Thursday, 25 August 2016
Wednesday, 24 August 2016
Kingunge awaomba Mwinyi, Mkapa kuzungumza na Rais Magufuli
Kada
huyo ambaye alijivua uanachama wa CCM Oktoba mwaka jana kwa madai
kwamba chama hicho kinaendeshwa kwa maslahi binafsi, amesema kuwa
mazungumzo hayo yataepusha uvunjifu wa amani nchini.
Kingunge
ambaye ameomba kwenye jopo hilo wawepo mawaziri wakuu wastaafu, Edward
Lowassa na Fredrick Sumaye na wanapaswa kutambua wajibu wao kwa
Watanzania na kwamba hawapaswi kukaa kimya wakati hali kama hiyo
inaendelea nchini.
Jeshi La Polisi Lahusisha Mauaji ya Polisi Wanne na Sakata la Oparesheni UKUTA Lapiga Marufuku Mikutano yote ya Ndani ya Vyama vya Siasa
KUFUATIA
mauaji ya askari wanne yaliyotokea Kata ya Mbande Temeke kwa watu
wanaodhaniwa ni majambazi kuvamia benki ya CRDB na kuwaua askari hao kwa
kutumia silaha za moto jeshi la Polisi limetangaza kiama na kuwataka
wahusika wote kujisalimisha.
Katika
hatua nyingine jeshi la polisi limehusisha tukio hilo na Umoja wa
Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA) kufuatia matamko ya baadhi ya viongozi
wa kisiasa ambao wamesikika katika majukwaa ya kisiasa wakihamasisha
wafuasi wao wawashambulie askari wa Jeshi la Polisi.
Kauli
hiyo imetolewa na Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi
nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), wakati akizungumza waandishi wa
habari Dar es Salaam leo mchana ambapo pia alikiri kuwa mazoezi
yanayofanywa na polisi yamelenga kukabiliana na Ukuta.
Akizungumza kwa hisia CP Mssanzya pia amepiga
marufuku mikutano ya ndani yenye viashiria vya uchochezi na hata
ikifanyika kwenye majukwaa watamshusha muhusika na kumfikisha kwenye
mkono wa sheria.
"Kwasababu hiyo basi,kwa
hali ya kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu kuvunja sheria na
kupambana na askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi nchini
linapiga marufuku mikutano yote ya ndani" amesema.
Amesema Jeshi hilo limebaini
kwamba mikutano hiyo imekuwa ikitumika kuchochea wananchi na
kuwahamasisha kuvunja sheria za nchi na kufanya mapambano na jeshi la
polisi
Aidha
CP Mssanzya aliwataja askari waliouawa katika tukio hilo wakati
wakibadilishana lindo kuwa ni E.5761 CPL Yahya, F.4660 CPL Hatibu, G
9524 PC Tito na G 9996 PC Gastoni na raia wawili waliojeruhiwa
aliowataja kuwa Ali Chiponda na Azizi Yahya wote wakiwa wakazi wa
Mbande.
"Katika
tukio hilo majambazi ambao idadi yao haikufahamika walifanikiwa kupora
silaha mbili aina ya MSG na lisasi 60 na hakuna pesa wala mali ya benki
hiyo kuibiwa au kuharibiwa, ni dhahiri kuwa waharifu hao walikuwa na
kusudio moja tu la kuwashambiulia askari polisi, " alisema.
Alisema
katika hali ya kushangaza baada ya tukio hilo kuna baadhi ya watu
waliandika mitandaoni kubeza na kukeji mazoezi ya kawaida ya jeshi la
polisi na wengine waliandika ujembe wa kushabikia tukio hilo la kuuawa
kwa askari polisi huku wengine wakidiriki kuandika ujumbe unaosema
endapo watapigwa na polisi Septemba1 mwaka huu basi viongozi wa jeshi hilo wawaondoe askari wanaoishi uraiani na kuwarudisha kambini.
Aliongeza kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kukabiliana na matukio yote ya uvunjifu wa amani nchini.
Taarifa Kwa Umma Kutoka Wizara ya Elimu, sayansi na teknolojia
Kwa muktadha huo, Wizara inawaagiza wachapishaji wote wa vitabu vya Darasa la Nne hadi Darasa la Saba ambavyo vina ithibati ya EMAC kuviwasilisha Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa ajili ya kufanyiwa tathmini. Ili kufanikisha zoezi hili nakala nne (4) za kila chapisho ziwasilishwe kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania kabla ya tarehe 30 septemba, 2016. Baada ya muda huo kupita, vitabu vyote ambavyo havitakuwa vimewasilishwa na kuhakikiwa na Taasisi hiyo vitafutwa katika orodha ya vitabu vyenye ithibati.
Baada ya zoezi la uhakiki kukamilika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na OR – TAMISEMI, itafanya ufuatiliaji kwenye shule na maduka ya vitabu ili kuhakiki utekelezaji wa agizo hili.
Aidha, hatua stahiki zitachukuliwa kwa wauzaji/wachapishaji watakaoendelea kuuza vitabu vitakavyokuwa vimefutwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Ufafanuzi Kuhusu Wasiokopeshwa Mikopo Na HESLB Kudaiwa
1.0 UTANGULIZI
Kumekuwepo
na taarifa zilizotolewa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya
habari, hasa gazeti la Jamboleo toleo namba 2541 la 23 Agosti, 2016
kuhusu Bodi ya Mikopo kuwadai wasionufaika na mikopo. Taarifa hizi
zinalenga kuleta hofu na mkanganyiko usiokuwa wa lazima kwa wadau.
Kufuatia hatua hiyo Bodi ya Mikopo inapenda kutoa ufafanuzi wa suala
hili kama ifuatavyo:-
2.0 MADAI KUHUSU KUDAIWA MIKOPO KWA WALE WASIONUFAIKA
Bodi
ya Mikopo inapenda kuufahamisha Umma kuwa ‘database’ yake ya wanufaika
wa mikopo ina taarifa zote muhimu zilizo sahihi. Hii inatokana na
utunzaji mzuri wa kumbukumbu za ukopeshaji kuanzia hatua ya utoaji
mikopo (loan allocation and disbursement) hadi urejeshaji wake (loan
repayment). Kutokana hamasa na elimu inayotolewa, kumekuwepo na
mwitikio mkubwa wa wanufaika wa mikopo na waajiri wao kujitokeza na
kuanza kurejesha mikopo. Hivyo, katika utekelezaji wa jukumu hilo,
tumebaini kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wadaiwa kwamba ama
hawakuwahi kukopa au hawajawahi kufikia kiwango cha elimu ya juu.
Hadi
sasa, imebainika kuwepo kwa baadhi ya wanufaika ambao wanadai hawakujua
iwapo fedha walizopatiwa na serikali wakati huo zilikuwa za mkopo. Pia
kuna wachache ambao vyeti vyao vilitumiwa na ndugu zao kwa ajili ya
masomo ya elimu ya juu. Katika hali hii, mdaiwa atalazimika kumtaja mtu
halisi anayepaswa kukatwa deni hilo ili Bodi iweze kusitisha makato hayo
kwake.
Ili kupata ufumbuzi wa malalamiko hayo, Bodi inawataka walalamikaji kuzingatia yafuatayo:
2.1
Kwa mtu anayedai kwamba hajasoma elimu ya juu kwa ufadhili wa serikali
au Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu; mtu huyu awasilishe
vielelezo vinavyodhihirisha kuwa hakusomeshwa kwa ufadhili wa serikali.
2.2
Kwa mtu anayedai amekatwa mshahara ingawa hajawahi kufikia kiwango cha
elimu ya juu; mtu huyo anapaswa kuwasilisha vielelezo vya kiwango cha
elimu yake.
2.3
Iwapo kuna mnufaika wa mkopo anadai amekatwa zaidi ya kiwango cha mkopo
anaodaiwa; mnufaika huyo anapaswa kuwasilisha vielelezo
vinavyothibitisha kumaliza kurejesha deni lake. Itakapothibitika kuwa
kuna makato zaidi yalifanyika, basi kiasi kilichozidi kitarejeshwa kwa
mhusika.
3.0 HITIMISHO
Bodi
inapenda kuwahakikishia wadau wake kuwa imetunza vizuri taarifa zote
muhimu za wanufaika wa mikopo ambazo ndizo zinazotumika kwenye zoezi la
urejeshaji wa mikopo. Kasoro ndogo ndogo zinazojitokeza zinatatuliwa
kwa kufanya rejea kwenye kumbukumbu zilizopo.
Aidha,
Bodi inaendelea kuwahimiza wanufaika wote wa mikopo ambao hawajaanza
kurejesha mikopo yao kuhakikisha wanawasilisha taaifa zao ofisi za Bodi
au wanajaza taarifa zao kweye fomu ‘Loan Inquiry Form’ iliyopo kwenye
tovuti ya Bodi na kuituma kwa anuani ya barua pepe info@heslb.go.tz ili
kila mmoja ajulishwe deni lake na kuanza kurejesha.
Kwa
mnufaika anayetaka kuanza kurejesha mkopo wake baada ya kuwa amepata
taarifa ya deni lake; aweke fedha kwenye akaunti za Benki zifuatazo na
kisha kuwasilisha hati ya malipo:
A/C No. 2011100205 – NMB
A/C No. 01J1028467503 – CRDB
A/C No. CCA0240000032 – TPB
Imetolewa na:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Agosti 24, 2016
VIDEO: Alichokiongea Waziri Nchemba baada yakufika eneo walipouwawa Askari Polisi Dar
Tukio
la kuwawa kwa Askari Polisi wanne katika shambulio lililofanywa na watu
wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi usiku wa August 23 2016 zimeendelea
kuchukua headline ambapo safari hii Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba alifika eneo la tukio ambapo pia Ayo TV ilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano.
Waziri Nchemba amesema…>>>’Kumetokea
shambulio la uvamizi lenye nia ya uovu ambalo limeua askari wanne,
vijana wamefika na wataendelea na msako kuhakikisha waharifu wote
wametiwa nguvuni‘
‘Tukio
lilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ambapo bado uchunguzi
unaendelea na taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi, kifupi ni
kwamba shambulio lilifanywa kwa kutumia usafiri wa pikipiki na niwakati
vijana wakibadilishana lindo lakini niwahakikishie wananchi kuwa
watuhumiwa wote watatiwa hatiani‘ –Waziri Mwigulu Nchemba
Tuesday, 23 August 2016
Polisi 3 wauawa na Majambazi Mbande Dar
Majambazi wamevamia Benki ya CRDB Mbande Mbele ya Chamanzi na Kuua Polisi 3..
Tutakuletea habari kamili muda sio mrefu,,
Watanzania 56 watekwa na kuuawa na askari wanaodhaniwa kuwa wa nchi jirani
Habari wakuu,
Kuna habari nimeona ITV sasa hivi kuwa kuna watanzania 56 maeneo ya Kagera wameuawa na wanajeshi wanaodhaniwa kutoka Rwanda.
Ni kweli nachokiona au ni miujiza hii?
Ndo huyu tunayemuita Rafiki wetu na tunataka tuite wataalamu wake wa IT au itakua ni watu wenye nia mbaya wanaotaka kuharibu mahusiano baina yetu na Rwanda.
Sijaelewa wakuu embu nielewesheni.
=========
Zaidi ya watanzania 56 katika vijiji vya Chamchuzi na Buguluka vilivyoko katika kata ya Bwelanyange iliyoko wilayani Karagwe mkoani Kagera waliokuwa wakijihusisha na shughuli za uvuvi ndani ya mto Kagera na ziwa hiema wanadaiwa kutekwa na kuuawa kikatili na watu wanaodhaniwa kuwa ni askari wa nchi jirani Rwanda ambao mara kwa mara hufanya doria ndani ya mto huo na ziwa hilo.
Vitendo vya watanzania kutekwa na kuuwawa kikatili vimeshtua mkuu wa wilaya ya Karagwe Godfrey Muheruka anayelazimika kufanya ziara ya kutembelea mwalo wa Rukombe ambao hutumiwa na wananchi wa vijiji vya Chamchuzi na Buguluka na baadae kukutana na wananchi wa vijiji hivyo viwili miongoni mwao wakiwemo wajane 59 ambao wanaume wao wanasadikiwa kuuwawa, baadhi ya watanzania walionusurika kifo wenye majeraha mbalimbali ya risasi na mtanzania aliyekombolewa hivi karibuni toka nchini Rwanda ambao wametoa shuhuda mbalimbali.
Afisa mtendaji wa kata ya Bwelanyange Nicolaus Lubambala kwenye taarifa yake iliyosomwa na Godwin Mbeikya ambaye mratibu elimu kata ya Bwelanyange ameeleza kuwa matukio ya watanzania kuuwawa yamekuwa yakiongezeka kila kunapokucha, kufuatia matukio hayo mkuu wa wilaya ya Karagwe Godfrey Muheruka amepiga marufuku shughuli za uvuvi ndani ya mto Kagera na ziwa hiema hadi ufumbuzi wa tatizo hilo utakapopatikana.
Hivi karibuni watanzania 9 katika wilaya ya Kyelwa waliokuwa wakifanya shughuli za uvuvi ndani ya mto Kagera waliuwawa na watu wanaodhaniwa askari wa nchi jirani ya Rwanda hali ambayo ilimsikitisha waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba aliyepata taarifa hiyo wakati akiwa mkoani Kagera.
Chanzo: ITV
Kuna habari nimeona ITV sasa hivi kuwa kuna watanzania 56 maeneo ya Kagera wameuawa na wanajeshi wanaodhaniwa kutoka Rwanda.
Ni kweli nachokiona au ni miujiza hii?
Ndo huyu tunayemuita Rafiki wetu na tunataka tuite wataalamu wake wa IT au itakua ni watu wenye nia mbaya wanaotaka kuharibu mahusiano baina yetu na Rwanda.
Sijaelewa wakuu embu nielewesheni.
=========
Zaidi ya watanzania 56 katika vijiji vya Chamchuzi na Buguluka vilivyoko katika kata ya Bwelanyange iliyoko wilayani Karagwe mkoani Kagera waliokuwa wakijihusisha na shughuli za uvuvi ndani ya mto Kagera na ziwa hiema wanadaiwa kutekwa na kuuawa kikatili na watu wanaodhaniwa kuwa ni askari wa nchi jirani Rwanda ambao mara kwa mara hufanya doria ndani ya mto huo na ziwa hilo.
Vitendo vya watanzania kutekwa na kuuwawa kikatili vimeshtua mkuu wa wilaya ya Karagwe Godfrey Muheruka anayelazimika kufanya ziara ya kutembelea mwalo wa Rukombe ambao hutumiwa na wananchi wa vijiji vya Chamchuzi na Buguluka na baadae kukutana na wananchi wa vijiji hivyo viwili miongoni mwao wakiwemo wajane 59 ambao wanaume wao wanasadikiwa kuuwawa, baadhi ya watanzania walionusurika kifo wenye majeraha mbalimbali ya risasi na mtanzania aliyekombolewa hivi karibuni toka nchini Rwanda ambao wametoa shuhuda mbalimbali.
Afisa mtendaji wa kata ya Bwelanyange Nicolaus Lubambala kwenye taarifa yake iliyosomwa na Godwin Mbeikya ambaye mratibu elimu kata ya Bwelanyange ameeleza kuwa matukio ya watanzania kuuwawa yamekuwa yakiongezeka kila kunapokucha, kufuatia matukio hayo mkuu wa wilaya ya Karagwe Godfrey Muheruka amepiga marufuku shughuli za uvuvi ndani ya mto Kagera na ziwa hiema hadi ufumbuzi wa tatizo hilo utakapopatikana.
Hivi karibuni watanzania 9 katika wilaya ya Kyelwa waliokuwa wakifanya shughuli za uvuvi ndani ya mto Kagera waliuwawa na watu wanaodhaniwa askari wa nchi jirani ya Rwanda hali ambayo ilimsikitisha waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba aliyepata taarifa hiyo wakati akiwa mkoani Kagera.
Chanzo: ITV
Ali Kiba and Ommy Dimpoz – Kajiandae (Video Coming Soon)
Alikiba was the first one to post picture on Instagram and write down a caption #Kajiandae.