Monday, 31 August 2020

Picha : KEMBAKI AZINDUA RASMI KAMPENI UBUNGE TARIME MJINI …AAHIDI MAKUBWA AKICHAGULIWA, MAKADA WATIA NENO



Mgombea ubunge Jimbo la Tarime mjini kupitia chama cha Mapinduzi CCM Michael Kembaki akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni zake.
**
Na Dinna Maningo - Tarime
Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) Michael Kembaki amezinduka Kampeni ya kugombea ubunge huku  akiahidi kufanya maendeleo makuwa ikiwemo upatikanaji wa huduma ya maji safi ,miundombinu ya barabara na ujenzi wa Soko kuu.

Katika uzinduzi huo walihudhuria Viongozi na wanachama wa CCM, Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara,kada maarufu wa CCM na mmiliki wa Mabasi,Peter Zakaria ,Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa mkoa wa Mara Christopher Gachuma,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Samwel Kiboye (Namba Tatu) na wananchi.

Kembaki alisema kuwa Tarime haina maji safi na salama  na kwamba hata chanzo cha maji mto Nyanduruma hakitoshekezi mahitaji na wakati wa kiangazi chanzo hicho hukauka.

"Nashukuru chama changu kuniamini na kuniteua,kura mlizonipa 2015 wakati nagombea Ubunge zilinipa imani nikaamua kurudi ,ndugu zangu muungwana ni yule anayeshukuru hata kwa kidogo,najua kuna wananchi waliniamini walinipigia kura",alisema Kembaki.

Aliongeza "Nakumbuka ahadi nilizozitoa niliona kero mbalimbali nikajinyima na baadhi nikazitatua hii kero ya maji imekuwa ni kilio, chanzo cha maji kipo Kenyamanyori lakini hata wananchi wa hapo hawapati maji na ni machafu ukifua nguo nyeupe ina badilika rangi naomba mnichague nitatue kero ya maji na soko kuu lililotelekezwa kwa muda mrefu bila kujengwa nitahakikisha linajengwa".

Akizungumzia ubovu wa miundombinu ya barabara Kembaki alisema kuwa wilaya ya Tarime ina rasilimali nyingi ambapo barabara za mjini zote zilitakiwa kuwa za lami na si za vumbi.

"Akina mama wanauza matunda kwenye vumbi huwa nikipita na kuwaona roho inauma, mkinichagua ntahakikisha naboresha mazingira rafiki ya biashara ,waendesha pikipiki wanapata tabu pikipiki zinawahi kuharibika kwa sababu ya ubovu wa barabara", alisema Kembaki.

"Nimezunguka kata 8 nimechangia maendeleo mwenzangu Esther Matiko wa CHADEMA wakati wa kugombea 2015 aliahidi kujenga ghorofa shule ya msingi Sabasaba ahadi ambayo mpaka leo hajaitekeleza ila mimi nilisema sina uwezo ntajenga darasa la kawaida nanyi ni mashahidi mnaona wanafunzi wanasoma niliyoyaahidi nimetekeleza kwa asilimia 80 ",alisema Kembaki.

Mke wa mgombea huyo Magreth Rhobi aliwaomba wananchi kumpa kura mmewe ili afanye maendeleo.

Katika uzinduzi huo  baadhi ya makada wa CCM waliokuwa wakitia nia kugombea ubunge kupitia chama hicho akiwemo Jackson Kangoye aliyekuwa mshindi namba moja ambaye hata hivyo jina lake halikurudi na badala yake vikao vya chama Taifa  vilimteua Michael Kembaki wamehudhuria uzinduzi huo wa Kampeni .

Kangoye aliwashukia watu wanaoeneza maneno kupitia mitandao ya kijamii kuwa yeye hamuungi mkono Kembaki na kusema habari hizo ni za uongo.

"Nimesikia maneno mengi kuwa mimi simuungi mkono Kembaki ni uongo mimi nitashiriki na Kembaki katika kampeni zake tumsaidie aweze kushinda,aligombea 2015 kura hazikutosha saizi kajipanga na ninaamini tutashinda na ikiwezekana aongoze miaka 10",alisema Kangoye.

Manchare Suguta ambaye ni ndugu wa mgombea ubunge jimbo la Tarime vijiini John Heche aliwaomba wananchi kumpigia kura Kembaki na Mwita Waitara anayegombea jimbo la vijijini.

"Hatuna muda wa kupoteza hapa ni kazi tu kwahiyo ndugu zanngu tumpe kembaki ni mtu wa kazi msidanganyike hapa ni kazi tu",alisema Susy Chambili.

Veronica Nyahende alisema "Wana Tarime tumepata nafasi tusiicheze tuwape kura CCM kwa maendeleo ya Tarime,akina mama tumechoka kubeba maji kichwani.

Wakili wa kujitegemea Onyango Otieno alisema"tuna matatizo mengi maji yetu ni shida UTI,Typhoid ni nyingi tunamtuma Kembaki atuletee maji,bararaba ni shida kama ya Kenyamanyorii".

"Mimi nilikuwa Mwenyekiti wa Vijana wa mkoani, nafahamu mambo mengi ambayo jimbo la Tarime mjini imeyakosa,huwezi kupata maendeleo kwa chama kisicho na Ilani  niwaombeni kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa ndiyo kosa mpigieni Kembaki",alisema Ditu Manko.

Hezbon Mwera alisema "Tarime mjini tunataka sasa tumtume Kembaki atuletee maendeo tunachohitaji sisi ni maendeleo tunataka mipango na miradi inayoonekana.

Mgombea ubunge viti maalum Mara Amina Makilagi aliwaomba wananchi" naomba mpigie CCM nina uzoefu ndani ya bunge sisi wabunge wa ccm tukikutana tunajadiliana kwanza kwenye vikao tupeni Kembaki atakayekwenda kusemea maendeleo, katika bajeti iliyopita tumepata mradi wa maji na Tarime imo,jiulize tangu tumepitisha fedha mbona hazijaja tupeni Kembaki maji yaje".

Roselina mgombea viti maalumu kundi la walemavu alisema "nashukuru kwa kunichagua hadi ngazi ya Taifa sisi watu wenye ulemavu tunapata shida hatuna mtu wa kutusemea nilitembelea shule moja hakuna vifaaa, walemavu wanahangaika mazingira si salama huku mgombea ubunge viti maalumu kundi la vijana akiwaomba vijana kumchagua Kembaki.

Wazee wa mila kutoka koo 12 za jamii ya Wakurya nao hawakuwa nyuma kumnadi Kembaki na Waitara, Nchagwa Mtongori mzee wa mila kutoka koo ya Wanchari alisema kuwa ili wananchi wapate maendeleo ni vema wachague CCM kwakuwa wao ni watekelezaji.

Mjumbe wa Kamati ya Siasa Charles Mniko aliwataka wazee wa mila kuungana pamoja kuiwezesha CCM kushinda.

Kada wa CCM ambaye pia ni mmiliki wa mabasi ya Zakaria yanayofanya safari zake Sirari-Mwanza Peter Zakaria alisema"nimejitahidi kuchangia maendeleo hospitali ilikuwa imeoza hatukutumia pesa za Serikali hata sh.100 najua nilipopata matatizo mlilia sana sasa naomba msiniangushe niko salama mpeni kura Kembaki"alisema Zakaria.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Tarime Daud Ngicho  alisema kuwa Rais Magufuli ametatua kero nyingi ikiwemo ya uanzishwaji wa masoko ya dhahabu ambayo yamewawezesha wafanyabiashara kuuza dhahabu huku akiwalalamikia waliokuwa wabunge wa Tarime kutoka CHADEMA kuingilia kesi zisizowahusu na kushindwa kushughulikia kero za watu wa Tarime  hili hali hawakuwa na kesi kwenye majimbo yao wanayotoka.

Mjumbe wa Halmashauri ya Taifa mkoa wa Mara Christopher Gachuma alisema uzinduzi ulikuwa wa kuwatambulisha wagombea nakwamba anaimani CCM itashinda kwa kishindo.

Mwenyekiti wa chama CCM mkoa wa Mara Samwel Kiboye (Namba tatu) alisema kuwa baadhi ya wanaCCM ni vigeugeu.

"Safari hii hatutawakubali wasaliti ndani ya chama,Kembaki Unapoenda kuomba kura mtangulize mungu ukimtanguliza shetani hakusogelei na mungu hasemi uongo mungu mambo yake yamenyooka safari hii lazima tukomboe majimbo.

"Tunataka kampeni ya Kiungwana sisi ndiyo tuna Serikali lakini tunaomba kampeni za heshima,tutangulize mungu mbele kwa kila jambo,tumeshavunja makundi ,mimi saizi Waitara namuunga hatuna utofauti lengo letu tunataka CCM ishinde tofauti zetu tumeziondoa,wanaccm msilizike tafuteni kura."alisema Keboye

Naye mgombea Ubunge jimbo la Tarime vijijini Mwita Waitara alisema "wagombea wote wa upinzani nawafahamu,kama tunataka kero zitatuliwe nakuomba pigia CCM ,kama mnataka tuachane na maji ya tope pigia Kembaki,mimi niiliona nijipendekeze ili nipate miradi nikaingia CCM ,Ukija spidi nitakutuliza ,ukija taratibu nitatulia vijana tumejipanga hii ngoma mtoto hatumwi sokoni",alisema Waitara.
Umati wa watu wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini kupitia CCM Michael Kembaki
Katibu wa CCM wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka wakicheza na wana CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini
Wafuasi wa mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni
Wafuasi wa mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni
Wafuasi wa mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni.
Makada wa CCM wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni .Kulia ni mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki,wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Samwel Keboye,wa kwanza kushoto ni mmiliki wa mabasi Peter Zakaria,wa pili kushoto ni Mjumbe wa NEC Christopher Gachuma
Wananchi wakicheza ngoma ya Ritungu wakati wa uzinduzi wa kampeni.
Wasanii wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge Michael Kembaki


Wasanii wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge Michael Kembaki
Share:

ACT WAZALENDO YAZINDUA ILANI YAKE YA UCHAGUZI MKUU 2020 IKIWA NA VIPAUMBELE 10


Chama cha ACT-Wazalendo leo Agosti 31, 2020 kimezindua Ilani yake ya Uchaguzi Mkuu 2020 ikiwa na vipaumbele 10 vyenye majibu ya changamoto mbalimbali za Watanzania.


Chama hicho kimezindua ilani hiyo itakayowawezesha wagombea urais, ubunge na udiwani kuinadi katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Mbali na uzinduzi huo, pia Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe alimkabidhi Ilani hiyo, mgombea urais wa chama hicho, Bernard Membe na mgombea mwenza Omar Fakih Hamad ili waitumie kusaka kura kwa Watanzania.

Kwa mujibu wa Ilani hiyo, chama hicho kimejinasibu kutekeleza na kuvisimamia vipaumbele hivyo ambavyo ni pamoja na:- Ujenzi wa Demokrasia na utoaji Haki za watu, Ufanisi na ubora wa Huduma za jamii, -Uchumi wa watu, Uhuru kwa kila mtu na Elimu bora itakayotolewa bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu.

Vipaumbele vingine ni Kilimo cha kimapinduzi na mazingira wezeshi ya biashara, Usawa na Ustawi wa Wanawake na Vijana, Hifadhi ya Jamii kwa kila mtu/Afya bora kwa wote, Ushirika wa kisasa kwa maendeleo jumuishi, Haki za watu wenye ulemavu, Maji safi, Salama na gharama nafuu na ajira mpya milioni 10.


Share:

Watumishi Wanne Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mikononi Mwa TAKUKURU

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwafikisha mahakamani watu watano wakiwemo wanne watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa makosa ya rushwa, uhujumu uchumi na ukwepaji kodi wa Sh.153.5 milioni.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020 na Doreen Kapwani, Afisa Uhusiano wa Takukuru kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo imesema, watumishi hao walikwisha fukuzwa kazi watafikishwa mahakamni leo.

Doreen imetangaza kutafutwa kwa Madaraka Robert Madaraka, aliyekuwa mhasibu wa Bandari ya Kigoma anayetuhumiwa kuhusika katika tuhuma hizo ili aweze kuunganishwa na wenzake.


Share:

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha CHAUMMA, Hashimu Rungwe Kuzindua Kampeni Septemba 5

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Chaumma, Hashimu Rungwe, ametangaza kuzindua kampeni zake za urais wa chama hicho Jumamosi tarehe 5 Septemba 2020 Manzese jijini Dar es Salaam.

“Chaumma itaongea na wananchi 5 Septemba 2020 katika Uwanja wa Manzese Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana. Wananchi waje wasikilize, tunachowaambia. Wakija pale watapata kila kitu na watauliza maswali na tutawajibu.Wako watu wenye hamu ya ubwabwa waje tutajua tunawapatiaje,” amesema Rungwe


Share:

WAZAZI WAFURAHIA KUWEPO MABASI YA KUTOSHA WATOTO WAO


 
Mfano wa Basi la shule

Na Abby Nkungu, Singida
TATIZO la wanafunzi  shule  za  mchepuo wa  Kiingereza (English Medium) kuchelewa kuchukuliwa kwenda shuleni  na kurejeshwa  nyumbani katika Manispaa ya Singida sasa limebaki historia baada ya  Serikali kuchukua hatua mbalimbali; ikiwemo kuwataka wamiliki wa Taasisi hizo kuwa na mabasi ya  kutosha.


Mwandishi wa habari hizi amebaini kuwa baada ya  janga  la Corona kupungua na  shule  kufunguliwa, Serikali  iliwahimiza  wamiliki wa shule hizo kuwa na mabasi ya kutosha kuepuka msongamano wa watoto wanapokwenda shuleni na kurejea  nyumbani ikiwa ni njia mojawapo ya kuzuia kusambaa zaidi  kwa  maambukizi ya virusi vya COVID-19.

Awali, baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma kutwa katika shule hizo walilalamika kwenye majukwaa mbalimbali watoto wao  kulazimika kuamka saa 11:00 alfajiri kila siku za masomo kwa ajili ya kujiandaa kwenda shule na kuchelewa kurejea nyumbani hadi  saa 2:00 usiku.

Walisema kuwa  hali hiyo ilikuwa ikileta adha kubwa  kwa mtoto wa shule za awali mwenye umri wa chini ya miaka sita kulazimika kuamka mapema  alfajiri na kurejea usiku; hivyo  kuchoka na kusababisha achukie shule kwa kuona kama vile ni adhabu.

Ilielezwa kuwa moja ya sababu kuu iliyochangia watoto wao kuamka mapema ni uhaba wa mabasi ya shule hizo; hivyo gari moja kulazimika kuanza mzunguko wa kuwachukua  watoto mapema alfajiri kuwapeleka shule ili kurudi kuchukua wengine. Vivyo hivyo, wakati wa kuwarejesha nyumbani jioni.

“Tunashukuru Mungu baada ya kupiga kelele kupitia vyombo  vya  habari, Serikali ikasikia na kuwabana wamiliki  wa shule.  Wengi wao wameongeza magari sasa mtoto anaweza kuamka saa moja akajiandaa na kurejeshwa saa 11 jioni” alisema  Halima Njiku mkazi wa Kibaoni mjini Singida.

“Janga la Corona limetusaidia sana, watoto hawapakatiani tena kwenye viti kwani shule nyingi zimeongeza magari  kuepuka  kufungiwa; hivyo kilio chetu  cha muda mrefu  kupitia vyombo vya habari kimesikika...tunashukuru” alisema  mzazi  mwingine, Juma Omari mkazi  wa Mwenge  mjini hapa.

Ofisa elimu Taaluma shule za Msingi Manispaa ya Singida, Gerson Mrua alisema baada ya  malalamiko ya wazazi na walezi, waliamua kuwaandikia barua wamiliki  wote  wa shule  hizo za English Medium kuwataka  wawe na magari ya  kutosha  kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma kutwa.

“Lakini pia tuliwaagiza warekebishe ratiba zao za kuwachukua asubuhi na kuwarejesha jioni wanafunzi ili kupunguza adha kwa wazazi, walezi na watoto pia" alisema  Ofisa  huyo.

Wataalam wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto wanasema mtoto anapaswa kupumzika  angalau kwa saa moja hadi mbili awapo shuleni na kwa shule zinazokaa na watoto kwa muda mrefu zaidi lazima ziwe na ratiba yenye huduma ya mapumziko; ikiwemo kulala kwa muda kwa kuwa kupumzika ni afya kwa mtoto kwani ubongo wake bado unakua kwa kasi.  MWISHO
Share:

HESLB yaongeza muda wa kuomba mkopo.....Sasa mfumo kufungwa Septemba 10 badala ya Agosti 31

Na Mwandishi Wetu
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza kuongeza muda wa siku kumi za kuomba mkopo kuanzia kesho (Jumanne, Septemba 1, 2020) ili kuwawezesha wanafunzi waombaji mkopo ambao hawajakamilisha maombi yao ya kukamilisha.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amewaambia wanahabari jijini Dar es salaam leo (Jumatatu, Agosti 31, 2020) kuwa uamuzi huo unafuatia maoni, ushauri na maombi kutoka kwa wanafunzi, wazazi na walezi ambao HESLB imepokea.

Maombi yaliyopokelewa hadi sasa
“Hadi leo asubuhi, tumeshapokea maombi 85,921 kwa njia ya mtandao, na kati ya hayo, maombi 71,888 sawa na asilimia 84 ni kamilifu na yana nyaraka muhimu na mengine 14,033 yanakosa nyaraka muhimu kama vyeti vya kuzaliwa au vya vifo vya wazazi wa waombaji ambavyo havijathibitishwa na RITA au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar maarufu kama ZCSRA,” amesema Badru.

Badru ameongeza kuwa HESLB imeendesha programu za elimu ya uombaji mkopo kwa usahihi kwa wanafunzi katika mikoa 14 ya Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na kwenye kambi 18 za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambako wamepokea maoni na maombi ya kuongezwa kwa muda na kutoa nafasi kwa wanafunzi waliopo kwenye kambi za JKT kuomba mkopo mara wamalizapo mafunzo.

“Kuhusu waliopo JKT hivi sasa, tunaendelea kuwasiliana na Makao makuu ya JKT ambao tunashirikiana kuhakikisha vijana wote wahitaji wanapata fursa bila kuathiri mafunzo ambayo ni muhimu,” amesema Badru.

Bajeti ya Mikopo kwa 2020/2021
Kuhusu bajeti ya fedha za mikopo, Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema katika mwaka wa masomo 2020/2021, Serikali imetenga TZS 464 bilioni kwa ajili ya wanafunzi 145,000 wa taasisi za elimu ya juu na kati yao, 54,000 wanatarajiwa kuwa ni wa mwaka wa kwanza.

“Hili ni ongezeko la kutoka jumla ya TZS 450 bilioni zilizotolewa mwaka huu 2019/2020 ambazo zimewanufaisha jumla ya wanafunzi 132,292 hadi sasa,” amesema Badru katika mkutano uliohudhuriwa na wawakilishi kutoka RITA na Shirika la Posta Tanzania (TPC), taasisi zinazowahudumia waombaji mkopo.

Ushauri wa RITA na Posta
Akiongea katika mkutano huo, Meneja Masoko wa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) Josephat Kimaro amewakumbusha wanafunzi waombaji mkopo waliowasilisha maombi ya uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa au vya vifo vya wazazi wao, kufungua barua pepe walizotumia kuwasilisha maombi yao RITA ili kupokea majibu.

Naye Meneja Mkuu anayesimamia Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Mwanaisha Said amesema wamekubaliana na HESLB kuendelea kupokea nakala ngumu za maombi ya mikopo katika ofisi za TPC nchini kote na kuziwasilisha HESLB hadi Septemba 15 na kuwataka wanafunzi kutokuwa na wasiwasi na kutokupokelewa kwa bahasha zao.

Mwisho.


Share:

Makonda Amshukuru Mungu Baada Ya Kupata Watoto Mapacha..."Niliitwa Tasa"

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  na mkewe, Maria,  wamepata watoto wengine wawili ambao ni mapacha wa kiume na wa kike.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda amethibitisha kuwa mkewe Maria amejifungua na kufanya idadi ya watoto wao kufikia watatu sasa huku akimshukuru Mungu kwa zawadi hiyo kwani hapo awali aliitwa tasa lakini leo ameuona ukuu wa Mungu.

"Heshima na Mamlaka ni zako eee Mungu wa Mbingu na Nchi na kwako wewe tunalia Aba, nitaendelea kutaja ukuu wako siku zote za maisha yangu kwakua hujawahi kuniacha hata dakika moja.

"Pamoja na mapito magumu na mazito lakini naiona nuru yako huku nikisikia sauti ya ROHO mtakatifu ikisema mwanangu Paul Christian Makonda nalikujua kabla sijakuumba na nikakutenga kwa kusudi langu usikubali TAA iwakayo ndani yako ikazimika.

"Ona sasa unavyozidi kuniheshimisha katikati ya machozi umenipatia zawadi tena itokayo kwako.

"Mimi nilieitwa tasa ulinipa mtoto KEAGAN ambaye alishangaza ulimwengu kwa ujio wake: Ukaona haitoshi LEO umenipa DOUBLE PORTION:Leo Mungu wangu umenipa MAPACHA tena wa KIUME na Wa KIKE hii yote ni kutangaza UKUU wako maishani mwangu.

"Kwa wale ambao bado hawajakuamini na wanateseka juu ya uzazi,naomba kupitia watoto hawa wakauone ukuu wako Ewe YESU mwana wa Mungu ulie hai. Hongera sana kipenzi changu Maria Mungu amejitwalia utukufu kupitia wewe.

"Asanteni sana watumishi wa Mungu, wazazi wetu, dada na kaka zetu kwa kuwa nasi nyakati zote, kama ambavyo mmekuwa baraka kwetu.Naomba pia Mungu awainulie watu wema nyakati za uhitaji wenu.

#EhhNafsiYanguMUHIMIDI-Bwana
#MoyoWaShukrani,” ameandika Makonda.


Share:

Mwenyekiti Wa CCM Rais Magufuli Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi CCM Jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM wakati wakiimba Wimbo wa Chama kabla ya kuongoza Kikao hicho cha Kamati Kuu jijini Dodoma leo tarehe 31 Agosti 2020



Share:

Waandishi wa Habari Waaswa kutoa elimu kwa umma kuhusiana na magonjwa ya mlipuko

Samira Yusuph
Simiyu.
Waandishi wa habari mkoani Simiyu wameaswa kutoa elimu kwa umma kuhusiana na magonjwa ya mlipuko ili kuongeza uelewa wa namna ya kujikinga na kukabiliana na magonjwa hayo kwa jamii.

Akiwafunda waandishi wa habari, Mratibu wa magonjwa ya mlipuko mkoani Simiyu Dk Hamis Kulemba amewataka waandishi wa habari kuwa kioo katika kutoa elimu ya magonjwa ya mlipuko ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa.

"Mkawe mabalozi wazuri kwa wananchi kwa sababu nyinyi mpo karibu na wananchi na mnaishi nao hivyo tumieni nafasi hiyo kuhakikisha kuwa elimu inafika kwa wananchi na wanaitumia ipasavyo," alisema Kulemba.

Aidha kulemba alisema kuwa kinga kubwa ya magonjwa ya mlipuko ni usafi hivyo wananchi wakielimishwa kuhusu usafi wa mazingira yao itakuwa ni msaada ambao ni kinga na utaleta manufaa katika jamii.

Akifafanua namna ambavyo wamekuwa wakikumbana na changamoto ya magonjwa ya mlipuko Dr Nyangi Thomas alisema kuwa katika mkoa huu ugonjwa mkubwa unaosumbua ni kuhara.

"Kumekuwa na namba kubwa ya wagonjwa wa kuhara hasa watoto na hii inatokana na hali ya mazingira ya huko vijijini inakuwa ni changamoto kukabiliana nayo sisi wakija hapa wanapata huduma lakini tunawapa elimu pia ili wakirudi vijijini wakafunfishane namna ya kujikinga," alisema Dr Nyangi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa wa mitaa ya bariadi wameeleza ufahamu wao kuhusiana na kujikinga na magonjwa ya mlipuko na kusisitiza kuwa elimu inahitajika zaidi katika jamii ili waweze kujilinda dhidi ya magonjwa hayo.

"Kidogo afadhari saizi baada ya mlipuko wa ugonjwa wa kovid-19 uelewa umeongezeka kwenye kunawa mikono na kuwa wasafi lakini bado kuna yale mazoea ndio yanatutesa inabidi tuelimishwe zaidi," alisema Raheri George mkazi wa Kidinda.

"Yaani mambo ya kunawa mikono tumeanza kuyasahau saizi, lakini ni vizuri sana kama tukiyazingatia kwa sababu ilikuwa ni vizuri na tuliepuka hata  virusi vya korona wapite hata na matangazo ili kutukumbusha tusijisahau,"alisema Zainabu Banemhi mkazi wa Bariadi.

Katika maeneo mengi ya kanda ya ziwa ugonjwa wa kuhara umekuwa ukishika kasi kutokana na hali halisi ya mazingira ya mazoea ambapo asilimia kubwa ya wakazi wake ni wakulima, wavuvi na wafugaji.

Mwisho.


Share:

Waziri Wa Kilimo Awataka Watumishi Wa Wizara Ya Kilimo Kuisoma Ilani Ya Uchaguzi Ya CCM Ili Kujiandaa Na Utekelezaji Wake

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Watumishi wa Wizara ya Kilimo wameagizwa kuisoma ilani ya Chama Cha Mapinduzi iliyotolewa na Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM Agosti 2020 kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha dharula na Menejimenti na watendaji wakuu wa Bodi za mazao pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo kilichofanyika Jijini Dodoma Leo tarehe 31 Agosti 2020.

Waziri Hasunga amesema kuwa Ilani ya CCM ina mambo mengi makubwa na muhimu ya kuhusu sekta ya kilimo ambayo yameainishwa katika ukurasa wa 33 mpaka ukurasa wa 46.

Maeneo hayo ambayo CCM imebainisha ili serikali yake itakapopewa dhamana kwa mara nyingine iyatekeleze ni pamoja na usimamizi madhubuti wa Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awwamu ya Pili (ASDP II) kwa kusimamia kwa weledi matumizi bora ya ardhi pamoja na maji ili kuwa na kilimo chenye tija.

Kuongeza uzalishaji wa mbegu bora za kilimo, Usimaizi madhubuti wa mbolea na viuatilifu ili kuondokana na changamoto ya viuatilifu na mbolea feki kadhalika kuhusu umuhimu wa kuongeza maeneo ya umwagiliaji ikiwa ni pamoja na usimamizi madhubuti wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji nchini ili kuondokana na dhana ya kutegemea kilimo cha msimu badala yake kuhamia katika kilimo cha Umwagiliaji, Tija na kuongeza uzalishaji.

Katika kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Prof Siza Tumbo, Waziri Hasunga amemuagiza kila mtumishi wa serikali katika Wizara ya Kilimo kuitafuta na kuisoma ilani ya uchaguzi ili kutafakari na kujiandaa kwa ajili ya utekelezaji wake kwani imani yake CCM itashinda kwa kishindo na hivyo kuendelea kuongoza dola.

Amesema kuwa katika ukurasa wa juu wa ilani uliopambwa na kauli mbiu isemayo “Tumetekeleza kwa Kishindo, Tunasonga mbele Pamoja” ilani inaonyesha dira na muelekeo wa utendaji wa shughuli mbalimbali za wizara ya kilimo ambapo miongoni mwa picha kumi zilizowekwa juu ni picha mbili zinahusu sekta ya kilimo hivyo ilani ya CCM imeonyesha umuhimu wa sekta ya kilimo nchini.

Ilani hiyo yenye kurasa 303 katika ukurasa wa 30 mpaka 33 imebainisha umuhimu wa usimamizi wa sekta ya Ushirika ikiwemo kusimamia masoko ya wakulima kadhalika kuongeza tija ya usiamamizi wa vyama vya Ushirika nchini ili kuwanufaisha wakulima nchini.

MWISHO


Share:

Mtoto darasa la pili, miaka (9) mkoani Kigoma alipukiwa na bomu

(Picha:Mtandao)
Mtoto mwenye mwenye umri wa miaka 9 katika kijiji cha Kasumo kata ya Kajana wilayani Buhigwe mkoani Kigoma amepoteza maisha baada ya kulipukiwa na bomu Agosti 28, 2020.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi James Manyama amesema,''Mtoto huyo ajulikanaye kwa jina la Abas Jeras, mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Lemba kijiji cha Kasumo Kata ya Kajana alipatwa na mkasa huo tarehe 28 mwezi wa nane mwaka huu baada ya kuokota bomu bila kujua na kuanza kulichezea kisha bomu hilo kulipuka na kusababisha apoteze maisha''.

Polisi inahusisha uwepo wa bomu hilo katika kijiji hicho huenda ni kilikuwa likitumiwa kama njia na makundi ya waasi waliokuwa wakitoka nchi ya Burundi kwenda kambi ya wakimbizi ya Mtabila hivyo kudhaniwa huenda liliangushwa na watu hao.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi wote wanaoishi vijiji vinavyopakana na nchi ya Burundi kuwakataza watoto kuokota vitu na kuvichezea ili kuepusha madhara kama yaliyotokea.


Share:

Picha : TCRA, UCSAF WAKUTANA NA WADAU WA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA….WASISITIZA KUJENGA MINARA YA PAMOJA


Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) umekutana na wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwemo wamiliki wa vituo vya Radio, Televisheni, watoa huduma za usafirishaji wa vifurushi na watoa huduma ya maudhui mtandaoni kwa lengo la kuwajengea uelewa watoa huduma na wadau hao kushiriki shughuli za mfuko wa UCSAF na kutimiza wajibu wao kisheria. 

Akizungumza katika Mkutano huo leo Agosti,31 2020 uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala UCSAF, Pius Joseph alisema mkutano ulilenga kuwajengea uelewa wadau wa mawasiliano namna mfuko wa UCSAF unavyofanya kazi na wajibu wao kisheria.

Joseph aliyataja miongoni mwa mafanikio yaliyofikiwa na mfuko wa UCSAF ni pamoja na kufikisha huduma ya mawasiliano ya simu katika kata 631 kati ya kata 994 zilizosainiwa mkataba,ufikishwaji wa matangazo ya runinga ya kidigitali katika mikoa ya Katavi, Geita,Simiyu,Njombe na Songwe pamoja na ujenzi wa vituo 10 vya TEHAMA Zanzibar na 11 Tanzania bara ambapo kituo kimoja kimejengwa katika kila wilaya. 

Hata hivyo alisema suala la ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi unaathiri kasi ya mfuko kufikisha mawasiliano,ukosefu wa fedha za kutosha kufikisha mawasiliano kwa kipindi kifupi zaidi kulingana na mahitaji na uelewa wa watoa huduma na wadau mbalimbali kushiriki shughuli za mfuko na kutimiza wajibu wao kisheria. 

Joseph aliwashauri wamiliki wa vituo vya utangazaji kushirikiana kujenga minara ya pamoja ili kupunguza gharama za kuendesha vituo vya matangazo na kwamba UCSAF inachofanya ni kuwawezesha watoa huduma kwa kuwapa ruzuku ili kujenga minara. 

Kwa upande wake, Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya UCSAF alisema upenyo wa kuenea kwa vyombo vya habari kanda ya Ziwa bado hauridhishi ambapo usikivu wa redio Kanda ya Ziwa upo chini ya asilimia 50 hivyo kuwaomba Watoa huduma za mawasiliano kuomba Ruzuku UCSAF kwa ajili ya kujenga minara ya pamoja ili walau usikivu ufikia asilimia 60. 

“Mkijenga minara maeneo mengine,kama kuna mnara umejengwa na wadau wa sekta ya utangazaji,gharama zitapungua. Tuache ubinafsi tutumie minara iliyojengwa kwa ruzuku ya serikali. Lengo tunataka kuongeza usikivu wa radio Kanda ya Ziwa”,alisema Mhandisi Mihayo. 

"Kuna watu wanawafanya nyinyi kama vitega uchumi, akili kubwa mnaelekeza kulipia kodi ya minara ili msizimiwe matangazo,hao wanaowapangisha silaha yao kubwa ni kuzima matangazo. Nawasihi wamiliki wa vituo vya utangazaji kuungana. 

Tumieni nafasi hii mji – organize, leteni maombi UCSAF kujenga mnara wa pamoja ili kupunguza gharama za uendeshaji wa vituo vyenu tuache wivu na ubinafsi. Jengeni na kumiliki vya kwenu kupitia ruzuku ya serikali, tunataka mjenge wote, utakachotakiwa kufanya ni utachangia umeme na kulipa mlinzi tu”,aliongeza Mihayo. 

Hata hivyo Mjumbe wa Bodi ya UCSAF, Samweli Nyalla  alisema lengo la UCSAF kuhamasisha watoa huduma za mawasiliano kujenga minara ya pamoja ni kutaka kupeleka matangazo sehemu ambazo hakuna mawasiliano.

"Sasa hatuangalii pale ulipo,tunaangalia kule ambako hufiki,kule unapotakiwa kupeleka mawasiliano ili kuboresha zaidi huduma za mawasiliano",alisema Nyalla. 

Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa na washiriki wa mkutano huo ni pamoja na kulipa tozo kwa mujibu wa sheria,maombi ya mnara kwenye maeneo husika ufanywe na watoa huduma za radio na TV kupitia wawakilishi waliopo katika mkoa husika na mnara unapoanzishwa utumike kwa watoa huduma watakaohitaji kwa kulipia ghrama za umeme na ulinzi na UCSAF ujikite kutoa elimu ya mfuko na wajibu wa watoa huduma za mawasiliano.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwemo wamiliki wa vituo vya Radio, Televisheni, watoa huduma za usafirishaji wa vifurushi na watoa huduma ya maudhui mtandaoni ulioandaliwa na TCRA kwa kushirikiana na UCSAF uliofanyika leo Agosti 31,2020  katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) akizungumza katika Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala UCSAF, Pius Joseph akielezea kuhusu mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na UCSAF. 
Kaimu Katibu wa UCSAF ,Ipyana Jengela akitoa mada kuhusu uanzishwaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote na malengo ya mfuko huo.
Mkuu wa Idara ya Uendeshaji UCSAF, Albert Richard akielezea kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwemo wamiliki wa vituo vya Radio, Televisheni, watoa huduma za usafirishaji wa vifurushi na watoa huduma ya maudhui mtandaoni wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na TCRA na UCSAF.
Mjumbe wa Bodi ya UCSAF, Samweli Nyalla akizungumza katika mkutano huo.
Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya UCSAF akiwahamasisha watoa huduma za mawasiliano kuungana kuomba ruzuku kujenga minara ili kuongeza usikivu wa vyombo vyao vya habari kwenye maeneo yasiyosikika. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala UCSAF, Pius Joseph.  Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji UCSAF, Albert Richard akifuatiwa na Kaimu Katibu wa UCSAF ,Ipyana Jengela.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala UCSAF, Pius Joseph akizungumza ukumbini.
 Mkurugenzi wa Malunde Media 'Malunde 1 blog', Kadama Malunde akiwa ukumbini.

Mkurugenzi wa Malunde Media 'Malunde 1 blog' , Kadama Malunde (kulia) na Estomine Henry kutoka Shinyanga Press Club blog wakiwa ukumbini.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwemo wamiliki wa vituo vya Radio, Televisheni, watoa huduma za usafirishaji wa vifurushi na watoa huduma ya maudhui mtandaoni wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na TCRA na UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakisoma vipeperushi vya UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakisoma vipeperushi vya UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakisoma vipeperushi vya UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakisoma vipeperushi vya UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini

Mdau wa Mawasiliano Emmanuel Msigwa kutoka Victoria FM akiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Maafisa wa TCRA Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger