Monday 17 August 2015
LAWRENCE MASHA AJIUNGA NA CHADEMA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana (2005-2010) jijini Mwanza
kwa tiketi cha Chama cha Mapinduzi(CCM) Lawrence Masha leo hii amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jijini Arusha wakati wa kumtabulisha mgombea wa UKAWA na CHADEMA mheshimiwa Edward Lowassa.

MAELFU YA WAKAZI WA MWANZA WAMLAKI MH EDWARD LOWASSA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mgombea urais wa UKAWA Mh. Edward
Lowassa ameendelea na ziara yake ya kutafuta wadhani ambapo alianzia
jijini Mbeya tarehe 14/8/2015 katika viwanja vya Rwanda nzovwe maarufu
kama uwanja wa Dr Slaa na kufuatiwa Jijini Arusha tarehe 15/8/2015
katika viwanja vya Tindigani na kumaliziwa Jijini Mwanza tarehe
16/8/2015 katika viwanja vya Furahisha. Katika mikutano yote hiyo
kumekuwa na mwamko mkubwa sana wa wananchi waliojitokeza kumpokea
mgombea urais wa UKAWA. Alipotua katika kiwanja cha ndege Mwanza
alikutana na umati mkubwa wa watu waliomsindikiza mpaka sehemu ya tukio.
Mbali na kuwa na umati mkubwa wa wafuasi katika mikutano hiyo viongozi wa vyama vinavyounda umoja huo wameendelea kusistiza kuwa Watanzania wajitokeza kwa wingi wao siku ya kupiga kura na walinde kura zao na huku wakitoa matamko mbalimbali juu ya vyombo vya Ulinzi na Usalama kusimamia haki na kulinda usalama wa Watanzania sio kutumika na baadhi ya viongozi kwa maslahi yao binafsi na kuwa hali hiyo ikipuuzwa italeta machafuko katika Taifa.