Tuesday, 15 April 2014
TAZAMA AJALI HII ILIYOTOKEA LUGALO DAR
AJALI hii imetokea leo asubuhi baada ya magari kusimamishwa ghafla
eneo la Lugalo, Makongo ili kuruhusu wanafunzi wavuke ndipo lori
liliposhindwa kusimama na kuparamia kingo za barabarani kisha kuiangukia
gari dogo aina ya Toyota Cresta 'GX 100'.
TAZAMA MATUKIO YA NYUMBANI YA MZEE NGURUMO
Wawakilishi
wa Global Publishers, Sifael Paul (anayeandika kwenye daftari) na Elvan
Stambuli mwenye kizibao, wakiandika mchango wa Kampuni ambao ni
shilingi 500,000 kabla ya kuwakabidhi ndugu wa marehemu Muhidini Gurumo
leo jioni nyumbani kwa marehemu Makubuli, Dar, leo. Atazikwa kesho
Masaki, Kisarawe.
Mwakilishi
wa Global Publishers, Elvan Stambuli akimkabidhi mjomba wa marehemu
Muhidini Gurumo, Yahya Mikole (katikati) shilingi 500,000 ambazo ni
rambirambi ya kampuni kwa msiba huo.
Mwakilishi
wa Global akizungumza, Stambuli akimtambulisha Mhariri wa Ijumaa
Wikienda, Sifael Paul kwa nguli wa muziki King Kikii ambaye alikuwepo
msibani leo.
Monday, 14 April 2014
TAARIFA MUHIMU TOKA CCM TAWI LA UINGEREZA
Website ccmuk.org,Blog ccmuk.org/blog, Facebook page Chama Cha Mapinduzi Uingereza, twitter CCMUK1
Contacts Phone +44 74 04 863333, +44 7545 213515
E-mail - itikadi-uenezi@ccmuk.org
MAINA OWINO ANG'ATUKA UENYEKITI WA CCM TAWI LA UINGEREZA - UNITED KINGDOMPIA HALMASHAURI KUU YA TAWI YAMSIMAMISHA KAZI KATIBU WA TAWI BI. MARIAM MUNGULA:
Mwenyekiti wa CCM UK, Ndugu Maina Ang'iela Owino jana ametangaza rasmi nia yake ya kujiuzulu Uongozi wa CCM Tawi la UK baada ya kutumikia toka mwaka 2007.
Ndugu Owino alitoa uamuzi huo wa hiari wakati akifungua rasmi kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Tawi la UK kilichokaa jana Jumamosi tarehe 12/04/2014 katika jiji la Reading, Berkshire, Uingereza.
Ndugu Owino aliwakumbusha wajumbe kuwa awali aliomba kukitumikia Chama kwa muhula mmoja wa uongozi na alitaja kumbukumbu ya vikao vya Chama vilivyomuomba aendelee kukisimamia Chama hasa baada ya kuchaguliwa viongozi wakuu wapya wa Tawi mwezi septemba 2012 jijini Manchester.
Ndugu Owino aliwakumbusha mafanikio waliyopata katika muda wa uongozi wake ikijumuisha harakati za kufungua mashina hadi 15 katika miji na Jiji mbalimbali; Kuhamasisha na kujenga mtandao wa kuanzisha Jumuiya ya kwanza ya Watanzania hapa UK na Kuwashirikisha wanaCCM kuanzisha miradi ya kujitegema ikiwepo ari ya kumiliki jengo la CCM UK.
Alikumbusha pia juhudi na msukumo wa kutaka CCM Taifa kuanzisha dawati rasmi la matawi ya nje na kuyapa uwakilishi wa kudumu katika vikao vya juu vya CCM Taifa.
Pia kupigania Sera ya CCM ya Diaspora iboreshwe kwa Kuanzisha Kituo Maalum cha Diaspora nchini Tanzania ili serikali iwashirikishe na kuratibu hoja na haja za wana Diaspora.
Aidha aliwataka wajumbe kutoa ushirikiano wa wazi kwa Idara ya uenezi ambayo kwa sasa inajenga Website ya kisasa na Online TV itakayowapa wanaCCM uhuru wa kutoa maoni na hoja zao bila uwoga lakini kwa nidhamu na kufungua soko la kutangaza bidhaa za Tanzania.
Ndugu Owino alisema wanaCCM hujenga umoja wa kweli na hawaogopi kusingiziwa au kusemwa vibaya na hivyo wasiogope changamoto mbalimbali wakati wanatekeleza Mapinduzi ya umma na kukijenga Chama hapa Uingereza.
Ndugu Owino aliiomba Halmashauri Kuu ya Tawi ishirikiane na Sekretariati ya Halmashauri Kuu ya Tawi kufanya maandalizi na kupanga tarehe ya Mkutano Mkuu wakati wowote kuanzia sasa ili wanaCCM wote wawe huru kumchagua kiongozi atakaye sukuma CCM UK toka hapa tulipofikia.
Wakati huohuo Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi la UK jana iliazimia kwa pamoja kumsimamisha Katibu wake wa Tawi Mariam Mungula baada ya majadiliano ya kina ya kutokuridhishwa kabisa na utendaji na uratibu wake wa kazi.
Kikao hicho kilipeleka shauri lake kwa Kamati ya Maadili na Usalama ili apate haki ya kujitetea ni kwa nini asiachishwe moja kwa moja kazi yake za Ukatibu wa CCM UK. Ndugu Leybab Mdegela anakaimu nafasi yake kuanzia jana 12/04/2014.
Kikao kiliendelea na hoja zake za kuboresha Chama hapa UK na kuweka mikakati yenye mawazo chanya katika kukisaidia chama katika mikakati kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wote wa Tanzania.
Imetolewa na Abraham Sangiwa
Idara ya Itikadi na Uenezi ya Halmashauri Kuu ya CCM UK.
13/04/2014
Dk.Bilal,Waziri Magufuli wanusurika ajali ya chopa
Dk.Bilal,Waziri Magufuli wanusurika ajali ya chopa
Baadhi ya watu wakiangalia helikopta iliyokuwa
imembeba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed
Gharib Bilal, muda mfupi baada ya ndege hiyo kuanguka eneo la Uwanja wa
Ndege Terminal One jijini Dar es Salaam jana.Picha: Mpigapicha Wetu
Wengine walionusurika katika ajali ya helikopta hiyo iliyokuwa imebeba watu 11 ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, waandishi wa habari wawili, walinzi wawili na maofisa wengine wa serikali.
Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Kamishna Khamis Suleiman,akizungumza na NIPASHE alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 3:15 asubuhi katika eneo la uwanja wa ndege wa Air Wing unaotumiwa na jeshi.
Suleiman alisema viongozi hao baada ya kupata ajali hiyo walikimbizwa hospitali ambayo hakuitaja jina kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Hata hivyo, taarifa ambazo NIPASHE ilizipata zilieleza kuwa viongozi hao baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa katika hospitali ya usalama wa Taifa iliyopo Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Kamanda Suleiman alisema viongozi hao walipata ajali hiyo wakati wanakwenda kukagua maeneo yaliyoathirika na mafuriko ya mvua zilizonyesha tangu juzi jijini Dar es Salaam.
Alisema helkopita hiyo muda mfupi baada ya kuruka katika uwanja huo wa Air Wing, ilipata hitilafu ikiwa angani na kuanguka.
Aliongeza kuwa hali za viongozi hao zinaendelea vizuri, na wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Waziri wa Uchukuzi, Dk.Harrison Mwakyembe, alipoulizwa na NIPASHE alisema taarifa za tukio hilo amezipata na kwamba ajali hiyo haijatokea upande wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere (JNIA) kama ambavyo baadhi ya watu wanaeleza.
“Kimsingi taarifa za tukio hili unaweza kuzipata zaidi kutoka kwa watu wa jeshi maana ajali imetokea upande wa air wing,”alisema Dk.Mwakyembe.
Wakati huo huo, Kurugenzi ya Habari ya JWTZ, imesema helikopta hiyo ilipata ajali katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere (JNIA) kwa upande wa Jeshi wakati ilipokuwa katika hatua ya kuanza kuruka.
Katika taarifa hiyo iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Msemaji wa JWTZ, Kanali Erick Komba imeeleza kuwa mbali na viongozi hao, wengine waliokuwemo ni Dk. Mnzava ambaye ni msaidizi wa Makamu wa Rais, Msaidizi wa Kamanda Kova na waandishi wa habari watatu.
Alisema ujumbe wa Makamu wa Rais ulikuwa katika safari ya kuzungukia maeneo yaliyoathirika na mafuriko katika jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kufuatia mvua hizo zilizoanza kunyesha kuanzia Aprili 11, mwaka huu.
Komba alisema Makamu wa Rais pamoja na ujumbe wake hawakupata majeraha katika ajali hiyo. Aidha, rubani na wasaidizi wake pia wametoka salama.
Aliongeza kuwa uchunguzi wa ajali hiyo umeanza mara moja kwa ajili ya kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Thursday, 10 April 2014
JK: Gas, oil policy in place in October
President Jakaya Kikwete opens 19th Annual
Research Workshop organised by Research and Poverty Allevation (REPOA)
in Dar es Salaam yesterday. (Photo: Tryphone Mweji)
Speaking at the 19th REPOA Annual Research Workshop held in Dar es Salaam yesterday, President Kikwete said there have been extensive discussions on the role natural resources should play in the country’s economy.
“This is particularly relevant today, considering the recent discoveries of large volumes of natural gas, now approximated at 46 trillion cubic feet, and the vast reserves of forests, minerals, diverse wildlife and land that Tanzania has,” he said.
The President also said that the challenge facing the country is how to link these resources with the aspirations of the 2025 Development Vision and the socio-economic transformation the nation desires.
“The strategies and policies are meant to ensure that our people participate productively in the utilisation of the natural resources we are blessed with.
We are also in the process of putting in place a local content policy that will provide a framework for ensuring adequate participation of Micro, Small and Medium Enterprises and local communities in exploiting and utilising our
natural resources,” he said.
He added: “We hope that the private sector, working closely with the government, will proactively engage in the efforts to build the capacity of Tanzanians in different disciplines that are relevant to the various segments of our natural resources’ value chain”.
He underscored that the oil and gas sector is a priority subsector, given the volume of the resources, the intensity of capital investments, and flow of revenues expected from their commercialisation.
“I hope that this workshop will dwell on these issues too, drawing from the experience of other countries as well, on how the enterprise sector including the MSMEs can be leveraged to participate more meaningfully in the desired socio-economic transformation,” the President said.
The president noted that a sound business environment and regulatory landscape have allowed enterprises, both large and MSMEs to thrive and effectively address the problem of unemployment, especially among the youths.
He added that the quest for inclusive development requires dramatic transformation of mind-sets and attitudes as well.
For his part, REPOA Executive Director Prof Samwel Wangwe said that reviews of trends in growth, employment and poverty in Tanzania have highlighted challenges and risks of achieving high growth which is not accompanied with the requisite transformation of the economy and widespread job creation.
“This signifies the challenge of low productivity and low returns to labour in agriculture and micro and small enterprises is predominantly in the informal economy where majority of Tanzanians derive their livelihoods from,” he said.
He added: “The low returns to labour in agriculture push people out of the sector in search of alternative sources of employment, but most of this migrating labour ends up in the lowest end of the non-farm sectors, mainly trade, other services and a few in manufacturing activities.”
He also said that the resulting kind of urbanisation where the informal economic activities provide low returns to labour carries with it the risk of turning rural poverty into urban poverty.
He insisted that there is a quest for deeper understanding of what it would take to transition from rural and urban poverty to prosperity in both the rural and urban economy.
The main objective of the two-day workshop is to achieve deeper understanding of the dynamics of micro and small scale economic activities and identify options for managing the enterprise transformation process with a view to realising more inclusive growth.
Bunge Maalum laanza kusikiliza taarifa za Kamati
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,
Samuel Sitta amesema mjadala kuhusu taarifa za Sura ya Kwanza na ya
Sita za Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
unatarajia kuanza wiki ijayo katika Bunge hilo mara baada ya kumaliza
kupokea taarifa za Kamati.
Sitta alisema hayo katika ukumbi wa
Bunge hilo mjini Dodoma baada baadhi ya wajumbe kumwomba kuchangia
mjadala wakati ripoti hizo zikiendelea kuwasilishwa.
Alisema mdajala wa kuchangia sura hizo
utaanza mara baada ya Kamati 12 za Bunge Maalum la Katiba
kuwasilisha taarifa zao za Sura ya Kwanza na ya Sita kuhusu Rasimu
ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge hilo.
Aliongeza kuwa kwa kujibu wa Kanuni ya
namba 33(6) ambayo inasema baada ya hoja za taarifa za Kamati Namba
Moja hadi Namba Kumi na Mbili kutolewa katika Bunge Maalum na
Mwenyekiti kuelekeza hoja hizo zijadiliwe , mjadala kuhusu taarifa hizo
utaanza.
Mwenyekiti huyo aliwataka baadhi ya
wajumbe hao kusubiri mpaka uwasilishaji wa taarifa hizo utakapokamilika
ndio watapata nafasi ya kuchangia kwa muda mrefu na kuwezesha wajumbe
wengi kupata nafasi hiyo.