mzee Malecela kwa sababu ni wa hukohuko Dodoma. Kwa sababu hakuna anayetaka kuzikwa Dodoma lile eneo nikaamua kuwapa wananchi na tayari walishaanza kujenga."-JPM

Akizungumzia mazishi ya Mzee Mkapa, Rais Magufuli amewashukuru viongozi wa dini, Serikali na Watanzania kwa kushiriki kikamilifu kuupumzisha mwili wa kiongozi huyo mstaafu katika makazi yake ya milele.

“Tumekuja hapa kwa kazi moja ya kumuaga Mzee wetu Benjamin Mkapa ambaye ametimiza kazi yake kwa miaka 82, nipende kwa mara nyingine kuwashukuru Watanzania wote mahali pote walipo, lakini kuwashukuru sana viongozi wetu wa dini zote,” amesema Rais Magufuli


Share:

Mwijaku afikishwa mahakamani akituhumiwa kusambaza picha za ngono

Msanii wa uigizaji nchini Tanzania, Mwemba Burton (35) maarufu Mwijaku amepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akituhumiwa kusambaza picha za ngon kinyume cha sheria
 
Mwinjaku ambaye alikuwa mmoja wa watia nia jimbo la Kawe, amefikishwa mahakamani hapo leo, Julai 29, 2020 na kusomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate.
 
Akisomewa shtaka lake, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon akisaidiana na Mwanaamina Kombakono, alidai kuwa mshtakiwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 110.
 
Wakili Kombakono alidai mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Septemba 17, 2019 na Oktoba 2019 katika jiji la Dar Es salaam.
 
Alidia katika kipindi hicho, Mwijaku anadaiwa kuchapishwa picha za ngono kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp uliuounganishwa katika Kompyuta.
 
Mshtakiwa amekana shtaka na amekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ambayo ni kuwa na wadhamini wawili kutoka ama Bongo Movie au tasnia ya muziki wenye barua zilizothibitishwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), ambao watasiani bondi ya Sh  500,000 kila mmoja.
 
Hakimu Kabate ameahirisha Kesi hiyo hadi Agosti 12, 2020 itakapotajwa.


Share:

KATIBU MKUU KILIMO KUSAYA AIPONGEZA TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya,akizungumza wakati wa kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya,akisisitiza jambo kwenye kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Titus Kamani,akitoa neno kwenye kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya.

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt.Benson Ndiege,akitoa taarifa wakati wa kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya.
Afisa Ushirika Mkuu Bi.Veneranda Mugoba,akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya mara baada ya kumaliza kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma
Sehemu ya Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakifatiliwa Hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakati wa kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma
.............................................................................................
Na.Alex Sonna,Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya ameipongeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kuendelea kuimarisha na kuendeleza Sekta ya Ushirika nchini katika Nyanja za Kilimo, ufugaji, uvuvi, madini kwani sekta hizo zimeendelea kuchangia uchumi wa Taifa. 

Umuhimu wa Sekta hizo umetokana na kuwaunganisha wanachama katika uzalishaji, ukusanyaji mazao na upatikanaji wa masoko.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma.

Kusaya amesema kuwa Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika imefanya na inaendelea na jitihada mbalimbali za kuimarisha Ushirika nchini. 

Serikali imejikita katika kuimarisha Usimamizi na Utawala Bora katika Vyama vya Ushirika, kupitia Sheria ya Ushirika Na 6 ya Mwaka 2013 na Kanuni za mwaka 2015. 

Aidha Kusaya amesema kuwa usimamizi wa vyama unaanzia kwa mwanachama mwenyewe, juhudi zimeelekewa kwenye Mafunzo kwa viongozi wa vyama vya ushirika na wanachama wao kupitia mpango kazi uliotolewa naTume ya Maendeleo ya Ushirika.

 Pia serikali imeendelea kuchukua hatua kupitia vyombo vya usalama pale ambapo kuna wizi na ubadhilifu kwenye vyama. 

Nia ya serikali ni kurudisha Imani ya wananchi juu ya ushirika.

“Kwa hatua hizi kumekuwepo na mabadiliko chanya kwenye ushirika ambapo wananchi wameendelea kuanzisha na kujiunga katika vyama vya Ushirika wa aina mbalimbali ikiwemo vyama vya Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS) hatua ambayo itawezesha kupanua shughuli zao za uzalishaji mali na kuongeza kipato na hatimaye kupunguza umasikini. 

Pia, kwa sasa wakulima wanauza mazao yao kupitia mfumo wa Ushirika. Mfumo ambao umesaidia kuimarisha ubora wa mazao, kupatikana kwa bei za ushindani, uhakika wa vipimo vya mazao,” alisistiza Bw.Kusaya

Mfumo wa Ushirika umesaidia upatikanaji wa takwimu sahihi za uzalishaji na uhakika wa mapato ya Halmashauri za Wilaya husika. 

Kwa kushirikiana na Soko la Bidhaa(TMX) na bodi za mazao, masoko ya mazao ya kimkakati na mazao mchanganyiko yameendelea kuimarika kama vile mazao ya tumbaku, choroko, kahawa, pamba, ufuta, kokoa na mbaazi yaliuzwa kupitia mfumo wa ushirika katika msimu wa 2019/20 kwa thamani ya Shilingi trilioni 2.7.

Awali akiwasilisha Mafanikio na changamoto za Tume, Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, ameeleza kuwa Vyama vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) vimeongeza mikopo kwa wanachama wake kutoka Shillingi Billioni 854 mwaka 2017 hadi kufikia Shillingi Trillioni 1.5 mwaka 2019 sawa na ongezeko la asilimia.

 Ushirika ni Sekta ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika kutoa ajira kwa vijana na wananchi kwakuwa ni sekta ambayo inagusa maisha na uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
 
“Tume imeendelea kusimamia masuala ya ajira na kuwezesha wananchi Zaidi ya 90,090 kupata ajira katika vyama vya Ushirika zikiwemo ajira za kudumu, mkataba na za msimu hadi kufikia Juni 2020 ikilinganishwa na ajira 32,668 mwaka 2018,” alisema Dkt. Ndiege

Kwa upande wake Kamishna Salome Tondi, amesema Sekta ya Ushirika inaweza kuendelea kukua na kuimarika kwa kuhakikisha elimu ya Ushirika inawafikia wengi katika jamii. 

Tondi alifafanua kuwa elimu ni moja ya nyenzo muhimu inayoweza kuwakomboa wanaushirika akitoa mfano wa masuala ya haki na wajibu wa wanaushirika, taratibu za uendeshaji wa Vyama vya Ushirika, taratibu za uchaguzi wa viongozi wa Vyama vya Ushirika na masuala mengine mengi.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilikuwa ni fursa ya Makamishna kukaa kwa pamoja na watumishi wa Tume kufanya tathmini ya masuala mbalimbali ya Ushirika katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 baada ya uteuzi wao kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na.6 ya mwaka 2013.
Share:

Waziri Mkuu wa Burundi Jenerali Alain Guillaume aondoka nchini leo

Waziri Mkuu wa Burundi Jenerali Alain Guillaume ameondoka nchini  leo Julai 29,2020 baada ya kuwasilisha salamu za pole kufuatia kifo cha Mzee Mkapa.

Mwenyeji wake Waziri wa Viwanda Mhe.Innocent Bashungwa ndiye aliyemsindikiza uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam.


Share:

DRIVERS – 252 POSTS  at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO)

DRIVERS – 252 POSTS  at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO)   TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY(TANESCO) Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) is a Parastatal organization  established by Memorandum and Articles of Association incorporated in 26th November 1931 which established Tanzania Electric Supply Company Limited (the then Tanganyika Electric Supply Company Limited -TANESCO). The Company generates purchases, transmits, […]

The post DRIVERS – 252 POSTS  at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

ELECTRICAL TECHNICIAN (GENERATION)- 6 POSTS  at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO)

ELECTRICAL TECHNICIAN (GENERATION)- 6 POSTS  at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO)   TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY(TANESCO) Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) is a Parastatal organization  established by Memorandum and Articles of Association incorporated in 26th November 1931 which established Tanzania Electric Supply Company Limited (the then Tanganyika Electric Supply Company Limited -TANESCO). The Company generates purchases, […]

The post ELECTRICAL TECHNICIAN (GENERATION)- 6 POSTS  at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MECHANICAL TECHNICIAN (GENERATION) – 10 POSTS  at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO)

MECHANICAL TECHNICIAN (GENERATION) – 10 POSTS  at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY(TANESCO) Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) is a Parastatal organization  established by Memorandum and Articles of Association incorporated in 26th November 1931 which established Tanzania Electric Supply Company Limited (the then Tanganyika Electric Supply Company Limited -TANESCO). The Company generates purchases, […]

The post MECHANICAL TECHNICIAN (GENERATION) – 10 POSTS  at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

ARTISAN – 186 POSTS  at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO)

ARTISAN – 186 POSTS  at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO)   TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY(TANESCO) Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) is a Parastatal organization  established by Memorandum and Articles of Association incorporated in 26th November 1931 which established Tanzania Electric Supply Company Limited (the then Tanganyika Electric Supply Company Limited -TANESCO). The Company generates purchases, transmits, […]

The post ARTISAN – 186 POSTS  at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

31 ELECTRICAL TECHNICIANS (DISTRIBUTION) at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO)

1.0 TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY(TANESCO) Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) is a Parastatal organization  established by Memorandum and Articles of Association incorporated in 26th November 1931 which established Tanzania Electric Supply Company Limited (the then Tanganyika Electric Supply Company Limited -TANESCO). The Company generates purchases, transmits, distributes and sells electricity to Tanzania Mainland and sells bulk power to […]

The post 31 ELECTRICAL TECHNICIANS (DISTRIBUTION) at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Ratiba ya Mazishi ya Hayati Benjamin William Mkapa,Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Leo Jumatano Julai 29, 2020




Share:

Je, una bidhaa yako mfano gari, simu unataka Kuiuza......NauzaOnline Wamekurahisishia

Je, una bidhaa yako mfano gari, simu, shamba unauza na hujui ni namna gani utaiuza?

NauzaOnline wamekurahisishia. Ingia kwenye Website yao kwa <<BOFYA HAPA>>, Bonyeza palipoandikwa Register ili ujisajili.

Baada ya kujisajili, basi weka hilo tangazo la bidhaa yako Bure


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger