ILIPOISHIA RISASI JUMATANO:
Martha ndiye aliyekuwa mchokozi pale
kitandani. Alimshikashika Roi kwa kuanzia kichwani, akaja kifuani,
akampa kidole chake kwenye kinywa, Roi akakipokea, akamlalia kifuani
huku akianza kuhema kwa staili ya mahaba.
Mara, mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni uligongwa…
“Mh! Martha! Si jamaa yako huyo kweli?”
JIACHIE NAYO MWENYEWE…
“Hapana baby, hakuna jamaa yangu. Si nilishakwambia lakini?”
“Sasa nani anagonga muda huu?”
“Ngoja nitoke,” alisema Martha akitoka.
Akaenda mlangoni. Roi alivaa sawasawa akasimama tayari kwa lolote…
“Inawezekana ameniingiza chaka huyu demu,” alisema moyoni Roi huku ukimdunda kwa kasi.
Mara, mlango ulisukumwa, Martha akarudi akiwa anatabasamu. Mkononi alishika hot pot…
“He? Baby, ulishavaa! Kwa nini sasa?”
“Ni nani aliyegonga?”
“Si mpangaji mwenzangu mmoja. Kanipa futari hii nikupe wewe,” alisema Martha huku akiendelea kutabasamu.
Martha aliliweka hot pot hilo kwenye stuli na kurudi kitandani kuendelea na Roi ambaye naye alishapanda tena kitandani.
Walianzia pale walipoachia, wakapaendeleza. Kila mmoja akiwa na mhemko mkubwa wa mahaba.
Martha, mara zote huwa hapendi kufika
mbali na kujiumiza wakati anajua anaweza kupona muda huohuo. Alimtaka
Roi kwa ishara ya vitendo kwamba sasa kipyenga kipulizwe. Kikapulizwa
kweli, mechi ikaanza huku kila mchezaji akiwa amekamia ushindi.
Kwa kawaida, Martha huwa hapendi kuingia
uwanjani kucheza huku kuna giza. Anapenda mwanga. Kwa hiyo alipotoka
kwenda nje, Roi alizima taa, sasa yeye akanyoosha mkono mpaka kwenye
swichi ya kitandani ‘bed switch’, akawasha taa! Mwanga waaa!
Alimwangalia Roi na kuachia tabasamu jingine akamuuliza…
“Au hujapenda kaka?”
“Nimependa dada.”
Wakacheka wote kwani walijua walitumia neno kaka, dada kimakosa na si mahali pake kwa hatua waliyokuwa wameifikia muda huo.
Ghafla, Martha aliacha kucheka, Roi naye
akakunja sura, mambo yakaendelea, sasa kilichojulisha nini kinaendelea
ni kuhema kwao kwa kasi huku Martha akishadadia katika maeneo
f’lanif’lani hawa pale mashambulizi yanapokuwa ya kasi.
Martha aliomba kutangaza nia, Roi
akamkubalia. Baada ya kutangaza nia hakufika hata mikoa mitatu kusaka
wadhamini akawa amewapata katika mikoa miwili tu, akatulia akiwa
amemng’ang’ania Roi mwilini kwa kumbana kwa nguvu zake zote.
Roi alihamasishwa kwa kitendo hicho na yeye akatangaza nia, akafika mpaka mwisho wa safari yake iliyojaa mashamsham.
Sasa walilala huku kila mmoja akiwa
anahema na kuchoka. Martha alichukua nafasi kwa kulala upande wa ukutani
huku Roi naye akilala upande wake kwa kuangalia mlangoni.
* * *
Kulikucha, Martha ndiye aliyeanza kuamka, akaenda kuandaa maji ya kuoga Roi kisha akarudi kumwamsha Roi…
“Baby…baby…’
“Mm…”
“Amka kumekucha baby wangu.”
“Mh! Mara hii baby?”
“Si unaona kumekucha, au?”
“Oke,” alisema Roi huku akiamka kwa tabu. Alinyoosha mkono na kuuingiza ndani ya begi, akatoa bukta.
“Darling si utaweza kwenda bafuni nje?” Martha aliuliza kwa sauti ya upendo.
“Yes. Haina shida.”
“Twende basi baby wangu.”
Roi alisimama, akatupiwa taulo begani,
akatoka huku Martha akiwa mbele yake mpaka uani, lakini kabla hajaingia
bafuni, wapangaji wenzake Martha ambao walikuwa hapo, walimsalimia Roi…
“Za asubuhi kaka..?”
“Umeamkaje kaka?”
“Kaka umeamkaje?”
“Nimeamka salama jamani. Sijui nyie?”
“Sisi wazima…”
“Siye hatujambo…”
“Sisi tuko poa sana.”
Martha alishangazwa na uchangamfu wa
wapangaji wenzake kwa mpenzi wake Roi, lakini pia alijua wao wanamwita
kaka kwa sababu ya utambulisho wake wa siku ya kwanza.
Martha alirudi ndani, Roi akaingia bafuni mwenyewe kwani maji yalishawekwa.
Wale wapangaji waliangaliana kwa macho
ya kuulizana maswali mengi kiasi kwamba, walitamani hata kutoa sauti.
Macho yao yalisema hivi…
“Sasa ukaka gani jamani wakati wamelala kitanda kimoja?”
“Jamani hawa ni kaka na dada kweli?”
“Mmewaona kaka na dada’ke?”
Mara, Roi akatoka. Yule mpangaji aliyesema atamwomba namba ya simu akamsogelea…
“Sasa kaka hunipi namba yako ya simu au unamwogopa dada yako mwingine?”
“Sifuri sita tano tano…ishirini…sabini na tano…”
Je, unajua nini kiliendelea? Usikose kusoma chombezo hili tamu sana kwenye Gazeti la Risasi Jumatano ijayo.
0 comments:
Post a Comment