Wakati
Jeshi la Polisi likisisitiza kupiga marufuku mikutano na maandamano ya
Chadema chini ya mwavuli wa Umoja wa Kupinga Udikteta nchini (Ukuta),
chama hicho kimepinga katazo hilo nakudai kuwa ni haramu kwa mujibu wa
Katiba ya nchi.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema katika
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Makao Makuu ya chama
hicho Mtaa wa Ufipa, jijini Dar es Salaam.
Kwenye
mkutano huo akiwa na Lawrance Masha, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani
(2005-2010) Lissu amesema, rais anayo nafasi ya kuzuia mikutano ya
hadhara kwa sharti la kupeleka hoja bungeni na kisha kujadiliwa na si
vinginevyo.
“Ipo
sheria ya kutangaza hali ya dharura, iliyotungwa mwaka 1995, hii
inamruhusu rais kupeleka hoja bungeni ya kutaka kutangaza hali ya
dharura kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu na kama Bunge likiridhia,
basi rais anatangaza, namshauri Magufuli afanye hivyo.
“Aitangazie
Tanzania na dunia kwa ujumla kuwa, nchi hii ipo katika hali ya hatari
na katika hali ya dharura, na kwamba mikutano yote itakuwa marufuku.
“Na
miezi mitatu ikiisha aende tena bungeni kuomba aongeze mingine.
Akifanya hivyo atakuwa hajavunja sheria na hata sisi tutamtii,” amesema Lissu.
Lissu
ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki amelitaka Jeshi la Polisi
kuacha kutoa matamko yanayoiingiza nchi katika utawala wa kidikteta.
Kauli
hiyo inakuja ikiwa ni siku moja tu, tangu jeshi hilo kupitia Nsato
Marijani, Kamishina wa Polisi, Operesheni na Mafunzo, litangaze kupiga
marufuku mikutano yote ya vyama vya siasa nchini, ikiwemo vikao vya
ndani vya vyama.
Katika
mkutano na wanahabari, makao makuu ya chama hicho, akiwa ameambatana na
Dk. Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa chama hicho, Profesa Mwesiga
Baregu, Mjumbe wa Kamati Kuu, pamoja na Masha amesema, Lissu amesema,
kamwe Chadema hakiwezi kuruhusu ukiukwaji wa katiba na sheria za nchi.
“Amri
ya jana ya polisi, wakipiga marufuku mikutano yote ya vyama vya siasa
ikiwemo vikao vya ndani ni muendelezo wa amri haramu na kitendo hicho
cha jana na vingine vilivyopita, ni mfano hai ya kwamba, nchi yetu
imeingia katika mfumo wa udikteta.
"Kwani,
kwa mujibu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1967;
udikteta ni utawala wa mtu mmoja au kikundi cha watu wachache
wanaofikiria kwamba, amri zao ndiyo sheria na wote wanaowapinga, hukiona
cha mtema kuni,” amesema Lissu.
Lissu
amesema kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya sasa pamoja na sheria zote
ikiwemo Sheria Na. 5 ya mwaka 1992 ya vyama vya siasa, Sheria ya Maadili
ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2007 pia sheria za Jeshi la Polisi, hakuna
mahali ambapo polisi au rais anaruhusiwa kupiga marufuku mikutano ya
kisiasa.
“Anayetakiwa
kujulishwa kuhusu uwepo wa maandamano na mikutano ya hadhara ni Mkuu wa
Polisi Wilaya (OCD) na kama kuna tatizo kwa muda huo, anaweza kuelekeza
isifanyike kwa muda fulani lakini siyo Rais Magufuli wala Nsato,” amesema.
Wakati Lissu akisema hayo, Masha amesema,
“nimekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwa miaka mitano, lakini sikuwahi
kupiga marufuku mikutano ya hadhara wala ile ya ndani. Nilifahamu kuwa,
kuna umuhimu wa watu kuzungumza, kukosoana na kuelimishana.
"Ni
vyema Rais Magufuli akajua, hii ni nchi ya kidemokrasia na kuna Katiba
na sheria ambazo kila mtu ni lazima afuate akiwemo yeye, matamko ya
kibabe ya Rais, Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la polisi ni kinyume
na sheria pamoja na Katiba yetu.”
Dk.
Mashinji, amesisitiza kuwa, Chadema kipo tayari kwa mazungumzo na
mamlaka yoyote ya serikali juu ya azma ya kufanya mikutano na
maandamano, ili mradi tu sheria na katiba ya nchi izingatiwe katika
mazungumzo hayo.
“Hatujafunga
milango ya mazungumzo na serikali, tunachosisitiza sisi ni kuwa hata
kama kuna mazungumzo yatafanyika, Katiba na sheria za nchi yetu lazima
zizingatiwe,” amesema Dk. Mashinji.
Viongozi
wa vyama vya upinzani nchini vimemshauri Rais John Pombe Magufuli
kuvifuta vyama vya upinzani kama anaona vinamsumbua anapofanya mambo
yake.
Hayo
yamesemwa leo na mwenyekiti mwenza wa UKAWA, James Mbatia ambapo
amesema kuwa kama Rais Magufuli anaona vyama vya upinzania vinamkera na
kumkwamisha anapotaka kufanya jambo basi serikali yake ipelekea mswada
kwa hati ya dharura bungeni ili kufanya mabadiliko katika sheria ya
vyama vya siasa na kuvifuta vyote.
Mbatia
amesema kuwa jambo hilo amelitafakari na kuwashirikisha viongozi
wenzake na huenda ikasaidia kwa sababu Rais Magufuli anaonekana kutaka
kuongoza kwa kutumia akili yake na hataki kukosolewa na mtu yeyote wala
chama chochote.
Katika
hatua nyingine, viongozi wa vyama vya upinzani wameitikia wito wa
viongozi wa dini uliowataka kurudi bungeni na wameahidi kuwa
watajadiliana na wanaamini watafikia muafaka na kurudi bungeni katika
mkutano ujao mwezi wa tisa.
Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza
wakati wa kuaga miili ya askari waliouawa katika eneo la Mbande, Temeke
baada ya kuvamiwa na majambazi .Ibada hiyo ya kuaga ilifanyika katika
Viwanja vya Polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu, akizungumza wakati wa
maombolezo na kuaga miili ya askari waliouawa katika eneo la Mbande,
Temeke baada ya kuvamiwa na majambazi.Ibada hiyo ya kuaga ilifanyika
katika Viwanja vya polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akipita kutoa
heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliyobeba miili ya askari
waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi katika eneo la Mbande,
Temeke ,bada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika viwanja vya polisi
vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akitoa mkono wa
pole kwa mmoja wa ndugu wa askari waliouawa baada ya kuvamiwa na
majambazi katika eneo la Mbande, Temeke ibada hiyo ya kuaga miili
ilifanyika katika viwanja vya polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini
Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ,
akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa askari waliouawa baada ya
kuvamiwa na majambazi katika eneo la Mbande, Temeke ,ibada hiyo ya
kuaga miili ilifanyika katika Viwanja vya Kambi Kuu ya Polisi iliyopo
barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
Askari
wakimsaidia mzazi wa mmoja wa askari waliouawa baada ya kuvamiwa na
majambazi katika eneo la Mbande, Temeke, ibada hiyo ya kuaga miili
ilifanyika katika viwanja vya polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini
Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amesema amri
ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mikutano ya nje na ndani ya vyama vya
siasa ni halali ambayo kila Mtanzania na mwanachama wa chama chochote
cha siasa anapaswa kuitii na kuizingatia na kwamba kutokufanya hivyo ni
kuvunja sheria za nchi.
Amesema
amri hiyo ni ya kudumu ambayo imelenga kuangalia na kufanya tathmini ya
hali ya nchi kutokana na viashiria mbalimbali vya uvunjifu wa amani
nchini ambavyo vimeanza kuonekana.
Dkt
Mwakyembe alikuwa akijibu swali kutoka kwa Kituo cha Televisheni cha
Taifa TBC 1 ambacho kilitaka kupata ufafanuzi kuhusiana na uhalali wa
kauli ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mikutano ya ndani na ya hadhara kwa
vyama vya siasa nchini.
“Jeshi
la Polisi ni chombo halali cha cha dola kilichoanzishwa kisheria chenye
wajibu wa kulinda usalama wa raia na mali zake ndani ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, na kuongeza kuwa uamuzi huo una lengo la kulinda
amani ya nchi na endapo kutakuwa na viashiria vya kutishia amani ya nchi
yetu lazima hatua za kisheria na kinidhamu zichukuliwe. Ni amri halali
na kila Mtanzania na mwanachama wa chama chochote nchini anapaswa kuitii
na kuizingatia na kwamba kwenda kinyume ni kukiuka sheria, ” alisisitiza Mhe. Mwakyembe.
Mhe.
Waziri amesema ni haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano ila
wanatakiwa kutoa taarifa Polisi ili waweze kutoa ulinzi wakati wa
mkutano huo na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi linaweza kuzuia mikutano
hiyo kwa sababu za kiusalama.
Mhe.
Waziri pia alisema sio kweli kuwa Mhe. Rais amezuia mikutano ya siasa,
bali alichofanya ni kudhibiti uendeshaji wa holela au huria wa shughuli
za siasa nje ya maeneo ya uchaguzi ya wanasiasa na kuongeza kuwa Mhe.
Rais amefanya hivyo kutokana na kiapo chake cha kuilinda, kuihifadhi na
kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taifa kwa ujumla.
“Mhe.
Rais hajapiga marufuku siasa, alichofanya ni kudhibiti uendeshaji
holela au huria wa shughuli za siasa nje ya maeneo ya uchaguzi ya
wanasiasa husika kuepusha shari na chuki na amefanya hivyo kutokana na
kiapo chake cha kuilinda, kuihifadhi na kuitetea Katiba ya Tanzania na
taifa kwa ujumla wake. Kwa hatua hiyo Mhe. Rais hajafunga milango ya
majadiliano. Milango iko wazi na tulitegemea wenzetu wangekuja na njia
mbadala na kulizungumzia hilo badala ya kuitisha maandamano ya nchi
nzima," alisema.
Mhe
Mhe. Waziri amevitaka vyama vya upinzani nchini kukaa na kuzungumza na
Serikali na kuacha kufanya vitendo vya kutishia uvunjifu wa amani kama
kuitisha maandamano kwa nchi nzima.
“Njooni
tukae tuzungumze tupime ushauri wenu, hili ni taifa letu sote na
milango iko wazi, tuache kuchochea vitendo vya uvunjifu wa amani kama
ambavyo inavyoonekana nchini hivi sasa,” alisisitiza.
Amasema
Sheria ya Vyama vya siasa hairuhusu kufanyika kwa maandamano kwa nchi
nzima, kufanya hivyo ni kuchochea wananchi kuasi “civil disobedience” ni
kinyume cha sheria na serikali haiwezi kuivumilia hali hiyo.
Mhe.
Waziri ametoa wito kwa Watanzania wote kutoshiriki maandamano ya Ukuta
ambayo alisema hayatakuwa na tija kwa nchi bali kuleta vurugu katika
jamii.
Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaukumbusha Umma kuwa mitihani ya
Taifa ya Darasa la 4 na Kidato cha 2 itaendelea kuwepo na mwaka huu
itafanyika kama kawaida.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo ameyasema hayo leo,
jijini Dar es Salaam alipokuwa akikanusha taarifa za kutokuwepo kwa
mitihani hiyo kwa mwaka 2016.
“Napenda
niukumbushe Umma kuwa mitihani hii ni muhimu sana katika ufuatiliji wa
maendeleo ya wanafunzi wetu. Kwa hiyo mitihani yote miwili itaendelea
kuwepo na mwaka huu itafanyika kama kawaida. Kama kuna watu wanawaambia
kuwa haitafanyika wawapuuze kabisa,” alifafanua Dkt. Akwilapo.
Dkt.
Akwilapo aliendelea kwa kusema kuwa, mitihani hiyo ina umuhimu mkubwa
katika kupima maendeleo ya mwanafunzi kwa lengo la kufanya maendeleo ya
kitaaluma. Aidha kwa wanafunzi ambao watakuwa hawajafikia viwango vya
ufaulu vilivyowekwa watatakiwa kukariri darasa au kidato.
Amebainisha
kuwa Baraza la Mitihani ndilo lenye jukumu la kushughulikia maandalizi
ya mitihani hiyo ikiwa ni pamoja na utungaji, uchapaji, ufungaji na
usafirishaji hadi ngazi ya Mkoa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) ikiwa na majukumu ya kuhakikisha kuwa
uendeshaji na usahihishaji wa mitihani hiyo unafanyika kikamilifu.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewapangia vyuo
wanafunzi wa programu maalum ya ualimu chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
ambao hawakupata nafasi ya vyuo katika awamu ya kwanza, walioagizwa
kuomba mafunzo kulingana na sifa zao kupitia Baraza la Taifa la Mafunzo
ya Ufundi (NACTE).
Hayo
yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo
leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa kuhusu wanafunzi
wanaosoma stashahada maalum ya ualimu wa sayansi chuo kikuu cha Dodoma.
“Mtakumbuka
tuliagiza kwamba wanafunzi ambao walikosa sifa za kujiunga na ualimu wa
sayansi waliombwa kuomba mafunzo yanayolingana na ufaulu wao kupitia
NACTE, Lakini baada ya taarifa hiyo tulipokea maombi mengi kutoka kwa
vijana hawa wakiomba kupangiwa vyuo moja kwa moja na Wizara, wizara
imetafakari na kuamua nao wapangiwe vyuo vya Serikali,” alifafanua Dkt.
Akwilapo.
Aliendelea
kusema kuwa, wanafunzi ambao waliachwa awamu ya kwanza na kupangiwa
katika awamu ya pili ni wanafunzi 290 ambao walikuwa wakisomea programu
ya stashahada ya ualimu wa sekondari na wanafunzi 1,181 ambao walikuwa
wakisomea stashahada ya ualimu wa msingi.
Dkt.
Akwilapo amesema kuwa Wizara imeamua kuwapangia wanafunzi hao vyuo
kutokana na kuonyesha nia ya dhati ya kusomea ualimu ambapo wanafunzi
hao wamepangiwa vyuo vya ualimu vya Marangu na Tabora.
Aidha,
Dkt. Akwilapo ameeleza kuwa wanafunzi hao watajigharamia masomo yao
kulingana na viwango vya ada vilivyowekwa na Serikali. Pia amewataka
kutembelea tovuti ya wizara ya hiyo ambayo ni www.moe.go.tz ili kuona
vyuo walivyopangiwa.
Mnamo
tarehe Mei 28, 2016 Serikali iliwarejesha nyumbani wanafunzi 7,805
waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati
katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Katika mchujo wa awamu ya kwanza wanafunzi
382 ndio waliokuwa na sifa ya kuendelea na masomo chuo kikuu cha UDOM
na wengine 4,586 walipangiwa vyuo vya ualimu vya Serikali.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewapangia vyuo
wanafunzi wa programu maalum ya ualimu chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
ambao hawakupata nafasi ya vyuo katika awamu ya kwanza, walioagizwa
kuomba mafunzo kulingana na sifa zao kupitia Baraza la Taifa la Mafunzo
ya Ufundi (NACTE).
Hayo
yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo
leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa kuhusu wanafunzi
wanaosoma stashahada maalum ya ualimu wa sayansi chuo kikuu cha Dodoma.
“Mtakumbuka
tuliagiza kwamba wanafunzi ambao walikosa sifa za kujiunga na ualimu wa
sayansi waliombwa kuomba mafunzo yanayolingana na ufaulu wao kupitia
NACTE, Lakini baada ya taarifa hiyo tulipokea maombi mengi kutoka kwa
vijana hawa wakiomba kupangiwa vyuo moja kwa moja na Wizara, wizara
imetafakari na kuamua nao wapangiwe vyuo vya Serikali,” alifafanua Dkt.
Akwilapo.
Aliendelea
kusema kuwa, wanafunzi ambao waliachwa awamu ya kwanza na kupangiwa
katika awamu ya pili ni wanafunzi 290 ambao walikuwa wakisomea programu
ya stashahada ya ualimu wa sekondari na wanafunzi 1,181 ambao walikuwa
wakisomea stashahada ya ualimu wa msingi.
Dkt.
Akwilapo amesema kuwa Wizara imeamua kuwapangia wanafunzi hao vyuo
kutokana na kuonyesha nia ya dhati ya kusomea ualimu ambapo wanafunzi
hao wamepangiwa vyuo vya ualimu vya Marangu na Tabora.
Aidha,
Dkt. Akwilapo ameeleza kuwa wanafunzi hao watajigharamia masomo yao
kulingana na viwango vya ada vilivyowekwa na Serikali. Pia amewataka
kutembelea tovuti ya wizara ya hiyo ambayo ni www.moe.go.tz ili kuona
vyuo walivyopangiwa.
Mnamo
tarehe Mei 28, 2016 Serikali iliwarejesha nyumbani wanafunzi 7,805
waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati
katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Katika mchujo wa awamu ya kwanza wanafunzi
382 ndio waliokuwa na sifa ya kuendelea na masomo chuo kikuu cha UDOM
na wengine 4,586 walipangiwa vyuo vya ualimu vya Serikali.
Baada ya vocalist, Rich Mavoko kusaini WCB ya Diamond, huwenda msanii
wa muziki wa R&B kutoka Morogoro, Belle 9 na yeye akasaini ndani ya
label hiyo.
Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Bugger Movie Selfie’
ameonekana akifanya mazoezi ya bendi ya Diamond katika ofisi za WCB. Kwa mujibu wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Belle pamoja na
Diamond wameonekana wakiimba wimbo ‘Mdogo Mdogo’ kwa pamoja huku
wakicheza. Hatua hiyo imefufua matumaini mapya kwa mashabiki wa kumuziki kuona
huweza WCB ikamsaini msanii hiyo kama ilivyofanya kwa Rich Mavoko. Kwa sasa label ya WCB ina wasanii wanne, Harmonize, Rich Mavoko, Raymond aka Rayvany pamoja Queen Darlin.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezitumia
salamu za pole familia, ndugu, jamaa na marafiki wa watu 12 waliopoteza
maisha kufuatia ajali mbili zilizotokea katika eneo moja la VETA Dakawa,
Tarafa ya Dumila, Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.
Ajali
ya kwanza imetokea majira ya saa 11:30 jioni ya tarehe 30 Juni, 2016
ambapo watu 5 wamefariki dunia kufuatia malori mawili, mojawapo likiwa
na shehena ya mafuta kugongana na kisha kuwaka moto, na ajali ya pili
ikatokea hapohapo majira ya saa 10:00 alfajiri ya tarehe 01 Julai, 2016
baada ya basi la kampuni ya Otta High Class kuligonga lori la mafuta
lililokuwa likiungua moto na kusababisha vifo vya watu 7 mpaka sasa.
Katika
salamu zake kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe,
Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshituko na masikitiko taarifa za
vifo vya watu hao ambao licha ya taifa kupoteza nguvu kazi muhimu,
ndugu, jamaa na marafiki wamepoteza watu waliowategemea na wapendwa wao.
“Ndugu
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe naomba unifikishie salamu
zangu za pole kwa wote waliopatwa na msiba na uwaambie naunga nao katika
kipindi hiki kigumu cha majonzi.
“Pia nawaombea wawe na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu na Mwenyezi awapumzishe marehemu wote mahali pema peponi, Amina”amesema Rais Magufuli.
Rais
Magufuli pia amewaombea majeruhi wote waliolazwa hospitali na wale
wanaoendelea kupata matibabu wakiwa majumbani, kupona haraka ili
waendelee na kazi zao za kila siku.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa halmashauri na Maofisa
Elimu nchini kutowaondoa katika nyadhifa zao Waratibu wa Elimu Kata na
Wakuu wa shule za sekondari wasiokuwa na shahada, walimu wakuu wa shule
za msingi wasiokuwa na diploma badala yake wawahamasishe kwenda kusoma.
“Maofisa
Elimu na Wakurugenzi msije mkawaondoa wale walimu wakuu kwa zile sifa
nilizosema bado muda ukifika tutatangaza.Msije mkawakurupusha sasa hivi
waacheni waendelee na kazi zao tutatoa muda ili wajipange viziri,” aliema.
Agosti
20 mwaka huu Waziri Mkuu alisema Waratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata
na Wakuu wa shule za sekondari wanatakiwa kuwa na shahada huku walimu
wakuu kwenye shule wanatakiwa kuwa na diploma.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Agosti 24, 2016) wakati
akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
kiwanja cha Mandela katika jimbo la Sumbawanga mjini.
Alisema
Mratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata ni lazima awe na shahada ili
aweze kutekeleza majukumu yake ya kusimamia utolewaji wa elimu katika
shule za sekondari na msingi.
“Wakuu
wa shule za sekondari na waratibu wa elimu kata wasiokuwa na shahada
wasiondolewe katika nafasi zao kabla ya kupewa nafasi ya kwenda
kujiendeleza kwa masomo ili waweze kuwa na vigezo vya kuendelea kushika
nyadhifa hizo,” alisema.
Alisema
katika kuboresha maslahi ya walimu Serikali imetenga zaidi ya sh.
bilioni tano kwa mwezi ambazo ni posho ya madaraka. Waratibu Elimu Kata
wanapewa sh 250,000 kwa mwezi huku Wakuu wa shule za sekondari na walimu
wakuu katika shule za msingi wanapewa sh. 200,000.
Waziri
Mkuu alisema badala ya kuwaondoa kwenye nyadhifa hizo ni vema
Wakurugenzi wakawahamasisha walimu hao kwenda kusoma ili na wao
wanufaike na posho ya madaraka iliyoanza kutolewa na Serikali hivi
karibuni.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka wazazi na walezi kwenda
kuwaandisha watoto wenye umri wa miaka mitano katika shule za awali
ambapo watapata fursa ya kujengewa msingi mzuri wa masomo kabla ya
kuanza darasa la kwanza.
Pia
aliagiza shule zote za msingi nchini zisizokuwa na madarasa ya awali
kuhakikisha wanaanzisha madarasa hayo haraka na kuanza kutoa elimu hiyo.