Saturday, 27 June 2015

MSANII AMRITHI KAPTENI JOHN KOMBA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
KUELEKEA Uchaguzi Mkuu 2015 utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu, msanii ambaye ni kiongozi wa Kundi la Sanaa la Jakaya Theatre linalorusha mchezo wake kupitia Televisheni ya ITV, Daudi Mponji a.k.a Lazi amerithi mikoba ya aliyekuwa mtunzi wa nyimbo za kuhamasisha za Chama Cha Mapinduzi (CCM), marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia Februari 28, mwaka huu.
Akizungumza na gazeti hili, Mponji alisema ametunga nyimbo tano ambazo ni Pambazuko, Sema Usiogope, CCM Imeweza, Tumpambe na Mambo Hadharani, zinazokamilisha albam inayokwenda kwa jina la Pambazuko.

Alisema nyimbo hizo zitatumika kuhamasisha CCM kuchagua mgombea bora ambaye atapambana na vyama vingine vya upinzani hasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
“Unajua kuna pengo kubwa aliloliacha Komba hivyo kwa nyimbo zangu na sauti nitahakikisha nafanya kazi hiyo ipasavyo kwenye Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika Dodoma mapema mwezi ujao kuwachuja wagombea,” alisema Mponji akimuomba Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Kepteni Komba ambaye pia alikuwa Mbunge wa Mbinga-Magharibi kwa tiketi ya CCM.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger