Tuesday 2 June 2020

Mkataba Mpya Waliosaini Yanga,GSM Na La Liga

Uongozi wa Klabu ya Yanga wakishirikiana na wadhamini wao Kampuni ya GSM Mei 31 wameingia mkataba wa misimu minne wa makubaliano ya kimaendeleo ya timu hiyo na kampuni La Liga 

Makubaliano ya kuingia mkataba huo yalifikiwa juzi kwenye Hoteli ya Serena, jijini Dar ambayo yatahusisha maendeleo ya mchezo wa soka nchini kupitia La Liga ambayo yanahusisha masuala ya ufundi na vifaa mbalimbali.

Klabu ya soka ya Yanga, mbali ya kufaidika na mfumo mpya wa uendeshaji, pia itapata fursa ya mafunzo kwa wachezaji, makocha na viongozi kutoka klabu ya Sevilla ya Hispania.

Mkataba huo ambao msingi wake ni kuifanya Yanga kuwa na mfumo wa kisasa wa uendeshaji, umeenda mbali zaidi ambapo licha ya kucheza mechi mbili kwa mwaka baina ya Sevilla na Yanga, pia utatoa fursa kwa wachezaji chipukizi kujiunga na shule ya michezo ya timu hiyo yenye historia kubwa ya soka.

Kwa mujibu wa ofisa habari wa Yanga, Hassan Bumbuli kutakuwa na mechi mbili kwa mwaka baina ya timu yao na Sevilla ambayo moja itafanyika Hispania na nyingine hapa nchini.

Malipo ya kwanza ya mkataba huo yanatarajiwa kufanyika kati ya kipindi walichoingia mkataba huo hadi Agosti 31, mwaka huu kwa Yanga na GSM kuilipa La Liga kiasi cha euro elfu 80 ambayo ni sawa na Sh milioni 204 baada ya makato iwapo yatatokea.

Wakati malipo ya pili ambayo yatafanyika msimu ujao katika kipindi kati ya Septemba mwaka 2020 hadi Juni 2021

Mbali ya mapendekezo ya mfumo wa uendeshaji, pia kutakuwa na suala mabadiliko ya Katiba ya klabu ambapo mpango wa klabu ya Yanga ni kuwahsirikisha wanachama na wadau wote kwa muda wa siku 21.

Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla alisema wawakilishi wa matawi kutoka kila pande za Tanzania watapata mafunzo maalumu jijini Dar es Salaam na kupewa makabrasha ambayo watayatumia kuendesha elimu ya mabadiliko hayo pindi watakaporejea kwenye matawi yao




Share:

Video Mpya: Kayumba – Kamwambie

Video Mpya: Kayumba – Kamwambie


Share:

Visa Vipya 32 Vya Corona Vyaongezeka Uganda, Maambukizi Yafikia 489

Wizara ya Afya nchini Uganda  imerekodi visa vipya 32 vya COVID19 nchini humo na idadi ya maambukizi hadi sasa ni 489, Wagonjwa wapya wote ni raia wa Uganda.

19 kati yao ni madereva wa malori , 13 waliosalia ni watu waliokuwa karibu na wagonjwa ambao tayari wamethibitishwa kuwa na virusi vya Corona.




Share:

Jarida la Billboard lawataka wasanii wa nje kujifunza kutoka kwa Daimond

Billboard wameachia makala wakielezea namna ya kupata mafanikio kimataifa kwa kutumia mtandao wa Youtube huku wakimtolea mfano star wa muziki wa Tanzania Diamond Platnumz
.
Makala hiyo imeandikwa "Wanamuziki wa Marekani wanatafuta njia za kutoboa kwenye Youtube, Wanapaswa kusoma mikakati ya kufanya na kuachia video kutoka kwa wasanii wa Kiafrika

"Wasanii wa Magharibi wanaweza kujifunza kutoka kwa kile wanachokifanya wasanii wa Kiafrika haswa wale ambao wamefanikiwa kimataifa," Amezungumza meneja wa 'Youtube Music Trends' Kevin Meenan, ambaye anasimamia ukusanyaji na uchambuzi wa data za chati za Muziki za YouTube

Ameelezea kuwa alivutiwa sana na mbinu pamoja na ubunifu ambao anautumia msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz kwenye chaneli yake ya YouTube na sehemu moja tu ya mkakati wa ujasiriamali ambao unajumuisha kituo cha redio ya FM pamoja na TV na usimamizi wa kampuni ya WCB Wasafi.

Kevin Meenan amesema Ukubwa wa Diamond kwenye Youtube ni wa kustaajabisha akiwa na Subscribers Millioni 3.6 na zaidi ya jumla ya views Millioni 980 huku 80% ya watamazaji wakiwa wanatokea nje ya Tanzania kutoka Mei 1, 2019 hadi Mei 1, 2020

Meenan anasema kwamba, kimataifa Diamond alitazamwa zaidi na watu wa Nchini Kenya ikifuatiwa na Tanzania na Marekani.

Billboard wameeleza kuwa Msimamizi huyo wa Youtube Trending alishangazwa kukuta Diamond ameweka zaidi ya video 600 kwenye mtandao wa Youtube "Kwa kweli ilibidi nichunguze mara tatu ili kuhakikisha kuwa ilikuwa sawa," Alielezea

Wamesifia kuwa Diamond anaweza kuweka hadi video 20 akitangaza Official video moja tu huku wakitolea mfano wa wimbo wa Jeje ambapo ukiachana na Official video, kuna dance video, cartoon video, lyrics video pamoja na official audio.

Kwenye Makala hiyo Billboard wameelezea kuwa uchunguzi wao umegundua kuwa wasanii wengi ambao wamefanikiwa kufikisha subscribers zaidi ya Million 1 basi huwa wanatazamwa zaidi na watu wa nje ya nchi zao

Credit: Bongo5


Share:

Donald Trump atishia kutuma jeshi kukabiliana na waandamanaji nchini humo

Rais wa Marekani Donald Trump ameahidi kumaliza maandamano ya vurugu ambayo yameikumba miji mikubwa nchini humo tangu kifo cha George Floyd, Mmarekani mweusi mwenye umri wa miaka 46.

George Floyd alifariki baada ya maafisa wa polisi wa Minneapolis kumbana kwa kutumia goti shingoni na mgongoni, uchunguzi wa kimatibabu uliosimamiwa na familia ya Floyd umebaini.

Rais wa Marekani pia alitangaza kwamba matukio ambayo yalifanyika Jumapili Mei 31 katika mji mkuu wa nchi hiyo ni "aibu", na kuyachukulia kama vitendo vya "kigaidi ndani ya nchi". Ametoa wito kwa magavana wa majimbo kuchukua maamuzi muhimu "kukabiliana na maandamano".

Wakati huo huo, vikosi vya usalama vimetumia gesi ya machozi kwa waandamanaji waliokusanyika nje ya ikulu ya White House.

Rais wa Marekani ametangaza sheria kuhusu uasi ambayo inamruhusu kutumia jeshi

"Ninavitaka vikosi vya ulizi na usalama kumaliza ghasia na visa vya uporaji vinavyoendelea, na kulinda haki za Wamarekani, "alisema.

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajia kukutana kwa faragha na msimamizi wake mkuu wa sheria , kufuatia maandamano ya vurugu yalioshuhudiwa katika miji kadhaa nchini humo, kupinga ubaguzi na ukatili wa polisi katika wakati huu wa janga la Corona.

Trump hajatoa tamko lolote kuzungumzia mzozo huo unaozidi lakini ameandika tweet kadhaa akiwaelezea waandamanaji kama vibaka na kuwahimiza mameya na magava kuchukuwa hatua kali zaidi. Alitishia pia kutumia jeshi lakini mshauri wake wa usalama wa taifa amesema serikali bado haiwezi kutumia udhibiti juu ya vikosi vya ulinzi wa taifa.

Lakini hadi sasa hakuna Gavana aliyetoa wito kwa jeshi kuingilia kati . Wengi wao wamebaini kwamba kutumia jeshi kunaweza sababisha hali inakuwa ngumu zaidi, ameripoti mwandishi wetu wa Washington, Anne Corpet.

-RFI


Share:

Ugonjwa wa Ebola waripotiwa tena kaskazini magharibi mwa Congo DR

 Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa, homa ya Ebola imeripotiwa tena katika maeneo ya kaskazini  magharibi mwa nchi. Taarifa hiyo imesema tayari watu wanne wameaga dunia katika siku chache zilizopita kwenye maeneo hayo kutokana na homa ya virusi vya Ebola.

Wizara ya Afya ya Congo DR imeongeza kuwa Taasisi ya Taifa ya Uhakiki wa Biomedical (INRB) imethibitisha kuwa, watu kadhaa waliofanyiwa vipimo katika mji wa Mbandaka wamepatikana na homa ya virusi vya Ebola.

Miezi miwili iliyopita Mkurugernzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) alitahadharisha kuhusu uwezekano wa mlipuko wa virusi vya homa ya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wimbi la maambukizi ya homa ya virusi vya Ebola lilianza tarehe 8 mei mwaka 2018 katika mji wa Bikoro mkoa wa Équateur uliko kaskazini magharibi mwa Congo DR na baadaye ikasambaa kwa kasi katika mji wa Mbandaka ambao ni makao makuu ya mkoa huo na mashariki mwa nchi hiyo.

Virusi hivyo vimesababisha vifo vya watu wasiopungua 2,200.


Share:

WAANDISHI WA HABARI KIGOMA WAPEWA VIFAA KUJIKINGA NA CORONA


Rais wa umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania Deogeatius Nsokolo akimkabidhi mwanachama wa chama cha waandishi wa habari matukiodaima mkoa wa Kigoma Editha Karlo vifaa vya kujikinga na virus vya corona anayeshuhudia ni katibu wa kigoma press Club Mwajabu Hoza : Picha na Kigoma Press Club 
Rais wa umoja wa klabu za waandishi wa habari (UTPC) Deogratius Nsokolo kushoto akikagua vifaa vya kujikinga na virusi vya corona vilivyotolewa na wadau mbalimbali pamoja na UTPC kwa ajili ya wanachama wake.
Na Editha Karlo - Kigoma

CHAMA cha waandishi wa habari wa Mkoa Kigoma(KGPC)imegawa vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kwa wanachama wake ili kuwasaidia kufanya kazi zao kwa ufanisi katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa huo.

Vifaa hivyo vimetolewa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC)kupitia mpango wa utekelezaji wa mpango mkakati wa kuzisaidia club za waandishi wa habari unaodhaminiwa na shirika la maendeleo la Sweden(SIDA).

Mratibu wa Klabu hiyo Diana Rubanguka alisema kuwa kila mwanachama atapata barakoa,glavu,chupa ya dawa ya kutakasa mikono(sanitaizer)ambavyo vitawasaidia kujilinda na kujikinga na ugonjwa huo.

Diana alisema vifaa hivyo vimetolewa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kupitia mpango wa utekelezaji wa mpango mkakati wa kuzisaidia club za waandishi wa habari unaodhaminiwa na shirika la maendeleo la Sweden (SIDA).

Rais wa UTPC, Deogratias Nsokolo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma alisema kuwa kutokana na hali ya mlipuko uliopo sasa wa ugonjwa virusi vya corona walikubaliana na SIDA kutumia baadhi ya fedha kununua vifaa vya kujikinga na ugonjwa huo na kutoa mafunzo kwa wanachama juu ya ugonjwa huo.

"Baadhi ya mambo yaliyokuwa yafanyike mwaka huu yamehairishwa na fedha zilizokuwa zimetengwa zimeelekezwa upatikanaji wa vifaa hivo kwaajili ya club zote za Tanzania Bara na visiwani",alisema Nsokolo.

Alisema kazi za waandishi wa habari zinahitaji kukutana na watu mbalimbali hivyo ni muhimu kuwa na vifaa vya kujikinga na maambukizi hayo.
Nsokolo aliwataka wanahabari wote nchini kuendelea kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya ugonjwa huo kwa kuzingatia na kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya na serikali ikiwa ni pamoja na kutumia vifaa hivyo kwa ufasaha.

Baadhi ya wanachama wa KGPC wakizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo wamesema kuwa wameupongeza uongozi wa club yao na UTPC kwa kuzingatia na kuona usalama wa wanachama wao wanapotekeleza majukumu yao ya kikazi katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona.

Share:

MWIZI ARUKA GETI NA KUIBA NYUMBANI KWA MWANDISHI WA ITV,...ASINZIA PAPO HAPO


Mwizi aliyekutwa ndani ya gari la Mwandishi wa Habari wa ITV Zanzibar, Farouk Karim.

Mwandishi wa Habari wa ITV Zanzibar, Farouk Karim, amesema kuwa siri kubwa ambayo mtu yeyote anaweza kuifanya ili wezi watakapofika nyumbani kwake waibe lakini wapitiwe na usingizi hapo hapo ni kumuamini na kumuomba Mungu ili awalinde wote ndani ya familia.

Farouk ameyabainisha hayo leo Juni 2, 2020, wakati wa mazungumzo mubashara kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, na ndipo aliposimulia mkasa wake baada ya mwizi kuruka geti la nyumba yake huko Fuoni visiwani Zanzibar na kuiba nguo na viatu lakini baadaye aliingia ndani ya gari na kupitiwa usingizi. 

"Huyu mwizi kaingia usiku wa manane karuka geti, na hatuna mlinzi pale nyumbani, kakusanya zile nguo zilizokuwa zimeanikwa kaziwekwa kwenye mfuko, katika magari yaliyokuwepo pale gari moja lilikuwa wazi akaingia, akapitia mlango wa abiria akachukua power window, akaenda upande wa dereva kuchukua power window ikamshinda ndiyo akalala hapo hapo" amesema Farouk Karim.

Akielezea siri ya mwizi kumuibia na kisha kupitiwa na usingizi Farouk amesema,"Tumempeleka Polisi kama ambavyo huwa tuna msindikiza Bi harusi, na ile kulala huenda kaiba sana hivyo karidhika, na dawa kubwa ya kumfanya mwizi alale ni moja tu kumuomba Mungu akulinde wewe na nyumba yako, na watu kama sisi ambao hatuna madhambi, Dua zinakubalika, kama unataka hiyo Dua nitafute inbox".
Chanzo - EATV
Share:

DC MBONEKO AKAGUA SHULE KUJIONEA UTEKELEZAJI NA MAPOKEZI YA WANAFUNZI KIDATO CHA SITA

Na Mwandishi wetu – Shinyanga 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga mkoani hapa, Jasinta Mboneko amewataka wanafunzi wote wa kidato cha sita katika shule zilizoko wilayani kwake kuacha hofu badala yake wasome kwa bidii na kutumia muda mchache uliosalia kuhitimisha masomo yao na kujiweka sawa kwa ajili ya mitihani ijayo. 

Mboneko ametoa kauli hiyo Juni mosi, 2020 mjini Shinyanga wakati akikagua na kuzungumza na wanafunzi mbalimabli kutoka shule tano zilizoko manispaa hiyo na Shinyanga Vijijini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya kuwataka wanafunzi wote wa kidato cha sita na vyuo kurejea huku suala la usalama wa afya na tahadhari ya ugonjwa wa covid 19 ukizingatiwa. 

Akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita shule ya Sekondari Old Shinyanga, Jasinta amesema kuwa kwa sasa wanapaswa kubadili fikra zao na kurejea katika masomo kutokana na muda uliosalia kuwa mchache kwao kwani wana uwezo wa kuhimili na kujiandaa vizuri. 

“Niwaombe nyinyi kidato cha sita hapa Shuleni Old Shinyanga mpo kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hakikisheni mnasoma na mnaacha kulala kwani muda siyo rafiki sana maana msipofanya bidii ya kupitia yale mliosoma mapema kabla ya COVID 19 kwa sasa mtashindwa kufanya vizuri katika mtihani wenu wa mwisho,” amesema. 

Akiwa shule za Sekondari Buluba,Savannah Plains na Don Bosco Mkuu huyo wa wilaya ameendelea kuwakumbusha na kuwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii kipindi hiki kilichosalia akiwataka kuondoa hofu kwani hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko tatizo lenyewe. 

Aidha amewataka wamiliki wa shule binafsi mkoani Shinyanga kuacha kuongeza gharama za aina yoyote kwa kisingizio cha ugonjwa wa COVID 19 huku akiwasisitiza walimu kuhakikisha wanafunzi wote wanarejea shuleni na kuendelea na masosmo kwani muda umebaki siku 27 pekee. 

Katika hatua nyingine Mboneko amewaomba wazazi nchini wenye watoto wanaosoma shule zilizoko wilayani Shinyanga ambao hawajafika wahakikishe watoto wao wanafika shule kwani muda unazdi kusonga hali itakayowafanya washindwe kufanya vyema. 

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Tinde iliyopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Pendo Matonange amesema kuwa shule hiyo ina idiadi ya wanafunzi mia 415 huku wanaotarajia kuhitimu kidato cha Sita wapo 204 tayari wamewasili wanafunzi 173 kati ya 204 wanaotarajia kufanya mitihani yao ya mwisho Juni 28, mwaka huu. 

Mwalimu Matonange amesema kuwa suala la usafi na usalama kwa wananfunzi wote juu ya kuchukua tahadhari ya Corona limepewa kipaumbele kutokana na tahadhari zinazotolewa na watalaam wa afya ikiwemo kuweka vitakasa mikono, sabuni na kukaa umbali wa zaidi ya mita moja. 

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari binafsi ya Savanah Plains, Yona Ludomya na Wiliam Makenge wa Sekondari ya Buluba wamesema kuwa tahadhari ya ugonjwa wa COVID imechukuliwa kwa hali ya juu kwa kuandaa mazingira rafiki kuhakikisha kuwa kila mwananfunzi anafanya mtihani wake akiwa na afya njema. 

Wameongeza kuwa kwa sasa jitihada na nguvu kubwa zimeelekezwa kwa wanafunzi hao ili waweze kukamilisha na kufanya mitihani yao kwa kzingatia kanuni na maagizo ya Serikali. 

Ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga imefanyika ikiwa ni kukagua na kujionea utekelezaji wa maagizo ya serikali iwapo shule zimezingatia maagizo yake kwa kuchukua tahadhari mbalimbali dhidi ya virusi vya Corona ikiwemo kuandaa vitakasa mikono na maji, ambapo amezitembelea shule za Sekondari Old Shinyanga, Tinde wasichana za Serikali na Buluba, Don Bosco na Savannah Plains zinazomilikiwa na watu binafsi. 
Wa Pili Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akitoa maelekezo kwa Mkuu wa shule ya wasichana Tinde Pendo Matonange 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta mboneko akiongea na wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Savannah plains
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari ya wasichana Tinde wakiendelea kumsikiliza mkuu wa wilaya. 
Wanafunzi wa kidato cha sita shule ya wasichana Tinde wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wakati akikagua utekelezaji wa maagizo ya Serikali dhidi ya Ugonjwa wa Corona 
Wanafunzi wa shule ya sekondari Old Shinyanga wakismikiliza mkuu wa wilaya wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa usalama wakiwa darasani
Wa Kwanza Kulia ni Mkuu wa wilaya Shinyanga Jasinta Mboneko akisisitiza jambo 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akihitimisha ziara yake shule ya Sekondari Don Bosco Didia
Share:

KIKUNDI CHA BARAKOA TZ CHAGAWA BARAKOA BURE ZAIDI YA 1000 MAENEO MBALIMBALI IKIWEMO VITUO VYA WATOTO YATIMA


 Rania Nasser akitoa msaada wa barakoa katika kituo cha watoto yatima Msimbazi


 Rania Nasser akitoa msaada wa barakoa katika kituo cha Mother Theresa Charity Center
Rania Nasser akishona barakoa

**Janga la ugonjwa wa virusi vya COVID-19 umeleta uhaba ya bidhaa nyingi humu nchini zikiwemo Barakoa. Rania Nasser ambaye ni mwanafunzi wa sekondari aliunda kikundi kinachojulikana kama Barakoa Tz cha kutengeneza na kugawa barakoa bure kwa wale wenye uhitaji. Nia yake kubwa ilikuwa ni kutengeneza barakoa nyingi na kuzigawa bure kwenye vituo vya polisi vilivyo karibu na nyumbani kwao bure kabisa.

Baada ya wiki moja, uhitaji wa barakoa uliongezeka maradufu na hivyo akaona umuhimu wake ukiongezeka. Kwa sababu hiyo, ilimlazimu kuomba uzaidizi kwa marafiki na ndugu zake wa karibu ili kukabiliana na uhitaji wa barakoa.

Kwa sasa imekuwa ni wiki kadhaa tangu kuanzishwa kwa kikundi cha Barakoa Tz na tayari washatengeneza na kugawa zaidi ya barakoa 1,000 kwenye vituo vya mayatima, wahudumu wa afya, polisi lakini zaidi kwa wale wenye uhitaji. Hii imefanikiwa kutokana na kutumia muda mrefu kwenye kushona barakoa kutoka kwa wasamaria wema pamoja na wafadhili.

Rania kwa sasa anao wasamaria wema pamoja. Kuna baadhi ya wasamaria ambao wanashona barakoa mkoani Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam pamoja na kusambaza kote mtaani. Lakini pamoja na kuwa na wasamaria wema wengi hivyo, Rania anaomba wengine wajitokeze. Rania anasema ‘Hata kama huwezi kushona kwa haraka, hiyo haina shida ni sawa kwani barakoa moja inaweza kuokoa maisha ya watu wengi.’

 Linapokuja suala la aina  ya kitambaa cha kushona, Rania anasema yeye hupata aina zote tofauti za mifumo na atachukua kitambaa cha aina yoyote ambacho anaweza kupata. Jambo moja la kuhakikisha ni kwamba ni pamba. Kitambaa cha kunyoosha kinaruhusu chembe zaidi kupita katikati, ambayo sio kile unachotaka kwa ajili ya kufunika uso. Kwa sasa yeye anatengeneza barakoa nyingi kwa ajili ya watot na anatoa wito kwa wenye miundo zaidi ya kitambaa cha watoto au mifumo mingine washirikiane ili kuja na aina mbali mbali tofauti.

Jambo lingine Barakoa Tz wanatarajia kutoa ni vifaa vidogo ambapo familia zinaweza kujishonea barakoa zaowenyewe. Rania Nasser alisema ni jambo rahisi sana kuweka pamoja na atatoa vifaa hivyo na maelekezo kwa watu kote Dar es salaam.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 2,2020




















Share:

Monday 1 June 2020

Agricultural Technology Solutions Specialist Abt Associates,

Job Opportunity at Abt Associates, Agricultural Technology Solutions Specialist Agricultural Technology Solutions Specialist   Abt Associates, a global leader in research and implementing technical programs in the fields of economic growth, international health, social and environmental policy, and climate change, seeks highly qualified candidates for the anticipated USAID-funded Tanzania Horticulture Activity. Candidates should possess the following qualifications: A university… Read More »

The post Agricultural Technology Solutions Specialist Abt Associates, appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Director, Project Operations and Finance at Abt Associates,

Director, Project Operations and Finance   Abt Associates, a global leader in research and implementing technical programs in the fields of economic growth, international health, social and environmental policy, and climate change, seeks highly qualified candidates for the anticipated USAID-funded Tanzania Horticulture Activity. Candidates should possess the following qualifications: A university degree in agriculture, business administration, economics, communications, health… Read More »

The post Director, Project Operations and Finance at Abt Associates, appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Agricultural Policy Specialist at Abt Associates,

Agricultural Policy Specialist  Abt Associates, a global leader in research and implementing technical programs in the fields of economic growth, international health, social and environmental policy, and climate change, seeks highly qualified candidates for the anticipated USAID-funded Tanzania Horticulture Activity. Candidates should possess the following qualifications: A university degree in agriculture, business administration, economics, communications, health and behavioral… Read More »

The post Agricultural Policy Specialist at Abt Associates, appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waziri Mkuu: Mali Zote Za Wakulima Wa Mkonge Kurudishwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli itahakikisha mali zote za wakulima wa zao la mkonge nchini zinarudishwa mikononi mwao na hakuna mtu yeyote atakayeonewa.

“Tutarudisha mali zote za wakulima na ninawahakikishia hakuna mtu yoyote atakayeonewa, kama tulivyorudisha hizi mali za Bodi ya Mkonge Tanzania tutafanya hivyo hivyo kote bila kumuonea yeyote na kuanzia leo Bodi hii ya Mkonge imethibitishwa kuwa bodi kamili.”

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Juni 1, 2020) wakati akifungua jingo la Bodi ya Mkonge Tanzania zilizopo jijini Tanga. “Mkonge ni fedha Halmashauri wekeni vitalu mzalishe mbegu muwape wananchi bure. Kama unashamba kubwa hujaliendeleza, kulingana na muda uliowekwa, tutalichukua.”

Amesema Serikali imedhamiria kulirudisha zao hilo, hivyo ametoa wito kwa wananchi hususani wa mkoa wa Tanga wajipange katika kuyafufua mashamba yao na kuanzisha mapya na Serikali itawasaidia kuhakikisha mbegu bora na pembejeo zinapatikana.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa rai kwa wananchi katika kila mkoa wenye ardhi nzuri ambayo inastawi zao hilo waanzishe kilimo cha zao mkonge walime na Serikali itawasaidia bila kujali ni mtu mmoja mmoja, wakulima wa kati na wakubwa.

“Wakuu wa wilaya waondoeni Maafisa Kilimo waliopo Ofisini waende vijijini wakawasaidie wakulima namna nzuri ya kulima zao hili kwa faida, mkonge ni pesa, Serikali yenu itasimamia. Tunataka mkonge urudi kwenye nafasi yake. Endeleeni kuwahamasisha walime mkonge, tunataka kila tunapopita tuone mashamba ya mkonge.”

Ameiagiza Bodi ya Mkonge kufanya utambuzi wa mashamba na wayarudishe kwa watu walime. Pia mapori yote makubwa yaliyoko kwenye halmashauri ambayo hayatumiki nayo wayatambue na waishauri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili nao wamshauri Rais Dkt. Magufuli kwa ajili ya kugawiwa kwa wananchi waweze kulima.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu amesema amewahusisha wadau kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na kwamba Serikali imeweka utaratibu utakaowawezesha wakulima wanaotaka kuboresha mashamba yao waweze kukopa. “Nendeni Benki ya Kilimo mkachukue mikopo.”

“Zao la mkonge ni muhimu nchini kwani linawanufaisha wakulima wadogo, wa kati na wakubwa. Mkonge kwa Tanga ni uchumi kwa wananchi na ni mkombozi kwa sababu unawawezesha kupata riziki zao. Zao hili hapo katikati halikuwa na tija, zao hili lilikuwa linalimwa na mikoa zaidi ya 12 lakini sasa limeachwa kwenye mikoa minne tu.”

Waziri Mkuu amesema kwenye miaka ya 60 Tanzania ilikuwa inaongoza kwa uzalishaji wa mkonge duniani, ambapo ilikuwa inazalisha tani 235,000 huku mahitaji ya mkonge duniani yakiwa tani 550,000. “Tulikuwa tunazalisha zaidu ya nusu ya mahitaji ya dunia, leo hii mchango wake haupo ukiuliza kwa nini hakuna sababu. Serikali imeagizwa na CCM kuwa ni lazima zao hili lirudi kwenye hadhi yake na litarudi.”

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu ameagiza mikoa yote inayolima zao la mkonge kuanzia sasa ijipange kwa sababu Serikali imeamua kulifufua zao hilo na inataka kulirudisha katika nafasi yake, hivyo viongozi wahakikishe wanaendelea kuwahamasisha wananchi walime kwa wingi.

“Tunataka mkonge ushamiri, Bodi tumieni vyombo vya habari kuhamaisha wananchi walime zao hili pamoja na kuwaeleza fursa zitokanazo na zao hilo. Wawekezaji wetu panueni mashamba, leteni mitambo ya kuchakata mkonge pamoja na vyote vitokanavyo na mkonge. Nampongeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga amefanya kazi kubwa katika hili.”

Naye, Naibu Waziri Kilimo, Omar Mgumba ametumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Mkuu kwa jitihada kubwa anazozifanya katika kusimamia sekta ya kilimo likiwemo zao la mkonge. “Uadilifu wako na uzalendo wako ulikufanya uunde kamati ya kuchunguza mali za Bodi ya Mkonge Tanzania na leo hii mali zao zimerudi.”

“Mheshimiwa Waziri Mkuu utaingizwa kwenye kumbukumbu za Tanzania kwa kujitoa kwako katika kuhakikisha zao hili linarudi kama ilivyokuwa awali. Tutafufuka katika mikoa yote ambayo imeonesha inaweza kulima zao hili la mkonge, lengo ni kuhakikisha zao hili linarudi kwenye hadhi yake.”

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amemshukuru Waziri Mkuu kwa kusimamia ajenda za maendeleo katika mkoa wa Tanga, hususani zao la mkonge.

“Tunashukuru uliporejesha hadhi ya zao hili.Tutawahimiza wananchi kulima mkonge kwani tunaona muelekeo na maono ni makubwa sana, Tanga tunajivunia jitihada hizi za maendeleo, uchumi wa Tanga utakuwa kwa kasi sana.”

Awali, Mbunge wa Lushoto Rashidi Shangazi alisema wanaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweza kuwarejeshea wananchi mashamba yao.

Nao, Wakuu wa Mikoa ya Pwani, Morogoro na Kilimanjaro waliishukuru Serikali kwa kulifufua zao hilo na kwamba wameshaweka mipango ya kuendeleza zao hilo na wameiomba Wizara ya Kilimo ishirikiane nao kwa kuwasaidia wakulima katika kuendeleza zao hilo, ikiwemo uandaaji wa mashamba, uendelezaji pamoja na utafutaji wa masoko. “Wizara ya Kilimo na Wizara ya Ardhi zitusaidie kutenga maeneo makubwa ya ardhi kwa ajili ya uzalishaji.”

MWISHO
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU  


Share:

Askofu Msonganzila: Tuendelee kumwombea Rais Magufuli

Na Anitha Jonas – WHUSM,Shirati
Watanzania tuendelea kumwombea Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ili aendelee kukua na kuongezeka imani na busara.

Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki Musoma ametoa wito huo hivi karibuni katika ibada maalum ya kumshukuru mungu  iliyofanyika katika Parokia ya Shirati kwa ajili ya kumshukuru mungu kwa kulisaidia taifa dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona tofauti na ilivyotabiriwa na mataifa ya nje nah ii ni kufutia maono Mheshimiwa Rais yaliyosaidia taifa kukabiliana na janga la maambukizi ya Virusi vya Corona.

“Kwanini tung’ang’ane kupata taarifa za idadi za  vifo, taarifa hizi hazisaidii sana bali  zinaongeza hofu tu na pia hata  taarifa za kweli zinapotolewa baadhi ya watu wanabeza kwa Musoma hii mpaka sasa tunakifo kimoja tu cha mgonjwa wa Corona hakuna taarifa zinazofichwa Kanisa Katolikili lina mfumo wa kupata taarifa kuanzia ngazi ya familia na tunafuatilia ” alisema Askofu Msonganzila.

Pamoja na hayo askofu huyo alieleza kuwa anafahamu katika kumshukuru mungu makundi mbalimbali ya imani tofauti yalifanya maombi yao na katika Wilaya ya Shirati
anafahamu kuwa wapo wazee wa kijadi katika eneo hilo nao walifanya tambiko.

Halikadhalika nae askofu huyo aliendeleea  kusisitiza kuwa pamoja na idadi ya maambukizi kupungua lakini ni vyema wananchi wanaendelea kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya wa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kuvaa barakoa na kuepuka msongamano.

Kwa upande wa Chifu wa Rorya Ngoje Ogati alisema kuwa tangu janga hilo la virusi vya Corona lilipotangazwa wazee wa eneo hilo kutoka koo mbalimbali walifanya tambiko la kuzuia ugonjwa huo usifike katika eneo lao na mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja katika eneo hilo amepata virusi hivyo.

“Katika ibada yetu ya tambiko tuliyofanya hivi karibuni nilakuzuia maambukizi ya virusi vya Corona katika nchi yote kwa ujumla pamoja na kushukuru kwa eneo la Rorya kutokupata maambukizi kabisa “alisema Chifu Ogati.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu alishukuru uongozi wa Wilaya ya Rorya kwa kuruhusu makundi yote ya kiimani ikiwemo la wazee wa jadi kufanya ibada ya kushukuru na kuliombea taifa.

Halikadhalika nae mmoja wa wakazi wa Wilaya ya Rorya kutoka Kijiji cha Buturi Bi. Hudo Odemba alisema katika eneo lao hawajawahi kupata maambukizi ya virusi vya Corona na anaamini kuwa matambiko yaliyofanywa na wazee wa eneo hilo yamesaidia kuwakinga pamoja na taadhari wanazochukua za kunawa mikono kwa maji tiririka kila mara.


Share:

5 New Temporary Jobs TANGA at Projekt Inspire Tanzania,

Overview Projekt Inspire are a company in Tanzania that aims at creating career awareness and lightening career paths for youth. We use our extensive knowledge to unleash youth and children potential by helping them to make informed career decisions that will align with the changes in the job market. We involve them by providing career consultancy with main… Read More »

The post 5 New Temporary Jobs TANGA at Projekt Inspire Tanzania, appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger