Wednesday, 4 November 2015

TEMCO: Uchaguzi Ulikuwa HURU na wa HAKI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

TIMU ya Waangalizi wa Ndani wa Uchaguzi Mkuu (TEMCO), imesema kwamba tathmini yao kwa Uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni, unastahili hati ya uchaguzi safi, huru na wa haki ambao umeangukia alama A. 

Aidha, Temco imesema kwamba hata hivyo ikizingatiwa hisia za kutoridhishwa na baadhi ya wadau wa uchaguzi kuhusu uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), sheria na kanuni pamoja na upungufu kadhaa, imeshindwa kuupa uchaguzi huo alama A na hivyo kutoa alama B kwamba ingawa uchaguzi ulikuwa wa huru na haki. 

Akitoa taarifa ya awali ya TEMCO kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kiongozi wa timu hiyo, Dk Benson Bana alisema upungufu mdogo hauepukiki hivyo timu yao kutoa alama 60-69 ambayo inaangukia kwenye alama B. 

“Waangalizi wa ndani tulipoangalia kutoka kwenye taarifa za waangalizi wetu waliokuwa wamesambaa nchi nzima, toka mwanzo wa uchaguzi huu yaani katika utengaji majimbo, uteuzi ndani ya vyama, kampeni na siku yenyewe ya kupiga kura uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania unaangukia alama A, lakini kutokana na dosari hizo tunatoa alama B,” alisema Dk Bana. 

Alizitaja baadhi ya sababu hizo kuwa ni pamoja na kutoruhusu Watanzania walioko nje ya nchi kupiga kura, kuwepo na mgombea binafsi na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa kwamba sio waajiriwa wa Tume. 

Aidha, Dk Bana aliyataja mapungufu mengine kuwa ni katika kampeni hizo wagombea walijinadi wao badala ya vyama vyao vilivyowasimamisha, jambo ambalo lilijitokeza hasa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

“Hili halikutufurahisha kabisa, mgombea kuwa mtu binafsi kuliko kunadi taasisi zao hilo halikuwa jambo jema katika kukuza demokrasia na hii imejitokeza hasa kwa CCM na Chadema,” alisema Dk Bana. Alisema kwa mujibu wao, kampeni za vyama kuna ambazo hazikuzingatia muda na pia maneno yasiyofaa kujitokeza katika kampeni hizo. 

Hata hivyo, alisema tathmini za Temco zilionesha siku ya kupiga kura, hakukuwa na mambo yoyote ya kusababisha uchaguzi usiwe wa huru na wa haki watu walipiga kura katika hali ya amani na pia kura zilihesabiwa katika hali hiyo bila kuwapo vurugu pamoja na matokeo kutangazwa. 

Dk Bana alisema tathmini yao inaonesha pia kuwa vyama vya CCM, Chadema na CUF vilitumia demokrasia vizuri katika kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya vyama na kwamba vyama vingine havikuwa na demokrasia hiyo na kwamba kulikuwa na matumizi makubwa ya fedha kwa CCM na Chadema. 

Kuhusu uchaguzi wa Zanzibar, Dk Bana alisema Temco imepokea kwa mshituko uamuzi wa kufutwa matokeo ya uchaguzi uliotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha wa kufuta uchaguzi wa Zanzibar kwa madai kuwa haukuwa wa huru na haki. 

“Tulikuwa na watazamaji 22 wa muda mrefu na 704 wa muda mfupi wa Temco Zanzibar, ambao waliangalia mchakato mzima wa uchaguzi na taarifa zao za awali zinaonesha kuwa shughuli zote za kabla ya uchaguzi zilifanyika kwa amani na utulivu, inashangaza uamuzi wa kusitisha kura zikiendelea kuhesabiwa,” alisema Dk Bana. 

Alisema Temco inaishauri ZEC kufikiria upya uamuzi huo kwa lengo la kufikia uchaguzi huru na wa haki kuimarisha amani, huku ikiitaka Serikali kuingilia kati kuleta amani kwa Zanzibar ikishirikiana na wadau wengine wa amani.
Share:

Sitta atangaza Kuwania Nafasi ya Kuwa Spika Bunge la 11

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta ametangaza kuwa atawania nafasi ya Spika ili kuliongoza Bunge la 11. Sitta aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tisa amekuwa kada wa kwanza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujitosa katika mchuano wa kuwania nafasi hiyo nyeti wakati huu ambao Bunge limevitaka vyama vya siasa viwe tayari kwa ajili ya kupeleka majina ya wateule wao wa nafasi hiyo mara itakapotangazwa kuwa wazi. 

Msemaji wa Spika huyo mstaafu, John Dotto alisema jana Dar es Salaam kuwa Sitta amemua kuwania nafasi hiyo kutokana na uwezo na uzoefu alionao wa kuendesha Bunge. Alisema Sitta anaamini kuwa uwezo wake aliouonesha katika kuendesha Bunge la Tisa akitumia kaulimbiu yake ya ‘Spika wa Kasi na Viwango’ itamfanya aendane na kasi ya utendaji wa Rais Mteule, Dk John Magufuli. 

Sitta alijizolea sifa wakati akiwa Spika wa Bunge la Tisa kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, ikiwamo Bunge hilo kufanyia marekebisho ya kanuni mbalimbali zilizolifanya liwe na makali na kuibua kashfa nzito ikiwamo ya Richmond ambayo ilisababisha Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu na alilirejeshea makali Bunge. 

Tayari Bunge la Jamhuri ya Muungano limetangaza kuanza kwa mchakato wa kumpata Spika mpya wa Bunge, atakayerithi mikoba ya Spika Anne Makinda. Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel akizungumza na vyombo vya habari Dar es Salaam mapema wiki hii alisema kuwa mgombea wa nafasi ya Spika, anaweza kuwa Mbunge au mwanachama yeyote wa chama kwa masharti kwamba kama si Mbunge, jina lake lazima liwasilishwe kwanza Tume ya Taifa ya Uchaguzi siku tano kabla ya uchaguzi kujiridhisha kuwa mgombea huyo ana sifa za kuwa Mbunge. 

Bunge hilo la Tisa lilipata ufanisi na mafanikio kadhaa kutokana na ubunifu na ujasiri wa baadhi ya wabunge wakiongozwa na utayari wa Sitta ambaye wakati akishika nafasi hiyo aliahidi kuwa ‘spika wa kasi na viwango.’ 

Mafanikio yaliyopatikana katika Bunge hilo ni pamoja na kutungwa kwa Kanuni mpya za Bunge za mwaka 2007, ambazo zimeelezwa kuwa zilisaidia kwa kiasi kikubwa kuliwezesha lifanye kazi kwa ufanisi kama vile kuondoa ukiritimba wa serikali kuwa ndiyo pekee inayoweza kupeleka muswada bungeni. 

Kanuni hizo mpya za mwaka 2007 ambazo zilitokana na kufanyia marekebisho makubwa kanuni za Bunge za mwaka 2004, zilitoa mamlaka kwa kamati za kudumu za Bunge kuwa na uwezo wa kupeleka mswada kwa ajili ya kujadiliwa bungeni na hatimaye kuwa sheria.
Share:

RC Dar aonya wanaoamsha hisia za uvunjifu wa amani

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


VIONGOZI wa vyama vya siasa wametakiwa kuheshimu Katiba ya nchi kwa kuacha kuendeleza mgogoro na kuamsha viashiria vya uvunjifu wa amani ya nchi kwa madai ya kutokukubaliana na matokeo ya Urais yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa Kamati ya Amani ya viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Dar es Salaam uliofanyika jana Dar es Salaam. 

Alisema kwa mujibu wa Katiba ya nchi NEC pekee ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza matokeo na ikishafanya hivyo hakuna mahali pa kwenda kupinga. Alisema wanasiasa hao kwa kusambaza taarifa za kufanya maandamano ya kupinga matokeo hayo ni uchochezi na kukiuka sheria za nchi ambapo kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani. 

“Wapo watu ambao hawataki kuheshimu hilo, wanasambaza meseji za uchochezi ambazo zinaweza kuvuruga amani yetu …” alisema Sadiki. Aliwaomba viongozi hao wa dini kuendelea kuhubiri amani kwani kamati hiyo imefanya kazi kubwa katika kuhakikisha nchi inapita salama katika uchaguzi licha ya kuwepo kwa matukio madogo ya uvunjivu wa amani. 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum alisema katika kipindi cha kuanzia kampeni, upigaji kura na baada ya uchaguzi, mambo yameenda vizuri kwa kuwa amani imetawala. 

Alisema kutokana na amani kutawala hata baadhi ya mataifa mengine ambayo yalikuwa yakitamani kuona Tanzania ikiingia katika machafuko yamepata mshangao kuona bado amani inaendelea kuwepo. 

Hata hivyo, alitaka wagombea ambao hawakuridhika na matokeo yaliyotolewa wafuate taratibu badala ya kuwashawishi na kuwatumia wananchi kuingia barabarani na kufanya vurugu na maandamano. “Walioshindwa wasiwatumie Watanzania kuingia barabarani kufanya vurugu, tuheshimu damu za Watanzania,” alisema Sheikh Alhad.
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO MUHIMBILI UNIVERSITY-MUHAS 2015/2016

Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBER 04 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:

Tuesday, 3 November 2015

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA MUST 3RD BATCH 2015/2016

Share:

TAARIFA MUHIMU KUHUSU "MALIPO" KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA SPECIAL DIPLOMA UDOM 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
slide1
IMPORTANT NOTICE TO SPECIAL DIPLOMA STUDENTS
ALL STUDENTS ARE REQUIRED TO PAY UNIVERSITY DIRECT COSTS FOR ACADEMIC YEAR 2015/2016 BEFORE REPORTING TO THE UNIVERSITY.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBER 03 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY











Share:

Monday, 2 November 2015

NAFASI ZA KAZI 640 UHAMIAJI KWA KIDATO CHA NNE NA SITA ,MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NOVEMBER 6 2015-SIFA UWE UMEPITA JKT

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Habari yako,
Uhamiaji wametangaza nafasi za kazi zipatazo 640 kwa wahitimu wa kidato cha SITA na NNE ,Tafadhali tuma Waweza fanikiwa mpe taarifa na mwenzako,

KUSOMA TANGAZO HILO BONYEZA HAPO CHINI,
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anatangaza nafasi za kazi katika Idara ya Uhamiaji. Nafasi hizo ni za Koplo wa Uhamiaji na Konstebo wa Uhamiaji. fuata ukurasa huu kwa maelezo zaidi.
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO CHUO KIKUU IFM 2015/2016-FIRST LOT

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Habari yako,
Kama kawaida yetu MASWAYETU BLOG tunanedelea kukuletea kitu roho inapenda,Hatimae IFM imetoa majina ya waliopata mkopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016.

Tunaendelea kutoa huduma yetu ya kuangalizia watu majina yao,endapo utahitaji kuangaliziwa jina fanya yafuatayo;


1.TUMA JINA LAKO MFANO JUMA JUMA S4050/0018/2012-HELSB 2015/2016-ifm

2.HUDUMA HII UTATOZWA TSHS 1000 AMBAYO UTAITUMA KWA MPESA KWENDA
   NAMBA 0768260834 AU TIGO PESA 
0652740927


3.TAFADHALI MAJINA YOTE YATUMWE KWENYE NAMBA YA VODA 0768260834
4.UTAJIBIWA MDA MFUPI TU BAADA YA KUTUMA PESA

5.TUMA PESA KWANZA NDIO UTUME JINA NA EXAM NAMBA YAKO.

NOTE:PIA TUNAYO MAJINA YA VYUO VYOTE YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO 2015/2016
BONYEZA HAPA KUONA MAJINA HAYO
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA NYONGEZA YA WANAFUNZI WA;IOCHAGULIWA MUHIMBILI 2015/2016

Share:

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Habari yako,
Kama kawaida yetu MASWAYETU BLOG tunanedelea kukuleteam kitu roho inapenda,Hatimae Bodi imetoa amjina ya wanafunzi waliopata mkopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016.

Tunaendelea kutoa huduma yetu ya kuangalizia watu majina yao,endapo utahitaji kuangaliziwa jina fanya yafuatayo;

Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MIKOPO YA ELIMU YA JUU VYUO MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Habari yako,
Kama kawaida yetu MASWAYETU BLOG tunanedelea kukuleteam kitu roho inapenda,Hatimae Bodi imetoa amjina ya wanafunzi waliopata mkopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016.

Tunaendelea kutoa huduma yetu ya kuangalizia watu majina yao,endapo utahitaji kuangaliziwa jina fanya yafuatayo;
1.TUMA JINA LAKO MFANO JUMA JUMA S4050/0018/2012-HELSB 2015/2016

2.HUDUMA HII UTATOZWA TSHS 1000 AMBAYO UTAITUMA KWA MPESA KWENDA
   NAMBA 0768260834 AU TIGO PESA 
0652740927

3.TAFADHALI MAJINA YOTE YATUMWE KWENYE NAMBA YA VODA 0768260834
4.UTAJIBIWA NDANI YA DK MOJA TU.
5.TUMA PESA KWANZA NDIO UTUME JINA NA EXAM NAMBA YAKO.
HESLB Officially welcomes Local Undergraduate loan applicants for Academic Year 2015/2016 to view their loan allocation status ( FIRST LOT )
To view your Loan Allocation, kindly type your Form IV Index number in the space provided and Type in the security code shown . 
TO FIND YOUR NAME
Share:

Sunday, 1 November 2015

SUA: Fourth Batch of Selected Students to join Undegraduate Degree Programmes For Academic Year 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

The following applicants have been selected to join various undergraduate degree programmes for the 2015/2016 academic year which starts on the 2nd November, 2015
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OCTOBER 31 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC01922 DSC01923
.
.
DSC01921
.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger