Tuesday, 18 October 2016

MPYA:TAARIFA KWA UMMA: KUHUSU UHAKIKI WA VYUO NA WANAFUNZI WANAOENDELEA NA MASOMO YA SHAHADA

 Image result for SERIKALI YA TANZANIA

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia Viongozi wa vyuo vyote vinavyotoa shahada nchini vya umma na vya binafsi kuwa kutakuwa na uhakiki wa ubora wa vyuo hivyo.
 
Uhakiki huo utaanza siku ya Jumatano Oktoba 19, 2016, hivyo, vyuo vyote vinatakiwa kutoa ushirikiano kwa timu za wataalamu zitakazofika kwa ajili ya kufanya uhakiki huo. 

Aidha, katika ukaguzi wa sifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo vyuo vyote, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), itatoa majina ya wanafunzi wanaotambuliwa na kwamba walidahiliwa kupitia TCU katika Programu zao za Shahada katika vyuo mbalimbali vinavyotoa shahada nchini siku ya Jumanne Oktoba 18, 2016.

Hivyo, wanafunzi wote wanatakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti ya TCU na kwa yeyote ambaye hataona jina lake awasiliane na Uongozi wa TCU haraka iwezekanyo ili kupata maelezo Zaidi. Mwanafunzi ambaye hatazingatia haya ndani ya wiki mbili atapoteza sifa za kuendelea na masomo.

Imetolewa na:
Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Share:

BREAKING NEWS:RAIS MAGUFULI KAMFUKUZA KAZI MRUGENZI WILAYA YA MKINGA-TANGA

Image result for RAIS MAGUFULI ATENGUA
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU MZUMBE SECOND ROUND 2016/2017

KUONA MAJINA

Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU NIT 2016/2017-1ST,2ND AND 3RD BATCH

Image result for NIT.AC.TZ
Share:

MPYA:SERIKALI KUTANGAZA ORODHA YA PILI(BATCH 2) YA WANAFUNZI WATAKAOPATA MKOPO 2016/2017

Image may contain: 9 people
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU ATC ARUSHA 2016/2017

 
List Of Students Selected By TCU To Join ATC Degree Programmes In 2016-17 Academic Year

The Arusha Technical College (ATC) is hereby releasing the names of selected candidates to join Bachelor’s
Share:

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU MBEYA UNIVERSITY-MUST 2016/2017 1ST,2ND AND 3RD ROUND


KUONA MAJINA
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU ST.JOHN DODOMA 2016/2017 BATCH 3

Image result for SJUT.AC.TZ
KUONA MAJINA HAYO 
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YOTE YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU MOUNT MERU 2016/2017

Header_text
Share:

MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SECOND ROUND VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017

Image result for TCU.GO
Habari yako,

Maswayetu blog,tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hapa
mjini,Tumeamua kukuwekea list ya vyuo vikuu ambavyo vimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa na joining instructions za  kujiunga na vyuo vikuu 2016/2017-SECOND ROUND



CHUO KIKUU TUMA-MBEYA                (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA MWL.NYERERE DAR & ZANZBAR CAMPUS                                   (2ND ROUND)                                                 >>BONYEZA HAPA<<                                                                                                                
CHUO KIKUU UDOM                             (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU SUA                                 (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU MUST                              (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO - OUT                                           (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO - KIKUU SEKOMU                      (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO - RUGAMBWA-SAUT BUKOBA  (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU ST.MARKS CENTER      (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU MIPANGO DODOMA    (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU ECKERN FORD             (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU RUAHA-IRINGA            (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU MWLNYERERE DAR     (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU TUMAINI-DAR              (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU ST.JOHN                         (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU MWENGE                       (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU ZANZBAR                        (2ND ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU IRINGA                         (2ND ROUND)     >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA MIPANGO DODOMA      (2ND ROUND)     >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA IFM                                      (2ND ROUND)     >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA UDSM,MUCE&DUCE       (2ND ROUND)   >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA MAKUMIRA-ARUSHA (SECOND ROUND)>>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA ARUSHA UNIVERSITY    (2ND ROUND)>>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA STEFANO MOSHI  (1ST &2ND ROUND)>>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA MARIAN (SECOND ROUND)                    >>BONYEZA HAPA<<


CHUO CHA SAUT-MWANZA (SECOND ROUND)       >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA TEKU(SECOND ROUND)                           >>BONYEZA HAPA<<


CHUO CHA MUCCOBS/MOCU(SECOND ROUND)     >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA BUGANDO(SECOND ROUND)                   >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA JORDAN (SECOND ROUND)                       >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA AMUCTA(SECOND ROUND)                       >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA KIU(SECOND ROUND)                                  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO CHA MUM(SECOND ROUND)                               >>BONYEZA HAPA<<


CHUO CHA MWEKA SECOND ROUND)                          >>BONYEZA HAPA<< 

 
CHUO CHA AJUCO SONGEA( 2ND ROUND)                  >>BONYEZA HAPA<< 
 
Share:

Jambazi Awajeruhi Kwa Bomu Askari na Raia Wanne Kigoma

Polisi na raia wanne wamejeruhiwa kwa bomu la kutupwa kwa mkono walipokuwa wakimkamata mtuhumiwa wa ujambazi kwenye Kijiji cha Uvinza mkoani Kigoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 14. 

Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Yahya Kamuhanda (49) mkazi wa kijiji hicho. Mtui aliwataja majeruhi hao kuwa ni askari polisi F.3187 Koplo Isaya na raia Saidi Mohamed, Seleman Kashali, Joseph Daudi na Hassan Nasibu, wote wakazi wa Kijiji cha Uvinza. 

Alisema askari walipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba Kamuhanda anajiandaa kufanya uhalifu hivyo waliweka mtego eneo la Uvinza Madukani alikokwenda kununua mahitaji. 

Alidai kuwa alipotambua anafuatiliwa alitupa bomu ndipo polisi walimpiga risasi mguuni na wananchi walimvamia na kumshambulia kabla ya askari kutumia nguvu kumwokoa asiuawe kwa kipigo. 

Mtui alisema mtuhumiwa alipohojiwa alisema alificha bunduki kijijini kwao Lukole wilayani Ngara mkoani Kagera, ambako askari walikamata SMG yenye namba 78GA5062 ikiwa imefukiwa ardhini.

 Pia, walikamata magazini saba, moja ilikuwa na risasi 40, nne (risasi 30 kila moja) na mbili (risasi 20 kila moja) na risasi 75 zilikuwa kwenye mfuko wa sandarusi. Pingu moja na funguo zake, maski tisa na laini 20 za mtandao wa Halotel ambazo hazijasajiliwa. 

Mtui alisema mtuhumiwa huyo alifariki dunia juzi akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni). Alisema majeruhi wote watano walipata matibabu hospitalini hapo na waliruhusiwa kurudi nyumbani. 

Share:

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Afikishwa Mahakamani Kwa Kosa La Kumtishia Bastola Askari wa Usalama Barabarani (Trafiki)

Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, Emmanuel Mkumbo kufikishwa ili apandishwe kizimbani kujibu mashtaka sita, likiwamo la kutishia kuua. 
Tukio zima la kumpeleka mahakamani, kumpandisha kizimbani na kumsomea mashtaka kwa muda wa dakika 30 hivi lilitawaliwa na vituko. Kwanza, ni jaribio la kuwaficha wanahabari. 
Kabla ya kufikishwa mahakamani, Polisi mkoani Morogoro iliwaarifu wanahabari kuwa ingetoa taarifa kuhusu mkurugenzi huyo lakini saa 4:30 asubuhi wakati Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Ulrich Matei akijiandaa kuzungumza nao, alipigiwa simu akatoka nje ya ukumbi na aliporejea alisema hawezi kutoa taarifa tena na akaondoka. 
Waandishi walipofika mahakamani saa 5:00 asubuhi walikuta Kamanda Matei akishuka kwenye gari na alipanda tena akasogea kando kuzungumza na baadhi ya askari wake. 
Pili, baada ya hakimu kumaliza kusikiliza kesi hiyo, Mkumbo hakurudishwa mahabusu mahakamani hapo kama ilivyo ada ili kusubiri utaratibu mwingine badala yake mshtakiwa huyo alihamishiwa chumba cha hakimu ambacho hakikuwa na kesi inayoendelea. 
Humo ndugu zake walimpelekea koti kubwa jeusi na kofia aina ya pama, hivyo alitoka akiwa tofauti na alivyoingia akiwa na fulana yenye rangi nyeupe, bluu na nyeusi. Baada ya kuvaa alitoka akiwa amezingirwa na polisi, huku ndugu wakiwazuia wanahabari kumpiga picha. 
Mashtaka dhidi yake
Mkumbo ambaye ni mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam alipandishwa kizimbani kujibu mashtaka sita, la kwanza likiwa la kutishia kuua kwa bastola na la pili ni la usalama barabarani lenye makosa matano.
Alisomewa mashtaka hayo na mawakili wa Serikali Sunday Hyera na Edgar Bantulaki. Katika shtaka la kwanza, mbele ya hakimu Agripina Kimaze anadaiwa Oktoba 15, saa 10:30 jioni alitenda kosa la kutishia kuua eneo la Mkambarani, Manispaa ya Morogoro.
Anadaiwa katika shtaka hilo la jinai namba 226 la mwaka 2016, alitishia kumuua kwa bastola askari namba 5057, Koplo Tuti Ndaga wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, kinyume na kifungu namba 89 (1),(2),(a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu namba 16. 

Katika shtaka la pili la ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani lenye makosa matano, ilidaiwa kuwa; kwanza, siku na muda huo eneo la Mbuyuni Mkambalani, mshtakiwa alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Prado lenye rangi ya kijivu bila kuwa na leseni. 
Pili, ilidaiwa alikuwa akiendesha gari hilo ambalo halikuwa na bima; tatu, alikutwa akiendesha kwa mwendo kasi; na nne, alikataa kupeleka gari Kituo cha Polisi cha Kingoluwira kama alivyoamriwa na askari, WP namba 5392 Sajenti Anna. 
Ilidaiwa katika shtaka la tano kwamba, wakati akiendesha alisimamisha gari katikati ya barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam kwa uzembe, bila uangalifu wala kuzingatia watumiaji wengine wa barabara. Mkurugenzi huyo alikana mashtaka yote yanayomkabili.
Hakimu Kimaze alitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kwamba awe na mdhamini mmoja kwa kila shtaka, yaani shtaka la jinai na la usalama barabarani lenye makosa matano, wote wawe wakazi wa Morogoro na mmoja akitakiwa kuweka dhamana ya Sh500,000 kwa kosa la kwanza na Sh1 milioni kwa kosa la pili. 

Mshtakiwa alikidhi masharti ya dhamana na kuachiwa huru, huku gari likiendelea kushikiliwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Morogoro.
Hakimu Kimaze aliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 31, usikilizwaji wa awali utakapoanza baada ya upande wa mashtaka kudai upelelezi umekamilika.
Share:

Watu 13 Kizimbani Kwa Mauaji ya Watafiti Dodoma

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger