Showing posts with label NEWS. Show all posts
Showing posts with label NEWS. Show all posts

Saturday 18 May 2024

Video Mpya : MWANAKWELA - NIBHONA MINGE

 

Share:

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MGENI RASMI KONGAMANO LA WAANDISHI WA HABARI WA MITANDAO YA KIJAMII TANZANIA


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) Shaaban Matwebe
Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) kwa kushirikiana na Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO) imeandaa Kongamano la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii nchini litakalofanyika tarehe 20/5/2024 kwenye ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti JUMIKITA, Shaaban Matwebe amesema Kongamano hilo linalotarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 500, litaongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

"JUMIKITA inapenda kuutaarifu umma kuwa, Kongamano hilo litakuwa na dhima kuu ya kujadili uandishi wa habari kupitia mitandao ya kijamiii pamoja na upashanaji wa habari kupitia mitandao hiyo. Pamoja na dhima hiyo kuu, Kongamano hilo litajadili mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani. JUMIKITA inawakaribisha wote kwenye Kongamano hili muhimu kwa ustawi wa nchi yetu",amesema Matwebe.

Amesema mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii na uzalendo, fursa zilizopo kwenye tasnia hii, mafanikio na changamoto ili kutoa mchango wa kiundeshaji kwa wadau kupitia JUMIKITA na mapendekezo yatakayosaidia serikali kwenye uratibu wa sera za jinsi ya kuunganisha sayansi ya uchumi wa taarifa (information economics) na uchumi wa taarifa (information economy).


Mawasiliano ; Mwenyekiti JUMIKITA~Shaaban Matwebe~0717073534

Sekretarieti~ Dickson Frank Mushi~0686379370
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 18, 2024

Share:

Friday 17 May 2024

DUKA LA KIPEKEE LA UREMBO WA NGOZI NA MANUKATO LAZINDULIWA SHINYANGA MJINI


Mfanyabiashara Maarufu mjini Shinyanga Georgia Buyamba amezindua Duka la kipekee la Vipodozi na Manukato ‘Unique Skin & Scents’ likiwa limesheheni bidhaa mbalimbali za urembo wa ngozi na manukato kwa ajili ya wanawake, wanaume na watoto.

Duka la Unique Skin & Scents lililopo Mjini Shinyanga Mkabala na Benki ya CRDB Shinyanga limezinduliwa rasmi leo Ijumaa Mei 17,2024.

Mkurugenzi wa Unique Skin & Scents bi. Georgia Buyamba amewakaribisha wakazi wa Shinyanga na maeneo jirani kufika katika duka hilo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya bidhaa za urembo wa ngozi na vipodozi vyenye ubora wa hali ya juu na kwa bei rahisi kabisa.

"Ninapenda kuwakaribisha sana wateja wetu, Njooni Unique Skin & Scents mjipatie bidhaa za urembo wa ngozi na manukato mazuri,. Tuna vitu vingi vizuri, vya kipekee, vyenye ubora, Original, kwa kweli tuna vipodozi na manukano ya kila aina kwa ajili ya wanaume, wanawake na watoto kutoka Dubai, UK, USA ",amesema Buyamba.

Wasiliana na Unique Skin & Scents kwa simu namba +255763814949 au +255753889105

Instagram :  uniqueskin-scents
Mfanyabiashara Maarufu mjini Shinyanga Georgia Buyamba akielezea kuhusu bidhaa zinazopatikana katika Duka la kipekee la Vipodozi na Manukato ‘Unique Skin & Scents’ lililopo Mjini Shinyanga Mkabala na Benki ya CRDB Shinyanga - Picha na Kadama Malunde  - Malunde 1 blog
Mfanyabiashara Maarufu mjini Shinyanga Georgia Buyamba akionesha bidhaa zinazopatikana katika Duka la kipekee la Vipodozi na Manukato ‘Unique Skin & Scents’ lililopo Mjini Shinyanga Mkabala na Benki ya CRDB Shinyanga - Picha na Kadama Malunde  - Malunde 1 blog

Share:

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA TIBA KWA WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya Nchini kwa mwaka 2023 kwa waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari Bungeni tarehe 16 Mei 2024 Jijini Dodoma.

Na Mwandishi wetu – Dodoma

Serikali imesema itaendelea kuboresha huduma za tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya ili kuhakikisha wanareejea katika hali zao za awali na kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakati akizungumza na waandishi kuhusu Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya nchini kwa mwaka 2023 tarehe 16 Mei 2024 katika Ukumbi wa Habari Bungeni Jijini Dodoma iliyoelezea mafanikio yaliyopatikana katika vita dhidi ya dawa hizo.

Mhe. Jenista alisema, mwaka 2023, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola vilifanikiwa kukamata jumla ya kilogramu 1,965,340.52 za dawa za kulevya aina ya heroin, cocaine, methamphetamine, bangi, mirungi, skanka na dawa tiba zenye asili ya kulevya na kuwakamata watuhumiwa 10,522.

“Takwimu za mwaka 2023 zinaonyesha mafanikio makubwa, kwani cha dawa za kulevya kilichokamatwa ni kiasi kikubwa kuliko kiasi kilichokamatwa wakati mwingine wowote nchini. Kiasi hiki ni karibu mara tatu ya kile kilichokamatwa kuanzia mwaka 2012 hadi 2022, ikiwa ni ishara ya dhamira ya dhati na utashi wa kisiasa wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupambana na janga hili” alisema Mhe. Jenista.

Alieleza kwamba hadi kufikia mwezi Disemba 2023, vituo vya tiba saidizi na unasihi kwa waraibu wa dawa za kulevya (MAT Clinics) vilivyohudumia waraibu 15,912 vilifikia 16, na nyumba za upataji nafuu (Sober Houses) na 56 zilizohudumia waraibu 3,488.

Waziri Jenista aliendelea kubainisha kwamba jumla ya waraibu 903,062 wa dawa za kulevya na vilevi vingine walipata huduma katika hospitali za wilaya, mikoa na rufaa nchini huku akisema Serikali imeanza ujenzi wa kituo cha Taifa cha Utengamao kwa ajili ya kuwahudumia waraibu wa dawa za kulevya waliopata nafuu.

‘Kituo hiki kitajengwa katika eneo la Itega Jijini Dodoma na kitasaidia kuwajengea uwezo waraibu wa dawa za kulevya waliopata nafuu ili waweze kujikimu kimaisha na kuepuka kurejea kwenye matumizi ya dawa za kulevya,”Alieleza.

Vilevile ameeleza kuwa, serikali imeweka jitihada kubwa katika kuzuia matumizi ya dawa za kulevya nchini kwa kuimarisha elimu na mikakati ya kukabiliana na tatizo hili kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, semina, makongamano, mikutano, vilabu vya kupinga rushwa na dawa za kulevya shuleni na vyuoni.

Akibainisha mafanikio yaliyopatikana Waziri Jenista alieleza kwamba, mwaka 2023, Serikali ilianzisha kituo maalumu cha Habari na Mawasiliano (Call Centre) kilichopo katika ofisi za DCEA ambapo wananchi wanaweza kupiga simu namba 119 bila malipo na kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za Akikulevya au kupata elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya.

“Serikali imefungua Ofisi mpya tano za Mamlaka katika ngazi ya kanda ambazo ni nyanda za juu kusini ambayo ofisi zake ziko Mkoa wa Mbeya inahudumia Mikoa ya Mbeya, Songwe, Katavi, Rukwa Njombe na Iringa. Kaskazini ofisi zake ziko Mkoa wa Arusha inahudumia Mikoa ya Arusha, Manyara Kilimanjaro na Tanga,”Alitaja Mhe. Jenista.

Akiendelea kutaja Miko hiyo alisema kuwa ni Pwani ambayo inatoa huduma katika Mkoa wa Mtwara,Lindi, Ruvuma na Morogoro wakati Kanda ya ziwa ambayo ofisi zake ziko Mkoani Mwanza inahudumia Mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Geita, Simiyu na Shinyanga, pamoja na Kanda ya kati yenye ofisi Mkoani Dodoma inayohudumia Mikoa ya Dodoma, Kigoma Singida na Tabora.

Pamoja na mafanikio hayo alifafanua kwamba bado Serikali imeendelea kuwekeza katika udhibiti wa dawa za kulevya ambapo mwaka 2023 imenunua boti yenye kasi (Speed Boat) itakayotumika kufanya doria baharini kukabiliana na uingizaji wa dawa za kulevya kama vile heroine na methamphetamine.

Katika hatua nyingine Mhe. Jenista alisema Serikali imetunga Sera ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Mwaka 2024 ili kuhakikisha ushiriki wa wadau wote katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

“Sera hii itaimarisha udhibiti wa dawa za kulevya zinazozalishwa nchini kama vile bangi na mirungi. Pia itatoa maelekezo ya kufanya utafiti wa mazao mbadala katika maeneo yanayolima mazao haya ili wananchi wapate kilimo cha mazao halali. Zaidi ya hayo, sera hii inaelekeza kuwajengea uwezo wadau mbalimbali katika udhibiti wa dawa za kulevya ili kuboresha ufanisi wa mapambano haya,” alisisitiza Mhe. Jenista.

Aidha Mhe. Jenista alitoa wito kwa jamii kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na kusisitiza kuwa elimu ya kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya inapaswa kuanzia ngazi ya familia pamoja na Wazazi na walezi kushiriki katika kwa kuwajengea misingi bora watoto wao ili wasijiingize kwenye vitendo viovu na makundi hatarishi yanayoweza kuwaingiza kwenye matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

Kamishna Jenerali  wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA) Aretas Lyimo akifafanua jambo kuhusu  Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya Nchini kwa mwaka 2023 katika Ukumbi wa Habari Bungeni tarehe 16 Mei 2024 Jijini Dodoma.
Kamishna wa Kinga na Tiba Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA) Dkt. Peter Mfisi akieleza jambo wakati wa Mkutano wa waandishi wa Habari.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger