Sunday, 21 February 2016

MPYA:APPLICATION ZA KUJIUNGA DIPLOMA YA AFYA 2016/2017-RUAHA UNIVERSITY

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

  • Application Requirement materials

     
  • Requirements for Diploma and Certificate Admission

     
  • Application Form For 2016-17

Share:

MPYA:CHUO KIKUU SUA KINAHITAJI NYUMBA KWA AJILI YA KUPOKEA WANAFUNZI KUTOKA ST.JOSEPH SONGEA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Mungai Arejesha Serikalini Ardhi Aliyokuwa Amejimilikisha Kinyemela

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Waziri zamani, Joseph Mungai amerejesha sehemu ya ardhi ya Hospitali ya Wilaya ya Mufindi, aliyodaiwa kuihodhi kinyume cha sheria.

Baada ya hatua hiyo ya Mungai ambaye aliwahi pia kuwa Mbunge wa Mufindi, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Dk Hamisi Kigwangalla ametoa siku saba kwa uongozi wa hospitali hiyo kujenga uzio ili kulinda mipaka yake.

Pia, ameutaka kupeleka ofisini kwake, ramani ya eneo lote la hospitali hiyo na taarifa itakayobainisha kumalizika kwa mgogoro huo.

“Haya ni mambo ya kisheria, isije ikawa leo mnasema mgogoro umekwisha halafu kesho tukasikia mzee Mungai kaenda mahakamani,” alisema Dk Kigwangalla.

Alizitaka halmashauri zote nchini kulinda maeneo yake kwa kuhakikisha yamesajiliwa na yana hati ili inapokuja mipango ya kuboresha au kutanua matumizi kusiwapo na changamoto.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jowika Kasunga alitoa taarifa ya kurejeshwa kwa eneo hilo na kusema lipo nyuma ya hospitali hiyo, mjini Mafinga.

Akizungumzia mipaka ya kiwanja cha hospitali hiyo baada ya waziri huyo kutaka kujua kama haijakumbwa na uvamizi kutoka kwa wananchi, Kasunga alisema eneo hilo lilikuwa na mgogoro wa muda mrefu baada ya Mungai kudai analimiliki kihalali.

Hata hivyo, alisema mgogoro huo umemalizika baada ya Mungai kuamua kulirejesha hospitalini.

Mbunge wa Mafinga Majini, Cosato Chumi alisema eneo hilo lilitengwa kwa  ajili majengo ya uzazi.

“Nashukuru mzee wetu ameamua kulirejesha eneo hilo na sasa lipo mikononi mwa Serikali,” alisema Chumi.

Katika hatua nyingine, Dk Kigwangalla alitoa miezi mitatu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Shaibu Nnunduma kukamilisha ukarabati wa vyumba vya upasuaji ambavyo hali yake ni mbaya vinginevyo, atatumbuliwa jipu.

Alisema kama angetembelea hospitali hiyo akiwa mkaguzi, angelazimika kufunga vyumba hivyo kutokana na hali yake kutoridhisha.

“Nimekagua na kujionea hospitali hii, kuna maeneo ya changamoto ikiwamo vyumba vyake vya upasuaji, nyie mnaona kama mnavyo lakini kiukweli ni kama hamna kwani vilivyopo vinafanana na stoo, siyo kipimo chake,” alisema Dk Kigwangalla.
Share:

Waziri Mkuu: Utumbuaji wa Majipu Haumuonei Mtu

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema utumbuaji wa majipu unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano haumuonei mtu, bali ni harakati za kupambana na wanaokwenda kinyume cha taratibu za nchi.

Akizungumza kwenye mkutano wa wadau uliolenga kutoa taarifa ya hali ya kiuchumi na maendeleo ya mikoa ya Katavi na Rukwa jana, Majaliwa alisema tangu Serikali ianze kuwawajibisha watendaji wazembe kumekuwa kukizuka maneno mbalimbali kwa baadhi ya watu wanaochukuliwa hatua hizo.

“Kaulimbiu yetu ya ‘Hapa Kazi Tu’ inalenga kuwakumbusha wananchi wote kuwajibika kwenye sekta zao ili kila mmoja azalishe na kutunisha pato la Taifa.

“Kipindi cha kampeni tuliahidi kupambana na hali hii, ndicho tunachokifanya ili kila mmoja atambue wajibu wake,” alisema Majaliwa.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Ibrahim Msengi aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Methew Sodeyeka kwa nyakati tofauti, walisema bado wakazi wa maeneo hayo wanakabiliwa na changamoto ya barabara. 
Share:

Chama cha ACT Wazalendo Chamvua Uanachama Ofisa Mipango Na Aliyekuwa Mgombea Urais Zanzibar Kwa Kuhudhuria Vikao Vya ZEC

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Chama cha ACT Wazalendo kimemsimamisha uanachama Ofisa Mipango wake, Ali Makame Issa kwa madai ya kukiuka maadili ya chama hicho.

Hata hivyo, Issa alisema jana kuwa hajapokea taarifa yoyote kutoka katika chama hicho.

Hatua hiyo dhidi ya kiongozi huyo mwandamizi ndani ya ACT, imekuja baada ya chama hicho kudai kuwa alishirikiana na aliyekuwa mgombea wa urais wa Zanzibar, Khamis Iddi Lila kuwahujumu.

Awali, Lila alisimamishwa uanachama kwa madai ya kutoa misimamo ya kushiriki uchaguzi wa marudio uliotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha.

Barua ya ACT, iliyosainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Juma Said Sanani imesema: “Kamati maalumu ya Zanzibar imekusimamisha rasmi uanachama kwa mujibu wa katiba ya ACT Ibara ya 11 (2) kuanzia leo Februari 19, 2016, kwa ukiukwaji mkubwa wa katiba Ibara ya 7 (3)(5)(9) Ibara ya 10 (2)(c) (d), Ibara ya 22 (1) (2) (4).”

Barua hiyo inabainisha kuwa mwanachama huyo amekiuka kanuni na maadili pamoja na kukidhalilisha chama.

“Huku ni kukiingiza chama katika mgogoro kwa kuandika barua ya kushiriki uchaguzi wa marudio na kuhudhuria katika kikao cha Tume ya Uchaguzi Februari 17 ukijua kuwa chama kimeshapeleka barua Febuari 9 ya kutoshiriki uchaguzi,” inaeleza.

Vyama vilivyowachukulia hatua viongozi wake kwa madai ya kukiuka kanuni ni Sauti ya Umma (SAU), kilichomfukuza aliyekuwa mgombea wake wa urais wa Zanzibar, Issa Mohamed Zonga, huku Alliance for Democratic Changes (ADC) kikimfukuza aliyekuwa mlezi wake, Hamad Rashid Mohamed
Share:

Wadaiwa Sugu Bodi ya Mikopo Kitanzini,CAG Apewa Jukumu La Kuwasaka Popote Walipo,Kutoajiriwa Sio Kigezo Cha Kukwepa Deni

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imetoa onyo kwa wadaiwa sugu ambao hawajajitokeza kuanza kulipa madeni yao, kwamba hatua mbalimbali dhidi yao zinatafuata kokote waliko.

Miongoni mwa hatua hizo, bodi hiyo imetaja kuwa ni kuwatoza wadaiwa hao sugu riba ya asilimia kumi katika deni lao na kutumia taarifa zao kuwazuia kufanya safari za nje ya nchi.

Taarifa ya hivi karibuni ya bodi hiyo , imeeleza kuwa wadaiwa hao wa tangu mwaka wa masomo wa 1994/95, wataanza kusakwa kupitia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambaye anawajibika kukagua mali zote za Serikali.

Mbali na CAG, ambaye ana mkono mrefu wa kuwasaka katika ofisi zote za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma, Serikali za Mitaa na katika miradi ambayo Serikali ina ubia na sekta binafsi, pia kampuni binafsi za ukaguzi wa hesabu, zenye mkono mrefu katika sekta binafsi, zitatumika kuwasaka katika kampuni binafsi na asasi za kiraia.

“Jukumu la CAG na kampuni zingine binafsi za ukaguzi wa mahesabu, ni kulazimisha waajiri kuwasilisha taarifa za wafanyakazi wao ambao ni wahitimu wa elimu ya juu na makato ya mkopo waliopewa,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imefanya marejeo ya Sheria ya Bodi namba 9 ya 2004 na marekebisho yake, inayomtaka kila mwajiri kutoa maelezo kwa maandishi kwa bodi, kuhusu mwajiriwa ambaye ni mnufaika wa mkopo huo, ndani ya siku 28 tangu mdaiwa alipoajiriwa.

Hatua
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mdaiwa yeyote wa bodi hiyo atakayeshindwa kulipa deni lake bila sababu za msingi, kwanza atakuwa akikabiliwa na kesi ya madai chini ya kifungu cha 6 C na H cha Sheria ya Bodi ya Mikopo namba 9 ya mwaka 2004.

Mbali na kukabiliwa na kesi hiyo, pia mkopo wake kwa namna unavyochelewa kuanza kulipwa, utakuwa ukijilimbikizia riba ya asilimia 10.

Taarifa hiyo ya bodi imeeleza kuwa mdaiwa huyo taarifa zake zitapelekwa katika taasisi za kumbukumbu ya mikopo zilizo chini ya Benki Kuu (BoT), ambazo zitazuia wadaiwa hao kupata mikopo katika mabenki na asasi zote za fedha.

Mdaiwa huyo pia atazuiwa kupata udhamini wa Serikali katika muendelezo wa masomo yake, lakini pia atazuiwa kujiunga na chuo chochote cha elimu ya juu ndani na nje ya nchi.

Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo, taarifa zao pia zitawasilishwa katika Idara ya Uhamiaji iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na katika ofisi zote za kibalozi, ili wakose kibali cha kusafiri nje ya nchi.

Hasara nyingine watakayokabiliwa nayo wadaiwa hao, ni Tozo ya Kulinda Thamani ya Mkopo (VRF) ya asilimia sita kila mwaka, itakayotozwa kwa kila mkopo, ili wadaiwa watakapoanza kulipa mkopo waliochukua, walipe kwa thamani ya sasa.

Tozo hiyo imelenga kuepuka athari ya mfumuko wa bei tangu mdaiwa aliponufaika, lakini pia kuwezesha urejeshwaji wa deni, uwe na thamani ya kumhudumia mwanafunzi mwingine mwenye mahitaji kwa sasa na baadaye.

Ambao hawajaajiriwa
Taarifa hiyo pia imeonya wadaiwa wanaodhani kuwa kutokuajiriwa ni sababu ya kutolipa mkopo huo, kwamba mkopo huo unatakiwa kulipwa baada ya kumalizika kwa mwaka mmoja tangu mdaiwa alipofanikiwa kuhitimu masomo yake, au mwaka mmoja tangu mhusika alipokatisha masomo yake kwa sababu yoyote.

Aidha, taarifa hiyo imeelekeza watakaojitokeza, kama wameajiriwa, asilimia nane ya mshahara wao wa kila mwezi, itatakiwa kukatwa na kuwasilishwa kwenye Bodi ili kulipa deni husika.

Lakini pia Bodi hiyo imetengeneza utaratibu kwa ambao hawajaajiriwa, kwamba wanaweza kulipa kiasi cha chini cha Sh laki moja kila mwezi katika akaunti za Bodi zilizopo Benki ya Posta yenye namba CCA0240000032; Benki ya NMB namba 2011100205 na Benki ya CRDB namba 01J1028467503.

Deni lenyewe
Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG, hadi Juni 2014, bodi hiyo ilikuwa imewakopesha wanafunzi Sh trilioni 1.8 kuanzia mwaka wa masomo 1994/95 na kati ya fedha hizo, Sh bilioni 51 zilitolewa na iliyokuwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.

Taarifa hiyo ya HESLB imetolewa siku chache kabla ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako  kusitisha ajira ya Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, George Nyatega kwa tuhuma za udhaifu katika fedha za mikopo zaidi ya Sh bilioni 3.2.
Share:

Wata Watatu Watiwa Mbaroni Kwa Kuvamia Kituo Cha Polisi Na Kuvunja Mlango Ili Kuwatoa Wenzao

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Watu watatu wamekamatwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuvamia Kituo cha Polisi cha Duthumi na kuvunja mlango kwa lengo la kuwatoa wenzao watatu wanaotuhumiwa kwa wizi wa mifugo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Graifton Mushi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 12.40 jioni.

Alisema polisi walilazimika kutumia silaha za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya watu hao.

Mushi alitaja silaha hizo kuwa ni mapanga, shoka na marungu. Hata hivyo, alisema wakati watu hao wanavamia kituo hicho watuhumiwa hao walishaondolewa kituoni hapo na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati. Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Katika tukio jingine; watu zaidi ya 20 wa Kitongoji cha Mazizini Kijiji cha Maseye Wilaya ya Morogoro wamevamia eneo la mwekezaji Ayubu Mngimbwa na kuteketeza vibanda vilivyokuwa na vifaa mbalimbali vya uchimbaji wa madini na kumshambulia kwa vipigo.

Kaimu Kamanda huyo alisema thamani ya vibanda na vifaa vilivyoteketezwa bado haijafahamika.

Alisema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro kati ya wananchi wa kitongoji hicho na mwekezaji anayedaiwa kutiririsha maji yenye kemikali za sumu.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARY 21 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger