Sunday, 22 March 2020

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili March 22













Share:

Rwanda Yatangaza Mikakati Kabambe ya Kukabiliana Na Virusi Vya Corona....Mipaka Yote Imefungwa, Baa, Kusafiri Hovyo Marufuku

Wakati ugonjwa wa virusi vya corona  ukiwa unaenea kwa kasi katika maeneo mbalimbali ulimwenguni,Waziri mkuu wa Rwanda Dkt.Ngirente ametoa maagizo 10 ya kukabiliana nao.

Baadhi ya maagizo aliyoyatoa Dkt.Ngirente ni pamoja na kutoruhusu safari zisizo za lazima,malipo ya kieletroniki zaidi yatatumika kuliko kutumia ATM ,Waajiriwa/Watumishi wote wa umma na sekta binafsi watafanya kazi wakiwa majumbani isipokuwa wale watoa huduma muhimu.

Maagizo mengine ni mipaka yote kufungwa,isipokuwa usafiri wa mizigo,safari kati ya miji na wilaya tofauti ndani ya nchi hairuhusiwi isipokuwa kwa sababu za matibabu,usafirishaji wa chakula au bidhaa muhimu zitaruhusiwa.

Pia Dkt.Ngirente ameagiza maduka na masoko yote kufungwa  isipokuwa yale yanayouza chakula,Dawa, vifaa vya usafi huku baa zote zikifungwa.


Share:

Saturday, 21 March 2020

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo yaripoti kifo cha kwanza kutokana na corona na visa vitano vipya

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo leo imeripoti kifo cha kwanza kutokana na virusi vya corona pamoja na visa vitano vipya vya maambukizi.Kupitia mtandao wa twitter, waziri wa afya nchini humo Eteni Longondo, amethibitisha kifo hicho kilichotokea hapo jana pamoja na visa hivyo vipya akisema wote walioathirika ni raia wa Congo na kwamba maafisa wake wanawashughulikia. 

Nchi hiyo imeripoti visa 23 kwa jumla tangu Machi 10 na kifo hicho kinaongeza idadi ya waliofariki kutokana na virusi hivyo katika eneo la jangwa la Sahara barani Afrika kufikia watu watatu baada ya vifo vilivyoripotiwa wiki hii katika nchi za Burkina Faso na Gabon.

Hapo jana, serikali ya Congo, iliratibu mikakati ya kinga hasa katika mji mkuu Kinshasa ambao ni makazi ya takriban watu milioni 10 na ambapo ndiko kwenye visa vingi vya virusi hivyo kwa sasa.


Share:

ALIYEKATA UMEME MWANZA AKIONA CHA MOTO....WAZIRI AONYA MAMENEJA WA TANESCO WANAOKATA HOVYO UMEME


Kulia ni Waziri wa Nishati Dkt Medadi Kalemani.

Waziri wa Nishati Dkt Medadi Kalemani amemuagiza Mkurugenzi wa TANESCO kumchukulia hatua kali Msimamizi wa Kituo cha kupooza umeme cha Ubungo Mhandisi Abubakar Issa kwa kukata umeme Ijumaa Machi 20, 2020.

Dkt Kalemani pia ametoa onyo kwa mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kote nchini kuacha tabia ya kukata umeme na kufanya mgao kwa kisingizio cha mitambo ya kuzalisha Umeme kushindwa kufanya kazi.

Katika Hatua nyingine Waziri Dkt Medadi Kalemani amewataka wananchi wanaofanya shughuli zao kandokando mwa mto ambako maji ya bwawa la Mtera yanaelekea kuondoka ili kujinusuru na athari za maji yanayofunguliwa kutoka bwawa la Mtera.

Kufuatia zoezi la Kufunguliwa kwa Maji katika daraja la Mtera ili kupunguza ujazo wa maji katika Bwawa hilo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amesema tayari tahadhari imetolewa kwa wananchi ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.

Imeelezwa kuwa Ujazo wa Maji katika Bwawa la Mtera umefikia mita za ujazo 698.74 kiwango kinachostahili kwaajili ya Uzalishaji wa Umeme jambo ambalo limesababisha serikali kufungua na kupunguza ujazo huo katika bwawa hilo.
Chanzo - EATV
Share:

Breaking : SOKO KUU MJINI SHINYANGA LANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO USIKU HUU


Soko Kuu Mjini Shinyanga limenusurika kuteketea kwa moto baada ya moto ambao haujajulikana chanzo chake kuunguza baadhi ya bidhaa ikiwemo maboksi na madumu na ndoo za plastiki.


Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde 1 blog iliyofika eneo la tukio kuwa moto huo umeanza kuwaka leo Jumamosi Machi 21,2020 majira ya saa moja na nusu usiku.

“Tukiwa nje ya Soko Kuu tumesikia yowe la watu wakipiga kelel tukafikiri labda ni wezi, Baadaye tukasikia Moto! Moto! Moto!,ikatubidi tuwahi,tukaingia ndani ya soko na kuona moto eneo la choo unawake ukiunguza bidhaa mbalimbali,Wasamaria wema waliokuwepo tumeshirikiana kuzima moto huu kwa maji”,amesema mmoja wa wananchi aliyejulikana kwa jina la Suleiman Abeid.

“Lakini moto huu umetushangaza kwani umewaka katika mazingira ya kutatanisha.Hii hali lazima ichunguzwe kwanini moto huo umewaka.Kuna vifaa vya mfanyabiashara ambaye huuza maboksi,kuna ndoo na maboksi kadhaa zimeungua hapa”,ameeleza Abeid.

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliojitokeza kuzima moto huo ambao umetokea wakati Umeme ukiwa umekatika Mjini Shinyanga,wamesema huenda moto huo huenda umetokana na sigara iliyorushwa na mtu aliyekuwa ndani ya choo ama moto huo umewekwa kwa maksudi kutokana na kile kinachoelezwa kuwa katika soko hilo kuna mgogoro wa vyumba.

Wameziomba Mamlaka zinazohusika kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo la moto.
Endelea kufuatilia habari zaidi kupitia Malunde 1 blog
Baadhi ya bidhaa zilizoungua katika Soko Kuu Mjini Shinyanga baada ya kutokea kwa moto ambao haujajulikana chanzo chake usiku huu Jumamosi Machi 21,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

MAJIBU YA MASWALI 10 YANAYOULIZWA SANA KUHUSU VIRUSI VYA CORONA

Mchakato wa ukuaji wa coronavirus hadi kufikia uwezo wa kusababisha ugonjwa huchukua siku 14, linasema Shirika la Afya Duniani (WHO)
Zaidi ya nchi 110 hadi sasa zimeripoti visa vya coronavirus na Shirika la Afya Duniani limetangaza virusi hivyo kuwa janga.

Yafuatayo ni majibu ya baadhi ya maswali ambayo wasomaji wamekua wakiyauliza.
1. Je inachukua kipindi gani mpaka mtu afahamike kuwa na coronavirus? - Swali lililoulizwa na Gillian Gibs
Inachukua siku tano kwa wastani kuanza kuonesha dalili, tangu mtu apate maambukizi, wanasayansi wamesema, lakini baadhi ya watu huanza kuonesha dalili hata baadae kuliko kipindi hiki.
Mchakato wa ukuaji wa coronavirus hadi kufikia uwezo wa kusababisha ugonjwa huchukua siku 14, Shirika la Afya Duniani (WHO), linasema. Lakini baadhi ya watafiti wanasema kipindi hicho kinaweza kuchukua hadi siku 24.
Kufahamu na kuelewa kipindi cha ukuaji ni muhimu sana. Huwasaidia madaktari na mamlaka za afya kuanzisha njia bora za kudhibiti usambaaji wa virusi.
2. Je ukipona coronavirus ina maanisha unakinga ? RubyRed aliuliza kwenye ukurasa wa Twitter.
Kusema ukweli ni vigumu kuelezea. Virusi hivi vimekuwepo tu tangu mwezi Disemba, lakini kutokana na uzoefu wa virusi vingine na coronaviruses unatakiwa kuwa na kinga ya mwili yenye uwezo wa kukabiliana na virusi ambayo itakulinda.
Mwanamke akikohoa

Kwa virusi vya Sars na virusi vingine vya aina ya coronavirus tulishuhudia maambukiuzi. Sasa kuna ripoti kutoka Uchina za watu ambao wanaruhusiwa kutoka hospitalini ambao walipatikana na virusi lakini hawakuwa na uhakika juu ya vipimo hivyo.

Hata hivyo, kitu muhimu ilikuwa ni watu hao hawakuwa na maambukizi tena.
3. Kuna tofauti gani kati ya coronavirus na mafua? - Brent Starr, Gresham, na Oregon, waliuliza kutoka Marekani.
Coronavirus na mafua ni maambukizi yenye dalili sawa jambo linalofanya utambuzi wake kuwa mgumu bila kufanyiwa kipimo.
Dalili ya kuangalia kupanda kwa joto la mwili na kikohozi. Mara kwa mara mafua huwa na dalili sawa na hizo pia, kama vile kuvimba koo, huku watu wenye virusi vya corona wakihisi kuishiwa na pumzi.
Watu ambao hufikiria kuwa huenda wameathiriwa na coronavirus wanahitaji kupata ushauri zaidi wa haraka wa kimatibabu.
Chati inayoonyesha dalili za coronavirus
4. Je kujitenga binafsi inamaanisha mtu afanye nini ? - Anauliza Alan Gel
Kujitenga binafsi inamaanisha mtu kukaa nyumbani kwa siku 14, sio kwenda kazini, shule au maeneo ya umma, na kuepuka kusafiri katika usafiri wa umma au teksi. Unapaswa pia kukaa mbali na wengine nyumbani kwako.
Omba msaada kama unahitaji huduma ziwe za chakula au matibabu , lakini hupaswi kumkaribisha mgeni yeyote,
5. Je corona ni hatari kwa watu wenye maradhi ya pumu? - Wameuliza Lesley-Anne, Falkirk
Maambukizi yatokanayo na mfumo wa hewa, kama vile coronavirus, yanaweza kusababisha mtu kuwa na dalili za pumu /asthma.
Wataalamu wa tiba ya ugonjwa wa pumu wanashauri watu wanaohofia virusi kufuata hatua za kudhibiti maradhi ya pumu.
Hii ni pamoja na kutumia vifaa maalumu vya kufungua njia ya hewa -inhaler kila siku kama inavyoshauriwa. Hii inasaidia kupunguza hatari za shambulio la pumu linaloweza kusababishwa na kirusi chochote cha mfumo wa kupumu, mkiwemo coronavirus.
Mwanamke akipiga chafya huku akiwa amejifunika pua na mdomo kwa kitambaa

6. Je coronavirus inaweza kuambukizwa kwa kufungua vitasa vya milango na vinaweza kuishi kwa muda gani? - Ameuliza Jean Jimenez

Kama mtu ameambukizwa kikohozi na kukoholea viganjani mwake na kugusa kitu fulani sehemu ya juu ya kitu hicho hua imeambukizwa.
Kitasa cha mlango ni mfano mzuri wa vitu ambavyo vinaweza kusababisha athari ya maambukizi ya coronavirus.
Wataalamu wanafikiria kuwa coronavirus inaweza kuishi kwenye eneo fulani huenda kwa siku kadhaa. Kwa hiyo ni bora kuosha mikono yako mara kwa mara ili kupunguza hatari ya maambukizi na kuenea kwa virusi.
7. Je ni salama kuogelea kwenye vidimbwi vya maji vya umma /Swimming pools? - Ameuliza Annette
Maji katika vidimbwi vingi vya kuogelea vya Umma huwa yana Chlorine, kemikali ambayo inaweza kuua virusi. Kwa hivyo kama inawekwa basi maji hayo yanapaswa kuwa salama kutumia vidimbwi vya kuogelea vya umma kwani huwa vinawekwa kemikali hiyo.
Hata hivyo, unaweza kupata virusi kutoka kwa mtu mwingine ambaye ameambukizwa hasa mnapokutana katika chumba cha kubadilisha nguo au kama jengo lina maambukizi kama vile kweye vitasa vya milango.
Na mtu fulani ana maambukizi ya virusi anaweza kuvisambaza kwa wengine kupitia kikohozi na chafya kama watagusana.
Kuna njia nyingi za kukusaidia kuepuka kupata au kusambaza maambukizi ya virusi.
Njia za kuzuia maambukizi
8Je ninapaswa kuanza kuvaa barakoa ili kupunguza uwezekano wa kueneza na kupata virusi? -Swali la Ann Hardman
Ingawa madaktari na wapasuaji mara kwa mara huvaa barako, kuna ushahidi mdogo sana kwamba uvaaji wa barakoa unaleta tofauti.
Mfano Idara ya afya kwa Umma nchini Uingereza imesema kuwa "haitoi ushauri matumizi ya barakoa kama njia ya kujilinda dhidi ya virusi".
Wataalamu wanasema usafi wa kutosha - kama vile kunawa mara kwa mara mikono yako na kabla ya kugusa uso wako-ni jambo la maana zaidi katika kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.
9Kuna hatari gani kwa watoto ? - Swali la Louise,
Kwa ujumla watoto wanaonekana kutoambukizwa sana coronavirus, kwa mujibu wa data kutoka China.
Hii huenda ikawa ni kwasababu wana uwezo wa kukabiliana na maambukizi au hawana dalili yoyote , au wanakua na dalili ndogo sawa na zile za mafua. Hatahivyo, watoto wenye matatizo ya mapafu, kama vile maradhi ya pumu, wanapaswa kuwa makini , kwani virusi vinaweza kusababisha shambulio la pumu.
Kwa watoto walio wengi, inaweza kuwa ni maambukizi ya mfumo wa kupumua kama mengine na hakuna sababu ya kuwa na hofu.
Watoto
11. Je unaweza kupata virusi kutoka kwenye chakula kilichoandaliwa na watu walio na coronavirus? - Aliuliza Sean
Mtu ambaye ameambukizwa coronavirus anaweza kusambaza virusi kwa mtu mwingine kama chakula walichoandaa hakikuandaliwa kwa usafi.
Virusi vinaweza kusambazwa kwa matone ya kikohozi yanayoanguka kwenye kiganja au mkono.
Kunawa mikono kabla ya kugusa au kula chakula ni ushauri mzuri kwa kila mtu katika kuzuia kusambaa kwa virusi.
CHANZO- BBC
Share:

MASHARTI YA USAFIRI AFRIKA KUZUIA VIRUSI VYA CORONA


Hatua zilizochukuliwa na mataifa ya Africa kukabiliana na coronavirus


Share:

WAZIRI MKUU AONYA WANAOPOTOSHA KUHUSU CORONA....AAGIZA TCRA IANZE KUWACHUKULIA HATUA KALI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameonya juu ya upotoshwaji na utoaji holela wa taarifa kuhusu ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababisha na virusi vya corona (COVID 19) unaofanywa na watu mbalimbali nchini.


Amesema kuanzia sasa taarifa hizo zitatolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na ikilazimika zitatolewa na Waziri Mkuu na ikilazimika sana zitatolewa na viongozi wakuu wa nchi ili kuepusha mikanganyiko.

Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Jumamosi, Machi 21, 2020) wakati akizungumza na Wakuu wa Mikoa yote nchini, Makatibu Tawala wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Mikoa kwa njia video kutokea ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ifuatile watu wote wanaofanya upotoshaji kwa kupitia mitandao ya kijamii ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

“Watu wote wanaopotosha umma na kuleta taharuki kuhusu ugonjwa wa corona badala ya kuelimisha namna ya kujikinga, wafuatiliwe na kuchukuliwa hatua,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema licha ya hali ya maambukizi ya corona nchini kutia matumaini, viongozi hao hawana budi kupeana taratibu za namna ya kukabiliana na tatizo hilo.

“Wakuu wa mikoa kila mmoja ahakikishe eneo lake linakuwa salama na endapo kutakuwa na mgonjwa tumieni zahanati ambazo bado hazijaanza kutumika kwa ajili ya kutolea huduma kwa wagonjwa wa corona,” amesema.

Amewataka wakuu hao wa mikoa waimarishe utoaji wa elimu kwa umma na ikiwezekana watumie magari ya matangazo ili wananchi waelewe athari za ugonjwa huo na namna ya kujikinga pamoja na kuwaondolea hofu ili waweze kuendelea na shughuli zao za kimaendeleo.

Pia amewataka watumie redio za kijamii katika maeneo yao kutoa elimu kwa umma juu ya kujikinga na ugonjwa huo na wasimamie maeneo ya utoaji huduma kama vituo vya mabasi na kuhakikisha kila abiria anakaa kwenye kiti.

“Nendeni kwenye maeneo ya mikusanyiko, vituo vya mabasi kutoa elimu kwa umma na kuwaondoa hofu. Upande wa maofisini, viwandani na kwenye mgodi kuwe na utaratibu wa kutoa elimu kwa wafanyakazi kila siku asubuhi watumie hata robo saa kabla ya kuanza kazi waelekezwe namna ya kujikinga.”

Waziri Mkuu amesema kwa wanaoishi katika maeneo ya makambi, viongozi wao waelekezwe namna ya kutoa elimu ya kujikinga na corona na pia wadhibiti utorokaji na Serikali kwa upande wake inaendelea kuimarisha udhibiti mipakani, uwezo wa kupima sampuli na upatikanaji wa vifaa.

Amewataka wakuu hao wa mikoa, wawashirikishe wakuu wa wilaya kwenye mikoa yao ili wasimamie utekelezaji wa maagizo hayo.

Wakati huohuo,Waziri Mkuu amewaagiza wakuu hao wa mikoa wahakikishe wanawafuatilia na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote watakaobainika kuongeza bei kwa bidhaa ambazo zinatumika katika udhibiti wa maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Kuhusu viongozi wa dini, Waziri Mkuu amewaomba waendelee kushirikiana na Serikali katika kuwaelimisha waumini wao wote kuzingatia tahadhari za ugonjwa huu. Pia awaendelee kuliombea Taifa.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

MSD Yawatahadharisha Wanaopandisha Bei Za Vikinga Korona

Na Mwandishi wetu- Maelezo
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Lawrean Bwanakunu amesema kuwa endapo wafanyabiashara wa bidhaa zinazosaidia kujikinga na maambukizi ya virusi vya korona wataendelea na tabia ya kupandisha bei ya bidhaa hizo itabidi MSD iingize bidhaa hizo mtaani.

Akielezea suala la bei ya vikinga virusi vya korona Bwanakunu alitolea mfano na kusema “Dawa za kuoshea mikono (sanitizer) ambayo bei yake halali katika soko ni shilingi 2,500 lakini kwa sasa wafanyabiashara wamepandisha zaidi na kuuza kwa shilingi 5,000. 

Aidha, bei halali ya dawa za kuoshea mikono ni shilingi 85,000 kwa lita tano badala ya bei wanayouza ya shilingi 200,000, pia vidonge vinavyotumika kuweka kwenye maji kwa ajili ya kunawa mikono bei halali kwa kidonge kutoka MSD ni shilingi 360, lakini wafanyabiashara wanauza shilingi 5,000. 

Inashangaza kopo lote lenye vidonge 100 huuzwa kwa shilingi 36,000 lakini wafanyabiashara kwa sasa wanauza shilingi 500,000”.

Bwanakunu, aliyasema hayo alipokuwa anahojiwa na kituo cha Independent Television – ITV, na kusisitiza kuwa MSD haifanyi kazi ya kuuza dawa za bidhaa zinazotumika kwenye masuala ya afya lakini itabidi ifanye kazi hiyo ya kusambaza mitaani ili kuwadhibiti wafanyabiashara wenye nia mbaya wanaotumia tishio la ugonjwa wa korona kuwaumiza wananchi.

Utaratibu wa MSD ni kuwauzia vituo vinavyotoa huduma za afya pekee na sio kuwauzia watu binafsi dawa au mtu mmoja mmoja. 

Amewaasa wafanyabiashara kwamba ikiwa wataendelea na tabia ya kupandisha bei dawa na bidhaa zinazosaidia kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo, serikali itachukua jukumu la kutoa bidhaa na vifaa hivyo ili kujaa kwenye soko hatua ambayo itasababisha bei kushuka.

Aidha, uamuzi wa Serikali wa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Korona kwa kufunga shule zote za awali, msingi, sekondari na vyuo vikuu, vya kati na vya chini, ikiwa ni pamoja na kusitisha mikutano, semina, warsha na shughuli za kijamii jambo ambalo ni msingi wa kuthibiti ugonjwa huo.

Akitadhaharisha na kutoa msisitizo juu ya suala la kuchukua tahadhari na kujikinga na ugonjwa wa Korona Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema “Watanzania wenye safari zisizo za lazima kwenye nchi zenye maambukizi wanashauriwa wasitishe safari hizo”.

Uamuzi huo wa Waziri Mkuu alioutoa alipokutana na Waandishi wa Habari ofisini kwake Magogoni Jijini Dar-es-salaam kwa siku mbili tofauti na kusisitiza taifa kuwa na tahadhari ya ugonjwa wa huo, ambapo kuna ongezeko la wagonjwa na washukiwa wa ugonjwa huo kwa taarifa za tarehe 20 Machi 2020 kuna washukiwa 112 na idadi ya wagonjwa kufikia watano.

Alitoa wito kwa Watanzania kumuomba Mungu kila mtu kwa imani yake na kuwa makini na kujikinga na ugonjwa huo, pia kutokuwa na taharuki na kuchukua hatua stahiki na kuendeleza kusitisha baadhi ya shughuli ambazo sio za lazima kama vile kupunguza msongamano na mkusanyiko isiyo ya lazima.

Akisisitiza Jambo la kujikinga Waziri Mkuu alisema kuwa huduma za usafirishaji ziendelee zikiambatana na utoaji wa elimu ya ugonjwa huu, lakini watu wakishajaa kwenye viti dereva aondoe gari badala ya kubaki na tabia ya kujaza kupita kiasi inayohatarisha afya za wasafiri. 

Pia, shughuli za masoko, maduka na huduma kama hizo bado zitaendelea kutolewa kama kawaida ili wananchi wasikose huduma ya kujipatia mahitaji ya lazima kama vile chakula bila kujihusisha na mikusanyiko isiyo ya lazima.

Pia, alielezea hatua nyingine zilizochukuliwa na serikali ili kuthibiti ugonjwa huo Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imesitisha Michezo yote inayokusanya makundi ya watu ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili na kuitaka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kuziandikia barua Taasisi zake kutekeleza agizo hilo.

“Tunatambua vyuo vya elimu vingetakiwa kufanya mitihani mwezi Mei mwaka huu namuagiza Waziri wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo Profesa Joyce Ndalichako afanye marekebisho ya muhula wa mitihani yao kama vile tulivyomuagiza kufanya marekebisho kwenye mihula yao katika shule za sekondari za kidato cha sita”, ameongeza Waziri Mkuu.

Aidha, haijalishi wewe ni nani mtu yeyote anaweza kuambukizwa anapopeana mikono na mgonjwa wa korona, kukumbatiana au kugusa majimaji au jasho, mafua, kupiga chafya mfululizo na kukohoa ikiwa ni pamoja na kupata homa za mara kwa mara au joto kupanda, ambapo vijidudu hivyo vya korona husambaa kwa njia ya hewa kutoka kwa mtu aliyepata maambukizi. 

Hivyo ni jambo la msingi kuchukua tahadhari ili kujikinga na maambukizi na kuzuia kusambaza kwa watu wengine katika maeneo yetu.

Kwa utafiti mdogo uliofanywa na Idara ya Habari Maelezo katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar-es-salaam hususan Gongo la Mboto, Chanika, Mbagala mpaka Chamazi, katikati ya Jiji Magomeni Buguruni, Idadi kubwa ya wakina mama wameathirika katika suala zima la upatikanaji wa fedha ikihusishwa na michango ya vikoba kwani wateja wakubwa wa bidhaa za kina mama hawa hawapo, uuzaji wa chakula, vitafunwa na vitu kama hivyo vimekosa wanunuzi na kulazimika kubaki nyumbani.

Akiongea na Idara ya Habari Maelezo Mama Faustine Nyambona mfanyabiashara wa vitafunwa pembezoni mwa Shule ya Msingi Nzasa amesema “Mimi binafsi nakubaliana kabisa na juhudi zinazofanywa na serikali katika kujikinga na ugonjwa wa Korona nawaomba wakina mama wenzangu ambao kwa kiasi kikubwa tumeathirika kiuchumi tuwe na subira na uvumilivu kwani afya ni kila kitu kwa mwanandamu. Tumuombe Mungu tutavuka katika hili na tutarudi katika shughuli zetu za kila siku hakuna jinsi”

Aidha, Naye Bibi Magreth Tilla ambaye ni Mwalimu katika Shule ya binafsi ya watoto wadogo maarufu kama chekechea amesema . “Hili ni janga la dunia ni lazima sisi tuwe sehemu ya kupambana na ugonjwa huu wa Korona kinyume cha hapo tutaangamiza dunia na kizazi chetu chote. Pamoja na kuwa nimeathirika kiuchumi lakini ni bora tuwe na afya zetu kama nchi na dunia kwa ujumla “

Naye, Dereva wa Daladala wa gari la kwenda Mbagala ambaye hakutaka jina lake litwaje amesema “Hali ya Dar-es-salaam imekuwa ngumu kwelikweli kiuchumi, mimi nadhani ule mzaha tuliokuwa tunaufanya eti siku hizi fedha hamna ilikuwa danganya toto na jambo la kudhihaki serikali. Binafsi Naomba msamaha kwa serikali na kusema siku hizi fedha hakuna tulikuwa tunafanya mzaha ambao haukuwa na ukweli, nakuambia Mwandishi hivi sasa fedha ni ngumu kwelikweli najiuliza wale wanaosema wanatamani vita ije kuliko kutokuwa na demokrasia hawajui kufa nawaomba wachungulie kaburi na waache kabisa kushawishi Watanzania mambo mabaya”.

Ipo mifano hai ambayo tunaona baadhi ya nchi kama Italia, zinapambana katika hali ya taharuki kutokana na idadi kubwa ya watu kuambukizwa ugonjwa huu, kutokana na kutochukua tahadhari na kupuuza kwa kuendeleza mikusanyiko na shughuli zao kama kawaida ambapo kwa sasa wanachukua tahadhari wakiwa wamechelewa na kusababisha idadi ya wagonjwa walioambukizwa na vifo kuwa kubwa zaidi duniani.

Watanzania tuchukue tahadhari kihalisia na sio kufanya mizaha na kupotosha jamii katika suala kubwa la ugonjwa wa Korona ambao unaangamiza watu kwa vifo, kupoteza nguvu kazi, kuleta athari za kudorora kwa uchumi kuanzia wa mtu mmoja mmoja, familia na Taifa bila kujali kama ni maskini au tajiri.

Tuache kodhoofisha mapambano dhidi ya Korona kwa kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wa maduka ya dawa ambao wamechukulia tatizo hili kwa kujinufaisha na kupandisha bei bidhaa muhimu zinazotumika katika kujikinga na ugonjwa huu kama vile dawa za kusafisha mikono (sanitizer) na kuvaa barakoa (mask) wanashirikiana na serikali ili kusambaza vikinga ugonjwa wa korona kwa bei stahiki na zinapatikana kila mahali kuanzia mijini hadi vijijini.

Aidha, ugonjwa huu ukisambaa hauchagui wala kubagua kwani haujui huyu ni mfanyabiashara wa vikinga Korona kwa hiyo asipate ugonjwa na huyu anastahili kupata. Kwani usipopata wewe atapata ndugu yako, rafiki yako, shangazi yako au mjomba wako bila wewe mfanyabiashara kujua kuwa hata ndugu yako linaweza kumfika. Tuombe Mungu atuepushe na janga hili hivyo jitihada za pamoja zinahitajika kwa kila Mtanzania.

Watanzania wametakiwa kuwa makini wanapomuona mtu mwenye dalili za ugonjwa au mtu binafsi unapopata dalili za ugonjwa wa Korona kama vile kuwa na homa kali za mara kwa mara, mafua, kuumwa na kichwa, kupumua kwa shida, kupiga chafya mfululizo, tafadhali piga simu namba zifuatazo ambazo hutatozwa gharama yeyote; 0800-119124, 0800-110125, na 0800-110037.



Share:

Njombe:Wataalamu wazunguka Stendi,Sokoni kutoa elimu ya virusi vya Corona

Na Amiri kilagalila,Njombe
Kufuatia uwepo ugonjwa wa virusi vya Corona nchini Tanzania,halmashauri ya mji Njombe imeanza kutoa elimu kwa wananchi wa halmashauri hiyo ili kuweza kuchukua hatua stahiki za kuepukana na maambukizi zaidi ambapo Idara ya afya imeanza kutoa elimu katika maeneo ya stendi,masoko,taasisi za kifedha na hoteli kuhusu dalili na njia za kujikinga na virusi hao.

Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe Dkt.Yesaya Mwasubila amewataka wananchi kuhakikisha kuwa wananawa mikono kwa kutumia maji yenye dawa kila wakati wanapokua katika maeneo ya huduma mbalimbali na amezitaka taasisi zote zinazotoa huduma kuhakikisha kuwa wanaweka maji na kutoa maelekezo kwa yeyote anayeingia au kutoka kunawa mikono ili kuepusha maambukizi.

Mwasubila amesema kwa sasa halmashauri imetenga eneo maalumu katika Kituo cha Afya Ihalula ambapo endapo kutabainika mgonjwa mwenye dalili za virusi vya Corona atawekwa chini ya uangalizi wa siku 14 katika kituo hicho.

Kinga ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya COVID 19 vinavyosababisha homa ya CORONA ni pamoja na kuepuka msongamano, kunawa mikono vizuri kwa maji safi yanayotiririka na sabuni, au maji yenye dawa, kutumia vitakasa mikono, kutumia vikinga pua na mdomo (masks) kwa wale wanaopiga chafya au kukohoa, kuepuka kugusana na kukaa mbali na mtu mwenye dalili za mafua.


Share:

TANZIA: Msanii mkongwe wa muziki wa country Kenny Rogers afariki dunia

Msanii Kenny Rogers (81) raia wa Marekani, amefariki Dunia akiwa nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa familia yake kifo cha Msanii huyo ni cha kawaida na wala hakihusishwi na jambo lolote .

Rogers, alitamba kwa nyimbo zake nyingi zikiwemo The Gambler, Lady, Islands in the Stream na Lucille, huku akiwa ameuza rekodi zaidi ya Milioni na kushinda tuzo 3 za Grammy.

Kama muigizaji ametokea kwenye filamu ya Six Pack mwaka 1982 na katika tamthilia kadhaa maarufu za runinga kama The Gambler franchise, Christmas in America na Coward of the County.


Share:

Wanaoongeza bei vifaa vya kujikinga na Corona kuchukuliwa hatua za kisheria

Serikali imeiagiza Tume ya Ushindani wa Kibiashara na Shirika la Ubora wa Viwango (TBS) kufanya msako na kuwachukulia hatua wafanyabiashara watakaobainika kuongeza bei kwa makusudi kwa lengo la kujipatia faida kubwa katika kipindi hiki kigumu cha mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

Agizo hilo limetolewa leo Machi 21, 2020 na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa ambapo pia amewaonya wafanyabiashara walioficha bidhaa za vitakasa (sanitizers) na barakoa (mask) kuacha mara moja huku akiwatoa hofu Watanzania kuhusu upatikanaji wa bidhaa hizo na kuongeza kuwa Serikali inafanya kila linalowezekana kuhakikisha bidhaa zinapatikana kirahisi na kwa bei nafuu.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger