Thursday, 3 April 2014

Tangazo la kazi:JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/G/09
01 Aprili, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki,
pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea
katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 482 za kazi kwa waajiri mbalimbali
kama ifuatavyo:
MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu
ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
1
vi.
Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne
na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo
mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa
sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Cheti cha Kompyuta
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
-
vii.
Shahada ya juu/Shahada/Stashahada ya juu/Stashahada/Astashahada.
Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
“Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati
matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
viii.
ix.
Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
xi.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 15 Aprili, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira
HAURUHUSIWI.
xiv.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
xv.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo;-
Katibu,
Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma,
SLP.63100,
Dar es Salaam.
AU
2
Secretary,
Public Service Recruitment
Secretariat,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.
1.0 AFISA TAWALA DARAJA LA II (ADMINISTRATIVE OFFICER GRADE II) –
(NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki.
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kusajili vizazi, vifo na ndoa na kutoa hati za viapo.
 Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu,
 Kuwapokea na kuwahoji wakimbizi wanaowasili,
 Kuweka kumbukumbu za Wakimbizi
 Kutunza na kugawa vifaa vya wakimbizi katika makazi.
 Kuainisha, kuchambua na kushauri kuhusu matatizo ya wakimbizi.
 Kusimamia nidhamu ya wakimbizi.
 Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu mbalimbali Serikalini
kutegemeana mahali alipo.
 Kusimamia kazi za utawala na uendeshaji katika ofisi za Serikali.
 Kutoa vitambulisho kwa wakimbizi.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na
Serikali katika fani zifuatazo:- Utawala, Sheria (baada ya internship), na
Menejimenti ya Umma
 Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
2.0 MCHUMI DARAJA LA II (ECONOMIST GRADE II) – (NAFASI 23)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki, Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya
Mipango na Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia .
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuhudumia kamati mbalimbali za Bunge (Kamati za mahesabu ya Serikali, Kamati
ya mahesabu ya mashirika ya Umma)
 Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya uchambuzi na
uandaaji wa sera na mipango ya kiuchumi na kijamii
 Kufanya utafiti na uchambuzi wa sera na vigezo vya kiuchumi jumla
 Kufanya utafiti na kubainisha fursa zilizopo katika sekta husika
3


Kukusanya taarifa na takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya
ustawi namaendeleo ya jamii.
Kutayarisha na kusambaza takwimu na taarifa za kiuchumi kwa wadau
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ambao wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya
fani zifuatazo;
 Uchumi (Economics)
 Takwimu (Statistics )
 Sayansi ya Uchumi Kilimo (BSc Agriculture Economics & Agribusness) kutoka
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Sokoine au Chuo kingine
chochote kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta
2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
3.0 MCHUMI DARAJA LA II (ECONOMIST GRADE II) – (NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuhudumia kamati mbalimbali za Bunge (Kamati za mahesabu ya Serikali, Kamati
ya mahesabu ya mashirika ya Umma)
 Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya uchambuzi na
uandaaji wa sera na mipango ya kiuchumi na kijamii
 Kufanya utafiti na uchambuzi wa sera na vigezo vya kiuchumi jumla
 Kufanya utafiti na kubainisha fursa zilizopo katika sekta husika
 Kukusanya taarifa na takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya
ustawi namaendeleo ya jamii.
 Kutayarisha na kusambaza takwimu na taarifa za kiuchumi kwa wadau
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya Uzamili ambao wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya
fani ya Uchumi (Economics) au Fedha (Finance) kutoka Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta
4
3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
4.0 AFISA MAENDELEO YA JAMII DARAJA II (COMMUNITY DEVELOPMENT
OFFICER GRADE II) – (NAFASI 2)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki na Katibu Mtendaji Ofisi
ya Rais Tume ya Mipango.
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandaa na kupendekeza mipango na mikakakati ya kubadili fikra za watu ili
waweze kuwa na mawazo ya maendeleo sawia na Sera za Serikali na wakati
uliopo
 Kupitia mbinu shirikishi kuwezesha jamii kuanzisha miradi ya kijamii kama vile:-
- Usafi wa mazingira
- Ujenzi wa nyumba bora
- Ujenzi wa shule
- Ujenzi wa zahanati
- Kuchimba au kuzifanyia matengenezo barabara hasa za vijijini
- Ujenzi wa majosho
- Uchimbaji wa visima vifupi
- Utengenezaji wa malambo
 Kuhamasisha matumizi endelevu ya mazingira
 Kusambaza na kuhamasisha matumizi ya teknolojia sahihi kama vile uvunaji wa
maji ya mvua, majiko sanifu, matumizi ya mikokoteni
 Kuhamasisha watu kutumia huduma za mafunzo ya Vyuo vya Maendeleo ya
Wananchi
 Kuwasadia wanachi vijijini kuandaa maandiko (Project Write ups) ya kuombea
fedha za kuendesha miradi yao
 Kuhamasisha, kuandaa na kutoa elimu kwa umma kuhusu uraia na Utawala bora
 Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kusambaza takwimu na kumbukumbu muhimu
kwa ajili ya matumizi ya jamii
 Kuwezesha wananchi kupambana na mila zenye madhara kwa afya za wanchi
hasa wanawake na watoto wa kike, kuenea kwa virusi vya UKIMWI na magonjwa
ya mlipuko.
 Kuelimisha viongozi wa Serikali za Vijiji, Dini na Mashirika yasiyo ya Kiserikali
kuhusu Sera mbalimbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na
kutumia Sera hizo
 Kutoa taarifa za hali ya jamii kwa ngazi mbalimbali
5
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa Shahada au Stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii
kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:-
 Maendeleo ya Jamii (Community Development)
 Elimu ya Jamii (Sociology)
 Masomo ya Maendeleo (Development Studies)
 Mipango na Usimamizi wa Miradi (Project Planning and Management)
 Maendeleo na Jinsia (Gender and Development)
4.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
5.0 AFISA HABARI II – (NAFASI 3)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki na Katibu Mtendaji Ofisi
ya Rais Tume ya Mipango.
5.1







MAJUKUMU YA KAZI
Kukusanya na kuandika habari.
Kupiga picha.
Kuandaa picha za maonyesho.
Kuandaa majarida na mabango (Posters).
Kukusanya takwimu mbalimbali.
Kuandaa majarida na vipeperushi.
Kuhifadhi picha na kuhudumia maktaba na marejeo.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Awe na Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu ya Uandishi wa Habari au sifa
inayolingana nayo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
6.0 MKAGUZI HESABU WA NDANI II (INTERNAL AUDITOR II) – (NAFASI 3)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki na Katibu Mtendaji Ofisi
ya Rais Tume ya Mipango.
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
6




Kufanya Ukaguzi wa hesabu katika Idara
Kusahihisha na kuidhinisha ripoti za ukaguzi
Kusahihisha na kuidhinisha hoja za Ukaguzi wa ndani
Kufanya kazi zingine atakazopangiwa.
6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiri wahitimu wa kidato cha sita (VI) wenye cheti cha kati cha uhasibu
(intermediate stage) kinachotolewa na NBAA au sifa zinazolingana na hizo.
 AU
 Wenye shahada/Stashahada ya juu ya uhasibu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na
serikali.
6.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
7.0 MHASIBU DARAJA LA II (ACCOUNTANT GRADE II) – (NAFASI 2)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki na Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuidhinisha hati za malipo.
 Kuandika taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi.
 Kusimamia Wahasibu Wasaidizi katika kazi zao za kila siku.
 Kusimamia shughuli za uhasibu kwenye Kitengo cha Idara.
 Kuandika taarifa ya maduhuli.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiri wahitimu wa kidato cha sita (VI) wenye cheti cha kati cha uhasibu
(intermediate stage) kinachotolewa na NBAA au sifa zinazolingana na hizo.
AU
 Wenye shahada/Stashahada ya juu ya uhasibu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na
serikali.
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
8.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III – (NAFASI 100)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
7
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
 Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
 Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
 Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
 Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
 Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
 Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
 Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
 Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na
kukusanya takwimu zao
 Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya Nchi
 Kudhibiti wanyamapori waharibifu
 Kudhibiti moto kwenye hifadhi
 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya
Uhifadhi Wanyamapori (Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka
Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa
na Serikali.
8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B2 kwa mwezi.
9.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III – (NAFASI 327)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
 Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
 Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
 Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
 Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
 Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
 Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
 Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
 Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na
kukusanya takwimu zao
8




Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya Nchi
Kudhibiti wanyamapori waharibifu
Kudhibiti moto kwenye hifadhi
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya Awali
ya Uhifadhi wa Wanyamapori (Basic Technician Certificate in Wildlife
Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.
9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B1 kwa mwezi.
10.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II – (NAFASI 10)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
10.1












MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
kusimamia uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
kulinda Nyara za Serikali
Kusimamia usafirishaji wa wanyamapori na nyara nje na ndani ya Nchi
Kusimamia matumizi ya magari ya doria
Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kutunza
takwimu zao
Kuratibu uingiaji wa wageni katika Mapori ya Akiba
Kudhibiti moto katika hifadhi
Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
Kukusanya takwimu za wanyama na mimea kwenye hifadhi
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Stashahada ya
Uhifadhi Wanyamapori (Diploma in Wildlife Management) kutoka Chuo cha
Usimamizi Wanyamapori Mweka au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
10.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
9
11.0 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – (NAFASI 2)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango.
11.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuendesha magari ya abiria, magari madogo na malori
 Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya
uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji
matengenezo,
 Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
 Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.
11.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C”
ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua
miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti cha Majaribio ya ufundi Daraja
la II (Trade test II).
11.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGOS.A kwa mwezi.
12.0 AFISA USAFIRISHAJI DARAJA LA II (TRANSPORT OFFICER GRADE II ) –
(NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango.
12.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kutayarisha gharama za uendeshaji wa usafiri kwa ajili ya kusaidia kutoa
maamuzi.
 Kuhakikisha kuwa takwimu na kumbukumbu zinazohusu vyombo vya usafiri
pamoja na mitandao yake zinatunzwa vyema na kwa usahihi. Kuandaa takwimu
zinazohusu maendeleo ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji, na kuwasilisha kwa
watumiaji ndani na nje ya nchi.
 Kukusanya takwimu za usafirishaji nchini.
 Kukadiria na kushauri juu ya utendaji wa miradi mbalimnbali ya sekta ya
usafirishaji.
 Kutekeleza majukumu mengine yanayohusu sekta ya usafirishaji
12.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Stashahada ya kawaida ya Usafirishaji kutoka Vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
10
12.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
13.0 AFISA MAZINGIRA DARAJA LA II – (NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango.
13.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kukusanya Takwimu na Taarifa mbalimbali zinazohusu Usimamizi na Hifadhi ya
Mazingira.
 Kutoa (disseminate) elimu ya Hifadhi ya Mazingira kwa Wadau mbalimbali.
 Kushiriki katika kuandaa Mpango wa kazi na bajeti.
 Kushiriki katika tafiti zinazohusu Usimamizi na Hifadhi ya Mazingira.
 Kufuatilia utekelezaji wa Sera na Sheria zinazohusiana na Usimamizi wa
Mazingira.
 Kufuatilia na Kuainisha Maeneo yanayopaswa kuhifadhiwa.
 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa kulingana na uwezo na taaluma yake.
13.2 SIFA ZA MWOMBAJI.
 Kuajiriwa wahitimu wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi/Sanaa yenye
mwelekeo wa Usimamizi na Hifadhi ya Mazingira katika moja ya fani zifuatazo,
‘Geography and Environmental Studies, Aquatic Environmental Science and
Conservation, Environmental Science and Management, Environmental
Laboratory Science Technology, Environmental Planning and Management’ au
sifa zinazolingana na hizo kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali.
13.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
14.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU (REGISTRY ASSISTANT) – (NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Mkurugenzi Mtendaji Mfuko wa Pembejeo za Kilimo na Mifugo.
14.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kusimamia usahihi (accuracy) wa kumbukumbu.
 Kugawa kazi na kusimamia kazi zote za masjala.
 Kuangalia barua zote zinazoingia, kutoka na kuweka kwenye majalada husika.
 Kutunza diary za (Bring up) na kuhakikisha zinafanyiwa kazi kwa wakati muafaka.
 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa kulingana na uwezo na taaluma yake.
11
14.2 SIFA ZA MWOMBAJI.
 Kuajiriwa wahitimu wenye Stashahada ya Kumbukumbu (Diploma in Records
Management) kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali.
 Awe na uzoefu wa miaka Sita (6) katika fani hii.
14.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Taasisi yaani GSS 5 kwa mwezi.
15.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II (WARD EXECUTIVE OFFICER
GRADE II) – (NAFASI 5)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri.
MAJUKUMU YA KAZI
 Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika
kata na atashughulikia masuala yote ya kata
 Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbal.i ya uzalishaji,
mali, kuondoa njaa na Umasikini.
 Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
 Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na Mtaa.
 Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata
yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika
Kata.
 Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo
lake.
 Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katikangazi ya Kata.
 Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na
nakala kwa Katibu Tarafa.
 Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa
vjiji, na NGO’S katika kata yake.
 Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji,
vitongoji, na kata yake.
15.1 SIFA ZA MWOMBAJI.
 Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social
Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Sheria au Sifa
nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali.
12
15.2 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D. kwa mwezi.
X.M. DAUDI
Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
13
Share:

Video:VURUGU BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


Share:

SIMULIZI TAMU YA WEMA SEPETU


Wema Sepetu.
WIKI iliyopita, Wema aliendelea kuelezea simulizi yake tamu ambayo imetokea kupendwa na wasomaji wengi wa Gazeti la Amani. Aliishia pale alipoweka wazi kisa cha kuachana na Chalz Baba, akaeda Marekani, aliporudi akawa na Diamond: Tujikumbushe kidogo kisha tuendelee…
Mwandishi: Nakumbuka ulipoondoka nchini kwenda Marekani ulikuwa na mapenzi na Chaz Baba, lakini uliporejea ikasikika kwamba upo na Diamond, nini kilitokea Wema?
Wema: (kicheko) yeah! Ni kweli kabisa, baada ya kuachana na Jumbe mwaka 2010 kama nilivyosema ndiyo nilianzana na Chaz Baba, nilimpenda, alinipenda. Na yeye ilikuwa tuoane, lakini nimeshasema nikiwa Marekani nilikuwa nasikia leo Chaz alikuwa na huyu, kesho alikuwa na yule, nikamwambia mimi na wewe basi.
Mwandishi: Kwa Chaz Baba mama yako alimkubali awe mumeo?
Wema: Kusema ukweli hakuwa muwazi kwa Chalz Baba, kwamba anamkubali au hamkubali. Lakini ikawa hivyo, tukaachana.
Mwandishi: Baada ya kuachana na Chalz ukajikuta upo kwa Diamond, nini kilikuvutia kwake?
Wema: Nasibu (Diamond) ilitokea kama nilivyokwishasema. Kwa hiyo mtu unajikuta umezama kwake. Wakati mwingine ni vigumu kusema mtu uliyenaye alikuvutia kitu gani!
KUHUSU KIINGEREZA CHA DIAMOND
Mwandishi: Wema, ni kweli Diamond amejua Kiingereza kwa ajili yako?
Wema: Kwanza niweke sawa hapo. Nasibu si kwamba amejua Kiingereza kwa ajili yangu, bali amejua kuzungumza Kiingereza vizuri. Ina maana tangu awali alikuwa anakijua lakini si kivile.
“Mimi na Nasibu tumekaa pamoja mwaka mzima kama mke na mume baada ya mimi kutoka Marekani mwaka ule 2011. Sasa si unajua mimi kidogo nakijua vizuri. Kwa hiyo kwa miezi kadhaa ya nyuma katika kuishi kwetu alikuwa akipata tabu kidogo.
“Ila nataka kukwambia kwamba, Nasibu ni makini sana. Hakuna mtu makini kama yeye. Akiwa hajui kitu lazima akuulize, hakai kimya.”
Mwandishi: Pamoja na sifa zote hizo, lakini mwisho wa siku wewe na Diamond mlimwagana kwa awamu ya kwanza, ilikuwaje?
ALIVYOMFUMANIA JOKATE
Wema: Tuliachana baada ya yeye kunisaliti na Jokate (Mwegelo). Unajua nilimwamini sana na sikuwahi kuwa na shaka naye hata siku moja, nilimwamini kupitiliza nikijua ni wangu na mimi ni wake.
“Lakini nadhani haya mambo ya kumwonesha mtu kwamba unampenda sana ndiyo tatizo. Hasa baadhi ya mwanaume.
“Siku moja nakumbuka nikiwa sina hili wala lile, nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi pale Piccolo, baada salamu akaniambia ‘unajua kama Diamond na Jokate wako hapa na wanapigana mabusu?’
“Nilichanganyikiwa sana, nikachukua teksi, nikaenda.
Kufika, kitu cha kwanza nililiona gari lake likiwa kwenye maegesho. Niliingia ndani, nikawakuta wamewekeana miguu. Niliwasalimia lakini hawakuitika.
“Kwa vile niliona kila kitu niliaga na kuondoka huku nikilia. Usiku Nasibu aliporudi alinikuta napanga nguo kwenye begi niondoke zangu, abaki mwenyewe. Hakutaka kuongea na mimi na mimi sikutaka kuongea naye, tukachuniana. Niliamua kutoondoka lakini mimi na yeye hatukulala kitanda kimoja kwa wiki moja. Alijua naumia lakini hakutaka kuanza.
AMWAGANA NA DIAMOND
“Siku moja isiyokuwa na jina, niliamka nikapanga nguo zangu kwenye begi nikaenda kwa dada yangu, Sinza. Ndiyo ikawa kimoja, nikamwacha yeye aendelee na maisha yake na mimi nikaendelea na maisha yangu. Lakini mimi na Jokate kwa sasa tuko vizuri tu.
Mwandishi: Oke, hiyo ilikuwa awamu ile ya kwanza, si ndiyo?
Wema: Yeah!
VIPI KUHUSU HARTMANN?
Mwandishi: Iliwahi kusemekana kuwa kuna wakati uliangukia kwenye penzi la mjasiriamali anaitwa Hartmann Mbilinyi, ni kweli?
Wema: Yale yalikuwa maneno ya watu. Unajua Hartmann nilikuwa nafanya naye kazi za filamu, wakati ule alikuwa na kampuni yake inaitwa Hartmann Production, watu wakadhani ‘nadate’ naye, si kweli bwana.
BAADA YA DIAMOND, NANI ALIFUATA?
Mwandishi: Wema, unaweza kutuambia mwanaume gani alifuatia baada ya wewe kuachana na Diamond akawa na Jokate?
Itaendelea wiki ijayo

Share:

WEMA AZUA TIMBWILI GLOBAL PUBLISHER KISA STORI YA DIAMOND


HOVYOOO! Wema Isaac Sepetu aliye pia Miss Tanzania 2006, amejitoa fahamu kwa kupandisha mzuka na kutinga makao makuu ya Kampuni ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar na kuzua timbwili la aina yake kisa kikiwa ni kuandikwa kwa habari zake na mpenziwe, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Wema akiwa ndani ya ofisi za Global na sura ya 'kuua mtu', mkononi akiwa na gazeti la Ijumaa Wikienda lenye stori: DIAMOND ATAMANI USHOGA. Kushoto ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
Tukio hilo la kumchoresha staa huyo mwenye vituko kila kukicha, lilijiri Jumatatu iliyopita kwenye ofisi za Global ambao ni wachapishaji wa gazeti hili (Amani), Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Risasi majira ya mchana kweupe hivyo kufunga mtaa huku wapita njia wakimzodoa kwa maneno ya kejeli.
ATINGA NA WAPAMBE DHAIFU
Akiwa na kundi la wapambe dhaifu na goigoi wakiongozwa na meneja wake, Martin Kadinda waliosimama nje ya ofisi hizo, Wema alifika kwa upole akionekana mkarimu kwa mlinzi ambapo aliomba kuonana na mwandishi nguli wa magazeti pendwa, Imelda Mtema.
Mlinzi alimruhusu kwa vile Global ni mjengo wa mastaa na watu wasio mastaa, huwa hawakauki kuingia na kutoka kwa mambo mbalimbali.
Wema alipofika mapokezi, pia aliomba kuonana na mwandishi huyo lakini tofauti na utaratibu ambapo huwa mgeni akifika huulizwa kama ana ‘apointimenti’ ili aitiwe anayemhitaji, Wema alipitiliza kwa nguvu hadi chumba cha habari akifuatana na kijana aliyekuwa akimrekodi.
Wema akiwa ndani ya News Room akimtafuta mwandishi wa Global Imelda Mtema, huku akisema yeye ni chizi!
Akiwa ndani ya chumba cha habari, Wema aliuliza kwa sauti ya juu na ya kujiamini: “Imelda yupo wapi? Nauliza Imelda yupo wapi?”

WEMA NA IMELDA
Katika kumtafuta Imelda kwa macho kwa sababu chumba cha habari ni kikubwa huku akionywa na wahariri kwamba atulize mzuka kisha aeleze shida yake, Wema alimuona Imelda akitoa maelezo kwa Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka kuhusu habari aliyokuwa ameifuatilia.
Cha kushangaza, Wema alimfuata Imelda mpaka kwenye meza ya mhariri huyo kisha kuanza kufoka kwa sauti ya juu.
MSIKIENI WENYEWE
“Kwa nini mnafuatilia maisha yangu? Kila siku mnaniandika na Diamond. Kwa nini Imelda unaniandika kuwa mimi msagaji?”
"Mimi ni chizi, nakwambieni mimi ni chizi zaidi ya machizi wote"....Wema alikuwa akifoka mwanamke!
ATULIZWA, AGOMA
Katika kuhoji huko, mhariri kiongozi alijaribu kumtuliza Wema ambaye alikuwa kama amewehuka: ”‘Wema tuelewane, eleza shida yako kwa utaratibu kwani hakuna ofisi isiyokuwa na utaratibu.”
Pamoja na kuambiwa hivyo bado Wema aliyekuwa ameshika Gazeti la Ijumaa Wikienda toleo la Jumatatu iliyopita, aliendelea kumng’ang’ania Imelda ambaye alikuwa akijaribu kumtuliza:
“Wema twende tukakae pale kwenye meza ya mkutano uwaeleze viongozi wangu tatizo lako. Hiyo stori kuwa wewe ni msagaji mbona haipo, ni gazeti gani?”
"Mimi ni chizi, msinitanie ohhh!!
Licha ya kupewa mwongozo huo, Wema aliendelea kufoka:
“Hivi mnajua mimi ni chizi? Kwa taarifa yenu mimi ni chizi zaidi ya machizi wote, ohooo!”

MLINZI ATONYWA, ATIA TIMU
Baada ya hali kuwa tete, mlinzi wa geti kuu alipigiwa simu ya mezani na kujulishwa juu ya Wema kusababisha kazi kusimama ambapo alifika haraka tayari kwa kumtoa nje kwa hiyari yake au lazima.
Ndipo kukatokea timbwili kubwa, wapambe wake ‘goigoi’ nao waliingia wakitaka kufanya vurugu ili kumteka mwandishi huyo lakini kikosi imara cha Global kikiongozwa na Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally kilijiimarisha na kutuliza fujo hizo huku kikiwa makini kuhakikisha Wema na timu yake hawajeruhiwi hata kidogo.
WEMA ATUMIA GAZETI KAMA SILAHA
Katika purukushani hiyo, Wema alionesha udhaifu wa kumudu varangati pale alipotumia gazeti aliloshika kumpiga nalo mwandishi Imelda, jambo lililodhibitiwa kama Waasi wa M23 wa Kongo walivyodhibitiwa na Majeshi ya Umoja wa Mataifa, akatolewa nje.
Wema akiwa nje ya ofisi sasa baada ya kutolewa kwa nguvu, yeye pamoja na wapambe wake
MBALI NA WEMA
Ukiachia mbali Wema kutulizwa kwa kutolewa nje kwa nguvu, vijana wake walegevu nao waliwekwa chini ya himaya ya Global kwa kunyang’anywa  kamera ya video iliyokuwa ikitumika kuchukua matukio huku nao wakipigwa picha za kutosha na wapiga picha wetu.
VITA KUBWA, WEMA AVUA VIATU
Nje ya ofisi, ‘vita’ kubwa kati ya Wema na walinzi wa Global (alifika mwingine kutoka lindo la mbali) ilizuka ambapo staa huyo alivua vile viatu vyake virefu vya rangi ya bluu bahari na kuanza kumpiga navyo mmoja wa walinzi hao akiamini anamkomesha lakini pia akadhibitiwa!
Wema akiwa ameshika viatu vyake vya mchuchumio mkononi baada ya kutolewa nje ya ofisi na wapambe wake akiwemo meneja wake, Martin Kadinda (kulia).
Wema akiwa anarandaranda kwenye geti kuu akiwa peku, alidondosha matusi ya nguoni ambayo hayaandikiki gazetini kwa namna yalivyokuwa makali. Ilikuwa si rahisi kuamini kuwa yeye ni kioo cha jamii.
Timbwili la Wema na wapambe wake akiwemo Petit Man, ambao hawakufua dafu kwa walinzi na vijana wa Global nje ya ofisi hizo, lilichukua zaidi ya nusu saa huku likikusanya kadamnasi na kusababisha mtaa kujifunga wenyewe.
Wema akiwa kafura ka' faru aliyekoswa koswa kung'olewa kipusa na majangili, kulia ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
POLISI HAO
Hata hivyo, uongozi wa Global uliwasiliana na Polisi wa Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar ambao walifika na kumkuta Wema na timu yake wakiwa wamepoa mlangoni, wakaambiwa timbwili limetulia hivyo wakatimua zao.
'Baby' wa Diamond Platnumz alikuwa hashikiki viatu viligeuka kuwa 'mzigo mzito' akivibagwa chini huku akitoa mkwara akiwa pekupeku na kufunga mtaa.
Ilibidi askari polisi waitwe kuja kuhakikisha utulivu unakuwepo huku wapita njia wakiwa hawaamini macho yao kuwa wanayemuona mbele yao 'peku peku' akimwaga mitusi ni Miss Tanzania, Wema Isaac Sepetu!
APEWA KAMERA, KADI NOOOO!
Baadaye Wema aliomba kupewa kamera yake ambapo zoezi hilo lilifanyika lakini ‘memori kadi’ yenye picha walizoanza kurekodi, ilitolewa ili kupisha maridhiano kwanza. Waliambiwa kadi hiyo ilitolewa kwa sababu walirekodi bila idhini au kibali cha Kampuni ya Global.
Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye msafara wa Wema ni pamoja na Ammy Nando (kushoto), mshiriki wa Big Brother Africa 'The Chase' ya mwaka jana ambaye alikuwa akificha sura kukwepa kamera za Global.
WEMA AGOMA KUONDOKA
Baada ya kugundua kadi ya kamera ipo chini ya ulinzi wa Global, Wema alitaka kulianzisha tena akidai hawezi kuondoka hadi apewe kadi hiyo lakini uongozi uliweka ngumu. Baadaye aliondoka kimyakimya. Wakati huo wapambe wake walishaondoka kitambo.
WEMA: CHIZI in action......
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, kadi ya kamera hiyo bado ilikuwa inashikiliwa na uongozi wa Global ili kumthibitishia Wema kuwa hawezi kufanya umafia wowote dhidi ya waandishi wa kampuni hiyo yenye nguvu kihabari nchini Tanzania.
Gari lake lililomleta Global kufanya timbwili.
KWA NINI?
Kwa mujibu wa Wema, magazeti ya Global yamekuwa yakimwandika vibaya yeye na mpenzi wake Diamond huku akitolea mfano wa habari iliyomhusu yeye na mwigizaji Aunt Ezekiel baada ya kunaswa kwa picha zao zilizoashiria vitendo vya usagaji.
Share:

VIDEO:SHOW YA DIAMOND AKIWA NA WEMA SEPETU

Tazama show ya msanii wa kizazi kipya diamond paltinumz
Share:

HALMASHAURI YA JIJI YABOMOA MEZA ZA MACHINGA POSTA DAR


HALMASHAURI YA JIJI YABOMOA MEZA ZA MACHINGA POSTA DAR

Maafande wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi leo wameendelea na bomoabomoa ya meza za wafanyabishara ndogondogo 'Wamachinga' kama walivyonaswa na kamera yetu maeneo ya Posta Mpya…
Maafande wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi leo wameendelea na bomoabomoa ya meza za wafanyabishara ndogondogo 'Wamachinga' kama walivyonaswa na kamera yetu maeneo ya Posta Mpya jijini.
Share:

Wednesday, 2 April 2014

VIDEO:KAMATI YA MARIDHIANO YA BUNGE NA VIAPO


Share:

VIDEO:TAZAMA VIGODORO VYA MABINTI WA KITANGA-SI MCHEZO


Share:

NAPE:CCM ITASHINDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 94 UCHAGUZI CHALINZE

Share:

MAJINA YA WALIMU WA DIPLOMA WALIOBADILISHIWA VITUO

ORODHA YA WALIMU WA STASHAHADA WALIOBADILISHIWA VITUO
ANWANI CHUO MASOMO F BOX 334 UKEREWE BUNDA HISTORY/ENGLISH GAIRO TARIME(V)
2 AGNESS KILEO F 31359 DSM MOROGORO HISTORY/ENGLISH MASWA MVOMERO
3 AIDANI EDWIN M BOX 4256 MBEYA DAKAWA GEOGRAPHY/KISWAHILI KARAGWE ILEJE
4 ANNA NGATUNGA F BOX 42100 DSM MTWARA GEOGRAPHY/KISWAHILI LINDI(M) LINDI(V)
5 AYUBU ASHERI M 1004 IRINGA KLERUU PHYSICS/CHEMISTRY BUKOBA(V) KILOLO
6 BERTHA M MWAKYEMBE F BOX9091 UKONGA MARANGU HISTORY/ENGLISH BUKOBA(M) ILALA
7 CHRISTINA W SAITOTI F BOX 43 KISONGO- MONDULI MARANGU KISWAHILI/ENGLISH MULEBA MONDULI
8 CONSOLATA F MDUMA F BOX 8 SAME MARANGU HISTORY/ENGLISH SERENGETI SAME
9 CORNELI JOHN M BOX 215 KARATU MONDULI CHEMISTRY/AGRICULTURE BABATI MERU
10 EDINA THEOBARD F 461 MOROGORO MOROGORO BIOLOGY/GEOGRAPHY KYERWA MOROGORO(V)
11 ELIZABETH MAKWAYA F BOX 197 NEWALA MTWARA KISWAHILI/ENGLISH KISARAWE MTWARA(M)
12 EMMANUEL MAJEMBE M BOX 3437, MBEYA MPWAPWA HISTORY/GEOGRAPHY BUKOMBE MBOZI
13 EMMANUEL J LUPENZA M BOX 889 MBEYA TUKUYU HISTORY/KISWAHILI MTWARA(M) MBEYA JIJI
14 EVA VEDASTO F BOX 843 BUKOBA BUNDA HISTORY/ENGLISH KARAGWE SHINYANGA(M)
15 EVALINA MYOVELA F BOX270 IRINGA SHINYANGA HISTORY/GEOGRAPHY UKEREWE NAMTUMBO
16 FABIOLA ELIUS F BOX 737 MOROGORO MARANGU HISTORY/KISWAHILI KYERWA TEMEKE
17 FABIOLA J AUGUSTINO F BOX 524,BABATI KOROGWE HISTORY/GEOGRAPHY ARUSHA(V) ARUSHA JIJI
18 FAINES J NGWEMBE F MBEYA CONSOLATA HISTORY/KISWAHILI KAHAMA MJI MUFINDI
19 FATUMA RAMADHANI F BOX 76549 DSM DAKAWA GEOGRAPHY/KISWAHILI URAMBO MKURANGA
20 FELIX NOMBO M S.L.P. 1495 IRINGA CONSOLATA HISTORY/KISWAHILI KISHAPU IRINGA(V)
21 FRANCIS MICHAEL M BOX 6337 MBEYA TUKUYU GEOGRAPHY/ENGLISH ITILIMA NJOMBE MJI
22 FREDY C KAYEGA M BOX 62 MLIMBA-KILOMBERO MARANGU HISTORY/GEOGRAPHY BARIADI KILOMBERO
23 FRIDA MANFRED F BOX 618 TUKUYU MBEYA-LUTHERAN KISWAHILI/ENGLISH NEWALA RUNGWE
24 FURAHA NGAVATULA F 691 MOROGORO MOROGORO GEOGRAPHY/MATHEMATICS MBINGA WANGING'OMBE
25 FURAHA KONZO F BOX 851 NJOMBE KASULU HISTORY/KISWAHILI ITILIMA NJOMBE MJI
26 GERDA JESSE F BOX 198 BUKOBA BUNDA KISWAHILI/ENGLISH SIKONGE MISUNGWI
27 GETRUDE PETER F BOX 10914 ARUSHA DAKAWA HISTORY/GEOGRAPHY NGORONGORO MERU
DAR ES SALAAM AL-HARAMAIN ISLAMIC KISWAHILI/CIVICS ROMBO ILALA
S/N JINA KAMILI
1 ABIA MGASA
28 HABIBA J ALLY
F
DSM
Page 1 of 3
HALMASHAURI YA
AWALI
ALIYOPANGIWA
SASA.
ORODHA YA WALIMU WA STASHAHADA WALIOBADILISHIWA VITUO
ANWANI 29 HAMISA MOHAMEDI F S.L.P 32654 DAR UNUNIO HISTORY/KISWAHILI GAIRO MTWARA(M)
30 VICTOR V MASSAWE M BOX 172 KATESH MARANGU HISTORY/GEOGRAPHY USHETU CHAMWINO
31 HILDA A KIGOMBA F BOX 63 MIKUMI DAKAWA HISTORY/GEOGRAPHY KIGOMA(V) KILOMBERO
32 HUSSEIN NGATALA M BOX 133 RUJEWA DAKAWA HISTORY/KISWAHILI KASULU KILOMBERO
33 IMANUEL K SAM M BOX 44, MWIKA MARANGU GEOGRAPHY/ENGLISH BUNDA MERU
34 INGLIDE NONGELE F BOX 1226 IRINGA TUKUYU HISTORY/KISWAHILI KILINDI MBEYA(V)
35 ISSA A KOKOLE M BOX 3 MAHENGE MTWARA HISTORY/KISWAHILI KIBONDO ULANGA
36 JANE D KAWAMALA F BOX 104899,DSM KOROGWE HISTORY/KISWAHILI MUSOMA(M) MVOMERO
37 JOSEPH J MWANGAKA M 947 MBEYA MOROGORO HISTORY/KISWAHILI SENGEREMA MBARALI
38 JOSINA DICKSON F BOX 9332 D'SALAAM TUKUYU HISTORY/ENGLISH MASWA KILOMBERO
39 JULIUS KWAY M S.L.P 1923 DODOMA TABORA KISWAHILI/ENGLISH TANDAHIMBA GAIRO
40 KISSA MWAKIBABA F 72719 DSM MOROGORO KISWAHILI/ENGLISH BUSEGA KIBAHA MJI
41 KISSA CHARLES F BOX 353 MBEYA TUKUYU KISWAHILI/ENGLISH NGARA CHUNYA
42 LABAN K MPOLI M BOX 921, ISANGA, DODOMA MARANGU HISTORY/KISWAHILI ILEJE BABATI
43 LAMECK LUSASI M S.L.P. 258 MAGULILWA KLERRUU GEOGRAPHY/MATHEMATICS IRINGA(M) MUFINDI
44 LIDA ADAM F BOX 4545 MBALIZI SONGEA HISTORY/KISWAHILI BABATI MJI MBEYA(V)
45 LILIAN MUGYABUSO F BOX 203 MWANZA NG'WANZA HISTORY/KISWAHILI MPWAPWA MULEBA
46 LUCIA Z MWITA F MOROGORO CONSOLATA HISTORY/KISWAHILI KISHAPU IRINGA(M)
47 LUCIANA LUCIAN F BOX 1424 IRINGA DAKAWA HISTORY/KISWAHILI KAKONKO IRINGA(V)
48 LUCY WILLY
S/N JINA KAMILI
CHUO MASOMO
HALMASHAURI YA
AWALI
ALIYOPANGIWA
SASA.
F 691 MOROGORO MOROGORO HISTORY/GEOGRAPHY LWITIKO HEZRON KILINDI UVINZA
                                          49 MWASHIBANDA
M MBEYA MBEYA MORAVIAN KISWAHILI/ENGLISH CHUNYA MBARALI
50 MABAMBA CELESTINE M BOX 70 BIHARAMULO BUNDA KISWAHILI/ENGLISH BUTIAMA ILEMELA
51 MALILO ATHUMANI M BOX 7944, DSM MPWAPWA HISTORY/GEOGRAPHY UVINZA MOROGORO(M)
52 MARIA MKHAI F BOX 188, SINGIDA MPWAPWA KISWAHILI/ENGLISH NKASI SINGIDA(M)
53 MARIA M GHULIKU F BOX 28018 PWANI MTWARA KISWAHILI/ENGLISH ULANGA MKURANGA
54 MASHAKA SIMYOTA M S L P 3040 MBEYA MBEYA-LUTHERAN HISTORY/KISWAHILI KYERWA ULANGA
55 MESHACK ROMAN M BOX 240 SENGEREMA BUNDA KISWAHILI/ENGLISH BIHARAMULO MISUNGWI
56 MOSHI KASSIMU F S.L.P 284, IGUNGA TABORA HISTORY/KISWAHILI KWIMBA IGUNGA
Page 2 of 3
ORODHA YA WALIMU WA STASHAHADA WALIOBADILISHIWA VITUO
ANWANI 57 MWISANI NGOMO M BOX 9121 DSM MTWARA KISWAHILI/PHYSICAL TABORA(M) MKURANGA
                                              EDUCATION
58 NEEMA MONYO F 41384 DSM MOROGORO KISWAHILI/ENGLISH ITILIMA MOROGORO(V)
59 NGOKOLO LUHENDE M S.L.P 280, MAGU TABORA HISTORY/KISWAHILI MBOGWE KISARAWE
60 NISAMEHE ALIKO F BOX 122 KYELA MBEYA-LUTHERAN GEOGRAPHY/KISWAHILI MASASI MJI KILOSA
61 OLIVER ALFRED F P.O.BOX 441 MOSHI CAPITAL HISTORY/KISWAHILI MOSHI(V) DODOMA(M)
62 PAULINA CHRISTOPHER F BOX 174 TABORA SHINYANGA GEOGRAPHY/KISWAHILI BUMBULI KASULU
63 PENDO CHARLES F 148 BUNDA MOROGORO KISWAHILI/ENGLISH KAHAMA MJI MOROGORO(M)
64 PETER WARIOBA M 53792 DSM MOROGORO KISWAHILI/ENGLISH MEATU BAGAMOYO
65 PONZIANO B MHUME M 700 TUKUYU KLERUU CHEMISTRY/MATHEMATICS IRINGA(M) MUFINDI
66 PROSISTA THOBIAS KAVISHE F MONDULI LINDI BIOLOGY/GEOGRAPHY KILWA MONDULI
67 RIZIKI T AGUTU F BOX 399 MAFINGA SHINYANGA KISWAHILI/ENGLISH ITILIMA SHINYANGA(V)
68 RUDIA H MWASHIYOMBO F BOX 299 MBOZI TUKUYU KISWAHILI/ENGLISH MTWARA(V) MBEYA(V)
69 SABINA ABRAHAMU F BOX 1050 SINGIDA SHINYANGA GEOGRAPHY/ENGLISH BIHARAMULO MKALAMA
70 SEKELAGA CHARLES F BOX 94 MOROGORO SONGEA HISTORY/KISWAHILI KIGOMA(V) MOROGORO(M)
71 SKOLA MATHIAS F BOX 1440, MWANZA BUTIMBA CHEMISTRY/BIOLOGY SENGEREMA MPANDA MJI
72 SOPHIA MPOLYA F BOX 260 MBEYA MTWARA HISTORY/KISWAHILI ILEJE KIBAHA MJI
73 STAN SASA M BOX 1059 IRINGA SONGEA KISWAHILI/ENGLISH BUTIAMA IRINGA(V)
74 SUZANA G SWAI F BOX 153, HIMO MPWAPWA HISTORY/KISWAHILI USHETU MVOMERO
75 TABU SIWINGWA F BOX 78 MAKETE MARANGU HISTORY/GEOGRAPHY KIGOMA(V) MBARALI
76 THERESIA DIONISI F BOX 10180, NAMANGA KOROGWE KISWAHILI/ENGLISH KARATU LONGIDO
77 TUBALE DAUD M S.L.P. 97, SHINYANGA BUTIMBA GEOGRAPHY/MATHEMATICS URAMBO IGUNGA
78 TUYONGE E KAYUNI M 2732 MBEYA AGGREY HISTORY/ENGLISH ILEJE ARUSHA(V)
79 UPENDO LUBOKA F 129 MAHENGE MOROGORO KISWAHILI/ENGLISH KILOLO ULANGA
80 YUSUPHU NYANGATUKE M 11 MWADUI SHINYANGA KLERRUU CHEMISTRY/BIOLOGY MBOZI IRINGA(V)
81 ZAINA BALAMA F 1483 IRINGA KLERRUU GEOGRAPHY/MATHEMATICS WANGING'OMBE IRINGA(V)
82 ZAINAB O KATITI F BOX 25024 DSM MTWARA HISTORY/ENGLISH MAFIA MKURANGA
83 ZUWENA Y NTAHALA F 691 MOROGORO MOROGORO KISWAHILI/ENGLISH KIGOMA(M) MOSHI(M)
S/N JINA KAMILI
CHUO MASOMO
Page 3 of 3
HALMASHAURI YA
AWALI
ALIYOPANGIWA
SASA.
Share:

VIDEO:KAULI YA MH.Mnyika KUWA TUMEFIKA HAPA TULIPO KWA AJILI YA UDHAIFU WA RAIS


Share:

WATANZANIA WENZANGU CCM hawakutaka Katiba Mpya na haitatokea

Nawasikitikia Watanzania wenzangu waliokaa mkao wa kula wakisubiri Katiba mpya.
Nasikia wengine wanafunga na kuomba ili Katiba ipatikane, wengine wamejawa tu na matumaini.
Ya Mungu mengi, inawezekana Katiba Mpya ikapatikana, lakini kwa mwendo huu, tayari matumaini yametoweka.
Kinachoendelea bungeni kwa sasa kimeanzia mbali. Mtoto wa nyoka ni nyoka, usijidanganye ukamsogezea kidole.
Wengi walijaa matumaini mwishoni mwa mwaka 2011 baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuanzishwa kwa mchakato wa Katiba mpya.
Ilikuwa ni ajabu kwani suala hilo halikuwepo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2010, tofauti na vyama vya upinzani kama vile, CUF na Chadema.
Kabla ya tangazo la Rais Kikwete aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani alipoulizwa kuhusu mchakato huo, aliruka kimanga akisema hautakuwepo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema naye aliwakaripia waandishi wa habari Ikulu mjini Dar es Salaam walipomuuliza kuhusu mchakato huo.
Maana yake CCM na serikali yake hawakuwa tayari na mabadiliko ya Katiba asilani,  lakini kwa mshangao, Rais Kikwete akatangaza mchakato huo.
Pengine aliusoma upepo wa siasa, akaona aweke kando woga wa CCM na kuichukua hoja ya Katiba mpya  katika muda ambao hakukuwa na maandalizi ya kutosha kubeba mzigo huo mkubwa.
Baada ya hapo Tume ya Mabadiliko ya Katiba (TMK) ikaundwa. Makamishna wakateuliwa na kulipwa mishahara na masurufu ili tu watayarishe rasimu bora ya Katiba.
Tayari rasimu ya kwanza na ya pili zimetolewa na mambo yamebadilika kabisa. Kisa tu, rasimu imetaja muundo wa Muungano wa serikali tatu, ambao CCM hawautaki; ukweli unauma.
Share:

VIDEO:MAN U YAKAZA MWANZO MWISHO




London, England. Manchester United na Barcelona zimeshindwa kutumia vizuri viwanja vyao vya nyumbani baada ya kulazimishwa sare 1-1 na Bayern Munich na Atletico Madrid katika michezo ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa jana.
Manchester United wakiwa kwenye uwanja wao wa Old Trafford, walipata bao la kuongoza dakika 58, kupitia nahodha wake Nemanja Vidic akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona, kabla ya Bastian Schweinsteiger kuwasawazishia mabingwa watetezi Munich dakika 67, akimalizia mpira wa kichwa kutoka kwa Mario Mandzukic.
Bayern walipata pigo dakika za mwishoni baada ya kiungo wake Schweinsteiger kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Wayne Rooney.
Kwa mara ya nne mfululizo msimu huu mechi kati ya Barcelona na Atletico Madrid inashindwa kutoa mshindi baada ya jana kutoka sare 1-1 kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Neymar aliinusuru Barcelona na kipigo kwa kufunga bao la kusawazisha dakika 71, baada ya Diego kuifungia Atletico goli la kuongoza dakika 56.
Timu zitakazofuzu kwa nusu fainali zitajulikana wiki ijayo kwenye mechi za marudiano.
Leo kuna mechi nyingine mbili za robo fainali kati ya PSG dhidi ya Chelsea na Real Madrid wataonyeshana kazi na Dortmund.
 Jose Mourinho ameitoa Chelsea katika mbio za ubingwa, lakini anaamini vijana wake watathibitisha ubora wao leo dhidi ya Paris Saint-Germain katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Share:

UTAJIRI WA MASANJA KUFURU


UTAJIRI wa komediani maarufu Bongo,  Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ni kufuru! Tena unatisha na sasa anaonekana kuwa miongoni mwa wasanii wanaomiliki fedha na mali nyingi Bongo, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.
Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa mbele ya usafiri na mjengo wake.
HABARI MEZANI
Awali, habari kuhusu utajiri wa Masanja ilitua mezani mwa gazeti hili kama kidokezo, hapo mwandishi wetu akaingia mzigoni na kuanza kuchunguza kwa kina mali anazomiliki msanii huyo na kugundua kuwa ni kati ya mastaa mabilionea Bongo.
“Masanja sio yule tena. Ana mpunga (fedha) mrefu sana. Hakuna msanii wa maigizo Bongo anayeweza kumfikia kwa sasa. Hao wengine ni mbwembwe tu, lakini pesa imelala kwa Masanja,” kilipasha chanzo chetu.
Kikaongeza: “Kwanza ana ghorofa lipo Tabata, hapo ndipo anapoishi. Pia ana magari kibao ya kifahari, mashamba ya mpunga na Kampuni ya OK Security inayolinda sehemu mbalimbali zikiwemo taasisi nyeti nchini.
Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa kwenye pozi na miongoni mwa magari yake.
“Ni msanii gani mwenye kampuni kubwa kama ya Masanja? Wengi wanaishia kudai wanatayarisha filamu ambazo hata matunda yake hayaonekani.”
RISASI MZIGONI
Mdogomdogo, Risasi Mchanganyiko likajitupa mtaani kuchimba kuhusu madai hayo ambayo awali liliyatilia shaka kama si wasiwasi.
Uchunguzi wetu ulibaini ukweli wa mali za msanii huyo na mambo mengine mengi yanayoingia kama vyanzo vya mapato yake.
MAGARI SITA
Ilibainika kuwa, Masanja anamiliki magari sita, yakiwemo ya kifahari. Baadhi ya magari hayo ni Toyota Land Cruiser V8, Nissan Hardboad na Toyota Verossa.

NYUMBA TATU BONGO
Pia, mkali huyo wa kuvunja mbavu, anamiliki nyumba tatu za maana jijini Dar es Salaam, moja ni ghorofa ipo Tabata, nyingine Kigamboni na nyingine haifahamiki eneo rasmi ilipo.
Hata hivyo, imebainika kuwa mbali na mijengo yake hiyo iliyopo jijini Dar, nyumbani kwao Mbarali, Mbeya ana mjengo wa maana.

MASHAMBA KIBAO
Msanii huyo hayupo nyuma kwenye kilimo, ana mashamba kadhaa Kigamboni jijini Dar es Salaam lakini linalotia fora ni lile lililopo Mbarali lenye ukubwa wa hekari 50 ambalo analima mpunga.

NI MSANII WAMAIGIZO TAJIRI ZAIDI?
Kwa utajiri huo, ipo minong’ono kuwa, nyota huyo anaweza kuwa kwenye namba za juu za wasanii wa maigizo wenye mkwanja mrefu.
Wengine wanaotajwa kwenye orodha ya waigizaji matajiri Bongo ni Husna Posh ‘Dotnata’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ na Amri Athumani ‘Mzee Majuto’.
MATAJIRI BONGO FLEVA
Katika muziki wa Bongo Fleva, wasanii wanaoaminika wana utajiri mkubwa zaidi ni Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Joseph Haule ‘Profesa Jay’.
Wasanii hao wanamiliki mijengo ya maana, achilia mbali magari ya kifahari na miradi kadhaa.

MASWALI KUHUSU MASANJA
Utajiri wa Masanja umeonekana kuibuka ghafla huku vyanzo vyake vya kumwingizia kipato vikijulikana ni sanaa ya uigizaji, muziki na huduma ya uchungaji.
Je, kwa uigizaji tu katika Kundi la Orijino Komedi ‘OK’ ndiko alikopata mkwanja huo na kuanzisha miradi hiyo mikubwa?
Kama ndiyo, kwa nini memba wenzake ndani ya kundi hilo hawana maendeleo makubwa kama yeye?
Kazi nyingine ya Masanja ni muziki wa Injili ambapo kwa sasa albamu yake ya Hakuna Jipya iko sokoni. Je, albamu hiyo na shoo anazofanya zinaweza kuwa chanzo cha utajiri huo?
Lakini pia Masanja ni mchungaji ambaye anahudumu katika Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) ‘Mito ya Baraka’ lilicho chini ya Askofu Bruno Mwakiborwa. Je, mshahara anaoupata kutokana na huduma hiyo unaweza kuwa chanzo cha mapato yake?
Risasi Mchanganyiko halikutaka kupasua kichwa, juzi lilimsaka Masanja kwa simu na kumhoji juu ya mali zake ambapo kwanza alithibitisha kweli anamiliki mali hizo na nyingine ambazo hakupenda kuzitaja.
“Ni kweli nina nyumba tatu hapa mjini, kampuni ya ulinzi na mashamba ya mpunga eka 50 nyumbani Mbarali, Mbeya. Kuhusu magari pia ni kweli kabisa. Mimi ni mtumishi sitakiwi kusema uongo,” alisema Masanja.
RISASI: Lakini mbona utajiri wako umekuwa wa haraka sana mtumishi, vipi vyanzo vya mapato yako?
MASANJA: Orijino Komedi ndiyo chanzo cha vyote... pale ndipo kwenye koki.
RISASI: Kuchekesha tu kaka? Au kwenye muziki wa Injili pia kunalipa?
MASANJA: Injili na uchungaji ninaotumika kanisani ni huduma kaka, sitegemei mapato kutoka huko. Nipo kwa ajili ya kulisha kondoo wa Bwana.
RISASI: Wasanii wenzako wa Orijino Komedi wanachukuaje mafanikio yako?
MASANJA: Wanafurahia, wananiunga mkono maana ni sehemu ya mafanikio yao pia. Sisi tunaishi kama ndugu. Kwa hiyo kuna baadhi ya aidia ni zao, hivyo wanajivunia sana mafanikio yangu.
Tuituitui! Simu ikakatika!

Share:

VIDEO:KUSHUKA KWA MAADILI


Share:

Tuesday, 1 April 2014

MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA GEREZA LA KEKO

PIPI 60 za madawa ya kulevya aina ya heroine yanayokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 60 yanadaiwa kukamatwa ndani ya Gereza la Keko jijni Dar es Salaam baada ya mtu mmoja kuingia nayo akiwa ameyameza.
Madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo, mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Mashujaa Udugu Matata, aliingia gerezani humo Machi 21, mwaka huu akitokea kusomewa shitaka la kukutwa na madawa ya kulevya katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa Matata alikamatwa na polisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Machi 17, mwaka huu, saa 8.25 usiku akitokea nchini Brazil.
Baada ya kukamatwa alitoa pipi 102 za madawa hayo. Alipofikishwa gerezani hapo, inasemekana mtuhumiwa huyo hakuwa na hali nzuri kiafya, jambo lililofanya awekwe chumba cha mahabusu wagonjwa ili aweze kufuatiliwa kwa karibu na madaktari.
Mashujaa Udugu Matata aliyekuwa na madawa ya kulevya.
“Kesho yake asubuhi kuna mfungwa alikwenda kufanya usafi katika chumba hicho, wakati anachukua takataka, akaitwa na Matata na kumuomba achukue mzigo uliofungwa kwenye karatasi ambao ulikuwa unanuka kinyesi, akamweleza ampelekee mahabusu mwenzake anayeitwa Abbas Gede,” kilisema chanzo chetu.
Inasemekana Gede ni rafiki wa Matata ambaye naye ana kesi ya ‘unga’ na kwamba awali waliwahi kuishi pamoja Brazil.
Kutokana na sheria kutoruhusu mfungwa kuonana na mahabusu, alilazimika kumpatia mahabusu mwingine ili aufikishe mzigo huo, lakini badala ya kuufikisha, mahabusu huyo aliambiwa na rafiki zake kuwa unga huo ni wa mamilioni ya shilingi, hivyo asubiri awape ndugu zake wakija kumpelekea chakula.
Kamishina Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Minja.
Hata hivyo, akiwa katika harakati za kutaka kuwapa ndugu zake, askari wa magereza walimkamata na alipoulizwa alikoyatoa, alimtaja Matata na hivyo kufanikisha kukamatwa kwa wote waliohusika na mzigo huo.
Mkuu wa gereza hilo, Sena Shida amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa watu wote waliohusika wataadhibiwa. “Kwa upande wake, Matata ataadhibiwa mara atakapopata nafuu kulingana na sheria ya mwaka 1967, huo unga tumeuchoma moto,” alisema Shida.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa alipoulizwa alikiri kukamatwa kwa Matata na kwamba alitoa pipi 102.
Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa.
Awali walijua kuwa zimeisha hata hivyo, Nzowa alisema alimwagiza mkuu huyo kuyapeleka madawa hayo ofisini kwake, akashangaa kusikia yalichomwa. Aidha, alisema aliwasiliana na mkuu huyo wa gareza ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo ingawa hakuweza kutoa ripoti kituo cha polisi kama ilivyo taratibu.
Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa, Matata aliwahi kukamatwa mwala 2007 kwa tuhuma ya kusafirisha madawa ya kulevya na kufikishwa mahakamani na alikuwa chini ya uangalizi wa jeshi hilo na wakati huo alikuwa hajabadili jina, aliitwa Abdallah Mauri Kaikai.
Kamishina Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Minja aliwahi kuufumua uongozi wa Gereza la Keko kutokana na tuhuma za kuwepo biashara ya madawa ya kulevya ndani ya gereza hilo.
Share:

LULU KAIBA BWANA WA MTU

Habari zinaeleza bifu lao limefikia hatua ya kuanikana waziwazi hadi kumwagiana matusi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram lakini huondoa majibizano yao machafu kila baada ya muda mfupi.
Chanzo cha habari hizi kinapasha kuwa ugomvi wa Lulu na Husna ni juu ya mwanaume huyo ambaye anaishi jijini Arusha aliyetajwa…
E LIZABETH Michael ‘Lulu’ anayetesa katika filamu za Kibongo, yupo kwenye bifu zito na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid ambaye anadai amempora bwana’ke.
Staa Elizabeth Michael ‘Lulu’ katika pozi.
Habari zinaeleza bifu lao limefikia hatua ya kuanikana waziwazi hadi kumwagiana matusi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram lakini huondoa majibizano yao machafu kila baada ya muda mfupi.
Chanzo cha habari hizi kinapasha kuwa ugomvi wa Lulu na Husna ni juu ya mwanaume huyo ambaye anaishi jijini Arusha aliyetajwa kwa jina moja la Seki anayeelezwa kuwa na pesa za kutosha kusumbua mjini. “Hao wanamgombea jamaa fulani wa Arusha, anaitwa Seki, ana mawe (pesa) mbaya.
Mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid.
Lakini wa kwanza kuwa na Seki ni Husna na Lulu alijua, sema Husna na huyo jamaa walikuwa wanagombana na kumwagana mara kwa mara. Sijui sasa nini kilimfanya Lulu kwenda kutembea tena na huyo jamaa wakati anajua ni wa shoga yake, labda ni baada ya kujua wamemwagana,” kilipasha chanzo hicho.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Baada ya kupata habari hizi, mwandishi wetu aliwatafuta Lulu na Husna kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo. Lulu alikuwa wa kwanza kupatikana ambapo alisema: “Jamani mimi simjui kabisa Husna Maulid wala hata katika fikra zangu hayupo... yaani kifupi simjui.”
Husna alipopatikana na kuelezwa mkanda mzima, kwanza alishangaa Lulu kutomjua, akasema: “Hakuna mtu asiyejua kuwa Lulu kanipora mwanaume wangu. Lakini anajifanya mjanja, tutaoneshana tu. Anajidai sana, anajifanya wa mjini hanijui mimi, lakini mimi ni wa mjini zaidi yake.”
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger