Habai zenu,
Nikiwa kama blogger ni mwanahabari kupitia mtandao,nimekuwa nikipokea
picha mbalimbali kutoka mitandao ya kijamii mfano watsup na facebook
zikiwaandika wasukuma kuwa ndi wanao fanya mambo mabaya na tabia ambazo
hazieleweki.
Napenda kuchukua nafasi hii kukemea mara moja tabia hizi mbaya kwani
wasukuma pia ni kabila kama yalivyo makabila mengine,nimetokea kuishi
nao japokuwa mimi sio msukuma ila ni kati ya watu wastaarabu
sana,japokuwa picha hizo inaweza kuwa ni utani,lakini kwa hali
inavyoendelea nimeona si mbaya nikitoa mawazo yangu kwamba jambo hili
sio zuri hata kidogo,fikiria endapo wewe ndio mtumaji wa picha
hizo,kabila lako mfano ni mjita au mhehe ,je,unaweza kutuma picha
ikimuonesha mwanamke ambae kwa umri ni sawa na mama ako kwa
kumdhalilisha?
Jambo hili sio zuri hata kidogo,naombeni wale wote wenye tabia kama hizi
muache mara moja,kwani sio picha nzuri katika jamii,NAKUOMBA
MH.MAGUFULI INGILIA KTI SWALA HILI AU WAZIRI MWENYE WIZARA HUSIKA
SHUGHULIKIA SWALA HILI,kwani hali inazidi kuwa ni mbaya kila kukicha.
Imeandaliwa na kuandikwa na mimi INNOCENT THE BLOGGER BOY
(MASWAYETU BLOG TEAM)
Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) inatangaza orodha ya watumishi 5536 wa Mamlaka za Serikali
za Mitaa waliokidhi vigenzo na kupata kibali cha uhamisho katika kwa
kipindi cha Desemba 2015 na orodha ya watumishi 91 wa Mamlaka za
Serikali za Mitaa ambao hawajakidhi vigezo vya kuweza kuhamishwa.
Vile
vile, OR-TAMISEMI inatangaza orodha ya watumishi 23 ambao
walikwishapata uhamisho awali na orodha ya majina yao hayakuonekana
kwenye mtandao na kupelekea kutokukamilika kwa uhamisho wao.
Barua za uhamisho wa watumishi hawa zinapatikana kupitia Ofisi za
Wakurugenzi wanakotoka kuanzia tarehe 22/01/2015 na sio OR-TAMISEMI,
Ofisi za Wakuu wa Mikoa au Ofisi za Wakurugenzi wanakohamia.
Imetolewa na: - OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA