Tuesday 30 June 2020

Picha : MRADI WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO KATIKA KIPINDI CHA CORONA WAZINDULIWA SHINYANGA


Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba akizungumza wakati akizindua Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba amezindua Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ utakaotekelezwa katika kata 10 za halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT).



Mradi huo utakaotekelezwa na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na Mashirika matatu yasiyo ya kiserikali ambayo ni Investing in Childrean and Societies (ICS Africa), Thubutu Africa Initiatives (TAI) na Rafiki SDO umezinduliwa leo Jumanne Juni 30,2020 katika ukumbi wa Hospitali ya wilaya ya Shinyanga uliopo katika kata ya Iselamagazi.

Akizungumza wakati wa kufungua mradi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba amesema suala la ukatili wa kijinsia ni suala mtambuka hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anapiga vita vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tunaendelea na mapambano dhidi ya Corona,lakini tukiwa katika harakati hizo bado ukatili wa kijinsia unaendelea na inawezekana katika kipindi hiki tukawa na ukatili wa namna tofauti tofauti japokuwa katika mradi huu tutalenga zaidi kundi la wanawake na watoto”,alisema Mahiba.

“Niwashukuru sana Women Fund Tanzania kwa kutuwezesha ruzuku kupambana na ukatili wa kijinsia katika kipindi hiki cha Corona na  tujipongeze wale tuliopata ruzuku, tukaitendee haki fedha tuliyopewa ili kuondokana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Naamini kabisa maeneo yaliyopata ruzuku yatatumika kama kata za mfano”,alisema Mahiba.

Naye Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kutoka Shirika la Women Fund Tanzania (WFT), Glory Mbia alisema shirika hilo linafanya kazi kwa kushirikiana na serikali ndiyo limetoa fedha za ruzuku kwa halmashauri ya Shinyanga katika jitihada za kupambana na athari zilizowakumba wanawake, mabinti  na watoto katika kipindi cha mlipuko wa Corona kilichopelekea wanafunzi kukaa majumbani kwa zaidi ya miezi mitatu  na baadhi ya shughuli za kila siku kubadilika.
“Yapo mengi yaliyojiri wakati wa COVID -19. Sisi tunalenga zaidi katika kipindi cha baada ya Corona,kuna maisha baada ya COVID -19 na tunajaribu kuangalia walengwa wetu ambao ni wanawake na watoto.Kuna changamoto gani walizipitia na hizo changamoto zinaweza kuwaathiri vipi nasi tunasaidiaje haya makundi ili yaweze kurudi katika maisha yao ya kawaida na kuishi katika hali iliyopo kwa mujibu wa miongozo inayotolewa na serikali”,alisema Mbia.

“Mwanzoni mwa Mwezi Aprili tulitoa matangazo watu waombe ruzuku,waliomba watu wengi nchi nzima. Mchakato ulifanyika kwa uhuru na uwazi kwa mujibu wa vigezo vilivyoainishwa wakati wa tangazo na kwa eneo letu hili la mradi tukafanikiwa kupata shirika la Rafiki SDO, Thubutu Africa Initiatives, ICS na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga”,alisema Mbia.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Edmund Ardon alisema lengo la Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ utakaotekelezwa kuanzia Julai 1,2020 hadi Septemba 2020 ukigharimu takribani shilingi milioni 60 ni kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Alizitaja kata zitakazonufaika na mradi huo kuwa ni Bukene, Didia, Mwantini, Iselamagazi, Pangagichiza, Mwakitolyo, Salawe, Lyabukande, Lyabusalu na Solwa.

 Nao Mameneja Miradi kutoka Mashirika yaliyopata Ruzuku, Paschalia Mbugani (Thubutu Africa Initiatives), Sabrina Majikata (ICS) na George Nyanda (Rafiki SDO) waliishukuru WFT kwa kuwapatia ruzuku na kueleza kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kikamilifu.

Kikao kazi hicho cha Kutambulisha mradi kimehudhuriwa na wajumbe wa kamati ya watalaamu wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (CMT),Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka kata 26 za halmashauri hiyo, Wajumbe wa kamati ya usimamizi wa mradi kutoka WFT,mashirika watekelezaji wa mradi na mashirika yanayofanya kazi za utetezi wa haki za wanawake na watoto.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba akizungumza leo Jumanne Juni 30,2020 wakati wa kuzindua Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ utakaotekelezwa na  Shirika la  Investing in Childrean and Societies (ICS Africa), Thubutu Africa Initiatives (TAI) na Rafiki SDO katika kata 10 za halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba akiyahamasisha mashirika ya  Investing in Childrean and Societies (ICS Africa), Thubutu Africa Initiatives (TAI) na Rafiki SDO  kutumia vizuri fedha zilizotolewa na WFT kwa ajili ya Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.


Wadau wa haki za wanawake na watoto wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba akiwataka wadau mbalimbali kushiriki katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za matukio ya ukatili pamoja na kutoa ushahidi pindi matukio ya ukatili yanapofanyika. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja.
Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kutoka Shirika la Women Fund Tanzania (WFT), Glory Mbia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ utakaotekelezwa na  Shirika la  Investing in Childrean and Societies (ICS Africa), Thubutu Africa Initiatives (TAI) na Rafiki SDO   kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT). 


Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kutoka Shirika la Women Fund Tanzania (WFT), Glory Mbia akielezea namna shirika hilo linavyoshirikiana na serikali katika jitihada za kupambana na Corona kwa kuangalia kundi la wanawake na watoto.


Mjumbe wa kamati ya usimamizi wa mradi kutoka WFT, Irene Laulent kutoka kata ya Usanda katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akiwahamasisha wazazi na walezi kukaa karibu na watoto wao wa kike na kueleza madhara ya kufanya ngono na kusaidia watoto pindi wanapofanyiwa vitendo vya ukatili.
Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja akielezea namna watakavyotekeleza Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ .


Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.

Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Meneja Miradi wa Shirika la ICS ,Sabrina Majikata akielezea namna shirika hilo lilivyojipanga kutekeleza Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Meneja Miradi kutoka Thubutu Africa Initiatives akielezea namna shirika hilo lilivyojipanga kutekeleza Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Edmund Ardon akielezea namna shirika hilo lilivyojipanga kutekeleza Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ kutoka Shirika la Rafiki SDO, George Nyanda akielezea namna watakavyotekeleza mradi huo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Mwalukwa, Elypendo John akielezea umuhimu wa kuwapa elimu ya kutoa ushahidi waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ili vitendo vya ukatili viweze kutokomezwa katika jamii.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Samuye, Magai Deogratius akichangia hoja wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la AGAPE ACP, John Myola akielezea uzoefu kuhusu namna ya kutekeleza miradi mbalimbali inayohusu wanawake na watoto. Alisema katika kipindi cha ugonjwa wa Corona shirika hilo limetoa vifaa vya kujikinga na maambukizi dhidi ya Corona ,elimu kuhusu Corona pamoja na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Wadau wa haki za wanawake na  watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na  watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na  watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na  watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na  watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na  watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na  watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na  watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na  watoto wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Waziri wa Viwanda ,Innocent Bashungwa Amuagiza Mkurugezi Wa TBS Kuwafukuza Kazi Wafanyakazi Wanaokwamisha Zoezi La Utoaji Nembo Za Ubora Kwa Wakati.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwafukuza kazi wafanyakazi wa shirika hilo wanaowatoza fedha na wanaochelewesha zoezi Kutoa nembo ya ubora kwa bidhaa zinazotengenezwa kwenye Viwanda vidogo nchini.

Waziri Bashungwa ametoa maelekezo  hayo leo 30 juni 2020 alipofanya ziara mkoani Simiyu na kutembelea kiwanda cha Usindikani wa Viazi lishe kilichopo wilaya ya Maswa kinachojulikana kwa jina la Ng’hami Industries Company Ltd.

Bashungwa amefikia maamuzi hayo baada ya kufika kiwandani hapo na kukagua bidhaa za kiwanda hicho ambayo ni unga wa viazi lishe na kugundua hazina nembo ya ubora ya TBS, ambayo changamoto hiyo imesababiswa na wafanyakazi wa shirika la TBS kwa kuwaomba fedha kwa ajiri ya kupewa nembo ya ubora pia kuchewesha kwa zaidi ya miezi saba bila kupewa  majibu au nembo ya ubora.

Waziri Bashungwa baada ya kuona changamoto hiyo alimpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa TBS na DKt. Yusuph Ngenya na kumuelekeza kuwafukuza kazi wafanyakazi wake wanaokwenda kinyume na maagizo ambayo amekuwa akiyatoa mara kwa mara ya kutowachelewesha wafanyabiasha kwa sababu ambazo sio za msingi zinazosababisha bidhaa kutopewa nembo za ubora kwa wakati ambazo zinasababisha mazingira ya Rushwa na usumbufu kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw. Ntobi Rufunga ameeleza kuwa barua ya kuomba nembo ya ubora ilipelekwa TBS tangu mwezi 11, 2019 lakini mpaka sasa hajapewa majibu yoyote na baada ya  kuchukuliwa kwa sampuli ya bidhaa hiyo wameombwa kutoa kiasi cha Tsh. 520,000/= ili wapewe nembo ya ubora ambayo ni kinyume na sheria na mashariti ya  shirika hilo.

Aidha Bw. Ntobi  amesema kuwa Kiwanda hicho mpaka sasa kinazalisha unga wa viazi lishe wa aina mbili ambao ni Unga wa kupika uji kwa ajiri ya matumizi ya rika zote pia Unga wa kutengeneza keki, mikate na andazi.


Share:

Msajili: Vyama Vyote Vina Haki Sawa Kushika Dola

Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini imesema ruzuku sio kigezo cha Chama Cha Siasa kuwa na nguvu ya kushika dola na vijenge  hoja na ushawishi  itikadi yake kwa wananchi katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba mwaka huu.

Rai hiyo imetolewa leo (Jumanne Juni 30, 2020) Jijini Dar es Salaam na Naibu Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini, Mohamed Ahmed wakati wa kufunga kikao kazi cha kuwajenga uwezo Viongozi wa Vyama vya Siasa na kusema  vyama vyote vipo sawa kwa mujibu wa sheria.

Ahmed alisema katika kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu, Vyama vya Siasa nchini havina budi kujitazama na kujikosoa kwa hoja zilizo imara zenye uwezo wa kuwashawishi wanachama wake katika msingi wa kushika dola baada ya kutazama ruzuku, kwani wakati wa kuanzisha mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992, vyama hivyo havikuwa na uwezo wa kifedha.

‘Ukitazama Vyama vya siasa vya mwaka 1992 sio vya leo, tulianza tukiwa wachanga kabisa na kushiriki katika chaguzi mbalimbali na leo hii vimeanza kujijenga siku hadi siku, tuvijenge vyama vyetu kwa ajili ya ushindani wa hoja katika uchaguzi na kushika hatamu ya uongozi’’ alisema Ahmed.

Aliongeza vyama voyte vyenye usajili wa kudumu vina haki sawa kwa mujibu wa sheria na kuwa hata vyama vyenye uwezo wa ruzuku vimejikuta vikiingia katika migogoro ya mara kwa mara baina yao na kuathiri dhana ya msingi mkuu wa vyama vya siasa, ambayo ni kushika hatamu ya uongozi na kuongoza dola.

Akifafanua zaidi alisema Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa itaendelea kushikiana na vyama vyote vya siasa katika kuwajengea uwezo katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu kwa kupokea maoni, changamoto na kuendesha mikutano ya mara kwa mara na wadau wa siasa.

Aidha Ahmed alivikumbusha vyama vya siasa kuendeleza dhana ya uvumilivu, mshikamano na ushirikiano baina yao na kushindana kwa hoja na kuepuka tofauti za itikadi za siasa, upinzani, kwa kuwa nchi ndiyo kipaumbele cha kwanza katika jamii yenye amani na utulivu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Anna Abdallah aliipongeza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kuitisha mkutano huo kwa kuwa umetoa fursa kwa vyama hivyo kufahamu wajibu wa msingi wa vyama vya siasa katika kushiriki katika maendeleo ya nchi.

Anna alisema mkutano huo umetoa taswira halisi ya mtazamo wa vyama vya siasa na nafasi ya wananchi katika kufanya uamuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu wajibu na haki yao ushiriki wao katika maendeleo ya nchi na kuvikumbusha vyama hivyo kuwa siasa sio uhasama.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini, John Shibuda alisema suala la amani na utulivu ni jambo muhimu linalopaswa kupewa kipaumbele na mamlaka na taasisi mbalimbali za dola katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

‘Mwezi Julai tunatarajia kuwa na kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa, ambapo tutakutana na mamlaka za dola ikiwemo Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ili kuweza kuwekana sawa na kujitafakari sote kwa pamoja nafasi tuliyonayo kuelekea katika Uchaguzi Mkuu’’ alisema Shibuda.

MWISHO



Share:

TAKUKURU Yakanusha taarifa za kumshikilia na kumhoji aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho gambo




Share:

Serikali Yafanikiwa Kuokoa Shilingi Tirioni 11.4

Na. Dennis Buyekwa- OSG
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi Tirioni 11.4 baada ya kushinda mashauri mbalimbali yaliyoendeshwa katika Mahakama mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Hayo yamezungumzwa mapema leo na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Mhe. Gabriel Malata alipokuwa akipokea msaada wa kompyuta mpakato tano zenye thamani ya shilingi milioni 7.5 zilizotolewa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Mhe. Malata ameeleza kuwa kiasi hicho cha fedha kimeokolewa katika mwaka wa fedha 2019/2020 kufuatia utendaji mzuri wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambao umepelekea kushinda mashauri mengi yaliyofunguliwa dhidi ya Serikali.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa fedha hizo zilizookolewa na Serikali zitasaidia katika kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kama vile ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), ununuzi wa ndege na meli kubwa  za abiria na mizigo katika kuhakikisha tunafikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Amesema kuwa kompyuta hizo zimekuja muda muafaka kwani zitawawezesha watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu Mkuu wa Serikali kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kwa haraka zaidi hatua itakayosaidia kuongeza ufanisi zaidi katika majukumu yao.

Aidha, Naibu Wakili Mkuu ameongeza kuwa kompyuta hizo zitakuwa msaada mkubwa kwa Ofisi yake kwa kuzingatia ukweli kuwa mwaka huu tunaenda kwenye zoezi la uchaguzi hivyo itawawezesha watumishi wake hususani mawakili katika kutekeleza majukumu ya usimamizi wa mashauri.

“Mwaka huu tuna jukumu la uchaguzi na uchaguzi huwa unapelekea kuibuka kwa mashauri mengi yanayofunguliwa kwa ajili ya kupinga matokeo ya uchaguzi”, alisema Mhe. Malata.

Naye Bw. Muungano Saguya ambaye ni Meneja Huduma kwa Jamii katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo ili kuwasaidia watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha zaidi hatua itakayopelekea kuendelea kuokoa fedha nyingi ambazo zingeweza kupotea kutokana na upungufu wa vitendea kazi ofisini hapa.

Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilianzishwa feburuari 12 mwaka 2018 kwa tangazo la serikali Na. 50 ikiwa na lengo la kuratibu, kusimamia na kuendesha mashauri yote ya madai pamoja na Katiba, Uchaguzi na haki za binadamu yanayofunguliwa dhidi ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.


Share:

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Avitaka Vyuo Vya Mafunzo Ya Kilimo Vihuishe Mitaala ili iendane na mahitaji ya nchi

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bwana Gerald Kusaya amewaasa Wakuu wa Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo vya Serikali na Binafsi Wanawajibu wa kuhuisha mitaala ya mafunzo ili iendane na mahitaji ya nchi ya sasa ambayo ni kuandaa wataalam ili wazalishe kwa tija kulingana na uchumi wa viwanda.
 
Katibu Mkuu Kusaya ameyasema hayo leo (30.06.2020) wakati wa mkutano aliouitisha Mjini Morogoro kwa ajili ya kukutana wa Wakuu wa Vyuo vya Mafunzo vya Serikali (Vyuo 14) na Wakuu wa Vyuo Binafsi (Vyuo 15) nchi nzima; lengo ni kuboresha utoaji wa mafunzo ya kilimo katika Tanzania ya viwanda.
 
Bwana Kusaya katika hotuba yake amewaeleza Wakuu hao wa Vyuo vya kuwa Wizara ya Kilimo ina lengo la kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo na kuongeza kuwa mchango wa Sekta ya Kilimo kwenye pato la taifa ni asilimia 28 ambapo mchango wa sekta ndogo ya mazao ni asilimia 16. 
 
Mchango huo unaweza ukaongezeka ikiwa Vyuo vya Mafunzo vya Serikali na Binafsi vitazalisha Wagani bora na siyo Wagani mizigo alisema Kusaya.
 
“Lengo hapa ni kuhakikisha mafunzo yatolewayo katika Vyuo hivi yanakuwa ni yale yanayo kwenda sambamba na hali ya sasa ya mahitaji ya maarifa katika Sekta ya Kilimo kwa kuondokana na mtindo wa kutumia mitaala iliyopitwa na wakati”. Amekaririwa Katibu Mkuu.
 
Bwana Kusaya ameongeza kuwa, tija na uzalishaji kwenye Sekta ya Kilimo inachangiwa na aina ya Wagani wanaozalishwa na Vyuo vya Mafunzo.
 
“Tunapokuwa na Wagani wenye weledi, ni dhahiri kuwa Sekta ya Kilimo inaweza kukua na kutoa mchango mkubwa kwa pato la Taifa. Kwa sasa Sekta ya Kilimo inachangia asilimia 28 ya pato la Taifa ambapo sekta ndogo ya mazao inachangia 16.2% ya pato la Taifa”.
 
“Ni muhimu sana kwa Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo; kujikita katika kuinua Sekta ya Kilimo kupitia mafunzo kwa vitendo na kubuni teknolojia ambazo zinaweza kumsaidia Mkulima. Vyuo vinapaswa pia kuwa chachu ya kueneza ubunifu kwa Wanafunzi ili waweze kuwa na maarifa na ujuzi wa kujiajiri.” Amekaririwa Bwana Kusaya.
 
Katibu Mkuu Bwana Gerald Kusaya ameongeza ili Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo vya Serikali na Binafsi viende sambamba na kasi ya mabadiliko ya hali ya ukuaji wa uchumi wa nchi ni vyema kuwe na ushirikiano na Wdau mbali ndani na nje ya nchi.
 
“Katika kufanya hayo yote Wakuu wa Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo wanapaswa kushirikiana na Wadau wengine wa maendeleo katika kuboresha teknolojia na mbinu za ufundishaji.”
 
“Kupitia Wadau mabalimbali; tumesikia wenyewe kupitia maelezo ya utangulizi namna ambavyo wameboresha mazingira ya ufundishaji Vyuoni, pia kushiriki katika uhuishaji wa mitaala na kuwajengea uwezo Wakufunzi katika nyanja za mbinu za ufundishaji.” Amesisitiza Katibu Mkuu.
 
Kipekee Katibu Mkuu Bwana Gerald Kusaya amewashukuru Wadau wa maendeleo ambao ni Viongozi na Wafanyakazi wa Mashirika ya Sustainable Agriculture Tanzania (SAT) na Lutheran World Relief (LWR). 
 
“Nimeelezwa kwamba, Mashirika haya yamekuwa mstari wa mbele kwa kufanya kazi za kuimarisha taaluma na mafunzo katika Vyuo vya Mafunzo ya kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo (Serikali) ili kufikia adhma ya kuwa na mitaala bora ya kufundishia kwa sasa na endelevu”. Amemalizia Katibu Mkuu.
 
Mwisho Katibu Mkuu aliwakaribisha Wadau wote; kwenda ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo yenye lengo la kuboresha na kuleta ufanisi katika maendeleo ya ugani na mafunzo ya kilimo.
 
Naye Dkt. Wilhelm Mafuru, Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo, Huduma za Ugani na Utafiti, Wizara ya Kilimo amesema maboresho ya mitaala katika Vyuo Mafunzo vya Serikali na Binafsi imehuishwa na itaendela kuhuishwa ili kuwaanda Wanafunzi na Wahitimu kujiajiri na si kufikiria kuajiriwa.
 
“Napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa mbinu za kisasa za ufundishaji na uhuishaji wa mitaala ni jambo endelevu; Sambamba na maelekezo ya Katibu Mkuu; Tutaendelea kushirikiana na Wadau wote na mfano mzuri ni mkutano kama huu aliouitisha Katibu Mkuu.”Amekaririwa Dkt. Wilhelm Mafuru, Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo, Huduma za Ugani na Utafiti, Wizara ya Kilimo.


Share:

Waziri wa Fedha Dkt. Mpango: Sijaridhishwa Na Eneo Lilipojengwa Soko La Kimataifa Kigoma

Na Josephine Majura, Peter Haule-KIGOMA
WAZIRI wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, kutafuta eneo jipya, kubwa, lenye hadhi ya kujengwa soko la Kimataifa badala ya eneo linapojengwa Soko la Kimkakati la Kimataifa la Mnanila, lililoko katika mpaka wa Burundi na Tanzania.

Maagizo hayo ameyatoa wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa soko hilo la Kimkakati la Kimataifa akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayopatiwa fedha na Serikali.

Dkt. Mpango alisema kuwa hajaridhishwa na ubora wa ujenzi wa soko hilo ambalo linatarajiwa kuwa la kimataifa kutokana na kujengwa katika eneo dogo, na ujenzi wake uko chini ya kiwango ikilinganishwa na kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kilichotumika kujenga miundombinu ya mradi huo uliolenga kuchochea shughuli za biashara na kiuchumi kati ya wananchi wa Tanzania na Burundi.

Alisema kuwa atatuma timu ya wataalamu kuchunguza na kufanya ukaguzi maalaum ili kubaini watu waliohusika kushauri soko hilo lijengwe katika eneo lisilokuwa na hadhi pamoja na kuchunguza matumizi ya fedha za mradi huo zilivyotumika.

Aidha, Dkt. Mpango alisema iwapo utabainika udanganyifu wa matumizi ya fedha hizo hatua kali zitachukuliwa na kwa kuanzia ataanza na ofisini kwake kujua vigezo vilivyotumiwa na wataalam wake walioishauri Wizara iidhinishe matumizi ya kiasi hicho cha fedha huku wakijua kuwa eneo linalojengwa mradi huo halina sifa ya kujengwa miundombinu

“Mtafute eneo lingine tofauti ambalo linaweza kweli  kubeba dhana ya Soko La kimataifa ili tukuze biashara  na wananchi wetu wapate kipato na Halmashauri iweze kulipa na kugharamia maendeleo ya nchi yetu lakini kwa mawazo madogo hivi hatuta sogea” alisema Dkt. Mpango.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina, amesema atashughulikia kwa haraka dosari zilizobainika katika ujenzi wa Soko la Mnanila. Ambalo malengo yake ni kuboresha maisha ya wananchi na kuongeza kipato cha Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe na mkoa wa Kigoma kwa ujumla ili iweze kujitegemea.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilayaya Buhigwe Bw. Anosta Nyamwoga, alimuahidi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kwamba Halmashauri yake itatafuta eneo jipya kwa ajili ya ujenzi wa soko kubwa la kimataifa kwa haraka.

Awali, baadhi ya wakazi wa Kata ya Mnanila, akiwemo Bw. Amon Ndabita, walieleza kutoridhishwa na ujenzi wa soko hilo na kwamba hawajashirikishwa katika kupendekeza eneo linalofaa kwa ujenzi wa soko hilo la kimkakati la kimataifa ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu shilingi bilioni 2.3 zinazotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango chini ya radi wa kuziwezesha Halmashauri kujitegemea kimapato.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alimpa muda wa siku 15 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Bw. Anosta Nyamwoga, kuwalipa mamalishe, vibarua, mafundi waliojenga Soko hilo la Kimkakati la Kimataifa Munanila ambao wamelalamika mbele yake kutolipwa fedha zao tangu mwezi Julai mwaka 2019.

“Nakuagiza uwalipe fedha zao zote wanazodai na utajua utakako zitoa fedha hizo, uwalipe na wewe utawadai wakandarasi wakulipe fedha zako kwani ulitakiwa kuhakikisha wananchi hawa wanapata haki zao” alisisitiza Dkt. Mpango

Dkt. Mpango yuko katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma kukagua miradi ya maendeleo inayopewa fedha na Serikali ambapo ametembelea Miradi ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Munzeze, Ujenzi wa Jengo la Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe na Ujenzi wa Soko la Kimkakati la Kimataifa Mnanila.

Mwisho


Share:

Waziri Kigwangalla Azungumza Na Balozi Wa China, India Na Umoja Wa Ulaya Kuelezea Utayari Wa Tanzania Kupokea Watalii.

Na. Aron Msigwa – WMU.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Tanzania iko tayari kupokea watalii kutoka China, India na mataifa mengine ambayo yameruhusu raia wake kusafiri nje ya nchi zao.

Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na Balozi wa China nchini Tanzania, Ms.Wng Ke, Balozi wa India nchini Tanzania, Sanjiv Kohli na Balozi  wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Manfredo Fanti.

Akizungumza na mabalozi hao amesema Tanzania imekwisha fungua anga na kuruhusu ndege za abiria za kimataifa kutua hali iliyochangia kufunguka kwa Sekta ya Utalii kutokana na kuwepo kwa utayari, mazingira salama na maandalizi mazuri ya kupokea na kuhudumia  watalii  watakaowasili nchini wakati huu wa janga la Corona.

Dkt. Kigwangalla amesema ameamua kukutana na kuzungumza na mabalozi hao kuwaelezea  utayari wa Tanzania kupokea watalii na hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania kufungua Sekta ya Utalii  wakati huu wa janga la Corona.

Aidha, amesema ameamua kukutana na mabalozi hao kwa kuwa  nchi zao zinaleta watalii wengi Tanzania pia mabalozi hao nafasi kubwa ya ushawishi na uwezo wa kuwahamasisha  mawakala wa Utalii, makampuni ya huduma za utalii na raia wa nchi zao kufanya safari za kitalii nchini Tanzania.

Amewaeleza mabalozi hao kuwa Tanzania ilichukua hatua mbalimbali kukabiliana na janga la Corona ikiwemo uzingatiaji wa masharti na matakwa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa Mamlaka za Afya nchini kuwaelimisha wananchi na kuwasisitiza kuzingatia kanuni za afya zikiwemo za uvaaji wa barakoa, matumizi ya vitakasa mikono, unawaji wa mikono mara kwa mara na kuepuka misongamano hatarishi  hali iliyochangia kuwepo kwa maambukizi madogo ya ugonjwa wa Corona.

Dkt. Kigwangalla amebainisha kuwa Tanzania haikuchukua hatua kali za kuwafungia watu majumbani (Lockdown) kama yalivyofanya mataifa mengine kutokana na uchumi na shughuli za wananchi wengi kutegemea kipato cha siku kujikimu kimaisha.

Amewaeleza  mabalozi hao kuwa tayari Tanzania imezindundua mwongozo wa Taifa wa uendeshaji wa Huduma na Biashara ya Utalii ambao kulinda afya na usalama  wa wadau wote wanaojihusisha na biashara ya utalii katika kipindi hiki cha janga la Corona.

Dkt. Kigwangalla amewaeleza mabalozi hao kuwa watalii wote wanaowasili Tanzania katika kipindi hiki cha janga la Corona watakuwa salama kutokana na uwepo wa mwongozo  kwa kuwa huo kwa kuwa unatoa usimamizi kwenye viwanja vya ndege, hoteli za kitalii, watoa huduma za utalii, upimaji wa afya za wahudumu na wageni wote wanaoingia nchini pamoja kukusanya taarifa za wasafiri wote wanaoingia nchini Tanzania.

Dkt. Kigwangalla amewahakikishia mabalozi hao kuwa mifumo ya huduma za afya  na dharula nchini Tanzania iko tayari  kuhudumia watalii watakaokuwa wakiwasili kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii  akibainisha kuwa Tanzania ina hospitali za kisasa, maabara za upimaji zenye vifaa vyote vya huduma za dharula katika maeneo tofauti tayari kuhudumia watalii na wageni watakaoonesha dalili za kuwa na ugonjwa wa Corona.

Pia, amewaomba mabalozi hao wapange muda wa kutembelea maeneo mbalimbali yanayotumika kupokelea watalii yakiwemo ya viwanja vya ndege, hoteli za kitalii na hifadhi mbalimbali ili kujionea utayari wa Tanzania katika kuwahudumia watalii.

Kwa upande wao mabalozi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa  juhudi anazozifanya kuhamasisha na kutangaza utalii na kuelezea hatua zilizochukuliwa na Tanzania kuonesha utayari wake wa  kupokea watalii.

Wameipongeza Serikali kwa kwa juhudi kubwa za kulinda uhifadhi na kuahidi kutoa ushirikiano katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhifadhi.

Mabalozi hao wamefurahishwa na uwepo wa Mwongozo wa Taifa wa  Uendeshaji wa shughuli za Utalii Tanzania pamoja na kuridhishwa na hali ya utulivu iliyopo inayowafanya wananchi waendelee na shughuli zao  za kila siku.

Aidha, wameridhishwa na hatua za haraka zilizochukuliwa na Tanzania kufungua anga jambo lililowezesha mashirika makubwa ya ndege ya kimataifa kuanza kurejesha safari za anga nchini Tanzania.

Mwisho.


Share:

Maswali 15 Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kwenye Usaili ( Interviews ) na Namna ya Kuyajibu

Usaili wa ajira (interviews) husababisha hofu na msongo wa mawazo kwa vijana wengi kabla au baada ya kutoka chumba cha usaili.

Tatizo hilo hutokana na hofu inayojenga wakati wa kujibu maswali unayoulizwa  na watu ambao wamekuzunguka wakati wa kufanyiwa usaili.

Njia moja ya kuzuia hii kutokea ni kufuatilia mfumo wa kujibu maswali.

Ifuatayo ni orodha yetu ya maswali 15 yanayoulizwa mara kwa mara kwenye interviews( Usaili) na namna ya kuyajibu;

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

1.Jitambulishe(Wewe ni Nani?)
Mara nyingi hili ni swali ambalo mtahiniwa huulizwa mara tu aingiapo kwenye chumba cha usaili. Kwa bahati mbaya watahiniwa wengi hudhani kuwa waajiri hutamani kujua majina yao. Hapana, majina yako wanayafahamu na pengine hata taarifa za ziada. Katika swali hili waajiri uhitaji kujua sifa zako zihusianazo na ajira zitakazo dhihirisha kuwa wewe ni mtu sahihi.

Mfano mtu anaweza kujibu hivi, “Jina langu ni Mti Mkavu, ni Mhitimu wa Shahada ya Masoko ya Chuo Kikuu Dodoma. Ni mtu makini, mbunifu, mchapa kazi na ninayependa watu. Pamoja na hayo ninao ujuzi usio na shaka kwenye masuala ya mawasiliano. Uwezo wangu unadhihirishwa na mrejesho ambao huwa na upata kwa kila mtu ninaye fanya naye kazi”.

Katika swali hili ni muhimu kujua kuwa halihitaji wewe kuzungumzia mambo yasiyo husiana na kazi na ajira. Kwenu mpo wa ngapi,jina la mama yako, mkoa unaotoka, kabila, kazi ya baba au mama yako havihitajiki katika taarifa unazotakiwa. 


2.Kwanini upewe ajira kwetu? | au unaweza ukaulizwa Kwa nini unahisi wewe ni mtu sahihi kwa kazi hii na siyo mwingine?

Kumbuka kuwa usaili wa kazi unahusisha ushindani hivyo swali hili linataka uoneshe utofauti ulionao. Katika kujibu swali hili zingatia mahitaji ya kazi husika kujenga hoja kwani hata kama una utofauti wa aina gani kama hautasaidia katika kufikia  malengo ya taasisi bado itakuwa ni kazi bure.

Mfano, “ Siyo kwamba mimi ni mchapakazi na mbobezi katika uhasibu pekee lakini pia ni mtu ambaye ninaweza kufanya shughuli zangu bila kusimamiwa. Mimi ni mtu wa matokeo hivyo kwa kila ambacho hufanya hulenga kutimiza malengo kwa wakati na kufikia viwango stahiki. 


"Ubora wangu unathibitishwa na tuzo kadhaa nilizowahi kupata ikiwemo mfanyakazi bora wa mwezi mara nne nilipokuwa nikifanya kazi na na Magogo Media. Hii inathibitisha kuwa mkinipa fursa hii hamtakuwa mnajaribu bali mtakuwa mnafanya maamuzi sahihi”.

3.Unajua nini kuhusu sisi?
Siku zote maandalizi ya usaili yanaenda sambamba na kutafuta taarifa sahihi za taasisi husika. Hivyo ni vyema kuhakikisha kuwa taarifa unazotoa hapa ni sahihi na muhimu katika kudhirisha kuwa ulishafanya utafiti wa kutosha kuhusu taasisi husika.

Mfano, “ Benki yenu ilianzishwa mwaka 1987 ina maono ya kuwa benki bora kuliko zote nchini kwa kutoa huduma za kifedha zinazo aminika na kufikia maeneo mengi nchini. Kwa sasa benki yenu ina matawi 700 na ATMs 500 huku ikiwa na mpango wa kufungua matawi mengine Kigoma hivi karibuni. 


Endapo mtanipa fursa ya kufanya kazi na nyinyi nitahakikisha natumia vyema uwezo wangu katika masuala ya masoko ili kuongeza wateja na kuhaikisha huduma bora mnayotoa inafahamika kwa watu wengi.”

4. Ni vitu gani unavyojivunia?
Katika swali hili waajiri huhitaji kujua mambo kadhaa ambayo unayaona kama mtaji mkubwa katika utendaji kazi. Ni vyema kukumbuka kuwa mambo utakayo yataja hapa ni yale yenye umuhimu katika kuongeza ufanisi au ubora katika kazi husika kwani kila kazi inamahitaji yake ya tofauti na kazi nyingine.

Kwa mfano, “mambo makuu mawili ninayojivunia ni ujuzi na uwezo katika huduma kwa wateja na kujisimamia katika majukumu yangu. Kila ninapowahudumia wateja huwa napokea mrejesho chanya juu ya namna wanavyoridhishwa na huduma yangu hivyo kutamani kuhudumiwa nami tena.


Hii hunifanya nijione kuwa mtu muhimu sana katika taasisi yoyote ninayofanya nayo kazi. Pia, uwezo wangu katika kufanya shughuli bila kusimamiwa au chini ya usimamizi mdogo unanifanya niwe mtu wa kuaminiwa na kutegemewa katika kufanya shughuli zangu.Haya ni baadhi ya mambo mengi yanayonifanya mimi kuwa mtu wa tofauti. Nina amini hamtaacha fursa ya kufanya kazi nami”
 

5.Udhaifu wako ni upi?
Hili ni moja ya maswali ambayo watainiwa wengi huyachukia na kuyaona kama yana lengo la kuwatafutia sababu za kuwanyima kazi. Wengine kwa lengo la kuonesha ukamilifu huthubu kusema kuwa hawana udhaifu wowote-usithubutu kusema hivyo. Kila mtu ana udhaifu wake kwani hakuna aliye mkamilifu.

Suala la msingi ni kujua namna ya kujibu suali hili. Mambo ya kuzingatia ni pamoja na kuchagua udhaifu ambao hauta athiri utendaji wako na pili hakikisha udhaifu huo unahusiana na ujuzi na sio tabia. 


Ujuzi ni rahisi kuutafuata lakini kubadilisha tabia ni ngumu zaidi hivyo usiseme kuwa wewe ni mvivu,mdokozi, na mengineyo ya kitabia. Na unapotaja udhaifu wowote kumbuka kuonesha jitihada ambazo umeshazifanya ili kudhibiti udhaifu huo.

Kwa mfano, kwa kazi ya uhasibu mtu anaweza sema, “Udhaifu nilio nao ni masuala ya ‘graphic designing’ niligundua hili nilipohitaji kuandaa tangazo kwa ajili ya ofisi niliyokuwa nikifanya nayo kazi. Hata hivyo, nimeanza kujifunza mwenyewe kupitia mtandao wa internet na naona napata mabadiliko chanya kila leo”.

Kwa jibu hili ni dhahiri kabisa graphic designing siyo mahitaji muhimu ya kazi ya uhasibu hivyo haita athiti utendaji wa kazi.


6. Kwa nini uliacha kazi yako ya mwanzo?
Hapa unahitajikua makini sana, kumbuka na epuka kuzungumza vibaya kuhusu muajiri yeyote kabla au sasa au uwezo wa muajiri. 


Hapa unaweza ukawajibu tu kwamba;" Kwa sababu ya kuboresha na kuongeza ujuzi, pia natafuta fursa bora zaidi."

7.Unatarajia kupata nini kutokana na kufanya kazi hapa? au unaweza ukaulizwa | Baada ya miaka mitatu wewe mwenyewe utakua wapi?
Ongelea unachotumaini kutimiza ila kuwa mkweli. Pia usiongee kwa ujumla. Chagua kitu maalum ambalo ni muhimu kwa kampuni alafu ilenge. Ila, uwe wazi kwa kusema itachukua muda kujifunza zaidi kuhusu kampuni ili kufanikiwa zaidi.

Kwa mfano; “Nikiwa mwalimu wa kiingereza, lengo langu ni kuongeza asilimia ya wanafunzi wanaofaulu mtihani wa taifa kuwa 85% ya darasa yangu. Najua itachukua muda kujua vizuri changamoto za wanafunzi ila, naamini nitafanikiwa”


Ni vizuri kusema kwamba unatumaini kuona uwajibikaji zaidi  katika kampuni hiyo na kuongeza thamani katika kampuni kwa mchango wako. 

8.Kwanini umekaa muda mrefu bila kupata ajira?

Wajibu kwamba; "Nilikuwa najiendeleza katika taaluma yangu "


9. Eleza namna unavyoweza kujisimamia mwenyewe
Wajibu kwamba: Nitakuwa nafanya kazi niliyopewa nikishirkiana na wasimamizi wangu na viongozi juu ya namna ya kumaliza kazi kabla ya muda uliopangwa.


10. Kitu gani kinakukera miongoni mwa wafanyakazi wenzako?

Wajibu kwamba; "Naamini katika kufanya kazi kwa pamoja. Hata kama nikikerwa na kitu chochote, huwa najaribu kuepuka isipokuwa kama ni kitu cha binafsi."

11.Unategemea kufanya kazi kwa muda gani kama ukipewa ajira?

Wajibu:Kwa muda mrefu kama nitaendelea kuongeza kitu katika taaluma yangu.

12:Je, mwenyewe unajiona kufanikiwa?

Wajibu: Ndio, ukiachana na uwezo wa taaluma yangu, nadhani nimepata watu sahihi wa kufanya nao kazi.

13. Uwezo wako ni upi katika kazi?
Wajibu: Mimi huwa naelewa na kufundishika kwa haraka na ni mchapakazi wa kweli.

14,Unapenda nafasi au cheo gani katika timu unayofanya nayo kazi?
Wajibu: Haijalishi hadi nitakapojifunza kitu kipya kwa kila mradi au kazi.

15.Je, unaswali lolote kwetu? 

Mwishoni wa interview, ni kawaida kwa mwajiri kuuliza kama una maswali kwao. Ukipewa nafasi hii, usiulizie mshaara na faida zingine. Badala yake, uliza:
  1.     Maadili ya kampuni
  2.     Aina ya uongozi
  3.     Wafanyakazi wenzako
  4.     Chochote ambacho hukuelewa kuhusu kazi hiyo.
  5.     Watakupa jibu baada ya muda gani?
==>>USIFANYE HAYA MAKOSA KATIKA SWALI HILO:
- Je, kuna fursa ya kukua / kupandishwa ngazi?
- Nitapata siku ngapi za likizo?

- waajiliwa wanafaidika vipi na kampuni hii. 

==>Tiba bora ya msongo wa interview ni kujiandaa
Ingawa interview inaweza ikakupa misongo mingi, ukijiandaa vizuri Utashangazwa na mafanikio yako.

Interview ni nafasi yako ya mwisho kumvutia mwajiri, na vidokezo vilivyoelezwa hapo juu vitakusaidia na hilo.

Kumbuka, hamna haja ya kuwa na wasiwasi ukiwa umejiandaa. 


Nakutakia Mafanikio mema kwenye Interview
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

👉Sasa, kwa kuwa umeshajua jinsi ya kujibu vizuri maswali ya Interview, anza kutafuta kazi unayoitaka kwa kubofya hapo chini. 


Hilo ni Jukwaa Maalumu la Ajira zote za Serikali, Makampuni Binafsi n.k. Kuna Nafasi za Kazi zaidi ya 7000 kwa ajili yako.

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://ajirazote.com/jobs


▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬


Share:

Rais Magufuli Arejesha Fomu za Kugombea Urais Kupitia CCM....Wanachama Zaidi ya Milioni 1 wa CCM wamdhamini

Jumla ya wanachama Milioni 1,023, 911 wa  chama cha Mapinduzi, CCM wamejitokeza kumdhamini Mwenyekiti wao Rais Magufuli katika fomu za kuwania kupitishwa na chama hicho kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo Jumanne tarehe 30 Juni 2020 makao makuu ya CCM, Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally wakati wa hafla fupi ya  kuzipokea Fomu za Kugombea Urais wa Tanzania Zilizowasilishwa na Rais Magufuli 
 
Hafla hiyo fupi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM, Serikali na wanachama wa chama hicho wakiwemo wenyeviti wa chama hicho nzima waliowasilisha kila mmoja fomu za udhamini.
 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa, Dk. Bashiru amesema, jumla ya wanachama Milioni 1,023, 911 walijitokeza kumdhamini  Rais Magufuli kutoka mikoa 32 na jumuiya zake tatu za wazazi, vijana na wanawake.

Amesema, leo Jumanne saa 10 jioni ndiyo siku ya mwisho ya uchukuaji na urejeshaji fomu za urais ndani ya chama hicho. Aliyechukua ni mmoja tu ambaye ni Rais Magufuli.


Share:

Tumefanya Maboresho Kwenye App Yetu ya Mpekuzi Ili Kukuwezesha Kupata Habari zetu Haraka

Tumefanya Maboresho Kwenye App Yetu ya Mpekuzi Ili Kukuwezesha Kupata Habari zetu Haraka

Usikubali kupitwa na taarifa muhimu zinazoendelea hapa nchini na Duniani  kwa Ujumla . Tumejipanga vizuri sana kukupatia taarifa sahihi na kwa wakati.

👉1. Tumebadili muonekano na kuufanya kuwa mzuri zaidi
👉2. Kila habari tunayoweka kuanzia sasa utapata notification kwenye simu yako 
👉3. Habari zote kwa sasa zinafika kwa haraka kwenye simu yako kuliko ilivyokuwa hapo awali

KUMBUKA: App yetu ni BURE. Unachotakiwa kukifanya ni kuingia Playstore na kupakua MPEKUZI APP

Kama tayari unayo, basi Ingia Playstore kwa ajili ya kupata UPDATE hii ya Toleo Jipya

Tumekurahisishia, Unaweza pia ...<<KU BOFYA HAPA>> Kupata toleo hili Bure Kabisa


Share:

Jaji Ndika : Sheria Ya Wanawake Na Watoto Zitafsiriwe Ziendane Na Wakati

Na Tawani Salum – Mahakama
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt. Jaji Gerald Ndika amewataka Majaji na Mahakimu kutafsiri sheria zinaohusu masuala ya wanawake na watoto ili ziendane na mazingira ya sasa katika kuendesha mashauri yanayohusu masuala la unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.

Akizunguza wakati wa Mafunzo ya Haki za Binadamu na Unyanyasaji hususani kwa  wanawake na watoto, yanayofanyika Mjini Bagamoyo Mkoa wa  Pwani Jaji Ndika   alisema  kuwa sheria zilizopo kwa kiwago kikubwa zinajitosheleza kinachotakiwa jinsi ya kuzitafasiri,  hivyo Majaji na Mahakimu watoe tafsiri ambayo inaendana na mazingira ya matukio yalivyo.

Jaji Ndika ambaye ni mshiriki katika mafunzo hayo,  alisema kuwa moja ya faida zake ni kuwaandaa wawezeshaji katika eneo hilo ili kusaidia Mahakama ya Tanzania, Majaji wa Mahakama ya Rufani,Majaji wa Mahakama Kuu, Mahakimu,watumishi mbalimbali ambao wanatoa maamuzi juu ya  vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa wanawake na watoto kuwa na umahiri.

‘‘Matukio haya yanatokana na mambo mengi ikiwemo mila potofu pamoja na  uelewa wao mdogo, wanaona kumpiga mke au mtoto ni jambo la kawaida na ana haki ya kufanya hivyo. Lakini ubora wa mafunzo haya yatasaidia kupata wakufunzi ambao wataenda kuwapa wengine elimu juu ya kuweza kupambana na ukatili na unyanyasaji wa wanawake na watoto,’’ alisisitiza Jaji Ndika. mafunzo hayo, alisema  ni ya mara ya tatu kufanyika yakiwa  ni endelevu katika kutoa elimu hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Joaquine De Mello akifungua rasmi mafunzo hayo, alisema kuwa  yana lengo la  kuwawezesha watoa maamuzi kuwa na uweledi zaidi  wa kutoa  haki na pia kuielimisha jamii  juu ya haki zao za msingi na tatizo la unyanyasaji na ukatili wa kijinsia ambalo limekithiri.

Aliongeza kwamba kumekuwa taarifa nyingi zinazotolewa na vyombo vya habari pamoja na wanajamii ambao wamejitokeza wazi kutoa matukio mbalimbali   juu ya suala hilo. Pia tafiti mbalimbali ambazo zimefanywa hivyo wamegundua kuwa matukio mengi ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia yanafanywa wahusika  wanaotuhumiwa kuwa  ni familia au ndugu wa karibu.

Alisema kuna mapungufu katika jamii kama vile utamaduni wa kutokuwa na utayari wa kusimamia na kuyapigia kelele  tatizo hilo,  ikiwa  ni sababu mojawapo ya unyanyasaji na ukatili huo.

‘‘Kupitia mafunzo haya kama watoa maamuzi tunataka wapate jicho la kipekee shauri linapokuja mbele yako mara moja unapata picha kuwa hili ni la kikatili na unalipa nafasi yake na hii itasaidia katika kuandaa taarifa ya matukio haya kwa usahihi, ikiwemo kuna takwimu ambazo tunazihitaji ili kujua nguiu gani ya ziada inahitajika katika kusimamia jambo hili,’’ alisema Jaji De Mello.

Mshiriki mwingine wa mafunzo hayo, ambaye Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine,iliyopo Jijini Dar es Salaam Mhe,  Hanifa Mwingira alisema jamii inapaswa kuona kuwa vitendo hivyo ni vibaya na kila mtu anapaswa kusema ‘ukatili sasa basi na mtoto wa mwenzako kuwa ni mtoto wako na hupaswi kumfanyia ukatili,’.

Mwingira alifafanua kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa viongozi wa dini ambao  watawaelimisha  waumini wao, wakiwemo  Wenyeviti wa vijiji, kata pamoja na mitaa na Maafisa wa Ustawi wa Jamii, Polisi, Magereza na wadau wengine wa  sharia.

Mafunzo hayo yanayoendelea Mjini Bagamoyo Mkoani Pwani yalihudhuriwa na Majaji Wataafu kama vile Mh. Jaji Salum Massati ambaye anashiriki kama mtoa mada,

Jumla ya washiriki 26 wanapatiwa   mafunzo juu ya masuala ya unyanyasaji na ukatili kijinsi. Mafunzo hayo yameanza Juni 27, mwaka huu na yatamalizika Julai Mosi,  mwaka huu.


Share:

Virusi vipya vya mafua vyabainika kwa nguruwe nchini China

Wanasayansi wamebaini uwepo wa aina mpya ya virusi vya nguruwe vinavyosababisha mafua  nchini China ambavyo vinahofiwa kuwa huenda vikasababisha janga la dunia.

Wataalamu hao wamesema virus hivyo vilivyobainika karibuni vinapatikana kwa nguruwe, na imeelezwa kuwa kuna uwezekano vinaweza kuongezeka kwa haraka na kuhamia kwa binadamu.

Licha ya kuwa hadi sasa havijawa tishio, lakini imeelezwa kuwa kuna dalili zote kuwa vinaweza kuathiri binadamu, hivyo kuhitaji ufuatiliaji wa karibu.

Kutokana na upya wake, virusi hivyo vitakuwa changamoto kwa sababu miili ya watu itakuwa na uwezo mdogo au kutokuwa na uwezo kabisa wa kukabiliana navyo.

Tishio hilo jipya limekuja wakati dunia ikiwa bado inaendelea kupambana na janga la virusi vya corona 
 
Aina mpya ya mafua iliyobainika nchini China ina ufanano kiasi na mafua ya nguruwe ya mwaka 2009, lakini kwa kiasi fulani yanatofautiana.


Share:

Uhusiano Uliopo Kati ya Punyeto na Ukosefu au Upungufu wa Nguvu za Kiume


Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.
 
 Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.
 

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   zaidi  tafadhali  tembelea :  <<HAPA>>


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger