Monday, 9 June 2025

TANZANIA YATANGAZA MATOKEO YA UTAFITI WA KITAIFA WA UKATILI DHIDI YA WATOTO NA VIJANA 2024, UKATILI WAPUNGUA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akitangaza matokeo ya Utafiti wa Kitaifa wa Ukatili Dhidi ya Watoto na Vijana wa mwaka 2024, Juni 9,2025 Jijini Dar es salaam - Picha na Kadama Malunde


* Serikali yaahidi kutumia matokeo hayo kupanga mikakati, mipango na programu mbalimbali kupambana na ukatili.

*Yasisitiza Takwimu za Ukatili ni nyenzo muhimu kwa mipango na mikakati ya ulinzi wa watoto na vijana.

*THPS yajivunia kuratibu Utafiti wa Kitaifa wa Ukatili dhidi ya Watoto na Vijana, yakazia ushirikiano na Serikali kuimarisha ulinzi wa mtoto.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

  Serikali ya Tanzania imetangaza matokeo ya Utafiti wa Kitaifa wa Ukatili Dhidi ya Watoto na Vijana wa mwaka 2024 (The 2024 Tanzania Violence Against Children and Youth Survey - VACS), ukionesha kupungua kwa viwango vya ukatili wa kingono, kimwili na kihisia kwa watoto wa kike na wa kiume ikilinganishwa na utafiti wa mwaka 2009.

Matokeo hayo yametangazwa leo, Juni 9, 2025 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, ambaye amesema utafiti huu ni wa pili kufanyika tangu mwaka 2009 na umefanywa kitaalamu kwa ushirikiano wa serikali na wadau wa maendeleo.

"Matokeo ya utafiti huu yanaonesha ukatili umeshuka kwa kiwango kikubwa. Kwa mfano, kwa watoto wa kike ukatili wa kingono umepungua kutoka asilimia 33 hadi 11, kimwili kutoka 76% hadi 24%, na kihisia kutoka 25% hadi 22%. Kwa watoto wa kiume, kingono umepungua kutoka 21% hadi 5%, kimwili kutoka 74% hadi 21%, na kihisia kutoka 31% hadi 16%", amefafanua.

 

Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akitangaza matokeo ya Utafiti wa Kitaifa wa Ukatili Dhidi ya Watoto na Vijana wa mwaka 2024

Dkt. Gwajima amesisitiza kuwa takwimu hizi zitasaidia serikali kufanya tathmini ya sera, sheria na programu za kisekta kupitia MTAKUWWA II (Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto), ili kuongeza ufanisi wa juhudi za ulinzi wa watoto na vijana.

“Matokeo haya yatawezesha serikali na wadau kuboresha mipango, mikakati na huduma za ulinzi wa watoto kwa kizazi cha sasa na kijacho,” ameongeza Waziri Gwajima.

Athari za ukatili – Hatari za muda mrefu

Waziri Gwajima amesisitiza kuwa ukatili dhidi ya watoto ni ukiukwaji wa haki za binadamu na huleta athari za muda mrefu za kiafya, zikiwemo matatizo ya afya ya akili, mawazo ya kujiua, matumizi ya dawa za kulevya, tabia hatarishi za ngono, maambukizi ya VVU, pamoja na kupungua kwa fursa za kimaendeleo kwa waathirika.

Amesema serikali itaongeza bajeti na rasilimali watu kuimarisha huduma kwa manusura wa ukatili na kuzuia ukatili kwa njia endelevu. 

Takwimu ni za Kitaifa na Zinaaminika

Kwa mujibu wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Amina Msengwa, utafiti huu umefanyika katika mikoa yote 31 ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa kutumia sampuli wakilishi ya kitaifa, hivyo takwimu zake ni sahihi na zinafaa kutumika kupanga mikakati ya kitaifa.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Amina Msengwa

“Huu ni utafiti wa kisayansi wenye viwango vya kimataifa. Takwimu hizi zitatumika kuboresha sera na afua za kitaifa za ulinzi wa mtoto,” amesema Dkt. Msengwa.

Ushiriki wa Wadau wa Kimataifa

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt. Redempta Mbatia, amesema kuwa THPS inajivunia kuratibu utafiti huu kwa weledi mkubwa kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) kupitia Kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (U.S. CDC), na kwa usimamizi mzuri wa Serikali ya Tanzania.

Dkt. Redempta Mbatia akizungumza na waandishi wa habari

“Utafiti huu umetupatia takwimu muhimu za kusaidia serikali kuongoza juhudi za kitaifa za ulinzi wa watoto na vijana kwa kushirikiana na wadau. THPS tumejidhatiti kuendelea kushirikiana na serikali na wadau katika kutekeleza afua hizi,” amesema Dkt. Redempta.

Ameeleza kuwa matokeo ya utafiti yanaonyesha maendeleo makubwa ya kitaifa katika kupambana na ukatili wa kingono, kimwili na kihisia, na kutoa mwongozo wa kisera na kimkakati kwa serikali na washirika wa maendeleo. 

Bi. Miranda Armstrong akizungumza na waandishi wa habari

Aidha, Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi wa Mtoto kutoka UNICEF, Bi. Miranda Armstrong, amesema shirika hilo limekuwa sehemu ya ufanikishaji wa utafiti huu kama sehemu ya wajibu wao wa kuwalinda watoto.

“Tunaamini kuwa takwimu hizi zitatumika kuimarisha sera, programu na huduma zinazolenga ustawi wa watoto wote nchini,” amesema Armstrong.


Utafiti wa Kitaifa wa Ukatili Dhidi ya Watoto na Vijana wa mwaka 2024 ulilenga kutoa takwimu muhimu za kusaidia serikali kuongoza juhudi za kitaifa za ulinzi wa mtoto. Utafiti uliongozwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum (WMJJWMM) Tanzania Bara na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WMJWW) Zanzibar, na kutekelezwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi-Zanzibar (OCGS), na kwa msaada wa kitaalamu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Watoto (UNICEF), Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS), na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Serikali ya Marekani (U.S CDC).


Utafiti huu ulifanyika kati ya mwezi Machi na Juni 2024 na uliwahoji watoto na vijana 11,414 wenye umri wa kati ya miaka 13 hadi 24 kutoka mikoa yote 31 ya Tanzania bara na Zanzibar. Utafiti huu ni wa pili wa kitaifa wa ukatili dhidi ya watoto kufanyika nchini Tanzania, utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2009 ambao ulionesha kuwepo kwa ukatili wa kingono,kimwili na kihisia miongoni mwa watoto na vijana.


Ripoti kamili ya utafiti wa ukatili dhidi ya watoto inatarajiwa kutolewa baadaye mwaka 2025. Serikali na washirika wake imejidhatiti kutafsiri takwimu hizi kwa vitendo ikihakikisha watoto na vijana kote Tanzania wanaishi bila ukatili na wafikie huduma za matunzo na usaidizi wanaostahili.


ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akitangaza matokeo ya Utafiti wa Kitaifa wa Ukatili Dhidi ya Watoto na Vijana wa mwaka 2024, Juni 9,2025 Jijini Dar es salaam - Picha na Kadama Malunde

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akitangaza matokeo ya Utafiti wa Kitaifa wa Ukatili Dhidi ya Watoto na Vijana wa mwaka 2024

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akitangaza matokeo ya Utafiti wa Kitaifa wa Ukatili Dhidi ya Watoto na Vijana wa mwaka 2024

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akitangaza matokeo ya Utafiti wa Kitaifa wa Ukatili Dhidi ya Watoto na Vijana wa mwaka 2024

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akitangaza matokeo ya Utafiti wa Kitaifa wa Ukatili Dhidi ya Watoto na Vijana wa mwaka 2024Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Amina Msengwa akielezea kuhusu utafiti huo

Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Amina Msengwa akielezea kuhusu utafiti huo

Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Amina Msengwa akielezea kuhusu utafiti huo

Share:

HERITAGE CAMP & LODGE YATOA AJIRA 100, YAPANUA MBAWA KUTANGAZA UTALII KIMATAIFA

 

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Heritage Camp & Lodge, Erick Mashauri akiongea na waandishi wa habari 

Na Woinde Shizza Arusha

Wamiliki wa kampuni za utalii nchini wameiomba serikali kuwasaidia katika kugharamia ushiriki wao kwenye maonyesho ya utalii ya kimataifa, ili kuwawezesha kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania na kukuza soko la sekta hiyo muhimu kiuchumi.

Wakizungumza katika maonyesho ya utalii ya KARIBU KILI FAIR yaliyofanyika jijini Arusha, baadhi ya wamiliki wa kampuni hizo walisema kuwa licha ya dhamira yao ya kutangaza nchi, changamoto ya gharama za usafiri na malazi imekuwa kikwazo kikubwa, hasa kwa kampuni ndogo na zinazochipukia.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Heritage Camp & Lodge, Erick Mashauri, alisema kuwa ni wakati muafaka kwa serikali kuingilia kati kwa kusaidia gharama kwa kampuni zinazotaka kushiriki kwenye maonyesho ya kimataifa, jambo ambalo litasaidia sio tu kukuza biashara zao bali pia kuitangaza Tanzania kwa ujumla wake.

"Kinachohitajika ni msaada wa serikali ili watu waweze kushiriki kwenye maonyesho, hususan kampuni changa ,Kwa mfano, tunapokuwa na maonyesho ya utalii Ujerumani, ndege zetu kama Air Tanzania ziweze kusaidia kuwasafirisha wajasiriamali wa utalii kwa gharama nafuu, kama inavyofanyika kwa wanamichezo na mashabiki," alisema Mashauri.

Aliongeza kuwa serikali inaweza pia kusaidia kwa kutoa nusu ya gharama za usafiri  hatua ambayo itawapa wamiliki wa kampuni fursa ya kushiriki katika maonyesho makubwa duniani na hivyo kuongeza watalii wanaoitembelea Tanzania.

Kwa upande mwingine, Mashauri alieleza kuwa kampuni yake ya Heritage Camp & Lodge imeajiri wafanyakazi zaidi ya 100, na ina mpango wa kuongeza ajira zaidi ya 150 kupitia mradi mpya wa hoteli ya nyota tano iitwayo Hakuna Matata Safari Lodge inayojengwa katika eneo la Serengeti.

"Mradi huu utakapokamilika si tu utaongeza ajira kwa Watanzania, bali pia utaongeza mapato ya serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali," alibainisha.

Katika juhudi za kuhamasisha utalii wa ndani, Mashauri alisema kampuni yake inatoa punguzo la asilimia 30 kwa watalii wazawa kulingana na msimu, ili kuwavutia zaidi Watanzania kutembelea vivutio vyao.

Aidha, aliwahimiza Watanzania kufika katika camp na lodge zao ambapo huduma bora zinapatikana, ikiwemo chakula kitolewacho bila mipaka kwa wateja waliolipia, huduma za vinywaji kama maji, maziwa na kahawa bila malipo, pamoja na mapishi bora yanayowafurahisha wateja wote.

"Huduma zetu ni za kiwango cha juu na tunatoa thamani halisi kwa pesa ya mteja Tunawaalika Watanzania waje wajionee wenyewe tofauti yetu," alisisitiza Mashauri.

Share:

TANESCO YAKABIDHI KIFAA CHA KUPIKIA KINACHOTUMIA UMEME MDOGO KWA AJILI YA KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI

Share:

Sunday, 8 June 2025

“WAKATI UNAPOHISI HOFU ZAIDI, NDIO WAKATI WA KUFANIKIWA” BABU HUYO ASIMULIA!



Yeye sio tu mzee anayengojea simu ya mwisho, hakuwa amekata tamaa, akiwa pale nyumbani, Babu yangu alitaka kutoa njia ya mwisho na muhimu katika maisha, ni ujumbe ambao alikuwa ameufikiria kwa muda mrefu.

Tulikusanyika huku tukitumaini kupata kila alichosema, kwanza, alituonya dhidi ya kuitikia kila aina jambo, alisema kufanya hivyo kutamaanisha kuwa tutakuwa tunafanya mambo kulingana na kile watu kinachotokea.

“Wakati unapohisi hofu zaidi, ndio wakati wa kufanikiwa, urahisi hautakufanya ukue, unajua kadiri unavyopinga mabadiliko, ndivyo unavyozidi kudumaa kimaisha na kiuchumi,” alisema Babu.

Alituonya dhidi ya kupuuza mila na maadili yetu na kukumbatia maisha ya kisasa tu ambayo yameletwa na nchi za magharibi, alisema mila zetu ni ukumbusho wa pale tulipotoka kwamba bila hizo mila tungepotea kabisa.

Pia alisisitiza juu ya umuhimu wa kuomba msaada kwa watu wengi ambao ni sahihi haswa wakati shida hiyo inahitaji akili zaidi ya moja kutatuliwaa.

Aliendelea kwa kusema kuwa wakati wa shida alikuwa na watu kadhaa ambao wangeweza kumpa ushauri na msaada ambao utamkwamua kutoka kwenye shida hiyo na mara zote alikuwa akifanikiwa.

Anasema alipotaka kupanua biashara yake na kujitosa katika ujenzi wa nyumba, alikwenda kutafuta huduma za mganga wa jadi maarufu kama Kiwanga Doctors ambao walimsaidia kupata fedha zake nyingi za kuikuza.

Babu alitabasamu huku akisimulia jinsi biashara yake ilivyokua ndani ya muda mfupi tu, ndipo akanunua kipande chake cha kwanza cha ardhi huko Upperhill Nairobi.

Anasema kwa msaada wa Kiwanga Doctors, himaya yake kibiashara ilikua kubwa sana, na sasaa anahitaji kukabidhi ufalme huo mikononi mwetu maana ndio vijana wenye nguvu kwa sasa lakini tusisahau kuwa karibu na Kiwanga kwani wanaweza kuongeza bahati katika kazi zetu.

“Ninajua jinsi hii inaweza kuonekana kuwa ngumu lakini ichukueni kutoka kwa mzee niliye na uzoefu. Ikiwa haifanyi kazi, kamwe nisingewaambia muwasiliane na Kiwanga Doctors, namewaambia hivyo kutokana najua wapi aliponitoa,” alisema Babu yetu.

Vilevile Kiwanga Doctors wana uzoefu wa miongo kadhaa ya kutibu kwa kutumia dawa kali za mitishamba kuponya magonjwa kama shinikizo la damu, kisukari, vidonda vya tumbo, kisonono, kaswende, TB, miguu kuvimba au kuwaka moto n.k.

Vilevile hushughulikia matatizo ya jumla kuanzia kushinda kesi za mahakama, kushinda bahati nasibu, ulinzi wa familia na mali na hutabiri kwa usahihi nyota.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio, uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +255 763 926 750 au tembelea tovuti yao, maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi.
Share:

CRJE YAKABIDHI MAJENGO MAWILI YA HOSTELI ZA WANAFUNZI KWA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI


"Wakati wa mradi wa ujenzi zaidi ya wafanyakazi na mafundi 200 wa kitanzania waliajiriwa na kampuni ya CRJE (East Africa) Limited katika kuimarisha ushirikiano kati ya China na Tanzania," Meneja mradi wa majengo hayo kutoka CRJE (East Africa) Limited Dai Yanwei alisema wakati wa hafla ya kukabidhi majengo hayo.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya ujenzi ya kutoka nchini China, ya CRJE (East Africa) Limited imekabidhi rasmi majengo mawili ya hosteli ya wanafunzi ambayo yamekamilika kwa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Kukamilika kwa majengo haya kunaashiria hatua kubwa katika maendeleo ya miundombinu inayoendelea katika taasisi hiyo. Hosteli hizo mbili ni sehemu ya mradi wa ujenzi ambao  umefadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya Mradi wa Ujuzi wa Afrika Mashariki wa Mabadiliko na Ushirikiano wa Kikanda (EASTRIP). Mpango huu unalenga kuimarisha mazingira ya kujifunzia na kuboresha vifaa vya malazi kwa wanafunzi.

Kukamilika kwa majengo hayo kunaonyesha ushirikiano mkubwa kati ya NIT, CRJE, na mradi wa EASTRIP, na kuinyesha dhamira ya pamoja ya kuendeleza miundombinu ya elimu kwenye eneo la ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mradi huo iliyofanyika katika Kampasi kuu ya NIT Mabibo, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, meneja mradi wa majengo hayo kutoka kampuni ya CRJE (East Africa) Limited Dai Yanwei alisema, "Tunamshukuru Mungu kwamba leo CRJE inakabidhi mradi wa ujenzi wa majengo haya mawili kwa mteja wetu (NIT) baada ya kufanya kazi mchana na usiku, ili kuhakikisha mradi huu unakamilika."

Dai Yanwei aliendelea kusema kuwa wakati wa mradi wa ujenzi wafanyakazi na mafundi wazawa zaidi ya 200 waliajiriwa na CRJE katika kuimarisha ushirikiano kati ya China na Tanzania.

Ujenzi wa majengo mawili ya hosteli za wanafunzi ulighalimu kiasi cha shilingi bilioni 10.8.

Majengo hayo mawili yatatumika kama hosteli za wanafunzi ili kukidhi uhaba wa huduma hiyo kwa Chuo cha NIT ambacho kwa sasa ina wanafunzi zaidi ya 16,000.

NIT ilitia saini mkataba wa mwaka mmoja wa ujenzi na Kampuni ya CRJE (East Africa) Ltd Novemba 2022 kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo mawili katika kampasi kuu ya Chuo hicho Mabibo, Dar es Salaam.

Hata hivyo, Yanwei alieleza kuwa mradi huo ulikabiliwa na ucheleweshwaji wa kukamilika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mwaka 2023 na 2024, ambayo ilileta changamoto kwenye kukamilika kwa 
muda muafaka.

Kwa upande wao, maofisa waandamizi kutoka Chuo cha NIT waliishukuru kampuni hiyo ya CRJE kwa kukamilisha mradi huo wa ujenzi.walithamini mradi wa ujenzi.

Kampuni ya CRJE imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 50 tangu ilipoanzishwa mwaka 1969 na baadhi ya miradi ambayo imeshatekeleza ni pampja na mradi wa Reli ya Uhuru-TAZARA na vile vile  imeshatunukiwa mara tatu kuwa mkandarasi bora wa kigeni nchini Tanzania na imepata tuzo ya kifahari ya Luban kwa ubora wa ujenzi.

Kampuni hii ina wafanyakazi zaidi ya 5,000 kote Afrika Mashariki na inaendelea kupanua biashara yake huku wakiendea kuimarisha uhusiano kati ya China na Tanzania.

Katika kipindi cha miongo mitano iliyopita, CRJE imeshajenga jumla ya mita za mraba milioni tatu za miradi mbalimbali ya kihandisi nchini Tanzania.

Miradi mimubwa ambayo imeshajenga ni pamoja na Daraja la Nyerere, Chumba Kipya cha Mijadala ya Bunge, Ukumbi wa Mikutano Dodoma, Chuo Kikuu cha Dodoma, Rita Tower, Uhuru Heights, na Mwalimu Nyerere Foundation Square.

Kampuni hiyo imeshaweka rekodi ya kuwa kampuni inayoongoza kwenye kasi ya ujenzi katika nchi za Afrika Mashariki, ambapo inakamilisha ujenzi wa ghorofa moja kwa muda wa siku sita tu.

Kampuni hiyo iliweza kusanifu na kujenga Kituo cha Mikutano cha Dodoma kwa muda wa miezi saba tu.

Pamoja na kufanya kazi nchini, CRJE (East Africa) hufanya kazi  katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Sudan Kusini, Zimbabwe, Zambia, Msumbiji, Ethiopia na Malaysia.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 8,2025

Magazeti

 



Share:

Saturday, 7 June 2025

WAHALIFU WATAKA KSH1.7 MILIONI ILI KUMRUDISHA MTOTO


Mama Sama kama ambavyo watu wengi humuita alishindwa kuzuia machozi yake kumtoka baada ya kubainika kuwa mwanawe Alen Kimani, hayupo, yaani ametoweka katika mazingira ya kutatanisha.

Alitoa taarifa polisi na kuweka msako wa masaa manne ambao haukuzaa matunda, karibia saa mbili usiku alipokea habari mbaya zaidi ikisema kuwa mwanawe alikuwa ametekwa nyara na wahalifu ambao walitaka Ksh1.7 milioni ili wamekuachia huru akiwa hai.

Moyo wake ulishtuka alipogundua kuwa hakuwa na pesa hizoo, mama huyo alikuwa akiishi peke yake huko Thogoto baada ya mumewe kurafiki kwa kulipuliwa ndani ya gari na wanamgambo wa Al-shabbaab huko Mandera ambako alikuwa afisa wa polisi.

Bado hajapokea aina yoyote ya fidia kutoka serikalini kwani mumewe alikufa akiwa kazini. Biashara yake ndogo huko Thogoto imekuwa ya kujikimu tu kimasha pamoja na mtoto wake huyo wa miaka minne.

Kila mara walikuwa wakimpigia simu na kumtaka kutuma fedha, alipoanza kuwasihi wamuachie mtoto wake asiye na hatia, mara moja walikata simu na kutuma jumbe za vitisho.

Huzuni yake iliongezeka ambapo kila mtu aliyewasiliana naye hakuwa na pesa za kumsaidia. Alikuwa peke yake alilia sana, macho yake yalikuwa yamevimba kwa kulia kwa muda mrefu.

Mawazo kwa kumpoteza mwanaye yalikuwa likimdhoofisha kila dakika, jirani yake Teresia Muthoni alimpikia wali lakini hakuweza kuula. Baada ya kijiko cha kwanza aliangua kilio kwa mara nyingine tena akikumbuka jinsi alivyokuwa akimlisha Alen wali wakati akiwa mdogo.

Teresia alipiga simu chache kutafuta msaada kwa niaba yake, rafiki yake mmoja alimshauri wawasiliane na wataalam wa mitishamba waliopo Magori, Kenya, Kiwanga Doctors ambao alisema wamesaidia watu wengi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Mara moja waliamua kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba +255 763 926 750 ambao ni waganga wenye weledi wa hali ya juu na wenye uwezo wa kipekee wa kuelewa matatizo ya kipekee ya mteja wao na kutoa suluhisho la kudumu.

Huuliza maswali machache kwa uchunguzi ambayo huwawezesha kutoa utambuzi sahihi, kisha hazikupita dakika nyingi wanakuja na majibu ya uhakika, ndivyo walivyofanya kwa Mama Alen ambaye haukupita muda mrefu alimpata mtoto wake.

Waliwasiliana na polisi ambao waliitikia kwa vitendo na kuwakuta majambazi hao wawili kwenye nyumba ndogo ya udongo nje kidogo ya mji wa Thogoto. Haraka haraka wakawavamia na kuwakamata kwa mahojiano zaidi na sasa wote wapo jela kwa matukio hilo.

Mama Alen alifurahi sana kumpata mtoto wake akiwa hai, naye Alen alionekana kufurahi kuungana na mama yake tena, na sasa wanaishi maisha mazuri ajabu.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio, uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +255 763 926 750 au tembelea tovuti yao, maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi.
Share:

TBS YASISITIZA UMUHIMU WA CHAKULA SALAMA


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wadau wa mnyororo wa thamani wa chakula kuanzia wakulima shambani, viwandani, wafanyabiashara hadi watumiaji wa mwisho kuhakikisha kuwa chakula kinachoingia sokoni ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Wito huo umetolewa leo Juni 6, 2025 jijini Dar es Salaam na Kaimu Meneja Uchanganuzi wa Hatari Zitokanazo na Chakula (TBS), Bi. Immakulatha Justin, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka ifikapo Juni 7.

Bi. Immakulata amesema suala la usalama wa chakula ni mtambuka, likihusisha hatua zote za uzalishaji hadi mlaji wa mwisho, hivyo linahitaji ufuatiliaji na uwajibikaji wa hali ya juu ili kuzuia athari zinazoweza kuzuilika.

“Kule shambani, wazalishaji hutumia pembejeo mbalimbali kama vile dawa za kuua wadudu. Ni muhimu dawa hizi zitumike kwa kufuata maelekezo ya wataalamu ili zisije kuathiri usalama wa chakula,” amesema Bi. Immakulata.

Aidha, amewahimiza walaji kuhakikisha wanachunguza chakula wanachonunua ili kubaini kama kuna viashiria vya uchafuzi kabla ya kukitumia, hatua itakayosaidia kuepuka athari za kiafya.

Kwa upande wa wafanyabiashara, amewaasa kuzingatia ubora na usalama wa chakula wanachouza badala ya kuangalia bei peke yake, pamoja na kuhifadhi chakula katika mazingira safi na salama.

Maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani mwaka huu yanafanyika kwa mara ya saba tangu kuanzishwa kwake mwaka 2019, na yanabeba kaulimbiu: "Chakula Salama: Sayansi Katika Vitendo"

Kaulimbiu hii inalenga kuhamasisha matumizi ya sayansi na mbinu bora kuhakikisha chakula kinachowafikia walaji ni salama.
Share:

Friday, 6 June 2025

Video Mpya : ROGETI - YOMBO

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger