MASTAA MATAJIRI WACHUNGUZWA
KIMENUKA! Jeshi la Polisi Tanzania kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali zimeanza kuwachunguza watu wenye majina makubwa ‘mastaa’ Bongo ambao wameibuka na utajiri wa ghafla, Uwazi limeambiwa.
Kwa mujibu wa chanzo nyeti ambacho kiko ‘jikoni’ kwenye jeshi hilo, mbali na mastaa, wengine ambao tayari orodha yao ipo ni wafanyabiashara, wafanyakazi wa serikali na viongozi wa dini ambao wameibuka kuwa mamilionea kwa muda mfupi huku shughuli zao za…
ANAYEISHI KWENYE HANDAKI BALAA JIPYA!
CHACHA Makenge (38) aliyeripotiwa awali kuishi ndani ya handaki katika eneo la pori la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani, amepatwa na balaa jipya baada ya makazi yake kuvamiwa na askari, kukamatwa na mwishowe kupelekwa Muhimbili kitengo cha wagonjwa wa akili kwa ajili ya matibabu.
Chacha Makenge (38) akiota moto nje ya handaki lake katika eneo la pori la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.
Kana kwamba haitoshi, Makenge ambaye aliwahi kuishi…MAAJABU YA MUNGU!
KATIKA hali ya kushangaza, wagonjwa wa mtindio wa ubongo, Paul Ngido na Asha Yahya wanaolelewa kwenye kituo cha watoto wenye matatizo mbalimbali wakiwemo yatima cha Ngido kilichopo Mazimbu FK mkoani hapa wamejikuta wakizaa watoto wawili, Keisha na Glory ndani ya kituo hicho.
Paul Ngido na Asha Yahya wanaolelewa kwenye kituo cha watoto wenye matatizo mbalimbali waliowazaa watoto Keisha na Glory.
Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho, Linda Cyprian Ngido amethibitisha kutokea…NJEMBA YAMBAKA MTOTO WA MIAKA MINNE
NI AIBU!Jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Iddi Mgosi anashikiliwa na Polisi wa Kituo cha Wazo jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka minne (jina linahifadhiwa) huko Mivumoni, Madale Machi 18, mwaka huu.
Mgosi, ambaye umri wake haukuweza kupatikana mara moja, anadaiwa kumrubuni mtoto huyo kutoka nyumbani kwao na kumpeleka kwake, ambako alimuingilia kwa nguvu na baadaye kumtisha…
TATIZO LA MACHINGA LINATAKA BUSARA
NINAWASALIMU kwa jina la Bwana Mungu, mwingi wa rehema na muweza wa
kila jambo. Siku zote nimekuwa nikiwasihi kumuweka mbele muumba wa nchi
na mbingu, kwani kwake hakuna lisilowezekana.
Hivi sasa kuna kampeni kubwa ya kusafisha jiji kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni kubomoa vibanda vya biashara vilivyojengwa kinyume na taratibu katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Jambo hilo limesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa jiji…

UNAKUBALIKA KWENYE JAMII-2
BADO tunaendelea na somo letu ambalo safari hii nagusia upande wa
maisha. Ndugu zangu, kukubalika kwenye jamii kuna manufaa makubwa kama
nilivyosema wiki iliyopita.
Niliishia pale nilipofafanua hasara za kutokubalika kwenye jamii. Sasa leo tuendelee.
KWA NINI HUKUBALIKI?
Wakati naanza kabisa kuandika mada hii, nimeeleza kwamba kila kinachotokea duniani huwa na sababu zake. Haiwezekani ukawa hukubaliki kwa chuki za watu au watu kukuonea wivu.
Lazima kuna sababu zinazosababisha usikubalike. Najua kila mmoja anaujua ukweli wa maisha yake ndani ya moyo wake.
Hapa nitakuandikia sababu muhimu…

MBWA WALIOMLA MTOTO NUSURA WAMLE BABA MTU
ZIMEKATIKA wiki mbili tangu kuzikwa kwa mtoto Christian Alex (6) aliyeuawa kwa kushambuliwa na mbwa watatu waliodaiwa ni wa Ubalozi wa Qatar nchini, mbwa hao wamemkosakosa baba mtu.
Tukio la kuuawa kwa mtoto huyo lilijiri Kunduchi Jangwani Beach jijini Dar Machi 26, mwaka huu.
Kwa mujibu wa chanzo, mara baada ya kumaliza shughuli ya kumzika marehemu katika Makaburi ya Mburahati jijini Dar, baba mzazi Alex Augustino alikaa kikao na ndugu ili kuangalia uwezekano wa kufika kwenye makazi hayo ya ubalozi na kuzungumza nao kujua hatima ya sakata hilo.
Baada ya makubaliano,…
TUUCHOKONOE, TUUPINDUE ILI TUUBORESHE
WAJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba wanaendelea na mchakato wa kupitia
vifungu vya Rasimu katika ngazi ya kamati, kabla ya keshokutwa kuanza
rasmi mjadala wa namna gani Tanzania inaweza kupata katiba mpya, miaka
50 baada ya kuungana kwa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar.
Katika hatua za awali ngazi ya kamati, tumeshuhudia mambo mengi hasa yanayohusu hatima ya Muungano, ambao umekuwa ndiyo simulizi kuu katika mchakato mzima.
Kwa miaka mingi Watanzania tumeishi tukiaminishwa kuwa Muungano huu uko safi na yeyote aliyeonekana kuuzungumzia kwa namna ya kuukosoa, alichukuliwa kama msaliti, mhaini na mtu asiye na nia njema na nchi yetu.
Mambo mengi yanayohusu uhusiano wa nchi hizi mbili umekuwa siri kubwa, baadhi ya mambo yameharibika au kwenda mrama kwa kuwa kila mmoja alikuwa hataki kuonekana…