Monday, 22 August 2016
Sunday, 21 August 2016
TANGAZO LA TIBA KUTOKA KWA DR.KANYAS
Dr.kanyas ni mtaalam wa Tiba asili anatibu magonjwa yote yanayokusumbua kwa kutumia dawa za mitishamba za kisuna na kwa kutumia kudra za mwenyezi Mungu na swala.
Pia anatibu matatizo yote ya;
-Uzazi
-gono
-kaswende
-malaria sugu
-Figo
-TB
-Pumu
-ugumba
-hedhi isiyo na mpangilio
-Changu ya uzazi
-Maumivu makali ya kiuno na wakati wa hedhi
Pia anazo dawa za kurudisha nguvu za kiume na kunenepesha uume.
Dawa zote ni za mitishamba na kisuna.
Mtafute kupitia namba ya simu 0764839091
Pia anatibu matatizo yote ya;
-Uzazi
-gono
-kaswende
-malaria sugu
-Figo
-TB
-Pumu
-ugumba
-hedhi isiyo na mpangilio
-Changu ya uzazi
-Maumivu makali ya kiuno na wakati wa hedhi
Pia anazo dawa za kurudisha nguvu za kiume na kunenepesha uume.
Dawa zote ni za mitishamba na kisuna.
Mtafute kupitia namba ya simu 0764839091
Wasimamizi wa Ukuta wa Chadema watangazwa
Chadema imetangaza safu yao ya kutoa elimu ya maandamano ya Ukuta.
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza mkakati wa chama hicho
kufanikisha mikutano na maandamano ya walichokiita Umoja wa Kupinga
Udikteta Tanzania (Ukuta), huku jeshi la polisi nalo likijiandaa
kukabiliana nao.
Mbowe ameitaja mikakati hiyo ikiwamo kamati za kuhamasisha Ukuta.
Mrithi wa Lipumba kupatikana leo CUF
Wajumbe zaidi ya 700 wa Mkutano Mkuu wa dharura wa CUF wanakutana mjini
Dar es Salaam leo kumchagua mwenyekiti mpya wa chama hicho kuziba
nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Ibrahim Lipumba aliyejiuzulu wadhifa
huo mwaka jana.
Profesa
Lipumba aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani kuanzia
1995 hadi mwaka, aliachia ngazi kwa kile alichodai kupinga uamuzi wa
viongozi wa vyama vinavyounda Ukawa kumpokea
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Mabasi kuendelea na safari nchini
Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), kimesitisha uamuzi wake wa kuacha kutoa huduma za usafiri kwa mabasi ya mikoani kupisha ukaguzi wa magari hayo ili kuzuia ajali za barabarani.
Hivi
karibuni Taboa walikubaliana kusimamisha safari za mabasi zaidi ya
4,000 kuanzia kesho kwa muda usiojulikana kutoa fursa kwa Kikosi cha
Usalama Barabarani kufanya ukaguzi huo.
Katibu
Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu amesema: “Serikali imeahidi kushughulikia
kero zilizotulazimisha kuamua magari yetu yaende kufanyiwa ukaguzi na
kusitisha safari zetu zote, hivyo tutaendelea na kazi.”
Janga la Watumishi Hewa: Waziri Asema Wameongezeka na Kufikia 16,127, Ripoti Rasmi Kukabidhiwa Kwa Rais Magufuli Agosti 26
Aidha, mbali ya serikali kuokoa Sh bilioni 16.15 kwa mwezi huu wa Agosti baada ya watumishi hewa hao kuondolewa kwenye mfumo wa utumishi, ambao kama wasingeondolewa fedha hizo zilikuwa ziwalipe mshahara, posho na malipo mengine, waajiri 145 hawajawasilisha taarifa kuhusu uhakiki wao.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki alipozungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais
Magufuli la kuwataka waajiri wote wa umma na serikali, kuwaondoa
watumishi hewa.
Akifafanua
taarifa hiyo, Kairuki alisema Agosti 26, mwaka huu watamkabidhi rais
taarifa rasmi ya utekelezaji wa agizo hilo huku akiwataka waajiri 145
ambao hawajawasilisha taarifa za ama uwepo wa watumishi hewa au la,
kuhakikisha wanaziwasilisha taarifa hizo kabla ya Ijumaa wiki ijayo.
“Tunawapa
muda hadi Ijumaa wiki ijayo wawe wamewasilisha taarifa za kama wana
watumishi hewa au la na sisi Agosti 26, mwaka huu ndio tunamkabidhi rais
taarifa rasmi ya mwisho ya utekelezaji wa agizo alilotoa,” alisema Kairuki akizungumzia hatua ya Rais Magufuli kuagiza uhakiki huo Machi mwaka huu.
Akielezea
hatua zilizochukuliwa hadi sasa na waajiri hao, Kairuki alisema nchi
ina jumla ya waajiri 409 wa serikali na taasisi mbalimbali za umma, na
kati ya waajiri hao, hadi sasa waajiri 264 ndio waliowasilisha taarifa
za utekelezaji wa agizo hilo.
Alisema
kati ya waajiri hao 264 waliowasilisha, waajiri 63 wamethibitisha
hawana watumishi hewa, huku waajiri 201 wakibaini uwepo wa watumishi
hewa kuanzia mmoja na kuendelea.
“Tumepokea
taarifa za utekelezaji wa agizo la rais alilitoa Machi 15, mwaka huu na
hadi sasa waajiri 264 kati waliotekeleza agizo hilo, 201 wamebaini wana
watumishi hewa,” alisema Kairuki.
Akizungumzia
hatua zitakazochukuliwa baada ya kufikia tarehe ya mwisho wa kupeleka
taarifa hizo, Kairuki alisema jukumu lao ni kuzipokea na kukabidhi
mamlaka ya uteuzi ambayo ndiyo iliagiza na ambayo ndiyo itaamua hatua za
kuchukua.
Sambamba
na hilo, Kairuki alisema hadi sasa jumla ya watumishi hewa 606,
wameanza kuchukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo mashauri yao kupelekwa
polisi na hivi sasa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru),
wanafanya uchunguzi na hatimaye watuhumiwa hao wafikishwe kwenye vyombo
vya juu vya sheria.
Aidha,
maofisa utumishi 233 waliohusika kwenye malipo ya mishahara hewa
mashauri yao, wamefikishwa kwenye mamlaka husika kwa uchunguzi, ilhali
watatu wamefukuzwa kazi, huku wizara ikiendelea kufanya uchunguzi kwenye
taasisi 75 za umma ili kujiridhisha kuhusu suala la watumishi hewa.
Kuhusu
waajiri 145 ambao hawajawasilisha taarifa za uhakiki wa watumishi wao,
Kairuki alisema zimo taasisi, wakala, bodi, mabaraza, vyuo, hospitali,
ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa, tume na mamlaka kadhaa ambazo
hazijawasilisha taarifa zao.
Kwa
upande wa mabaraza nchini, Kairuki alisema mabaraza mbalimbali 10
hayajawasilisha taarifa za uhakiki wa watumishi na baadhi yao ni kama
vile Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), Baraza la Elimu ya Ufundi
(Nacte), Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Baraza la Mitihani la Taifa
(NECTA) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Aidha,
jumla ya vyuo vya umma 25 nchini havijawasilisha taarifa zao za uhakiki
wa watumishi hewa na baadhi yao ni Dodoma (Udom), Chuo KIkuu Huria
(OUT), Chuo Kikuu Mzumbe, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (MUHAS), Chuo cha Diplomasia, Chuo Kikuu cha Elimu Dar es
Salaam (Duce), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo cha Kumbukumbu
ya Mwalimu Nyerere na Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Upande
wa Bodi mbalimbali ambazo hazijawasilisha taarifa zao jumla yake ni 10
na baadhi ya bodi hizo ni pamoja na Bodi ya Korosho Tanzania, Bodi ya
Tumbaku, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Bodi ya
Utalii na Bodi ya Maziwa.
Pia
zimo hospitali teule za rufaa tatu ambazo ni Hospitali ya CCBRT,
Hospitali ya Rufaa Bugando na Hospitali ya Rufaa KCMC na kwamba katika
hospitali kama hizo zilizowasilisha taarifa zake, wamebainika na
kuondolewa watumishi hewa 4,000.
Kwenye
taasisi za Umma na Wakala ambazo hazijawasilisha taarifa zao jumla ziko
30 na baadhi yao ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mfuko wa
Pembejeo za Kilimo, Makumbusho ya Taifa, Shirika la Utangazaji la Taifa
(TBC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Madini la Taifa
(Stamico), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Wakala wa Vitambulisho vya
Taifa (NIDA) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).
Pia
zipo Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa 12 ambazo baadhi yake ni Ofisi
ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Dodoma, Dar es Salam, Mbeya, Pwani na
Kagera; kwa upande wa mamlaka zipo sita ambazo ni Mamlaka ya Elimu
Tanzania (TEA), Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje
(EPZA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na
Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA).
Aidha,
zipo tume 10 ambazo hazijawasilisha taarifa zake na baadhi yake ni Tume
ya Pamoja ya Fedha, Tume ya Atomiki, Tume ya Elimu Taifa, Tume ya
Kudhibiti Dawa za Kulevya, Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania na
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Pia
zipo Mamlaka za Serikali za Mitaa 38 zikiwemo Halmashauri ya Jiji la
Mwanza, Manispaa ya Iringa, Nyamagana, Halmashauri ya Mji, Kasulu,
Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi.
Polisi wachunguza kupigwa diwani
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linachunguza madai ya kupigwa kwa Diwani wa Kidahwe katika Halmashauri ya Kigoma Vijijini, Heri Kigufa na maofisa uhamiaji.
Diwani
huyo, Heri Kigufa amedai kupigwa na maofisa tisa wa idara ya uhamiaji
na kumnyang’anya vitu vyake kisha kumfunga pingu mikononi wakati
alipokwenda kumwekea dhamana ndugu yake ili atolewe rumande.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Fredinand Mtui amesema upepelezi wa madai hayo unaendelea ili kubaini ukweli.
Saturday, 20 August 2016
Bi Shakila kuzikwa leo, ni baada ya kufariki ghafla Jana Ijumaa
Muimbaji mkongwe wa muziki wa Taarab nchini, Bi. Shakila Said, atazikwa Jumamosi hii. Bi. Shakila alifariki ghafla jana Ijumaa.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais wa shirikisho la muziki Tanzania,
Addo November, muimbaji huyo alifariki ghafla mara baada ya kumaliza
kuswali nyumbani kwake, Mbagala Charambe jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa mwanae, Shani, mama yake alianguka na kupoteza maisha na
kwamba hakuwa akiumwa. Mazishi yake yanafanyika kwake Mbagala.
Bi
Shakila aliwahi kuwika na nyimbo kadhaa ukiwemo ule maarufu, MACHO
YANALIA MOYO UNACHEKA aliouimba akiwa na bendi ya JKT miaka ya 90.
Mwaka
1960, aliolewa akiwa na umri wa miaka 11 tu na kuachana akiwa na mtoto
mmoja kabla ya kuolewa tena na mwanaume aliyedumu naye kwa miaka 18 na
kuzaa naye watoto watano kabla ya mumewe kufariki mwaka 1975.
Alikuja
kuolewa tena na mwanaume mwingine aliyezaa naye watoto watano kabla ya
kuja kuolewa tena mara ya nne na mwanaume aliyezaa naye watoto wawili.
Alipokuwa
na mimba ya mtoto wake wa mwisho, Shani, mume wake alimwacha. Shani
alizaliwa mwaka 1993 na hapo ndipo alidai alichukia wanaume na kuamua
kuishi mwenyewe.
Pamoja
na kustaafu kazi JKT, Shakila aliendelea kufanya muziki na miaka miwili
iliyopita alikuwa akirekodi album yake Mama na Mwana ambayo ingekuwa na
nyimbo nane.
Mfanyabiashara Moshi Ajimwagia Petroli na Kujipiga Kiberiti
lnawezekana
likawa tukio baya lililoacha gumzo na simanzi baada ya mfanyabiashara
wa mjini Moshi, Romani Shirima (74), kujiua kwa kujilipua kwa petroli
nje ya nyumba yake.
Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema mfanyabiashara huyo alijifunika kwa blanketi, kisha kujimwagia petroli na kutumia kibiriti kuwasha moto ambao ulimlipua na kusababisha kifo chake.
Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema mfanyabiashara huyo alijifunika kwa blanketi, kisha kujimwagia petroli na kutumia kibiriti kuwasha moto ambao ulimlipua na kusababisha kifo chake.
Ingawa hakuna taarifa rasmi ya nini kiini cha mfanyabiashara huyo kuchukua uamuzi huo mgumu ulioacha maswali mengi, lakini baadhi walidai ni msongo wa mawazo uliotokana na madeni.
Hili
ni tukio la pili kwa mfanyabiashara mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro, kwani
miaka kadhaa iliyopita, mfanyabiashara anayemiliki hoteli eneo la
Marangu alijilipua kwa petroli akiwa katika gari lake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, saa 11.25 asubuhi maeneo ya Mjohotoni.
Alisema, mfanyabiashara huyo ni mmiliki wa shule ya sekondari ya Merinyo iliyopo mjini Moshi, na kusema kuwa aliamka asubuhi nyumbani kwake na kujimwagia mafuta hayo na kisha kujilipua na kiberiti.
Kamanda
Mutafungwa alisema chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika ingawa
kuna maneno yanayoongelewa na watu, lakini hawawezi kuyachukua moja kwa
moja na kwamba jeshi hilo linachunguza ili kubaini chanzo chake.
Taarifa
za tukio hilo la aina yake zimekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali ya
mji wa Moshi na vitongoji vyake, hasa njia aliyoitumia kukatisha uhai
wake.
Waziri Mkuu Ziarani Katavi
MAPOKEZI
makubwa yanamsubiri Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anayetarajiwa kuwasili
leo mchana mjini Mpanda kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani
Katavi inayoambatana na kutembelea, kukagua miradi kadhaa ya maendeleo
na kuhutubia mikutano ya hadhara.
Hii
itakuwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa juu wa kitaifa kutembelea
mkoa wa Katavi tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani,
ziara ambayo itamfikisha pia katika mkoa jirani wa Rukwa.
Katibu
Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Katavi, Lauteli Kanoni amesema ziara ya
Waziri Mkuu mkoani humo itaanza leo na kutarajiwa kuhitimisha ziara yake
Agosti 23, mwaka huu.
Kwa
mujibu wa ratiba, Waziri Mkuu atawasili leo mchana kwenye Uwanja wa
Ndege wa Mpanda kisha ataelekea Ikulu Ndogo ambako atasomewa taarifa ya
mkoa na kuzungumza na watumishi wa serikali katika viwanja vya ikulu
ndogo.
Siku
itakayofuata atakwenda katika Kijiji cha Majalila, kunakojengwa Ofisi
za Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na kutembelea mradi wa maji kijijini
humo kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara.
Kwa
mujibu wa ratiba yake, anatarajiwa kuhutubia mikutano ya hadhara katika
kijiji cha Ndui kilichopo kwenye makazi ya wakimbizi ya Katumba na
katika uwanja wa Azimio, Manispaa ya Mpanda.
Aidha,
Agosti 22, mwaka huu Waziri Mkuu atafanya ziara ya siku moja katika
wilaya ya Mlele ambapo atawahutubia wananchi wa Inyonga katika
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kabla ya kuelekea katika Kijiji cha
Majimoto, Halmashauri ya Mpimbwe atakapokagua ujenzi wa daraja la mto
Kavuu na baadaye kuhutubia mkutano wa hadhara.
Waziri
Mkuu Majaliwa anatarajiwa kufanya majumuisho ya ziara yake Agosti 23,
mwaka huu katika ukumbi wa Idara ya Maji mjini Mpanda kabla ya kuelekea
wilayani Nkasi kuanza ziara ya siku tatu mkoani Rukwa.
Tundu Lissu Aibwaga Serikali Mahakamani
Serikali imeendelea
kupigwa mweleka katika kesi ya uchochezi dhidi ya mshitakiwa Tundu Lissu
baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutupa pingamizi la Wakili wa
Serikali wakitaka wakili Peter Kibatala kujitoa kumtetea mwanasiasa
huyo.
Lissu, ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema
alipandishwa kizimbani Agosti 5, na kusomewa mashtaka matatu, mawili
kati yake yakiwa ni ya uchochezi na moja la kuidharau mahakama.
Pigo la
kwanza la upande wa mashtaka ni pale Lissu alipopangua hoja na
kufanikiwa kupata dhamana, wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani kwa
mara ya kwanza.
Jana ilikuwa ushindi mwingine kwa upande wa utetezi,
baada ya Mahakama kutupa pingamizi la upande wa mashtaka lililotaka
Kibatala ajitoe katika jopo la mawakili wanaomtetea Lissu.
Upande wa
mashtaka ulioongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi,
uliweka pingamizi hilo kwa maelezo Kibatala ni shahidi wao kwa kuwa
alikuwapo siku na mahali wakati Lissu akitoa maneno yanayodaiwa ya
uchochezi.
Wakili Kibatala ambaye ni kiongozi wa jopo la mawakili
wanaomtetea Lissu, alipinga hoja za Serikali za kutaka ajitoe katika
kesi hiyo, mvutano ambao ulisababisha kesi hiyo kuahirishwa mara mbili.
Wakili Kibatala alipinga kuwa hakuna kifungu cha sheria kinachomzuia
wakili kumtetea mteja wake kwa sababu tu ya kushuhudia akitoa maelezo
yake Polisi.
Akitoa uamuzi wa pingamizi hilo la Serikali, Hakimu Mkazi
Mfawidhi, Cyprian Mkeha anayesikiliza kesi hiyo, hakukubaliana na hoja
za upande wa Jamhuri (mashtaka) na hivyo akalitupa pingamizi hilo.
Hakimu Mkeha alikubaliana na hoja za wakili Kibatala kuwa hakuna kifungu
chochote cha sheria kinachomzuia kumtetea Lissu.
Alisisitiza kuwa
Kibatala ataendelea kuwa wakili wa Lissu katika kesi hiyo na kwamba
kama upande wa mashtaka ukimhitaji awe shahidi wao utalazimika kumuomba.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 19.