Sunday, 3 July 2016
BODI YA MIKOPO YAKANUSHA KWAMBA TAARIFA ILIYOSAMBAA KWAMBA HAINA PESA
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
TAARIFA KWA UMMA
KUKANUSHA TAARIFA KWAMBA BODI HAINA FEDHA
Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa za upotoshaji zinazoenezwa
kwa sasa kwamba haina fedha.
Si kweli kwamba
Bodihaina fedha, ila ni kweli kwamba kumekuwa na ucheleweshaji wa kufikisha
fedha za wanafunzi vyuoni kutokana na zoezi la kuhakiki wanafunzi wanaonufaika
na mikopo linaloendelea vyuoni hivi sasa.
Hata hivyo,
maandalizi ya malipo hayo yameshafanyika na ‘pay sheets’ zimeshapelekwa vyuoni
tayari kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo kusaini.
Bodi inatarajia
wakati wowote wiki ijayo baada ya zoezi la uhakiki kukamilika; itapeleka fedha
hizo vyuoni.
IMETOLEWA
NA:
KITENGO
CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
BODI
YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
TAREHE
2 JULAI 2016
Breaking News:GARI AINA YA NOAH YAPATA AJALI WILAYANI MASWA-MKOA WA SIMIYU
Gari aina ya NOAH imepata ajali maeneo ya zanzui wilayani MASWA mkoani SIMIYU,Hakuna mtu aliepoteza maisha.
(Picha zote na Samweli Mwanga)
Friday, 1 July 2016
Mtumishi wa umma atakayekwenda kusomea 'first degree' sasa kuchukua likizo isiyo na malipo
Mtumishi atakayekwenda kusomea FIRST DEGREE anatakiwa achukue LIKIZO
ISIYO NA MALIPO na hastahili kulipwa chochote na Mwajiri wake ikiwa ni
pamoja na kutolipwa Mshahara kwakuwa HAYUPO KAZINI.
Hakuna malipo yoyote ya UHAMISHO kwa Mtumishi atakayehamishwa umbali usiozidi kilometa 10.
Hakuna malipo yoyote ya UHAMISHO kwa Mtumishi atakayehamishwa umbali usiozidi kilometa 10.
MPYA: Serikali imezuia Benki kupandisha viwango vya tozo katika miamala yake
TRA wamesema taasisi za fedha wanapoongeza makato ya miamala ya fedha wanakosea kwa kupandishia wananchi kwa kuwa sheria hiyo inahusu fedha ambayo mwanachi alikuwa anakatwa na taasisi hizo ambayo hapo mwanzoni zilikuwa azilipiwi kodi kwa hiyo hizo ndizo zitakazokatwa 18%.
Mfano kama umetoa fedha ukakatwa 1000 na taasisi ya fedha ilikuwa haikatwi kodi lakini kwa sheria hiyo ada hiyo ndio itakatwa 18% na sio mwananchi kuongezewa makato kama ilivyofanyika kwa baadhi ya taasisi za fedha.
PICHA :Ajali Ya basi iliyotokea Mkoani Morogoro -imeua 11
Habari iliyoripotiwa hivi punde na kituo cha ITV ni kuhusu ajali ambayo imetokea eneo la Veta Dakawa mkoani Morogoro ikihusisha magari matatu ambayo ni lori la mafuta, kontena lililobeba mchele pamoja na basi.
Taarifa hiyo inasema kuwa watu 11 wamefariki dunia na wengine ambao idadi yao bado haijajulikana wamejeruhiwa.
Tunaendelea kufuatilia taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo.