Wednesday 30 March 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MARCH 30 2016


Share:

Tuesday 29 March 2016

Mpya Kuhusu Ajira za Walimu na Nyinginezo...Wenye Vyeti Zaidi ya Kimoja Kutopangiwa Kituo cha Kazi Serikalini.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

KUNA TAARIFA ZINAENEA KWA KASI MITANDAONI KUHUSU SERIKALI KUTO KUWAPOKEA WASOMI WENYE CHETI ZAIDI YA KIMOJA KATIKA AJIRA..UJUMBE WENYEWE UNAMUHUSISHA WAZIRI SIMBACHAWENE NA UKISOMEKA HIVI:-

Waziri Simbachawene ametoa tamko la serikali kuwa , Serikali ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania haiko tayari kuajiri wasomi wenye vyeti vya baraza la mitihani kuanzia vyeti viwili na kuendelea,watakaopata ajira yoyote ile ya moja kwa moja serikalini ni wasomi wenye cheti kimoja tu. Wale waliosoma kwa kuunga unga, mara kutafuta credit, mara kurudia mitihani watafute ajira kwa mashirika binafsi.Serikali inataka kuwaajiri wasomi wenye cheti kimoja tu waliosoma moja kwa moja. System hii itaanza kwenye ajira za walimu za mwaka huu 2016 zinazoenda kutangazwa mda si mrefu mwezi wa nne mwanzoni. Simbachawene ameyasema hayo akiwa na waandishi wa habari jijini Dar leo majira ya asubuhi ili kuwajuza watanzania kuwa ni tamko la serikali.
Rai kwa wenye vyeti vingi, mtakua mnaomba ajira kivyenu serikalini au kwa mashirika binafsi na si kuajiliwa moja kwa moja kutoka serikali kama ilivyokua awali.
Samahani kwa usumbufu uliojitokeza.
Imetolewa na Afsa mawasiliano, wa Tamisemi.

Ndg.Elnest kimash
Dar es salaam.
Share:

Rais Magufuli Akabidhiwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Rais John Magufuli, ambaye amejipa kazi ya “kutumbua majipu”, sasa anaweza kufanya kazi yake vizuri zaidi baada ya kukabidhiwa ripoti tano na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambazo anaweza kuzitumia kama kitendea kazi.

Tangu aingie Ikulu, Rais Magufuli na Serikali yake amekuwa akifanya kazi ya kuibua uozo kwenye taasisi za Serikali, kusimamisha na kutengua uteuzi wa watumishi wa umma wanaojihusisha na ufisadi na wakati fulani amekuwa akiitaja ripoti iliyopita ya CAG kuwa ndiyo iliyoanika uozo anaofanyia kazi.

Jana, “mtumbua majipu” huyo alikabidhiwa ripoti ya kwanza ya CAG tangu aapishwe kuwa Rais Novemba 5 mwaka jana na sasa ana kitendea kazi rasmi cha kufanyia kazi.

CAG Mussa Assad alimkabidhi Rais Magufuli taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ikiwa ni kwa mujibu wa Katiba inayomtaka akabidhi ripoti hizo kwa Rais kabla ya mwisho wa mwezi Machi.

Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, kaimu mkurugenzi wa mawasiliano – Ikulu, Rais Magufuli, ambaye aliwaomba wabunge kumpa ushirikiano katika kutekeleza kazi za wananchi wakati akizindua Bunge Novemba 20, atazikabidhi ripoti hizo kwenye chombo hicho ndani ya siku saba za mwanzo za Mkutano wa Tatu wa Bunge la Kumi na Moja utakaofanyika mjini Dodoma kuanzia Aprili 19.

“Rais Magufuli amempongeza CAG na timu yake kwa kuandaa taarifa hiyo na ametoa wito kwa chombo hicho kuendelea kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi. Ameahidi kuwa serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kazi zake,” inasema taarifa hiyo. 
Share:

Vigogo Wawili Maliasili Waliotoa Vibali vya Kusafirisha Tumbili Watiwa Mbaroni

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Kikosi kazi maalumu cha kuchunguza makosa makubwa ya kihalifu kimewatia mbaroni vigogo wawili wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wakihusishwa na utoaji wa kibali cha kusafirisha tumbili 61 kwenda nchini Albania.

Maofisa hao ni Mkurugenzi wa Idara ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Dk Charles Mulokozi na ofisa mfawidhi wa kituo cha uwindaji wa kitalii, utalii wa picha na Sites cha jijini Arusha, Nyangabo Musika.

Kikosi hicho kinaundwa na wachunguzi kutoka Polisi, Idara ya Uhamiaji, Usalama wa Taifa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kikosi cha kupambana na ujangili nchini na Takukuru.

Wakati Dk Mulokozi anakamatwa, tayari alikuwa amesimamishwa kazi kwa agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe kwa kutoa kibali wakati Serikali ilishazuia.

Vyanzo mbalimbali vimesema jana kuwa Dk Mulokozi alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana alisafirishwa chini ya ulinzi kwenda kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).

“Hivi tunavyozungumza, Dk Mulokozi yuko njiani anapelekwa Kia chini ya ulinzi mkali wa polisi.Nyangabo yeye tayari yuko mikononi mwa vyombo vya ulinzi na usalama pale Kia,” kilidokeza chanzo chetu cha uhakika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alipoulizwa jana hakukanusha wala kukiri kuwa na taarifa za kukamatwa vigogo hao, lakini alisema atakuwa na mamlaka ya kuliongelea wakiingia mkoani kwake.

“Bado sijapewa hizo taarifa, lakini hata kama ningezijua nisingeweza kuzungumzia tukio la kukamatwa kwao lililofanyika mkoa mwingine. Nikikabidhiwa ndiyo naweza kusema chochote,” alisema Kamanda huyo. 
Hata hivyo, Waziri Maghembe alithibitisha kukamatwa kwa vigogo hao, akisema katika tukio hilo yeyote aliyetia mkono wake lazima akamatwe na kushitakiwa.

“Ni kweli Dk Mulokozi amekamatwa na siyo yeye tu kuna ofisa mwingine pale ofisi yetu ya Arusha naye tumemkamata. Hatuna mchezo katika suala hili,” alisisitiza.

Profesa Maghembe alitumia fursa hiyo kusisitiza kuwa raia wa Uholanzi waliokamatwa na polisi hawakuwa na vibali halali vya kufanya biashara ya kusafirisha wanyama hai kwenda nje ya nchi kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Hawa Waholanzi walikuwa na tourist visa (waliingia kama watalii). Halafu Watanzania waelewe mtu hawezi kupata kibali cha kusafirisha mnyama hai kabla ya kumkamata, kuhesabiwa, akakaguliwa na kupata vibali stahiki,” alisisitiza.

Raia hao wa kigeni ambao ni ndugu wa familia moja, Artem Alik Vardanyian (52) ni mkurugenzi wa mgahawa huko Uholanzi na Eduard Alik Vardanyian (44), meneja wa hoteli huko huko Uholanzi.

Hata hivyo, vyanzo vingine vimedai  kuwa pamoja na kuwapo kwa vibali hivyo, lakini hapakuwapo na “release order” inayotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kama sheria inavyoelekeza.

Chanzo hicho kilidai wanyama hao walikuwa wasafirishwe kwa kutumia ndege ya mizigo ya kukodi ambayo ilitokea Afrika Kusini na ilikuwa iwapeleke wanyama hao Albania kupitia Nairobi nchini Kenya na Nigeria.

“Hao marubani wa hiyo ndege waliitwa pale Polisi (Kia), wakaandikisha maelezo yao kuwa walikuja kuchukua wanyama hao na wakaambiwa wao waondoke tu hakuna mnyama anaondoka,” alidokeza ofisa mmoja katika uwanja wa Kia.
Share:

Dk Shein amteua Balozi Seif Ali Idd Kuwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein amemteua Balozi Seif Ali Idd kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa visiwa hivyo.

Kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk Shein amemteua Balozi Idd ambaye alikuwa na wadhifa huo hata kipindi kilichopita.

Uteuzi wa Balozi Idd aliyezaliwa Februari 23, mwaka 1942, ulianza jana ikiwa ni siku nne tangu kuapishwa kwa Shein kuwa Rais wa Zanzibar.

Balozi Idd anakuwa mtu wa pili kuteuliwa na Dk Shein baada ya kuteuliwa kwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said mwishoni mwa wiki.

Dk Shein sasa atakuwa na wakati mgumu wa ama kumteua au kutomteua Makamu wa Kwanza wa Rais ili kukidhi matakwa ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwani hakuna chama cha upinzani kilichokidhi vigezo vya kushirikishwa katika kuunda Serikali.
Share:

Picha na WEMA SEPETU akiwa katika Instagram Party Mwanza

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Usiku wa tarehe 27, ulipambwa na Show ya Instagram Party kwa upande wa Mwanza 88.1, mastaa kadhaa wa Tanzania walikuwepo kunogesha Party kutoka Bongo movie Wema Sepetu, alikuwepo na kundi la Weusi liliwakilishwa na Joh Makini pamoja G nako.Party imefanyika Rock City Shopping mall Mwanza.





Share:

Mkurugenzi Asimamishwa Kazi Itilima, Posho Zafutwa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, John Aloyce amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kushindwa kuisimamia halmashuari hiyo na kusababisha kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara kati ya madiwani na watendaji.

Uamuzi huo umechukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani kilichofanyika jana mjini Langangabilili wilayani humo. 
Mbali na uamuzi huo, amefuta posho zote kwa wakuu wa idara na vitengo katika halmashauri zote zilizoko mkoani hapa wanaoingia katika vikao vya madiwani.

Vikao hivyo ni pamoja na Baraza na kamati za halmashauri kwa madai kuwa hazina tija yoyote, na kuelekeza fedha hizo zilizotengwa zifanye kazi nyingine za maendeleo kama vile utengenezaji wa madawati.

Alisema alipata malalamiko dhidi ya Mkurugenzi huyo kupitia wajumbe wa Kamati ya Fedha na Mipango wa halmashauri hiyo waliofika ofisini kwake, hivyo kuamua kuitisha kikao hicho cha dharura ili kuyasikiliza.
 Katika kikao hicho madiwani hao walisema serikali ilitoa Sh milioni 450 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika halmashauri hiyo lakini kazi hiyo haikufanyika, wanapohoji na kutoa uamuzi umekuwa haufanyi kazi.

“Wilaya yetu ni mpya na katika kuondoa tatizo la watumishi wa halmashauri hii kuishi mbali na makao makuu ya wilaya tuliamua kuanza ujenzi wa nyumba za watumishi na tukaletewa Sh milioni 450. Lakini kila tunapohoji matumizi ya fedha hizo hatupatiwi majibu na tunapomwagiza Mkurugenzi atuletee hakubaliani na maamuzi yetu,”alisema Kuzenza William (CCM), ambaye ni Diwani wa Kata ya Zagayu.

Walisema kuwa hata mapato ya ndani yanayopatikana hayafahamiki licha ya kuwepo kwa ushuru wa mazao mchanganyiko haulipwi na wafanyabiashara walio wengi, hivyo kusababisha shughuli nyingi za halmashauri kukwama na kuzua migogoro ya mara kati ya madiwani na ofisi ya Mkurugenzi.

“Mapato ya ndani hayafahamiki kabisa kuwa ni kiasi gani cha fedha kimepatikana, maana hatusomewi na inaonekana hata ushuru wa mazao mchanganyiko wafanyabiashara hawalipi hii timu ya mkurugenzi inayosimamia mapato sina imani nayo,” alisema Diwani Kata ya Lugulu, Robert Jongela. 
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Daud Nyalamu alisema madiwani wa halmashauri hiyo wanaonekana hawana uamuzi kwani waliagiza kuwa vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 320 vilivyokopwa na halmashauri hiyo kwa ajili ya ujenzi wa maabara 35 za shule za sekondari vifanye kazi, lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika na vingi vimeharibika.

“Tulikopa benki Sh milioni 320 kwa ajili ya ujenzi wa maabara 35 zilizoko katika halmashauri yetu, vifaa vimenunuliwa lakini hadi sasa vimesambazwa maeneo mbalimbali havijafanyiwa kazi. Vimeharibika kwani saruji imeganda na mbao zimepinda na hazifai kwa ujenzi. Hii inatokana na uzembe wa Mkurugenzi wetu na kila kukicha halmashauri inadaiwa hadi madiwani hatulipwi stahili zetu,” alisema.

Akizungumzia tuhuma dhidi yake, Aloyce alisema tangu ateuliwe kuwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo miezi sita iliyopita alikuta Sh milioni 126 zilizokuwa zimebaki katika ujenzi wa nyumba za watumishi.

“Mimi wakati nafika katika halmashauri hii nilikuta kati ya Sh milioni 450 za ujenzi wa nyumba za watumishi zilikuwa zimebaki Sh milioni 126, tulikaa na wakuu wa idara tukaamua tuzikope na kujenga ukumbi ukizingatia ya kuwa tulikuwa tunaelekea uchaguzi mkuu hivyo tungeshindwa mahali pa kukusanyia matokeo ya kura,” alisema.

Alisema licha ya tuhuma mbalimbali dhidi ya halmashauri hiyo, iliundwa tume kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuzichunguza lakini hadi sasa hawajawaletea majibu, hivyo kuomba iundwe tume huru kutoka nje ya mkoa ili kuweza kuzichunguza tuhuma zilizotajwa na madiwani dhidi yake na ikibainika yuko tayari kuachia ngazi.
Share:

Magazeti ya Leo Jumanne ya March 29 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY




















Share:

Rais Magufuli Amuapisha Mkuu Wa Mkoa Mpya Wa Songwe Mhe. Chiku Gallawa Ikulu Dar Es Salaam

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Luteni Mstaafu Chiku Gallawa kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshuhudia Luteni Mstaafu Chiku Gallawa akiweka sahihi katika hati ya kiapo mara baada ya kuapa kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisaini hati ya kiapo cha Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  mara baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi  Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  mara baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe Samia suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim  na  Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  mara baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016. Kulia ni mume wa mkuu huyo wa Mkoa Bw. Juma` Boma na kushoto ni bintiye.

PICHA NA IKULU
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger