Friday, 30 May 2025

TANZANIA NA JAPAN WATIA SAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA MPANGO WA PAMOJA WA UWEKEZAJI BIASHARA YA KABONI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan zimetia saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika mpango wa pamoja wa uwekezaji katika Biashara ya Kaboni utakaowezesha kampuni za nchi hizo mbili kuwekeza katika Biashara ya Kaboni nchini Tanzania.

Utiaji saini wa makubaliano hayo umefanyika Mei 28, 2025 Tokyo, Japan kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni na Serikali ya Japan ikiongozwa na Waziri wa Mazingira, Mhe. Asao Keiichiro (Kei).

Akizungumza mara baada ya utiaji saini huo, Waziri Masauni amesema Makubaliano ya Mashirikiano yaliyosainiwa yamekusudiwa kuimarisha uhusiano kati ya Japan na Tanzania kwa maendeleo endelevu na hatua za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Amesema ushirikano huu utaongeza fursa ya kupanua soko la Biashara ya Kaboni kutoka kwa wawekezaji wa Japan watakaowekeza katika miradi ya biashara ya Kaboni itakayoibuliwa nchini.

Waziri Masauni ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anawataka wataalamu kutoka nchi hizi mbili kufanya kazi haraka,kwa bidii, na kwa pamoja kwa manufaa ya nchi zote mbili ili kuhakikisha kuwa makubaliano hayo yanaenda katika hatua ya utekelezaji.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa “Tuko tayari kufanya kazi kwa ukaribu na wenzetu wa Japan ili kuhakikisha makubaliano haya yanatekelezwa kwa faida ya nchi zote mbili. Tayari Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeimarisha uwezo wa kitaasisi na kisheria katika usimamizi wa Biashara ya Kaboni ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais iliandaa kanuni za mwaka 2022 za kuratibu biashara ya Kaboni”.

Aidha, Mhandisi Mhandisi alibainisha kuwa katika Mfumo wa Kitaasisi, Serikali imeanzisha Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) kupitia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira iliyofanyiwa marekebisho ya 2025.

Hafla ya utiaji saini ilihudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja, na Watendaji kutoka Ofisi hiyo.
Share:

Thursday, 29 May 2025

NDOA YANGU ILIKARIBIA KUVUNJIKA, HIVI NDIVYO NILIVYOIOKOA!


Jina langu ni Anna, na miezi michache iliyopita, mimi na mume wangu tulikaribia kutengana. Iliniogopesha sana kwa sababu nilimpenda sana. Tulikuwa pamoja kwa miaka 15, hivyo tulikuwa tumejenga maisha pamoja na kujaliwa watoto wawili.

Siku moja alirudi nyumbani na akatangaza kuwa anaondoka. Alisema hanipendi tena, hivyo anataka kunipa talaka. Nilivunjika moyo. Sikuamini kuwa ndoa yetu inaenda kuvunjika kwa urahisi kiasi hicho.

Nilimpigia simu mama yangu na kumueleza jambo hilo. Mama alinishauri niwasiliane na Kiwanga Doctors ambao walikuwa wamemsaidia katika hali kama hiyo kipindi cha nyuma.

Alisema wanaweza kukomesha talaka mara moja. Nilipata namba zao na kuwapigia mara moja ikiwa ni baada ya mume wangu kuondoka.

Siku iliyofuata, nilifika kwa Kiwanga Doctors huko Migori, Kenya, huko punde tu walifanya uchawi wa kuokoa ndoa yangu na mwingine wa kurudisha penzi la mume wangu kwangu kama ilivyokuwa hapo awali kipindi ambacho tunaoana.

Kusema kweli nilihisi kama miujiza maana jioni hiyo tu, mume wangu alirudi nyumbani, huku akiniomba msamaha mimi na watoto kwa kuwa mbali nasi bila kujali lolote kuhusu familia yake ambayo inamtegemea.

Usiku huo, tuliungana tena kwa njia ambayo hatukuwa nayo kwa muda mrefu. Sasa, mume wangu ananipenda zaidi kuliko hapo awali, na ninawashukuru sana Kiwanga Doctors kwa kuokoa ndoa yetu.

Ikiwa unapitia kitu kama hicho, ninakushauri kuwa fika au wasiliana na Kiwanga Doctors. Tiba zao zinafanya kazi haraka na wanaweza kukusaidia katika changamoto mbalimbali za kimaisha, kuanzia masuala ya uhusiano hadi matatizo ya kiafya.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio, uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +255 763 926 750 au tembelea tovuti yao, maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 29,2025





Magazeti
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger