Monday, 30 September 2024

UKAGUZI WA VYAKULA VYA MIFUGO NI ZOEZI ENDELEVU- DKT. OMARCH


Hayo yamesemwa na Meneja wa Maabara Kuu ya Veterinari kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Geofrey Omarch alipokuwa akifanya ukaguzi wa vyakula vya Mifugo kwa wazalishaji, wauzaji na watumiaji wa vyakula hivuo Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar Es Salaam Septemba 30, 2024 kwa lengo la kufuatilia ubora wa vyakula vya Mifugo vinavyosindikwa pamoja na kujiridhisha taratibu za usindikwajwi wa vyakula hivyo.

Dkt. Omarch aliongeza kuwa TVLA kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inalenga kuwalinda watumiaji wa vyakula hivyo ili kulinda ubora wa vyakula vinavyozalishwa vitokanavyo na zao la Mifugo pamoja na kuongeza soko la Mifugo kimataifa.

“Tumekuwa tukifanya ukaguzi huu mara kwa mara kwa wasindikaji, wauzaji na watumiaji wa vyakula vya Mifugo ili watumiaji wa mazao hayo wawe salama wakati wote. TVLA imedhamilia kuwapitia wazalishaji wote Tanzania nzima kwa nyakati tofauti ili kujiridhisha kile kinachozalishwa kama kinakidhi ubora, kukagua marighafi za uzalishaji, hatua za uzalishaji pamoja na kukagua vibali vya uzalishaji.” Alisema Dkt. Omarch.

Baadhi ya wazalishaji wa vyakula vya Mifugo Wilaya ya Kinondoni wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwafanyia ukaguzi wa mara kwa mara kwani ukaguzi huo unaowaongezea umakini kwenye uzalishaji wa vyakula.

Sambamaba na hilo wameiomba Serikali kutochoka kwenda kuwakagua na kuwapa ushauri na kuendelea kuwadhibiti baadhi ya wazalishaji ambao sio waaminifu wanaowaharibia soko la vyakula kwa kuzalisha vyakula vyenye mapungufu na kuvipiga chapa za kampuni zingine.

Wakala ya Maabara ya Veterinali Tanzania (TVLA) imekuwa ikifanya ukaguzi wa vyakula vya mifugo mara kwa mara kwa wazalishaji, wauzaji na pamoja na wanunuzi wa vyakula vya Mifugo kwa kushirikiana na wakaguzi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi za Wakuu wa Mikoa pamoja na Halmashauri.
Meneja wa Maabara Kuu ya Veterinari kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Geofrey Omarch (katika) pamoja na timu ya ukaguzi wakipata maelezo kuhusina na hatau za uzalishaji wa vyakula vya Mifugo kutoka kwa Meneja wa Uzalishaji kutoka kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa vyakula vya Mifugo (Falcon Animal Feeds Ltd) Bw. Nassor Ali Nassor (mwenye koti ya blue) Septemba 30, 2024 walipotembelea kiwanda hicho Wilaya ya Kinondoni Dar Es Salaam kwa ajili ya kufanya ukaguzi na uhakiki wa ubora wa vyakula hivyo.
Meneja wa Uzalishaji kutoka kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa vyakula vya Mifugo (Falcon Animal Feeds Ltd) Bw. Nassor Ali Nassor (mwenye koti ya blue) akikabidhi sampuli ya vyakula vya mifugo kwa Mkaguzi wa vyakula vya hivyo wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Dkt. Pius Ntanga Septemba 30, 2024 alipotembelea kiwanda hicho Wilaya ya Kinondoni Dar Es Salaam pamoja na wakaguzi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwa ajili ya kufanya ukaguzi na uhakiki wa ubora wa vyakula hivyo. Aliesimama kulia ni Meneja wa Maabara Kuu ya Veterinari kutoka TVLA Dkt. Geofrey Omarch.
Meneja wa Maabara Kuu ya Veterinari kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Geofrey Omarch (wa pili kushoto) akipimiwa vyakula vya Mifugo vinavyozalisha na makampuni ya usindikaji kwa ajili ya kwenda kufanya ukaguzi kama vinakizi viwango vya ubora kutoka kwa mmoja wa wauzaji wa vyakula hivyo Bunju-Dar Es Salaam septemba 30, 2024 alipokwenda kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa vyakula hivyo kwa lengo la kujiridhisha kama vinakidhi ubora unaohitajika.
Meneja wa Maabara Kuu ya Veterinari kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Geofrey Omarch (wa pili kulia) akipimiwa vyakula vya Mifugo vinavyozalisha na makampuni ya usindikaji kwa ajili ya kwenda kufanya ukaguzi kama vinakizi viwango vya ubora kutoka kwa mmoja wa wauzaji wa vyakula hivyo Tegeta-Dar Es Salaam septemba 30, 2024 alipokwenda kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa vyakula hivyo kwa lengo la kujiridhisha kama vinakidhi ubora unaohitajika.
Share:

RAIS SAMIA : WATUNZENI WATOTO TUSIJE KUSIKIA KESI ZA UJAUZITO, SITAKI KUSIKIA MSURURU WA WALIOPATA ZERO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mchepuo wa Sayansi na Sanaa Namtumbo Mkoani Ruvuma iliyopewa jina la ya Dr.Samia Suluhu Hassan ambayo ujenzi wake umegharimu Shilingi Bilioni 4.6 leo September 27,2024.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais Samia amesema:
"Nizungumze kidogo na walimu, kwanza hongereni mwalimu mkuu hongera na walimu wenzio wote ambao mmekabidhiwa Watoto hawa. Ninalotaka kuongea nanyi ni kwamba tumewakabidhi Watoto wetu, mazingira ni mazuri lakini niwaombe sana ninyi ndiyo Mungu amewachagua kuwa na watoto hawa, naomba watunzeni”. 

"Lakini jingine niwatake Watoto wangu mliopata fursa ya elimu kuitumia vizuri sana nafasi hii. Sitaki nisikie shule hii ina msururu wa walipata zero, hawakupata vyeti sijui daraja la nne aaah aaah, na mmeniambia kwenye kupasi hakuna wasiwasi,” amesema  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.




Share:

RAIS SAMIA AFURAHISHWA NA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA SHULE YA WASICHANA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mchepuo wa Sayansi na Sanaa Namtumbo Mkoani Ruvuma iliyopewa jina la ya Dr.Samia Suluhu Hassan ambayo ujenzi wake umegharimu Shilingi Bilioni 4.6 leo September 27,2024.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais Samia amesema:
"Nimefurahishwa pia kwamba Watoto mmeniimbia wimbo mzuri san. Wimbo ulionihakikishia kwamba huduma zote zinapatikana. Na nimekwenda kuona bwalo tu, nimeona huduma zote zinapatikana. Kilichonifurahisha zaidi ni matumizi ya nishati safi ya kupikia. Huu ni mradi wangu nilioubeba kwa ajili ya wanawake wa Afrika".


Share:

RAIS SAMIA AZINDUA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA 'DR SAMIA SULUHU HASSAN GIRLS SEC. SCHOOL'



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mchepuo wa Sayansi na Sanaa Namtumbo Mkoani Ruvuma iliyopewa jina la Dr. Samia Suluhu Hassan Girls Secondary School ambayo ujenzi wake umegharimu Shilingi Bilioni 4.6 leo September 27,2024.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger