Wednesday, 7 September 2016
HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO VYA TIA -UHASIBU KAMPASI YA DAR,MBEYA,SINGIDA,MTWARA&KIGOMA 2016/2017
Selected Candidates for Academic Year 2016/2017
The
following applicants have been selected to join various programmes
offered by the Tanzania Institute of Accountancy for the Academic year
2016/2017.
The selected candidates for Basic Technician Certificate and Diploma should report to their respective campuses on 12th September 2016. Postgraduate studies will commence on 15th October 2016.
This list includes the names of applicants who had applied before 3rd June 2016. Click the campus name below to view the list;
Basic Technician Certificate in Accountancy
Basic Technician Certificate in Business Administration
Basic Technician Certificate in Human Resource Management
Basic Technician Certificate in Marketing and Public Relations
Basic Technician Certificate in Procurement and Logistics Management
Basic Technician Certificate in Public Sector Accounting and Finance
Diploma Programmes
Postgraduate Programmes
1. All selected applicants must bring relevant original and copies of
their certificates, transcripts, result slips, a duly filled medical
examination form, one passport size photographs, birth certificate and
other relevant documents for registration.
2. The Institute has limited accommodation facilities for its students. Those who wish to stay at the Institute’s hostels should apply in advance before the start of the academic year.
3.Second selection list will be released soon after receiving the names from NACTE
The selected candidates for Basic Technician Certificate and Diploma should report to their respective campuses on 12th September 2016. Postgraduate studies will commence on 15th October 2016.
This list includes the names of applicants who had applied before 3rd June 2016. Click the campus name below to view the list;
DSM CAMPUS
MBEYA CAMPUS
SINGIDA CAMPUS
MTWARA CAMPUS
MWANZA CAMPUS
2. The Institute has limited accommodation facilities for its students. Those who wish to stay at the Institute’s hostels should apply in advance before the start of the academic year.
3.Second selection list will be released soon after receiving the names from NACTE
MPYA: TCU YATANGAZA SECOND ROUND APPLICATION KWA FORM SIX,DIPLOMA NA RPL 2016/2017

TAARIFA KWA UMMA
Tunapenda
kuutangazia Umma kuwa tulifunga mfumo wa pamoja wa udahili tarehe 31/08/2016
saa sita usiku ili kuchakata maombi ya waombaji waliofanikiwa kuomba udahili
kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Hata
hivyo kutokana na wengine kushindwa kufanikiwa kutokana na sababu mbali mbali,
Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 12 hadi
23 Septemba 2016 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili.
•
Waombaji
watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza
•
Waombaji
wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanza
•
Waombaji wenye vigezo vya Stashahada ambao
walishindwa kuomba kutokana na matokeo yao kuchelewa kufika NACTE kwa wakati,
•
Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya
“Cambridge” mwaka 2016 na matokeo yao yameshatoka,
•
Waombaji
waliofaulu mitihani ya RPL,
•
Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao
kuwa na uthibitisho toka vyuo vyao vya awali.
Baada ya hapo Tume haitaruhusu tena maombi ili kuruhusu
taratibu zingine za kiudahili kuendelea kwa ngazi ya Bodi ya Mikopo na vyuoni.
Asanteni
Imetolewa
na Prof. Eleuther Mwageni Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya
Vyuo Vikuu Tanzania 02 Septemba 2016
VIUNGO VYA MTOTO MCHANGA VYAZAGAA MTAANI SHINYANGA
VIUNGO vinavyodhaniwa kuwa ni vya mtoto
mchanga vimeonekana kuzagaa katika mtaa wa Butengwa, Kata ya Ndembezi,
Manispaa ya Shinyanga bila kufahamika ni nani aliyesababisha vizagae.Mwenyekiti wa mtaa huo, Juma Derefa alisema kuwa jana saa 5:00 asubuhi waliona viungo vya mtoto mchanga vikiwa vimezagaa mtaani na kutoa taarifa.
“Viungo hivyo vimeonekana mbali na makazi ya watu jirani wa kwenye mtaa wa Mwadui. Viongozi wake tumewashirikisha na hadi sasa hatujamtambua aliyefanya kitendo hicho cha kikatili cha kutupa au kutelekeza viungo hivyo,” alisema.
Alisema huenda wananchi wanafahamu nani aliyekuwa na mtoto au mjamzito na kufanya kitendo hicho.
“Ndio tumeanza uchunguzi kwa kushirikiana na Polisi,” alisema Derefa.
Diwani wa kata hiyo David Nkulila alisema tukio hilo alilipata baada ya kupewa taarifa na mmoja wa mjumbe wa serikali ya mtaa huo kuwa viungo vya mtoto mchanga vimebainika kuzagaa hovyo mitaani huku vingine vikiwa vimeng’atwa na mbwa lakini alishirikiana na viongozi wengine wa kata na kutoa taarifa jeshi la polisi.
“Sasa sisi tumeanza uchunguzi kwa kushirikiana na jeshi la polisi na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kubaini kichanga hicho kilitupwa na mhusika ni nani je? kilitupwa kikiwa hai au kimekufa hicho nacho tunafuatilia”,alisema Nkulila.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Elias Mwita alisema kuwa taarifa hizo wamezipata na wameanza kuzifanyia uchunguzi.
WATAHINIWA 795,761 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI LEO NA KESHO TANZANIA
WATAHINIWA 795,761 wanatarajia kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) unaofanyika leo na kesho nchini kote. Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde alisema wanafunzi 372,883 ambao ni sawa na asilimia 46.86 ni wavulana na wasichana ni 422,878 ambao ni asilimia 53.14.
Mwaka 2015 watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 775,729 huku 763,602 ndio waliofanya mtihani huo na wanafunzi 518,034 walifaulu.
Dk Msonde alisema watahiniwa 765,097 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 30,664 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiingereza ambayo wamekuwa wakiitumia katika kujifunzia. Masomo yatakayotahiniwa ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi, Hisabati na Maarifa.
Alisema watahiniwa wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani ni 95 wakiwemo wavulana 57 na wasichana 38 wakati wale wenye uoni hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 810 ambao kati yao wavulana ni 402 na wasichana ni 408.
“Maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika kiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za mitihani, fomu maalum za kujibia mtihani na nyaraka zote muhimu katika halmashauri na manispaa zote nchini,” alisema Dk Msonde.
Aidha, Dk Msonde alitoa mwito kwa kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha taratibu za mitihani ya Taifa zinazingatiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mazingira ya vituo vya mitihani yanakuwa salama, tulivu na kuzuia mianya ya udanganyifu.
“Wasimamizi wanatakiwa kusimamia kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu. Nawaaasa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani Baraza litachukua hatua kali kwa yeyote yule atakayebainika kukiuka taratibu za uendeshaji wa mitihani ya Taifa,” alieleza.
Na Anastazia Anyimike