Tuesday, 26 September 2023

TPDC YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA KUHUSU MRADI WA EACOP... DC SAMIZI ATAKA TAARIFA SAHIHI

   
 Na Sumai Salumu  & Kadama Malunde - Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi amewataka waandishi wa Habari kuandika habari sahihi na kutoa elimu sahihi kwa wananchi kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

Akizungumza leo Jumanne Septemba 26, 2023 wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) yaliyolenga kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa EACOP, Samizi amesema waandishi wa Habari wana jukumu kubwa la kutoa taarifa sahihi kwa wananchi ili kujua faida za mradi huo.

“Nitoe wito kwa waandishi wa Habari muandike taarifa na Habari sahihi kuhusu mradi,waweze kuufahamu mradi huu, tunaimani kabisa mtaenda kutoa taarifa sahihi kuhusu mradi. Nawasihi mtumie kalamu, kamera zenu vizuri kuhabarisha jami",amesema.

"Serikali inaendelea kutekeleza mradi huu mkubwa kwa manufaa ya Watanzania hivyo ni vyema Watanzania wakaufahamu mradi huu”, ameongeza Mhe. Samizi.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu amesema wananchi ambao maeneo yao yamepitiwa na mradi asilimia kubwa wamelipwa fidia ikiwemo kujengewa nyumba za kisasa, huku wakandarasi wazawa wakipata kazi katika mradi huo.

Amesema asilimia 80 ya mradi wa Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga inapatikana Nchini Tanzania,huku mikoa 8 ikiguswa na mradi huo ambayo ni Tanga,Shinyanga,Geita,Tabora,Singida,Kagera,Manyara na Dodoma.

Mratibu wa Mradi wa EACOP kitaifa, Asiadi Mrutu  amesema kuwa mradi huu utagharimu kiasi cha zaidi Dola za Kimarekani  Bilioni 5 na utatekelezwa kwa miezi 24 ( miaka 2) kwanzia Januari 2024 bomba hilo la kusafirisha  mafuta ghafi lenye urefu wa mita 18.

"Huu mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga nchini Tanzania una jumla ya wanahisa 4 Tanzania ikiwa itatoa mchango wa  fedha za mradi kwa 15%  na mdhabuni wa akiwa ni China Petroleum Pipeline Coperation (CCP) ambaye atajenga kwa luti tatu kwanza ni Uganda-Mtukula Km296, Mtukula-Singida Km614 pamoja na Singida -Tanga km533 ambapo kampuni yetu ndani ya mradi EACOP wanasimamia pia kufuatilia namna ya makampuni ya ndani yatakavyonufaika nahuduma yatakazotoa",amesema.

Afisa Uhusiano TPDC Francis Lupokela amesema TPDC inasimamia miradi mikuu minne(4) ikiwemo wa bomba la mafuta ambapo hivi sasa uko kwenye hatua za ujenzi wa makambi kwenye maeneo mbalimbali yakiwa na jumla ya 14.

"TPDC  inatekeleza mradi huu kwa 15% na unapita kwenye mikoa nane mradi huu una jumla ya kilometa 1443 kwa Tanzania na km1147 sawa na  80% kwa Uganda ni Km 296 Sawa 20% na mpaka Agosti 2023 tumetoa ajira za makundi matatu kwa watu zaidi ya 3619 ikiwemo wazawa wa maeneo husika",amesema Lupokela.

Nao waandishi wa habari  waliopata mafunzo hayo wamesema yamewasaidia kujua kuhusu maendeleo ya mradi huo na faida kwa jamii yote inayopitiwa na mradi pamoja na nchi kwa ujumla.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mafunzo yakiendelea
Mratibu wa Mradi wa EACOP kitaifa, Asiadi Mrutu akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Afisa Uhusiano TPDC, Francis Lupokela akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Afisa Uhusiano TPDC, Francis Lupokela  akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano EACOP, Catherine Mbatia  akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano EACOP, Catherine Mbatia  akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano EACOP, Catherine Mbatia  akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Afisa Habari EACOP, Abbas Abraham akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Afisa Habari EACOP, Abbas Abraham akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Afisa Habari EACOP, Abbas Abraham akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Afisa Habari EACOP, Abbas Abraham akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Afisa Fursa kwa Wazawa EACOP, Maryam Mandia akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Afisa Fursa kwa Wazawa EACOP, Maryam Mandia akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mratibu wa Mahusiano ya jamii EACOP Shinyanga, Cecilia Nzeganije akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mratibu wa Mahusiano ya jamii EACOP Shinyanga, Cecilia Nzeganije akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP


Share:

KWAYA YA MWENYEHERI MARIA THERESA LEOCHOWSKA KIWANJA CHA NDEGE DODOMA YAWAITA WATANZANIA TAMASHA LA UIMBAJI





Mwenyekiti wa kwaya ya Mwenyeheri Maria Theresa Leochowska, Dk.Paul Loisulie,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya zoezi la utoaji damu katika kuelekea kwenye uzinduzi tamasha la uimbaji wa nyimbo za Injili,Oktoba 22 Mwaka huu jijini Dodoma.


Na Alex Sonna-DODOMA


Kuelekea uzinduzi wa tamasha la uimbaji wa nyimbo za injili,Oktoba 22 mwaka huu,waumini wa Parokia ya Kiwanja cha Ndege wamechangia damu huku wakiwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo.


Akizungumza na Waandishi Habari wakati wa zoezi la utoaji wa damu, Mwenyekiti wa kwaya ya Mwenyeheri Maria Theresa Leochowska, Dk.Paul Loisulie, amesema katika kuadhimisha miaka 27 tangu kuzaliwa kwa kwaya hiyo watafanya tamasha kubwa ambalo watashiriki waimbaji mbalimbali.


Amesema kuelekea tamasha hilo kuna matukio ambayo wameyandaa kama shukrani ya kuwaweka pamoja hai na kumshukuru Mungu kwa miaka 27.


Amesema tukio mojawapo ni kujitolea damu kama sadaka hivyo wameshirikiana na Hospitali ya Benjamini Mkapa hasa waumini wa Parokia ya Kiwanja cha ndege kwa kutoa damu ambayo itaokoa maisha ya watanzania.


"Kitendo hichi ni kama shukrani kwa Mungu kwa kutuweka hai na tunapofikia kilele Oktoba 22 tuna amani kuna mambo tumefanya kwa sababu hawa watu wanaoimba ni binadamu hivyo ni lazima ili kushiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii,"amesema


Amesema malengo waliyoweka ni kuhamasisha watu wengi kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watanzania.


Amesema pia wameweka mikakati katika suala la mazingira na maadili kwa kutunga nyimbo ambazo zitazinduliwa siku ya kilele.


"Tunalenga kuna vitu vinaisumbua jamii ili sisi tuweze kuimba vizuri ni lazima watu wawe na afya waishi katika mazingira mazuri na wawe na maadili na tumeishaenda katika Gereza la Isanga kwa ajili ya kuwatembelea wafungwa,"amesema


Pia Mwenyekiti Loisulie ameitaka Jamii kuungana katika matendo ya huruma ikiwa ni pamoja na kutoa damu kwa watu wengine.


"Niwaombe tarehe 22 wahudhurue katika tamasha,wakishiriki watakuwa wameshiriki katika masuala ya mazingira na maadili na kutafakari maisha yetu bila kujali dini,wala kabila,tunawakaribisha sana.


"Tunaona namna ambayo mmonyoko wa maadili unaisumbua jamii na mengine mengi tunataka tuwe sehemu ya kupaza sauti kupitia uimbaji,"amesema


Amesema mgeni rasmi siku ya kilele anatarajiwa kuwa Mkuu wa Majeshi Mstaafu Generali Venance Mabeyo


Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Damu Salama, Hospitali ya Benjamin Mkapa, Kucy Kibaja, amesema wakati zoezi hilo likiendelea wamepata chupa za damu 66.

Ametoa rai kwa watanzania wengine kuiga mfano huo uliofanywa na waumini hao.


"Nenda kachangie chupa moja ambayo inaokoa maisha ya kuanzia watu wawili mpaka watatu.Nawaomba watanzania tembeleeeni vituo vya damu salama ili kujitolea damu ili iokoe maisha ya watanzania,"amesema


Naye, Mchangia damu,Rachel Mrema ameomba watanzania kujitokeza kujitolea damu kwani mahitaji ni makubwa kwenye jamii.


"Kuchangia damu ni jambo zuri na tunapaswa kuwa ni utaratibu wa kawaida kwetu,"amesema Rachel




WANAKWAYA wa Mwenyeheri Maria Theresa Leochowska,Parokia ya Kiwanja cha Ndege wakichangia damu kuelekea kuadhimisha miaka 27 tangu kuzaliwa kwa kwaya hiyo watafanya tamasha kubwa ambalo watashiriki waimbaji mbalimbali Oktoba 22 jijini Dodoma.
Share:

NSSF FUNGA KAZI, MKURUGENZI MKUU ABAINISHA MAFANIKIO LULUKI

*Mkurugenzi Mkuu abainisha mafanikio lukuki, asema yamechangiwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

*TEF yakoshwa na utendaji wa NSSF yapongeza kazi kubwa inayofanywa

Na MWANDISHI WETU


Ni funga kazi pengine unaweza kusema hivyo! Baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba kubainisha mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Mfuko katika kipindi cha Machi 2021 hadi kufikia tarehe 30 Juni 2023.


Mshomba amesema hayo tarehe 25 Septemba, 2023 jijini Dar es Salaam, wakati akitoa wasilisho la utekelezaji wa majukumu ya NSSF kati ya Machi 2021 hadi Juni 2023 kwenye kikao kazi baina ya Mfuko, wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).


Amesema NSSF imefanikiwa kuandikisha wanachama wapya 547,882, kati ya tarehe 1 Machi 2021 na 30 Juni 2023 na kwamba idadi ya wanachama wachangiaji iliongezeka kwa asilimia 36 kutoka 874,082 tarehe 1 Machi 2021 hadi kufikia wanachama 1,189,222 tarehe 30 Juni 2023.


“Siri ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja na mkakati wa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sera nzuri za kuvutia wawekezaji, pamoja na utekelezaji wa mpango wa Mfuko katika uandikishaji wanachama na matumizi ya TEHAMA,” amesema.

Kuhusu makusanyo ya michango amesema katika mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2023, kwa mwezi yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 97.67 iliyofikiwa tarehe 1 Machi 2021 hadi kufikia TZS bilioni 143.05 kwa mwezi katika mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2023.


Hata hivyo, amesema makusanyo ya michango kwa mwaka yameongezeka kwa asilimia 43 hadi kufikia shilingi bilioni 1,718.28 katika mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2023 ukilinganisha na shilingi bilioni 1,201.05 zilizokusanywa katika mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2021.


Amesema uwekezaji wa Mfuko pia uliongezeka kwa asilimia 111 kutoka shilingi bilioni 3,395.46 tarehe 1 Machi 2021 hadi kufikia shilingi bilioni 7,153.23 tarehe 30 Juni 2023. Kati ya mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2021 na mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2023, thamani ya vitega uchumi vya Mfuko imekua kwa asilimia 55 hadi kufikia shilingi bilioni 7,153.23 tarehe 30 Juni 2023 kutoka shilingi bilioni zilizokuwa tarehe 30 Juni 2021.


Mshomba amesema katika mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2023, NSSF ilitumia wastani wa shilingi bilioni 61.93 kwa mwezi kulipa mafao mbalimbali kwa wanachama na wategemezi ikiwa ni ongezeko la asilimia 22 ukilinganisha na wastani wa shilingi bilioni 50.58 kwa kipindi kilichoishia tarehe 1 Machi 2021.


Aidha, kati ya mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2021 na mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2023 malipo ya mafao yaliyolipwa kwa wastaafu, wanachama na wanufaika wengine yaliongezeka kwa asilimia 25 na kufikia shilingi bilioni 743.17 katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2023 ukilinganisha na bilioni 594.33 zilizolipwa Juni 30, 2021.

Kuhusu Mpango wa Taifa wa Sekta isiyo Rasmi (NISS), Mshomba amesema Mfuko umefanya mapitio ya Mpango wa utoaji wa huduma za Hifadhi ya Jamii katika sekta isiyo rasmi (NISS).

Naye, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deusdatus Balile amepongeza mafanikio mbalimbali ya NSSF yakiwemo ya ongezeko la michango, ongezeko la wanachama wachangiaji, ongezeko la mapato pamoja na ulipaji wa mafao.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, akizungumza katika kikao kazi kilichoratibiwa kati ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika kipindi kilichoanza tarehe 1 Machi 2021 hadi Juni 30, 2023 ambapo amesema NSSF imepata mafanikio kwa upande wa uandikishaji wanachama, ukusanyaji michango, uwekezaji na kulipa mafao.

Kikao kazi hicho na wahariri wa vyombo vya habari kimefanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JINCC), Dar es Salaam, tarehe 25 Septemba 2023 chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Wakurugenzi kutoka Kurugenzi mbalimbali pamoja na baadhi ya Mameneja wa NSSF wakifuatilia kwa makini mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba (hayupo pichani) na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina. Mkutano huo umefanyika tarehe 25 Septemba 2023, katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JINCC), Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele akitoa neno la utangulizi katika mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ambao umefanyika tarehe 25 Septemba 2023, katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JINCC), Dar es Salaam.
Matukio katika picha wakati wa mkutano wa wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili Hazina.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 26,2023




















Share:

Monday, 25 September 2023

MBUNGE MTATURU ALIPIGA JEKI KANISA




MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amechangia Sh Milioni tatu katika harambee ya ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ikungi huku akilipongeza Kanisa kwa kuendelea kuiombea amani nchi.

Kiasi hicho cha fedha ni kwa ajili ya ununuzi wa saruji mifuko 50,nondo za Sh Milioni moja,matofali 300 na gharama ya kumlipa fundi Sh 600,000 ambapo mbali na hayo ameahidi pia kutoa pikipiki moja ili kusaidia kwenye kazi ya utume kanisani hapo.

Akichangia harambee hiyo Septemba 24,2023,kanisani hapo,Mtaturu amesema serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inaleta fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Miradi hiyo ipo katika sekta ya afya,maji,umeme,elimu na barabara,miradi hii inaletewa fedha nyingi kwa ajili yetu hivyo ni jukumu letu kuendelea kumuombea Rais wetu na kuiunga mkono serikali yetu,”amesema.

Awali Paroko Padre Vincent Alute amemshukuru sana mbunge huyo kwa kwenda kushiriki nao ibada na kuwaunga mkono kwenye harambee ya ujenzi wa kanisa jipya uliofikia usawa wa madirisha.

“Sisi tumefarijika sana na ujio wako hii leo,lengo letu hapa ni kupata Sh Milioni 10 ili tukamilishe ujenzi huu,lakini kupitia mchango wako Mbunge wetu utaenda kutusogeza kwa kiasi kikubwa,tukuahidi kuwa tutaendelea kumuombea Rais wetu na serikali yake kwa ujumla ili iendelee kukidhi matamanio ya wananchi,”amesema.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger