Tuesday, 8 April 2014

SOMA HABARI HIZI KUHUSU MASTAA WA BONGO

MASTAA MATAJIRI WACHUNGUZWA



KIMENUKA! Jeshi la Polisi Tanzania kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali zimeanza kuwachunguza watu wenye majina makubwa ‘mastaa’ Bongo ambao wameibuka na utajiri wa ghafla, Uwazi limeambiwa.
Masanja Mkandamizaji.
Kwa mujibu wa chanzo nyeti ambacho kiko ‘jikoni’ kwenye jeshi hilo, mbali na mastaa, wengine ambao tayari orodha yao ipo ni wafanyabiashara, wafanyakazi wa serikali na viongozi wa dini ambao wameibuka kuwa mamilionea kwa muda mfupi huku shughuli zao za…

ANAYEISHI KWENYE HANDAKI BALAA JIPYA!


CHACHA Makenge (38) aliyeripotiwa awali kuishi ndani ya handaki katika eneo la pori la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani, amepatwa na balaa jipya baada ya makazi yake kuvamiwa na askari, kukamatwa na mwishowe kupelekwa Muhimbili kitengo cha wagonjwa wa akili kwa ajili ya matibabu.
Chacha Makenge (38) akiota moto nje ya handaki lake katika eneo la pori la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.
Kana kwamba haitoshi, Makenge ambaye aliwahi kuishi…

MAAJABU YA MUNGU!


KATIKA hali ya kushangaza, wagonjwa wa mtindio wa ubongo, Paul Ngido na Asha Yahya wanaolelewa kwenye kituo cha watoto wenye matatizo mbalimbali wakiwemo yatima cha Ngido kilichopo Mazimbu FK mkoani hapa wamejikuta wakizaa watoto wawili, Keisha na Glory ndani ya kituo hicho.
Paul Ngido na Asha Yahya  wanaolelewa kwenye kituo cha watoto wenye matatizo mbalimbali waliowazaa watoto Keisha na Glory.
Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho, Linda Cyprian Ngido amethibitisha kutokea…

NJEMBA YAMBAKA MTOTO WA MIAKA MINNE


NI AIBU!Jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Iddi Mgosi anashikiliwa na Polisi wa Kituo cha Wazo jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka minne (jina linahifadhiwa) huko Mivumoni, Madale Machi 18, mwaka huu.
Mtoto wa miaka minne aliyefanyiwa unyama huo.
Mgosi, ambaye umri wake haukuweza kupatikana mara moja, anadaiwa kumrubuni mtoto huyo kutoka nyumbani kwao na kumpeleka kwake, ambako alimuingilia kwa nguvu na baadaye kumtisha…

TATIZO LA MACHINGA LINATAKA BUSARA

NINAWASALIMU kwa jina la Bwana Mungu, mwingi wa rehema na muweza wa kila jambo. Siku zote nimekuwa nikiwasihi kumuweka mbele muumba wa nchi na mbingu, kwani kwake hakuna lisilowezekana.
Wagambo wakiwa kazini katika operesheni bomobomoa maeneo ya Posta mpya.
Hivi sasa kuna kampeni kubwa ya kusafisha jiji kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni kubomoa vibanda vya biashara vilivyojengwa kinyume na taratibu katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Jambo hilo limesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa jiji…

UNAKUBALIKA KWENYE JAMII-2

BADO tunaendelea na somo letu ambalo safari hii nagusia upande wa maisha. Ndugu zangu, kukubalika kwenye jamii kuna manufaa makubwa kama nilivyosema wiki iliyopita.

Niliishia pale nilipofafanua hasara za kutokubalika kwenye jamii. Sasa leo tuendelee.
KWA NINI HUKUBALIKI?

Wakati naanza kabisa kuandika mada hii, nimeeleza kwamba kila kinachotokea duniani huwa na sababu zake. Haiwezekani ukawa hukubaliki kwa chuki za watu au watu kukuonea wivu.

Lazima kuna sababu zinazosababisha usikubalike. Najua kila mmoja anaujua ukweli wa maisha yake ndani ya moyo wake.
Hapa nitakuandikia sababu muhimu…

MBWA WALIOMLA MTOTO NUSURA WAMLE BABA MTU

Mtoto Christian Alex aliyeliwa na mbwa enzi za uhai wake.


ZIMEKATIKA wiki mbili tangu kuzikwa kwa mtoto Christian Alex (6)  aliyeuawa kwa kushambuliwa na mbwa watatu waliodaiwa ni wa Ubalozi wa Qatar nchini, mbwa hao wamemkosakosa baba mtu.

Tukio la kuuawa kwa mtoto huyo lilijiri Kunduchi  Jangwani Beach jijini Dar Machi  26, mwaka huu.
Kwa mujibu wa chanzo, mara baada ya kumaliza shughuli ya kumzika marehemu katika Makaburi ya Mburahati jijini Dar, baba mzazi Alex Augustino alikaa kikao na ndugu ili kuangalia uwezekano wa kufika kwenye makazi hayo ya ubalozi na kuzungumza nao kujua hatima ya sakata hilo.
Baada ya makubaliano,…

TUZO YA MWANAMKE BORA, HESHIMA YA KWELI YA MWANAMKE, PINDA NI MSOMI WA UWAZI


Mgeni rasmi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akihutubia kabla ya kukabidhi tuzo.

Mwanamke wa…

TUUCHOKONOE, TUUPINDUE ILI TUUBORESHE

WAJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba wanaendelea na mchakato wa kupitia vifungu vya Rasimu katika ngazi ya kamati, kabla ya keshokutwa kuanza rasmi mjadala wa namna gani Tanzania inaweza kupata katiba mpya, miaka 50 baada ya kuungana kwa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar.
Katika hatua za awali ngazi ya kamati, tumeshuhudia mambo mengi hasa yanayohusu hatima ya Muungano, ambao umekuwa ndiyo simulizi kuu katika mchakato mzima.
Kwa miaka mingi Watanzania tumeishi tukiaminishwa kuwa Muungano huu uko safi na yeyote aliyeonekana kuuzungumzia kwa namna ya kuukosoa, alichukuliwa kama msaliti, mhaini na mtu asiye na nia njema na nchi yetu.
Mambo mengi yanayohusu uhusiano wa nchi hizi mbili umekuwa siri kubwa, baadhi ya mambo yameharibika au kwenda mrama kwa kuwa kila mmoja alikuwa hataki kuonekana…

Share:

ANGALIA MAJINA HAPA YA WALIOPANGIWA VITUO VYA AFYA (AJIRA) 2013/2014

Share:

SOMA MAGAZETI YA LEO 08/04/2014

1_df6c1.jpg
2_60742.jpg
3_abfda.jpg
4_146e8.jpg
5_46469.jpg
6_6457f.jpg
66854_688389021225559_7905396027206939490_n_b7655.jpg
984038_688393924558402_8227931919131465226_n_48ad2.jpg
1012133_688388851225576_7974244423289239200_n_15ad8.jpg
1511914_688393854558409_4524716445678454352_n_6ca0e.jpg
1618432_688389154558879_4227702238964895763_n_49548.jpg
10150701_688389124558882_2727082128162427829_n_1_968cf.jpg
10151186_688392871225174_6366814600379550084_n_ab357.jpg
10154011_688392311225230_3505961519200983127_n_a0890.jpg
10155426_688398157891312_7651917783195626200_n_35ea1.jpg
10171238_688389074558887_9140776556010772895_n_46b35.jpg
Share:

Monday, 7 April 2014

VIDEO:ANGALIA FUMANIZI HILI HATARI SANA MKE WA MTU SUMU


Share:

MATOKEO YA AWALI UCHAGUZI CHALINZE

Share:

VIDEO:ANGALIA LIVE SHOW YA KHANGA MOJA ILIVYOFANA


Share:

Thursday, 3 April 2014

VIDEO:MTOTO ALIEZALIWA AKIWA HANA UBONGO


Share:

Tangazo la kazi:JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/G/09
01 Aprili, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki,
pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea
katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 482 za kazi kwa waajiri mbalimbali
kama ifuatavyo:
MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu
ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
1
vi.
Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne
na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo
mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa
sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Cheti cha Kompyuta
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
-
vii.
Shahada ya juu/Shahada/Stashahada ya juu/Stashahada/Astashahada.
Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
“Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati
matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
viii.
ix.
Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
xi.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 15 Aprili, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira
HAURUHUSIWI.
xiv.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
xv.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo;-
Katibu,
Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma,
SLP.63100,
Dar es Salaam.
AU
2
Secretary,
Public Service Recruitment
Secretariat,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.
1.0 AFISA TAWALA DARAJA LA II (ADMINISTRATIVE OFFICER GRADE II) –
(NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki.
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kusajili vizazi, vifo na ndoa na kutoa hati za viapo.
 Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu,
 Kuwapokea na kuwahoji wakimbizi wanaowasili,
 Kuweka kumbukumbu za Wakimbizi
 Kutunza na kugawa vifaa vya wakimbizi katika makazi.
 Kuainisha, kuchambua na kushauri kuhusu matatizo ya wakimbizi.
 Kusimamia nidhamu ya wakimbizi.
 Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu mbalimbali Serikalini
kutegemeana mahali alipo.
 Kusimamia kazi za utawala na uendeshaji katika ofisi za Serikali.
 Kutoa vitambulisho kwa wakimbizi.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na
Serikali katika fani zifuatazo:- Utawala, Sheria (baada ya internship), na
Menejimenti ya Umma
 Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
2.0 MCHUMI DARAJA LA II (ECONOMIST GRADE II) – (NAFASI 23)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki, Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya
Mipango na Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia .
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuhudumia kamati mbalimbali za Bunge (Kamati za mahesabu ya Serikali, Kamati
ya mahesabu ya mashirika ya Umma)
 Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya uchambuzi na
uandaaji wa sera na mipango ya kiuchumi na kijamii
 Kufanya utafiti na uchambuzi wa sera na vigezo vya kiuchumi jumla
 Kufanya utafiti na kubainisha fursa zilizopo katika sekta husika
3


Kukusanya taarifa na takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya
ustawi namaendeleo ya jamii.
Kutayarisha na kusambaza takwimu na taarifa za kiuchumi kwa wadau
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ambao wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya
fani zifuatazo;
 Uchumi (Economics)
 Takwimu (Statistics )
 Sayansi ya Uchumi Kilimo (BSc Agriculture Economics & Agribusness) kutoka
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Sokoine au Chuo kingine
chochote kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta
2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
3.0 MCHUMI DARAJA LA II (ECONOMIST GRADE II) – (NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuhudumia kamati mbalimbali za Bunge (Kamati za mahesabu ya Serikali, Kamati
ya mahesabu ya mashirika ya Umma)
 Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya uchambuzi na
uandaaji wa sera na mipango ya kiuchumi na kijamii
 Kufanya utafiti na uchambuzi wa sera na vigezo vya kiuchumi jumla
 Kufanya utafiti na kubainisha fursa zilizopo katika sekta husika
 Kukusanya taarifa na takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya
ustawi namaendeleo ya jamii.
 Kutayarisha na kusambaza takwimu na taarifa za kiuchumi kwa wadau
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya Uzamili ambao wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya
fani ya Uchumi (Economics) au Fedha (Finance) kutoka Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta
4
3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
4.0 AFISA MAENDELEO YA JAMII DARAJA II (COMMUNITY DEVELOPMENT
OFFICER GRADE II) – (NAFASI 2)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki na Katibu Mtendaji Ofisi
ya Rais Tume ya Mipango.
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandaa na kupendekeza mipango na mikakakati ya kubadili fikra za watu ili
waweze kuwa na mawazo ya maendeleo sawia na Sera za Serikali na wakati
uliopo
 Kupitia mbinu shirikishi kuwezesha jamii kuanzisha miradi ya kijamii kama vile:-
- Usafi wa mazingira
- Ujenzi wa nyumba bora
- Ujenzi wa shule
- Ujenzi wa zahanati
- Kuchimba au kuzifanyia matengenezo barabara hasa za vijijini
- Ujenzi wa majosho
- Uchimbaji wa visima vifupi
- Utengenezaji wa malambo
 Kuhamasisha matumizi endelevu ya mazingira
 Kusambaza na kuhamasisha matumizi ya teknolojia sahihi kama vile uvunaji wa
maji ya mvua, majiko sanifu, matumizi ya mikokoteni
 Kuhamasisha watu kutumia huduma za mafunzo ya Vyuo vya Maendeleo ya
Wananchi
 Kuwasadia wanachi vijijini kuandaa maandiko (Project Write ups) ya kuombea
fedha za kuendesha miradi yao
 Kuhamasisha, kuandaa na kutoa elimu kwa umma kuhusu uraia na Utawala bora
 Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kusambaza takwimu na kumbukumbu muhimu
kwa ajili ya matumizi ya jamii
 Kuwezesha wananchi kupambana na mila zenye madhara kwa afya za wanchi
hasa wanawake na watoto wa kike, kuenea kwa virusi vya UKIMWI na magonjwa
ya mlipuko.
 Kuelimisha viongozi wa Serikali za Vijiji, Dini na Mashirika yasiyo ya Kiserikali
kuhusu Sera mbalimbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na
kutumia Sera hizo
 Kutoa taarifa za hali ya jamii kwa ngazi mbalimbali
5
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa Shahada au Stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii
kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:-
 Maendeleo ya Jamii (Community Development)
 Elimu ya Jamii (Sociology)
 Masomo ya Maendeleo (Development Studies)
 Mipango na Usimamizi wa Miradi (Project Planning and Management)
 Maendeleo na Jinsia (Gender and Development)
4.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
5.0 AFISA HABARI II – (NAFASI 3)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki na Katibu Mtendaji Ofisi
ya Rais Tume ya Mipango.
5.1







MAJUKUMU YA KAZI
Kukusanya na kuandika habari.
Kupiga picha.
Kuandaa picha za maonyesho.
Kuandaa majarida na mabango (Posters).
Kukusanya takwimu mbalimbali.
Kuandaa majarida na vipeperushi.
Kuhifadhi picha na kuhudumia maktaba na marejeo.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Awe na Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu ya Uandishi wa Habari au sifa
inayolingana nayo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
6.0 MKAGUZI HESABU WA NDANI II (INTERNAL AUDITOR II) – (NAFASI 3)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki na Katibu Mtendaji Ofisi
ya Rais Tume ya Mipango.
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
6




Kufanya Ukaguzi wa hesabu katika Idara
Kusahihisha na kuidhinisha ripoti za ukaguzi
Kusahihisha na kuidhinisha hoja za Ukaguzi wa ndani
Kufanya kazi zingine atakazopangiwa.
6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiri wahitimu wa kidato cha sita (VI) wenye cheti cha kati cha uhasibu
(intermediate stage) kinachotolewa na NBAA au sifa zinazolingana na hizo.
 AU
 Wenye shahada/Stashahada ya juu ya uhasibu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na
serikali.
6.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
7.0 MHASIBU DARAJA LA II (ACCOUNTANT GRADE II) – (NAFASI 2)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki na Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuidhinisha hati za malipo.
 Kuandika taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi.
 Kusimamia Wahasibu Wasaidizi katika kazi zao za kila siku.
 Kusimamia shughuli za uhasibu kwenye Kitengo cha Idara.
 Kuandika taarifa ya maduhuli.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiri wahitimu wa kidato cha sita (VI) wenye cheti cha kati cha uhasibu
(intermediate stage) kinachotolewa na NBAA au sifa zinazolingana na hizo.
AU
 Wenye shahada/Stashahada ya juu ya uhasibu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na
serikali.
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
8.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III – (NAFASI 100)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
7
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
 Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
 Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
 Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
 Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
 Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
 Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
 Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
 Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na
kukusanya takwimu zao
 Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya Nchi
 Kudhibiti wanyamapori waharibifu
 Kudhibiti moto kwenye hifadhi
 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya
Uhifadhi Wanyamapori (Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka
Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa
na Serikali.
8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B2 kwa mwezi.
9.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III – (NAFASI 327)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
 Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
 Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
 Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
 Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
 Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
 Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
 Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
 Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na
kukusanya takwimu zao
8




Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya Nchi
Kudhibiti wanyamapori waharibifu
Kudhibiti moto kwenye hifadhi
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya Awali
ya Uhifadhi wa Wanyamapori (Basic Technician Certificate in Wildlife
Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.
9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B1 kwa mwezi.
10.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II – (NAFASI 10)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
10.1












MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
kusimamia uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
kulinda Nyara za Serikali
Kusimamia usafirishaji wa wanyamapori na nyara nje na ndani ya Nchi
Kusimamia matumizi ya magari ya doria
Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kutunza
takwimu zao
Kuratibu uingiaji wa wageni katika Mapori ya Akiba
Kudhibiti moto katika hifadhi
Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
Kukusanya takwimu za wanyama na mimea kwenye hifadhi
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Stashahada ya
Uhifadhi Wanyamapori (Diploma in Wildlife Management) kutoka Chuo cha
Usimamizi Wanyamapori Mweka au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
10.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
9
11.0 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – (NAFASI 2)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango.
11.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuendesha magari ya abiria, magari madogo na malori
 Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya
uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji
matengenezo,
 Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
 Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.
11.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C”
ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua
miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti cha Majaribio ya ufundi Daraja
la II (Trade test II).
11.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGOS.A kwa mwezi.
12.0 AFISA USAFIRISHAJI DARAJA LA II (TRANSPORT OFFICER GRADE II ) –
(NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango.
12.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kutayarisha gharama za uendeshaji wa usafiri kwa ajili ya kusaidia kutoa
maamuzi.
 Kuhakikisha kuwa takwimu na kumbukumbu zinazohusu vyombo vya usafiri
pamoja na mitandao yake zinatunzwa vyema na kwa usahihi. Kuandaa takwimu
zinazohusu maendeleo ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji, na kuwasilisha kwa
watumiaji ndani na nje ya nchi.
 Kukusanya takwimu za usafirishaji nchini.
 Kukadiria na kushauri juu ya utendaji wa miradi mbalimnbali ya sekta ya
usafirishaji.
 Kutekeleza majukumu mengine yanayohusu sekta ya usafirishaji
12.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Stashahada ya kawaida ya Usafirishaji kutoka Vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
10
12.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
13.0 AFISA MAZINGIRA DARAJA LA II – (NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango.
13.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kukusanya Takwimu na Taarifa mbalimbali zinazohusu Usimamizi na Hifadhi ya
Mazingira.
 Kutoa (disseminate) elimu ya Hifadhi ya Mazingira kwa Wadau mbalimbali.
 Kushiriki katika kuandaa Mpango wa kazi na bajeti.
 Kushiriki katika tafiti zinazohusu Usimamizi na Hifadhi ya Mazingira.
 Kufuatilia utekelezaji wa Sera na Sheria zinazohusiana na Usimamizi wa
Mazingira.
 Kufuatilia na Kuainisha Maeneo yanayopaswa kuhifadhiwa.
 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa kulingana na uwezo na taaluma yake.
13.2 SIFA ZA MWOMBAJI.
 Kuajiriwa wahitimu wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi/Sanaa yenye
mwelekeo wa Usimamizi na Hifadhi ya Mazingira katika moja ya fani zifuatazo,
‘Geography and Environmental Studies, Aquatic Environmental Science and
Conservation, Environmental Science and Management, Environmental
Laboratory Science Technology, Environmental Planning and Management’ au
sifa zinazolingana na hizo kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali.
13.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
14.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU (REGISTRY ASSISTANT) – (NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Mkurugenzi Mtendaji Mfuko wa Pembejeo za Kilimo na Mifugo.
14.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kusimamia usahihi (accuracy) wa kumbukumbu.
 Kugawa kazi na kusimamia kazi zote za masjala.
 Kuangalia barua zote zinazoingia, kutoka na kuweka kwenye majalada husika.
 Kutunza diary za (Bring up) na kuhakikisha zinafanyiwa kazi kwa wakati muafaka.
 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa kulingana na uwezo na taaluma yake.
11
14.2 SIFA ZA MWOMBAJI.
 Kuajiriwa wahitimu wenye Stashahada ya Kumbukumbu (Diploma in Records
Management) kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali.
 Awe na uzoefu wa miaka Sita (6) katika fani hii.
14.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Taasisi yaani GSS 5 kwa mwezi.
15.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II (WARD EXECUTIVE OFFICER
GRADE II) – (NAFASI 5)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri.
MAJUKUMU YA KAZI
 Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika
kata na atashughulikia masuala yote ya kata
 Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbal.i ya uzalishaji,
mali, kuondoa njaa na Umasikini.
 Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
 Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na Mtaa.
 Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata
yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika
Kata.
 Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo
lake.
 Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katikangazi ya Kata.
 Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na
nakala kwa Katibu Tarafa.
 Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa
vjiji, na NGO’S katika kata yake.
 Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji,
vitongoji, na kata yake.
15.1 SIFA ZA MWOMBAJI.
 Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social
Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Sheria au Sifa
nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali.
12
15.2 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D. kwa mwezi.
X.M. DAUDI
Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
13
Share:

Video:VURUGU BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


Share:

SIMULIZI TAMU YA WEMA SEPETU


Wema Sepetu.
WIKI iliyopita, Wema aliendelea kuelezea simulizi yake tamu ambayo imetokea kupendwa na wasomaji wengi wa Gazeti la Amani. Aliishia pale alipoweka wazi kisa cha kuachana na Chalz Baba, akaeda Marekani, aliporudi akawa na Diamond: Tujikumbushe kidogo kisha tuendelee…
Mwandishi: Nakumbuka ulipoondoka nchini kwenda Marekani ulikuwa na mapenzi na Chaz Baba, lakini uliporejea ikasikika kwamba upo na Diamond, nini kilitokea Wema?
Wema: (kicheko) yeah! Ni kweli kabisa, baada ya kuachana na Jumbe mwaka 2010 kama nilivyosema ndiyo nilianzana na Chaz Baba, nilimpenda, alinipenda. Na yeye ilikuwa tuoane, lakini nimeshasema nikiwa Marekani nilikuwa nasikia leo Chaz alikuwa na huyu, kesho alikuwa na yule, nikamwambia mimi na wewe basi.
Mwandishi: Kwa Chaz Baba mama yako alimkubali awe mumeo?
Wema: Kusema ukweli hakuwa muwazi kwa Chalz Baba, kwamba anamkubali au hamkubali. Lakini ikawa hivyo, tukaachana.
Mwandishi: Baada ya kuachana na Chalz ukajikuta upo kwa Diamond, nini kilikuvutia kwake?
Wema: Nasibu (Diamond) ilitokea kama nilivyokwishasema. Kwa hiyo mtu unajikuta umezama kwake. Wakati mwingine ni vigumu kusema mtu uliyenaye alikuvutia kitu gani!
KUHUSU KIINGEREZA CHA DIAMOND
Mwandishi: Wema, ni kweli Diamond amejua Kiingereza kwa ajili yako?
Wema: Kwanza niweke sawa hapo. Nasibu si kwamba amejua Kiingereza kwa ajili yangu, bali amejua kuzungumza Kiingereza vizuri. Ina maana tangu awali alikuwa anakijua lakini si kivile.
“Mimi na Nasibu tumekaa pamoja mwaka mzima kama mke na mume baada ya mimi kutoka Marekani mwaka ule 2011. Sasa si unajua mimi kidogo nakijua vizuri. Kwa hiyo kwa miezi kadhaa ya nyuma katika kuishi kwetu alikuwa akipata tabu kidogo.
“Ila nataka kukwambia kwamba, Nasibu ni makini sana. Hakuna mtu makini kama yeye. Akiwa hajui kitu lazima akuulize, hakai kimya.”
Mwandishi: Pamoja na sifa zote hizo, lakini mwisho wa siku wewe na Diamond mlimwagana kwa awamu ya kwanza, ilikuwaje?
ALIVYOMFUMANIA JOKATE
Wema: Tuliachana baada ya yeye kunisaliti na Jokate (Mwegelo). Unajua nilimwamini sana na sikuwahi kuwa na shaka naye hata siku moja, nilimwamini kupitiliza nikijua ni wangu na mimi ni wake.
“Lakini nadhani haya mambo ya kumwonesha mtu kwamba unampenda sana ndiyo tatizo. Hasa baadhi ya mwanaume.
“Siku moja nakumbuka nikiwa sina hili wala lile, nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi pale Piccolo, baada salamu akaniambia ‘unajua kama Diamond na Jokate wako hapa na wanapigana mabusu?’
“Nilichanganyikiwa sana, nikachukua teksi, nikaenda.
Kufika, kitu cha kwanza nililiona gari lake likiwa kwenye maegesho. Niliingia ndani, nikawakuta wamewekeana miguu. Niliwasalimia lakini hawakuitika.
“Kwa vile niliona kila kitu niliaga na kuondoka huku nikilia. Usiku Nasibu aliporudi alinikuta napanga nguo kwenye begi niondoke zangu, abaki mwenyewe. Hakutaka kuongea na mimi na mimi sikutaka kuongea naye, tukachuniana. Niliamua kutoondoka lakini mimi na yeye hatukulala kitanda kimoja kwa wiki moja. Alijua naumia lakini hakutaka kuanza.
AMWAGANA NA DIAMOND
“Siku moja isiyokuwa na jina, niliamka nikapanga nguo zangu kwenye begi nikaenda kwa dada yangu, Sinza. Ndiyo ikawa kimoja, nikamwacha yeye aendelee na maisha yake na mimi nikaendelea na maisha yangu. Lakini mimi na Jokate kwa sasa tuko vizuri tu.
Mwandishi: Oke, hiyo ilikuwa awamu ile ya kwanza, si ndiyo?
Wema: Yeah!
VIPI KUHUSU HARTMANN?
Mwandishi: Iliwahi kusemekana kuwa kuna wakati uliangukia kwenye penzi la mjasiriamali anaitwa Hartmann Mbilinyi, ni kweli?
Wema: Yale yalikuwa maneno ya watu. Unajua Hartmann nilikuwa nafanya naye kazi za filamu, wakati ule alikuwa na kampuni yake inaitwa Hartmann Production, watu wakadhani ‘nadate’ naye, si kweli bwana.
BAADA YA DIAMOND, NANI ALIFUATA?
Mwandishi: Wema, unaweza kutuambia mwanaume gani alifuatia baada ya wewe kuachana na Diamond akawa na Jokate?
Itaendelea wiki ijayo

Share:

WEMA AZUA TIMBWILI GLOBAL PUBLISHER KISA STORI YA DIAMOND


HOVYOOO! Wema Isaac Sepetu aliye pia Miss Tanzania 2006, amejitoa fahamu kwa kupandisha mzuka na kutinga makao makuu ya Kampuni ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar na kuzua timbwili la aina yake kisa kikiwa ni kuandikwa kwa habari zake na mpenziwe, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Wema akiwa ndani ya ofisi za Global na sura ya 'kuua mtu', mkononi akiwa na gazeti la Ijumaa Wikienda lenye stori: DIAMOND ATAMANI USHOGA. Kushoto ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
Tukio hilo la kumchoresha staa huyo mwenye vituko kila kukicha, lilijiri Jumatatu iliyopita kwenye ofisi za Global ambao ni wachapishaji wa gazeti hili (Amani), Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Risasi majira ya mchana kweupe hivyo kufunga mtaa huku wapita njia wakimzodoa kwa maneno ya kejeli.
ATINGA NA WAPAMBE DHAIFU
Akiwa na kundi la wapambe dhaifu na goigoi wakiongozwa na meneja wake, Martin Kadinda waliosimama nje ya ofisi hizo, Wema alifika kwa upole akionekana mkarimu kwa mlinzi ambapo aliomba kuonana na mwandishi nguli wa magazeti pendwa, Imelda Mtema.
Mlinzi alimruhusu kwa vile Global ni mjengo wa mastaa na watu wasio mastaa, huwa hawakauki kuingia na kutoka kwa mambo mbalimbali.
Wema alipofika mapokezi, pia aliomba kuonana na mwandishi huyo lakini tofauti na utaratibu ambapo huwa mgeni akifika huulizwa kama ana ‘apointimenti’ ili aitiwe anayemhitaji, Wema alipitiliza kwa nguvu hadi chumba cha habari akifuatana na kijana aliyekuwa akimrekodi.
Wema akiwa ndani ya News Room akimtafuta mwandishi wa Global Imelda Mtema, huku akisema yeye ni chizi!
Akiwa ndani ya chumba cha habari, Wema aliuliza kwa sauti ya juu na ya kujiamini: “Imelda yupo wapi? Nauliza Imelda yupo wapi?”

WEMA NA IMELDA
Katika kumtafuta Imelda kwa macho kwa sababu chumba cha habari ni kikubwa huku akionywa na wahariri kwamba atulize mzuka kisha aeleze shida yake, Wema alimuona Imelda akitoa maelezo kwa Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka kuhusu habari aliyokuwa ameifuatilia.
Cha kushangaza, Wema alimfuata Imelda mpaka kwenye meza ya mhariri huyo kisha kuanza kufoka kwa sauti ya juu.
MSIKIENI WENYEWE
“Kwa nini mnafuatilia maisha yangu? Kila siku mnaniandika na Diamond. Kwa nini Imelda unaniandika kuwa mimi msagaji?”
"Mimi ni chizi, nakwambieni mimi ni chizi zaidi ya machizi wote"....Wema alikuwa akifoka mwanamke!
ATULIZWA, AGOMA
Katika kuhoji huko, mhariri kiongozi alijaribu kumtuliza Wema ambaye alikuwa kama amewehuka: ”‘Wema tuelewane, eleza shida yako kwa utaratibu kwani hakuna ofisi isiyokuwa na utaratibu.”
Pamoja na kuambiwa hivyo bado Wema aliyekuwa ameshika Gazeti la Ijumaa Wikienda toleo la Jumatatu iliyopita, aliendelea kumng’ang’ania Imelda ambaye alikuwa akijaribu kumtuliza:
“Wema twende tukakae pale kwenye meza ya mkutano uwaeleze viongozi wangu tatizo lako. Hiyo stori kuwa wewe ni msagaji mbona haipo, ni gazeti gani?”
"Mimi ni chizi, msinitanie ohhh!!
Licha ya kupewa mwongozo huo, Wema aliendelea kufoka:
“Hivi mnajua mimi ni chizi? Kwa taarifa yenu mimi ni chizi zaidi ya machizi wote, ohooo!”

MLINZI ATONYWA, ATIA TIMU
Baada ya hali kuwa tete, mlinzi wa geti kuu alipigiwa simu ya mezani na kujulishwa juu ya Wema kusababisha kazi kusimama ambapo alifika haraka tayari kwa kumtoa nje kwa hiyari yake au lazima.
Ndipo kukatokea timbwili kubwa, wapambe wake ‘goigoi’ nao waliingia wakitaka kufanya vurugu ili kumteka mwandishi huyo lakini kikosi imara cha Global kikiongozwa na Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally kilijiimarisha na kutuliza fujo hizo huku kikiwa makini kuhakikisha Wema na timu yake hawajeruhiwi hata kidogo.
WEMA ATUMIA GAZETI KAMA SILAHA
Katika purukushani hiyo, Wema alionesha udhaifu wa kumudu varangati pale alipotumia gazeti aliloshika kumpiga nalo mwandishi Imelda, jambo lililodhibitiwa kama Waasi wa M23 wa Kongo walivyodhibitiwa na Majeshi ya Umoja wa Mataifa, akatolewa nje.
Wema akiwa nje ya ofisi sasa baada ya kutolewa kwa nguvu, yeye pamoja na wapambe wake
MBALI NA WEMA
Ukiachia mbali Wema kutulizwa kwa kutolewa nje kwa nguvu, vijana wake walegevu nao waliwekwa chini ya himaya ya Global kwa kunyang’anywa  kamera ya video iliyokuwa ikitumika kuchukua matukio huku nao wakipigwa picha za kutosha na wapiga picha wetu.
VITA KUBWA, WEMA AVUA VIATU
Nje ya ofisi, ‘vita’ kubwa kati ya Wema na walinzi wa Global (alifika mwingine kutoka lindo la mbali) ilizuka ambapo staa huyo alivua vile viatu vyake virefu vya rangi ya bluu bahari na kuanza kumpiga navyo mmoja wa walinzi hao akiamini anamkomesha lakini pia akadhibitiwa!
Wema akiwa ameshika viatu vyake vya mchuchumio mkononi baada ya kutolewa nje ya ofisi na wapambe wake akiwemo meneja wake, Martin Kadinda (kulia).
Wema akiwa anarandaranda kwenye geti kuu akiwa peku, alidondosha matusi ya nguoni ambayo hayaandikiki gazetini kwa namna yalivyokuwa makali. Ilikuwa si rahisi kuamini kuwa yeye ni kioo cha jamii.
Timbwili la Wema na wapambe wake akiwemo Petit Man, ambao hawakufua dafu kwa walinzi na vijana wa Global nje ya ofisi hizo, lilichukua zaidi ya nusu saa huku likikusanya kadamnasi na kusababisha mtaa kujifunga wenyewe.
Wema akiwa kafura ka' faru aliyekoswa koswa kung'olewa kipusa na majangili, kulia ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
POLISI HAO
Hata hivyo, uongozi wa Global uliwasiliana na Polisi wa Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar ambao walifika na kumkuta Wema na timu yake wakiwa wamepoa mlangoni, wakaambiwa timbwili limetulia hivyo wakatimua zao.
'Baby' wa Diamond Platnumz alikuwa hashikiki viatu viligeuka kuwa 'mzigo mzito' akivibagwa chini huku akitoa mkwara akiwa pekupeku na kufunga mtaa.
Ilibidi askari polisi waitwe kuja kuhakikisha utulivu unakuwepo huku wapita njia wakiwa hawaamini macho yao kuwa wanayemuona mbele yao 'peku peku' akimwaga mitusi ni Miss Tanzania, Wema Isaac Sepetu!
APEWA KAMERA, KADI NOOOO!
Baadaye Wema aliomba kupewa kamera yake ambapo zoezi hilo lilifanyika lakini ‘memori kadi’ yenye picha walizoanza kurekodi, ilitolewa ili kupisha maridhiano kwanza. Waliambiwa kadi hiyo ilitolewa kwa sababu walirekodi bila idhini au kibali cha Kampuni ya Global.
Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye msafara wa Wema ni pamoja na Ammy Nando (kushoto), mshiriki wa Big Brother Africa 'The Chase' ya mwaka jana ambaye alikuwa akificha sura kukwepa kamera za Global.
WEMA AGOMA KUONDOKA
Baada ya kugundua kadi ya kamera ipo chini ya ulinzi wa Global, Wema alitaka kulianzisha tena akidai hawezi kuondoka hadi apewe kadi hiyo lakini uongozi uliweka ngumu. Baadaye aliondoka kimyakimya. Wakati huo wapambe wake walishaondoka kitambo.
WEMA: CHIZI in action......
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, kadi ya kamera hiyo bado ilikuwa inashikiliwa na uongozi wa Global ili kumthibitishia Wema kuwa hawezi kufanya umafia wowote dhidi ya waandishi wa kampuni hiyo yenye nguvu kihabari nchini Tanzania.
Gari lake lililomleta Global kufanya timbwili.
KWA NINI?
Kwa mujibu wa Wema, magazeti ya Global yamekuwa yakimwandika vibaya yeye na mpenzi wake Diamond huku akitolea mfano wa habari iliyomhusu yeye na mwigizaji Aunt Ezekiel baada ya kunaswa kwa picha zao zilizoashiria vitendo vya usagaji.
Share:

VIDEO:SHOW YA DIAMOND AKIWA NA WEMA SEPETU

Tazama show ya msanii wa kizazi kipya diamond paltinumz
Share:

HALMASHAURI YA JIJI YABOMOA MEZA ZA MACHINGA POSTA DAR


HALMASHAURI YA JIJI YABOMOA MEZA ZA MACHINGA POSTA DAR

Maafande wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi leo wameendelea na bomoabomoa ya meza za wafanyabishara ndogondogo 'Wamachinga' kama walivyonaswa na kamera yetu maeneo ya Posta Mpya…
Maafande wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi leo wameendelea na bomoabomoa ya meza za wafanyabishara ndogondogo 'Wamachinga' kama walivyonaswa na kamera yetu maeneo ya Posta Mpya jijini.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger