Ofisi ya DVC SUA imtoa taarifa kwa uuma na wanafunzi wote kwamba ,Chuo hadi sasa hakijapokea pesa ya field kutoka BODI YA MIKOPO,hivyo basi chuo kinwaomba wanafunzi waendelee kukaa nyumbani hadi hapo maelekezo mengine yatakapotolewa.
WAZIRI
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba amewanyooshea kidole
maofisa ugani wa mifugo na uvuvi kwa maelezo kuwa wameacha kutimiza
majukumu yao na badala yake wanakamata zana haramu za uvuvi, kuuza dawa
na kuomba hongo.
Dk
Tizeba alisema hayo juzi alipotembelea maonesho ya kitaifa ya mifugo
katika viwanja vya maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea katika
Viwanja vya Maonesho ya Kilimo Kanda ya Kati Nzuguni mjini Dodoma.
Alisema
maofisa ugani upande wa kilimo, ufugaji na uvuvi hawawajibiki ipasavyo
na wamejibadilisha kuwa wafuatiliaji na wakamataji wa zana haramu za
uvuvi, kuuza dawa za mifugo na kupokea hongo.
Pia alisema maofisa nyama wamebaki kuchukua baadhi ya nyama kama hongo na kuruhusu nyama kuuzwa bila kukaguliwa kitaalamu.
Alimuagiza
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Mary Mashingo kufuatilia utendaji kazi
wa Baraza la Usajili wa Maofisa Ugani hao, huku akimtaka pia mwenyekiti
wake wa bodi hiyo kumpatia mpango kazi walionao na changamoto zilizopo
katika kuwasimamia ili wawajibike vyema zaidi.
Dk
Tizeba alisema baraza hilo, mwenyekiti wake wa bodi kuhakikisha kuwa
anatengeneza mfumo utakaotoa vibali vya muda utakaowezesha bodi yake
kuwapima utendaji wao kwanza kabla ya kuwapatia usajili wa kudumu.
Pia
alimuagiza katibu mkuu kutoa maagizo kwa halmashauri zote nchini ili
maofisa ugani hao wanapotekeleza wajibu wao chini ya usimamizi wa
wakurugenzi wao wawe na mfumo ulio wazi na wenye tija katika kuwahudumia
walengwa vizuri zaidi na si kama wanavyofanya sasa kwani hawawajibiki
na hawasimamiwi ipasavyo.
Ofisa
Mifugo wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Gracian Mwesiga alisema inawezekana
kuwepo kwa maofisa mifugo wasiotimiza majukumu yao, lakini kwa mwenendo
wa sasa wa serikali wanatakiwa kupendekeza na kupitisha sheria
itakayompa meno mwenyekiti wa bodi ya usajili wa maofisa ugani ikiwamo
kufuatilia utendaji wao baada ya kuwasajili.
“Usimamizi wa maofisa mifugo upo kwenye halmashauri na si katika baraza ambalo kazi yake ni kusajili wataalamu,” alisema Mwesiga.
MWANAFUNZI
aliyekuwa akisoma Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Zimba, Bonde la
Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, Susana Kauzeni (15) ameuawa baada ya
kupigwa na wazazi wake wakimtuhumu kuwa ni mtoro sugu wa shule.
Ofisa
Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga (Shule za Msingi), Peter
Fusi amesema kuwa mwanafunzi huyo alizikwa kijijini humo Julai 23, mwaka
huu.
“Baba
na mama yake walichangia kumpiga binti yao huyo wakimtuhumu kuwa ni
mtoro sugu wa shule pia nyumbani amekuwa haonekani. Baba yake mzazi
amekimbia baada ya kufanya uhalifu huo huku mama yake akiwa ameshikiliwa
na Jeshi la Polisi,” alieleza Fusi.
Fusi
alieleza kuwa kuanzia Agosti 3 na 4, mwaka huu alitembelea baadhi ya
shule za msingi zilizopo kwenye Bonde la Ziwa Rukwa ikiwemo Shule ya
Msingi Zimba kufuatilia kazi ya utengenezaji wa madawati mapya kwa ajili
ya shule za msingi pia kufuatilia takwimu sahihi za wanafunzi ili
kubaini wanafunzi hewa.
“Nilipofika
kwenye Shule ya msingi Zimba, Mratibu Elimu Kata, Daudi Moga na Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo, Fidelis Mwangurumba walithibitisha kutokea kwa
mauaji hayo ya mwanafunzi huyo,” alisema.
Kwa
mujibu wa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mwangurumba, mwanafunzi huyo
alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi watoro sugu shuleni hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo.
Wakati
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akiwa nje kwa dhamana baada ya
kupandishwa kizimbani kwa makosa matatu yakiwamo ya uchochezi, Jeshi la
polisi mkoani Geita limevamia Hoteli ya KG iliyopo mjini Geita
aliyokuwa amefikia Katibu wa Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Miku na
Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Geita, Neema Chazaile na kuwashikilia kwa
tuhuma za uchochezi wa kutumia mitandao ya kijamii.
Taarifa
zilizopatikana kutoka kwa uongozi wa Chadema Mkoa wa Geita na
kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa, Mponjoli Mwabulambo zimedai
kuwa katibu huyo alikamatwa jana saa 12 asubuhi.
Katibu
wa Chadema Mkoa wa Geita, Sudy Mtanyagala alidai kwamba askari wa
polisi zaidi ya 10 wakiongozwa na Kamanda wa Upelelezi Mkoa (RCO)
waliizunguka hoteli aliyokuwa amelala katibu huyo wakidai wanatafuta
majambazi yenye silaha.
Mtanyagala
alidai kuwa polisi hao waliingia chumba baada ya chumba na walipofika
katika chumba cha mwisho ambacho ndicho alichokuwa amelala katibu huyo
walimkamata na kuchukua simu yake.
Alisema
baada ya kumkamata walisoma nyaraka za chama alizokuwa nazo kisha
kumtaka yeye na mwenyekiti wa Bavicha kuongozana na polisi hadi kituoni
kwa uchunguzi zaidi.
Alisema
katibu huyo wa kanda pamoja na mwenyekiti wa Bavicha mkoa walikuwa
wakijiandaa kwa kwenda katika ziara Wilaya ya Nyang’wale ambako
wangefanya mikutano ya ndani na viongozi wa chama hicho.
Katibu
wa Chadema Wilaya ya Geita, Hellena Thobias alisema walipata taarifa za
kukamatwa kwa viongozi hao asubuhi na kufika polisi.
Alisema
baada ya kufika polisi, maelezo yalibadilika na kuelezwa katibu wao
anatuhumiwa kwa uchochezi kwa kutumia mitandao ya kijamii.
Alisema
wamejitahidi kuomba dhamana lakini imeshindikana baada ya kuelezwa kuwa
watuhumiwa hao watakuwa chini ya uangalizi wa polisi kwa uchunguzi
zaidi.
“Polisi
wametunyima dhamana hadi saa 10 jioni tuko polisi tumeomba dhamana
wamekataa sijui ni sheria gani inayomzuia mtu kupata dhamana lakini pia
sijui ni sheria gani ya polisi kumnyang’anya mtu simu yake bila ridhaa
na kuichunguza. Hatutanyamaza juu ya uonevu huu,” alisema.
Alisema
Serikali imekataza mikutano ya hadhara na kueleza kusikitishwa kwake
na hatua ya jeshi la polisi kufuatilia hadi mikutano ya ndani ya chama
hicho ambayo ni haki yao kikatiba.
Akizungumza
kwa simu na mwandishi, Kamanda Mwabulambo alikiri jeshi lake
kuwashikilia katibu huyo wa Chadema wa kanda na mwenyekiti wa Bavicha
mkoa lakini akasema yupo nje ya ofisi hivyo hawezi kulizungumzia jambo
hilo kwa undani.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Ada Tadea, John Shibuda amesema Rais John Magufuli
“ni katili kwa wahujumu wa ustawi na maendeleo ya Taifa na rafiki kwa
waadilifu”, na kuwataka Watanzania kumuunga mkono kwa ukatili huo ambao
amesema unabezwa na baadhi ya watu.
Shibuda,
ambaye alikuwa mbunge wa Maswa Magharibi kwa tiketi ya Chadema na CCM
kwa vipindi tofauti, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi
wa habari mjini Shinyanga.
Alisema
wanaodai Rais Magufuli ni dikteta hawajui viwango vya ubora wao katika
kutoa hukumu hiyo na kuwataka kuchagua kupendezesha waadilifu ili kwenda
peponi au waovu waliojipanga kwenda jehanamu.
“Ndugu
zangu ukweli haulogeki. Mahimizo ya Rais si udikteta, bali ni dhamira
ya kuibua msisimko wa uhuru na maendeleo na uhuru ni kazi na asiyefanya
kazi asinufaike na jasho la Watanzania,” alisema Shibuda ambaye anasifika kwa uwezo wake wa kutumia vizuri lugha ya Kiswahili.
Shibuda
alisema kama Magufuli ni katili, basi dini zote ni katili kwa kuwa zina
amri za Mungu ambazo zinawakataza watu kufanya mambo wanayoyapenda.
Alisema ndiyo maana viongozi wa dini nao wamekuwa wakisisitiza uadilifu, jambo ambalo Rais Magufuli analifanya.
“Napongeza ukatili wa Rais kukemea maovu,” alisema Shibuda.
Alisema
Serikali ya Awamu ya Tano imekuja katika dunia ya mabadiliko ya mila,
jadi na utamaduni wa utendaji wa umma na kukomesha uzembe katika
uwajibikaji, ufisadi na kuleta msisimko unaoshangiliwa na jamii na
kuondoa zomeazomea dhidi ya Serikali.
Kiongozi huyo wa upinzani alisema ajenda ya vyama vya upinzani imenyauka na kuvitaka kuacha kutafuta mfereji wa kutorokea.
Badala yake, alivitaka vyama vya upinzani kujipanga upya ili viwe na mtazamo mpya wa utendaji wa shughuli za kisiasa.
Aliifananisha
Serikali ya Awamu ya Tano na mabadiliko ya tabianchi duniani, akisema
Taifa limepata Rais mwenye utumishi changamfu na kugusa hisia za jamii.
“Vyama
vya upinzani viache siasa za mipasho na vijembe. Siasa hizi hazitatui
kero za umaskini, ujinga, uchumi wa kaya na wananchi,” alisema Shibuda.
“Wanasayansi
walianza na dawa ya panado zakutuliza maumivu, lakini leo kuna dawa
tatu na mseto kwa kuwa walishindana kugundua dawa bora, basi na
wapinzani wawe na vikosi kazi vya kubuni tiba mbadala ya kutengua
utumishi wa Rais Magufuli,” alisema Shibuda.
Alisema
hakuna chama chochote cha kisiasa Tanzania ambacho kipo kwa masilahi ya
kukweza chama kingine, bali kila chama kipo kwa ajili ya kugombania
kushika hisia za jamii na kuwa na dola na wala chama hakilazimishwi
kufungamana na tafsiri ya chama kingine kwani kina sera zake zaidi ya
kufungamana siasa na itikadi ya chama chenyewe.
Alisema
vyama vinaweza kuwa na ushirikiano wenye dhamira sahihi ya kukuza
masilahi ya jamii, ndiyo maana chama chake cha Ada Tadea kinashirikiana
na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Shibuda aliwataka wanasiasa kuwa
na mawazo makini ya kunufaisha fikra za Watanzania.
Mmiliki wa kituo cha Foreplan
Clinic, Juma Mwaka, maarufu Dk Mwaka’ bado hajauepuka mkono wa Serikali
na sasa Jeshi la Polisi limesema linataka limtie mikononi mwake ndani ya
saa 24.
Tangu Baraza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Tano liapishwe
mapema mwaka huu, Dk Mwaka, ambaye ni tabibu wa tiba mbadala amekuwa
kwenye hali ngumu.
Sakata lake lilianza baada ya Naibu Waziri wa Afya,
Dk Hamisi Kigwangalla kufanya ziara ya kushtukiza kwenye kituo chake
kilichoko Buguruni, lakini hakumkuta na kuamua kuagiza awasilishe
nyaraka zake wizarani.
Siku chache baadaye kituo hicho kiliendelea na
shughuli zake za tiba, kikijitangaza kwenye vituo vya redio na
televisheni na kudhamini mashindano, lakini Serikali ilitangaza
kukifunga takriban wiki mbili zilizopita.
Juzi, Dk Kigwangalla alifanya
tena ziara ya kushtukiza na kukuta lundo la dawa za asili, kitu
kilichomfanya aamini kuwa kituo hicho kinaendelea na shughuli zake
kinyume na agizo la Serikali na hivyo kuagiza tabibu huyo akamatwe.
Jana, Kamanda wa Polisi wa Ilala, Salum Hamdan alisema jeshi lake
linaendelea kumsaka Dk Mwaka kama lilivyoagizwa na Waziri Kigwangalla.
“Vijana wangu wapo kazini kuhakikisha wanampata ndani ya saa 24,”
alisema Kamanda Hamdan.
“Nia ni kumfikisha mahakamani, lakini tutafanya
hivyo endapo tutakuwa na ushahidi wa kutosha kuhusu madai dhidi yake,
kama kudanganya umma kwa kujiita daktari, kuvaa mavazi na kutumia vifaa
vinavyopaswa kutumiwa na madaktari na si waganga wa tiba mbadala.
“Kosa
jingine kama yalivyoainishwa ni pamoja na kukiuka agizo la kufungiwa na
kuendelea kutoa tiba ndani ya jiji na nje kama vitabu vilivyokutwa
ofisini kwake.”
Baada ya kupata kibali
cha Jeshi la Polisi juzi, Dk Kigwangalla aliingia ndani ya jengo kukagua na
kukuta wateja wakiendelea kumiminika kufuata huduma, wengi wao wakiwa
kina mama.
Mara baada ya kufanya upekuzi na kukuta ndani ya jengo hilo
kuna dawa, Dk Kigwangalla alizungumza na wateja hao.
“Nimekuja kufuata
huduma na hata juzi nilikuwa hapa. Taarifa kuwa kituo hiki kimefungiwa
ninazo, lakini naona kila siku kwenye matangazo anayotoa kuwa bado
anatoa huduma na kweli nikija hapa napata,” alisema mwanamama
aliyejitambulisha kwa jina moja la Agnes na kukataa kutaja jina la pili.
Tume
ya Haki na Utawala Bora imeandaa kikao cha pamoja kati ya Chadema, CCM,
Jeshi la Polisi na taasisi nyingine tatu, wakati joto la Operesheni
Ukuta likizidi kupanda kwa viongozi wa Serikali na vyama vya siasa kutoa
kauli zinazotofautiana.
Chadema imetangaza kufanya mikutano nchi nzima kuanzia Septemba Mosi katika operesheni iliyobatizwa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), ikidai Serikali ya Awamu ya Tano inakandamiza haki na demokrasia nchini.
Kabla
ya kikao hicho, viongozi wa upinzani wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa
kuwapo maridhiano katika suala hilo pamoja na Ukawa kususia vikao vya
Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, lakini kumekuwa
hakuna harakati zozote zaidi ya majibizano.
Hali
hiyo ilizidi baada ya Chadema kutangaza operesheni hiyo ambayo
imesababisha viongozi wa Serikali, hasa wakuu wa mikoa kuanza kutoa
matamko ya kupiga marufuku mikutano yote ya Ukuta kwenye maeneo yao huku
chama hicho kikisisitiza kuwa kitaendesha operesheni yake bila ya
kujali amri ya kuizuia kwa kuwa kina haki kikatiba.
Katika
kile kinachoonekana ni jitihada za kutuliza hali hiyo, Tume ya Haki na
Utawala Bora imeandaa mkutano utakaohusisha taasisi sita, likiwamo
Jeshi la Polisi lililozuia mikutano, CCM inayoendesha Serikali na
Chadema inayopinga maamuzi ya Serikali kwa madai kuwa yanakandamiza
demokrasia na kukiuka misingi ya utawala bora.
Habari tulizozipata
zinaeleza kuwa wanaotakiwa kuhudhuria kikao hicho ni makatibu wakuu wa
vyama hivyo, Abdulrahman Kinana (CCM), Vincent Mashinji (Chadema) na
Ernest Mangu (Mkuu wa Jeshi la Polisi).
Wengine
ni Jaji Francis Mutungi (Msajili wa Vyama vya Siasa), George Masaju
(Mwanasheria Mkuu wa Serikali) na katibu mkuu wa Kituo cha Demokrasia
Tanzania (TCD).
Habari
hizo zinasema kuwa mwenyekiti wa Tume, Bahame Nyanduga, ndiye ambaye
amewaita viongozi hao Jumatano ijayo jijini Dar es Salaam.
Tume
ya Haki na Utawala Bora ina jukumu la kuhamasisha hifadhi ya haki za
binadamu, kuchunguza jambo lolote, kutoa ushauri kwa Serikali na vyombo
vingine vya umma na kuchukua hatua za kukuza, kuendeleza, usuluhishi na
suluhu miongoni mwa watu na taasisi.
Kutokana
na hali ya kisiasa ilivyo sasa, mkutano huo hautaweza kumalizika bila
ya kuzungumzia majibizano yanayoendelea kuhusu operesheni Ukuta na madai
ya ukandamizwaji demokrasia unaodaiwa kufanywa na Serikali.
Alipoulizwa
kuhusu mkutano huo, Nyanduga alimtaka mwandishi kuwahoji kwa kina watu
waliotoa habari hizo kwa sababu yeye hakutoa taarifa yoyote kwa vyombo
vya habari kuhusu ajenda za mkutano huo.
“Sikutoa mwaliko wala taarifa kwenu (wanahabari),” alisema Nyandyga alipoulizwa kuhusu ajenda za mkutano huo. “Aliyekwambia (suala hilo), akupe taarifa kamili. Nikisema tunajadili nini, haitakuwa na maana ya kuitisha mkutano.”
Mwezi
mmoja uliopita, Rais John Magufuli alitangaza kuzuia mikutano ya
kisiasa wakati akipokea ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliopita, akisema
wanasiasa watafanya siasa mwaka 2020 wakati wa uchaguzi mwingine,
akisema wakati huu ni wa kazi na asingependa kuona “mtu yeyote akinizuia
kutekeleza ahadi nilizozitoa kwa wananchi wakati wa uchaguzi”.
Ndani
ya kipindi hicho, Chadema imezuiwa kufanya mkutano wa hadhara Kahama
mkoani Shinyanga, imezuiwa kufanya hafla ya wahitimu wa vyuo vikuu vya
Dodoma na ACT Wazalendo imezuiwa kufanya mkutano wake wa ndani kujadili
bajeti ya 2016/17.
Hatua
hizo zilisababisha Chadema kufungua kesi Mahakama Kuu ikitaka itoe
tafsiri baada ya polisi kuzuia mkutano Kahama na baadaye kuzuia viongozi
wa chama hicho kuingia ofisi za Chadema za wilaya hiyo.
Wiki
iliyopita akiwa njiani kuelekea Kahama, Rais Magufuli alifafanua kauli
yake kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, akisema waliozuiwa ni wale
walioshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu na kwamba wale walioshinda wafanye
mikutano kwenye maeneo yao na wasialike mwanasiasa kutoka sehemu
nyingine.
Ufafanuzi
huo uliotolewa siku chache baada ya Chadema kutangaza operesheni hiyo
ya Ukuta, umeibuka mjadala mpya, huku Jeshi la Polisi na wakuu wa mikoa
wakitangaza kupiga marufuku mikutano ya Ukuta, huku wakizuia mwaliko wa
wanasiasa kwenye mikutano itakayopata kibali.
Chadema
inasema kuwa ina haki ya kufanya mikutano popote pale kwa kuwa hakuna
sehemu ambayo Sheria ya Vyama vya Siasa inakataza kufanya siasa baada ya
uchaguzi.
Takriban
wiki mbili zilizopita, Mbowe alitangaza mikakati mitatu iliyoazimiwa na
Kamati Kuu ya Chadema, ikilenga kupinga kile ambacho chama hicho
inakiita kuwa ni ukandamizaji wa haki na demokrasia unaofanywa na
Serikali.
Mbowe
alisema moja ya mikakati hiyo ni kufanya maandamano na mikutano nchi
nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu, kama ishara ya kupinga kauli ya
Rais na polisi kuhusu mikutano na maandamano.
Mbali
na mkakati huo, Chadema imeanzisha operesheni Ukuta, ikitaja matukio 11
inayodai kuwa ya ukandamizaji wa demokrasia nchini na mengine 24 kuwa
yamesababisha kuanzishwa kwa operesheni hiyo.
Mikakati hiyo ya Chadema ilipingwa na viongozi wa CCM na Jaji Mutungi kwa madai kuwa imejaa uchochezi.
Wakati
CCM ikiwataka Watanzania kutafakari kabla ya kuamua kuungana na
viongozi wa Chadema kudai demokrasia na kugeuka kafara kwa vyombo vya
ulinzi na usalama, Jaji Mutungi alisema kauli za chama hicho cha
upinzani ni kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa.
Wiki
moja iliyopita, Jeshi la Polisi lilitoa kibali kwa Mbunge wa Iringa
Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kufanya mkutano wa hadhara
jimboni kwake likizuia wanasiasa kutoka maeneo mengine na pia
kuzungumzia chama kingine na kuisema Serikali.
Mkutano
mwingine uliofanyika Ikungi na kuhutubiwa na Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu, uliisha salama lakini muda mfupi baadaye
mwanasheria huyo wa Chadema alimakatwa na Polisi na kusafirishwa hadi
Dar es Salaam ambako amefunguliwa kesi ya uchochezi.
NAIBU
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni amesema askari
wa usalama barabarani watakaobainika kupokea rushwa watashughulikiwa kwa
kuwa wataweka mitego kwa ajili ya kuwakamata.
Alisema
wananchi wamekuwa wakilalamikia askari hao kuwa wanapenda rushwa na
ndio chanzo cha ajali barabarani na kwamba wanachafua taswira ya jeshi
hilo.
Akizungumza
na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam jana jijini humo, Masauni alisema mtego watakaouweka ndilo kaburi
lao na kwamba watafungwa kwa sababu ya tamaa ya Sh 10,000, hivyo
wajihadhari.
Alisema
Taifa linakabiliwa na changamoto ya ajali za barabarani na kwamba wana
wajibu wa kuwalinda raia wa nchi hii, badala ya kushiriki kuwaangamiza
kwa tamaa ya fedha. Alisisitiza kuwa hawataweza kufikia uchumi wa kati
endapo nguvu kazi zitaendelea kupotea kutokana na ajali za barabarani.
“Kuondoa
ajali inawezekana na watu watakaoleta sababu za ajabu ajabu hiki sio
kipindi chake ni lazima tuzitekeleze kama tulivyopanga kwenye mkakati
wetu kwamba ndani ya miezi sita tuwe tumepunguza ajali kwa asilimia 10,” alisema akisisitiza askari kubadilika, kwani ndio wasimamizi wakubwa wa usalama barabarani.
Akizungumzia
changamoto zinazowakabili askari hao, alisema kuwa wapo baadhi ya
askari ambao wanafanya kazi katika mazingira hatarishi na magumu kama
vile kupigwa risasi, kugongwa na magari na kwamba jitihada zao
zinatakiwa zitambulike kwa kupandishwa vyeo na mishahara kwa kazi nzuri
wanazofanya.
Kamanda
wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga alisema
mkutano huo ni sehemu ya kutoa elimu kwa askari watakaosimamia mkakati
huo kuhakikisha ajali zinapungua.
Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Abdulrahman Kaniki alisema ajali za
barabarani ni miongoni mwa changamoto zinazolikabili Taifa.
Alisema
ni wakati wa askari kuongeza chachu, ari na mbinu katika kutekeleza
majukumu yao kwa wananchi na kwamba wapo imara kutekeleza maagizo halali
kutoka kwa viongozi wao.
SERIKALI
imetangaza mwongozo mpya kuwa kuanzia sasa masomo ya sayansi ni lazima
kusomwa na wanafunzi wote wanaosoma elimu ya sekondari kuanzia kidato
cha kwanza hadi cha nne.
Kwa
mujibu wa Sera ya Elimu iliyopo, wanafunzi wanaosoma elimu ya sekondari
wanaweza kuchagua aina ya masomo watakayo wafikapo kidato cha tatu na
kuacha mengine.
Uamuzi
huo ulitangazwa jana mjini Tanga na Waziri wa Elimu, Teknolojia,
Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wakati
akizungumza na mamia ya walimu wa elimu ya msingi kwenye mafunzo ya muda
mfupi kuhusu mtaala mpya wa kufundishia wanafunzi wa darasa la tatu na
nne.
Alisema
hivi sasa nchi imedhamiria kuingia kwenye uchumi wa kati ambao ni wa
viwanda, hivyo suala la sayansi haliwezi kuepukwa kwa sababu ni wakati
sasa wa kuwa na wataalamu wengi wa fani za sayansi watakaoweza
kutosheleza mahitaji ya sekta ya viwanda nchini.
Alisema
kutokana na uhaba wa wataalamu wa sayansi nchini kwenye maeneo mengi,
wizara imeamua kuanzia sasa wanafunzi wote wa elimu ya sekondari kuanzia
kidato cha kwanza hadi cha nne, watalazimika kusoma masomo ya sayansi
na kufanya mtihani wa masomo hayo, na kwamba baada ya matokeo kutoka
ndipo watafanya uamuzi ama wa kuendelea nayo au la.
Hatua
hii kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, itamlazimisha mwanafunzi kusoma
kwa bidii ili kuhakikisha anafaulu masomo hayo ingawa hivi sasa
wanafunzi walio wengi wanadai masomo hayo ni magumu, ndiyo maana
wanachagua kusoma masomo ya sanaa.
Alisema
ili kuhakikisha azma ya serikali ya wanafunzi wanapata vitendea kazi
vya masomo hayo, Sh bilioni 12 zimetengwa kwenye bajeti ya fedha ya
mwaka huu kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabara kwenye shule zote za
sekondari nchini ili kuwepo na zana za kufundishia kwa ajili ya masomo
ya sayansi.
"Mafunzo
ya vitendo sasa sio mbadala ni lazima, na yatafanywa kama sehemu ya
masomo na wanafunzi wote watalazimika kuyafanya kwa vitendo ili wawe na
uelewa wa walichosoma kwa manufaa ya taifa,” alisema Profesa Ndalichako.
Alisema
Serikali ya Awamu ya tano imedhamiria kuona kiwango cha elimu
kinachotolewa nchini kina hadhi sawa na elimu itolewayo na mataifa
mengine ili kupata wataalamu wenye sifa zinazokidhi mahitaji ya soko
hata kama sio wote wataajiriwa ila hata wale wasiopata ajira wajiajiri
kupitia elimu waliyopata.
Aliwataka
walimu waliohudhuria mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia uwezo wao na
elimu waliyopata kufanya kazi kwa mujibu wa maadili ya taaluma ya ualimu
ili kuwajengea msingi mzuri wa elimu wanafunzi wa shule za msingi.
Akizungumzia
kauli ya Profesa Ndalichako, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Shule Binafsi
Tanzania (TAMANGOSCO), Mahmoud Mringo alisema ni uamuzi mzuri ila
umekuja kwa kuchelewa kwa sababu mahitaji ya wataalamu wa sayansi nchini
ni makubwa kuliko idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo.
Alisema
pamoja na uamuzi huo mzuri uliochukuliwa na serikali, lakini bado
kutakuwa na changamoto ya uhaba wa walimu wa masomo hayo, maabara na
maktaba na kwamba hali hiyo inaweza kusababisha mahitaji ya walimu hao
kutoka nje yakaongezeka.
Katibu
wa Tamangosco, Benjamin Mkonya alisema ni hatua nzuri ingawa
utekelezaji wake utakuwa na changamoto nyingi kwa sababu hali halisi ya
mazingira ilivyo nchini.
Alisema
ikiwa serikali inadhamiria kutekeleza azma hiyo ni vyema kipengele cha
vigezo vya shule kuwepo ambavyo vimeainishwa ndani ya sheria ya elimu
nchini, vikaangaliwa ambavyo ni uwepo wa maabara ya kutosha, maktaba
yenye vifaa na walimu wa kutosha.
Alisema
iwapo vigezo hivyo vikiangaliwa shule ambazo hazijakidhi vigezo hivyo
zikafutwa na vifaa vilivyopo kwenye maabara na maktaba hizo zikaongezwa
kwenye shule zenye vifaa hivyo ili kusaidia utekelezaji wa azma hiyo ya
kufundisha masomo ya sayansi kwa wanafunzi wote kuanzia kidato cha
kwanza hadi cha nne.
Walimu
washiriki wameishukuru serikali kwa mafunzo hayo ambayo walisema ni
mazuri na yameongeza kiwango chao cha uelewa na kuwaongezea mbinu za
ufundishaji sambamba na kukuza morali ya kazi zao.
Pamoja
na kushukuru, wameomba wizara hiyo iangalie jinsi ya kuweka posho kwa
baadhi ya maeneo ya kazi, hususan kwenye vituo vya kazi vilivyopo
pembezoni na kwenye mazingira magumu ili kuwajengea walimu motisha wa
kufundisha maeneo hayo.
Walimu waliohudhuria mafunzo hayo ni 480 wanaotoka halmashauri za Bumbuli, Mji wa Handeni na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Mkuu
wa Idara ya Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule akisisitiza
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa
taarifa ya kukamatwa kwa watumishi wawili wa Serikali ambao sio raia wa
Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa
ambao sio raia wa Tanzania waliokuwa wakifanya kazi serikalini wakiwa
chini ya ulinzi wa askari wa Uhamiaji, kushoto ni Bw. Bahilanya
Milingita aliyekuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)na kulia ni Dkt.
Esther Green Simon Mwenitumba ambaye alikuwa Mganga Mkuu Kituo cha Afya
Mburahati.
Bw.Bahilanya
Milingita maarufu kwa jina la Roy Bilingita raia wa Congo ambaye
anatuhumiwa kuingia nchini mwaka 1986 na kufanya kazi katika Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) kinyume na sheria za nchi.
Dkt.
Esther Green Simon Mwenitumba raia wa Malawi ambaye alikuwa Mganga Mkuu
katika kituo cha Afya Mburahati anatuhumiwa kufanya kazi Serikalini
wakati si raia wa Tanzania.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Idara ya
Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule wakati alipokuwa akitoa
taarifa ya kukamatwa kwa watumishi wawili wa Serikali ambao sio raia wa
Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imevuka lengo la ukusanyaji wa kodi wa jumla
ya kiasi cha shilingi trilioni 1 sawa na asilimia 95.6 tofauti na lengo
lililokuwa limekusudiwa la kukusanya trilioni 1.1 kwa mwezi Julai 2016.
Kiasi
hicho ni sawa na ongezeko la asilimia 15.43 ukilinganisha na makusanyo
ya awali ya mwaka 2015 ambapo mamlaka hiyo ilikusanya jumla ya kiasi cha
shilingi Bilioni 914.
Takwimu
hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA,
Richard Kayombo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jjijini
Dar es Salaam.
“Kwa
mwezi Julai mwaka huu makusanyo yameongezeka kwa asilimia 15.43
ukilinganisha na kipindi cha mwezi Julai 2015 ambapo tulikusanya
shilingi Bilioni 914” alisema Kayombo.
Aidha
aliongeza kuwa mamlaka imeweka mikakati thabiti ya kuhakikisha kuwa
inafikia au inavuka lengo la Serikali la kukusanya shilingi trilioni
15.1 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 huku mkakati mmoja wapo ukiwa ni
kuhakikisha kuwa walipa kodi wapya wanasajiliwa zaidi.
Bw.
Kayombo aliongeza kuwa mkakati mwingine ni kuhuisha taarifa za walipa
kodi kwa kuhakikisha kwamba namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN)
zisizotumika zinafutwa katika mfumo wa TRA.
Pia
amefafanua kuwa maandalizi ya kuhuisha taarifa za walipa kodi yapo
katika hatua za mwisho ikiwemo upigaji picha,uchukuaji wa alama za
vidole pamoja na vielelezo muhimu.
TRA
inawakumbusha wananchi kuhakikisha wanakagua tiketi/risiti zao za
manunuzi na kuangalia usahihi wa pesa walizolipa na uhalali wa risiti
yenyewe.
HATIMAYE
Jeshi la Polisi Jijini Dar es salaam limemfikisha rasmi kizimbani
Mwanasheria Mkuu wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo Singida
Mashariki wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Tundu
Lissu ambaye alikamatwa Juzi mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano
wa hadhara Ikungi, Singida na kusafirishwa usiku, kulazwa Chamwino
Dodoma na kufikishwa Dar jana saa saba mchana alilazwa rumande kabla ya
kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mchana wa leo.
Akionekana
mwenye kujiamini, Lissu amewasili Mahakamani Kisutu akitokea mahabusu
ya Kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam saa nane na
dakika arobaini na nane (14:48) akiwa kwenye gari yenye namba za
usajili T 517 BET Corolla na akisindikizwa na ulinzi mkali wa jeshi la
polisi.
ALL STUDENTS COLLEGE OF INFORMATICS AND VIRTUAL EDUCATION THIS IS TO INFORM ALL STUDENTS
REQUIRED TO ATTEND INDUSTRIAL PRACTICAL TRAINING WITHIN AND OUTSIDE THE
UNIVERSITY THAT, THE TRAINING WILL START EFFECTIVELY ON MONDAY 15TH
AUGUST, 2016.
Vyama
tisa vya siasa kati ya 22 vyenye usajili wa kudumu vipo hatarini
kufutwa kutokana na kushindwa kukidhi vigezo na matakwa ya kisheria
yaliyoviwezesha kupata usajili wa kudumu.
Hatua
ya kufutwa vyama hivyo, vikiwamo baadhi visivyo na ofisi za kudumu
(vyama vya mfukoni) itafikiwa ikiwa vitashindwa kujieleza kutokana na
makosa ambayo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imebaini katika
ukaguzi uliofanyika hivi karibuni Bara na Visiwani.
Jukumu
kubwa la Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni kusimamia, kuboresha,
kuendeleza na kudumisha demokrasia ya vyama vingi hapa nchini majukumu
ambayo yanatokana na Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 5 ya mwaka 1992 na
Sheria ya Gharama za Uchaguzi Na. 7 ya mwaka 2010.
Majukumu
mengine ya ofisi ya msajili ni kusajili vyama vya siasa na kuvifuta
vyama ambavyo havikidhi matakwa ya sheria hiyo na kusimamia ugawaji wa
ruzuku ya Serikali kwa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza
ofisini kwake jana, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis
Mutungi alisema uhakiki uliofanywa na ofisi yake katika vyama hivyo
upande wa Bara na Visiwani umebaini kasoro nyingi zikiwamo za ukiukaji
wa masharti ya usajili.
“Katika uhakiki uliofanywa na ofisi yangu tumebaini kasoro mbalimbali
ambazo kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ni miongoni mwa vigezo
muhimu vinavyoangaliwa ili chama kiwe na sifa ya kusajiliwa,” alisema.
“Kasoro
tulizozibaini ni nyingi na baadhi ya vyama kutokana na mapungufu waliyo
nayo huhitaji kutoa nafasi tena….unaweza kuvifuta hapohapo.”
Msajili
hakutaka kutaja majina ya vyama hivyo ambavyo tayari vimeandikiwa barua
lakini alitaja makosa kuwa baadhi havina ofisi za kudumu Tanzania Bara
na Visiwani au upande mmoja na vingine havina anuani ya posta.
“Unakuta chama fulani kina ofisi labda Zanzibar lakini hakina ofisi Bara,”
alisema Jaji Mutungi. Alisema vyama vingine havina viongozi wa kitafa
kutoka pande mbili za Muungano na pia havina bodi ya wadhamini
iliyosajiliwa kwa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (Rita) kama
sheria inavyohitaji.
Katika
ukaguzi huo, Msajili alibaini pia kasoro nyingine kuwa ni kukosekana
kwa orodha ya wanachama wa chama husika jambo alilosema nalo ni muhimu
kila chama kuwa na orodha ya idadi ya wanachama wake.
Vilevile, baadhi ya vyama hivyo vimeshindwa kuonyesha akaunti ya fedha ya chama hali inayotia shaka namna vinavyojiendesha.