Monday, 12 December 2022

RAFIKI - SDO WAKUTANISHA BARAZA LA WATOTO NGAZI YA HALMASHAURI KUWASILISHA CHANGAMOTO ZA WATOTO KWA WATOA MAAMUZI



Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga John Tesha, akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la watoto ngazi ya Halmashauri.


Meneja wa Mradi wa Uimarishaji wa Mabaraza ya watoto (MKUA) kutoka Shirika la Rafiki-SDO Tangi Clement, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la watoto ngazi ya Halmashauri na watoa maamuzi Manispaa ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA la Rafiki-SDO ambalo linajihusisha na utetezi wa haki za watoto, limekutanisha baraza la watoto ngazi ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, pamoja na watoa maamuzi wa Halmashauri hiyo, ili kuwasilisha changamoto zinazowakabili watoto na kufanyiwa kazi.
 
Kikao hicho kimefanyika leo Desemba 12, 2022 katika ukumbi wa Shypark Hotel, kwa kukutanisha watoto ambao ni Wenyeviti wa Mabaraza ya watoto ngazi ya Kata zote 17 za Manispaa ya Shinyanga, wakiwamo na walimu wao walezi wa Mabaraza hayo, pamoja na watoa maamuzi ambao ni Wakuu wa idara Manispaa ya Shinyanga.

Meneja wa Mradi wa Uimarishaji wa Mabaraza ya watoto (MKUA) kutoka Shirika la Rafiki-SDO Tangi Clement, amesema Shirika hilo limefanikiwa kuunda Mabaraza ya watoto katika Mitaa 28 na vijiji 17 vya manispaa ya Shinyanga, pamoja na madawati 77 ya watoto shule, ambapo shule za Msingi madwati 57 na Sekondari 20, lengo ni kuwaweza watoto waweze kupaza sauti kwenye masuala yote yanayohusu watoto vikiwamo vitendo vya ukatili.

Amesema baada ya kumaliza kuunda Mabaraza hayo ya watoto ngazi ya Mitaa na Vijiji, wakawajengea uwezo ili watoto watambue wajibu wao na haki zao, ndipo watoto hao wakaomba wakutane na watoa maamuzi wa Manispaa ya Shinyanga ili kuwaeleza changamoto ambazo watoto wanakumbana nazo na kutafutiwa ufumbuzi.

“Mabaraza haya ya watoto yana msaada mkubwa katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto, sababu watoto ni virahisi kuambiana wenyewe juu ya vitendo vya ukatili ambavyo wanafanyiwa,”amesema Tangi.

Nao viongozi hao wa Mabaraza ya watoto ngazi ya Kata, waliwasilisha changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili watoto katika maeneo yao, zikiwamo za ukosefu wa miundombinu rafiki shuleni, upungufu wa madawati katika shule za msingi na vifaa vya kujifunzia.

Changamoto zingine upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi shule za Sekondari, hakuna Maabara, vyumba maalum vya kujistili hedhi, huku wakiomba pia suala la ulaji chakula shuleni lizigatiwe kwa shule zote, kudhibiti majanga ya moto shuleni, pamoja na kushirikishwa kwenye uaandaji wa bajeti za Halmashauri na kuingizwa kwenye Kamati za Mtakuwwa na kupatiwa usafiri wa mabasi madogo kwenda shule.

Pia watoto waliomba Manispaa itenge Bajeti kwa ajili ya maadhimisho mbalimbali ya siku ya watoto.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga John Tesha, akizungumza kwenye mkutano huo, amelipongeza Shirika la Rafiki-SDO pamoja na wadau wengine kwa kuunda Mabaraza ya watoto na kuifanya Manispaa hiyo kuwa ya kwanza kukamilisha zoezi la uishwaji wa mabaraza ya watoto kutoka na muongozo mpya wa kitaifa.

Aidha, amewataka watoto wayatumie vyema Mabaraza hayo kupasa sauti juu ya vitendo vya ukatili ambavyo wanafanyiwa ili hatua za haraka zipate kuchukuliwa kabla ya kuleta madhara.

Amesema changamoto zote ambazo wameziwasilisha watoto hao, nyingine tayari zipo kwenye utekelezaji na nyingine zitafanyiwa kazi,likiwamo suala la usafiri kwa watoto, ambapo mwakani Halmashauri hiyo itatoa Hiace Sita za mikopo kwa vijana, lakini masharti yake ni kupeleka shule kwanza watoto na kuwafuata jioni kwa nauli ya Sh.200 hadi 300.

Pia akijibu maombi ya watoto kushirikishwa kwenye mchakato wa uundaji wa bajeti za Halmashauri, amesema kwa sasa Manispaa ipo kwenye uandaaji wa bajeti hivyo kwenye vikao vya kamati vya bajeti watashirikishwa watoto kupitia viongozi wao Mwenyekiti na Katibu.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga John Tesha, akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la watoto ngazi ya Halmashauri.

Afisa utumishi Manispaa ya Shinyanga Getruda Gisema akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la watoto.

Afisa Maendeleo ya Jamii Sifa Amon akizungumza kwenye kikao hicho.

Meneja wa Mradi wa Uimarishaji wa Mabaraza ya watoto (MKUA) kutoka Shirika la Rafiki-SDO Tangi Clement, akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la watoto ngazi ya Halmashauri na watoa maamuzi Manispaa ya Shinyanga.

Meneja wa Mradi wa Uimarishaji wa Mabaraza ya watoto (MKUA) kutoka Shirika la Rafiki-SDO Tangi Clement, akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la watoto ngazi ya Halmashauri na watoa maamuzi Manispaa ya Shinyanga.

Mdau wa watoto John Eddy akizungumza kwenye kikao hicho.

Wakuu wa Idara Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la watoto ngazi ya Halmashauri wakisikiliza uwasilishwaji wa kero za watoto na kuona namna ya kuzitafutia ufumbuzi.

Viongozi wa Mabaraza ya watoto wakiwasilisha kero za watoto kwenye kikao hicho.

Viongozi wa Mabaraza ya watoto wakiwasilisha kero za watoto kwenye kikao hicho.

Viongozi wa Mabaraza ya watoto wakiwasilisha kero za watoto kwenye kikao hicho.

Viongozi wa Mabaraza ya watoto wakiwasilisha kero za watoto kwenye kikao hicho.

Kikao cha viongozi wa baraza la watoto ngazi ya Halmashauri na watoa maamuzi kikiendelea.

Kikao cha viongozi wa baraza la watoto ngazi ya Halmashauri na watoa maamuzi kikiendelea.

Kikao cha viongozi wa baraza la watoto ngazi ya Halmashauri na watoa maamuzi kikiendelea.

Kikao cha viongozi wa baraza la watoto ngazi ya Halmashauri na watoa maamuzi kikiendelea.

Kikao cha viongozi wa baraza la watoto ngazi ya Halmashauri na watoa maamuzi kikiendelea.

Kikao cha viongozi wa baraza la watoto ngazi ya Halmashauri na watoa maamuzi kikiendelea.
Kikao cha viongozi wa baraza la watoto ngazi ya Halmashauri na watoa maamuzi kikiendelea.

Kikao cha viongozi wa baraza la watoto ngazi ya Halmashauri na watoa maamuzi kikiendelea.

Kikao cha viongozi wa baraza la watoto ngazi ya Halmashauri na watoa maamuzi kikiendelea.

Walimu ambao ni walezi wa Mabaraza ya watoto wakiwa kwenye kikao hicho.

Walimu ambao ni walezi wa Mabaraza ya watoto wakiwa kwenye kikao hicho.

Walimu ambao ni walezi wa Mabaraza ya watoto wakiwa kwenye kikao hicho.

Walimu ambao ni walezi wa Mabaraza ya watoto wakiwa kwenye kikao hicho.

Picha ya Pamoja ikipigwa.
Share:

ZAINA FOUNDATION YATWAA UBINGWA WA KUTUMIA BUNIFU KUTOKOMEZA UKATII WA KIJINSIA MTANDAONI





Balozi wa Switzerland nchini Tanzania, Didier Chassot akimkabidhi mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ijulikanayo kwa jina la ZAINA FOUNDATION bi Zaina Njovu zawadi ya ubingwa kwa kutumia ubunifu katika kutokomeza ukatili wa kijinsia mtandaoni kwa wanawake na wasichana.

Na Woinde Shizza - Arusha

TANZANIA ni nchi ya Afrika Mashariki yenye takribani watu milioni 61,hadi kufikia Aprili 2022 nchi hii ina jumla ya watumiaji wa intaneti milioni 30 nkati yao asilimia 18 wanawake.



Wanawake wengi nchini Tanzania hawatumii nafasi za mtandaoni kutokana na vurugu za mtandaoni kama vile uonevu wa kimtandaoni na kulipiza kisasi kuhusu ngono.



Hayo yamebainishwa katika kilele siku 16 za kupinga ukatili wa kimtandao hafla iliofanyika mapema mwezi Desemba mwaka huu katika Kituo cha kijamii cha Kardinali Rugambwa, Dar es salaam Tanzania ambapo washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya bara na visiwani walihudhuria.


Mwaka huu nchini Tanzania, WiLDAF na Muungano wa Ukatili wa Kijinsia (GBV) MKUKI kwa kushirikiana na UNFDP na washirika wa Maendeleo nchini Marekani kama vile Denmark, Finland, Uswisi na Balozi za Ireland nchini Tanzania Mashirika na washirika wa Maendeleo wameathimisha Siku 16 za kupinga ukatili kwa kuheshimu na kutambua harakati za wanawake.


Uongozi katika kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana waliamua kutoa tuzo ya Mabingwa wa ANT-OGBV


Zaituni Njovu ni mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiokuwa ya kiserikali ijulikanayo kwa jina la ZAINA FOUNDATION alikabidhi zawadi ya ubingwa kwa kutumia ubunifu katika kutokomeza ukatili wa kijinsia mtandaoni kwa wanawake na wasichana, tuzo ambayo ilitolewa na balozi wa Switzerland nchini Tanzania, Didier Chassot.



Zaituni alishinda tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kukomesha ukatili wa mtandaoni kwa wasichana na kuendeleza nafasi ya kiraia miongoni mwa wanaharakati vijana wa kike kutoka vyuo vikuu kutoka nchini Tanzania kupitia Mradi wa Digital Voice unaolenga kuongeza ushirikishwaji wa raia na uhamasishaji wa usalama wa kidijitali kwa vijana wa kike katika vyuo vikuu wenye umri wa kuanzia miaka 17 hadi 25.


Pia aliweza kuwa jengea uwezo kuhusu jinsi wanavyoweza kulindwa dhidi ya Ukatili wa kijinsia mtandaoni na unyanyasaji wa nje ya mtandao na kuboresha ushiriki wa wanawake katika nafasi za mtandaoni.


Aidha pia Zaituni imeteuliwa kuwa miongoni mwa mabingwa 16 wa mabadiliko ya Siku 16 za Uanaharakati kutoka kwa wateule zaidi ya 3600 walioshiriki katika tuzo hii.


Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia ni kampeni ya kila mwaka ya kimataifa ambayo inaanza tarehe 25 Novemba, Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake, na kilele chake huwa Desemba10, katika siku ya haki za binadamu.


Siku hii ilianzishwa na wanaharakati katika Taasisi ya Uongozi ya Kimataifa ya Wanawake mwaka wa 1991 na inaendelea kuratibiwa kila mwaka na Kituo cha Uongozi wa Kimataifa wa Wanawake.
Aidha pia siku hii inatumika kama mkakati wa kuandaa watu binafsi na mashirika kote ulimwenguni kutoa wito wa kuzuia na kukomesha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana.
*****

Zaituni ilitoa shukrani kwa kwa wafanyakazi wote wa Zaina Foundation , wafuasi na wadau wote wanaounga mkono kazi ya kukuza hali ya haki za kidijitali nchini Tanzania
Share:

DKT.MPANGO AUTAKA UONGOZI WA CHUO KIKUU HURIA KUKABILIANA NA WANAFUNZI WANAOFANYA UDANGANYIFU KATIKA UANDISHI WA TAFITI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Chuo Kikuu Huria cha Tanzania leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akitembelea mabanda ya maonesho ya tafiti zinazofanywa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Chuo hicho leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akitembelea mabanda ya maonesho ya tafiti zinazofanywa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Chuo hicho leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akitembelea mabanda ya maonesho ya tafiti zinazofanywa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Chuo hicho leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo ya matumizi ya Maabara ya Sayansi kutoka kwa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Profesa Elisaf Bisanda wakati alipotembelea na kukagua miundombinu ya Makao Makuu ya Chuo hicho yaliyopo Kinondoni Jijini Dar es salaam leo tarehe 12 Desemba 2022. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akizungumza na wageni waalikwa pamoja na watumishi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Chuo hicho leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango kufanya ziara chuoni Kikuu Huria cha Tanzania leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Pinda akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango kufanya ziara chuoni hapo leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Baraza(Bodi) ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Joseph Kuzilwa akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango kufanya ziara chuoni hapo leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam.Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Prof.Elifas Bisanda akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango kufanya ziara chuoni hapo leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam.Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Rasilimali Fedha na Mipango) Prof.George Oreku akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango kufanya ziara chuoni hapo leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania -Taaluma, Tafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof. Deus Ngaruko akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango kufanya ziara chuoni hapo leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikagua miundombinu ya Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria Tanzania kilichopo Kinondoni Jijini Dar es salaam leo tarehe 12 Desemba 2022.

Baadhi ya wageni waalikwa wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango baada ya kufanya ziara Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria Tanzania leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ameitaka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia hapa nchini kutoa kipaumbele cha juu zaidi katika kusaidia kukamilisha malipo ya majengo yanayotakiwa kununuliwa na Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliopo eneo la Biafra Kinondoni Jijini Dar es salaam ili Chuo hicho kiweze kuwa na miundombinu ya kutosha.

Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 12 Desemba 2022 wakati alipotembelea Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliopo Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Amesema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya chuo hicho ili kiweze kutoa elimu iliyo bora na hasa inayolenga kuwajengea wahitimu uwezo wa kujiajiri, kushindana katika soko la ajira, kuwa wabunifu na kushiriki katika fursa mbalimbali za kiuchumi.

Aidha ametoa wito kwa watafiti kujielekeza zaidi katika vipaumbele vya taifa ili kutatua changamoto mbalimbali.

Makamu wa Rais amesema ni muhimu kuendeleza jitihada za vijana walioanzisha ubunifu unaotatua changamoto ikiwemo wale wanaotumia taka katika hatua za kutengeneza chakula cha mifugo na Samaki, wanaotengeza nishati mbadala pamoja na bidhaa za lishe zinazovutia Watoto hapa nchini.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango ameutaka uongozi wa Chuo Kikuu Huria kukabiliana na wanafunzi wanaofanya udanganyifu katika uandishi wa tafiti zao ikiwemo kutumia watu wengine katika uandishi na kupata shahada mbalimbali.

Amesema hali hiyo imeendelea kushusha hadhi ya Chuo Kikuu Huria pamoja na athari kubwa zimeendelea kuonekana katika soko la ajira ambapo wahitimu wanashindwa kukidhi mahitaji ya soko hilo.

Ameongeza kwamba ili kufikia maendeleo ya haraka ni lazima kuwekeza kwenye ubora wa rasilimali watu ambao wanatokana elimu bora.

Awali akitembelea Mabanda ya maonesho katika Chuo hicho , Makamu wa Rais ametoa wito wa kwa vyuo hapa nchini kuzalisha wahitimu watakaoweza kuendana na sekta ya ajira ikiwemo mahitaji ya sekta binafsi.

Pia ameiagiza Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia kuhakikisha vitendea kazi kwa ajili ya elimu ya Tehama kwa watu wenye mahitaji Maalum vinapatikana ili kuwasaidia kuweza kujifunza kirahisi.

Aidha ameutaka uongozi wa chuo hicho kutangaza zaidi elimu inayotolewa katika chuo hicho ikiwemo Elimu adimu ya Anga na Nyota (Astronomy).

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolph Mkenda amesema Chuo Kikuu Huria kimeendelea kutoa fursa ya kuwafikia watanzania wengi katika maeneo walipo ili waweze kuongeza elimu yao kwa kupitia elimu ya Masafa.

Pia Prof. Mkenda amesema serikali imeendelea kutoa kipaumbele kwa elimu ya juu ikiwemo kuongeza kiwango cha mikopo kwa wanafunzi kutoka Bilioni 464 hadi kufikia bilioni 654. Aidha ameongeza kwamba wizara hiyo itasimamia utaoaji wa haki wa mikopo kwa kuzingatia zaidi wanafunzi wenye uhitaji mkubwa.

Vilevile Prof. Mkenda amemuhakikishia Makamu wa Rais Dkt Mpango kuwa ataendelea kusimamia utoaji wa mikopo bila kutetereka ili kuwe na uwazi na utoaji wa mikopo kwa haki.

Nae Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Pinda amesema walilazimika kufanya harambee ili kuweza kujenga kumbe kwaajili ya mitihani katika mikoa ya Manyara,Tabora na mikoa mingine.

Hata hivyo amemueleza Waziri wa Elimu kuwa waaangalie tafiti ambazo zimekuwa zikifanywa na Chuo hicho na kuzifanyia kazi Serikalini ili ziweze kuwa na ufumbuzi wa matatizo kutoka katika jamii yetu.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Prof.Elifas Bisanda ameiomba serikali kusaidia gharama za mtandao ambazo hufikia bilioni 1 kwa mwaka kutokana na utoaji wa elimu ya Masafa. Pia ametaja changamoto zinazokabili chuo hicho zikiwemo za ukosefu wa majengo katika baadhi ya mikoa hapa nchini unaohitaji shilingi bilioni 4.5 katika ujenzi wake pamoja na upungufu wa vifaa vya TEHAMA.

"Tunahitaji bilioni moja na milioni mia tisa kukamilisha ununuzi. Hili ni la dharura na haraka sana kwa sababu kuna matajiri wako tayari kulipa zaidi ya hapo, na kama si mahusiano mema kati yetu na wamiliki, eneo hilo lingeshaondoka". Amesema Prof.Bisanda.

Prof.Bisanda amesema wanahitaji makao makuu ya chuo yenye hadhi, hivyo wameshapatiwa eneo lenye hekari nne mkoani Dodoma huku wakikadiria kuwa kiasi cha bilioni 12 zitatosha kuweka majengo na vifaa vya msingi katika makao makuu ya chuo huko mkoani Dodoma.

Pamoja na hayo ameiomba serikali kuongeza umri wa kustaafu walimu wanataaluma wenye PhD hadi miaka 65, na miaka 70 kwa Maprofesa ambapo wengi wamestaafu wakiwa bado ni vijana, na kuendelea kufanya kazi katika vyuo binafsi huku wakiacha mapengo ambayo hayawezi kuzibwa katika vyuo vya umma.

Share:

BIBI HARUSI AZUA GUMZO KUVAA SHELA YA RANGI NYEUSI KWENYE HARUSI YAKE

Bibi harusi kutoka Nigeria kwa sasa anavuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha zake za harusi kusambaa mtandaoni.

Katika picha hizo, bibi harusi huyo aliyetambulika kwa jina la Dasplang Rinset Lisa, ameamua kubadilisha tamaduni ya kuvalia gauni jeupe kwenye harusi na kuvaa gauni jeusi na alionekana kupendeza ndani yake.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Lisa alifichua kwamba watu wengi walimuuliza maswali mengi kuhusu kwa nini aliamua kuvaa nguo nyeusi siku ya harusi yake.

“Nilipata maswali mengi kuhusu kwa nini nilichagua kuvaa gauni jeusi kwenye harusi yangu. Sawa nina majibu mengi ya maswali, hili nitaandika baadaye, lakini kwa sasa kuna mtu yeyote anaweza kuniambia kwa nini atapendelea gauni jeupe na kwa nini asipende rangi nyingine yoyote ya mavazi?” alimaka.
Share:

WANANCHI MWAMALA WATAKA WATUMISHI ZAHANATI YENYE WATUMISHI WAWILI...NYINGINE INA NESI TU

Share:

YUSUPH NASSOR AJITOSA KUWANIA NAFASI YA MWENYEKITI WA SIMBA SC

 

MKURUGENZI wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Yusuph Nassor amechukua Fomu ya Kuwania Nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Januari 29 Mwaka 2023 .


Kamati ya Uchaguzi wa Simba ilifungua mlango wa kuchukua fomu Desemba 5 kwa wagombea wenye nia ya  kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo ya Uenyekiti ambayo kwa Sasa  ipo chini ya Murtaza Magungu aliyeuchaguliwa kwenye uchaguzi mdogo baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Swedy Mkwabi kujiuzuru.


Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo Nassor  ambaye aliyewahi kuwa MKUU wa Kitengo Cha Fedha ,Utawala na Uendeshaji cha Klabu hiyo amesema ameamua kutumia nafasi yake hiyo ya kikatiba Ili kuingoza Klabu hiyo kongwe baada ya kuona ana kila sababu ya kuhakikisha  ana iletea maendeleo.


"Ninaifahamu vizuri Simba kwani mbali ya  kuwa kwanza nina mapenzi nayo kwa kipindi kirefu, pia nimefanya nayo kazi vizuri hadi wakati huu nilipoamua kuchukua fomu hii, malengo yangu ni kuiongoza na kuifikisha mbali zaidi kimafanikio" amesema Nassor


Amesema kupitia nafasi mbalimbali za uongozi anazozitumikia na alizowahi kuzitumikia kwa nyakati mbalimbali atahakikisha anaiongoza klabu hiyo na kuipa mafanikio makubwa katika mchezo wa mpira wa miguu ndani na nje ya nchi.


"Site tunatambua kuwa Simba imepata mafanikio makubwa , malengo yangu ni kuifikisha mbali zaidi kwa kushirikiana na viongozi wenzangu na hiyo ndiyo hasa sababu kuu iliyonifanya nijitokeze kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti" ameongeza Nassor


Simba wanafanya uchaguzi huo baada ya viongozi waliopo madaraka kuongoza kwa miaka minne kwa mujibu wa katiba ambapo nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti na wajumbe wanne pekee.


Kwa mujibu wa katiba yao, mwenyekiti atakayechaguliwa ana nafasi ya kuteua wajumbe wawili ambao wataingia kwenye Bodi ya Wakurugenzi wakitimiza idadi ya wajumbe saba kutoka upande wa klabu kuingia katika bodi hiyo.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 12,2022


Magazetini leo Jumatatu  December 12 2022









Share:

Sunday, 11 December 2022

MAKAHABA WAPELEKANA MAHAKAMANI WAKIGOMBANIA MTEJA 'MMOJA ALISHUSHA BEI, KACHAPWA MANGUMI BALAA"

Mnamo Ijumaa, Disemba 9,2022 kahaba alifikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kumpiga kitutu mwenzake, mbele ya Hakimu Mkuu wa Mombasa.

Mariam Issa Mohammed aliyefika mbele ya Hakimu Mkuu Vincent Adet alikiri shtaka la kumpiga na kumjeruhi mwenzake Anita Mtengo.

Mahakama iliacha kinywa wazi baada ya Mariam kusimulia peupe chanzo cha ugomvi hadi kupigana kwa mangumi na mateke. 

Alisema kuwa yeye ni kahaba na mwathiriwa ni mwenzake wanaofanya kazi hiyo katika Soko la Sega, eneo la Majengo Mombasa.

Kulingana na Mariam, walitofautiana na mwenzake baada ya kushusha bei ya huduma kutoka bei ya kawaida ya KSh 350 (sawa na takribani shilingi shilingi 6000 ya Tanzania) hadi KSh 150 sawa na shilingi 3000 ya Tanzania)  na hivyo basi kumharibia biashara.

 Tukio hilo lilifanyika mnamo Jumatano, Disemba 7, kwa mujibu wa maelezo ya kesi hiyo. Wawili hao walikatizwa mara kwa mara na hakimu wakati walipoanza kubishana na kurushina maneno machafu ambayo hawapaswi kutamka ndani ya kortini.

"Mheshimiwa ni kweli mimi ni kahaba. Biashara hii inanilipia kodi ya nyumba na karo ya shule ya watoto wangu. Uzuri wa biashara hii ni kwamba unapata pesa za haraka mkononi," Mariam alisema kwa ujasiri. 

Mtengo aliiomba mahakama kumshurutisha mshatkiwa alipe gharama zote za matibabu, baada ya kumpiga kitutu na kumjeruhi. "Nimeumia sana na mkono wangu umejeruhiwa. Ninataka nilipwe fidia ya KSh 40,000 niliyotumia kwa matibabu," Mtengo alisema.

Chanzo - Tuko News
Share:

WANAFUNZI WA SHULE ZA MSALALA WAPATIWA ELIMU YA KUJITAMBUA NA KUPINGA VITENDO YA UKATILI WA KIJINSIA KUPITIA PROGRAM YA BARRICK BULYANHULU

Katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mwaka huu, Barrick iliendesha program mbalimbali za kutoa elimu mashuleni dhidi ya vitendo hivyo ambapo mgodi wa Bulyanhulu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali umewezesha elimu hiyo kufikia shule za msingi na sekondari zilizopo katika vitongoji vinavyozunguka mgodi huo.
Wanafunzi wa shule za Bugarama,Buyage,Ibanza na Igwamanoni wamefikiwa na elimu ya kujitambua na kupinga vitendo vya Ukatili wa Kijinsia

Share:

KKKT DKMZV YAPATA ASKOFU WA PILI WA DAYOSISI HIYO

 

(Dkt. Yohana Ernest Nzelu, Askofu mteule wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria)

Na Isaac Masengwa - Masengwa Blog

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria limemchagua Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu kuwa Askofu wa pili wa Dayosisi hiyo baada ya kufanya uchaguzi katika mkutano mkuu wa Dayosisi uliofanyika Desemba 9-10, 2022 katika usharika wa Tumaini Bariadi mkoani Simiyu.

Uchaguzi huo ulisimamiwa na Mkuu wa Kanisa hilo Dkt. Fredrick Shoo ambapo kwa mujibu wa katiba ya KKKT DKMZV majina yaliyopendekezwa na kupelekwa mbele ya mkutano mkuu Kwa ajili ya nafasi hiyo yalikuwa majina ya wachungaji watatu,  Mchungaji Jackson Maganga, Mchungaji Dkt. Daniel Mono na Mchungaji Dkt. Yohana Ernest Nzelu.

Dkt. Yohana Ernest Nzelu alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 187 kati ya kura 244 za wajumbe wa mkutano mkuu wa Dayosisi hiyo walioshiriki mkutano huo. Nafasi ya pili ilienda kwa Mchungaji Daniel Mono aliyepata kura 31 huku Mchungaji Jackson Maganga akipata kura 26.

Askofu Mteule Mch. Dk. Yohana Ernest Nzelu ambaye alizaliwa tarehe 15 Novemba 1974 Kiomboi Mkoa wa singida ataanza kukalia kiti hicho kutoka kwa mtangulizi wake Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala, baada ya kusimikwa kuwa Askofu kwa ibada maalum ambayo kwa mujibu wa katiba inapaswa kuwa ndani ya miezi sita tangu kuchaguliwa kwake

Dkt. Yohana Ernest Nzelu kama mwalimu wa shule kwa taaluma anachukua kiti cha uongozi wa Dayosisi hiyo inayotimiza miaka 10 tangu kuzaliwa kwake tarehe 12/12/2012 saa 12:00 jioni kukiwa na matarajio makubwa ya kufuata nyayo za mtangulizi wake Dkt. Emmanuel Joseph Makala ambaye ameipa mafanikio makubwa dayosisi katika katika kipindi chake Cha miaka kumi Kwa kazi kazi za utume wa kuinjilisha katika Dayosisi iliyopo mikoa ya Shinyanga na Simiyu ambapo kuna kazi kubwa ya umisionari.

Dkt. Yohana Ernest Nzelu katika utumishi wake kwa mara ya kwanza alifanya kazi katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria akiwa kama mratibu wa Maendeleo ya Jamii na miradi mwaka 1999 na baadaye alibarikiwa kuwa Mchungaji mnamo Septemba 18, 2005 na alitumikia nafasi hiyo katika sharika mbalimbali zilizopo Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria na baadaye Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria

Pia mteule huyo akiwa mkuu wa Shule ya Sekondari Mwadui ametumika kama Mkuu wa majimbo mbalimbali ya Dayosisi hiyo kwa zaidi ya miaka 11.

Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi ya Kiomboi Hospital mwaka 1984 - 1990 na baadaye alijiunga na Shule ya Sekondari Minaki iliyopo katika mkoa wa Pwani.

Dkt. Yohana Ernest Nzelu kitaaluma ni mwalimu, Mchungaji na pia ni Doctor of Ministry in Theology aliyosoma kiomboi hospital , Tumaini university kituo Cha mwika, baadae Stefano Moshi memorial university Moshi.

Baadaye akajiunga na Chuo kikuu huria Cha Tanzania ambacho bado anasoma mpaka leo. Pia amesoma Masters na Doctorate ( shahada ya udaktari katika huduma) huko Forty Wayne Marekani

Hadi anachaguliwa kuwa Askofu Mteule Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu alikuwa ni msaidizi wa Askofu KKKT DAYOSISI KUSINI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA alipochaguliwa na mkutano mkuu wa Dayosisi hiyo mwaka 2020 akichukua nafasi hiyo baada ya mtangulizi wake Mchungaji Trafaina Assery Nkya kustaafu

Alifunga ndoa na Lilian Nzelu Desemba 19, 1999 na wamejaliwa kupata watoto watano, ambao ni Agness Nzelu, Doricas Nzelu, Elizabeth Nzelu, Noel Nzelu na Suzan Nzelu

Pia katika mkutano mkuu huo, waumini wa Kanisa hilo walimchagua Dkt. Daniel Mono kuwa Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi baada ya mtangulizi wake kuchukua nafasi ya uaskofu.

Masengwa Blog iliongea na baadhi ya waumini kupata kufahamu wamepokeaje kuchaguliwa kwake Askofu mteule Dkt. Yohana Ernest Nzelu. 
Ibrahim Lyanga kama msharika wa Dayosisi hiyo yeye binafsi amesema ameridhishwa na maamuzi ya mkutano mkuu kwani anamfahamu vyema Dkt. Yohana Ernest Nzelu.

"Mimi binafsi namfahamu Mchg Nzelu kama mtu ambaye ni mwaminifu, mtulivu na msikivu, ni mchg makini sana anayefanya kazi zake kwa kufuata utaratibu. Ana sikiliza vizuri maoni na changamoto za wengine ili kuwasaidia" Alisema Lyanga

"Kwa kipindi akiwa mkuu wa shule ya sekondari Mwadui na ameisaidia shule hata kuongeza ufaulu na idadi ya wanafunzi na miundombinu ya shule kuwa bora sana. Ameisaidia kukua na kuimarika kwa majimbo mbalimbali alioyaongoza likiwemo Jimbo la Shinyanga, Jimbo la kusini Kati, Jimbo la kusini Mashariki mhunze na Jimbo la Maswa ambayo hayo nilifanya naye kazi akiwa mkuu wangu wa Jimbo 2018 - 2020." Aliongeza Lyanga ambaye pia ni Katibu/Mtunza hazina wa Jimbo la Shinyanga la Dayosisi hiyo 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger