Baadhi ya wabunge wameitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina katika mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka-DART-kwa madai ya kuwepo kwa ufisadi mkubwa na uchotwaji wa mabilioni ya fedha ya ujenzi wa mradi huo.
Akichangia maoni ya hotuba ya bajeti ya serikali ya mwaka 2015/16, mbunge wa viti maalum, Mhe Esther Matiko amesema barabara hiyo haina maeneo ya watembea kwa miguu, pikipiki, na upana wa barabara hiyo hauwezi kuruhusu malori mawili kupita kwa wakati mmoja na kusisitiza inaufisadi wa hali ya juu, huku mbunge wa Singida Magharibi akiitaka serikali kuhakikisha inafuatilia fedha katika benki ya Exim ili kutekeleza mradi wa umeme wa upepo ulioanza takribani miaka saba iliyopita.
Aidha, suala la ongezeko la tozo katika mafuta limechukua nafasi kubwa ya miongoni mwa wabunge katika mjadala wa hotuba ya bajeti kwa siku ya tano mfululizo ambapo mbunge wameendelea kuilalamikia serikali kwa kuweka tozo katika mafuta hususani ya taa na kuhacha vinywaji baridi na vikali ambavyo simahitaji ya lazima ukilinganisha na umuhimu wa mafuta ya taa, huku wengine wakisisitiza lazima wananchi wa sasa waumie kwa faida ya vizazi vijavyo.
Aidha bunge limeitimisha mjadala wa hituba ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2015/16 ambapo siku ya jumatatu mawaziri mbalimbali wataanza kujibu hoja zilizokuwa zikitolewa na wabunge kwa takribani siku tano za mjadala wa hituba ya bajeti ya serikali ya shilingi trillioni 22.495 kwa mwaka wa fedha 2015/16.

0 comments:
Post a Comment