Sunday, 8 November 2020

Mtumishi Hospitali Ya Rufaa Shinyanga Mbaroni Tuhuma Za Wizi Wa Vifaa Tiba


 JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu wawili akiwemo Muuguzi wa Hospitali ya Serikali ya Rufaa mkoani Shinyanga wakituhumiwa kwa makosa ya wizi wa vifaa tiba vya hospitali hiyo ya mkoa vyenye thamani ya sh. milioni 26.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga ACP, Debora Magiligimba amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Madaraka Joseph (32) mkazi wa Mageuzi kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni muuguzi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Mtuhumiwa mwingine aliyekamatwa ametajwa kuwa ni Suka Charles (42) mkazi wa Mtaa wa Buzuka Manispaa ya Shinyanga ambapo pia anamiliki zahanati ya iliyopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Akifafanua zaidi Kamanda Magiligimba amesema mnamo Oktoba 13, mwaka huu saa 12.00 jioni kulitokea wizi wa mashine mbili za kuangalia wagonjwa katika chumba cha upasuaji aina ya EDAN 1MB na DATA SCOP 1 zenye thamani ya shilingi milioni 26.

Kamanda Magiligimba amesema baada ya kutokea kwa wizi huo, Jeshi la Polisi lilianza kufanya uchunguzi ambapo lilibaini kuwa mtuhumiwa Madaraka Joseph ambaye ni mtumishi kwenye chumba cha upasuaji katika Hospitali ya mkoa ndiye aliyeiba vifaa tiba hivyo.

“Tulibaini baada ya kuiba vifaa hivyo alikwenda kuviuza kwa Suka Charles kwa makubaliano ya shilingi 4,000,000 na alitanguliziwa kiasi cha shilingi 2,000,000 hata hivyo tulimkamata Suka baada ya kumfanyia upekuzi nyumbani kwake maeneo ya Mhongolo wilayani Kahama na kufanikiwa kukamata vifaa hivyo,” alieleza Magiligimba.

Amesema pia Polisi walikamata vifaa vingine vinavyotumiwa na vifaa hivyo ikiwemo, Patient monitor S/N 301237 – M16 CO9160006-01, Patient monitor S/N PG 63700-B2, BP Machine Accessories (5), Cable wires Accessories (7), Medical molecular sieve, Oxygen Concentrator (1) Serial no. 598 na Oxygen Concentrator Intesty S/N 601-1.

Kamanda Magiligimba amesema watuhumiwa wote wawili wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika ambapo ametoa wito kwa watumishi wa umma kuacha tabia ya wizi wa mali za umma zinazosababishwa na tamaa ya mafanikio ya muda mfupi.


Share:

Rais Mteule wa Marekani Joe Biden atangaza kuunda Jopo la wataalam kuhusu Covid-19


Jopo hili la "wataalam mashuhuri" litateuliwa kuanzia Jumatatu na litatakiwa kuanzisha mpango wa utendaji kuanzia Januari 20, 2021, siku ya kuapishwa kwa rais mpya.

Joe Biden amekua akilitaja jopo hili kila mara katika hotuba yake: vita dhidi ya janga la Covid-19, ambalo limeua watu 237,000 nchini Marekani itakuwa kipaumbele chake cha kwanza. 

Kwa kufanya hivyo, Joe Biden ametangaza kwamba ataanzisha kitengo cha kukabiliana na ugonjwa huo hatari kuanzia Jumatatu, Novemba 9, akiwaleta pamoja "wanasayansi mashuhuri na wataalam" kupambana na changamoto kuu inayoikabili sasa serikali ya Marekani.

"Jumatatu, nitaanzisha, nitateuwa jopo la wanasayansi na wataalam" kufanya kazi "juu ya mpango ambao utaanza kutumika mnamo Januari 20, 2021", siku ya kuapishwa kwangu, amesema rais mteule mbele ya umati wa wafuasi wake waliokusanyika huko Wilmington, Delaware kusherehekea ushindi wake.

Katika wiki hii ya uchaguzi wa urais, Marekani imerekodi idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona kutokana na mlipuko mpya wa janaga hilo kwa siku kadhaa. Marekani ilirekodi zaidi ya visa vipya 122,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona siku ya Jumamosi kwa muda wa saa 24, kulingana na takwimu za shirika la habari la AFP




Share:

Rais Dkt Magufuli Ashiriki Misa Ya Dominika Ya 32 Mwaka A Katika Parokia Ya Bikira Maria Imakulata

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Misa ya Dominika ya 32 Mwaka “A” katika Parokia ya Bikira Maria Imakulata Chamwino Ikulu  Dodoma leo Jumapili Novemba 8, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipokea Sakramenti Takatifu toka kwa Padre Paul Mapalala waliposhiriki Misa ya Dominika ya 32 Mwaka “A” katika Parokia ya Bikira Maria Imakulata Chamwino Ikulu Dodoma leo Jumapili Novemba 8, 2020.


Share:

Pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli


 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inapenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuapishwa Novemba 5, 2020 ili kuendelea kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Kuchaguliwa kwa Mhe. Magufuli kwa mara ya pili kuiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ishara ya matumaini mema na imani ya hali ya juu waliyonayo wananchi wa Tanzania kwake.

Aidha, ni utambuzi siyo tu wa uwezo alionao, bali pia kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2015 – 2020) ambapo  Taifa letu limeshuhudia ongezeko la maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inaendelea kuwa na matumaini makubwa na uongozi wake katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi na kijamii, sambamba na kulinda, kuhifadhi na kutetea haki za binadamu, utawala bora, utawala wa sheria na uwajibikaji.

 Tume inatambua kuwa dhamana aliyopewa Mhe. Rais na Watanzania ni kubwa. Ili kuitekeleza kikamilifu dhamana hii inahitaji kumtanguliza mbele Mwenyezi Mungu na ushirikiano wa Watanzania wote. Tume inamwomba Mwenyezi Mungu amjalie afya njema, hekima na maarifa zaidi ya kuweza kulitumikia Taifa letu.

Tume inaamini kwamba baada ya Mhe. Rais kuapishwa mchakato wa uchaguzi umekwisha.  Kilichobaki mbele yetu hivi sasa ni mshikamano na ushirikiano katika kuijenga nchi yetu. Hivyo, Tume inatoa wito kwa Watanzania na wadau wote wa maendeleo kutoa ushirikiano na kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mwisho, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inawatakia kila la kheri Mhe. Rais Magufuli pamoja na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza majukumu yao katika kipindi cha miaka mitano kilicho mbele yetu, 2020 – 2025.


Share:

CHADEMA YASEMA HAIJATEUA WABUNGE WA VITI MAALUMU


Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika
***
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika, amesema chama hicho hakijafanya uteuzi wa wabunge wa Viti Maalum.

Mnyika ameeleza hayo leo Jumapili Novemba 8, 2020, wakati akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wafuasi wa chama hicho kupitia ukurasa wake wa Twitter ikiwemo kama chama hicho kimeshateua wabunge wa viti maalum.

''Kamati Kuu Chadema haijafanya uteuzi wa wabunge wa viti maalum mpaka sasa. Hivyo hakuna orodha iliyopelekwa na Katibu Mkuu kwa NEC'', ameandika Mnyika.

Kikao cha kwanza cha mkutano wa kwanza wa Bunge la 12 kinatarajiwa kuanza Novemba 10 mwaka huu kama ilivyotamkwa kwenye tangazo la Rais ambapo katika mkutano huo shughuli sita zitafanyika.

Katibu wa Bunge Stephen Kaigaigai, amesema shughuli ambazo zitafanyika ni kusomwa kwa tangazo la kuitisha Bunge, Uchaguzi wa Spika, Kiapo cha uaminifu kwa wabunge wote, kuthibitisha uteuzi wa waziri mkuu, uchaguzi wa naibu Spika na ufunguzi rasmi wa bunge.

CHANZO - EATV
Share:

WAANDISHI WA HABARI WAKUMBUSHWA KUANDIKA HABARI ZA KULINDA AMANI BAADA YA UCHAGUZI


Waandishi wa habari wametakiwa kuandika habari za kujenga Amani nchini na kuacha kupendelea kuandika habari za uchochezi na zenye kuleta taaruki.

Wito huo umetolewa leo na Mwezeshaji wa mafunzo ya kujenga Amani hasa baada ya Uchaguzi Denis Mpagaze yaliyoandaliwa na mtandao wa redio za kijamii nchini (TADIO)

Mpagaze amesema kuwa waandishi wa habari wana nafasi kubwa katika kujenga Amani nchini na kwamba taaluma yao inaweza kujenga au kuharibu kwani jamii inaviamini sana vyombo vya habari.

Katika hatua nyingine Mpagaze amewataka waandishi wa habari kuacha kuandika habari kwa kutumia habari za mitandaoni zenye mihemko na kwamba wafuate kanuni za uandishi kabla ya kusambaza habari zisizo na uhakika.

Mpagaze ameongeza kuwa yapo mambo mengi ya kuisaidia jamii na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Amani na maendeleo na kuwataka waandishi kuacha kuandika habari zenye kuleta taharuki na kuleta hisia hasi kwa jamii.

Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo hayo kutoka mtandao wa Redio za kijamii nchini Cosmas Lupoja amewataka washiriki kuzingatia mafunzo hayo na kuwataka waende kuyatumia katika vituo vyao ili kujenga Amani na kuwa kichecheo cha kuleta maendeleo nchini.

Nao baadhi ya waandishi wanaoshiriki semina hiyo Elias Maganga kutoka Pambazuko Fm ya wilaya ya Kilombero na Mwanaidi Kopakopa kutoka Redio jamii Mtwara wameshukuru mtandao wa redio za kijamii nchini TADIO kutoa mafunzo hayo kwani yamekuja wakati mzuri na yatawasaidia katika kaundaa habari na vipindi vyao.

Mafunzo hayo siku tano yameshirikisha washiriki sabini kutoka Redio thelathini na nne za bara na visiwani pamoja na chama cha waandishi wa habari Pemba.

CHANZO- KAHAMA FM
Share:

TUPIGIE 0622666692 TUKUPE MCHONGO KUTOKA JAMBO!!


Je Unapenda kuwa Wakala wa Bidhaa za Kampuni ya Jambo Food Products Ltd??
Usijali!! 
Wasiliana nasi kwa namba 0622 666 692 Popote Ulipo ndani ya Tanzania uwe Wakala wa Bidhaa kutoka Jambo Food Products Ltd ili ujipatie Ubora wako kwa Bei ya Mwananchi.

#JAMUKAYA
Share:

Lecturer / Assistant Lecturer (Education Psychology) (1 Post) at SUMAIT University

JOB OPPORTUNITIES The Abdulrahman Al-Sumait University (SUMAIT University) was built on the foundation of the former University College of Education Zanzibar established in 1998 by Direct Aid a charity organization based in Kuwait, SUMAIT University invites qualified Tanzanians and non-Tanzanians to fill the academic vacant posts as follows:- Lecturer / Assistant Lecturer (Education Psychology) (1 […]

The post Lecturer / Assistant Lecturer (Education Psychology) (1 Post) at SUMAIT University appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Lecturer/Assistant Lecturer (Education Curriculum and Instruction) (1 Post) at SUMAIT University

JOB OPPORTUNITIES The Abdulrahman Al-Sumait University (SUMAIT University) was built on the foundation of the former University College of Education Zanzibar established in 1998 by Direct Aid a charity organization based in Kuwait, SUMAIT University invites qualified Tanzanians and non-Tanzanians to fill the academic vacant posts as follows:- Lecturer/Assistant Lecturer (Education Curriculum and Instruction) (1 […]

The post Lecturer/Assistant Lecturer (Education Curriculum and Instruction) (1 Post) at SUMAIT University appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Lecturer/Assistant Lecturer Information Technology at SUMAIT University

JOB OPPORTUNITIES The Abdulrahman Al-Sumait University (SUMAIT University) was built on the foundation of the former University College of Education Zanzibar established in 1998 by Direct Aid a charity organization based in Kuwait, SUMAIT University invites qualified Tanzanians and non-Tanzanians to fill the academic vacant posts as follows:- Qualifications Bachelor’s degree in Information Technology (IT) […]

The post Lecturer/Assistant Lecturer Information Technology at SUMAIT University appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Lecturer/Assistant Lecturer (Counseling Psychology) (2 Posts) at SUMAIT University

JOB OPPORTUNITIES The Abdulrahman Al-Sumait University (SUMAIT  University) was built on the foundation of the former University College of Education Zanzibar established in 1998 by Direct Aid a charity organization based in Kuwait, SUMAIT University invites qualified Tanzanians and non-Tanzanians to fill the academic vacant posts as follows:- Lecturer/Assistant Lecturer (Counseling Psychology) (2 Posts) Qualifications […]

The post Lecturer/Assistant Lecturer (Counseling Psychology) (2 Posts) at SUMAIT University appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Lecturer/Assistant Lecturer (Mathematics) (2 Posts) at SUMAIT University

JOB OPPORTUNITIES The Abdulrahman Al-Sumait University (SUMAIT University) was built on the foundation of the former University College of Education Zanzibar established in 1998 by Direct Aid a charity organization based in Kuwait, SUMAIT University invites qualified Tanzanians and non-Tanzanians to fill the academic vacant posts as follows:- Lecturer/Assistant Lecturer (Mathematics) (2 Posts) Qualifications Bachelor’s […]

The post Lecturer/Assistant Lecturer (Mathematics) (2 Posts) at SUMAIT University appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Lecturer/Assistant Lecturer (Islamic Shari’ah and Jurisprudence) (1 Post) at SUMAIT University

JOB OPPORTUNITIES The Abdulrahman Al-Sumait University (SUMAIT University) was built on the foundation of the former University College of Education Zanzibar established in 1998 by Direct Aid a charity organization based in Kuwait, SUMAIT University invites qualified Tanzanians and non-Tanzanians to fill the academic vacant posts as follows:- Lecturer/Assistant Lecturer (Islamic Shari’ah and Jurisprudence) (1 […]

The post Lecturer/Assistant Lecturer (Islamic Shari’ah and Jurisprudence) (1 Post) at SUMAIT University appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Lecturer/Assistant Lecturer (Chemistry) (2 Posts) at SUMAIT University

JOB OPPORTUNITIES The Abdulrahman Al-Sumait University (SUMAIT University) was built on the foundation of the former University College of Education Zanzibar established in 1998 by Direct Aid a charity organization based in Kuwait, SUMAIT University invites qualified Tanzanians and non-Tanzanians to fill the academic vacant posts as follows:- Lecturer/Assistant Lecturer (Chemistry) (2 Posts) Qualifications Bachelor’s […]

The post Lecturer/Assistant Lecturer (Chemistry) (2 Posts) at SUMAIT University appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Various Jobs at Lodhia Group

Interested candidates should send CVs and application letters to info-dar@lodhiagroup.co.tz The deadline for submitting the application is 15 November 2020

The post Various Jobs at Lodhia Group appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

PLANNING/DEVELOPMENT ENGINEER (5 POSTS) at ATCL

Air Tanzania Company Limited (ATCL) is in the process of revamping its operations and has introduced new equipment to its fleet as part of implementation of its five years Corporate Strategic Plan (2017/2018-2021/2022. In line with this expansion, the Company is also making some reforms in Engineering and Maintenance section to accommodate the business needs. […]

The post PLANNING/DEVELOPMENT ENGINEER (5 POSTS) at ATCL appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

DIAMOND ROCK KWA LADHA SAFIII!!! FURAHA YAKO, FAHARI YETU!!



Mbele Daima, Nyuma mwiko furaha yako fahari yetu... Bidhaa Bora kutoka EAST AFRICAN SPIRITS (T) LTD




Hanson's Choice!!



Diamond Rock!!




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger