Friday, 2 September 2016
Thursday, 1 September 2016
KIDATO CHA SITA KWA MUJIBU WAFUNGA MAFUNZO-DC KASULU AFUNGA MAFUNZO YA OPERESHENI MAGUFULI (JKT) KAMBI YA 825 KJ KIGOMA
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akikagua paredi ya vijana 1140 wa operesheni Magufuli kwa mujibu wa sheria katika kikosi cha 825 KJ kilichopo Mtabila katika Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma.
Na Abel Daud, Globu ya Jamii, Kigoma
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya operesheni Magufuli (kwa mujibu wa sheria) kutoka wilayani hapo kwenda kutekeleza falsafa ya hapa kazi tu.
Hayo ameyasema alipokuwa akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana 1140 operesheni Magufuli kwa mujibu wa sheria katika kikosi cha 825 KJ kilichopo Mtabila katika Wilaya ya Kasulu na kuwataka kwenda kuungana na watanzania wengine wote katika kuiamini kuitekeleza na kuiishi falsafa ya hapa kazi tu kwa vitendo.
Akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi, Mkuu wa kambi ya 825 KJ, Meja George Kazaula amesema kikosi kimefanikiwa kutengeneza madawati 1074 ikiwa ni agizo la Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli.
Pia ameelezea changamoto zinazoikabili kambi hiyo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa umeme wa gridi ya taifa pamoja na miundombinu ya barabara kuwa mibovu hali inayopelekea matumizi makubwa ya uendeshaji wa umeme wa genereta pamoja na matengenezo ya mara kwa mara ya magari ya kikosi.
Nae mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga taifa hapa nchini Luten col. Philipo Mahende amewataka vijana hao kuwa wazalendo wa kweli ambao watakuwa tayari kulilinda taifa kwa gharama yoyote ile ili amani,umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania unakuwa endelevu, na kuwaomba kujiepusha na kutokuwa miongoni mwa watanzania wachache wanaoshabikia mgawanyiko miongoni mwetu kwa misingi ya itikadi za kisiasa,kidini au mahali anapotoka mtu.
Akisoma lisara kwa mgeni rasmi mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo ameiomba serikali kuiongeza bajeti Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa ili vijana wengi wapate nafasi kujiunga na mafunzo ya JKT ili waweze kujifunza uzalendo na shughuli za uzalishaji mali ili kuwatengenezea uwezo wa kujiajiri wenyewe pasipo kuitegemea Serikali.
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akitoa zawadi kwa baadhi ya vijana waliofanya vizuri katika mafunzo hayo
Vijana hao Wakipita kwa mwendo wa haraka.
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akipokea heshema ya kijeshi kutoka kwa vijana wanaohitimu
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi wa kwanza kushoto akielekea yalipo madawati.
Baadhi ya madawati yaliyotegenezwa.
Baadhi ya vijana wa JKT Mtabila wakiendelea na kazi ya kupaka rangi madawati.
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akiangalia madawati yaliyotegenezwa kambini hapo.
Vijana wanaomaliza mafunzo ya opeteshen Magufuli wakipita kwa mwendo wa kasi mbele ya mgeni rasmi.
Meja George Kazaula akisoma taarifa fupi
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akitoa hotuba
TAARIFA KWA UMMA KUTOKA NACTE :TAHADHARI KWA WAKUU WA VYUO, WADAU NA UMMA KWA UJUMLA
Baraza linaendelea na kuwatahadharisha wateja wetu kuwa msikubali kupokea simu zenye kuwaomba fedha au kutoa kitu chochote wakati mnapotekeleza maelekezo ya Baraza au hata baada ya kutekeleza maelekezo hayo.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza anatoa tahadhari hii baada ya ofisi yake kupokea malalamiko hivi karibuni kutoka kwa baadhi ya Wakuu wa Vyuo na Wamiliki ambao wamedai kupigiwa simu na watu wanaojitambulisha kuwa Maafisa wa NACTE na kuwadai kiasi cha fedha kama masharti ya kutatuliwa matatizo yao. Pia Baraza limepokea taarifa kutoka kwa Wadau wanaolalamika kuwa kuna kundi la watu wanaodai kupewa fedha ili wasaidiwe kupangiwa vyuo fulani vya ufundi kwa masomo mbali mbali.
Baraza halina utaratibu wa kuomba fedha au zawadi ya aina yeyote kwa Mkuu wa Chuo au Mtu yoyote kama sharti la kupata huduma/msaada fulani.
Ni imani yetu kwamba wakati Baraza likiendelea na uchunguzi wa kuwabaini matapeli hao ili kuwachukulia hatua za kisheria, Wadau wetu wataongeza umakini na kuchukua tahadhari binafsi na watu wa namna hiyo.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji – NACTE
01 Septemba, 2016.
Rais Magufuli Afungua Mkutano Mkuu Wa Wahandisi, Atembelea Kikosi Cha Anga Majumba Sita Ukonga
Na Sheila Simba-MAELEZO
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewataka
wahandisi nchini kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuiwezesha nchi
kufikia uchumi wa kati kupitia ujezi na uendelezaji viwanda.
Amesema hayo leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa 14 wa Bodi ya Wahandisi Nchini,na kuwaasa kutumia taaluma yao kusaidia nchi kufikia uchumi wa kati ili kuleta maendeleo kwa haraka kwa watanzania.
“mkiamua nchi iende kwenye uchumi wa kati inawezekana lakini kama mtaamua isiendi pia inawezekana hivyo basi uzalendo unahitajika katika kufanya kazi na kufikia malengo tuliyojiwekea,”Alisema Rais Magufuli.
Aidha amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano,kujitambua na kuaacha ubinafsi miongoni mwao hasa kwenye utendaji kazi na miradi ya maendeleo.
“Tumemsikia waziri akisema serikali inamapango wa kukarabati na kununua meli mbili, wahandisi jiulizeni mmejipangaje kutumia fursa hii kwa kuomba tenda na naamini serikali haiwezi kukataa ombi hasa kwa wahandisi wa ndani”Alisema Rais Magufuli
Akimkaribisha rais Magufuli katika mkutano huo waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa alisema kuwa licha sekta ya miundo mbinu kufanya vizuri hasa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami,Serikali itaendelea kulipa kipaumbele ujenzi wa barabara kuanzia viijiji,Halmashauri na za mikoa.
“serikali inafanya jitahada kujenga miondo mbinu imara ili kurahisisha usafiri wa kutoka sehemu moja kwenda nyinfine na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma umekamilika kwa asilimia 98,” Alisema Prof. Mbarawa.Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Prof.Ninatubu Lema amemuomba Rais kutoa nafasi kwa wahandisi wa ndani kushiriki katika miradi mikubwa ili kujifunza kupitia miradi hiyo.
Aidha Mhandisi Lema kwa niaba ya bodi hiyo wametoa kiasi cha fedha shilingi milioni 100 kwaajili ya kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule za sekondari nchini.akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mhe.Paul Makonda alitangza tarehe mosi oktoba kuwa siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dae Es Salaam.
“Katika kuhakikisha miundo mbinu inakua safi natangaza rasmi hapa tarehe mosi oktoba itakua ni siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dar Es Salaamu na kampeni hiyi itaitwa MTI WANGU”alisema Makonda
Amesema hayo leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa 14 wa Bodi ya Wahandisi Nchini,na kuwaasa kutumia taaluma yao kusaidia nchi kufikia uchumi wa kati ili kuleta maendeleo kwa haraka kwa watanzania.
“mkiamua nchi iende kwenye uchumi wa kati inawezekana lakini kama mtaamua isiendi pia inawezekana hivyo basi uzalendo unahitajika katika kufanya kazi na kufikia malengo tuliyojiwekea,”Alisema Rais Magufuli.
Aidha amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano,kujitambua na kuaacha ubinafsi miongoni mwao hasa kwenye utendaji kazi na miradi ya maendeleo.
“Tumemsikia waziri akisema serikali inamapango wa kukarabati na kununua meli mbili, wahandisi jiulizeni mmejipangaje kutumia fursa hii kwa kuomba tenda na naamini serikali haiwezi kukataa ombi hasa kwa wahandisi wa ndani”Alisema Rais Magufuli
Akimkaribisha rais Magufuli katika mkutano huo waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa alisema kuwa licha sekta ya miundo mbinu kufanya vizuri hasa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami,Serikali itaendelea kulipa kipaumbele ujenzi wa barabara kuanzia viijiji,Halmashauri na za mikoa.
“serikali inafanya jitahada kujenga miondo mbinu imara ili kurahisisha usafiri wa kutoka sehemu moja kwenda nyinfine na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma umekamilika kwa asilimia 98,” Alisema Prof. Mbarawa.Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Prof.Ninatubu Lema amemuomba Rais kutoa nafasi kwa wahandisi wa ndani kushiriki katika miradi mikubwa ili kujifunza kupitia miradi hiyo.
Aidha Mhandisi Lema kwa niaba ya bodi hiyo wametoa kiasi cha fedha shilingi milioni 100 kwaajili ya kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule za sekondari nchini.akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mhe.Paul Makonda alitangza tarehe mosi oktoba kuwa siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dae Es Salaam.
“Katika kuhakikisha miundo mbinu inakua safi natangaza rasmi hapa tarehe mosi oktoba itakua ni siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dar Es Salaamu na kampeni hiyi itaitwa MTI WANGU”alisema Makonda
Kutoka Rujewa/mbarali Katika Kupatwa kwa Jua
LEO Septemba Mosi, watalii na wanaanga kutoka mataifa mbalimbali duniani wakiwemo wanafunzi wa shule wameungana kushuhudia tukio kubwa na la kihistoria la kupatwa kwa jua katika Kata ya Rujewa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Ikumbukwe kuwa tukio kama hilo la
kupatwa kwa jua lilitokea Julai 31,1962 takribani miaka 50 iliyopita na
tukio lingine lilitokea Aprili 18, 1977, na wataalamu wa anga
wanabainisha kuwa tukio kama hilo litatokea tena hapa nchini Mei 21,
2031.
Tukio hili la kupatwa kwa jua katika
eneo hilo la Kata ya Rujewa litatokea leo kuanzia majira ya saa 4:17
asubuhi ambapo eneo hilo litaonekana kwa asilimia 90 hadi umbali wa
kipenyo cha kilometa 100.
Serikali ya Wilaya ya Mbarali mkoani
Mbeya ambayo itakuwa mwenyeji katika kushudia tukio kubwa na la
kihistoria la kupatwa kwa jua, imewahakikishia ulinzi na usalama wa
kutosha wageni wote watakaojumuika leo kushuhudia tukio hilo.
Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune
anaeleza kuwa ni umbali wa Kilometa 3.5 kutoka Barabara kuu ya Iringa
hadi Mbeya ili kulifikia eneo hili lililopendekezwa na wana anga kuwa
mahali sahihi pakushuhudia tukio hilo.
Ili kuweza kutazama tukio hilo la
kupatwa kwa jua kwa uzuri zaidi wataalamu wa anga wameeleza kuwa tayari
wamefanya maandalizi ya vifaa maalumu kwa ajili ya tukio hilo.
Madalali wa NHC wavamia ofisi ya gazeti la Tanzania Daima linalomilikiwa na Freeman Mbowe na Kuanza Kutoa Vitu Nje
Madalali
wa NHC wamefika katika ofisi za gazeti la Tanzania Daima asubuhi hii
na kuanza kutoa vifaa ofisini kutokana na deni la pango la mmiliki wa
gazeti hilo, Freeman Mbowe.
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Neville Meena amesema wako kwenye msukusuko mkubwa lakini wanafanya jitihada za kukabiliana na hali hiyo ili kuhakikisha uzalishaji wa gazeti unafanyika kama kawaida.
Rais Magufuli apongezwa kwa kupambana na rushwa na kujenga mazingira bora zaidi kwa uwekezaji nchini
Mwenyekiti
wa Taasisi inayoshughulikia masuala ya Afrika (Africa Matters Limited)
Mhe. (Baroness) Lynda Chalker wa Wallasey - Uingereza, amempongeza Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi
kubwa alizozifanya kupiga vita rushwa na kujenga mazingira bora zaidi
kwa uwekezaji.
Mhe.
Lynda Chalker ametoa pongezi hizo jana tarehe 31 Agosti, 2016 Ikulu
Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli
kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo hali ya uwekezaji hapa nchini.
"Mhe
Rais amefanya uamuzi sahihi wa kupiga vita rushwa na kuiweka nchi hii
katika njia mpya ya uwekezaji mzuri na hicho ndicho tumekuwa
tukikizungumza, nimejitahidi kutoa ushauri wangu wa namna mimi na
kampuni yangu binafsi tunaweza kumsaidia, nionavyo mambo yanakwenda
katika mwelekeo mzuri" Amesema Mhe. Lynda Chalker.
Kwa
Upande wake Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Lynda Chalker kwa ushauri na
dhamira yake ya kutaka Tanzania ipige hatua kimaendeleo na amemuomba
kutumia ushawishi wake kuwahamasisha wawekezaji mbalimbali kutoka nchini
Uingereza na kwingineko duniani kuja kuwekeza nchini Tanzania ili
kuharakisha zaidi maendeleo.
Hata hivyo Dkt. Magufuli amesema wawekezaji wanaokuja Tanzania hawana budi kuwa wawekezaji makini.
"Ninawakaribisha
wawekezaji makini kutoka Uingereza na mahali popote dunia, lakini
nisingependa kupata wawekezaji wababaishaji" Amesisitiza Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
31 Agosti, 2016
Waziri Mwinyi: Mipaka ya Tanzania iko Salama.
Na: Lilian Lundo- Maelezo
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi
amewahakikishia watanzania kwamba mipaka ya Tanzania ni salama.
Mhe.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika kipindi cha Tunatekeleza
kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) alipokuwa akieleza mikakati
ya wizara hiyo katika kuhakikisha mipaka ya Tanzania iko salama.
“Nchi
iko salama, mipaka ya nchi iko shwari, ziko changamoto chache za nchi
zinazotuzunguka kuwepo katika machafuko mfano Burundi hivyo wananchi
wake kukimbilia Tanzania,” alifafanua Mhe. Dkt. Mwinyi.
Amesema
Tanzania sio kisiwa, imejiunga na jumuiya mbali mbali kama Jumuiya ya
Afrika Mashariki, Jumuiya ya Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Umoja wa
Mataifa hivyo kupitia Jumuiya hizo Tanzania hupata maelekezo ya
kuwapokea wakimbizi kutoka nchi zenye machafuko.
Hata
hivyo Mhe. Dkt. Mwinyi amesema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inahakikisha wakimbizi wanaoingia
nchini wanafuata utaratibu unaotakiwa bila kuvunja sheria za nchi.
Pia
ameeleza kuwa Tanzania inaendelea na mazungumzo ya amani na nchi ya
Malawi juu ya mgogoro wa umiliki wa Ziwa Nyasa baina ya nchi hizo mbili
ili kupata ufumbuzi wa amani, ambapo mazungumzo hayo ya yanaongozwa na
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William
Mkapa.
Aidha,
Mhe. Dkt. Mwinyi amesema kuwa kutokana na Wizara hiyo kufanya vizuri
katika Ulinzi na Amani ya Nchi, Jumuiya ya Umoja wa Afrika na Jumuiya ya
Umoja wa Mataifa imeiomba nchi ya Tanzania kutoa Ulinzi wa Amani kwa
nchi za Sudani, Kongo na Lebanoni kutokana na machuko yanayoendelea
katika nchi hizo.
Vile
vile ameeleza kuwa, ushiriki wa Jeshi la Tanzania katika nchi zenye
machafuko kunaisaidia Jeshi hilo kupata mafunzo ya kivita kutokana na
Tanzania kuwa ni nchi ya amani hivyo kufanya baadhi ya wanajeshi
kutoshiriki mafunzo ya uhalisia ya kivita tangu wanapoajiriwa mpaka
kustaafu.
Kamati ya Bunge yaibana Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
Wabunge
wameibana Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) kwa
kuongeza posho na kufikia jumla ya Sh1 bilioni katika kipindi kifupi
kiasi ambacho hakilingani na kazi wanayoifanya.
Kwa
kipindi kirefu, bodi hiyo imekuwa ikitupiwa lawama kwa kuchelewesha
mikopo, kushindwa kukusanya fedha za wanafunzi waliokopa na kutoa mikopo
kwa wanafunzi hewa.
Hivi
karibuni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce
Ndalichako alisema bodi hiyo imetoa fedha za kujikimu na mafunzo kwa
vitendo kwa zaidi ya wanafunzi hewa 1,000.
Hata
hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa HELSB, Abdul-Razaq Badru alijitetea mbele
ya kamati hiyo akisema ni mgeni katika bodi hiyo na kwamba wanaweka
mikakati mizuri ya kurekebisha mambo hayo ili kuhakikisha inafanya kazi
kwa weledi zaidi.
Wakizungumza
katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) cha
kukagua Ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
ya mwaka wa fedha 2014/15 ya bodi hiyo, wabunge hao walisikitishwa na
kitendo cha bodi hiyo kushindwa kukusanya zaidi ya Sh3 trilioni
walizowakopesha wanafunzi mbalimbali tangu ianze kutoa mikopo kwa
wanafunzi wa elimu ya juu.
Walisema isipobadilika katika utendaji wake, kuna haja ya Serikali kuivunja na kuchagua benki moja kusimamia shughuli hiyo.
“Mnatakiwa
kuongeza juhudi na mikakati ili kuhakikisha kwamba madeni yote
yanakusanywa kwa wakati la sivyo naona kuna haja ya Serikali kuivunja
bodi nakutafuta njia nyingine,” alisema Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Raisa Mussa.
Mbunge
wa Same Mashariki (Chadema), Naghenjwa Kaboyoka alihoji kwa nini pamoja
na bodi hiyo kuwa na mameneja 18 na wafanyakazi wa kudumu 144, bado
utendaji wao umekuwa siyo wakuridhisha.
“Kwa idadi yenu tulitegemea kupata ripoti inayojitosheleza na hata utendaji wenu ulitakiwa kuwa wa ufanisi zaidi,” alisema.
Akijitetea
zaidi, Badru alisema kuna changamoto nyingi zinazoikabili bodi yake
lakini kwa sasa wamepiga hatua kubwa katika ukusanyaji wa madeni kutoka
kwa wanufaika wa mfuko huo.
“Kwa mfano Mei mwaka huu tulikusanya kiasi cha Sh2 bilioni na Juni tulikusanya Sh6 bilioni,” alisema.
Aliongeza
kuwa ipo mikakati mingi ambayo wamejiwekea katika kuhakikisha kwamba
bodi hiyo inakusanya madeni kikamilifu kutoka kwa wadeni wake wote.
“Kwa
kupitia mikakati yetu, tumeweza kuongeza idadi ya wanafunzi ambao
tunawapa mikopo kutoka 42,729 hadi 123,783. Katika kipindi hicho fedha
za mikopo zimeongezeka kutoka Sh56 bilioni hadi kufikia Sh465.3
bilioni,” alisema.