Saturday, 9 April 2022

CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TAWLA CHAFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA DAR


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Bi. Lulu Ng'wanakilala  akifungua mkutano Mkuu wa 32 wa Mwaka wa Chama hicho unaofanyika kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam ambapo wanasheria mbalimbali wananwake ambao ni wanachama wa chama hicho wanashiriki. Picha na John Bukuku
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) Bi. Tike Mwambipile akitoa maelezo kwenye mkutano huo kabla ya kumkaribisha Bi. Lulu Ng'wanakilala Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya (TAWLA) ili kuzungumza.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya (TAWLA) Bi. Lulu Ng'wanakilala  na Jaji Mstaafu Joaquine De- Melo wakiwa katika mkutano huo.
Dr. Hellen Kijo Bisimba akitoa mada katika mkutano huo unaofanyika kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam.
Jaji Mstaafu Joaquine De- Melo ambaye ni mwanachama wa (TAWLA) akitoa nasaha zake kwa wanachama katika mkutano huo.
Dr.  Gavin Kweka mwanasaikilojia akizungumza na wananchama wa (TAWLA) na kuwapa mada mbalimbali kuhusu msongo wa mawazo unavyoathiri watu wengi katika maisha.
Picha mbalimbali zikiwaonesha wanasheria wanawake ambao ni wanachama wa TAWLA wakifuatilia hoja mbalimbali katika mkutano huo.
Share:

RC AWAAGIZA WAKUU WA WILAYA KUANDAA MICHE MILIONI 1.5 KWA AJILI YA KUIPANDA KWA MWAKA


Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela, akiwahutubia wakazi wa Arusha, kwenye kilele cha siku ya upandaji miti mkoa wa Arusha, maadhimisho yaliyofanyika kwenye shule ya msingi Enaboishu Academy, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru.

Na Rose Jackson,Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa wa Arusha, kuweka mkakati kwa kushirikiana na wadau kuandaa miche milioni 1.5, kwa kila halmashauri kwa ajili ya kuipanda kwa mwaka, ili kufikia lengo la mkoa la kupanda miti milioni 10.5 kwa mwaka.

Mongela maetoa maelekezo hayo, kwenye maadhimisho ya kilele cha upandaji miti mkoa wa Arusha, yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Enaboishu Academy, halmasahuri ya Arusha na kuwataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuandaa mkakati wa kuoanda miti milioni 1.5 kwa kila halmashauri kwa mwaka.

"Mkakati wetu ni huu, kila halmashauri kupanda miti milioni moja 1.5 kwa mwaka, tunataka kila mdau, wadau wa mistu, watupe miche ya miti ili kufikia lengo la mkoa la kupanda miti milioni 10.5 ifikapo mwezi Aprili 2023", amesisitiza Mongela.

Aidha amezitaka taasisi zote za serikali, taasisi binafsi na zile za dini kuwawezesha watu wanaowahudumia, kuhakikisha kila watu wawili wanapanda mti mmoja sambamaba na kuuhudumia mti huo, kwa kipindi cha mwaka mzima na kuongeza kuwa, kila shule iwape jukumu kila wanafunzi wawili wapande mti mmoja, kila kanisa na msikiti waumini wawili wapande mti mmoja na kuutunza mpaka ukue.

"Tunafahamu miti ndio chanzo kikubwa cha maji, miti ni chanzo cha hewa safi, tumeshuhudia mabadiliko ya hali ya hewa, kwa sababbu ya uharibifu wa mazingira, tusifanye uzembe, watalamu na wadau tusidieni kubadilisha maeneo makame kwa kupanda miti ya kutosha, ili kuyafanya mazingira yetu yatutunze", ameweka wazi mkuu huyo wa mkoa.

Naye Mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, ameahidi kutekeleza agizo hilo la mkuu wa mkoa, kwa kushirikiana na wadau, kwa kuhakikisha wanafikia lengo la kupanda miti milioni 1.5, huku akiwataka wadau kuelekeza nguvu kuwekeza kwenye upandaji miti kwenye taasisi zote za Umma hususani kwenye shule zote za serikali na binafsi.

Kauli mbiu ni "Mti wangu, Taifa langu, Mazingira yangu, Kazi Iendelee".

Share:

JINSI YA KUSHIRIKI SHINYANGA MADINI MARATHON 2022

 

Share:

NIT MABINGWA BONANZA LA DIWANI WA MABIBO


TIMU ya Mpira wa Miguu ya Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT)imeibuka mabingwa katika Bonanza maalumu lililoandaliwa na Diwani wa Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam baada ya kuifunga timu ya Azimio kwa magoli 3-0.

Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Loyola, mbali na mchezo wa mpira wa miguu ambao ulizishirikisha jumla ya timu 11, lilikuwa na michezo mingine ikiwemo mpira wa pete kwa wanawake, kukimbia, kuvuta kamba pamoja kufukuza kuku.

Kutokana na ushindi huo, timu hiyo ya N.I.T ilizawadiwa kikombe, seti moja ya jezi pamoja na mpira mmoja huku timu ya Azimio ambayo ndiyo imeshika nafasi ya pili ikizawadiwa seti moja ya jezi na mpira mmoja.


Akizungumza wakati wa bonanza hilo lililohudhuriwa pia na uongozi wa taasisi ya 'African Youth Empowerment' (AYE) inayojisghulisha na utafutaji wa vijana wenye vipaji vya mpira, Diwani wa Kata ya Mabibo Joseph Klerruu alisema lengo lake ni kujenga umoja miongoni mwa wanajamii wa kata hiyo.

"Tumekutana hapa kwa nia moja ya kujenga ujamaa miongoni mwetu na kufahamiana, michezo ni undugu, urafiki hivyo naamini kupitia jumuiko hili la pamoja tunazidi kuukuza undugu wetu", alisema Klerruu


Alisema pamoja na hilo, kufanyika kwa bonanza hilo limesaidia kujenga umoja na mshikamano miongoni wananchi wa kata hiyo ya Mabibo na majirani zao huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kujiandaa na Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa wananchi kujitokeza na kushiriki katika sensa hiyo ili kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika jitihada anazozifanya kuliletea maendeleo Taifa hili.
Share:

Friday, 8 April 2022

CAMARTEC YAISHUKURU COSTECH KWA UTOAJI FEDHA ZA UBUNIFU TEKNOLOJIA



Mhandisi Kilimo kutoka kituo cha CAMARTEC Godrey Mwinama akionesha baadhi ya zana ambazo zinatengenezwa katika kituo hicho

Na Rose Jackson,Arusha

Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia vijijini CAMARTEC wameishukuru Tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia kwa kuwa wadau muhimu wa kuwapatia fedha za ubunifu na uendelezaji wa teknolojia vijijini.


Akizungumza na waandishi wa habari waliopatiwa mafunzo na COSTECH Mara baada ya kufika kwenye kituo hicho kwa lengo la kujifunza habari za matokeo ya sayansi na utafiti mhandisi kilimo kutoka CAMARTEC Godfrey Mwinama amesema kuwa COSTECH wamekuwa na mchango mkubwa katika kituo hicho.


Aliongeza kuwa kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imewezesha kuibua zaidi ya bunifu mia moja ambapo COSTECH imekuwa ikiwapatia fedha kwa ajili ya kuendeleza bunifu hizo.

"Kuna trekta ambalo linatengenezwa hapa CAMARTEC na fedha zake tumepewa na COSTECH hivyo tunakiri kuwa wamekuwa bega kwa bega na sisi kuhakikisha kuwa tunazalisha teknolojia ambazo zinaweza kuwafikia wananchi na wadau mbali mbali",alisisitiza Mwinama.


Naye Kaimu Meneja wa uzalishaji wa CAMARTEC Mhandisi Boniface Masawe amesema kuwa kituo hicho kimefanikiwa kubuni na kutengeneza jiko la mfumo jua ambalo Lina uwezo wa kutumika kipindi Cha kiangazi na hivyo kuweza kuokoa matumizi ya gesi na umeme.


Masawe amesema kuwa jiko hilo lina uwezo wa kufyonza mionzi ya jua na kukusanya sehemu moja kwa ajili ya kupika.

"Jiko hili ni rahisi kwenye maeneo ambayo yana jua la kutosha kwani linatumia mionzi ya jua ambapo pia Lina uwezo wa kudumu muda mrefu kwa kuwa sio la kuhamisha hamisha likishafungiwa sehemu moja halihamishwi tena",aliongeza Masawe.


Amesema kuwa jiko hilo ni rahisi na limekuwa likifanya vizuri kwa mikoa ya Singida na Dodoma na Lina uwezo wa kupika maharagwe kwa dakika 45 na hivyo kuweza kuokoa gharama nyingine za nishati ya gesi.

Share:

AKINA MAMA WASISITIZWA KUJIFUNGULIA KWENYE VITUO VYA AFYA BADALA YA NYUMBANI



Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa akiwa watoto waalioletwa Kliniki kwenye zahanati ya Imbibya kata ya Mwandet, kuonyesha hali ya upatikanaji huduma za afya kwenye maeneo ya vijijini.

Na Rose Jackson,Arusha

Jamii imetakiwa kuwahudumia kina mama wajawazito na watoto kwa kuhakikisha wanahudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito, sambamba na kuwapatia lishe bora, huku wakisisitizwa wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na sio nyumbani.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti halmashauri ya Arusha, na Diwani wa Kata ya Laroi, Mhe. Ojung'u Salekwa, alipotembelea zahanati ya Imbibya kata ya Mwandeti, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hali ya upatikanaji wa huduma za afya katika vituo vya afya vya halmashauri hiyo.

Mwenyekiti Ojung'u licha ya kuridhishwa na upatikanaji wa huduma za afya katika vituo vya afya vya serikali katika halmasahuri hiyo, lakini pia amebaini changamoto za baadhi ya akina mama wajawazito kutokuhudhuri kliniki, wengine kujifungulia nyumbani, kutokuzingatia lishe bora kwa siku 1000 za ujauzito huku baadhi ya kinamama kuacha kuwapekeka kliniki watoto wa kabla ya kutimiza umri wa miaka mitano.

"Tunapaswa kutambua kuwa, suala la ujauzito ni la familia na jamii nzima, hivyo ni vema wote kuzingatia kumlea mjazito kwa kuhakikisha anahudhuria Kliniki mara anapohisi ana ujauzito, kumpa lishe bora kwa siku 1000 za ujauzito pamoja na kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na si nyumbani, na baadaye kiwapeleka watoto kliniki mpaka watakapofikisha umri wa miaka mitano" ,amesisitiza Ojong'u.

Aidha Ojung'u amesisitiza kuwa serikali inaendelea kutekeleza mkakati wa kufikisha huduma za afya karibu na wananchi na zaidi imewekeza nguvu nyingi katika kuboresha miundombinu ya afya na kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeimarika, hivyo amewasisitiza wananchi kutumia huduma hizo kwa kuwa zinapatikana katika maeneo yao sasa.

Naye mama Yohana, aliyemleta mtoto wake kliniki, zahanati ya Imbibya, amesema kiwa kwa sasa jamii yao ya kimaasai imepata uelewa mkubwa wa kuhudhuria kliniki na kujifungulia hospitali jambo ambalo hapo awali halikiwepo kabisa.

"Kwa sasa akina mama wengi tunajifungulia hospitali, zahanati yetu ya Imbibya inatoa huduma zote za afya ya uzazi, tunapewa ushauri wa masuala ya lishe, kujikinga na magonjwa, niwashauri kina mama wajawazito wote wa Mwandeti, kuhudhuria kliniki, kujifungulia hospitali pamoja na kuwapeleka watoto klini mpaka watakapofikia miaka mitano, jambo ambalo linahakikishia afya ya mama na mtoto", amesisitiza mama Yohana.

Hata hivyo Mratibu wa Afya ya Uzazi, Muuguzi Bujiku Butolwa amewasisitiza wajawazito kuhudhuria klini na wenza wao, ili wote kwa pamoja wafahamu maendeleo ya afya ya mama na mtoto aliyeko tumboni, pamoja na kupata elimu na ushauri wa utunzaji na ukuaji wa mimba.

Pia mtatibu huyo, amefafanua umuhimu wa mama mjamzito kuhudhuria kliniki kwa wakati ni pamoja na kupata dawa muhimu za kuongeza damu, kuzuia minyoo na malaria, kupima vipimo muhimu, kama uuna tatizo litatuliwe mapema, vipimo hivyo Ni wingi na group la damu, kupata elimu ya Lishe wakati wote wa ujauzito.

"Ni jukumu la familia kumuwezesha mama mjamzito kuhudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito, kumuwahisha kituo cha afya pindi anapohisi uchungu wa kujifungua, ni hatari mjazito kujifungulia nyumbani anaweza kupoteza maisha yake na mtoto, ni vema familia nzima kumtunza na kumsaidia mama mjamzito kujifungulia hosoitali" ,amesisitiza Mratibu huyo wa Afya ya Uzazi.

Halmashauri ya Arusha ina jumla ya hospitali 2, vituo 7 vya afya na zahanati 49, huku kukiwa na huduma za mkoba 'mobile clinic', vituo hivyo vyote vinatoa huduma zote za afya na uzazi, kwa kina mama wajawazito na watoto.
Share:

SHINYANGA MADINI MARATHON KUFANYIKA AGOSTI 7,2022.... PJFCS YAKABIDHI JEZI KWA RC MJEMA

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon, Roland Mwalyambi (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema Jezi ya uhamasishaji wa Shinyanga Madini Marathon 2022.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mbio za Shinyanga Madini Marathon 2022 zilizoandaliwa na Klabu ya Mazoezi maarufu Police Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayolelewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga zinatarajiwa kufanyika Agosti 7,2022 Mjini Shinyanga.

Akizungumza leo Ijumaa Aprili 8,2022 wakati Kamati ya Maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon ilimpotembelea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kwa ajili ya kujitambulisha na Kukabidhi Jezi ya uhamasishaji pamoja andiko la mbio, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Roland Mwalyambi amesema maandalizi yanaendelea vizuri.

“Tumefika hapa katika Ofisi yako Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mama yetu Sophia Mjema kwa ajili ya kujitambulisha kwako na kuomba ridhaa ya kufanya Mbio za Marathon na kukabidhi Jezi ya uhamasishaji na andiko la mbio hizi”,amesema Mwalyambi.

Mwalyambi amesema maandalizi ya Mbio hizo yanaendelea vizuri na kwamba Mbio hizo zitafanyika Agosti 7,2022 wakati wa Kilele cha Maonesho ya Madini Mkoa wa Shinyanga.


“Tutakuwa na mbio za kilomita 21, 10, 5 na 2.5 kwa watoto pamoja na mbio za Baiskeli na michezo mbalimbali. Tunatarajia kuwa washiriki zaidi ya 1000 tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kushiriki katika mbio hizi”,amesema.

Katika hatua nyingine amesema PJFCS inashirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kutembelea Vivutio vya Utalii na Utamaduni na upandaji miti.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ameipongeza Klabu ya Mazoezi Police Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) kwa kuandaa Shinyanga Madini Marathon huku akiwashauri kushirikisha wadau kikamilifu mapema ili kufanikisha mbio hizo.

“Serikali ya Mkoa wa Shinyanga inaunga mkono Mbio hizi mlizoandaa. Tunataka Vibe! kweli kweli, hakikisheni mnajiandaa vizuri ili mbio hizi ziwe na tija. Hakikisheni mnashirikisha pia wasanii wa nyimbo za asili kwani wana wafuasi wengi ili mbio hizi ziwe za mfano..Ni matumaini yangu mtafanya vizuri”,amesema Mjema.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiangalia Jezi ya uhamasishaji wa Shinyanga Madini Marathon 2022. Kushoto Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon, Roland Mwalyambi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon, Roland Mwalyambi (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema Jezi ya uhamasishaji wa Shinyanga Madini Marathon 2022.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon, Roland Mwalyambi akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kuhusu Shinyanga Madini Marathon 2022.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon, Roland Mwalyambi (kulia) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kuhusu Shinyanga Madini Marathon 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akisoma andiko kuhusu Shinyanga Madini Marathon 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akisoma andiko kuhusu Shinyanga Madini Marathon 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza na waandaaji wa Shinyanga Madini Marathon 2022
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiwasisitiza waandaaji wa Shinyanga Madini Marathon 2022 kujiandaa kikamilifu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza na waandaaji wa Shinyanga Madini Marathon 2022. 

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

MWANZA KUANZA ZOEZI LA KUWAONDOA WATOTO MITAANI

Serikali mkoani Mwanza inatarajia kuanza zoezi la kuwaondoa watoto wanaoishi mitaani ambao wamekithiri hususani katika Jiji la Mwanza na kuhakikisha watoto hao wanarejea katika familia zao na kupata haki yao ya msingi ya kurejea shule.

Hayo yameelezwa Aprili 08, 2022 kwenye kikao kazi cha Kamati ya Kamati ya Kupambana na Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA) ngazi ya Mkoa Mwanza ambacho kimelenga kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya kuwaondoa watoto mitaani na kutokomeza utoro katika Shule za Msingi na Sekondari mkoani Mwanza.

Akifungua kikao hicho, Katibu Tawala Mkoa Mwanza Ngusa Samike ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ametaka uwepo mkakati wa kuwaelimisha wazazi na walezi ili wasiwe chanzo cha watoto wao kukimbilia mitaani.

Ameonya kuwa baada ya wazazi na walezi kupata elimu, watakaoshindwa kutoa ushirikiano ili kuhakikisha watoto wao hawakimbilii mitaani hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao hatua itakayosaidia kudhibiti wimbi la watoto kukimbia mitaani kiholela.

Samike amebainisha kuwa Serikali ya Rais Samia Sauluhu Hassan imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya sekta ya elimu ambapo katika kipindi cha miezi mitano iliyopita, Mkoa Mwanza umepokea shilingi bilioni 20.5 hivyo si vyema watoto kukosa haki ya kupata elimu na kukimbilia mitaani.

Naye Afisa Maendeleo Mkoa Mwanza, Isack Ndassa amesema zaidi ya asilimia 90 ya watoto walio mitaani wana umri wa kwenda shule lakini wanakosa haki hiyo ya kupata elimu kutokana na sababu mbalimbali ambazo zinazuilika.

Ameshauri viongozi wanaounda Kamati ya MTAKUWWA wakiwemo Polisi Kata, Watendaji wa Kata, Maafisa Elimu Kata, Maafisa Maendeleo Kata, Maafisa Ustawi wa Jamii Kata na viongozi wa dini kushiriki ipasavyo kwenye zoezi la kuwabaini watoto walioacha shule na kukimbilia mitaani ili kuwarejesha katika familia zao na kwamba zoezi hilo lisimamiwe kwa kuzingatia misiki ya haki za binadamu.

Naye Kaimu Afisa Elimu Mkoa Mwanza, Mwl. Maenda Chambuko amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Aprili mwaka huu 2022 kuna jumla ya wanafunzi watoro 19,133 katika Shule za Msingi na walipo Shule ni 913,335 huku kwa Shule za Sekondari wanafunzi watoro wakiwa ni 7,594 na walio Shule wakiwa ni 222,132. 

Amesema Serikali imeweka mifumo rafiki kwa wanafunzi ambao hawako shuleni kutokana na sabababu mbalombali ikiwemo mimba na utoro kurejea shuleni hivyo jitihada zifanyike ili kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya kwenda Shule.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally ameshauri mbinu rafiki kutumika wakati wa kutekeleza zoezi la kuwaondoa watoto mitaani pamoja na kutokomeza utoro mashuleni akishauri mbinu kama za utoaji uji ama chakula mashuleni kutumika ili kuhamisha watoto kupenda Shule.

Yassin ameshauri pia waalimu kuwa na mbinu rafiki kwa wanafunzi na kuacha tabia ya kuwashughulikia kwa adhabu kali kutokana na kukosa mahitaji ya shule ikiwemo sare ama viatu hatua itakayosaidia kupunguza utoro mashuleni. Pia ameshauri utaratibu wa kuwaondoa shuleni wanafunzi watoro ndani ya siku 90 kwani linakinzana na azma ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha wanafunzi kurejea shule.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza la Watoto Mkoa Mwanza, Glory Theonest amesema changamoto kubwa ambayo imekuwa ikisababisha utoro kwa wanafunzi hususani wa kike ni tabia ya baadhi ya waalimu kuwataka kingono na wanapokataa wanakuwa wanaadhibiwa vikali hata kwa makosa madogo na kuomba waalimu ambao pia ni walezi na wazazi kuwa marafiki wa wanafunzi na kuwasaidia kimasomo ili kufikia ndoto zao.

Kikao kazi hicho cha MTAKUWWA Mkoa Mwanza ni kikao cha kwanza katika kuweka mikakati ya kuwaondoa watoto wanaoishi mitaani na kutokomeza utoro mashuleni ambapo vikao zaidi vitafanyika ili kuja na mbinu zitakazosaidia zoezi hilo linalotarajiwa kuanza kati ya mwezi Mei ama Juzi mwaka huu 2022 kufanikiwa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Ngusa Samike (kushoto) akifungua kikao kazi cha Kamati ya MTAKUWWA Mkoa Mwanza kilicholenga kuweka mikakati ya kuwaondoa watoto wanaoishi mitaani pamoja na kutokomeza utoto kwa wanafunzi mashuleni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ni Katibu Tawala Mkoa Mwanza. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally na kulia ni Afisa Programu Mwandamizi wa Shirika hilo, Grace Mussa.
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Ngusa Samike akifungua kikao kazi cha Kamati ya MTAKUWWA Mkoa Mwanza kilicholenga kuweka mikakati ya kuwaondoa watoto wanaoishi mitaani pamoja na kutokomeza utoto kwa wanafunzi mashuleni.
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Ngusa Samike akifungua kikao kazi cha Kamati ya MTAKUWWA Mkoa Mwanza kilicholenga kuweka mikakati ya kuwaondoa watoto wanaoishi mitaani pamoja na kutokomeza utoto kwa wanafunzi mashuleni.
Afisa Maendeleo Mkoa Mwanza, Issack Ndassa (kushoto) akizungumza kwenye kikao kazi hicho cha MTAKUWWA Mkoa Mwanza kilicholenga kuweka mikakati ya kuwaondoa watoto wanaoishi mitaani pamoja na kutokomeza utoro mashuleni.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa Mwanza, Maenda Chambuko akiwasilisha takwimu za hali ya utoro katika Shule za Msingi na Sekondari mkoani Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto na Wanawake KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye kikao kazi cha kuweka mikakati ya kuwaondoa watoto wanaoishi mitaani pamoja na kutokomeza utoro katika Shule za Msingi na Sekondari mkoani Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye kikao hicho.
Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA Mkoa Mwanza wakifuatilia kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kuondoa watoto wanaoishi mitaani pamoja na kuzuia utoro katika Shule za Msingi na Sekondari mkoani Mwanza.
Wajumbe wa MTAKUWWA Mkoa Mwanza wakiwa kwenye kikao kazi cha kupanga mikakati ya kuwaondoa watoto wanaishi mitaani na kutokomeza utoro mashuleni.
Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA Mkoa Mwanza wakiwa kwenye kikao kazi hicho.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger